Home


  • Je, Kuna Namna Na Kutengeneza Fedha Kupitia Affiliate Marketing Ukiwa Nchini Tanzania?

    Habari ya huko upande wa pili. Mimi kutokea hapa mkoani Morogoro naendelea vizuri tu.

    Siku ya leo napenda kujibu swali la mmoja wetu hapa kwenye jukwaa ambaye ameniuliza kama kuna namna ya kutengeneza fedha kupitia affiliate marketing ukiwa hapa nchini Tanzania.

    Na mimi kwa ufupi napenda kusema kwamba INAWEZEKANA.

    Ila naomba usome ujumbe huu mpaka mwisho, ili uweze kuelewa hii dhana ya affiliate marketing kwa undani.

    Kwanza kabisa tujibu swali la inawezekanaje?

    Kwa hiyo kama kozi inauzwa kwa gharama ya laki moja. Punde tu baada ya hiyo ebook kununuliwa kwenye akaunti yako utaingiziwa elfu kumi ambayo unaweza kuitoa hapohapo au ukasubiri iongezeke pale watu watakaponunua kozi au ebooks zaidi kupitia kwako .

    Kwa hiyo kama wewe ukiitangaza na mtu akainunua kupitia link maalumu ya affiliate marketing ambayo ni ya kwako. kikiuzwa tu, unapata elfu moja hapohapo bila ya kuchelewa.

    Kadiri utakavyouza kitabu kwa watu wengi zaidi ndivyo utakavyopata kiasi kikubwa zaidi…

    Nadhani upande huo umeisha…

    Ukitaka kujua namna ya kutengeneza akaunti ya affiliate marketing, unaweza kuangalia video hii hapa chini

    Sasa hapa nataka niongee kitu, ambacho ni zaidi ya kutengeneza akaunti.

    Mpaka hapa umeshajua kwamba inawezekana wewe kutengeneza akaunti ya affiliate marketing, na umeshajua kwamba unaweza kupata hela kwa njia hii.

    Sasa kifuatacho nataka nikwambie kwamba, unapaswa kukifanya kwa uendelevu. Kwa miaka ambayo nimekuwa naandika na kuuza vitabu, nimegundua kwamba huwezi kumwambia mtu mara mmoja kwamba una kitabu akanunua, kuna watu ni wagumu kununua. Na hili siyo kwenye vitabu tu, lakini pia kwenye karibia kila bidhaa kutoka kwenye kila sekta. Ndio maana kampuni za magari zinajitangaza kila siku. Ndio maana kampuni za simu zinajitangaza kila siku pia. Kwa sababu kuna watu hawachukui hatua mara moja.

    Hivyo, basi, kama unategemea kuingiza kipato kwa hii njia, hakikisha kwamba, unatangaza na kuwakumbusha watu wako mara kwa mara ili waweze kununua na hatimaye wewe uweze kuingiza kipato kizuri tu.

    Pili ni kwamba, tangaza bidhaa ambazo ni nzuri kwa watu wako, ili wakinunua hizi bidhaa, mwisho wa siku waweze kurejea kwako kujua bidhaa gani zaidi wanaweza kununua, na hivyo uendelee kutengeneza pesa kupitia hao watu kwa mara nyingine.

    Tatu, weka mpaka utaratibu wa kuwaelimisha watu wako. Ili kupitia elimu unayotoa, watu wahamasike na waweze kuchukua hatua, kitu kitakachopelekea wewe kupata kiasi fulani cha fedha.

    Mpaka wakati mwingine, mimi sina la ziada

  • Songambele

     
    Rafiki yangu, muda wote na mara zote unapaswa kuwa mtu wa kusonga mbele. Usikubali kukwama na wala kubaki eneo lile bila ya kusongambele.

    Vitu ambavyo vinakaa sehemu moja bila ya kusongambele huwa vina sifa mbaya kweli.
    Maji yaliyotuama, ndio huwa yanazalisha mbu wa malaria. Hata mdomo wako ukiufunga bila kuongea kwa muda mrefu unatoa harufu mbaya.

