Home


  • JINSI YA KUANZA UPYA BAADA YA KUANGUKA

    Huwa inatokea mtu anaanza kitu unakikuza lakini inafikia hatua ambapo unapata anguko na kurudi chini. Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha kuanguka, ikiwa ni pamoja na kupumzika kwa nguvu baada ya kuwa umefika juu. Au inaweza kutokana na sababu kuwa mwanzoni ulikuwa na lengo kubwa, ila baada ya kuwa umefikia juu au baada ya kuwa umefikia hilo lengo, sasa umekosa lengo kubwa zaidi.

    Unakuta labda mtu ana lengo la kujenga nyumba, na kuitunza familia yake. Anapambana, anafikia hatua ambapo anapata hela ya kutosha kumwezesha yeye kujenga na kuitunza, sasa mtu huyu unakuta analala na kujisahau, sasa kitu hiki, na mwingine ni ile hali ya kupokea fedha nyingi kwa wakati mmoja. Anakuwa hajui namna ya kuzitunza na kuzitumia vizuri, anazitumia hovyo, mwisho wa siku, anaingia mkenge.

    Sasa leo nataka nikueleze ni kwa namna gani unaweza kuanza upya baada ya kuanguka.

    Lakini kabla sijakwambia hiyo, nataka nikwambie hauko peke yako. Kiuhalisia ni kwamba watu wengi huwa wanaanguka. Hakuna mtu ambaye huwa anaanzisha kitu na kukifanikisha moja kwa moja bila kupitia anguko lolote. Laiti kama maisha yangekuwa hivi, basi ni wazi kuwa kila mmoja angekuwa amefanikiwa sana.

    Maisha ni kama huwa yana tabia ya kumjaribu mtu kuona kweli huyo mtu yuko siriazi na mafanikio anayoyataka? Yupo siriazi kweli.  Na hapo ndipo kushindwa hutokea, ila kushindwa kwa kawaida siyo kushindwa, kushindwa ni fursa.

    Leo hii nataka nikuoneshe namna gani unaweza kuanza upya baada ya kuwa umeanguka.

    Kitu cha kwanza kabisa kama umeanguka ni wewe kujua kwa nini umeanguka. Jiulize, hivi imekuwaje mpaka nimeanguka wakati nilikuwa juu kabisa. halafu hizo sababu zitunze vizuri ili zisije zikakuangusha tena baadaye, maana ukifuatilia, vitu ambavyo huwa vinawaangusha watu ni vile vile. Hivyo, ukijua kilichokuangusha  wewe, hata ukianza upya utakiepuka.

    pili, kama umeanguka, hakikisha sasa unaweka mipango mipya ya kule unapotaka kwenda. Anzia palepale ulipo. Kisha endelea kusonga mbele. Unaweza kufika unapotaka na hata zaidi ya hapo. ubora ni kwamba kama ulishawahi kufika juu ukaanguka, unajua mchakato wote wa kufika huko. Na zamu hii itakuchukua muda kidogo zaidi maana mbali ya kuwa unaanzia chini, ila kuna baadhi ya vitu ulishavijenga tanagu mwanzoni ambavyo utavitumia sasa. mfano, vitu kama konekisheni, hata kama ulianguka, haimaanishi kuwa na konekisheni zako zote zilianguka. Kuna konekisheni ulizonazo sasa hivi, ambazo unaweza kuanza kutumia ili kusonga mbele.

    Tatu penda kujifunza. unapaswa kuzama zaidi kwenye kujifunza ili upate maarifa yatakayokusaidia wewe kuinuka na kusongambele. Kama ambavyo nilikudokeza ni kuwa makosa ambayo watu wanafanya na kuwaangusha siyo kwamba ni mapya, ni makosa ambayo yamekuwa yakifanyika enzi na enzi, tokea enzi za mababu zetu. Ila tatizo ni kwamba watu hatujifunzi.

    Mfano kama mahusiano yako yanaenda vibaya, haimaanishi kwamba, hilo tatizo linalokukumba wewe ni la kipekee na halijawahi kutokea hapa duniani, unachopaswa kujua ni kuwa limewahi kutokea na kuna watu wengine wamewahi kupitia kwenye hali mbaya zaidi ya kimahusiano kuliko hata wewe hapo. ila waliweza kutatua hiyo changamoto.

