Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Ni marufuku kwako kutumia hii kauli kuanzia leo hii

    Moja ya kauli ambayo watu wamekuwa wanapenda kutumia ni kauli ya ninapoteza muda. Mtu anapotumia kauli hii maana yake hana kitu chochote cha maana cha kufanya kwa sasa, hivyo, kitu pekee anachoweza kufanya ni kupoteza muda.

    Hivi kweli rafiki yangu, unaweza kukosa kitu cha maana cha kutumia kwenye muda wako. Kuanzia leo hii nataka kabisa uachane na dhana ya kuwa unapoteza muda. Ukijikuta upo kwenye hali ya kupoteza tu muda ili saa zisogee, basi jiulize ni kitu gani cha maana ambacho unaweza kufanya

    Au jiulize ni uzalishaji  gani ambao unaweza kuutumia ndani ya huo muda wako. Rafiki yangu, kwa vyovyote vile usikubali kuwa mmoja wa watu ambao wanapoteza muda.

    Muda ni mali, sasa kwa nini ukubali kupoteza mali. Utumie muda wako kwa manufaa kuanzia leo hii. kama huoni kitu gani ambacho unaweza kufanya na muda wako, basi chukua kitabu usome. Tena unaweza kuanza kwa kusoma hata kitabu cha bure ambacho huwa natoa hapa jukwaani. Kukipata nitumie ujumbe wenye baruapepe yako kwa whatsap namba 0755848391. Name nitaktuma kwako bila kuchelewa.

    Kwa vyovyote vile rafiki yangu, usikubali kabisa kuwa unapoteza muda kwenye maisha yako. Muda ni mali, ujali na utumie vizuri sana. Kila la kheri

  • Kitu cha kufanya kama unataka kupata matokeo ya tofauti

    Moja ya kitu ambacho watu huwa wanapenda kwenye maisha ni kupata maisha ya tofauti na maisha mazurri. Sasa leo nataka nikuoneshe ni kitu gani haswa unapaswa kufanya kama unataka kupata matokeo ya tofauti kulinganisha na vile ambavyo umekuwa unapata siku zote.

    Kwanza kabisa kama unataka kupata matokeo ya tofauti unapaswa kuwa mtu wa tofauti. Hapa maana yake matendo yako na hata maneno yako ambayo umekuwa unatumia siku zote vipaswa kubadilika ili uweze kuendana na haya matokeo mapya ambayo unayataka. Huwezi kupata matokeo ya tofauti kwa kuendelea kufanya vitu vilevile kila siku, ambavyo umekuwa unafanya siku zote.

    Albert Einstein aliwahi kunukuliwa akisema kwamba ujinga ni kufanya vitu vilevile huku ukitegemea kupata matokeo ya tofauti. Kumbe kama unataka kupata matokeo ya tofauti rafiki yangu sharti uwe tayari kufanya vitu vya tofauti kuliko ambavyo umekuwa ukifanya siku zote. Labda utakuwa unajiuliza hivi hivi vitu vya tofaut ambavyo ninapaswa kufanya ni vitu gani.  Ninachotaka kukwambia ni kuwa kama hujui ni kitu gani cha tofauti ambacho unaweza kufanya, basi fanya kazi kwa bidii kwenye kazi yako kuliko ambavyo umekuwa unafanya na kuliko mtu mwingine yeyote.

    Kama hujui kitu cha tofauti cha kufanya, basi soma vitabu mbalimbali kuhusiana na fedha, malengo na maendeleao binafsi, kisha fanyi kazi kile unachojifunza kutoka kwenye vile vitu unavyojifunza.

    Kwa jinsi hiyo utakuwa umeanza kufanya kitu cha tofauti.

    Tumia muda wako vizuri, badala ya kutumia muda wako kufanya vitu ambavyo siyo sahihi, tumia muda wako vizur kufanya kitu ambnacho ni sahihi kwako mara zote.

  • Umefanya uamuzi uliobora sana

    Habari ya leo

    Mimi ni Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE
    Ninajua kwamba umeomba kupata KITABU CHA BURE . lakini pia nimeona siyo vibaya ukijua mimi ni nani na kitu gani utegemee kupata kwangu na SONGAMBELE kiujumla.