    Kwa kawaida asili haipendi kitu kikae bila ya kuwa kwenye mwendo. Ndio maana dunia linajizungusha kwenye mhilimi wake kila sekunde, matokeo yake ni usiku na mchana pamoja na majira (kiangazi, vuli, kipupwe..)
    Ardhi ikikaa bila ya kupandwa kitu, utakuta kwamba ndani yake yanaota majani (magugu)
    Hata watalaam wa afya hawashauri ukae eneo moja bila kuzunguka na kule.
     
    Kwa hiyo, mara zote jiulize unapiga hatua? Unafanya  kitu cha kukufanya usonge mbele.
    Usikubali kubaki eneo moja ukiwa umetuama kama maji…songambele la sivyo utazalisha mbu wa malaria.

    Waingereza nao wana usemi wao, unaosema kwamba the idle  mind is the devils workshop. Ukimaanisha kuwa akili inayokaa bure ni karakakana ya shetani.

    Sasa wewe unataka akili yako ichezewe na shetani..ukiona unakaa bila ya kufanya kitu, ujue kwamba unakaribisha shetani. Kwa hiyo badala yake songambele.
     
    Nipo najiuliza ni kitu gani kinakuzuia wewe kusonga mbele? Je, ni kwa sababu huna mtaji? Je, ni kwa sababu ni kwa sababu unajiuliza kuhusu wazo lako la biashara ni bora au siyo?
     
    JIFUNZE ZAIDI: USIISHIE TU KUKAA KWENYE KOCHI NA KUSEMA ONE DAY YES

    Kumaliza tatizo hilo, nimekuandalia ofa ya vitabu vitatu kwa gharama ya elfu 12,000 tu. Hii ni ofa ambayo nadhani itakuwa ya mwisho mwisho kwa mwaka huu. siriaz! Unaweza usipate ofa nyingine kutoka kwangu mpaka mwaka huu unaisha. Kwa hiyo cha kufanya, ni wewe kuhakikisha kwamba unaichangamkia.
    Tuma 12,000/- leo nikutumie ebooks tatu ambazo

    MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA

    NGUVU YA WAZO (the Powe Of An Idea): Jinsi wazo linavyoweza kubadili dunia pamoja na

    KIPAJI NI DHAHABU: Jinsi ya kukigundua, kukinoa na kutumia kipaji chako.

    Hizi ni ebooks tatu za kipekee sana kutoka kwangu ambazo zenye thamani kubwa sana ambazo unaenda kupata kwa bei ya ofa. Nadhani hii inaweza kuwa miongoni mwa ofa zangu za mwisho kabisa kwa mwaka huu. ichangamkie sasa…
     
    Mpaka wakati mwingine, mimi ni Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • Fedha Chanzo Chake Ni Thamani

    Wachezaji Lionel Messi na Ronaldo wanacheza dakika 90 uwanjani na wanalipwa kiasi kikubwa Cha fedha kuliko wachezaji wengine.

    Unadhani kwa nini wanalipwaa kiasi kikubwa hivyo? Ni kwa sababu ya thamani yao wanayotoa.

    Kitu chenye thamani kubwa kinauzwa kwa bei kubwa ukilinganisha na kitu chenye thamani ya ndogo.

    Kama unataka kupata fedha basi unapaswa kuwa tayari kutoa thamani kwa watu.

    Labda unajiuliza, thamani ni kitu gani? Na Mimi nawezaje kuongeza thamani kwa watu.

    Iko hivi, ebu chukulia sasa hivi umetoka nje na umekutana na sura ngeni mtaani kwako. Mgeni akakuuliza, naomba kujua kwa mzee Daudi. Na wewe Daudi unamjua ni mzee pale nyumba ya tatu kutoka UNAPOKAA.. ukasema ngoja nimpeleke huyu jamaa mpaka kwa mzee Daudi…

    Kwa upande wako unakuwa umetoa thamani…
    Huyu jamaa alikuwa na shida na na umemwonesha kwa mzee Daudi, na shida yake imeisha.

