Home


  • Jibu la kuwapa watu wanaokuja kukopa kwako

    Rafiki yangu nadhani moja ya shida Kubwa ambazo zinawakumba watu wengi ni kushindwa kuwa na nidhamu ya fedha. Hivyo, kwa sababu hawana nidhamu ya na fedha. Wanatumia fedha zao hovyo na bado wanakuja kwako wakitaka uwakope.

    Ninachotaka kukwambia leo ni kuwa  kama hawana nidhamu na fedha zao, usitegeemee  kwamba ukiwakopa watakuwa na nidhamu Na fedha yako. Na Wala siyo kwamba unakuwa unawasaidia kama unavyodhani, badala yake unakuwa unazalisha tatizo.

    Hawakuwa na nidhamu Na fedha yao, hawatakuwa na nidhamu yako. Wataitumia hovyohovyo. Itaisha na watashindwa kukulipa.

    Wewe utakuwa umejipa jukumu la kudai. na kama unavyojua, kukopa ni sherehe ila kulipa ni matanga.

    Sasa ili kuondokana na Hali hiyo, hakikisha kuwa haukopi kabisa. Ipende pesa yako, vizuri sana kuliko unavyopenda kitu kingine rafiki yangu.

    MTU akikwambia naomba unikopeshe kiasi fulani Cha fedha, mjibu hivi.

    Nashukuru sana kwa KUNIAMINI sana na kuniona mimi kuwa mtu ambaye naweza kukusaidia

    Nilitamani sana nikusaidie siku ya leo, Ila umechelewa kidogo kuniambia. Laiti ungekuja asubuhi ningeweza kukusaidia vizuri Sana.

    Maana muda si mrefu nimetoka kufanya muamala mkubwa. Hivyo sitaweza kukupa hela maana muamala niliyofanya umechukua hela nyingi na bado hapa natafuta nyingine za kuongezea.

    Kwa Leo nakushauri ujitahidi uangalie sehemu nyingine.

    Asante sana kwa KUNIAMINI.

    Kalili hii kauli, na itumie hii mara zote. Ukishamwambia mtu hivyo, anakuwa hana cha kusema zaidi ya hapo.

    Itakusaidia sana

  • Dakika moja ya vitendo, ni bora kuliko maelfu ya dakika za maneno

    Wakati tunasoma O-Level tulikuwa na jamaa mmoja hivi ambaye angeweza kukutisha kuwa atakupiga. Kwa vitisho vyake tu, ungeweza kudhani jamaa ana manguvu kama HAWAFU? Kwanza unamjua Hawafu kweli? HAHAH.

    Hii stori ya Hawafu mwenye nguvu tuiache kwa ajili ya siku nyingine. Ila kama umeikumbuka vizuri unaweza kunijuza kikashani kwa kujibu ujumbe huu.

    Ssasa tuendelee na jamaa yetu. Jamaa angeweza kukutishia kwa maneno tu mpaka ukanyoosha mikono juu kuwa umeshindwa. Sasa kutokana na vitisho vyake, siku moja alikuja kumtishia jamaa ambaye hatishiki. Siku hiyo moto uliwaka…..

    Unataka kujua nini kilitokea…

    Hahah, niache kwanza. Maana ilikuja kugundulika kuwa jamaa hana nguvu ila vitisho tu.

    Sasa ninataka kukwambia nini siku ya leo.

    Ninachotaka kusisitiza kwako siyo kwamba uanze kupigana na watu kuonesha kwamba una nguvu. Badala yake, nataka nikusisitize jambo moja la msingi sana. na jambo hili ni kwamba mwaka huu ukawe wa vitendo kwako kuliko maneno. Ndio maana mwaka huu tunaenda kwa kauli mbiu kwamba haturembi mwandiko.

    Ni vitendo tu rafiki yangu.

    Kwa hiyo mwaka huu, punguza maneno. weka kazi. punguza maneno. weka kazi. punguza maneno weka kazi

    Ni hivyo tu.