    Bila kuongeza la ziada napenda kukutaarifu kuwa kitabu chako kimeshatumwa kwenye baruapepe yako, ila kama hukioni unaweza kukipakua kwa KUBONYEZA HAPA

    Kwa miaka zaidi ya mitano sasa nimekuwa nikiandika kwenye blogu hii ya SONGA MBELE. Kwenye blog hii nimekuwa nikiandika makala mbalimbali kuhusu biashara, ndoto zako na malengo yako na jinsi ambavyo unaweza kuyafikia.

    Lakini zadi ya hapo, nimewasaidia watu kama wewe kuweka malengo, kuyafanyia kazi mpaka kuyatimiza. Wengine bado ninaendelea nao mpaka leo hii.

    Hiki kitu ndicho ningependa nifanye kwako pia

    Kila mara nitakuwa nakutumia jumbe fupi na makala zenye kukuelimisha na zitakazokusaidia wewe kuweza kupiga hatua na kufika mbali zaidi kwenye baruapepe yako. Nitafanya hivyo aidha kupitia kwenye makala, video na mafunzo ya sauti.
    Lengo ni kukusaidia wewe kufikia malengo yako haraka iwezekavyo.
    Na hilo litawezekana kama wewe utaendelea kuwa na mimi
    Kiufupi, ukikaa pamoja nami

    • utajifunza namna ambavyo unaweza kuweka malengo.
    •  kuyafanyia kazi mpaka kuyatimiza kwa kutumia mbinu ambazo mimi na wengine wengi tumetumia kwa manufaa
    • Pia utajifunza namna ya kuanzisha na kukuza biashara yako
    • Bila kusahau kipaji chako

    Baada ya kusema hayo, naomba ubonyeze hapa kupakua kitabu chako cha BURE

    Kitabu hiki kitakusaidia wewe; kuanza kusoma vitabu. kitu ambacho ni muhimu sana hasa kama unataka kufikia malengo yako.
    Vitabu vina mchango mkubwa kwa mtu ambaye anataka kufanya  makubwa na kuufikia ukuu.
    Na ndio maana kwenye safari yetu tunaanza kwa kukuonesha MAAJABU KUSOMA VITABU.
    Na bado nina vitu vingi vya bure vya kukusaidia wewe kufanyia kazi malengo mpaka ukayafikia.

    Kitu unachopaswa kufanya wewe ni kuhakikisha kila mara unatembelea barua pepe yako ili kupata mafunzo zaidi lakini pia kutembelea blogu ya SONGAMBELE. kila mara maana hapa naandika makala mbili mpya kila siku

    Tutaongea
    Ni mimi Godius Rweyongeza (Songambele).
    SONGAMBELE

    NB: Kama umepokea kitabu hiki cha zawadi. Naomba unitumie ujumbe kwa barua pepe yangu ya godiusrweyongeza1@gmail.com kuniambia umekipokea.
    Nitafurahi sana kuona ujumbe wako. na nitaweza kuujibu ujumbe wako punde tu baada ya kuupokea. Huwa najibu jumbe zote ambazo zinatumwa kwangu.

  • Jiwe la uzito wa tani moja kwa wale ambao hawataki kuweka akiba

    Moja ya sababu ambazo watu huwa wanatoa linapokuja suala zima la kuweka akiba ni kuwa hawawezi kuweka akiba kwa sababu wana vitu vingi vya kufanya na fedha. Utakuta mtu anakwambia kwamba nina kodi, ya nyumba na bili nyinginezo ambazo ninapaswa kulipa na hata fedha hainitoshi.

    Kitu kimoja cha muhimu sana na cha kushangaza ni kuwa watu hawa watu huwa wanapambana kuhakikisha kwamba wanalipa hizi bili ila huwa wanajisahau kwenye suala zima la kuweka akiba na kuwekeza.

    Bili zao hata zikiongezeka huwa wanahakikisha kuwa wanatafuta namna ya kuzilipa ila huwa hawatafuti namna ya kuhakikisha kuwa wanaweka akiba.