    Tungekuwa sehemu nyingine, basi ilibidi akulipe jero kwa kitendo cha kukuuliza kwa mzee Daudi ni wapi na buku ya kumwonesha kwa mzee Daudi….Hahah

    Ulivyomfikisha yule jamaa kwa mzee Daudi amefurahi, kuthibitishwa kwamba amepata thamani kutoka kwako.

    Hivyohivyo kwa fedha, fedha ni matokeo ya thamani unayotoa..

    Unataka watu wakulipe? Toa thamani..
    Ukitatua matatizo ya watu, unakuwa umetoa thamani.
    Ukisogeza huduma karibu yao, unakuwa umeongeza thamani.

    Kwa hiyo badala ya kukazana kuikimbiza fedha, kazana kutoa thamani kwanza. Fedha itakuja tu.

    Sijui umenielewa….

    Kama umenielewa kaangalie video hii YouTube kwanza, Kisha SUBSCRIBE

    anyaway, tuendelee..

    Si umewahi kusikia habari za fuata nyuki ule asali. Unajua kwa Nini Watu wanawafuafa nyuki mbali na kuwa nyuki ni wakali..

    Kwa sababu nyuki wanatoa thamani kubwa kiasi hakuna MTU anayeweza kuitega mgongo.

    ukizalisha thamani nzuri watu watakuwa tayari kukufuata hata Kama upo kijijini. Kwani nyuki huwa tunawafuata wapi?

    Hakuna nyuki wenye mzinga Kariakoo… Mizinga yote ipo misituni Ila tunawafuata tu. Rafiki yangu, zalisha thamani…

    Bado tuko pamoja? Basi mpaka hapa Sina shaka utapendaa kitabu changu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI. Kitabu hiki Ni 20,000 tu na unatumiwa popote ulipo duniani.

    wasiliana na 0755848391 kukipata.

    Umekuwa nami
    Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE CONSULTANCY
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • Fanya Yafuatayo Kuepuka Kuwa Miongoni mwa Walalamikaji

    Moja ya kitu rahisi sana ni kulalamika. Kila mtu anaweza kukifanya. Lakini kitu kigumu kufanya ni vitendo na kuonesha matokeo.

    Sasa siku ya leo, nataka uepukane na malalamishi ili mwisho wa siku uwe mtu wa kuleta matokeo ambayo wewe mwenyewe unayatamani

    Unajua kwa Nini Watu wanalalamika?

    Kwa sababu kuna matokeo mazuri wanayataka ila  wanataka mtu mwingine awasaidie kupata hayo matokeo. Kwa hiyo, wanataka MTU mwingine azalishe matokeo na siyo wao.

    Mtu anataka kupata afya njema, anawalaumu wazungu kwa kuleta vyakula vya makopo.

    Mtu anataka utajiri na fedha, anailaumu serikali kwa kutokutoa hela. Wakati fedha chanzo chake ni thamani.

    Sasa badala ya kulaumu, sikiliza. Kuwa mtu wa kuzalisha matokeo.

    Kwanza, kuwa na malengo ambayo unayafanyia kazi. Zama kwenye kufanyia kazi malengo yako na sahau Mambo mengine

    Pili, kabla ya kulaumu jiulize wewe umezalisha matokeo gani. Kila utakapojiuliza swali hili, utakuta kwamba unalazimika kukazana na malengo yako zaidi kuliko kulaumu MTU mwingine

    Tatu, fahamu kuwa maisha ni wajibu wako. Hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kupiga push-up kwa ajili yako.

    Nne, usifuatilie maisha ya watu wengine. Kadiri unavyofuatilia maisha ya watu wengine, ndivyo unavyojinyima fursa ya kufanyia kazi malengo yako.

