Home


  • Mambo MATATU USIYOYAFAHAMU KUHUSU KIPAJI

     

    Kwanza ni kwamba, KIPAJI hakiazimwi kama nguo. Ni kitu ambacho unazaliwa nacho.

    Pili, kwa kuwa kipaji tunazaliwa nacho hivyo hukilipii gharama yoyote kuwa nacho. Kitu hicho kinafanya kipaji kuwa na bei rahisi sana kuliko chumvi, pengine ndio maana watu wengine hata hawakithamini wala kukipa kipaumbele maishani mwao.

    Tatu, kipaji huwezi kukitumia ukakimaliza. Kadiri unavyokitumia kipaji chako ndivyo unavyozidi kukiboresha na kukifanya kuwa bora zaidi. Ukisikia wanasema mtu fulani ameshuka viwango kwenye kutumia kipaji chake, basi ujue kuna namna anajibana kwenye kukitumia.

    Kipaji ni kama misuli ya mwili, kadiri unavyokitumia, ndivyo inazidi kuimarika zaidi, usipoitumia inafhoofu.

    Umekuwa nami,

    GODIUS RWEYONGEZA

    Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

    Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

    Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

    Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

    kila la kheri

  • Kitu Kimoja Cha Kufahamu Kuhusu Umaskini Na Utajiri

    Kuna kitu kimoja ambacho leo ninataka ukifahamu kuhusu utajiri na umasikini.
    Kitu hiki ni kwamba maskini wapo siku zote, ila kazana usiwe mmoja wao.

    Kwenye kila jamii unakuta kuna watu wachache wenye utajiri mkubwa   ukilinganisha na wengine wengi.

    Sasa lengo lako linapaswa kuwa ni wewe kuingia kwenye wale wachache ambao wana utajiri mkubwa.

    Utajiri ni kitu ambacho unaweza kukitengeneza kwa kufuata kanuni chache tu kama
    kuweka akiba
    Kutunza akiba hiyo na hatimaye kuiwekeza
    Kuifanya fedha ikufanyie kazi na vitu vingine vya aina hiyo

    Kwa hiyo kitu cha kwanza kabisa ambacho ninataka ufahamu ni kwamba; masikini wapo siku zote. Ila chagua kutokuwa mmoja wao.

    Pili, upende utajiri na ipende fedha, huwezi kupata wala kuishi na kitu ambacho hukipendi. Huwezi kupata fedha wala kuishi na utajiri kama huupendi utajiri. Upende utajiri nao utakupenda. Zipende fedha nazo zitakupenda.

    Wewe si unaona hata kwa watu. Mtu unapoonesha dalili za kumpenda ndio na yeye anakupenda. Ukionesha kumchukia na mwenyewe anakuchukia pia.

    Ndio maana utasikia mtu anasema, Mimi na mtu fulani huwa hatuendani. Maana yake huwa hawapatani, huwa haziivi. Hawawezi kukaa pamoja.

    Sasa kama na wewe huzipendi fedha maana yake wewe na fedha hamwendani, hampatani, haziivi na hivyo huwezi kukaa pamoja na fedha (ndio maana ukizipata unazifuja kwa kuzitumia hovyo).

    Kuanzia leo, anza kuzipenda fedha. Zipende zikupende.

    Nashauri usome vitabu vyangu vya MAISHA NI FURSA ZITUMIE ZIKUBEBE pamoja na kitabu cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA
    Rusha elfu 20 leo nikutumie ebooks zake leo kwa WhatsApp au barua pepe.

    Rusha fedha kwa 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    SOMA ZAIDI:

    Umekuwa nami,

    GODIUS RWEYONGEZA

    Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

    Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

    Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

    Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

    kila la kheri

  • Sababu 03 Kwa Nini Mwezi Januari Unakuwa Mgumu Kwako

    Januari ni mwezi wa kwanza wa kila mwaka. Mwezi unaofuata mara tu baada ya sikukuu za mwisho wa mwaka. Mwezi wenyewe wa januari unaanza kwa shamrashamra za kuushangilia mwaka.

    Ni mwezi ambapo watu wanakuwa wamejichana na kula bata siku chache kabla, huku wakiwa wametumia hata fedha ambazo hawakupaswa kutumia, kitu kinachowafanya waanze mwaka wakiwa wamefuria.