    Tatizo lako ni kwamba hujifunzi na hupendi kusoma vitabu. na ndio maana unaendelea kurudia makosa yaleyale waliyofanya wengine, na kitu hiki kitakufanya uendelee kuanguka zaidi. Penda sana kujifunza.

    Jifunze kuhusu biashara

    Jifunze kuhusu mahusiano

    Jifunze kuhusu fedha na mambo mengine ambayo unaweza kujifunza.

    Kuanguka chini siyo tiketi ya wewe kutojifunza au kuwekeza kwenye vitabu. kuanguka chini kunapaswa kuwa ni tiketi yako ya kuanza upya, na tena zamu hii ukianza upya unapaswa ukue bila kurudi nyuma mpaka watu washangae.

    Nne, jenga utaratibu wa kujifanyia tathimini kila mwezi , kila wiki na kila siku. Jiulize, hivi kweli nazidi kusongambele au ndio narudi nyuma. Kutojifanyia tathimini kunaweza kukufanya uanguke chini, kwa sababu kila mara utakuwa unajiona kama uanafanya vitu vinaenda sawa, ila kumbe kuna sehemu unakosea. Unaona ee. Hivyo, kila mara jiulize hivi kweli nipo kwenye njia sahihi? Hivi ni kweli nazidi kusongambele kama ninavyostahili au ndio narudi nyuma?

    Jifanyie tathimini mara kwa mara.

    Hii itakusaidia kwanza kuwekeza vitu na nguvu zako kwenye vitu vichache unavyoweza kufanya kwa ustadi.

    NB. Tumeanza kusambaza vitabu vya jinsi ya kufikia ndoto zako. nakala ngumu (hardcopy). Kitabu hiki kinatumwa popote pale ulipo Afrika Mashariki. Hakikisha unapata nakala yako leo hii kwa bei ya punguzo. Yaani badala ya 20,000/- unapata nakala yako kwa 15,000/- tu. Mwisho wa kupata kitabu kwa bei ya oda ni tarehe 20. Jionee mwenyewe chini hapa muda uliobaki kupata nakala kwa bei hiyo hapo chini

    [wpcdt-countdown id=”5798″]

    Umekuwa nami,

    Godius Rweyongeza

    0755848391

    Kwa maoni, ushauri au maswali: godiusrweyongeza1@gmail.com au info@songambele.co.tz

    For bookings: songambele.smb@gmail.com au songambele@songambele.co.tz

  • Unafanyaje ili kupata mbia sahihi wa biashara

    Leo nataka tuongeelee kuhusu ubia wa biashara. Ikiwa ni moja ya kitu muhimu sana kwenye biashara ambacho unakihitaji hasa kama umelenga kufika mbali. Ubia kwenye biashara unakutanisha watu wenye ujuzi, elimu na hata fedha ambapo wanaungana kutengeneza kitu kimoja. Kwenye biashara ubia ni muhimu sana hasa kama unataka kufika mbali.

    Kitu kikubwa unachohitaji kujua kuhusu biashara ni kwamba biashara ni mchezo. Na kama mchezo, una kanuni na taratibu zake, hivyo unapaswa kuzifuata hizi kanuni na taratibu za biashara au kwa manufaa yako, au la unapaswa kuzivunja kwa hasara yako pia.

    Sasa vifuatavyo ni vitu muhimu unavyohitaji kujua kuhusu mbia wako.

    Kwanza unahitaji kumjua mbia wako vizuri.  Hiki kitu ni muhimu sana kwenye biashara kutokana na ukweli kuwa huyu mtu unaenda kufanya naye kazi kwa muda mrefu.Ni mtu ambaye ambaye mnaenda kujenga kitu kikubwa, hivyo, unahitaji kumjua vizuri huyu mtu wako

    Pili fahamu kuwa mbia wako siyo lazima awe mtu mwenye fedha nyingi sana, siyo mtu mwenye ushawishi mkubwa, siyo mwanasiasa, mwenye jina kubwa au mtu wa aina hiyo. Mbia wako ni mtu kama wewe ambaye mnaweza kuendana kwenye kufanyia kazi kile unachofanya. Kikubwa awe ni mtu ambaye mnaweza kuendana kwenye biashara yenu.

    Tatu, Mbia wako awe na ujuzi ambao unaweza kujazilia kwenye kile ulichonacho wewe na yupoo tayari kufanya kazi kwa bidii, naam bidii sana.