    Sasa leo ninachotaka kukwambia ni kuwa fanya uwekaji wa akiba na uwekezaji kama ulipaji wa bili. Yaani, kama ambavyo unalipa bili zote bila kujali bili hizo zimeongezeka au zimebaki palepale. Hivyo hivyo, unapaswa kuweka kipaumbele kwenye kuweka akiba na kuwekeza. Kamwe usikubali kuishi maisha bila ya kuweka akiba wala kuwekeza. Ni muhimu sana kwako kuweka akiba. Ni muhimu mno kiasi kwamba haupaswi kupuuzia kitu kama hiki hapa rafiki yangu.

    Kuweka akiba kwako kuwe kipaumbele kama vile unalipa kodi ya nyumba. Kuweka akiba kwako kuwe kipaumbele kama vile unanunua luku ya umeme.

    Kuna baadhi ya familia umeme ukikitatika, utakuta kwamba kwenye familia wanahaha, kama baba au mama ambaye anapaswa kununua umeme hayupo wakati umeme unakatika, basi wanafamilia wote watatafuta namna ya kuhakikisha kwamba wanawasiliana naye hata kwa kumpigia simu, hata kama wanaomba simu kwa jirani.

    Sasa nataka na wewe ufanye uwekaji wa akiba kuwa kipaumbele. Mwambie mpaka mwenza wako awe anakukumbusha kuweka akiba kama kitu cha kwanza. Asikukumbushe tu kulipa kodi ya nyumba kwa sababu mkifukuzwa kwenye nyumb mtaaibika, asikukumbushe tu kulipia umeme kwa sababu mkikaa bila umeme hawezi kuangalia tamthiliya, akukumbushe pia kuweka akiba na kuwekeza kwa sababu usipofanya hiki kitu, itakuwa aibu kwako miaka mingi ijayo mbeleni. Fanya uwekaji wa akiba kuwa kipaumbele kwenye maisha yako tena kiwe kipaumbele kikubwa sana. Usipuuzie uwekaji wa akiba na uwekezaji rafiki yangu.

    Kila la kheri, hilo ndilo jiwe langu kwa watu ambao hawataki kuweka kuweka akiba siku ya leo.

    Kujifunza zaidi nashauri usome kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA.

    Hiki kitabu kitakufungua vitu vingi sana kuhusu uwekaji wa akiba na namna ambavyo unaweza kuwa wenye manufaa kwenye maisha yako. Halafu kitabu chenyewe ni elfu tano tu. Ndio, elfu tano ya kitanzania. Namba ya malipo ni 0755848391 na jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    Karibu sana

    Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli

    Godius Rweyongeza (Songambele)

    0755848391

    Morogoro-Tz

  • Kitu ambacho kitakufanya uweze kulipwa zaidi ya unavyolipwa sasa

    Watu huwa wanatafuta siri za mafanikio na kuwafikisha mbali. Kama Kuna Siri ya mafanikio ambayo Unapaswa kuifahamu ambayo itakuwezesha kuongeza kipato Chako zaidi ni kufanya kazi zaidi ya vile unavyolipwa.

    Yaani, kujituma zaidi na kuchapa kazi zaidi ya ambavyo unalipwa. Hiki kitu kitakufanya uweze kulipwa zaidi.

    Kwa sababu kama MTU akikupa kazi yake na ukaifanya kwa viwango vikubwa Kuliko alivyokuwa anatarajia tangu Mwanzo. Ni wazi kuwa Huyu MTU hawezi kukusahau.

    Lakini pia huyu MTU atakuletea watu wengine zaidi.

    Ebu tuchukulie mfano wa kawaida labda wewe Ni fundi cherehani. Mtu amekuja kwako na kitambaa anataka suti. Ukamtengenezea suti nzuri sana kwa viwango vya juu Kuliko hata alivyotazaamia.
    Unadhani zamu ijayo akitaka kutengeneza suti atamtafuta nani? Au unadhani rafiki yake akitaka kutengeneza suti atamwelekeza kwa nani?

    Jibu lipo wazi kabisa… yeye atakuja kwako na rafiki yako atamwelekeza kwako.

    Hiki kitu ukiendelea kukifanya kwa muda mrefu. Utaweza kupongeza kipato Chako Mara dufu mpaka Mara Kumi zaidi.

    Wakati wengine watakuwa wanalia kuwa hawana kazi za kufanya wewe utakuwa nazo za kutosha.