    Kwenye kitabu changu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI nimemwongolea jamaa mmoja ambaye alikuwa anapenda sana kazi. na yeye muda wa kufanya kazi alikuwa anajua maneno matatu tu pale ulipokuwa ukimwongolesha.

    Nashauri na wewe utumie haya maneno pia. Kujua haya maneno muhimu ya kutumia wakati wa kazi na kupata kitabu chenyewe basi fanya hivi.

    Pata nakala yako leo hii.

    Nakala laiani ni 10,000/- na nakala ngumu ni 15,000/.

    Kitu kingine muhimu sana kwako ni kwamba tuna semina.

    SEMINA YA KUFUNGUA MWAKA MPYA 2023. Na semina hii itaanza tarehe 15. Januari, hii. na itadumu kwa siku 15 mfululizo mpaka tarehe 30.

    Semina hii itafanyi ka kwa njia ya mtandao. Na kwa siku 15 zote za semina utalipia 15,000/-.

    Ili kujiunga na semina hii. wasilina nami kwa 0755848391.

    Karibu sana.

  • KITABU: MAAJABU YA KUSOMA VITABU

    Mwezi septemba mwaka 2019 niliandaa kitabu kifupi cha Maajabu Ya Vitabu. Kitabu hiki hapa nilikisambaza bure mtadaoni. Kimetokea kuwa moja ya kitabu cha Kiswahili ambacho kimesomwa na watu wengi sana.

    Mwanzoni sikutegemea kama kitabu hiki kingesomwa na watu wengi sana. Ila kilichotokea toleo la kwanza la kitabu hiki hapa kilisomwa na maelfu kwa maelfu ya watu. Asilimia kubwa ya wasomaji wa toleo la kwanza wakawa wananitafuta na kueleza jinsi kitabu hiki kilivyobadili fikra zao kuhusu usomaji wa vitabu. Kuna watu wamejenga tabia ya kusoma vitabu mara baada ya kuwa wamesoma kitabu kile na sasa hivi watu hao ni wasomaji wazuri wa vitabu.

    Kwa hiyo, kitabu hiki kikaniunganisha na wahariri, wasomi, wakulima na watu wa kila aina kutoka ndani na nje ya nchi. Wengi wao tumejenga urafiki baada ya kuwa wamesoma hiki kitabu mpaka leo hii. Wapo waliosoma kitabu hiki hapa wakasema kwamba mimi lazima nisome na vitabu vyako vingine. na kweli wakawa wamechukua hivyo vitabu na kuvisoma pia.

    Kila aliyesoma kitabu hicho alimtumia na mwenzake ili asome. Hivyo, kwa njia hiyo kikazunguka kila kona ya nchi hii na dunia nzima kiujumla kwa wasomaji wote wa lugha ya Kiswahili.

    Hata hivyo, kadiri muda ulivyokuwa unaenda nikaendelea kuboreshakitabu hiki hapa. na hivyo, leo hii napenda kukwambia kwamba lile toleo la kwanza la kitabu cha Maajabu Vitabu halipo tena. Sasa tuna toleo la pili ambalo limeboreshwa mara 30 zaidi ya lile toleo la kwanza. Kama ulisoma toleo la kwanza ukasema, “looo, hiki ni kitabu cha kipekee kweli!”

    Sasa ukisoma toleo la pili ni wazi kuwa , hizo looo, zitakuwa mara 30 zaidi. hahah.

    Utatumiwa kitabu chako bila kuchelewa.

  • Kwa nini huwa tunarudia kusoma vitabu

    umeshapata nakakla zako? Wasiliana na 0755848391 sasa kupata nakala zako. kila nakala bei yake ni 20,000/-
    umeshapata nakakla zako? Wasiliana na 0755848391 sasa kupata nakala zako. kila nakala bei yake ni 20,000/-

    Rafiki yangu umewahi kujiuliza kwa nini huwa tunarudia kusoma vitbu ambavyo tulishavisoma siku za nyuma. Nimeanza mwaka huu kwa kurudia kusoma kitabu cha THINK AND GROW RICH. Na mwaka huu kuna vitabu vingi ambavyo nitakuwa narudia kusoma zaidi ya hiki. Unajua kwa nini huwa tunarudia kusoma vitabu.

