Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Utajiri haudaiwi mahakamani, ila ukifanya hivi utaupata

    Rafiki yangu mpendwa salaam, utajiri ni haki yako ya msingi ambayo unapaswa kupata. Tofauti kubwa ya haki hii na nyingine ni kwamba unapaswa kuipambania.

    Wakati haki nyingine zinadaiwa mahakamani, utajiri haudaiwi mahakamani. Utajiri unakuja kwa kutokwa na jasho, damu na machozi.

  • Malengo yako Yasome Kila Siku

  • Semina ya Juni 2024

  • Umewahi kujiuliza kuwa unaweza kupata wapi muda wa Kuandika Kitabu Chako?

    Umewahi kujiuliza kuwa unaweza kupata wapi muda wa Kuandika Kitabu Chako? Jibu ni rahisi sana. Na jibu Hilo lipo kwenye SoMo la leo. kupata kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU, wasiliana na 0684408755 Jina ni GODIUS RWEYONGEZA karibu sana

  • Dhana ya jeshi la mtu mmoja, je ni dhana halisi au tunahitaji kufikiri nje ya boksi?

    Moja ya dhana ambazo zimekuwepo miongoni mwa watu wengi ni dhana ya JESHI LA MTU MMOJA, kuna watu wamekuwa wanaamini kwamba kwenye shughuli zao ambazo wanafanya basi wao wanasimama kama jeshi la mtu mmoja.

    Wakimaanisha kuwa wao ndiyo kila kitu kwenye shughuli au jambo fulani ambalo wanafanya, sasa ambacho leo hii ningependa tujadili hapa ni kwamba je, dhana ya jeshi la mtu mmoja ni dhana halisi au tunahitaji kufikiri kwa namna nyingine?

    Tukitafakari kidogo kuhusiana na dhana hii ya jeshi la mtu mmoja, tuanze labda kwa kujiuliza. Jeshi ni kitu gani. Kujua hili nimezalimika kuangalia kwenye kamusi ya kiswahili sanifu, ambayo inasema kwamba Jeshi ni jumla ya askari ambao wameajiriwa kwa ajili ya kuilinda nchi. Maana ya pili ya neno Jeshi kutoka kwenye kamusi hii hii inasema kwamba jeshi ni jumla ya watu.

    Tukiangalia maana hizi zote mbili tunagundua mambo yafuatayo.

    Kwanza tunagundua kwamba tunapoongelea JESHI. Tayari tunakuwa hatuongelei mtu mmoja bali kikundi cha watu (jumla ya watu).

    Lakini pia ukifuatilia zaidi kwenye maana hiyo, utagundua kwamba jeshi, siyo tu jumla ya watu, bali watu ambao wanafanya kazi kwa ushirikiano ili kufanikisha lengo au kusudi fulani. Hilo ndilo jeshi.

    Sasa mpaka hapo unafikiri Dhana ya jeshi la mtu mmoja bado ni dhana halisi?

    Tukija kwenye biashara kwa mfano. Kwenye biashara kuna vitu vingi ambavyo vinahitajika kufanyika. Unahitaji ufanye masoko, unapaswa kuuza, unapaswa kutengeneza bidhaa na mengine mengi…

    Inawezekana kwenye biashara yako uko peke yako, ila kiuhalisia siyo kwamba wewe ni jeshi la mtu mmoja. Bado kuna watu ambao unashirikiana nao, wasambazaji, watu wa usafiri, wateja n.k

    Kwa hawa watu wote ambao unashirikiana nao, bado huwezi tu kusema kwamba wewe ni jeshi la mtu mmoja.

    Kama wewe ungekuwa ni jeshi la mtu mmoja maana yake ni kwamba ungekuwa unafanya kila kitu mwenyewe bila kuhitaji mtu yeyote, na hata wateja ambao wananunua kwako hawapaswi kuwa wanwanunua kwako, badala yake unapaswa wewe kuwa ndiyo mteja wako kwenye biashara yako, ili tuseme kweli wewe NDIYE JESHI LA MTU MMOJA.

