Home


  • Kitu Chenye Thamani Unachopaswa Kuwa Nacho Kuanzia Leo Hii

    Rafiki yangu ili uweze kuishi vizuri kwenye dunia ya sasa. Ni vizuri sana ukihakikisha kwamba una ujuzi wa kufanya jambo au kitu fulani.

    Hiki ni kitu ambacho wewe mwenyewe unaweza kujenga. Ujuzi wako unaweza kukutambulisha popote na kwa yeyote. Ujuzi wako unaweza kukulipa.

    Kama hauna ujuzi ni muda wako sasa wa kuhakikisha kwamba unaanza kujenga ujuzi. Badala ya wewe kupoteza muda kwenye mitandao ya kijamii ukiangakia vitu ambavyo havina manufaa, utumie muda huohuo kuhakikisha kwamba unajenga ujuzi wako.

    Utakuwa hujitendei haki kama unalalamika Kuwa maisha Ni magumu. Vyuma vimekaza halafu baada ya hapo unapoteza muda kwenye mitandao ya kijamii au kwenye vijiwe ukipiga stori. Badala ya kujenga ujuzi ambao utakulipa zaidi.

    Ubora wa ujuzi ni kwamba ukishakuwa nao unakuwa nao. Hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kuuiba kwako.

    Hivyo basi rafiki yangu, kuanzia sasa chagua aina ya ujuzi ambao unaweza kujenga. Kwenye kitabu changu cha NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA nimeeleza Aina 21 za ujuzi ambazo unaweza Kuwa nazo. Simaanishi kwaamba unapaswa Kuwa na Aina zote. Hapana.

    Badala yake unapaswa kuchagua Aina moja tu ya ujuzi na kukomaa na huo kwanza.

    Baadhi ya ujuzi unaoweza Kuwa nao ni Kama
    1. Kuchora
    2. Kuandika
    3. Kuongea na kuwasilisha mada watu wakakusikiliza (uneni)
    4. Graphics
    5. Kuuza

    Zipo Aina nyingi za ujuzi, Ila ujumbe wangu kwa leo ni kwamba chagua Aina moja tu ya ujuzi na hakikisha kwamba unakomaa na hiyo Aina ya ujuzi bila ya kurudi nyuma.

    Kila la kheri.

  • Kama Unatumia Nguvu Kubwa Kujitambulisha…

    Kama unatumia nguvu kubwa  kujitambulisha jua bado unapaswa kuweka nguvu kubwa kwenye kufanya kazi kwa bidii pia.

    Unajua kwa nini? Kwa sababu watu hawakujui.

    Pata picha Sasa hivi umepigiwa simu na
    Samia Suluhu Hassan
    Vile tu akijitambulisha kwako, hutahitaji KUANZA KUMWULIZA maswali mawili au matatu. Utakachofanya utaanza kumsikiliza anataka kusemaje?

    Lakinj he, vipi wewe kwa upande wako. Ukimpigia mtu mgeni ambaye hana namba Yako inakuwaje? Atakufahanu? Atasema ndio nakufahamu .. na KUANZA kukusikiliza unasemaje au utaanza kujitambukisha Mara tatu, tatu.

    Ukiona unatumia nguvu kubwa kujitambulisha, basi jua kazi unayo.
    Bado unapaswa kufanya kazi kwa bidii. Tena kwa bidii sana.

    Sasa kazi yako ya leo. Chukua namba kumi ngeni ambazo hujawahi kuzipigia. Watu ambao hawakujui.
    Wapigie simu.
    Je, unajitambulisha kilaini? Wanaelewa jina lako? Je, ulipowaambia bidhaa yako wameitambua haraka? Unaweza kufanya hivyo kwa watu wengine 100 nao wakakutambua wewe na bidhaa yako mapema.

    Kama siyo kaongeze bidii kwenye kazi.

    Imeandikwa na
    Godius Rweyongeza
    www.songambele.co.tz
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • Tofauti Kati ya wale wanaofanya makubwa na wale wanaofanya vitu vya kawaida

    Kwenye kitabu cha 10X Rule Grant Cardone,  anasema kwamba tofauti pekee Kati ya wale watu wanaofanya makubwa na wale wanaofanya mambo ya kawaida imelala kwwnye  kanuni ya mara kumi zaidi.

    Kadiri ya kanuni hii Ni kwamba kama unataka kupata matokeo makubwa zaidi ya unavyopata sasa hivi, sharti uwe tayari kufanya vitu mara kumi zaidi ya unavyofanya sasa hivi.

