-
Hakuna shida katika kupenda fedha…
Mara nyingi sana huwa nasikia watu wananiambia kuwa unaipenda sana fedha wewe? Au wengine huwa wanasema “unaijua hela”! Na Mimi huwa nawajibu kuwa “ ndiyo naipenda fedha ndiyo maana na yenyewe inanipenda”. Au huwa nawaambia nilizaliwa nayo.
Ninachotaka ufahamu ni kwamba kitu ambacho hukipendi hakiwezi kukupenda wewe. Kama huipendi fedha, ndiyo maana wewe ni masikini kwa sababu fedha nayo inawapenda watu wanaoioenda.
Kuanzia leo, Anza kuipenda fedha.
Soma zaidi: Ijue maana nzuri ya MASIKINI
Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza
Hakikisha Umesuscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
kila la kheri
-
Kutana na Mwajiriwa Ambaye Haitaji Mshahara Ila Anafanya Kazi Kwa Bidii. Nakushauri Baada Ya Kusoma Makala Hii Umwajiri Huyu Jamaa
Leo napenda kumtambulisha kwako mwajiriwa mtiifu kuliko wote duniani, anafanya kazi kwa saa 24 siku saba za wiki. Hadai mshahara wala marupurupu yoyote. Yeye anachojua ni kufanya kazi kwa bidii kila wakati na kutoa matokeo kadiri unavyomwelekeza. Nimekuwa namtumia mwajiriwa huyu kwa siku nyingi sasa na hizi ndizo sifa nilizobaini kwake.
Anaweza kusalimia wateja,
Anaweza kueleza jinsi bidhaa zangu zinavyofanya kazi
Anajibu maswali yanayoulizwa mara kwa mara.
Anatoa mawasiliano yangu ya wateja wanaohitaji kufahamu zaidi kuhusu huduma zangu.
Anatoa shuhuda za watu walionufaika na kazi zangu.
Anatoa maelekezo ya jinsi ya kulipia huduma zangu au vitabu vyangu.Kama kuna kitu kingine cha ziada, bado anaweza kukifanya. Mwajiriwa huyu siyo mwingine bali ni tovuti na blogu.
Kimojawapo kati ya hivi kinaweza kukupa matokeo ila kwa upande wangu natumia blogu.Soma zaidi tofauti Kati ya tovuti na blogu.
Nikiandika kitu kwenye blogu yangu leo hii, hakibadiliki wala kutoweka labda pale nitakapoamua kufanya hivyo. Kama ni ujumbe wa kuelimisha kama huu utaendelea kuwa hewani. Utasomwa leo hii na utasomwa miaka mitano ijayo bila kubadilika.
Hii ndio maana na wewe unahitaji kuwa blogu. Ebu kwa mfano jiulize status yako ya whatsap uliyoandika januari mosi, 2022 iko wapi? Kwa mfano kama kuna mtu aliisoma na akaipenda na leo hii angependa kurejea tena kuiona atafanyaje kuiona? Kiufupi, jibu ni haiwezekani.
Sasa mambo ni tofauti kwa blogu. Yenyewe ukiweka kitu hakitoweki baada ya saa 24 au baada ya muda fulani. Kinaendelea kuwepo. Kama mtu atakisoma au kukisikiliza leo, anaweza pia kurejea kwake miaka kadhaa mbeleni na kusoma tena.
Blogu inafanya kazi saa 24 kwa siku Saba 7 za wiki.
Mtu akiingia mtandaoni usiku na kufungua blogu yako, atanufaika sawasawa na yule atayeingia wakati wa jua kali saa saba mchana.
Blogu yenyewe inafanya kazi bila kujali kuna baridi au mvua.
Kwenye blogu unaweza kuweka makala au mafunzo kuhusu bidhaa au huduma zako.
Unaweza kuwapa watu maelekezo ya namna ya kununua bidhaa yako yoyote.
Unaweza kuwaelekeza watu jinsi ya kuwasiliana na wewe au watu wengine.
Unaweza kujibu maswali yanayoulizwa mara kwa mara n.k.Kwa hakika blogu ni mwajiriwa mzuri ambaye unaweza kumtumia kwenye biashara yako na akafanya kazi bila kuchoka.