    Ili biashara yako ikue, inahitaji watu. tena watu sahihi, kama hauna hawa watu utaishii tu kufanya biashara kama ambavyo watu wengine huwa wanafanya. Kwa namna ya ukawaida.

    Hata kwenye maisha ya kawaida ya kila siku, dhana ya jeshi la mtu mmoja haipo. Haipo kwa sababu wewe haufanyi kila kitu mwenyewe. Dhana ya JESHI LA MTU MMOJA ingekuwa halisi kwenye maisha ya kawaida maana yake ungekuwa unapika chakula chako mwenyewe kwa sufuria ambazo umezitengeneza mwenyewe, unajisafirisha mwenyewe kwa gari ambayo umeitengeneza mwenyewe, unalima chakula chako mwenyewe kwa jembe na trekta ambayo umetengeneza, unapanda mbegu zako mwenyewe ambazo umezitengeneza mwenyewe, unaangalia runinga ambayo umeitengeneza mwenyewe na vipindi ambavyo umeviandaa mwenyewe na kuendelea na kuendelea.

    Kiuhalisia ni kwamba dhana ya jeshi la mtu mmoja kwenye maisha haipo. Maisha ni kushirikiana na watu.

    Upo kwa sababu fulani yupo, na yeye yupo kwa sababu wewe upo.

    Ninavyoandika makala hii nimemkumbuka Harmonize maarufu kama Konde Boy ambaye anajiita jeshi.

    Akimaanisha JESHI LA MTU MMOJA.

    Kwa maoni yako unadhani Harmonize ni jeshi la mtu mmoja?

    Siyo kweli kwamba harmonize ni Jeshi la mmoja. Harmonize ana meneja wake. Harmonize ana producer. Harmonize ana watu wa video. Harmonize anafanya kazi na watu wa redio na vyombo mbalimbali vya habari n.k

    Hajifanyii interview mwenyewe.

    Hasikilizi muziki wake mwenyewe baada ya kuutoa.

    Haendi kwenye show kujitumbuiza mwenyewe…..

    Ni kwa sababu kuna watu.

    Kumbe dhana ya jeshi la mtu mmoja kwenye maisha ya kila siku, haifanyi kazi.

    Kijana mmoja alimwambia baba yake kuwa baada ya hapa ninaenda kuwa naishi mwenyewe na nitakuwa sihitaji msaada wa mtu yeyote.

    Hili jambo lilionekana kuvuta umakini wa baba yake.

    Hivyo alitaka kuhoji na kuuliza zaidi kuwa je, ataanyaje?

    Mtoto aliendelea kujieleza kwa kusema kwamba nitatatoka hapa, nitaita TEKSI ambayo itanipeleka uwanja wa ndege.

    “Enhee” baba yake alionekana kumakinika.

    Mtoto aliendekea kusema kwamba, nikifika uwanja wa ndege nitapanda ndege na kuelekea sehemu ambapo nitaanza kuishi maisha yangu.

    Baba yake alivuta pumzi kidogo kisha akamwambia je, kwa nini unawatumia watu kufanikisha mambo yako. Kwa nini usifanye kila kitu mwenyewe. kwa nini wewe mwenyewe usijipeleke uwanja wa ndege. Kwa nini wewe mwenyewe usiwe rubani wako mwenyewe?

    Mtoto alibisha kidogo na kusema.

    Lakini si nitakuwa nawalipa?

    Ndipo baba yake alimwambia “kuwalipa watu hakukufanyi wewe kuwa jeshi la mtu mmoja”

    Ukweli ni kuwa, kwenye maisha ya kawaida ya kila siku, naam, kwenye maisha ya kila siku, hakuna jeshi la mtu mmoja. Maana unamkuna mmoja na yeye anakukuna, tunakunana.

    Makala hii imeandikwa nami rafiki yako wa ukweli. Godius Rweyongeza

    Hakikisha umepata vitabu vyangu ili kujifunza zaidi. Kupata nakala za vitabu vyangu ni rahisi sana. Wasiliana nami kwa 0684 408 755 sasa. Namba hiyo ipo whatsap na inapatikana kwa meseji na simu za kawaida.

