Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • App mbili ambazo kila mfanyabiashara anapaswa kuwa nazo

    Kuna app mbili ambazo kila mfanyabiashara anapaswa Kuwa nazo.

    1. Thl accounting
    Hii inakusaidia kutunza hesabu zako zote za biashara. Na bidhaa ZAKO zote ulizonazo kwenye Biashara yako, itakuonesha bidhaa zinazokaribia kuisha au zilizoisha, itakusaidia kutengeneza invoice, itakusaidia kutunza hesabu za mauzo, mapato mpaka matumizi.
    Hata Kama uko mbali bado unaweza kuona mwenendo wa  biashara yako. Kitu hiki Ni muhimu Sana kwako wewe mfanyabiashara.

    Rafiki yangu, hii ni moja ya app ambayo nakushauri Sana uwe nayo kwenye biashara yako. Itakusaidia kufanya mengi kwa manufaa.

    2. Beem
    Hii inakusaidia kutuma SMS kitalaam. Yaani, unatuma sms zenye jina la biashara. Kama umewahi kuona SMS za voda, Tigo au halotel wanazotuma. Sms ambazo huwa zinakuja kwa msomaji Ila hawezi kujibuoja kwa moja. Badala yake unaweza kumwekea link au namba ya kujibu. Kama hii hapa

    Hii Ni muhimu kwako mfanyabiashara.
    Kwanza utafanya biashara yako ionekane kitalaamu zaidi.

    Lakini pia utafanya wateja wakuamini. Kuna wateja wakiona tu kuwa unaweza kutuma jumbe za aina hiyo, watashawishika na kuona wewe unawafaa zaidi.

    Unaweza kuwatumia wateja SMS za kuwajulia Hali
    SMS za kuwakaribisha kununua
    Ofa za sikukuu na kawaida
    Mzigo mpya unaposhuka
    N. K.

    Hizo ndizo app mbili ambazo ni lazima kila mfanyabiashara awe nazo.

    Kama ungependa kujifunza zaidi namna bora ya kuzitumia, Basi usisite kuwasiliana nami kwa 0755848391

    Karibu sana.

  • Ni makosa Yapi Kati Ya Haya Matatu Umewahi Kuyafanya Maishani Mwako?

    1. Kuwa na wazo la BIASHARA au uwekezaji Ila ukachelewa na baadaye watu wengine wakalifanyia kazi

    Umewahi Kuwa na wazo la BIASHARA ambalo ulikuwa ukifikiria kulifanyia kazi Ila ukachelewa kulifanyia kazi. Baadaye likafanyiwa kazi?

    2. Kuweka Mipango mikubwa mwanzoni mwa mwaka ambayo hukuwahi kufanyia Kazi?
    Au labda umewahi Kuwa na mpango mkubwa sana, mwanzoni mwa mwaka. Mpango  wa kuanza kusoma
    Mipango ya kupanda miti
    Mipango ya Kujenga n.k Ila hukuwahi kuifanyia kazi?

    3.  Kuwa na kazi kubwa ambayo ulisubiri kuifanya siku ya mwisho.

    Au pengine umewahi kupewa kazi ya kufanya ofisini, ukaisubirisha mpaka siku za mwisho mwisho ndio ukaja kuifanya na baadaye ukawa uneifanya hovyo.

    Kama umewahi kufanya kosa lolote hapo na kama bado Kuna kosa unafanya hapo, maana yake umekuwa unasubiri kufanya kitu kikubwa kwa wakati mmoja. Yaani, umekuwa unasubiri ufanye kitu kwa mapinduzi badala ya kufuata mfumo wa mageuzi.

    Unajua mapinduzi ni Nini.

    Mapinduzi ni mabadiliko ambayo huwa yanatokea ndani mfupi Sana. Yanaweza kuchukua sekunde, dakika au siku chache. Ila yakitokea huwa yana tabia ya kurudiwa tena.

    Ila mageuzi kwa upande mwingine huwa yanachukua muda. Miaka na miaka. Ila yakitokea, huwa yametokea na huwa hayarudi nyuma.

    Sasa wewe kwenye maisha yako unahitaji mageuzi. Kufanya vitu hata kama ni kidogokidogo bila ya kurudi nyuma. Na hapa ndipo unahitaji mwongozo wa kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA.