    Huwa tunarudia kusoma vitabu kwa sababu kwenye kusoma hicho kitabu kuna kitu cha ziada ambacho tutapata kutoka kwenye hicho kitabu ambacho pengine mara ya kwanza wakati tunasoma hicho kitabu hatukukipata.

    Huwa tunarudia kusoma vitabu kwa sababu mara ya kwanza wakati tunasoma kile kitabu tulikosoma kwa mlengo fulani.

    Mfano, kama inawezekana WAKATI nasoma kitabu hicho nilikuwa nataka kujifunza zaidi kuhusu kuweka akiba, kipindi hicho mambo ya kuwekeza yalikuwa hayajaingia kichwani maana hata hela yenyewe ya kuweka akiba ilikuwa ni shida, ila sasa hivi nasoma kitabu ili nijifunze zaidi kuhusu uwekezaji.

    Au pengine nilisoma kitabu kwa sababu nilikuwa nataka kujua namna bora ya kuingia kwenye mahusiano. Ila sasa hivi nimeshaingia kwenye mahusiano na sasa nataka kujifunza zaidi kujenga na kuboresha mahusiano.

    Au pengine nilisoma kitabu nikiwa najifunza namna ya kuanzisha biashara. Lakini sasa hvii nataka kujenga timu kwenye biasahara yangu.

    KWA HIYO RAFIKI YANGU, hivyo ndivyo vitu ambavyo vinatufanya tusome vitabu na turudie kusoma vitabu zaidi na zaidi.

    Unaporudia kusoma kitabu ambacho ulishasoma mara ya kwanzpata unajikuta kwamba kuna itu vya ziada ambavyo unakuwa unapata kutoka kwenye kile kitabu ambavyo hapo mwanzoni huku

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

  • Mambo Muhimu Utakayojifunza Kwenye Kitabu Cha JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO

    Kitabu cha jinsi ya kuongeza thamani yako ni moja ya kitabu bora utakachosoma mwaka huu. Na leo nimetamani sana nikufungulie ndani ya hiki kitabu ili uweze kuona ni kitu gani hasa unaenda kupata kutoka kwenye hiki kitabu. Kipakue hapa chini

  • Ushauri Muhimu Kwa Mtu Yeyote Ambaye Ana Lengo La Kuweka Akiba 2023

    Hivi ulivyo mwanzo wa mwaka najua kuna watu wengi ambao wameweka lengo la kuweka akiba. Watu wanataka waweke akiba ili waweze kupata uhuru wa kifedha. Sasa siku ya leo ningependa kukwambia kitu kimoja muhimu sana, wewe ambaye umeweka lengo la kuweka akiba

    KABLA sijakwambia hiki kitu naomba kujua ni wapi utakuwa unaweka fedha zako za akiba. Je, fedha hizi utakuwa unaziweka benki, au fedha hizi utakuwa ukiziweka chini ya godoro?

    Kitu kimoja kikubwa ambacho ningependa kukwambia siku ya leo ni kwamba mwaka huu FUNGUA AKAUNTI YA UTT na fedha yako ya akiba uwe unaiweka huku.

    Pengine unajiuliza UTT amis ni nini?

    UTT ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja ulio chini ya wizara ya fedha. Ambao wenyewe kazi ni kukusanya mitaji kutoka kwa watu na kuiwekeza kwa niaba ya watu.

    Kwenye hii makala sitaeleza kwa undani zaidi kuhusiana na UTT. Kama utapenda kujifunza zaidi kuhusiana na UTT nashauri sana usome kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Hiki kitabu kina kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uwekezaji kwenye UTT.

    Humu kwenye blogu pia kuna makala nyingi kuhusiana na uwekezaji huu. ila kikubwa ninachotaka kusisitiza kwenye makala ya leo ni kuhusu mrejesho pale unapoweka hela yako.

    BENKI nyingi hazitoi riba kubwa kama ilivyo UTT. Na UTT imedhihirisha kuwapa mrejesho mzuri wawekezaji wake kwa muda mrefu zaidi.