    Unapaswa KUANZA kwa kuweka malengo MAKUBWA mara kumi zaidi.
    Unapaswa kuchukua hatua mara kumi zaidi.
    Unapaswa kwenda hatua ya ziada mara kumi zaidi.
    Kiufupi kwenye maisha yako unapaswa kuwa MTU wa mara kumi zaidi ili uweze kupata Yale unayotaka.

    Hivyo ndivyo unapaswa kuishi kwenye maisha yako.

    Unaweza usinielewe vizuri sana ninapokwambia kanuni ya mara kumi zaidi. Ila ngoja nikueleweshe kwa undani ZAIDI. Tuchukulie wewe ni mwanachuo. Unasoma chuo AA

    Na kuna notsi ambazo profesa alitoa Ila Sasa kwa bahati mbaya hizo notes umezipoteza.
    Ila unajua marafiki zako wanazo. Ila kwa bahati mbaya, unazihitaji hizi notes SAA tano usiku na marafiki zako wamelalala tayari. Sasa inafanyaje?

    Unaweza kuamua kumtumia Innocent ujumbe ili akutumie hizo notes halafu ukatulia. Japo utakuwa umefanya uamuzi mzuri wa kuomba notsi kwa Innocent. Ila inawezekana Innocent asiingie hewani usiku huo au hata akawa mbali na simu. Au akaona ujumbe wako Ila akaaanza kufanya Mambo mengine mpaka akasahau kukutumia notsi.
    Au hata akaona ujumbe wako Ila akawa Hana kifurushi Cha kukutumia hizo notsi.

    Hivyo, kama upo makini utatumia kanuni ya Mara kumi zaidi kuomba notsi.
    Utatuma kwa ujumbe wa kuomba notsi hizo kwa
    Innocent
    Janet
    Jeni
    Said
    Abdallah
    Joseph
    Ashura
    ……..yaani, kiufupi utatuma kwa watu wasiopungua kumi.

    Nakuhakikishia siyo wote watakujibu kwa wakati.
    Siyo wote watakutumia hizi notsi
    Na wengine wanaweza hata wasiwe nazo Kama wewe.
    Wengine watakuwa wanazitafuta Kama wewe
    Na wengine wataona Ila watasahau kukutumia.
    Ila hatakosa mmoja au wawili au watatu wa kukutumia notsi zako.

    Kwa jinsi hiyo, notsi zako utakuwa umezipata.

    Sasa huu mfano unafanya kazi kwenye vitu vingine kwenye maisha. Mara zote fikiri Mara kumi zaidi.
    Chukua hatua Mara kumi zaidi.
    Piga simu kwa wateja mara kumi zaidi
    Kutana na wateja Mara kumi zaidi
    Weka LENGO la kuuza Mara kumi zaidi.
    Soma vitabu Mara kumi zaidi ya wengine
    FANYA mazoezi Mara kumi zaidi

    Hii inakuweka kwenye eneo zuri Sana kuliko MTU ambaye anakuwa anafanya vitu kwa namna ya kawaida.
    Usiwe mtu wa kawaida. FANYA kazi Mara kumi zaidi

    Kila la kheri

  • Hii Ni Sanaa Unayopaswa Kuitumia Kila Siku Kwenye Maisha Yako

    Rafiki yangu, nipe dakika moja tu nikufundishe Sanaa unayopaswa kuitumia kwenye maisha Yako kuanzia leo hii.

    Wakati tunasoma Sekondari tulikuwa tunasikia stori kuwa masomo ya sayansi yanalipa sana. Hivyo, NGUVU kubwa tukaiweka huko

    Nilipoingia chuoni, ni kozi ya horticulture. Hapa kitu Cha kwanza kabisa unachofundishwa, unaambiwa kuwa horticulture is an art and sayansi. Halafu kumbe siyo sayansi ni science kwa kiingereza. Hahaha.

    Hii maana yake ni kwamba horticulture Ni Sanaa, lakini pia ni sayansi. Hapa ndipo nilianza kuuona umuhimu wa sanaa kwenye maisha. Maisha yanahitahi vyote viwili. Maisha yanahitaji sayansi na sanaa. Na vyote viwili tunavitumia kila siku bila kujali chuo ulisoma nini nala hukusoma Nini. Iwe ulikuwa mkali Sana kwenye fizikia kama Einstein, au ilikuwa MTU wa kawaida. Bado utaihitaji Sanaa. Na hata Kama ilikuwa hupendi sayansi kiasi ulikuwa unailaani, kwenye maisha ya kila siku, unaihitaji. Hivyo, vyote viwili tunavihitaji. Na kwa Leo nataka nikufundishe Sanaa moja Itakayokusaidia wewe Kufanikisha mengi

    Na Sanaa hii siyo nyingine, bali Ni kusikiliza.

    kusikiliza ni sanaa ambayo itakufikisha mbali Sana.