    Hiki kitabu kimeeleza kwa kina, namna unavyoweza kuitumia NGUVU Hii ya VITU VIDOGO kufanya MAKUBWA.

    Hakikisha unapata nakala yako leo hii. Nakala moja ya kitabu hiki ni 20,000/- tu.

    Na unatumiwa popote pale ulipo duniani.
    Audiobook na softcopy pia vipo.
    Fanya malipo kwa 0755848391 Sasa ili utumiwe  nakala yako.

    NAKUKUMBUSHA TU: Endapo hutachukua hatua ya kupata kitabu hiki cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA miaka mitano ijayo utakuwa unaendelea kufanya makosa hayahaya Tena kwa kuyarudia.

    Na hicho kitu ndicho Albert Einstein alikiita ujinga pale aliposema, “ujinga Ni kurudia kufanya Mambo yaleyale huku ukitegemea kupata matokeo ya tofauti.”

    Chukua hatua sasa. Pata nakala yako kwa elfu 20,000 tu. Tuma fedha kwa namba 0755848391

    Umekuwa nami
    Godius Rweyongeza
    Morogoro-Tz
    +255755848391

    Karibu sana

  • Njia hii itakusaidia kufanya majukumu yako kwa mwendelezo na kuchana na kughairisha (Seinfeld Calendar)

    Nadhani imewahi kukutolea maishani kwamba unapenda kuanzisha kitu na kukifanyia kisha baada ya muda kidogo unaachana nacho. Au baadaye unaanza kujiambia kwamba nitakifanya kesho au wiki ijayo.

    SIKU ya leo Nina mbinu ambayo inafahamika kama  Seinfeld Calendar.
    Kuifahamu Seinfeld Calendar ngoja kwanza tujue  Seinfeld mwenyewe alikuwa nani kiufupi.

    Huyu alikuwa ni mwigizaji ambaye kwa miaka mingi alikuwa akitengeneza maigizo yaliyokuwa yanakonga nyoyo za watu. Watu walishangaa kwa nini alikuwa hashuki kwenye chati.

    Sasa SIKU moja ndipo alipoeleza hii Siri take ya mafanikio. Akisema kwamba, Siri kubwa ya mafanikio yake ni kuwa huwa anaandika maigizo kila SIKU. Kadiri anavyoandika ndivyo anapata hamasa na mawazo mapya ya kuigiza kila SIKU.

    Aliendelea kwa kusema kwamba yeye huwa ana kalenda kubwa ambayo huwa anaiweka chumbani kwake au sehemu yoyote ambapo inaonekana. Halafu anakuwa na mark pen kubwa nyekundu.  Kwenye kalenda  anaweka  X kubwa SIKU ya mwisho ambayo anataka igizo lake liwe limekamilika.  Halafu anaanza kulifanyia kazi Sasa.


    Kila siku anapofanya kazi anaweka X kubwa. Muda siyo mrefu anakuwa ameweka X nyingi, kiasi kwamba mchakato wake unakuwa Ni kupongeza X ZAIDI kwenye kalenda. Anasema kadiri inavyokaribia siku ya mwisho ya kukamilisha jukumu, ndivyo anakuwa anajisukuma zaidi ili kukamilisha jukumu husika. Huku akifurahia mchakato wa KUWEKA X ZAIDI kwenye kalenda.

    Rafiki yangu, una jukumu kubwa? Unataka liwe limekamilika Mpaka siku gani? Basi chukua kalenda leo. Weka X kwenye tarehe ambapo ungependa kukamilisha jukumu lako. Kisha anza kulifanyia kazi kuanzia Leo ukiweka X moja baada ya nyingine.

    Kila la kheri
    Godius Rweyongeza (songambele)
    0755848391
    Morogoro

  • Kama Wewe Ni Mpenzi wa Kuandika kwenye Status Za WhatsApp Basi Leo Kuna kitu Nataka Nikwambie.

    Siku hizi imekuwa ni rahisi kuandika mtandaoni. Status za WhatsApp, Facebook na maeneo mengine.

    Kitu hiki kinawafanya watu waandike jumbe fupi Ila nzuri ambazo huwa zinapotea baada ya muda.