    Hivyo kama kuna kitu ambacho nakushauri rafiki yangu ni kimoja tu. mwaka huu akiba yako iweke UTT badala ya kuiweka sehemu nyingine.

    Kila la kheri.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Baadhi ya vitabu vyangu vimesomwa kwa mfumo wa sauti yaani, audiobook. Na mojawapo ya kitabu cha aina hiyo ni kitabu hiki CHA NGUVU YA VITU VIDOGO KUELELEA MAFANIKIO MAKUBWA. Hakikisha unapata kitabu hiki mapema iwezekanavyo. Tuwasiliane kwa 0755848391

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

  • Kama utashindwa kufanya vitu vyote ndani ya mwaka 2023, hakikisha kwamba haushindwi kufanyia kazi hiki kitu kimoja tu

    Rafiki yangu, sasa hivi ndio kwanza moto wa mwaka 2023 unakolezwa. Kama bado hujaanza kufanyia kazi malengo yako, kuna nafasi kubwa kuwa unaweza usije ukakamilisha haya malengo yako kama niliyoveleza kwenye makala ya jana.

    Siku ya leo ningependa kukwambia kuwa kama mwaka huu tutashindwa kufanyia kazi malengo yako na vitu vingine, basi hakikisha kwamba haushindwi walau kuanzisha biashara mwaka huu.

    Kweli. Uanzishaji wa biashara ni moja ya hitaji la muhimu sana, muhimu mno ambalo unapaswa kulifanyia kazi ndani ya mwaka huu mpya wa 2023. Pengine kwa siku umekuwa unajipa sababu na kujiambia kwamba mwaka huu nitaanzisha biashara, ila umekuwa huanzishai hizo biashara.

    Kitu kikubw aambacho ninataka kuhakikisha kwamba nimekwakwambia ndani ya huu mwaka mpya ni kuwa biashara ina faida nyingi sana ambazo pengine ulikuwa huzijui, au pengine umekuwa unazijua ila umekuwa unapuuzia. Au pengine siyo tu umekuwa unapuuzia, bali muda mwingine ni  uoga ambao umekuwa unakusumbua.

    Ukiwa na biashara, uwezekano wa wewe kulipwa mara mbili mpaka mara tatu au hata mara kumi zaidi ya unavyolipwa sasa hivi upo. Unaweza kulipwa zaidi ya unavyolipwa sasa hivi, endapo utakuwa na biashara kuliko pale ambapo unakuwa hauna biashara kabisa.

    Kama umeajiriwa utakubaliana na mimi kuwa mshahara wako huwa una ukomo. Yaani, hata ufanyeje kazi, mshahara wako hauwezi kuongezeka.

    Ila kwenye bisahra hali ni tofauti. Kadiri ambavyo unakuwa unaongeza juhudi ndivyo unakuwa unaongeza nafasi yako ya kufanya vizuri zaidi,

    Hivyo basi, rafiki yangu kama kuna kitu ambacho unapaswa kufanya ndani ya mwaka huu wa 2023 ni kuhakikisha kwamba umefungua biashara. Rafiki yangu, uwanja sasa upo wazi kwa ajili yako kufanya makubwa ndani ya huu mwaka wa kipekee wa 2023. Hakikisha kwamba mwaka huu haupiti bila ya wewe kuhakikisha umefungua biashara. Kila la kheri

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

  • Hii ndiyo aina pekee ya malengo ambayo hayatafanikiwa ndani ya mwaka 2023

    Rafiki yangu, najua mwanzoni mwaka huu watu wengi wameweka malengo mengi ambayo watakuwa wakiyafanyia kazi.