Je, wewe upo tayari kumtumia mwajiriwa huyu?Karibu nikutengenezee blogu yako leo hii. Tuwasiliane kwa 0755848391
Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza
Hakikisha Umesuscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
kila la kheri
-
Kitu Kimoja Ambacho Hujawahi Kuambiwa kuhusu Kufanya Makubwa
Kama unataka kufanya makubwa, unapaswa kuwa tayari kuishinda hofu na uoga unaokukabili unapoanza kufanya kitu hicho mwanzoni.
Nakumbuka Kuna wakati nilikuwa naogopa na kujiuliza kwamba nitaongea nini nikukutana na mtu fulani. Ila cha kushangaza muda kidogo baada ya kukutana na mtu huyo mazungumzo yalikuwa yanajiendesha yenyewe kiasi kwamba nilikuwa sijiulizi nitaongea nini.
Hapo ndipo nilipogundua kuwa mazungumzo yanakuwa rahisi unapoanza kuzungumza.
Wakati mwingine nilikuwa najiuliza hivi nitaanzaje kuandika? Ila nilipokuwa naanza, ndipo mambo yalikuwa yanakuwa rahisi. Kumbe, kuandika ni rahisi unapoanza kuandika.
Nilikuwa rafiki yangu aliyekuwa anapenda kufanya mazoezi. Kila nilipokuwa nikijipanga kuanza, nilikuwa najihoji, hivi itakuwaje. Mbona Kama mwili hautaki kufanya mazoezi? Baadaye nilikuja kugundua kuwa mwili wenyewe unapenda kufanya mazoezi pale unapoanza kufanya mazoezi.
Kitu hiki kinafanya kazi hata kwa vitu vingine kwenye maisha. Urahisi wa jambo haupatikani pale unapoanza bali kadiri unavyoendelea kukifanya hicho kitu. Kuna vitu ni vigumu mwanzoni, vigumu zaidi katikati ila rahisi mwishoni.
SOMA ZAIDI: KONA YA SONGA MBELE; IKO WAPI MOTISHA YA JANUARI MOSI?.🤷🏽♂🤷🏽♂
Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza
Hakikisha Umesuscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
kila la kheri
-
USHAURI MUHIMU: Kama una ndoto ya kuwa mwandishi na unawaza nani ATAHARIRI, ATACHAPA na jinsi utakavyouza kazi zako Basi Soma hapa.
Siku ya leo najibu swali nililoulizwa na mmoja wa wasomaji wangu. Anasema;
Hi Godius.
Naitwa Juma Mazengo Malale, kwa sasa nipo Shinyanga, ndoto yangu nikuwa mwandishi wa vitabu. Mpaka sasa nipo kwenye mchakato, changamoto ipo kwenye mambo kama haya.
1. Nani atahariri kazi yangu.
2. Nani atachapa.
3. Wapi nitauza.
4. Nitamudu gharama
5. Kitabu kibebe page ngapi?Habari yangu ni njema ndugu yangu. Karibu kwenye ulimwengu wa waandishi na hongera sana kwa hatua hiyo uliyoamua ya kuwa mwandishi.
Hata hivyo pongezi zangu hupaswi kuzichukua zote kwa sababu kwa maelezo yako, inaonekana umeamua kuanza kuandika ila bado hujaanza kuandika; kitu ambacho ni muhimu sana, linapokuja suala zima la uandishi.
Kiufupi hakuna mtu anaitwa mwandishi kwa sababu eti anatamani kuwa mwandishi au kwa sababu ana mpango wa kuja kuwa mwandishi siku moja. Kama ilivyo kweli kwamba hakuna mtu anaitwa mwanasheria kwa kutamani kuwa mwanasheria bali kwa sababu ameingia darasani, amesomea, amefuzu na anafanyia kazi fani yake.
Mwandishi ni mwandishi kwa sababu anaandika. Kwa hiyo, nataka na wewe uanze kuitwa mwandishi tena kuanzia leo, na utaweza hilo kwa kuanza kuandika.