    Kwa mfano, mtu anaandika status ya WhatsApp, lakini  inapotea baada ya saa 24. Ule ujumbe wake mzuri alioandika unapotea na hauonekani Tena. Na wengi wanaoandika kwenye status huwa hawatunzi kumbukumbu za kile walichoandika. Kwa hiyo baada ya mwaka akitaka kurejea alichoandika mwaka mmoja uliopita. Kinakuwa hakipo! Halafu eti ninasema baada ya mwaka. Mwaka wote huo.
    Hata baada ya saa 24. Ebu fikiria jumbe nzuri ngapi zinapotea tu kama upepo kila siku. Jumbe ambazo watu wanaweka WhatsApp na bado hazimnufaishi mtu yeyote.

    Kama wewe ni mpenzi wa kuandika kwenye status za WhatsApp Basi leo Kuna kitu nataka nikwambie.

    Unaonaje badala ya kuandika jumbe zako hizo nzuri na kuziweka WhatsApp tu Ambapo zinapotea baada ya saa 24 ukiziweka  sehemu Ambapo hazipotei Kama kwenye blogu.  Unaweza hata kutengeneza blogu ya bure mtandaoni. Ukawa unaziweka  huko kwa ajili  ya kumbukumbu ya baadaye.

    Unaonaje badala ya kuandika status fupi za WhatsApp ukiandika makala ndefu ya kuweka kwenye blogu, halafu ukatoa kipande tu cha kuweka status Kama kawaida yako.

    Unaonaje ukiendeleza jumbe zako fupi na kuzifanyia KUWA kitabu?
    Siyo kwamba huwezi kuandika kitabu. Unaweza vizuri tu, Mimi nina hakika ukijumuisha status zako zote ambazo umekuwa unaandika whatsap kwa miaka sasa, utakuwa umeshaandika kitabu kikubwa. Sasa kwa nini usiamue kuanzia hapa kuandika kitabu chako.

    Nina uhakika Kati ya wote watakaosoma ujumbe huu, wengi wataupuuzia, mmoja ataufanyia kazi na baada ya mwaka atatoa kitabu chake. Na nitamwandika  hapa jamvini. Sasa kwa nini mmoja huyo asiwe wewe?

    Ebu chukua HATUA.
    Najua utakuwa unakwama kwa kujiuliza, nawezaje kuanza kuandika kitabu? Jibu ni rahisi sana. Hakikisha unapata kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA (Hardcopy) na kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU (softcopy). Kuvipata hivi Vitabu wasiliana nami kwa 0755848391

    Hivi vitakupa mwongozo wote unaouhitaji.

    Kila la kheri.

  • Hiki ni kitu ambacho unapaswa kukitafuta kwa nguvu zako zote

    Ni kitu gani hiki….
    Ni kutafuta kuwaelewa wengine kabla ya kutaka kueleweka.

    Kwenye maongezi ya kila siku kila mtu huwa anapigana kuhakikisha kuwa anaeleweka kwenye kile anachofanya.

    Hiki kitu tu huwa kinasababisha ubishi mkubwa. Ninachotaka kukwambia leo ni kwamba tafuta kuwaelewa wengine kwanza kabla wewe hujaeleweka. Hilo litakusaidia sana maana ukishajua upande mwingine unataka nini itakuwa rahisi kwako kuweza kuwasilisha hoja yako na kuongea nao  waweze kukubaliana na wewe.

    Hilo ndilo Jambo la msingi na KUBWA Sana ambalo unapaswa kupambania kila mara. Maana watu wengi huwa wanapenda kueleweka wao kwanza wakiwa hawataki kuwaelewa wengine. Sikiliza, kama hujawaelewa wengine, hata ukishinda kwenye mjadala bado ushindi wako haitakuwa wa maana. Hivyo Mara zote tafuta kuelewa watu kwanza kabla ya kueleweka.

  • Business to Business (B2B) Ni Nini?

    Business to business ni mfumo wa BIASHARA unaofanyika kati ya Kampuni na Kampuni au kati ya BIASHARA moja na nyingine.

    Yaani, Kampuni inatengeneza bidhaa kwa ajili ya kuuza kwa Kampuni nyingine na siyo kwa walaji wa mwisho.