    Ila leo hii nipo hapa kukwambia aina moja tu ya malengo ambayo watu wameweka na nina uhakika haya  malengo hayatimia. Malengo haya ni yale malengo ambayo watu wameweka na hawajaanza kuchukua hatua kuyafanyia kazi

    Sifa moja kubwa ya malengo ni kwamba ukishayaweka ni lazima uweze kuyafanyia kazi ili yaweze kuja kwenye uhalisia. Kama mwaka huu, umeweka malengo na bado hujachukua hatua kuhakikisha kwamba malengo yako hayo yanakuja kwenye uhalisia. Basi ujue kwamba malengo hayo hayatakaa yatimie, na hayo ndiyo malengo ambayo hayatafanikiwa kwa mwaka huu wa 2023.

    Rafiki yangu, hakikisha kwamba unaanza kuyafanyia kazi malengo yako ambayo umejiwekea kwa ajili ya mwaka huu wa 2023.

    Melngo makubwa+hatua kubwa=mafanikio

    Kila la kheri.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

  • Viashiria vitano kuwa umeuanza mwaka mpya kwa kishindo

    Rafiki yangu, naomba nichukue nafasi hii kuhakikisha kwamba nakutakia kheri ya mwaka mpya 2023. Kheri ya mwaka mpya rafiki yangu.

    Mwaka huu naamini, utakuwa ni mwaka wako wa kipeke na mwaka wako wa kufanya makubwa. mwaka huu nina hakika ni mwaka ambao hautaremb  mwandiko. Na njia bora ya wewe kutoremba mwandiko ni kuhakikisha kwamba unaanza sasa hivi kufanyia kazi malengo yako bila ya kuchelewa. kwenye makala ya leo, ningepend akuingia kwa undani zaidi na kukueleza viashiria vitano vinavyoonesha kwamba kweli mwaka huu 2023 umeuanza kwa kishindo kikubwa kabisa.

    Kiashiria cha kwanza ni kuweka malengo.

    Kama tayari umeshaweka malengo. Basi hicho ni kiashiria cha kwanza kabisa kwamba mwaka huu umeuanza kwa kishindo kikubwa.

    Watu ambao huwa wanaweka malengo ni wachache sana. tafiti zinaonesha kwamba asilimia tatu tu ya watu ndio huwa wanakuwa na malengo. Yaani, malengo ambayo ni SMART. Unajua malengo SMART ni malengo gani.

    Neno SMART ni neno la kiingereza ambalo linasimama kwa ajili ya vitu vifuatavyo

    • S=Specific. Yaani, kwamba lengo lako ni lengo ambalo linaeleweka. Yaani, unapoweka lengo, wewe mwenyewe unapaswa kuelewa ni kitu gani unataka. Kinachowakwamisha watu wengi kikiwa kitu cha kwanza ni kuwa wenyewe huwa hawajui ni kitu gani ambacho wao wanataka.

    Lengo lako linapaswa kueleza kwa uhakika hasa ni kitu gani ambacho unataka, mpaka rangi ya hicho kitu.

    Lengo lako linapaswa kuwa linaeleweka kiasi kwamba akilisoma mtoto wa miaka sita, anapaswa kulielewa na kuweza kumweleza mtoto mwenzake wa miaka sita akaelewa.

    • M= Measurable. Lengo lako linapaswa kuwa linapimika. Ninaposema kwamba lengo linapimika nnamaanisha kwamba unaweza kupima na kuona kama unaelekea kwenye lengo lako au la!

    Mwishoni mwa mwaka jana, nilikuwa nikiwasiliana na rafiki zangu wengi, huku nikiwauliza ni nini malengo yao makubwa ndani ya mwaka 2023? Mmoja aliniambia kwamba lengo langu ni kufanya zaidi. Kufanya zaidi maana yake nini?

    Kufanya zaidi siyo lengo ambalo linapimika. Kama mwaka jana ulikuwa unakimbia mita 100. Mwaka huu ukikimbia mita 101 si utakuwa umefanya zaidi?

    Kama mwaka jana ulikuwa huweki akiba, mwaka huu ukianza kuweka shilingi mia moja si utakuwa umefanya zaidi. lengo lako linapaswa kuwa linapimika.

    Kwa mwaka huu wote ninaenda kuweka akiba ya shilingi laki mbili kila siku. Hilo ni lengo linapimika.