    Nne, Usivunje makubaliano uliyowekeana na mbia wako hata kama utagudua kuwa ule ubia mlioweka, kuna hila fulani zilifanyiaka wakati mnaweka huo ubia. Badala ya kwenda kinyume na makubaliano, utapaswa kumwita ili mkae chini na kuweka sawa kile ambacho unaona kwamba hakijakaa sawa.

    Kwa leo nimeona nikushirikishe hayo mambo machache kuhusu ubia na namna ambavyo unaweza kuutumia ubia kwa manufaa.

    NB. Tumeanza kusambaza vitabu vya jinsi ya kufikia ndoto zako. nakala ngumu (hardcopy). Kitabu hiki kinatumwa popote pale ulipo Afrika Mashariki. Hakikisha unapata nakala yako leo hii kwa bei ya punguzo. Yaani badala ya 20,000/- unapata nakala yako kwa 15,000/- tu. Mwisho wa kupata kitabu kwa bei ya oda ni tarehe 20. Jionee mwenyewe chini hapa muda uliobaki kupata nakala kwa bei hiyo hapo chini

    [wpcdt-countdown id=”5798″]

  • Ukifanya kitu unachopenda Ubunifu unakuwa mwingi.

    …….muda si mrefu nimetoka kuongea na mteja wetu mmoja ambaye yuko mkoani Mara (Msoma mjini).
    Ambaye amepokea kitabu Cha jinsi ya kufikia NDOTO ZAKO na kuanza kukisoma.

    Kitu cha pekee nilichopenda kutoka kwake ni usemi wake anaosema kuwa ukifanya kitu unachopenda, Ubunifu unakuwa mwingi.

    Na hiki kitu nimeona nikushirikishe na wewe pia.

    Kuna utafiti unaonesha kuwa watu wengi wanakufa siku ya jumatatu baada ya kula Bata wikendi halafu jumatatu wanaamka na kwenda kufanya kazi wasiyopenda. Hicho kitu tu, kinawakatisha tamaa.

    Ndiyo maana nimeupenda huu usemi, kiasi cha kuwa tayari kukushirikisha huu usemi na wewe.

    Ujumbe mkubwa nilio nao kwako siku ya leo ni kwamba ufanye kazi au kitu unachopenda.

    Ukifanya kitu unachopenda hutachoka
    Ukifanya kitu unachopenda ubunifu unakuwa mwingi.

    Thomas Edison alikuwa analala saa tatu kwenye maisha yake na kuamka mapema kwenda kazini. Siku moja aliulizwa kwa nini unafanya sana kazi.

    Aliwajibu watu kwa kuwaambia kuwa sijawahi kufanya kazi.

    Umeona ee! Alikuwa anafanya kitu anachopenda. Hivyo, kwake hakuona kama hiyo ilikuwa kazi.

    Hivi wewe unafanya unachopenda kweli? Unafanya unachopenda?

    Ngoja nikukumbushe, “ukifanya kitu unachopenda, ubunifu unakuwa mwingi”.

    Kwa jioni ya leo naishia hapa.

    Halafu ujue kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO kipo tayari. Na watu wanapokea nakala zao popote pale walipo. Wewe pia unaweza kupata nakala yako kwa Bei ya oda. Ujue gharama ya kitabu hiki ni 20,000/- Ila habari njema ni kuwa ukilipia kitabu hiki kabla ya tarehe 20 Mei. Utakipata kwa 15,000/- unaanzaje Sasa kwa mfano kukosa nakala yako.

    Ebu nitumie ujumbe wako sasa hivi

    Tuma ujumbe kwa
    0755848391
    Au WhatsApp
    https://wa.me/message/3PMZSAFONLHAP1

    Ili utumiwe kitabu chako.

    Umewkuwa nami
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

    Ukifanya kitu unachopenda ubunifu unakuwa mwingi.

  • Tumebaki Na Siku 3 Tu Za Kupata Kitabu Cha Jinsi Ya Kufikia Ndoto Zako Kwa Bei Ya Oda

    [wpcdt-countdown id=”5798″]

    Hello, habari ya leo. Bila sahaka unaendelea vyema.

    Kwa siku sasa nimekuwa nikikwambia kuhusiana na kitabu cha jinsi ya kufikia ndoto na jinsi ambavyo unaweza kupata nakala yako. Kitabu hiki kinazinduliwa tarehe 20 Mei, hata hivyo, oda zimeshaanza kuwekwa.