    Kampuni nyingine zinaweza kuwa na bidhaa za aina mbili. Bidhaa moja ya kuuza kwa walaji wa mwisho na bidhaa nyingine kwa kampuni nyinginezo.

    Au bidhaa moja inaweza kuuzwa kwa watu kwa bei tofauti. Walaji wa mwisho wakauziwa kwa bei ya juu kidogo wakati biashara au kampuni ikiiuziwa kwa bei ya chini.

    Mfano bidhaa ya inayouzwa elfu ishirini kwa walaji wa mwisho inaweza kuuzwa elfu kumi na tano au chini kwa biashara nyingine.

    Hiyo ndiyo business to business (B2B)

  • Hii Ni Zawadi Ya Kipekee ambayo Unaweza Kutoa Kwa Baba Yako (Happy Father’s Day)

    Kila mzazi huwa anapenda kuona mtoto wake anafanikiwa na kufanya makubwa. Anaweza akawa hasapoti ndoto yako.
    Anaweza akawa hayuko nyuma yako wakati wa mapambano, Ila ukifika ukifanikiwa atakuwa nyuma yako.

    Kumbe zawadi ya kipekee ambayo unaweza kutoa kwa wazazi wako ni kufikia ndoto zako.

    Jipe muda wa kufanyia Kazi ndoto zako na kuhakikisha kuwa haurudi nyuma hata kidogo linapokuja suala zima la kufanyia Kazi ndoto zaako. Amua kuwa utapambana uzifikie ndoto zako au utakufa ukizifanyia kazi Ila hakuna kukata tamaa wala kurudi nyuma.

    Ukizifikia wazazi wako watafurahi. Na hii ndiyo zawadi ya kipekee ambayo unaweza kutoa kwa wazazi wako rafiki yangu.

    Ili uweze kuzifikia ndoto zako vizuri nimekuandalia mwongozo wa vitabu vya kipekee sana.

    Mwongozo huu unahusisha vitabu vya
    JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO pamoja na
    NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA

    Vitabu hivi vya kipekee sana, vitakusaidia wewe kwenye kufanyia kazi ndoto zako mpaka kuzifikia.

    Vitabu hivi vinapatikana kwa mfumo wa nakala ngumu (hardcocopy), Audiobook na softcopy.

    Na kila nakala gharama yake Ni 20,000/-
    Hii ndio kusema kwamba ukichukua nakala zote mbili gharama yake inakuwa ni 40,000/-

    Ila kwa kuwa leo ni siku ya baba duniani. Basi nakupa ofa wewe. Na hii Ni ofa ya leo tu.

    Ukilipia elfu 40 ya vitabu, nitakutumia vitabu kwa gharama yangu mwenyewe.

    Unaonaje hapo?

    Chukua hatua sasa.

    Lipia kwa 0755848391 jina Ni GODIUS RWEYONGEZA

  • Viashiria Vitano Kuwa Wewe Ni Genius (Kiashiria Namba Tano Ni Muhimu Sana Rafiki Yangu)

    Siku ya leo nimekuandalia video inayoeleza viashiria vitano ambavyo vinaonesha kuwa wewe ni Genius? Je, upo tayari kujua hivi viashiria?

    hakikisha umesubscribe kwenye channel yangu ya youtube kwa ajili ya mafunzo zaidi hapo baadaye.

  • Mwongozo Unapouhitaji Kufikia Ndoto Zako

    Jana nilikuwa naongea na rafiki yangu ambaye amechukua vitabu vya JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO pamoja na NGUVU YA VITU VODOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA

    Inaonekana rafiki yangu kaelewa vizuri sana dhana ya hivi kitabu. Anasema hivi,

    Unahitaji kuwa na ndoto KUBWA. Ila haitoshi. Ili uifanikishe hapo ndipo utapaswa kutumia nguvu ya vitu VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA.

    Yaani, ni sawa na kuwa na ugali mezani. Haumezi wote kwa wakati mmoja, Bali unameza tonge moja baada ya jingine.

    Mwisho wa siku unamaliza ugali wako.