     

  • Usikope Fedha Kwa ajili ya kufunga Ndoa au harusi

    Usikope fedha kwa ajili ya kufunga ndoa ukitegemea kuwa fedha utakazopata zitarehesha ule mkopo. Mara nyingi huwa haiko hivyo, Kumbuka sijasema mara zote, ila mara nyingi.

  • Natamani kila kijana mwenye simu janja (smartphone) aingize kipato cha milioni moja kwa mwezi. Huu hapa mkeka wa kufanya hivyo

    Rafiki yangu wa ukweli, salaam, hongera sana kwa siku hii nyingine nzuri sana. Siku ya leo, ningependa kukushirikisha kitu muhimu sana. Kitu hiki ni kwamba kama unamiliki simu janja, kama una simu kubwa, ukweli ni kuwa unaweza kuingiza milioni moja kwa mwezi. 

    Lakini ukweli mwingine usiopingika ni kwamba, kiasi hiki ni kikubwa si ndio? Ndio, ni kikubwa.

    Lakini kinawezekana. Hapa tunaenda  namna unavyoweza kufanya hivyo hatua kwa hatua.

    Robert Kiyosaki, nadhani utakuwa unamfahamu vizuri sana, aliwahi kusema kwamba kama unamiliki simu kubwa na bado wewe siyo tajiri basi kuna sehemu unakosea. Hivyo, lengo langu kubwa ni kukuonesha wapi unakosea na mambo ya msingi kabisa ambayo unaweza kufanya.

    Kumbuka kuingiza kipato cha milioni kwa mwezi kunaweza kuhitaji juhudi kubwa na mikakati madhubuti. Hapa kuna baadhi ya njia unazoweza kuzingatia:

    1. Biashara ya Mtandao: Kuanzisha biashara mtandaoni inaweza kuwa njia ya haraka ya kufikia malengo yako. Unaweza kuanzisha duka la mtandaoni, kufanya biashara ya usafirishaji, au hata kuuza huduma au maarifa yako mtandaoni.

    2. Uwekezaji: Wekeza katika masoko ya hisa, mali isiyohamishika, au biashara nyingine zenye uwezekano mkubwa wa kurudisha faida kubwa. Hata hivyo, wekeza kwa busara na ufanye utafiti wa kina ili kuepuka hatari.

    3. Biashara ya Kimkataba: Ikiwa una ujuzi fulani au talanta katika uga fulani, unaweza kujitangaza kama mtaalamu huru na kuuza huduma zako kwa bei nzuri.

    4. Kuongeza Mapato ya Saa za Kazi: Angalia njia za kuongeza mapato yako kutoka kwa kazi au biashara unayofanya sasa. Huenda ukahitaji kuongeza saa za kazi au kuboresha mikakati yako ili kuongeza mauzo au mapato.

    5. Kupanua Biashara Yako: Ikiwa tayari una biashara, fikiria njia za kupanua shughuli zako au kuzindua bidhaa au huduma mpya ambazo zinaweza kuleta mapato ya ziada.

    SOMA ZAIDI: 

    Kumbuka kwamba kufikia lengo la kuingiza milioni kwa mwezi kunaweza kuchukua muda na jitihada nyingi. Ni muhimu pia kuwa na mkakati madhubuti na kuendelea kujifunza na kubadilika kulingana na mazingira ya biashara na masoko.

    Makala hii imeanikwa na Godius Rweyongeza.

    Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu.

    Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

    Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

    SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea.

    Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

    Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

    Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

    Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

    For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com

  • Mtoto Ni Urithi Wako

    Kwa kitabu “1,000 YENYE NGUVU”Mwandishi : Jegi Bassu

    Mwandishi huyu kwa kitabu hiki kutoka sura ya kwanza hadi mwisho anaendelea kutupa masomo muhimu sana kuhusiana na urithi wa mali tutazoacha duniani wakati ambapo tutaaga hii dunia.