    Watu wanaanza mwaka wakiwa hawana fedha huku upande mwingine fedha zikiwa zinahitajika sana.
    Kuanzia ada za watoto, kodi za nyumba, na mambo mengine

    Vyote hivyo vinahitaji hela na wakati huohuo   mahitaji mengine ya kawaida kama chakula, umeme, kulala, vikiwa vinahitaji hela pia. Hicho kitu kinawafanya watu wachanganyikiwe.

    Kuna utani mtandaoni unaosema

    Watu wafupi mwezi huu mnatupa shida, ukiwa barabarani unatembea unamwona mtu mfupi, unadhani mwanao karudishwa nyumbani kwa sababu ya ada.

    Utani mwingine unasema,
    Kuna ile minyoo ambayo ukiwa nayo unakosa hamu ya kula. Naipataje, maana hii ni januari?

    Wakati hizo kauli hizi mbili zimekaa kiutani, utani tu, ila pia zimebeba ujumbe mzito kuhusu uhalisia wa watu wengi walivyo mfukoni.

    Kwenye makala hii ninaenda kukuonesha kwa nini umefulia mwezi huu wa Januari na hatua za kuchukua ili kuondokana na hiyo hali.

    1. Umefulia kwa sababu unategemea chanzo kimoja cha kipato.
    Hakikisha unakuwa na vyanzo vya kipato zaidi ya kimoja, vitakusaidia kuondokana na ukata.

    2. Umefulia kwa sababu ulitumia fedha nyingi mwishoni mwa mwaka.ulitumia hata fedha ambazo hakupaswa kutumia.

    Suluhisho: kuanzia januari hii anza kuweka akiba maalumu utakayotumia mwishoni mwa mwaka.  Na akiba nyingine kama ambavyo nimekuwa nikikushauri. Na uwe na na nidhamu ya fedha, usitumie fedha za malengo yako mengine kwa ajili kula bata

    3. Umefulia kwa sababu huna hela za kulipa ada za watoto.

    Suluhisho: naomba ufahamu kuwa suala zima la ada za watoto, halipaswi kuwa kitu kigeni kwako. Ni kitu ambacho unakuwa unakifahamu kuanzia januari mpaka disemba. Hivyo kwa mwaka huu uanze kujiandaa kwa kuweka pembeni fedha kidogo kidogo maalumu tu kwa ajili ya ada za watoto.

    Hizo Ni baadhi ya sababu ambazo zinakufanya ufurie januari hii, ziepuke kwa manufaa yako ya sasa na miaka ijayo. Kila la kheri.

    Umekuwa nami,

    GODIUS RWEYONGEZA

    Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

    Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

    Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

    Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

    kila la kheri

  • Mwaka Mpya Mambo Mapya: Kauli Inayopoteza Watu Wengi Na Kuwafanya Washindwe Kupiga Hatua Kila Mwaka

     

    Kauli ya mwak mpya na mambo mapya si kauli ngeni masikioni mwa watu. kila mwaka mpya unapoanza huwa unasikia watu wakiisema kauli hii tena kwa kujidai. Binafsi naiipenda pia kuauli hii, japo kuna watu ambao wanaitafsiri vibaya na hivyo kuitumia ndivyo sivyo.

     

    Unakuta mtu kila mwaka mpya unapoanza yeye anakazana kuhakikisha kwamba anaanza kitu kipya kwa kusema kwamba ni mwaka mpya na kuachana na vitu ambavyo alikuwa akifanya hapo mwanzo. Kama ni fursa utakuta mtu anakimbizana kudaka fursa mpya na kuachana na ile ya zamani.

     

    Ubaya wa hiki kitu ni kwamba kinakufanya ushindwe kubobea na watu wanashindw akukuelewa kuwa wewe ni mtu wa aina gani.

     

    Tafsri nzuri ya mwka mpya na mambo mapya ni kwamba unapaswa kuongeza juhudi zaidi kwenye kile ambacho wewe umekuwa unafanya kwa siku zote. Nyingine ni kwamba unapaswa kufanya mambo mapya kwa kuachana na tabia mbovu ambazo zilikuwa zinakuzuia wewe kusonga mbele na kufikia mafanikio makubwa, badala yake unapaswa kuendelea kushikiliai tabia ambzo zitakufanya uzidi kusonga mbele zaidi.

    Tafsiri nzuri ya mwaka mpya na mambo mapya ni kwamba unapaswa kutoa huduma kwa viwango vya hali ya juu sana (viwango vya nyota tano).