    Watu wanapenda kusikilizwa aisee. Naomba kwanza nieleweke kwamba Kuna TOFAUTI kubwa Kati ya kusikia na kusikiliza.

    Unaweza kumsikia MTU  ila ukawa hujamsikiliza. Kama MTU amewahi kuongea Jambo na ukawa umemwambia arudie japo alikuwa ameongea kwa sauti. Hapo jua wazi kuwa hukumsikiliza.

    Kumsikiliza MTU kunahitaji uweke umakini wake wote kwake

    Kuna watu unakuta kwamba hawana shida Wala tatizo lolote, wao wanachohitaji kwako ni kuwasikiliza na kuwapa umakini wako. Hivyo basi rafiki yangu, ninaomba kitu kimoja kwako kuwa msikilizaji.

    Yaani, unapokuwa unaongea na MTU, NGUVU zako na Akili Yako yote iweke kwake badala ya kutawanya nguvu zako.

    Inalipa sana kusikiliza.

  • Kama Kuna Kitu Unataka Kufanya Kifanye

    Badala ya kukaa na kusubiri MTU au watu fulani waje wakusaidie kufanya na kukamilisha kitu au jambo fulani, nakushauri kwamba Kama Kuna Kitu unataka kufanya. Kifanye. Ukiendelea kumsubiri mtu au watu fulani waje wakusaidie kukifanya ukweli Ni kwamba utasubiri sana na hawa watu unaweza usije kuwaona maisha yako yote.

    Kwenye hii dunia kuna watu wa aina tatu.
    Kuna wale ambao huwa wanatamani vitu, Ila huwa hawachukui hatua na kuvifanya.

    Kuna wale ambao huwa wanaona vitu vinafanyika na kuishia kuangalia na namna vinavyofanyika

    Mwisho Ni wale wanaochukua hatua kuhakikisha kwamba wamefanyia kazi vile wanavyotamani kufanya.
    Wewe unapaswa kuwa kwenye Aina ya tatu.
    Hawa ndio wale watu ambao huwa wakiamua jambo huwa wanalifanya bila kusita.
    Hawa ndio wale watu ambao huwa wapo tayari kuweka kazi inapohitajika ili waweze kupata matokeo wanayotaka.

    Dunia imekuwa hivi ilivyo Leo hii kwa sababu ya watu wanaochukua hatua.
    Leo hii naandika makala hii kwa kutumia simu simu ambayo imetengenezwa na watu wanaochukua hatua. Leo hii napanda gari lililotengenezwa na watu wanaochukua hatua.
    Hata Kama ukisikiliza muziki jua kuwa umetengenezwa na watu wanaochukua hatua.
    Kama unapendelea kuangalia tamthiliya, jua wazi kuwa zimetengenezwa na watu wanaochukua hatua.
    Na wewe kuwa tayari kuchukua hatua.
    Hakuna namna ambavyo unaweza kupata matokeo ya tofauti kama hutachukua hatua.

    Kama Kuna kitu ungependa kufanya Leo hii, Basi uchukue hatua na uanze kukifanya rafiki yangu.

    Naomba siku ya leo tukubaliane kitu kimoja tu. Na kitu hiki Ni wewe kufanya kile unachotamani kufanya bila kurudi nyuma kuanzia leo hii.

  • Hii Ndio Njia Pekee Ya Kuhakikisha Kwamba Unapata Upendeleo Popote Pale Utakapoenda

    Hii ndio njia pekee ya kuhakikisha kwamba unapata upendeleo popote pale utakapoenda

    Sisi binadamu huwa tunapenda sana kuonekana mbele ya watu kama watu wa thamani sana. Tunataka tukikuta sehemu fulani tusianze kupanga foleni, badala yake tupite kwenye hiyo foleni na kuhudumiwa.

    Tunapenda tukiwa kazini tupandishwe vyeo.

    Tunapenda tukiwa kwenye foleni, gari letu lipishwe lipite haraka ili tuwahi kufika.

    Sasa siku ya leo nataka nikuoneshe namna ambavyo unaweza kupata upendeleo sehemu yoyote ile utakapokuwa.

    Ndio namaanisha hilo.

