Viashiria kumi na sita (16) Kuwa Umebeba Ajira Za Watu


Rafiki yangu mpendwa salaam, ujue mara kwa mara nimekuwa nakwambia kwamba inawezekana wewe umezaliwa kuajiri na siyo kuajiriwa. Siku ya leo ninaenda kukuonesha viashiria ishirini ambavyo vinaonesha kuwa wewe umebeba ajira za watu.

Baada ya kuwa umesoma hapa sasa, kazi itabaki kwako kuhakikisha umefanyia kazi haya utakayokuwa umejifunza au la

1. Kiashiria cha kwanza kwamba umebea ajira za ni ndoto yako kubwa

Kama una malengo na ndoto kubwa, fahamu wazi kuwa haya malengo na hizi ndoto kubwa unaweza kuzikuza mpaka kufikia hatua ambapo watu watahitajika ili kukusaidia ili kuzifanikisha. Ni ukweli kuwa hakuna ndoto kubwa ambayo unaweza kuifanikisha peke yako. Ndoto kubwa zinahitaji watu pia.  Hivyo, kama una ndoto kubwa hakikisha unazifanyia kazi maana hizi ndizo zitakupelekea wewe kwenye kuajiri wengine.

2. kiashiria cha pili kuwa umebeba ajira za ni kipaji chako

Kiashiria cha pili kuwa umebeba ajira ni kipaji chako. Kama una kipaji ni wazi kuwa hiki kipaji, huwezi kukifanyia kazi peke yako. Unahitaji watu kufanyia kazi kipaji chako na kukifanikisha. Hiki ni kiashiria kingine kuwa inawezekana umebeba ajira za watu.

3. kiashiria cha tatu kuwa umebeba ajira za watu hicho kitu unachopenda kufanya

Kama kuna kitu unachofanya na unaona kwamba unapenda kukifanya hicho kitu, hiki ni kiashiria kingine tosha kwamba inawezekana wewe umebeba ajira za watu. Kwenye hili unaweza kuwa unajiuliza, kivipi? Ngoja nikuelekeze vizuri ili uweze kunielewa. kama unafanya unachopenda maana yake kinaeanda kuwagusa watu wengi. Itafikia hatu ambapo utakuwa na majukumu mengi ambayo utakuwa unapaswa kuyafanyia kazi. Baadhi ya haya majukumu sasa watahitajika watu wa kuyafanya na kuyatekeleza. Na hapo ndipo utakapoajiri!

3. kiashiria cha nne kuwa umebebea ajira za ni changamoto ambazo zinaikumba jamii

Kama kuna changamoto ambazo unaziona kwenye jamii na unaona unaweza kuzitatua, hicho ni kiashiria kwamba umebeba ajira za watu. Unachotakiwa kufanya ni kuchukua hatua na kutatua hizo changamoto unazoona. na hapa siyo tu kwamba unakuwa umebeba ajira za watu, lakini pia unakuwa umebeba suluhisho la matatizo na changamoto kubwa zinazowakumba watu.

4. Kiashiria cha tano kuwa umebeba ajira za watu ni ushauri ambao watu huwa wanakuja kukuomba

Kama kuna watu wanakuja kwako kukuomba ushauri kwenye jambo fulani, fahamu wazi kuwa umebeba ajira zao. Unachotakiw kufanya ni kuhakikisha kwamba unaweka vizuri kile unachojua, ili kiweze kuwasaidia watu katika ngazi kubwa na katika viwango vikubwa. Nimeeleza hili kwa undani zaidi kwenye kitabu cha TENGENEZA FEDHA KWA KUUZA KILE UNACHOJUA.

Unaweza kupata nakala ya hiki kitabu mtandaoni moja kwa moja kupitia HAPA au kwa kuwasiliana nami kwa +255 684 408 755

SOMA ZAIDI: KITABU: TENGENEZA FEDHA KWA KUUZA KILE UNACHOJUA

5. Kiashiria cha Tano ni kuwa na Uwezo wa Kujenga Timu:

Kujenga na kuongoza timu ni sifa muhimu kwa wale wanaotaka kuwaajiri wengine. Watu wenye uwezo wa kufanya kazi na kusimamia wafanyakazi wanaweza kufanikiwa katika kuendesha biashara na kutoa ajira. Hii inamaanisha kwamba kama una uwezo mzuri wa kuwasiliana na kuwasilisha kile ambacho kimoo ndani yako  kwa timu yako, kutoa majukumu yanayoeleweka kwa timu yako, kuwa na namna ya kuifuatilia timu yako na kuifanyia tathmini ili iweze kuzalisha matokeo n.k.