    Tafsiri ya mwaka mpya na mambo mapya ni kwamba kama kuna kitu kitu ulikuwa unakifanya kwa namna ya ukawaida sana, sasa unapaswa kuanza kukifanya kwa viwango vikubwa tena vya hali ya juu sana.

    Kama ulikuwa na tabia mbaya (kaa kuvuta bangi na kunywa pombe) achana nazo.

     

    Hiyo ndiyo tafsiri nzuri y mwaka mpya na mambo mapya, ila siyo kwamba kila mwaka wewe uwe unakimbizana na fursa mpya.

    Nakutakia kila la kheri rafiki yangu. umekuwa nami rafiki yako wa ukweli, Godius Rweyongeza.

     


  • Ni Vigumu Sana Kupata Mafanikio Makubwa Bila Ya Kuwa Na Sifa Hii Moja Muhimu

     

    Kwenye vitabu vitakatifu wanaeleza wazi kuwa mlango wa kuingia mbinguni ni mwembamba. Muda mwingine watakuambia kwamba wanaoitwa ni wengi ila wanaochaguliwa ni wachache.

    Sasa kitu hiki pia huwa kinajitokeza kwenye maisha ya kawaida ya mafanikio. Ni vigumu sana kupata mafanikio makubwa kirahisi, wengi wanapenda mafanikio makubwa ila wachache ambao wanaweza kufanikiwa na kufika mbali. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mlango wa kufikia mafanikio ni mlango usiopitwa na wengi. Ila huwezi kukutana na mtu ambaye amefanikiwa huku akiwa amepitia njia laini.

    Japo njia hii ni ngumu na mbovu, ila ukiweza kuhimili vishindo na kuipita, itakufanya kuwa imara zaidi.

    Hivyo kama kuna sifa kubwa ambayo unaihitaji ili kuweza kufikia ndoto yako kubwa ni kuwa tayari kuhimili vishindo na magumu unayopitia kwenye kazi au biashara au kitu chochote unachofanya.

    Magumu ambayo unapitia japo unaweza kuyaona mabaya, ila yanakuwa yanalenga kukuimarisha na kukufanya wewe kuwa bora zaidi. na hii ndiyo sifa kubwa sana ambayo unaihitaji sana ili kuweza kufikia mafanikio makubwa.

    Umekuwa nami,

    GODIUS RWEYONGEZA

    Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

    Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

    Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

    Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

    kila la kheri

  • Huu Ni Upande Ambao Ni Marufuku Kwako Kuuchagua

     

    Rafiki yangu, najua unafahamu kuwa una uhuru wa kuchagua chochote kile unachotaka kuwa. Unaweza kuchagua kuwa mwalimu, mchekeshaji, mshereheshaji, dereva, mkulima, mwanamichezo, mwanasiasa, mwanaharakati au chochote kile. Huo uhuru unao na wala hakuna mwenye uwezo wa kukuzuia wewe kwenye hilo.

    Hata hivyo, kuna kitu kimoja tu ambacho ningependa kukutahadharisha, na kitu hiki siyo kingine bali kuchagua kuwa mlaji tu. Haupaswi kuwa mlaji wa kazi za watu wengine tu, hila wewe kuzalisha kazi.

    Kwa kitu chochote kile ambacho umechagua kwenye maisha, hakikisha unachagua kuwa mzalishaji.
    Dunia tunayoishi, haipungukiwi hata kidogo na walaji, ila wazalishaji ndio wachache. Wewe kuwa huu upande wa wazalishaji

    Kama ulizoea kuingia YouTube na kuangalia video tu, kisha kuondoka, sasa ni zamu yako pia ya kuzalisha.

    Kama ulizoea kusoma vitabu vya watu wengine, na wewe zalisha hata kwa kutupa mrejesho juu ya mambo uliyojifunza kwenye vitabu husika.

    Rafiki yangu, kuanzia leo. Anza kuwa mzalishaji.

    Umekuwa nami,

    GODIUS RWEYONGEZA

    Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

    Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

    Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

    Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

    kila la kheri

  • Hiki Kitu Tu,Kitakufanya Uwe Na Maisha Ya Kawaida

    Imewahi kukutokea ukaangalia labda igizo au ukasoma kitabu na kuona ni cha kawaida sana na wewe ungeweza kabisa kuigiza hilo igizo au ungeweza pia kuandika kitabu husika?