    Na njia hii ya kupata upendeleo ni wewe kufanya kazi kwa bidii. Rafiki kufanya kazi kwa bidii kutakufanya upendelewe sehemu yoyote ile utakapoenda. Hakuna mwajiri ambaye huwa anapenda kukaa na wafanyakazi wazembe. Ila ukifanya kazi kwa bidii, mwajiri wako atakupendelea.

    Hakuna mtu ambaye yuko makini ambaye anapenda kukaa na watu wanazembea kwenye kazi zao.

    Hivyo basi, kuanzia leo hii, uamuzi wako uwe mmoja tu, kufanya kazi kwa bidii.

    Kufanya kazi kwa bidii kunaweza kukufanya ukae meza moja na wafalme. Na kwa jinsi hiyo utakuwa umesababisha watu wakupendelee.

    Kufanya kazi kwa bidii kuutakufanya ulipwe zaidi. hivyo, kwa jinsi hiyo, utakuwa umejipendelea.

    Kumbe basi kufanya kazi kwa bidii ni kujipendelea mwenyewe. Maana kabla mtu hajaona juhudi zako na kuzipia zawadi atahitaji kuona utendaji kazi wako.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

  • Jinsi Ya Kubobea Kwenye Kitu Chochote

    Rafiki yangu habari ya leo. Bila shaka unaendelea vyama, siku ya leo ningependa kukwambia njia ambayo itakusidia wewe kuweza kubobea kwenye kitu chochote ambacho unafanya, na njia hii siyo nyingine bali ni kufanya kitu husika kwa marudio na mara kwa mara.

    Yaani, kama unataka kubobea kwenye kitu chochote kile usikifanye kitu  hicho mara moja kisha ukaacha, badala yake weka nguvu na muda wako mwingi kwenye hicho kitu kwa muda mrefu mpaka kieleweke.

    Watu wengi huwa wanapenda kubobea kwenye vitu ila sasa tatizo ni kwamba huwa wanajikuta kwamba wanafanya vitu vingi sana kwa wakati mmoja. Yaani, unakuta kwamba mtu anafanya kitu fulani siku ya leo. Halafu kesho yake hicho kitu anakisahau, kesho anapambana na kitu kingine, hivyo hivyo.

    Wewe unayesoma hapa nakupa mbinu ya kubobea kwenye kitu chochote kile. Na mbinu hii ya kubobea ni wewe kufanya kitu hicho kila mara bila kuacha.

    Tatizo la watu wengi wanafanya vitu vizuri kwa mazoea

    Ninaposema kwamba ufanye kitu kila mara, simaanishi kwamba ufanye kitu hicho kwa mazoea. Kuna tofauti kati ya kufanya hicho kitu kila siku na kwa moyo na kufanya kitu hicho kila siku kwa mazoea. Kuna stori ya mfanyakazi mmoja ambaye alienda kuomba kuongezea mshahara kwa bosi wake. Baada ya kupitia maombi yake, bosi alimwambia kwamba, hawezi kuwmongezea mshahara kwa sababu  huwa anafanya kazi siku moja kwa mazoea au kwa marudio. Yaaani, kwamba huyo mfanyakazi, alikuwa kila siku anaenda kazini kweli, ila hakukuwa na kitu cha tofauti ambacho alikuwa anafanya.

    Alikuwa anaenda kazini ili kupoteza muda. Nadhani umewahi kuwasikia wale watu ambao huwa wanasema kwamba ninapoteza muda tu. Kwako haipaswi kuwa hivi, yaani, usifanye kazi au kitu chochote kile kwa ajili ya kupoteza muda tu. Mara zote na siku zote hakikisha kwamba kila siku yako inakuwa ni bora zaidi ya jana. Yaani, usiweke mazoea kwenye kazi.

    Kila dakika ambayo unafanya kazi, weka nguvu, akili yako na kila kitu humo.

    Ebu tuchukulie mfano unataka kubobea kwenye uandishi.

    Unahitaji kuhakikisha kwamba unafanya mazoezi kila siku. Yaani, unapaswa kuandika kila siku. Huwezi kukaa tu kwenye kochi huku ukiw aunategemea kwamba siku moja utakuwaj akuwa mwandishi mbobevu bila ya kuchukua hatu aya ziada. Unataka kubobea kwenye uandishi kuanzia siku ya leo? Anza kuandika.

    Au labda tuseme kwamba unataka kubobea kwenye uwekezaji, unapaswa kuhakikisha kwamba unawekeza nguvu na muda wako kwenye kujifunza uwekezaji na kufanyia kazi yale unayojifunza kwa uhalisia.