6. Kiashiria cha Sita ni Kuwa na Ujasiri wa Kuchukua Hatari:

Kuna hatua nyingi za hatari ambazo utapaswa kuchukua kwenye maisha yako ya kila siku.kama hiili unaona liko sawa kwako, basi huu ni muda wako wa kujiandaa kuja kuajiri siku moja.

SOMA ZAIDI: Haya Ndio Maneno Yanayotumiwa Na Watu Kujifariji Linapokuja Suala La Pesa

7. Kiashiria cha saba ni uwezo wa Kusimamia Rasilimali:

Hili somo wengi linawapiga chenga. Kusimamia rasilimali kama vile fedha, wafanyakazi, na vifaa ni muhimu katika uendeshaji wa biashara. Watu wenye uwezo wa kusimamia rasilimali hizi wanaweza kuwa na uwezo wa kuajiri na kusimamia wafanyakazi.

8. Kiashiria cha nane ni Kuwa na Mtazamo wa Muda Mrefu:

Biashara siyo kitu cha kufanya ndani ya siku moja. ni kitu cha muda mrefu, hivyo mtazamo wa muda mrefu ni kitu cha muhimu sana hasa tunapoongea biashara.

Jinsi Ya Kubadili Mwelekeo Wa Kile Umachofanya Bila Kuathiri Matokeo (True Story)

9. Kiashiria cha Tisa ni Uwezo wa Kuhamasisha Wengine:

Hiki ni kipengele kingine muhimu sana hasa unapokuwa unafanya kazi na watu. Kuna wakati ambapo utapaswa kuwa mkali, n akuna wakati ambapo utahitaji kuwahamasisha wengine kazi ifanyike. Kuna wakati watu watatakiwa kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi ya ule muda wa kawaida. haya yote utaweza kuyafanikisha kama utakuwa mtu wa kuhamasisha watu na kuwafanya waone maono makubwa ambayo wewe mwenyewe utakuwa unaona.

10. Kiashiria cha kumi ni kuwa na Uwezo wa Kufanya Maamuzi ya Haraka:

Katika biashara, mara nyingi kuna haja ya kufanya maamuzi haraka ili kukabiliana na mabadiliko ya haraka katika soko au mazingira ya biashara. Watu wenye uwezo wa kufanya maamuzi ya haraka na kwa ufasaha wanaweza kufanikiwa katika kuajiri na kusimamia wafanyakazi. na ukweli ni kuwa zipo nyakati nyingi ambazo utatakiwa kufanya maamuzi ya haraka. Ni nyingi zipo mbele yako. Kitu kikubwa unachopaswa kuwa tayari kuzikabili.

SOMA ZAIDI: Mambo Matano Unayopaswa Kufahamu Ili Utengeneze Marafiki Wazuri Na Wa kudumu

11. Kiashiria cha kumi na moja ni kuwa na Uwezo wa Kujifunza na Kubadilika:

Biashara mara nyingi inahusisha kujifunza kutokana na makosa na kubadilika kulingana na mabadiliko katika mazingira ya biashara. Watu wenye uwezo wa kujifunza na kubadilika wanaweza kufanikiwa katika kuendesha biashara na kutoa ajira kwa wengine.

Miaka ya nyuma mtandao wa intaneti ulipoingia mjini ni biashara chache zilikuwa tayari kubadilika na kuukumbatia huu mtandao wa intaneti, leo hii hizi biashara biashara zimeweza kukua sana. Kwa upande mwingine kuna biashar aambazo zilipuuza hii mitandao, nyingine zimetoweka kwenye biashara na nyingine sasa hivi ndio zinajikongoja kuingia kwenye hii mitandao. Ukweli ni kuwa kama mfanyabiashara unapaswa kuwa tayari kujifunza kila maa bila ya kuacha.

Wakati mwingine kujifunza kitu kimoja tu mfano kwenye kitabu unaweza kuwa ni uamuzi wenye busara sana. Hivyo, ni muhimu sana kwako kuhakikisha kwamba unajifunza na unabadilika pale inapohitajika.