    Unajua kitu gani kinakutofautisha wewe na huyo aliyeigiza hilo igizo au aliyeandika kitabu husika?

    Kinachokutofautisha ni kuchukua hatua. Mwenzako anachukua hatua na kuigiza igizo alilo nalo ndani yake, wewe unaogopa na kusubiri kila kitu kikae sawa kwa upande wako, unasubiri mpaka ubobee kwenye kuigiza ili uanze kuigiza. Kitu Kikubwa ni kwamba huwezi kubobea bila ya wewe kuchukua hatua ya kwanza na kukamilisha kazi yako ya kwanza, hata Kama ni kidogo.

    Kazi ya kufanya leo: fikiria kitu ambacho umekuwa unafikiria kufanya kwa siku nyingi, kisha anza kukifanya mara moja. Kuanza kufanya kitu ndiyo kutakupelekea kwenye kubobea ba hatimaye kuwa bingwa.

    Umekuwa nami,

    GODIUS RWEYONGEZA

    Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

    Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

    Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

    Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

    kila la kheri

  • Kwa Nini watu wengi husahau malengo ya mwaka mpya Mapema Sana

     

    Juzi tarehe 19 ilikuwa ni siku rasmi ambapo watu wengi huwa wanaacha kufanyia kazi malengo yao na kuanza kuishi maisha ya kawaida. Hii siyo siku ambayo nimeibuni bali ni kutokana na tafiti kuntu zilizofanywa na watafiti wanaoaminika duniani. Na siyo kwamba zimefanywa kwa watu kumi au ishirini, bali zimefanyika kwa watu zaidi ya milioni 800. Ndio milioni mia nane!

    Katika kuwafuatilia watu hawa, iligundukilika kuwa WATU HAWA WANAKUWA NA MOTISHA KUBWA sana wanapoanza mwaka mpya, ila motisha hiyo inapungua zaidi na kwa wengi siku ya 19 ndipo wanaagana kabisa na malengo yao.

    Sasa kwa nini watu huwa wanaachana na malengo yao mapema? Hiki ndicho naenda kueleza kwenye makala ya leo.

    Kwanza ni kuwa na matamanio makubwa huku wakipenda kupata matokeo ya haraka. Mtu anaanza mwaka mpya akiwa na unene wa kupitiliza, anapoanza mwaka anaweka malengo ya kuagana na unene wake huku akiwa anataka kuagana na unene huo ndani ya siku chache tu. Baada ya hapo anaanza mazoezi, ila ndani ya siku 14 za kwanza kunakuwa hakuna mabadiliko yotote ya maana anayoyaona, anaanza kuvunjika moyo. Mpaka siku ya 18 bado pia kunakuwa hakuna kitu kikubwa akbacho kimeonekana. Mtu anaamua kuagana na malengo yake na hiyo inakuwa imeishia hapo.

    Ambacho huyu mtu anasahau ni kwamba kufanyia kazi na kufikia malengo kunahitaji mchakato. Mwanzoni kabisa unaweza usione matokeo yotote, Ni mpaka pale utakapong’ang’ania tena na tena, ndipo matokeo yataanza kujitokeza.

    Siku 18 za kwanza zinakuwa bado sana kwa wewe kuachana na malengo yako.

    Pili, ni msukumo wa vyombo vya habari.
    Mwishoni mwa mwaka vyombo vya habari vinasisitiza sana kuhusu malengo na neno MWAKA MPYA linaibwa sana. Watu mpaka wanafundishwa namna ya kuweka malengo, ila sasa ule mchakato wa kufanyia kazi malengo huwa unasahaulika.  Na vyombo vyenyewe huwa haviendelei kuweka msisitizo  baada ya mwaka mpya kufika. Na hicho ndicho huwa kinawafanya watu kuachana na malengo yao mapema.

    Ninachotaka ufahamu ni kuwa malengo unayoweka yanapaswa kutoka ndani yako, wala kusiwepo na msukumo wa nje au mtu mwingine. Ukiwa na msukumo kutoka nje utaishia njiani mapema sana.

    Hivyo ni vitu viwili ambavyo huwafanya watu washindwe kufanyia kazi malengo yao na kuachana nayo mapema. Viepuke ili uweze kufanyia kazi malengo yako mwaka huu na kuyakamilisha kwa kishindo.