    Nikieleza Jambo kuhusu kitabu

    Na ubora ni kuwa nakala za kitabu zimetoka mapema. Hivyo, nimeona badala ya kusubiri mpaka tarehe 20 Mei ndio nitume vitabu. NI bora nianze kutuma nakala sasa hivi, maadam zipo. Kwa hiyo, kila aliyeweka oda ya kitabu na kulipia. Tayari ametumiwa kitabu chake au la anatumiwa leo na wengine vitabu vyao vipo njiani.

    Sasa leo wakati naagalia kwenye tarehe hapa, nikaona kwamba, zimebaki siku chache tu kabla ya tarehe ya mwisho ya wewe kupata kitabu hiki kwa bei ya oda.

    IPO HIVI, kitabu hiki gharama yake ni 20,000/- ila ukiweka oda siku ya leo unaenda kupata kitabu hiki kwa gharama ya 15,000/- tu.

    Sasa kilichobaki rafiki yangu ni wewe kuchangamka ili uweze kupata kitabu hiki.

    Cha kufanya sasa hivi, weka oda yako kwa kutuma ujumbe kwenda namba 0755848391

    Tuma ujumbe wenye jina lako

    Namba yako na mahali ulipo.

    Mfano: Godius Rweyongeza 0755848391 (Morogoro mjini-Morogoro)

    Ukishatuma huo ujumbe utapewa maelekezo ya kulipia, ili uweze kupata nakala yako mapema.

    Karibu sana rafiki yangu, tuko pamoja.

    Audiobook ya kitabu pia ipo

  • Kitu Kimoja Cha Kufanya Kama Hauna Fedha Sasa Hivi


    Chukua hatua. 


     Tafuta bidhaa yoyote unayoweza kuuza. Nenda kwa watu uuze. Unachopaswa kujua ni kuwa fedha zako wanazo watu. Ila huwezi kwenda kwa watu na kuwalazimisha wakupe hiyo fedha. Huo utakuwa wizi au unyang’anyi. Njia bora ya wewe kupata fedha kwa watu ni kuwapa hao watu huduma au bidhaa wanayotaka.


    Zig Ziglar aliwahi kunukuliwa akisema; unaweza kupata chochote unachotaka kama utawasaidia watu kupata kile wanachotaka.


    Huwa napenda kuwaambia watu kuwa matajiri nao wanaomba fedha. Ila hawaombi kama ombaomba wa mtaani, wenyewe wanaomba fedha kwa kukuletea kitu unachotaka. 


    Na wewe anza kuomba fedha kitajiri. 
    Kumbuka: unaweza kupata chochote unachotaka kama utawasaidia watu kupata kile wanachotaka.
    Kila la kheri.

    subscribe pia kwenye channel yangu ya YouTube.

    Umekuwa nami rafiki yako, Godius Rweyongeza. Tuwasiliane kwa 0755848391

    For booking: songambele.smb@gmail.com au songambele@songambele.com

  • Nidhamu ni nini?

    Nidhamu ni kuamua kufanya kitu, bila kujali unajisikia kufanya kile kitu au hujisikii. Matendo yako ya kila siku ndiyo yanaweza kutuambia kuwa una nidhamu kwenye eneo gani na hauna nidhamu kwenye eneo gani. Kwa mfano, kama umejiwekea utaratibu wa kuweka akiba kila siku, na ukaweka akiba kila siku, hapo unakuwa umejijengea nidhamu binafsi.

    Nidhamu ni kitu ambacho kinawatofautisha wanaofanikiwa na wale ambao hawafanikiwi kwenye maisha. Ni kitu kidogo ambacho unahitaji ili uweze kufika mbali kimaisha. Bila nidhamu rafiki yangu, unaweza kuanza na mamilioni ya fedha kwenye maisha na ukayapoteza. Na ukiwa na nidhamu, unaweza kuanza na shilingi kidogo tu, ukazibadili kuwa mamilioni ya fedha.

    Sasa jiulize, je, wewe una nidhamu kwenye kile unachofanya? Una nidhamu kweli?

  • Vitu vinazaliwa, vitu vinakua na hatimaye kuzeeka

    Ni kanuni ya maisha kuwa vitu lazima vinazaliwa, vitu vinakua na hatimaye kuzeeka. Hakuna kitu ambacho kinapaswa kubaki hivyo hivyo, kila kitu kinapaswa kuwa kwenye mwendo muda wote na sehemu zote. kumbe, kuna wakati unaweza kutakiwa kuwa sehemu fulani, ambayo ni sehemu ya chini kwenye mchakato wako wa kupanda, sehemu mbayo pengine wewe kwa upande wako huipendi, ila haipaswi kuwa hivyo, ikiwezekana unapaswa kuipenda kwa sababu, kila kitu kina wakati wake.