    Unataka kubobea kwenye mchezo wowote. Unapatakiwa kila siku kufanya mazoezi ya kutosha kuhusiana na mchezo husika.

    Kwa jinsi hiyo rafiki yangu, utakuwa umejiweka kwenye nafasi ya kufanya makubwa na kwenda mbali zaidi kuliko pale ambapo utakuwa hufanyii kazi haya utakayojifunza.

    Kuna siku nilikuwa nasoma wasifu wa Kobe Bryant, kitu kikubwa nilichokuja kugundua kutoka kwake ni kwamba alikuwa mtu wa mazoezi na mazoezi ndiyo yalimfanya kuweza kufikia alipofikia. Nahakufanya hicho mara moja. bali alikifanya mara kwa mara mpaka akaweza kupata matokeo makubwa.

    Hivyo basi, nipende kusisitiza ujumbe muhimu kwako rafiki yangu ambaye unapenda kufika mbali. Kitu hiki kwamba kama unataka kubobea kwenye kitu chochote kile basi kuwa tayari kufanya kitu hicho mara kwa mara na marudio bila ya kuacha mpaka pale utakapopata matokeo unayotaka.

    Asante sana na nikutakie wakati mwema.

  • Vitu Vitano Vinavyotofautisha watu wanaopata mafanikio ya kawaida na mafanikio makubwa

    Watu wawili, wanaweza kuzaliwa na wazazi walewale, wakapata elimu ileile, chini ya walimu walewale. Na kwenye mazingira yaleyale. Ila mmoja akatokea kuwa mwenye mafanikio makubwa sana, huku mwingine akiwa na mafanikio ya kawaida sana au hata pengine kuishia kwenye umasikini. Unajua kwa nini kitu kama hiki kinatokea.

    Kwenye makala hii ya siku yaleo ninaenda kukuonesha kwa nini hili huwa linatokea na kitu gani hasa ambacho unaweza kufanya ili uweze kuwa na mafanikio makubwa. Au mafanikio ambayo wengine wanaona kama vile siyo mafanikio ya kawaida.

    Lakini kabla sijakwambia kitu kama hiki ningependa ufahamu stori moja ambayo kiuhalisia ipo kwenye maisha ya kila siku. Vijana wawili walizaliwa na baba mmoja ambaye alikuwa mlevi. Kipindi chote wanakua watoto wale, kitu kikubwa sana walichokuwa wanaona kwa mzazi wao, yaani, baba yao, kilikuwa ni kulewa. Kwa hiyo, hiki kitu kiliwafanya wawe na mtazamo tofauti kuhusu maisha.

    Kijana mmoja alipokua. Alianza kulewa.

    Huku kijana mwingine alipokua alikuwa mfanyabiashara.

    Wandishi wa habari siku moja walikuwa na shauku ya kutaka kujua kwa nini mapacha wawili wawe na maisha ya tofauti kiasi hicho.

    Mwandishi wa habari alimfuata kijana wa kwanza ambaye alikuwa ni mlevi na kutaka kujua kwa nini alikuwa mlevi. na kwa nini alilewa kila siku.

    Yule mlevi alijibu kwa kusema kwamba nilijifunza kwa baba yangu.

    Mwandishi wa habari alimfuata kijana mwingine ambaye alikuwa ni mfanyabiashara na kumwuliza kwa nini alikuwa mfanyabiashara, na yule alijibu kwa kusema kwamba nilijifunza kwa baba yangu,

    Yaani, vijana wote wawili walijifunza kwa baba yao. Yule mlevi alichoona kwa baba yake ulikuwa ulevi, hivyo, aliishia kulewa.

    Yule mfanyabiahsara aliona namna ambavyo baba yale alikuw anatumia fedha zake hovyo hovyo kwenye mambo ambayo hayakuwa ya msingi. Aliona jinsi ambavyo wafanyabishara walikuwa wanakusanya pesa kutoka kwa baba yake na walevi wengine kila siku katika vinywaji, mishikaki na vinginevyo vingi. Hivyo, akaona kwamba ukiwa mfanyabiashara basi unakuwa unakusanya pesa kutoka kwa watu.

    Alijiambia kwamba, kuna watu wanapenda kutumia hela zao na kuwapa wengine. Ila hawawezi kukupa hiyo pesa kama wewe mwenyewe huna cha kuwapa. Na utapata cha kuwapa kupitia biashara, hivyo, kwa namna hiyo, akawa ameamua kuwa na biashara.

    Hiki kitu kilimsukuma kufanya makubwa na kujituma zaidi kwenye kazi zake na hivyo kuwa mfanyabishara mkubwa wa nyakati zake.