    SOMA ZAIDI: KONA YAA SONGA MBELE; IKO WAPI MOTISHA YA JANUARI MOSI?.🤷🏽‍♂🤷🏽‍♂

    Lengo Lako Kuu La Mwaka 2022 Ni Lipi? Au Ndio Unamwachia Mungu🤔?

    Umekuwa nami,

    GODIUS RWEYONGEZA

    Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

    Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

    Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

    Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

    kila la kheri

  • Usidharau vitu vidogo vina uwezo wa kukufikisha mbali Sana

    Mwaka 1969 binadamu kwa mara ya kwanza aliingia mwezini. Unaambiwa kompyuta iliyotumika kipindi hicho kumwingiza mtu mwezini ilikuwa na uwezo mdogo sana, uwezo wake ulikuwa mdogo mno kiasi cha kuzidiwa na simu janja tunazotumia sasa.

    Ila iliweza kutumika kutufikisha mwezini. Ndiyo maana nimekuwa nakushauri kuwa makini na vitu vidogo, kutokana na madhara au matokeo yatokanayo na vitu hivyo.

    Mbu ni wadogo, ila madhara yake kwa watu ni makubwa. Wana uwezo wa kusababisha malaria ambayo najua unajua madhara yake.

    Wewe pia usidharau hatua ndogo ndogo. Akiba kidogo kidogo unayoweka kila siku, ina uwezo wa kukufikisha mbali. Usidharau.

    Maneno 500 ya kitabu chako unayoandika kila siku, Kuna siku yatakufanya wewe utambulike Kama mwandishi MBOBEVU.

    Mazoezi hayo unayofanya kila siku, yanazidi kuimarisha mwili wako zaidi.

    Ni kitu gani kidogo unekuwa unafikiria kufanya kwa siku nyingi, ila hujakifanya. Ebu nenda kakifanye leo.

    Soma zaidi: NGUVU YA RIBA MKUSANYIKO

    Umekuwa nami,

    GODIUS RWEYONGEZA

    Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

    Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

    Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

    Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

    kila la kheri

  • Leo ndiyo Siku Ambayo Watu Wengi Husahau Malengo Yao Ya Mwaka Na Kuanza Kuishi Kwa Mazoea

     

    Leo ni tarehe 19 jnuari 2022.  Ukiangalia tangu tuuanze mwaka huu, hata hatuna siku nyingi. Ila cha kushangaza ni kwamba kuna watu ambao tayari wameshasau malengo yao.

    Zimefanyika tafiti na imethibitishwa  kuwa tarehe 19 ya kila mwaka mpya, ni tarehe ambayo watu wengi huwa wanasahau malengo yao na hivyo kuendelea kuishi kimazoea.

    Swali langu la kwanza kwako leo bado unayakumbuka malengo yako uliyoweka mwanzoni mwa mwaka huu? Kama huyakumbuki, basi jua wazi kuwa Kuna sehemu kuna tatizo na hizi hapa ni mbinu za kukusaidia siyo tu kuyambuka malengo yako bali kuyafikia.

    SOMA ZAIDI: Lengo Lako Kuu La Mwaka 2022 Ni Lipi? Au Ndio Unamwachia Mungu🤔?

    Moja, jikumbushe malengo yako kila siku. Tena ujikumbushe kwa kuyaandika chini. Fanya hivyo, asubuhi na jioni kila siku kwa siku zilizobaki mpaka ufikie lengo lako. Haufanyi hivyo tu ilimradi umefanya, badala yake unafanya hivyo kwa sababu unaukumbusha ubongo na akili yako kwamba inapaswa kuwekeza nguvu kwenye kutimiza malengo na siyo kingine.

    Pili, kila siku andika chini mbinu au njia za kukusaidia wewe kufikia lengo lako. Jiulize kila siku, Ni kitu gani kimoja ambacho naweza kufanya Leo kikanisaidia kufikia lengo langu. Ukikipata, kifanyie kazi.

    Tatu, ungana na timu ya watu sahihi ambayo inaweza kukusaidia wewe kufikia lengo lako.

    Nne, usikimbizane na malengo mengi kwa wakati mmoja. Fanyia kazi lengo moja kwa wakati

    Tano, ipangilie kila siku inayokuja kwako na itumie vizuri kuhakikisha umefikia lengo lako.

    Sita, kila siku, fanya kitu kuelekea malengo yako.

    Kwa leo ni hayo tu. Nakutakia kila la kheri.

X