    Anza kufanya kazi zaidi ya unavyolipwa. Kila la kheri.

  • Jinsi Ya Kupata Wazo La Kuandika Kitabu

    Kuna watu huwa wanafikiri labda ili kuandika kitabu basi unapaswa kuwa na wazo la kipekee sana ambalo halijawaji kutokea Hapa duniaani.

    Siyo kweli. Unaweza kuwa na wazo la kawaida tu, Ila wazo Hilo ukalikuza na kulifanya kuwa kitabu kizuri sana. Bado huamini!

    Mfano kwenye picha ya kawaida tu ambayo watu wanachukulia poa wewe unaweza kupata kitabu kizuri sana.

    Nakumbuka juzi nikikushirikisha kuhusu mama aliyenunua kitabu changu Cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU wakati wa maonesho ya nanenane.

    Wakati namtumia kitabu hiki kwa WhatsApp niligundua kitu kimoja. Na kitu hiki ilikuwa Ni picha aliyokuwa ameweka kwenye profile yake. Niliipenda ile picha, kiasi nikamwambia hii picha ina kitabu ndani yake.

    Unaweza kuiona picha yenyewe hapa

    Akiwa bado haamini amini Kama hiyo picha inaweza kutoa kitabu, nilichukua karatasi na kalamu na kuanza kuandika kichwa Cha kitabu. Nikamwambia kutoka kwenye hii picha kichwa Cha kitabu kinaweza kuwa hiki.

    Baada ya hapo nikashuka chini na kuandika UTANGULIZI. Nikakwambia kwenye utangulizi andika hiki na hiki.

    Kisha nikaendelea mbele kwenye sura ya kwanza mpaka ya nne.

    Kisha nikakwambia sura nyinginezo utatafuta mwenyewe.

    Hivyo, ndivyo waandishi huwa tunapata vitu vya kuandikia.

    Kwa kitu chochote unachokiona kuna kitu chaa kuandika ndani yake, itategemea tu na mamna unavyokiangalia kitu.

    Tukichukulia mfano wa mti.

    Daktari akiona mti, anaona dawa ndani yake.

    Mwimbaji akiona mti, anaona wimbo ndani yake.

    Mpishi akiona mti anaona kuni

    Wakati msafiri akiona mti, anaona kivuli na sehemu ya kupumzila

    Fundi seremala kwenye mti huohuo ataona kitanda Safi kabisa.

    Kumbuka mti ni uleule Ila kile watu wanachoona kwenye ule mti ndio kinatofautiana.

    Na kwenye uandishi hivyohivyo, unaweza kuona kitu ukakichukulia kawaida. Mwingine akaona kuna Kuna kitabu ndani yake.

    Ukiwa Kama mwandishi jitahidi kupata walau wazo moja la kuandika kwenye kila kitu unachokiona au watu unaokutana nap.

    Bado unaona haiwezekani tu. Sikiliza, nenda kasome kitabu changu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU. Hiki kina kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uandishi wa vitabu na Makala.

    Halafu kinauzwa elfu tano tu. Na unatumiwa kwa simu au baruapepe yako.

    Yule mama wakati anaendelea kukisoma akisema haya

    Mambo ndiyo hayo. Lipia elfu tano sasa kwa 0684408755jina Ni GODIUS RWEYONGEZA

    Godius Rweyongeza

    0755848391

    Morogoro-Tz

  • Usikubali ufe na ndoto yako ya kuwa Mwandishi mkubwa.

    Wakati wa maonesho ya nanenane Kuna watu wengi walikuwa wanapita eneo la vitabu kwa nguvu zao zote. Wengine walikuwa wanasimama kidogo na kuangalia kinachoendelea Kisha kuendelea na safari

    Siku ya tarehe 3.Agosti alitokea mama mmoja ambaye alisimama kwenye banda letu kwa muda. Nilimkaribisha na kadiri nilivyokuwa nazidi kuongea naye alionekana kuwa anapenda nilivyokuwa naongea ila hakuwa tayari kununua kitabu chochote…

    Baada ya kuongea naye kwa muda, nilikuja kugundua huyu mama alikuwa anapenda kuandika kitabu…


    Na muda wote huo alikuwa akinisikiliza kwa sababu tu ya Ile raha ya kukutana na mwandishi wa vitabu….