    Kitu kama hiki pia unawez akukiona kwa watu wengi ambao unakutana nao kila siku. Kuna watu wengi wanaiga maisha na kuishi maisha ambayo siyo ya kwao kwa lengo la kutaka kuonekana au kuwa na maisha ya aina fulani. Wengine wanaiga kwa kujua hukau wengine wakiwa wanaiga kwa kutokujua.

    Na hivyo kitu cha kwanza kabisa kinachofanya watu wafanikiwe na kuwa na maisha bora ni watu ambao wanawatazama. Kwa kiingereza hawa watu wanajulikana kama mentors au role models.

    Hwa ni watu ambao unakuwa unawatazama na kujifunz kutoka kwao.

    Kama unataka kufanikiwa na kufanya makubwa zaidi. hakikisha kwamba unatafuta mentors au role models ambao utajifunza mazuri kutoka kwako. Hkauna role model hata mmoja ambaye anaweza kuwa amekamilika kwa asilimia 100. Ila kwa kila mtu hata kama hafanyi vizuri, bado unaweza kujifunza kitu ambacho kinaweza kukusaidia wewe kupiga hatu akwenye safari yako ya mafanikio.

    Mfano kwa mtu ambaye hajafanikiwa, unaweza kujifunza vitu ambavyo vimemfanya kutofanikiwa na kuvipeuka ili ufanikiwe.

    Kwa mtu ambaye hana akiba, unaweza kujifunza namna ya kuweka akiba na kuiweka ili ufanikiwe.

    Kwa mtu ambaye hana mahusiano mazuri unaweza kujifunza vitu ambavyo anakosea ili uboreshe mahusiano yako.

    Hivyo hivyo kwa watu ambao wamefanikiwa. Kwa hawa watu unaweza kujifunza vitu ambavyo vinawafanya wafanikiwe mpaka kufikia walipo na hivyo kukuwezesha wewe kupiga hatu akubwa sana.

    Kitu cha pili kinachowatofautisha wale wanaofanikiwa sana na wale wenye mafanikio ya kawaida ni kwenye kuchapa kazi. Ujue nguvu ambazo mtu unaweka kwenye kazi ni zilezile. bila kujali kwamba unapata mafanikio kidogo au unapata mafanikio makubwa. Sasa kama nguvu ni zilezile kwa nini usiweke nguvu kubwa kuhakikisha kwamba unapata matokeo makubwa mara zote.

    Mtu ambaye ana lengo la kawaida atapata matokeo ya kawaida kwa kutumia nguvu ileile ambayo mtu mwenye lengo kubwa analo. na mwenye lengo kubwa atapata matokeo makubwa kulingana na lengo lake.

    Na hiki kitu kinanileta kwenye kitu cha tatu kinachowatofautisha watu wa kawaida na wale ambao wanakuwa na amfanikio makubwa. Kitu hiki ni kuwa na malengo. Na watu wanaopata mafanikio ya kawaida siyo tu kwamba wanakuwa na malengo, bali wanakuwa na malengo ambayo wanayafanyia kazi na kuhakikisha kwamba hayo malengo yamekuja kwenye uhalisia.

    Sasa wewe unayo malengo rafiki yangu?

    Kama hauna malengo, hakikisha kwamba siku ya leo unakaa chini na kuandika malengo yako. kabisa, yaandike malengo yako rafiki yangu ili yaweze kuja kwenye uhalisia.

    Malengo ambayo hayajaandikwa rafiki yangu ni kazi bure. Yaandike malengo yako, na kila siku yarudie malengo yako kwa kujikumbusha.

    Hiki kitu ndicho kinaleta kwenye jambo letu la nne kwa siku ya leo ambalo ni kujikumbusha malengo yako. Utafiti ambao ulifanyika, ulionesha kwamba mabilionea wanajikumbusha malengo yao, siyo chni ya mara 29 kila siku. Yaani, hawa hawamezwi na kitu kingine chochote kile isipokuwa tu malengo yao.

    Vitu vingine vyote wameweka chini, wanachopambana nacho ni malengo yao. Hawajikumbushi kwamba kuna msanii katoa wimbo mpya. hawajikumbushi kwamba kuna watu wanapendana na siku ya vlentine wametokaje. wanajikumbusha malengo yao rafiki yangu.