    Kama huu ni muda ambao unapaswa kuwa kwenye ngazi fulani, basi kazi kama mtu ambaye yuko kwenyehiyo ngazi, ifanye kazi ukiwa kwenye hiyo ngazi kwa weredi na uaminifu wa hali ya juu. Baadaye kadiri muda unavyoenda utakua na kupanda juu zaidi. hii ni kanuni ya asili.

  • Nguvu Ya Vitu Vidogo Kuelekea Mafanikio Makubwa

    Helo leo ninayo furaha kutambulisha kwako kitabu cha Nguvu ya vitu vidogo kuelekea mafanikio makubwa. Ni kitabu cha kipekee sana. kabla sijasema mengi kuhusu kitabu hiki, nataka nikupe kwanza utangulizi wa kitabu ili uweze kuuusoma. Karibu

    Hivi umewahi kujiuliza kuwa vitu vidogo vinaweza kukusaidia kitu gani maishani mwako?

    Hivi kwa mfano, kitu kidogo kama kuamka asubuhi na mapema kinaweza kukusaidia nini maishani mwako kikifanywa kila siku na kwa mwendelezo? Au je, kitu kidogo kama kuwekeza au kuweka akiba kikifanywa kila mara kwa muda mrefu kinaweza kukusaidia nini? Kwenye kitabu hiki hapa tunaenda kuona nguvu ya vitu vidogo na jinsi nguvu hii inavyoweza kukusaidia wewe kufikia mafanikio makubwa maishani mwako.

    Mara nyingi sana watu huwa wana ndoto kubwa na malengo makubwa ya kufikia kifedha, kimahusiano, kibiashara au kikazi. Lakini cha kushangaza ni kwamba huwa hawafanyii kazi hizo ndoto kubwa walizonazo bali huwa wanasubiri itokee siku moja ya muujiza ambapo ndoto yao itatimia kwa asilimia zote.

    Kitu kama hiki hapa hakiwezekani. Ni wazi kuwa lengo lako la mwaka haliwezi kutimia siku ya mwisho ya mwaka baada ya wewe kuwa umekaa mwaka mzima bila ya kufanya kitu chochote, badala yake kama kweli utaweka kazi na kufuata hatua zote unazopaswa kufuata ili kulifikia hilo lengo lako la mwaka basi utalifikia kwa kufanya vitu kidogo kidogo kila siku.

    Kitu chochote kikubwa kinaweza kufanikishwa kwa kuchukua hatua ndogondogo na kwa mwendelezo na hatimaye kuzifanya ziwe hatua kubwa. Mafanikio makubwa siyo kufanya vitu elfu moja mara moja, ila kufanya vitu vidogo mara elfu moja, yaani, kwa mwendelezo na bila kuchoka. Hivi vitu vidogo hatimaye vinapelekea kitu kikubwa na mafanikio makubwa.

    Confucius, mwanafalsafa wa Kichina aliwahi kunukuliwa akisema kwamba, “safari ya maili elfu moja huanza na hatua moja”. Hii ndiyo kusema kwamba mambo makubwa siku zote huwa yanaanza kwa hatua ndogondogo kisha kuendelea kukuzwa. Hakuna kitu kikubwa ambacho unakiona leo hii ambacho kilianza kikiwa kikubwa hivyohivyo. Ndiyo maana wahenga walisema kwamba; “hata mbuyu ulianza kama mchicha.” Jogoo anayewika kuna siku alikuwa kifaranga.

    Ukitaka kugundua kwamba vitu vikubwa huanza kwa udogo basi unaweza kuangalia ujenzi wa ghorofa. Huwa unaanza kwa hatua ndogo ndogo za kuchimba msingi, baadaye huwa wanaanza kuweka jiwe au tofali moja baada ya jingine hatimaye kitu kilichokuwa chini huwa kinaendelea kusimama na kufikia hatua ya kuwa kitu kikubwa sana.