    Na ndoto yako hivyohivyo. Hauifanyii kazi kwa wakati mmoja na kuifanikisha bali unaifanyia kazi hatua kwa hatua kwa kutumia nguvu ya vitu VIDOGO huku ukiyaelekea mafanikio makubwa.

    Huyu Ni msomaji ambaye amevielewa vizuri hivi vitabu na kutoa maoni yake kuhusu hivi vitabu.

    Hivi kwa mfano, wewe unaanzaje kukosa kupata nakala yako leo? Unaanzaje eti!

    Gharama ya kila kitabu ni 20,000/- (Hardcopy).
    Unatumiwa popote pale ulipo.
    Ebu tuwasiliane Sasa kwa 0755848391

    Au bonyeza hapa chini
    https://wa.me/message/3PMZSAFONLHAP1

  • JINSI YA KUJUA THAMANI YA MUDA WAKO

    Tuna rasilimali nyingi ambazo tunaweza kutumia kwenye maisha yetu ya kila siku.

    Rasilimali hizo ni kama

    • Ardhi
    • Madini
    • Maji
    • Fedha
    • Muda ……

    Kati ya hizo rasilimali zote, muda ndio rasilimali ambayo ukiipoteza huwezi kuipata. Hivyo, unahitaji kuweza kuitumia vizuri rasilimali hii ya kipekee.

    Na leo nataka nikwambie namna ambavyo unaweza kujua thamani ya muda wako. Kujua thamani kutakusaidia zaidi kuwekeza nguvu zako kwenye kufanya kazi na majukumu ambayo ni ya muhimu, huku ukiachana na majukumu ambayo siyo ya muhimu

    Ili tujue thamani ya muda wako, kwanza unapaswa kujua kiasi gani unataka kuingiza kwa mwaka mmoja ujao. Je, unataka kuingiza kiasi gani kwa mwaka mmoja ujao? Ebu kwa mfano tuseme kwamba una mpango wa kuingiza milionoi 100. (Hiki kitu tukiite A)

    Kitu cha pili cha kujiuliza ni muda kiasi gani ambao uko tayari kufanya kazi kwa wiki? Kama kwa siku unafanya kazi kwa saa 15 na kwa wiki unafanya kazi kwa siku sita. maana yake kwa wiki unafanya kazi kwa saa 90 (Hiki kitu tukiite B).

    Na kitu cha tatu ambacho tunataka tujue ni je, kwa mwaka utakuwa tayari kufanya kazi kwa wiki ngapi? Kwa kawaida mwaka una wiki 52. Sasa ni wiki ngapi utakuwa tayari kufanya kazi ukiondoa wiki za mapumziko. Kama unapumzika kwa mwezi mzima kwa mwaka, maana yake unafanya kazi kwa wiki 48 tu kwa mwaka (hiki kitu tukiite C).

    Sasa kifuatacho, ngoja tuone thamani ya muda wako kwa kutumia vipengele hivyo hapo juu. Kujua thamani ya muda wako utachukua.

    Thamani ya muda ni sawa= (A÷B÷C)

    Kwa hiyo kama una mpango wa kuingiza milioni 100 kwa mwaka na kufanya kazi kwa saa 90 kwa wiki kwa wiki 48. Hivyo,

    Thamani ya muda wako= (100,000,000÷90÷48)=23,146

    Kwa hiyo wewe thamani ya muda wako ni sawa na 23,148. Ukifanya kazi yoyote ambayo ni ya chini ya hivyo viwango, basi unakuwa umejishusha.

    Kama ulikuwa hujawahi kupima thamani ya muda wako, Ebu fanya hivyo siku ya leo. Utajifunza vitu vingi na kikkubwa zaidi ni kwenye utunzaji mzuri wa muda wako. Rafiki yangu, tunza muda wako vizuri kulingana na viwango vyako vya fedha ambavyo unatakiwa kulipwa kwa saa.

    Kama bado hujasoma kitabu changu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA pamoj anakitabu na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO nashauri sana usome vitabu hivi.

    Unaweza kupata vitabu hivi kwa kuwasiliana na 0755848391

    Fanya hivyo sasa hivi.

    Umekuwa nami

    Godius Rweyongeza

    0755848391

    Morogoro-Tz

    Kwa maswali, maoni au booking: songambele.smb@gmail.com

X