    Akitoa nukuu mbalimbali kutoka Baiblia takatifu anatufundisha waziwazi kwamba:

    1.Urithi wetu kama wazazi nambari moja ni watoto. Kwa hivyo basi, wazazi tunapaswa kuwaanda hawa warithi vyema katika nyanja mbalimbali kielimu, kiafya, kifedha, kibiashara, kimaadili n.k ili kazi zao zote na mali wanakusanya leo na siku zambeleni haitapotea bure.

    2. Aligusa jambo la kutowajua watoto wetu kuwa nani siku za mbeleni. Akanukuu pia kutoka bablia takatifu kuwa mtoto ni zawadi au thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambaye yeye ndio anamfahamu kwa makusudi huyo mtoto alizaliwa na atafanya nini.

    Mwandishi anaendelea kuwambia wazazi kwamba hawachukulie watoto wao kama kawaida au kuwadharau ila wajue kwamba watoto hawa kwa mtazamo wa Mungu watafanya makubwa, huwa na vyewo na mamlaka japo wakati wao ku’angaa nakujitambulisha kwa dunia nzima haijafika.

    Nukuu kutoka Biblia takatifu kuhusu Daudi baado alikuwa mchanga na baado hajakuwa mfalme wa ISRAELI nzima:

    1 samueli 16:10 1 mambo ya nyakati 29:263.

    Mwanao ni balozi mpambanaji wakati mwanao akipambania maisha yake mwanzoni kama akiwa shuleni, vilevile anafanya kwa bidii na kuwakilisha wazazi, familia, jamii na mahali alipotoka kama balozi na kamwe hauwezi kuwaangusha.

    Mwandishi anatueleza wazi kabisa kuwa mwanao akiwa shule mbali na pale alipozaliwa au alipokulia, hawezi tena kufikiria mawazo ya kijijini bali anajenga malengo makubwa ya kufika mbali kimaendeleo.

    4. kujitengenezea “CONNECTION” Sambamba na kupata hamasa akiwa mbali na nyumbani kwao, mwanao anapofunza shule anajijengea mahusiano, udugu na marafiki na wale wenzake kutoka sehemu mbalimbali za nchi husika ili kumsaidia siku za mbeleni atapopambania riziki yake.

    Mwandishi alisisitiza kuwa ofisi au mahali ambapo atapokwenda siku a mbeleni atawakuta wenzake walisoma naye darasani na jambo lolote lite litakuwa mezani au litalomsumbua, litatatulia kwa urahisi sana na marafiki wake wa shule walizosomea pamoja.

    5. Mwandishi anatuambia kama wazazi kwamba kamwe tusipojiambia kitu fulani ” HAIWEZEKANI” kwa ajili ya kumtayarisha mwanao na kumkabidhi kuwa urithi wako badala yake tujiulize hivi jambo fulani hili ”

    LITAWEZEKANAJE?”Kama tunajiuliza litawezekanaje, basi akili yetu itaanza kuwaza na kujipangilia namna ya kuyaleta shuluhiso za kuondoa hilo tatizo au changamoto na kulifanyia kazi.

    6. Mwandishi aligundua siri kubwa inawazuia baadhi ya wazazi kutowezesha watoto wao kupata elimu bora ili iwawezeshe watoto kujimudu na kujipambania vyemu dunia, ni gharama kubwa za ada za shule bora.

    Japo kuna hio changamoto ya ada, lakini anatoa baadhi ya mipangilio na biashara mbalimbali ukiwemo zile za kuwekeza kwa muda mrefu wakati mtoto anapokuwa mchanga na hatimaye huo wekezaji hutaweza kumnusuru mzazi na kulipa ada ya mtoto kwa urahisi sana wakati atakapoanza shule.

    Mwandishi wa makala hii ni Dkt. Amos Busingye

    Ambaye ni daktari wa binadamu na mwanzilishi wa Zahanati ya Busingye Clinic iliyo nchini Uganda, unaweza kutembelea blogu yake kupitia

  • Je, wewe utashiriki hii semina ya kipekee?

  • Nguvu ya mwandishi

X