    Kwa mwaka huu wote ninanenda kuwa naandika makala yenye maneno 1500 kila siku. Hili ni lengo jingine ambalo linapimika.

    Kwa mwaka huu wote ninaenda kuwa naongea na wateja hamsini kila siku kwa simu. Hili ni lengo jingine ambalo linapimika.

    Siku ambayo unafikia lengo lako unajua. Na siku ambayo unakuwa hujafikia lengo unajua.

    Ila ukisema niteboresha biashara yangu. Sasa unaenda kuwa unaboresha nini kwenye biashara yako? Ukiongeza hata mfuko wa pipi mmoja si utasema umeboresha?

    Ila ukisema kwamba biashra yangu ina mtaji wa milioni 70. Mwaka huu, ninakuza mtaji wangu mpaka milioni 200 hapo sasa ndio unakuwa umeweka lengo linalopimika? Sijui unanielewa?

    • A= attainable. Moja ya kitu ambacho pengine hukijui ni kwamba watu wengi huwa wanaweka malengo makubwa sanasana kwa mwaka mmoja huku wakiweka malengo madogo ya miaka mingi ijayo. Mtu anataka akamilishe na kufanikisha kila kitu masiahani mwake ndani ya mwaka mmoja. Rafiki yangu, ninachotaka kukwambia ni kwamba, malengo yako ya mwaka mmoja yawe makubwa na ambayo yatakusukuma kufanya vitu zaidi ya vile ulivyokuwa umezoea.
    • R=Relevant., hapa maana yake malengo yako makubwa yanapaswa kuendana na ndoto zako kubwa za mbeleni au kazi au  biashara. Usiweke tu malengo ilimradi umeweka malengo
    • T= Lengo lako pia linapaswa kuwekewa ukomo wa muda. Yaani, lini unataka lengo liwe limekamika. Yaani, hakikisha umeweka lengo lako katika namna ambayo ineonesha lini ungependa kuwa umefikia lengo lako.

    Andika kufikia tarehe………..ninamiliki…….

    Kama umeuanza mwaka wako kwa kuhakikisha kwamba una malengo ambayo ni SMART, hicho ni kiashiria kuwa umeauanza mwaka wako kwa ushindi

    Kishiria cha pili kuw umeuanza mwka wako kwa ushindi ni kuwa umeshaanza kufanyia kazi malengo yako. Rafki yangu, ikumbukwe kwamba kuweka malengo ni kitu kimoja ila kufanyia kazi malengo ni kitu kingine kabisa. hivyo, basi kama unataka kujua kama kweli umeuanza mwaka wako kwa ushindi ni mpaka pale utapokuwa umeweza kuanza kufanyia kazi malengo yako.

    Kuweka malengo ni kitu kimoja, ila kufanyia kazi malengo ni kitu kingine.

    Na watu wengi huwa wanaweka malengo, ila wachache sana ndio huwa wanachukua hatua ya kuhakikisha kwamnba wamefanyia kazi malengo yao na kuyaleta kwenye uhalisia. Rafiki yangu, usiwe mtu ambaye anaweka malengo tu bila ya kuyafanyia kazi. weka malengo kisha anza kuyafanyia kazi.

    Kama ulikuwa hujaanza kufanyia kazi malengo yako anza leo hii. na siyo lazima ufanye kitu kikubwa sana ndani ya siku moja.

    Unaweza kuanza kidogokidogo kwa kuchukua hatua ndogondogo ambazo utaanza kufanyia kazi. ndio maana nakushauri sana uweze kusoma kitabu changu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA.

    Hiki kitabu kitakufaa sana rafiki yangu

    Hiki ni kitabu ambacho kimesaidia wengi ndani ya mwaka 2022. Kitakusaidia na wewe kufanya makubwa ndani ya mwaka 2023.

    Pata nakala ya kitabu hiki leo hii.

    Gharama ya kitabu ni 20,000/-

    Kama upo nje ya mkoa wa Morogoro, utaongeza gharama ya usafiri ili kutumiwa kitabu.