Hatua hiyo moja tu itaweza kukufungulia fursa za kujua vitu vingine vingi. Kwenye swali lako umeuliza
1. Nani atahariri kazi yangu.
2. Nani atachapa.
3. Wapi nitauza.
4. Nitamudu gharama
5. Kitabu kibebe page ngapi?Naweza kuanza kujibu maswali hayo baada ya kujihakikishia kuwa umeanza kuandika.
Kwa kuwa najua baada ya kusoma hapa utaendelea mbele na kuanza kuandika , basi acha niendelee kukujuza zaidi, ila sharti langu kwako ni moja tu. Uweke mpango wa kuandika mara tu baada ya kusoma makala haya.
UTAANDIKA KUHUSU NINI
Kuna maeneo mengi ambayo wewe unaweza kuandikia. Unaweza kuandika mengi kuhusu
👉maisha yako (maisha yako ni ya tofauti sana, unaweza kuwa unayachukulia poa, ila kuna mengi kutokana na maisha yako ambayo yanaweza kuwa msaada kwa watu wengine).👉 Unaweza kuandika kuhusu ujuzi ulio nao ambao uliwahi kuupata kwa kufanya kazi fulani.
👉 Unaweza kuandikia eneo la taaluma yako. Kama kuna vitu umejifunza basi kuna watu wengine ambao wangependa kuvifahamu kwa kina hivyo vitu, unaweza kuwaelimisha watu kuhusu hivyo vitu kupitia maandishi yako.
👉 Unaweza kuandika kuhusu kitu unachopenda kufuatilia. Kama kuna kitu unapenda kufuatilia, basi unaweza kuamua kuzama ndani zaidi ili kukifuatilia hicho kitu huku ukiwa unawajuza wengine kwa kuwaandikia.
👉 Yapo mambo mengine ya kuandikia, ila kwa leo hayo yatoshe. Mengine utayasoma kwenye kitabu changu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30.
NANI ATAHARIRI KAZI YANGU
Wewe ndiye unapaswa kuwa mhariri wa kazi yako ukiwa mtu wa kwanza. Pia kuna wahariri watalaam ambao utawasiliana nao baada ya kukamilisha kazi yako, nao watakuwa tayari kukusaidia. Hivyo, Anza kuandika kwanza, ukifikia hatua ya uhariri wa kazi yako, itakuwa rahisi tu kukuunganisha na wahaririNANI ATACHAPA KAZI YAKO
Wachapaji pia wapo wa kutosha. Anza kuandika kwanza na soma kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30 ili uweze kupata zaidi mambo mengine kwa undani.NITAMUDU GHARAMA
Ndio utaweza kumudu gharama.KITABU KIBEBE PAGE NGAPI.
Itategemea unandikia nini na unataka kueleza mada kiundani kiasi gani. Binafsi nikiwa naandika kitabu huwa sifikirii sana kuhusu kurasa za kitabu. Ila huwa nafikiria zaidi kuhusu kile nilichonacho kuhusu mada husika. Huwa najitahidi kuandika kila kitu ninachojua na mwisho wa siku upande wa kurasa huwa unajipanga wenyewe. Ila kwa kuwa umeuliza kuhusu kurasa, basi acha nikwambie kwamba viwango vya kimataifa vya kuita kitu kitabu ni kurasa 50. Ila hili lisikuwazishe sana, Anza kuandika kwanza mambo mengine yanajipanga kadiri utakavyoendelea.Kwa leo inatosha na ninakomea hapo. Hata hivyo, nakushauri sana, usome kitabu changu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30. Kitabu hiki kina kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uandishi wa vitabu na makala.
Kipate kitabu hiki kwa 6,500/- tu. Kupata kitabu hiki utatuma hicho kiasi kupitia 0684 408 755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.
Umekuwa nami,
GODIUS RWEYONGEZA
Morogoro-Tz
0755848391
-
USIPOJITAMBUA, KUNA WATU WACHACHE WANAOJITAMBUA WATAKUTUMIA WANAVYOTAKA
Kuna stori moja ya mchungaji huko Nigeria, ambayo nimelazimika nikushikirishe kwa lengo la kukwambia kitu. Na stori hii ni ya mchungaji Dr. JS Yusuf wa Nigeria ambaye yeye ameanzisha utaratibu wa kuuza chupi kwa wanawake. Chupi hizi zina picha yake na anasema kwamba, mwanamke yeyote atakayevaa chupi hizi, atakuwa na mvuto kwa wanaume na ataweza kumpata mwanaume bora, asiyedanganya, na Wala hawezi kuachika.