    Tano, Mara zote kuwa mtu wa kujifunza na kusoma vitabu. Jifunze , jifunze jifunze.

    Kila la kheri.

    Umekuwa nami
    Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE CONSULTANCY
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • Usikubali Kuendelea Kubaki Hivyo hivyo

    the simba mentality

  • Njia Mpya Ya Kutengeneza Utajiri Tanzania

    Kwa kila sekunde inayopita, mtandao wa google unapokea maombi 40,000. Hawa ni watu mbalimbali wanaotafuta majibu ya maswali yao kwenye mtandao huu.
     
    KWA NINI WATU WANATAFUTA MAJIBU GOOGLE?
    Moja ni kwa sababu majibu waliyonayo hayatoshelezi hivyo wanatafuta suluhisho jipya.

    Pili, kwa sababu hawajawahi kupata suluhisho la swali hilo kabisa maishani mwao. Hivyo njia pekee ni kukimbilia Google kuona kama kuna mtu ambaye anaweza kutoa suluhisho.

    SASA HILI LINA MAA GANI KWAKO?
    Hii maana yake kwamba, ukiweza kujibu swali moja tu kati ya hayo 40,000 ambayo yanaulizwa  kila sekunde basi utakuwa umeweza kuwasaidia watu kupata kile WANACHOTAKA.

    Na kumbuka kwamba, unaweza kupata kitu chochote unachotaka kama utawasaidia watu kupata kile WANACHOTAKA.

    Wewe, hapo ulipo umebeba majibu ya maswali ya baadhi ya watu. Kwa nini hutaki kuyatoa ili uwasaidie.

    Ebu chukua hatua leo uanze kujibu walau swali la mtu mmoja kuanzia siku hii ya leo.

    USIBANIE HAYO MAJIBU UMEPEWA WEWE KWA AJILI YANGU. Nisaidie mimi kujibu maswali yangu ili nikulipe.

    Asante Sana.

    Kitabu hicho unachokiona kwenye picha ni nakala tete (soft copy), na kinapatikana kwa 10,000 tu. Kichukue leo ili kikupe msingi wa kuanzisha kitu kitakachotoa majibu ya maswali ya watu.


    Lipia kwa nambari 0755848391 jina Godius Rweyongeza Kisha nitumie ujumbe wenye neno BIASHARA ili nikutumie kitabu

    Usisahau pia kuingia YouTube Leo na kuangalia video hii yenye masomo matatu ya kibiashara.

    Karibu sana

  • Leo ikiwa Ni siku ya Idd napenda kutoa ofa kwa mtu mmoja tu ambaye atajiunga na kozi yangu ya UANDISHI

    Eid Mubarak Kwako rafiki yangu

    Kozi ya kipekee ambayo inadumu kwa siku 30 Ina Mambo mengi ndani yake.

    Kwa kawaidaa gharama ya kozi hii huwa ni laki mbili (200,000). Ila kwa ofa ya leo. Mtu mmoja tu ambaye atalipia 120,000/- nitamuunganisha kwenye hii kozi.

    Ukiwa ndani ya hii kozi utapata

    • Utajifunza mbinu za kitabu chako kuanzia mwanzo mpaka mwisho
    • Nitakusimamia na kusoma kazi zako unazoandika kila siku na kukupa mrejesho wa kuziboresha
    • Nitakufungulia blogu ya bure.
    • Utajifunza mengi kutokana na yale wanayoandika wenzako na maoni nitakayokuwa natoa kuhusu kazi za wenzako.
    • Utapata kitabu Cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30 bure.
    • Utapata jarida lenye hatua 15 za kufuata ili kuandika magazetini.
    • Utapata mafunzo ya audio zaidi ya 10. Yakiwemo mahojiano na waandishi wakubwa hapa nchini.

    Uko tayari?

    Basi wasiliana nami kwa 0755847391 Sasa hivi

    First come. First Served

    NB: hii ni nafasi ya kipekee ya kufundishwa uandishi, na kutimiza ndoto yako ya siku nyingi ya kuwa mwandishi.