    Kiashiria cha tatu kuwa umeuanza mwaka wako kwa ushindi ni  kama unafuatilia maisha yako zaidi ya unavyofuatilia maisha ya watu wengine.

    Kuna watu huwa wanapenda kufuatilia maisha ya watu wengine kuliko wanavyokuwa wanafuatilia maisha ya watu wengine. Unawakuta mtandao ni wakiwa wanafuatilia labda maisha ya msanii fulani au mtu fulani. Lakini wanachosahau ni kuwa wao wenyewe wana mambo mengi ya kufuatilia juu yao wenyewe. Hivyo, basi ili mwaka wako uweze kuwa wenye baraka n yingi na mafanikio makubwa unapaswa kuhakikisha kwamba unajifuatilia wewe mwenyewe kuliko ambaavyo unamfuatilia mtu mwingine.

    Jenga utaratibu wa kujifuajtilia wewe mwenyewe ndani ya huu mwaka kuliko ambavyo unamfuatilia mtu mwingine.

    Kila siku asubuhi weka orodha ya vitu ambavyo unaenda kufanya ndani ya siku husika.

    Kisha baadaye jioni, hakikisha kwamba unajifanyia tathmini kuona ni kwa namna gani umeweza kufanyia kazi orodha ya vitu ambavyo ulipanga asubuhi. Kwa kufanya hivyo, utaona wapi umeweza kufanya vizuri na wapi hukuweza kuafanya vizuri, lakini hilo litakupa picha na kukuonesha ni wapi ambapo unapaswa kubadili kwenye maisha yako ili kufanya maisha yako kuwa bora sana.

    Kiashiria cha nne kuwa umeuanza mwaka wako kwa kishindo ni kujikukumbusha malengo yako kwa kuyasoma walau mara mbili kila siku.

    Unapoweka malengo, unapaswa kujenga utaratibu wa kuyarudia kuyasoma pia kila mara.

    Unafanya hivyo kwa lengo la kuifanya akili yako, ijenge ione kwamba inaweza kufikia lengo lako na linawezekana vizuri sana bila ya shida yoyote ile.

    Kiashiria cha tano ni kuwa tayari umeshaanza kujifunza kitu kuhusiana na lengo lako. Rafiki yangu, kama kuna kitu muhimu sana ambacho haupaswi kusahau ni kwamba usisahau kujifunza na kujiendeleza zaidi kuhusuaiana na lengo lako.

    Kwa mfano, una lengo la kuwekeza kwenye hisa mwaka huu. unapaswa kuanza mara moja kujieleimisha kuhusiana na elimu ya hisa. Na kwa kuanzia unaweza kupata kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE ambacho kitakusaidia sana kwenye hili.

    Au pengine una lengo la kuanzisha kilimo cha samaki. Hapa unahitaji pia kuhakikisha kwamba unaaanzakujiendeleza kielimu kuhusiana na elimu ya kilimo na ufugani wa samaki.

    Haya ni mambo machache sana ambayo unapaswa kuhakikisha kwamba unayafanyia kazi na kuyuaeta kwenye uhalisia.

    Kujifunza ni jambo ambalo haliepukiki hasa kama umeweka malengo makubwa na unataka kufakika mbali ndani ya mwaka 2023. Rafiki yangu, malengo makubwa yanahitaji ujifunze na ufanyie kazi kile unachojifunza.

    Kiashiria cha ziada, umebadilli tabia zako. Yaani, kuna tabia ambazo najua unazo. Na tabia hizo haziwezi kukusaidia wewe kufanikisha malengo yako. Rafiki yangu, kama unataka kuhakikisha kwamba umeweza kufanikisha malengo yako ndani ya mwaka 2023, basi hakikisha kwamba unabadili tabia zako. niambie tabia zako, nami nitakwambia kama utawza kufanikisha malengo yako au la!

    Una lengo la kupunguza uzito, ila bado hujaacha tabia yako ya kula hovvyohovyo? Una lengo la kuweka akiba ila bado unahonga? Una lengo la kuongeza kisomo ila bado unazembea kusoma.

    Una lengo la kuanzisha biashara ila hata hujifunzi kuhusiana na biashara?