Kiufupi, mchungaji anawahidi wanawake kuwa wakivaa chupi zake, basi hawatakuwa na maumivu yoyote ya moyo na pia itawakinga dhidi ya magonjwa. Na chupi hizi zinauziwa madhabahuni.
Kutokana na kijistori hiki, nimeona niseme haya ili yaweze kukusaidia.
Kwenye dunia hii kujitambua ni muhimu sana, unapaswa kufanya chini juu, kuhakikisha kwamba unakuwa na ndoto kubwa na kusudi la kuwa hapa duniani na kujiweka bize na mambo yako.
USIPOJITAMBUA kuna watu wachache wanaojitambua watakutumia wewe, kadiri watakavyo. Watakuendesha na wewe utaendesheka. Mfano mzuri unaweza kuuona kwa wanasiasa. Huwa wanawaendesha wafuasi wao kwa sera na maoni ya hapa na pale. Leo anaweza kusema hili, wafuasi wake wakashangilia, na kesho yake akasema lile wafuasi wakashangilia.
Pia, ujifunze kuwa na msimamo na kusimamia ndoto zetu, malengo na kusudi la maisha yetu. Usiwe mtu wa kuyumbishwa, usiwe bendera hufuata upepo.
Tatu, fahamu kuwa nguvu ya kweli ya kukusaidia wewe kusonga mbele, tayari unayo. Ndio maana James Allen aliwahi kusema; ugunduzi mkubwa niliougundua kwenye zama zangu ni kuwa binadamu ana uwezo mkubwa kuliko unavyoweza kufikiri. Na watalaamu wengi wamethibitisha hili. Utafiti mwingine umeonesha kuwa watu wengi wanatumia chini ya asilimia kumi ya uwezo wao. Hata wale unaowaona kama wamefanya makubwa, jua kabisa wametumia chini ya asilimia kumi.
Kwa hiyo, wewe tayari unao uwezo mkubwa ndani yako. Ila sasa ukikaa na kuanza kusubiri sijui chupi ziamshe uwezo huo, utasubiri sana. Nashauri uwe mtu wa kutumia nguvu na uwezo ulionao. Anza leo.
Nashauri uanze kusoma kitabu changu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. Pata hardcopy kwa elfu 20 tu. Na soft copy kwa elfu kumi.
SOMA ZAIDI: Jinsi ya kuwa na fedha kama serikali
Jitambue uoke maisha yako. Wasiliana nami leo kupata nakala yako kupitia 0755848391.
-
Lengo Lako Kuu La Mwaka 2022 Ni Lipi? Au Ndio Unamwachia Mungu🤔?
Jana nilienda kumtembelea mwalimu wangu wa shule ya msingi ambaye kwa sasa ni mstaafu. Kama ilivyo kawaida ya watanzania wengi, nilipofika alifungulia runinga ili tuburudike kwa kuangalia manjonjo ya kimambele.
Alifungulia channel ya Clouds na nilipoangalia tu kwenye kioo cha runinga nilikutana na swali lililosema, *Lengo lako kuu la mwaka 2022 Ni lipi? Au ndio unamwachia Mungu🤔?*
Sikutanii, swali hili lilivuta sana umakini wangu. Kwa miaka kadhaa ambayo nimekuwa nikiongea na vijana na watu mbalimbali kuhusu maisha, wengi wamekuwa wakiishia kuniambia hawana malengo badala yake wanamwachia Mungu maana yeye ndiye kila kitu/ mweza yote/ alpha na omega.
Hawajui wanataka nini badala yake wanamwachia Mungu.