    Na siyo tu kijikumbusha malengo yao kwa maneno bila kutimiza wajibu, bali kwa vitendo pia. hiki kitu kinanileta kwenye pointi ya tano na ya mwisho kwa siku ya leo ambayo ni vitendo. Yaani, kufanyia kazi vile vitu ambavyo unapaswa kufanyia kwa vitendo. Haitoshi tu kuwa role model mzuri, haitoshi tu kuwa na malengo, haitoshi u kujikumbusha malengo yako hata mara 100 kila siku. Vitendo rafiki yangu. Yaani, kufanyia kazi kile ambacho unajifunza na kuhakikisha kwamba kimekuja kwenye uhalisia. hiki ni kitu muhimu kwako na unapaswa kuwa unakifanyia kazi kila siku.

    Panga, ila fanyia kazi pia kile ulichopanga.

    mipango bila vitendo ni kazi bure.

    Kwa hiyo rfiki yangu, kafanyie kazi haya uliyojifunza hapa kwa vitendo.

  • Inawezekana kuondokana na madeni..

    Madeni ni moja ya kitu ambacho kinawasumbua watu wengi na hivyo kuwafanya washindwe kuwa na uhuru lakini hapohapo kuwanyima mwanya wa kuufikia uhuru wa kifedha. Sasa ukweli ni kwamba, inawezekana wewe hapo kuufikia uhuru wa kifedha na kuondokana na madeni.

    Vifuatavyo ni vitu muhimu vya kufanya ili uweze kuondokana na madeni.

    Kwanza orodhesha madeni yako yote. Makubwa kwa madogo. Yaorodheshe hata kama ni mengi. Hata kama Kuna mtu ulishapanga kumdhurumu mweke kwenye hii orodha.

    Pili, tenga asilimia 20 kutoka kwenye kila fedha unayopata kwa ajili ya kulipa madeni. Wakati huohuo usisahau kuweka akiba asilimia 10 tu. Hiyo asilimia 70 iliyobaki ndiyo unapaswa kutumia.  Kwa kipindi hiki unapaswa kupunguza matumizi yako yote makubwa na kubaki na matumizi yale ya lazima tu (Yale ambayo endapo hutayafanya utakufa). Jipange kuachana na anasa katika kipindi hiki hapa.

    Tatu, pangilia namna ya kuwalipa wadeni wako wote. Unaweza kuanza kuwalipa watu wanaokudai fedha kidogo, kisha ukaenda kuwalipa wale wanaokudai fedha nyingi. Au unaweza kuanza ma fedha nyingi ukamalizia na wa kidogo japo ukianza na wale wenye madeni kidogo inakupa hamasa ya kuedelea kwa kuwa unakuwa unapunguza orodha ndefu ya wanaokudai na kubaki na watu kidogo. Pia kama Kuna wadeni wasumbufu Basi unaweza kuanza kuwalipa hao ili waache kukusumbua

    Nne, Kila unapomaliza kumlipa mtu mfute kwenye daftari au karatasi yako  ili wabaki wale ambao ulikuwa hujawalipa tu. Hii itakupa hamasa ya kusonga mbele.

    Tano, weka mkakati wa kuongeza kipato chako. Kinachofanya watu wengi waingie kwenye madeni ni kwa sababu kipato hakikidhi mahitaji. Au wengine ni kwa sababu wanapenda vitu vizuri kama gari, nyumba n.k. ila hawana fedha ya kuvilipia. Sasa unapaswa kuweka mpango wa kuongeza kipato chako ili kuondokana na madeni kabisa. Njia ya wewe kuongeza kipato chako ni kuanzisha walau kibiashara kitakachoanza kukuingizia kipato hata kama ni kidogo.

    Sita, katika kipindi hiki ni marufuku kukopa tena. Jikite katika lengo lako na kuondokana na madeni hata kama litachukua muda mrefu kulitimiza.

    Kila la kheri

    [youtube https://www.youtube.com/watch?v=pt2EHXylCWQ]

  • Ni muda upi mzuri kuanzisha bishara

    Rafiki yangu, unaweza kuwa unajiuliza hivi ni muda upi mzuri kwangu kuweza kuanzisha biashara? Rafiki yangu hili swali limekaa kimtego sana.

    Kuna watu ambao huwa wanaanza kufanya utafiti kuhusiana na biashara ambayo wanataka kufanya, ila huo utafiti wao huwa haufiki mwisho.

    Kuna watu ambao kila mwaka huwa wanajiambia kwamba wataanza biashara ila huwa hawaanzi, mwaka huwa unaisha na tena mwaka mwingine huwa wanasema kwamba nitaanzisha biashara mwakani. Rafiki yangu, pengine tujiulize hivi muda upi ni mzuri kwako kuanzisha biashara?