    Rafiki yangu,  hizi tabia unapaswa kuhakikisha kwamba unaziiishi ndani ya mwaka 2023 ili kupiga hatua. Na kama unavyoona. Wengi walitamanani kusikia nikiwambia kwamba kama ulikseha usiku kuusubiri mwaka mpya, basi umeuanza mwaka wako kwa ushindi.

    Au wengine walitaka niwaambie kwamba kama umeuanza mwaka wako kwa kuchati sana hapo umeuanza kwa ushindi. Kiufupi utakuwa umeuanza mwaka wako kwa ushindi kama umefanyia hivyo vitu vitano ambavyo nimekwambia kwenye makala ya leo.

    Bila kuongeza la ziada, mimi naishia hapo

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

  • Nimepata kusoma kitabu cha THE YOUNG INVESTOR (Projects and activities for making your money grow)

    Hiki ni kutabu cha uwekezaji ambacho kimeandaliwa maalumu kwa ajili ya watoto, kinalenga kuwafundisha watoto juu ya uwekezaji na namna gani wanaweza kuanza kufanya uwekezaji.

    Hata hivyo mtu mzima kama wewe unaweza (na unapaswa) kukisoma kitabu hiki pia. Na kwa kuwa lugha iliyotumika kwenye hiki kitabu ni lugha rahisi kwa ajili ya kuwafanya watoto waelewe, wewe mtu mzima ukisoma kitabu hiki, utakielewa zaidi.

    Kitabu ni kidogo tu, kina kurasa kama 124 hivi, hivyo unaweza kukisoma ndani ya wiki moja kikaisha. Binafsi nimekisoma na kukielewa.

    Kuhusu mwandishi wa kitabu hiki
    Mwandishi wa kitabu hiki ni Katherine R. Bateman. Mwandishi ameandika kitabu hiki kwa ajili ya wajukuu wake. Anasema kwamba alikuwa na shauku kubwa ya kuwafundisha wajukuu wake kuhusu uwekezaji.

    Hivyo alianza kukusanya taarifa kwa ajili ya wajukuu wake, kila alipokuwa   anaongea na watu juu ya hilo, jibu alilopata kutoka kwa watu lililuwa kwamba akishaandika kitabu awataarifu wanunue nakala pia.

    Hili jambo lilimfanya mwandishi ahakikishe anaandika kitabu kinakamilika.

    Sasa hapa ningependa kukwambia yafuatayo ambayo nimejifunza kutoka kwenye kitabu.

    1. Kitu cha kwanza ambacho ningependa na wewe uondoke nacho ni kuwa na wewe utapaswa kuandika kitabu. Siyo lazima kiwe cha fedha kama hiki, lakini unaweza kuandika kitabu kinachoendana na ujuzi wako. Nakuhakikishia wanao na wajukuu wako watakipenda kitabu hicho. Kama wewe umekuwa mwanakwaya kwa miaka sasa, ebu hata tuandikie kuhusu safari yako ya kuimba, najua una mengi ya kuandika. Kama bado unakwama uandike nini, hakikisha unapata kitabu changu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU (kwa saaa softcopy ni 5,000/).

    2. Hisa siyo makaratasi tu, na wala siyo cheti unachopata baada ya kununua hisa. Bali ni umililiki wa kampuni.

    3. Unapaswa kutawanya uwekezaji wako kwenye maeneo tofautitofauti. Kwenye hisa, hatifungani pamoja na vipande.

    4. Kama kuna kampuni unapenda kutumia bidhaa zake, hakikisha unanunua hisa zake pia.

    Kitabu kina mambo mengi, binafsi nimeandika machache tu kwa sababu nilitaka niweke kumbukumbu kuwa niliwahi kusoma kitabu hiki. Na njia ya mimi kuweka kumbukumbu ni kuandika makala kama hii hata kama ni fupi

    Ili unufaike na kitabu hilo, hakikisha unakisoma mwenyewe.
    Kipakue mwenyewe kwa kufuata mwongozo huu hapa

    Karibu sana

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

    Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA

X