Hawana mipango ya kesho kwa kusema kwamba huwezi kupanga, mambo yajayo kwa kuwa Mungu tu ndiye anajua. Hawajifunzi hata kwa serikali inayoweka bajeti kila mwaka na yenye mipango ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima unaofuata. Yaani unakuta kamtu hakana malengo, kanisani hakaendi, dhambi kanafanya kila siku halafu ukikauliza lengo lake kanakwambia namwachia Mungu.???Sasa kabla sijaendelea mbele naomba kukuuliza wewe [WEKA JINA LAKO HAPA], Lengo lako kuu la mwaka 2022 Ni lipi? Au ndio unamwachia Mungu🤔?
USIMBEBESHE MUNGU MSALABA USIO WAKE.
Ndio Mungu ndio kila kitu, lakini amekuumba wewe na mauwezo makubwa sana na bado amekupa UHURU WA KUCHAGUA mazuri na mabaya. Hivyo, jukumu la kuchagua aina ya maisha unayotaka ni la kwako.
Mungu hawezi kukuchagulia wewe kuwa masikini wala tajiri, huo ni uchaguzi unaouchagua mwenyewe kupitia maamuzi unayofanya na vitendo vyako vya kila siku. Na hata mamuzi ya mwaka 2022 iweje yapo mikononi mwako. USIMBEBESHE MUNGU MSALABA USIO WAKE.
Kwenye Biblia Mungu aliwapa uhuru wa kuchagua watoto mapacha (Esau na Yakobo). Mmoja alichagua kuwa mwindaji (mtu aliyekuwa anafanya kazi za nguvu) na mwingine alichagua kukaa nyumbani (alikuwa anafanya kazi kwa akili).
Sasa na wewe usipochagua wapi unataka kwenda, wapi unataka kufika na aina ya mtu unayetaka kuwa, utakuwa unamwangusha Mungu aliyekupa uwezo wa kipekee na shetani atakuzomea wewe!
Na hata Mungu akitaka kushusha baraka zake juu yako, atashindwa azishushie wapi kwa sababu hujaegenea popote. Wewe kwako maisha ni bora liende. Ukisukumwa unasukumika, wakienda unaenda, wakirudi unarudi, upepo wa kaskazini ukivuma unakupeperusha, wa kusini nao unakupeperusha….wewe ni bendera gazeti, mlingoti tope!
MAISHA YAKO NI WAJIBU WAKO
Maisha yako ni wajibu wako, ukishinda ni juu yako, na ukishindwa ni juu yako.Ndiyo maana wewe unapaswa KUWEKA mipango ya wapi unataka kwenda na wapi unataka kufika. Na hapo ndipo sasa Mungu atatokea KUBARIKI KAZI ZA MIKONO YAKO.
Watu wengi wanatumia kigezo cha Mungu kama kigezo cha wao kutofanya kazi. Ndio maana wengine wanasema aliyekupa wewe ndio kaninyima mimi. Wakati wanasema hivyo Mungu anawaambia kasome Mithali 6:6-11.
Lakini pia Mungu anawasisitizia kuwa hana upendeleo bali anaibariki mikono ya mtu yeyote anayejishughulisha.LENGO LAKO KUU LA MWAKA
Ili mwaka wako uweze kwenda vizuri, unapaswa kuwa na malengo ambayo utayafanyia kazi ndani ya mwaka huu.
Kuwa na lengo kuu moja ambalo utalifanyia kazi, kiasi kwamba mpaka mwaka huu unafika mwishoni uweze kusema kwamba kweli mwaka huu nimeweza kufanya kitu.
Kitu cha kufanya leo.
Weka lengo lako kuu la mwaka huu.
Kisha baada ya hapo andika malengo yako mengine. Hivyo, unaweza kuwa na zaidi ya lengo moja ila lengo lako kuu la mwaka 2022 liwe moja.Ukiwa na lengo moja kuu inakuwa rahisi kwako kuwekeza nguvu zako kwenye hilo lengo. Ukiwa na lengo kuu utakuwa tena siyo bendera hufuata upepo.
Kazi yako ya kufanya leo, andika lengo lako kuu la mwaka 2022?
Unaweza kunishirikisha lengo lako kupitia simu/WhatsApp +255755848391
Naomba nimalizie kwa kukuuliza, “Lengo lako kuu la mwaka 2022 Ni lipi? Au ndio Unamwachia Mungu🤔?”