    Wahi sasa hivi Tena bora ubonyeze HAPA TU KUWAHI KIKASHANI

  • MAISHA YA NYOTA TANO

    Leo nimesikiliza audiobook ya kitabu cha Oprah Winfrey. Nimejifunza mengi sana ila hapa kuna kimoja tu ambacho ningependa na wewe ukijue.
    Oprah anasema kwamba, unaweza kuishi maisha ya nyota tano hata   hauna pesa sasa. Sio lazima ulale kwenye hoteli zenye viyoyozi ndio uanze kuishi maisha ya aina hii. Ebu ona

    ukiamka asubuhi na mapema. Basi jipe nyota tano kwa ushindi huo.

    ukitoka nje ukavuta pumzi na kufanya tafakari pamoja na kunywa maji. Jipe nyota tano kwa kitu hicho kikubwa.

    Ukisoma kitabu, kurasa kadhaa, jipe nyota tano, maana hilo ni jambo kubwa.

    ukiwahi kazini, jipe nyota tano pia.

    ukimpigia ndugu, mke, mme, mzazi simu na mkaongea hadi mkacheka kiasi unasikia kichwa kama kinauma. hiyo ishara ya wewe kupata nyota tano kwenye hilo.

    Yaani kiufupi ni kwamba. Maisha ya kila siku ukiyaishi vizuri sana. Basi utakuwa unaishi maisha ya nyota tano.

    Bila shaka utakuwa umeona ilivyo rahisi kuishi maisha ya nyota tano.

    Je, wewe leo umeishi maisha ya nyota tano?

    Nashauri usome au usikilize audiobook ya kitabu hiki hapa. imebeba mambo mazito na muhimu kwa maisha yako.

    kila la kheri.

    Kitabu kinaitwa WHAT I KNOW FOR SURE.
    Mwandishi Oprah Winfrey

    makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
    Tembelea pia www.songambeleblog.blogspot.com

    kuna makala nzuri mimeweka.

    kwenye youtube pia usikose kuangalia video hii. https://youtu.be/LrBROehGr64

    nyingine zaidi zinakuja.
    cha kufanya wewe SUBSCRIBE ili uwe wa kwanza kupata video hizi

    haya twende https://youtu.be/LrBROehGr64

  • VITENDO VIZIDI MANENO

    Dunia ina tabia ya kukupatia kitu kama utaonesha nia, kuwa wewe ungependa kupata hicho kitu. Huwa ninapenda kuwaambia watu kuwa, hata kama ni bahati itakukuta njiani unatembea wala sio chumbani kwako ukiwa umelala.

    Kwa hiyo, wewe kama unahitaji kupata bahati maishani mwako basi kuwa tayari kuweka kazi inayoendana na bahati unayotaka. Bahati unaitengeneza wewe mwenyewe na vitendo vyako ndivyo vinapaswa kuonesha hilo.

  • Leo najisikia kutoa ofa. Sema Toa Ofa basi 😂😂😂

    Hii ofa ni ya kipekee kwa ebooks zangu ambazo watu wanapenda sana.

    Ebooks hizi ni

    1. MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA
    2. KIPAJI NI DHAHABU: Jinsi ya kugundua, kunoa na kuendeleza Kipaji
    3. NGUVU YA WAZO (The power of an idea): How An Idea Can Change The World. Jinsi Wazo kinachoweza kubadili Dunia

    Thamani ya ebooks, hizi Ni kubwa Sana. Ila unajua Nini? Nataka nikupe wewe ofa ya kupata ebooks hizi kwa 12,000/- tu.

    Changamkia fursa hii ya kipekee sasa. Lipia kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    BAADA YA HAPO UTANITUMIA UJUMBE ILI NIKUTUMIE EBOOKS HIZI.

    Karibu

    By
    Godius Rweyongeza
    www.songambele.co.tz
    0755848391

X