    Siku moja nilikuwa nasoma historia ya jengo ambalo limo kwenye maajabu saba ya dunia. Jengo hili siyo jingine bali ni jengo la Taj Mahal. Hili ni miongoni mwa majengo yaliyojengwa kwenye karne ya 15, na jengo lenye historia ndefu na kubwa sana. Unajua jengo hili lilijengwa kwa miaka mingapi? Unaweza kuwa sahihi. Lilijengwa kwa miaka ishirini na mbili (22). Kila siku watu walikuwa wanaweka tofali moja, siku nyingine tofali jingine, siku nyingine nondo, hatimaye lile jengo lilikamilika baada ya miaka 22!

    Wajenzi hawakusubiri mwaka wa 22 ili wajenge hilo jengo. Ila walikuwa wakilifanyia kazi hilo jengo hatua kwa hatua kila siku bila kuchoka. Hili nalo litupe picha ya kuwa vitu vikubwa vinawezekana kufanyika na kuja katika uhalisia endapo vitafanyiwa kazi kwa kuanza kidogo kidogo, na kwa mwendelezo na kupewa muda ili viweze kuanzia chini na kukua.

    Usidharau vitu vidogo. Kuna mfano, wa nyuki aliyeingia kwenye sikio la tembo na kuanza kupiga kelele. Tembo yule alianza kuruka huku na kule ili nyuki yule atoke kwenye sikio lake ila nyuki hakutoka. Tembo alianza kuangusha miti na kujibamiza kwenye miti pengine akidhani kwamba huyo nyuki atatoka ila huyo nyuki hakutoka. Baada ya muda mrefu wa kuhangaika, tembo alianguka na hivyo akawa amepoteza maisha. Kinaweza kuonekana kama kitu cha kushangaza, ila vitu vidogo muda mwingine huwa vina madhara makubwa sana.

    Mbu ni wadogo, ila madhara yake ni makubwa. Sindano ni ndogo sana ila ikikuchoma, wewe mwenyewe ni wazi kuwa utakipata cha mtema kuni. Kwa hiyo basi, nikuombe kuwa ujenge utaratibu wa kuheshimu vitu vidogo maana vinaweza kukupelekea kwenye mafanikio makubwa au la vikakupelekea kwenye anguko kuu maana kuna nguvu katika vitu hivi vidogo. Nguvu hii inaweza kukuinua ukiitumia vizuri ila ukiitumia vibaya itakuangusha. Na nguvu hii ndiyo tunaenda kuiona kwenye kitabu hiki hapa.

    Endapo utakisoma kitabu hiki na kuanza kufanyia kazi yale utakayojifunza, sipati picha jinsi ambavyo utaanza kujenga six packs ambazo umekuwa unatamani kwa siku nyingi, akiba utakayoweka, vitabu utakavyoweza kuandika, utakavyoweza kukamilisha majukumu yako kwa wakati, jinsi utakavyoboresha mahusiano yako na mengine mengi.

    Kila la kheri

    Godius Rweyongeza

    Februari 15,2020

    Morogoro-Tz

  • Kama haupo tayari kupoteza, hautaokota

    KUNa wakati unahitaji upoteze kitu ili uweze kupata kitu. Kama haupo tayari kupoteza usitegemee kuokota.

    Kama hauko tayari kupoteza mbegu za mahindi, usitegemee kwamba unaenda kuvuna mahindi.

    Nadhani hii inaenda vizuri na ule usemi wa kihenga unaosema kwamba mtaka cha uvunguni sharti ainame. Au ule usemi wa kuwa mficha uchi hazai

    Sasa swali ni kwako ni kitu  gani upo tayari kupoteza kwa sasa ili uweze kunufaika kwa hapo baadaye.

  • Audiobook ya kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO hii hapa

    Habari ya upande wa huko rafiki yangu. bila shaka kila kitu kinaenda vyema kabisa. Leo hii nina furaha kukutaarifu kuwa kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO, kina audiobook yake pia.

    Audio hii itaanza kupatikana kuanzia mei 20, 2022.

    hata hivyo, leo hii nina sample kidogo tu kukuonjesha.

    unaweza kuisikiliza hapa.

    ukimaliza kuisikiliza, usiache kuweka oda ya audiobook au kitabu chenyewe.

    kitabu kinauzwa 20,000. ila ukiweka oda unakipata kwa shilingi 15,000 tu.

    audio inauzwa kwa 15,000 ila ukiweka oda unaipiata kwa 10,000 tu.

    chaguo ni lako, chagua kimoja kati ya hivyo, kisha nitumie ujumbe. tuma ujumbe wa kuweka oda kwenda namba 0755848391. Karibu sana.

X