NAKUKUMBUSHA TU!
Unaweza kupata nakala yoyote ya kitabu changu kwa elfu 3 tu. Chagua nakala unayopenda hapa (BONYEZA HAPA KUONA VITABU VYANGU)
https://www.getvalue.co/home/seller_collection/393Kisha tuma elfu 3 ili niweze kukutumia kitabu ulicholipia.
Ukihitaji kupata vitabu vyangu vyooote kwa pamoja. Utalipia elfu 50 tu. Vipo vitabu 17.
Lipia kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.MWISHO WA OFA HII NI TAREHE 10 JANUARI 2022
Karibu.GODIUS RWEYONGEZA
+255755848391
Bukoba-Tanzania
www.songambeleblog.blogspot.com -
Kheri ya mwaka mpya 2022
Huu ni mwaka ambao kwa hakika ulikuwa umeusubiria kwa hamu kubwa sana. Sasa hatimaye umefika. Wakati unajipongeza kwa mwaka mpya hakikisha
1. Umeweka mipango dhabiti kwa ajili ya huu. Usiishi mwaka huu bila malengo. Ongozwa na malengo 2022.2. Hakikisha unachagua kitu kimoja ambacho utakifanya kwa nguvu zako zote bila kuchoka mwaka 2022. Binafsi nimechagua kuandika na kuweka NGUVU zaidi kwenye uandishi, mwaka huu tegemea makubwa kwa upande wa maandiko yangu.
Hayo ndiyo machache niliyotaka nikushikirishe leo.
Mwaka huu ukawe mwaka bora kwako.
GODIUS RWEYONGEZA
0755848391
Leo naandika nikiwa Bukoba-Tanzania -
Kama hujui unachotaka sasa hivi, ukikiona kesho hutakifahamu pia
Kuna watu huwa hawaweki malengo kwa kisingizio kwamba kitu chochote wanachotaka wakikiona watakifahamu. Ila ukweli ni kwamba, kama kitu unachotaka hukijui, hata kesho ukikiona hutakifahamu.
Ndiyo maana inashauriwa uwe malengo kwa sababu yanakufanya uone unachotaka. Na chochote kile ambacho akili yako inaweza kuona, basi inaweza kukifikia.
Tembelea blogu yangu kupitia
-
ANZA KIDOGO
Kama kuna kitu nimekuwa nasisitiza kila siku ni kuanza kidogo, kuanza na kile ulichonacho, kisha kuendelea kukuza hicho kidogo ili kutengeneza kikubwa zaidi.
Ebu leo jiulize ni kitu gani kikubwa nimekuwa nataka kuanza kufanya ila sijaanza. Anza leo kidogo.
-
Masomo Matano Kuhusu Fedha Unayopaswa Kuyafahamu Katika Maisha
Fedha ni kitu ambacho kinahitajika sana kwenye maisha. Kila siku lazima tu utatumia fedha iwe ni katika chakula, mavazi, malazi, elimu, afya au maeneo mengine.
Kutokana na umuhimu huo wa fedha, leo ninakuletea masomo matano muhimu kuhusu fedha, unayopaswa kuyafahamu.
1. Unapaswa kufahamu namna ya kutafuta, kutunza na kuwekeza fedha zako.
2. Fahamu kuwa maisha ni wajibu wako Wala siyo mzazi, mme, mke, shangazi n.k.
Ukishindwa ni juu yako na ukishinda ni juu yako pia. Pambana mara zote kufanikiwa kifedha.3. Kwa kila kiasi cha fedha unachopokea bila kujali ni kidogo kiasi gani, hakikisha unaweka akiba. Akiba haiozi.
4. Tengeneza vyanzo mbalimbali vya kipato vitakavyokusaidia kuongeza kipato chako. Kuwa navyo hata kama Ni vidogo, vutakusaidia.
5. Fedha inafuata sana kanuni ya aliyenacho anaongezewa zaidi. Ukiwa na fedha ni rahisi kupata fedha, kuliko pale unapokuwa huna fedha. Hivyo pambana mara zote kuwa nazo.
Soma zaidi: TUKUZE AKAUNTI ZETU AISEE