    Baada ya kuongea kwa muda nilimshauri asome kitabu changu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU. Palepale nikamtumia kitabu kwenye WhatsApp yake.
    Tukaagana, akawa ameondoka…

    Siku nne mbeleni alinitumia ujumbe huu hapa👇🏿👇🏿

    Kaka Tyk, Unaendeleaje ? na maonyesho? Me namshukuru Mungu nimesoma kile kitabu sijamaliza, ila nimeshaanza kuandika kitabu. Na pia nimepata title nyingi za vitabu vitavuofuata.
    Tumpe Mungu utukufu

    Huu ndio ulikuwa ujumbe wake rafiki yangu. Tumpe Mungu utukufu au unasemaje?

    Najua na wewe unatamami kuwa Kama huyu. Hicho kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU kinapatikana kwa elfu tano tu (5,000/-) tu.

    Unalipia kwa namba hii ya 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Ukishalipia unanitumia ujumbe kwa WhatsApp, halafu Mimi nakutumia kitabu. Ni rahisi sana rafiki yangu.

    Usikubali ufe na ndoto yako ya kuwa Mwandishi mkubwa.

    Godius Rweyongeza (SONGAMBELE)

  • Mtu pekee anayeweza kufanya ufeli kwenye maisha

    Rafiki yangu, Kama Kuna MTU ambaye anaweza kukufabyavufeli kwenye maisha yako Basi Ni wewe mwenyewe.

    Hakuna mtu mwingine wa nje ambaye anaweza kukufanya ufeli. Watu wa nje wanaweza kufunga njia ya wewe kupitia lakini hawawezi kukuzuia kutafuta njia nyingine.

    Wanaweza kukusema vibaya lakini hawawezi kuzuia motisha yako na NGUVU yako ya ndani ya kufanya makubwa.

    Rafiki yangu, mara zote na sehemu zote, pambania malengo yako makubwa.

    Watu wa nje hawawezi kukuzuia wewe kuyafikia mafanikio unayotaka. Labda ukijizuia mwenyewe.

  • Ufanyeje unapopata fedha nyingi kwa wakati mmoja huku ukiwa hujui wapi unaweza kuiweka

    Huwa inatokea mtu anapata fedha nyingi kwa wakati mmoja wakati akiwa hajui Cha kufanya. Sasa siku ya leo nataka tuone wapi unaweza kuweka fedha yako pale inapotokea umepata fedha nyingi kwa wakati mmoja.

    Haijalishi fedha hiyo umeipata kutokana na kubeti 😂
    Au labda wewe Ni mkulima umeuza mazao yako ila sasa unasubiri msimu.
    Au pengine hata inaweza kuwa ni pensheni.
    Au fedha ambayo umekuwa unaifanyia kazi kwa muda mrefu na sasa umepewa kwa siku moja.

    Kuna vitu baadhi ambavyo unapaswa kuangalia kabla ya kuwekeza fedha zako.

    Kwanza ni usalama wa fedha zako.
    Pili Ni uharaka wa wewe kuipata ukiihitaji Tena
    Tatu utaangalia usimamizi wa fedha zako ambazo ukiwekeza utakuwa chini ya Nani na uzoefu wake kwenye kusimamia fedha za watu wengine. Huwezi kumpa fedha ambaye hana uzoefu ili ajifunzie kwenye fedha zako.

    Kitu kingine cha kufahamu ni kuwa Kuna maeneo mengi ya kuwekeza kama kwenye hisa, hatifungani, vipande, kilimo, madini, fedha za kidigitali (forex na crypto currency) na mengine mengi Sana.

    Vigezo vichache nilivyokwambia hapo juu vinatumika kwenye maeneo hayo yote.

    Makala hii haitoshi kujadili maeneo hayo yote kwa kina. Ninachotaka kukwambia leo ni eneo unapoweza kuwekeza fedha zako ikitokea umepata fedha nyingi kwa wakati mmoja. Basi.