    Wengine huwa wanasema kwamba wanatafuta mtaji. Yaani, kwamba wakishapata mtaji basi moja kwa moja wataweza kuanzisha biashara bila kuchelewa. Na pengine huwa wanaingia kwenye ajira ili waweze kupata mtaji. Ila cha kushangaza ni kwamba miaka huwa inazidi kupita wakiwa bado hawajaanzisha hizo biashara, kumbe, kuajiriwa kwa ajili ya kutafuta mtaji, linaweza kuwa ni wazo zuri sana, na wakati huo huo, linaweza lisiwe wazo zuri sana.

    Sasa ni muda gani mzuri wa wewe kuanzisha biashara. Kwa mfano, ukikutana na mimi na kuniuliza swali la aina hii, nitakwambia kwamba anzisha biashara sasa hivi. Ndio sasa hivi. hata kama huna mtaji. Hata kama huna mtaji mkubwa

    Hata kama umeajiriwa. Hata kama unasoma. Wewe anzisha biashara sasa hivi, kisha kutokea hapo sasa ndio uendelee kubore

    Lakini kitu kikubwa ni kwamba, ukianzisha biashara inakuweka kwenye mwendo. Unakuwa umejinodoa kwenye ile hali ya utulivu. Yaani, ile hali ya kuendelea kusubiri. Mtu ambaye anasubiri kwamba siku moja atakuja kuanzisha bishara, kuna uwekano mkubwa akwamba huyu mtu hatakuja kuanzisha biasharamaisha yake yote.

    Unajiuliza kwa nini?

    Ngoja nikujibu sasa,

    Kadiri ya sheria ya Netwton. Anasema kwamba kitu chochote kile ambacho kimetulia au kimekaa kwenye utulivu, kitaendelea kukaa hivyohivyo mpaka pale nguvu ya ziada itakapotokea. Na kitu kilicho kwenye mwendo kitaendelea kuwa kwenye mwendo mpaka pale nguvu ya ziada itakapotokea kukizuia.

    Sasa wewe unapoanzisha bashara, unajiweka kwenye mwendo. Unaanza

    Kuna mengi ambayo utajifunza ukiwa kwenye mwendo, kuliko pale ambapo unakuwa haupo kwenye mwendo.

    Kuna mengi utajifunza ukiwa na biashara kuliko pale ambapo unakuwa hauna biashara. Ndio maana unahitaji uanzishe biashara yako rafiki yangu. siyo hilo tu, ngoja tuendelee kuona hili

    Ukianzisha biashara katika hizo nyakati ambazo pengine kwa upande wako unahisi kwamba haupaswi kuanzisha biashara, na hiyo biashara ukaweza kuisimamisha mpaka ikaweza kuwa biashara bora. Ni ukweli usiopingika kuwa lazima utakuja kuwa shujaa kwenye maisha yako.

    Kuna watu watataka kujifunza kutoka kwako kuhusiana na namna ya kuanzisha biashara na kuziendesha katika namna kama hiyo. na wewe utaweza kuwapa ushauri mzuri bila shida yoyote ile.

    Rafiki yangu, nadhani siku ya leo uondoke na kitu kimoja tu. KUANZISHA BIASHARA.

    Kama umekubaliana na mimi kwenye hili. Njoo whatsap sasa hivi, nitumie ujumbe unaoonesha kwamba biashara utakayoenda kuanzisha ili tuweze kushauriana.

    Lakini pia hakikisha umepata mwongozo ambao watu wengi wanaoanzisha biashara wameutumia kwa manufaa makubwa sana. Na mwongozo huu siyo mwingine bali kutoka kwenye kitabu cha MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA B ISHARA. Watu wengi waliosoma hiki kitabu wamethibitisha kuwa hiki ni moja ya kitabu chao bora sana kwao kuwahi kusoma. Ningependa na wewe uweze kupata nakala yako bila ya kuchelewa rafiki yangu.

    Hardcopy ya kitabu hiki ni 20,0000/- na SOfrtcopu ni 10,000/- tu karibu sana rafiki yangu.

    Ni kitabu kizuri sana, ambacho watu wengi waliokisoma wamekipenda sana. Lipia kitabu hiki sasa kwa 0755848391 jinan i GODIUS RWEYONGEZA

    kUMBUKA. Kama unataka kuanzisha biashara ambayo itafika mbali. basi hiki kitbu ndio mwongozo wako ambao unapaswa kuhakikisha umeupata. Gharama ya mwongozo huu ni 20,000 kwa hardcopy na 10,000/- kwa soft copy.

    Karibu sana.

X