Kutana na Mwajiriwa Ambaye Haitaji Mshahara Ila Anafanya Kazi Kwa Bidii. Nakushauri Baada Ya Kusoma Makala Hii Umwajiri Huyu Jamaa. Kitu Kimoja Cha Ziada Ni Kwamba anafanya Kazi saa 24/7

12. Kiashiria cha kumi na mbili kuwa na Uwezo wa Kufanya Kazi Kwa Timu:

Wakati shuleni wengi tunafundishwa kufanya kila kitu peke yako. Kwenye biashara hali ni tofauti, uwezo wa kufanya kazi kwa timu na kushirikiana na wengine ni muhimu katika biashara. Kama una uwezo wa kufanya kazi kwa ushirikiano na kusaidiana na wenzao wanaweza kuwa na uwezo wa kufanikiwa katika kuajiri na kusimamia timu yako.

ACTIVE MODE ACTIVATED

12. Kiashiria cha kumi na mbili ni uwezo wa Kufanya Mawasiliano

Mawasiliano mazuri ni muhimu katika biashara na uongozi. Watu wenye uwezo wa kufanya mawasiliano mazuri na kusikiliza wengine wanaweza kufanikiwa katika kuajiri na kusimamia wafanyakazi\

Njia Tano Za kuwa na Ukuaji Kwenye Maisha, Biashara na Kila kitu unachofanya

13. Kiashiria cha kumi na tatu ni kuwa na Maono ya Ubunifu:

Ubunifu ni muhimu katika kufanikiwa katika biashara. Watu wenye uwezo wa kuona njia mpya za kufanya mambo na kubuni suluhisho mpya wanaweza kuwa na uwezo wa kuajiri na kusimamia wafanyakazi. Kiukweli ubunifu ni m oyo wa biashara na biashara yoyote ambayo haina ubunifu ni suala la muda tu hiyo biashara itatoweka kwenye soko. Unahitaji ubunifu kwenye uzalishaji wa bidhaa, unahitaji ubunifu kwenye kufanya masoko, unahitaji ubunifu kwenye kuuza. Yaani, karibia kila kitu ni ubunifu.

SOMA ZAIDI: JINSI UBUNIFU UNAVYOWEZA KUKUINUA KWENYE BIASHARA

14. Kiashiria cha kumi na nne ni kuwa na Uwezo wa Kufanya Kazi Kwa Bidii:

Biashara mara nyingi inahitaji ufanye kazi kwa bidii. Muda mwingine inahitaji ufanye kazi muda mwingi zaidi ya kawaida, na hata muda mwingine ufanye kazi siku za sikukuu. Mfano Rweyongeza hapa nipo naandika makala hii ikiwa ni siku ya pasaka saa tano asubuhi, muda ambao najua wazi kuwa watu wengine wapo wanakula bata au wanapanga kwenda kula bata.

Jack Ma kuna siku aliwahi kusema kwamba wakati mwingine unahitaji kufanya kazi kwa takribani saa 16-18 kwa siku. Hii yote ni kwa ajili ya biashara yako. Kama unaona hizi gharama unaweza kuzilipa, inawezekana siku siyo nyingi utahitajika kuajiri na utakuwa boss kwenye biashara yako. Jiandae sasa.

SOMA ZAIDI: Gharama Sita Unazopaswa kulipa ili kufikia ndoto zako.

15. Kiashiria cha kumi na tano kufanya Maamuzi Yasiyoepukika

Mara nyingine katika biashara, kunahitaji kufanya maamuzi ambayo siyo rahisi na hata wewe mwenyewe yanakuogopesha. Kwa lugha nyigine, haya ni maamuzi magumu.

wakati mwingine unaweza kufanya maamuzi kama haya, ila yakawa siyo maamuzi maarufu, watu kwenye timu yako wakayapinga, kwa sababu hawaoni kule unapoona wewe. sasa unahitaji kuwa mtu wa kufanya maamuzi na kuyasimamia. Watu wenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu na kusimamia matokeo yake wanaweza kufanikiwa katika kuajiri na kusimamia wafanyakazi.

SOMA ZAIDI: KONA YA SONGA MBELE; Jinsi Ya Kuongeza Ufanisi Kazini

16. Kiashiria cha kumi na sita ni uwezo wa Kusimamia Muda:

kWENYE biashara muda ni kitu chenye thamani kubwa sana. Kama mfanyabiashara hauna muda wa kutosha wa kufanya kile kitu. Kama mfanyabiashar aunapaswa kuhakikish kwamba umewekeza muda wako na unautumia vyema kabisa bila ya kuupoteza.

Usimamizi wa muda ni muhimu katika biashara na uongozi. Watu wenye uwezo wa kusimamia muda wao na wa wafanyakazi wao vizuri wanaweza kufanikiwa kwenye biashara

SOMA ZAIDI: Wafanyabiashara Waliofanikiwa Wanavyotunza Muda


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X