    Na mimi nasema hivi, ikitokea umepata fedha nyingi kwa wakati mmoja basi IWEKEZE KWENYE MFUKO WA UKWASI WA UTT AMIS

    Mfuko huu wa ukwasi (liquid fund) ulianzishwa 2013 ukiwa na malengo makuu matatu ambayo ni:
    (i)   Kulinda mtaji wako;
    (ii) Kutoa ukwasi (liquidity); na
    (iii) Kutoa mrejesho shindani kulinganisha na maeneo mengine ambayo unaweza kuweka hela  kwa muda mfupi.

    Mfuko huu unampa muwekezaji uwezo wa kuweka hela zake kwa muda mfupi au mrefu. Mfano, kama muwekezaji amepata fedha ya ghafla au ambayo bado hana malengo nayo kwa wakati huo.

    Mwekezaji anaweza kuiweka kwenye mfuko huu wakati anafikiri nini cha kufanya na fedha yake ikawa inapata faida ya ongezeko la kiasi cha pesa yake wakati hakatwi makato ya aina yoyote.

    Hakuna uwezekano wa fedha hiyo kupungua kutokana na makato Fulani Fulani lakini mfuko wa ukwasi unaweza kukupa msaada sana hapa kwani utatuza fedha zako pasipo kupungua kwa fedha yako wakati wa kuichukua.

    Mathalani, unaweza kuwa mkulima wa msimu (unategemea mvua) baada ya kuvuna na kuuza mazao pesa yako ya mtaji ambayo utatumia kwa ajili ya kilimo mwaka ujao unaweza kuiweka katika mfuko huu wakati unasubiri msimu hapa utapata faida ya ongezeko la mtaji bila kupoteza chochote.

    Kumbe ukiweka fedha yako huku,
    Hakuna makato utakayopata kwa kuweka fedha yako.
    Hakuna makato ya kukutunzia fedha yako. Kikubwa zaidi utapata ongezeko la faida.
    Na hakuna makato wakati wa kutoa fedha.

    Halafu fedha yako ukitaka kuitoa unaipata kwa wakati. Ndani ya siku tatu tu fedha yako inakuwa tayari. Hii Ni tofauti na uwekezaji maeneo mengine kama kwenye hisa ambapo ukinunua hisa na baadaye ukija kuuza Kuna kiasi Cha fedha kinakatwa.

    Au kwenye kilimo ambapo unaweza kuwekeza na fedha yako isirejee kwako Kama ilivyokuwa unatarajia kulingana na hali ya hewa.

    Kitu kimoja Cha ziada. Ukitaka kufuatilia kujua taarifa kuhusu uwekezaji kwenye mfuko wa UKWASI, taarifa zake Ni rahisi kupatikana na hauchukui muda mrefu. Ila ukisema ufuatilie crypto currency mzee baba…utatuatilia mwaka mzima na bado hutaelewa.

    Kwa leo wacha niishie tu hapo.  Hii makala Ni maalumu tu kwako wewe ambaye umepata fedha nyingi, Mara moja na unawaza wapi unaweza kuiwekeza. Ila Kama unataka kujifunza zaidi kuhusu uwekezaji kwenye hisa HATIFUNGANI NA VIPANDE basi nashauri usome kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Hutajutia kukisoma

    Kila kheri

    Godius Rweyongeza

  • Maoni Ya Watu KuhusuVitabu Vya Godius Rweyongeza

    Leo nimekuandalia baadhi ya maoni na shuhuda za watu waliosoma vyangu.

    Huyu wa kwanza alichukua kitabu Cha MAISHA NI FURSA wakati wa nanenane. Na haya ndiyo anasema kuhusu hiki kitabu

    Huyu mwingine wakati naongea naye aliniambia anataka kuwa Mwandishi. Nikamtumia kitabu kwa njia ya mtandao. Na Sasa amekisoma na kuanza kuandika.

    Ndoto yake ya siku nyingi ya kuwa Mwandishi imeshaanza kutimia

    Na huyu hapa Yuko Zanzibar

    Na wewe ungependa kupata kitabu kipi kutoka kwetu?
    Orodha kamili ya vitabu vyetu hii hapa


    BONYEZA HAPA KUONA ORODHA YA VITABU VYETU VYOTE

    Tuwasiliane kwa 0755848391

    Godius Rweyongeza

    Morogoro-Tz

    Maoni mengine kuhusu kitabu CHA AKILI YA DIAMOND haya hapa

X