-
THE SIMBA MENTALITY

Karibu sana kwenye makala ya leo. Ni makala ndefu kidogo. Kwa wale wasiopenda kusoma vitu virefu sana hii ya leo inaweza isiwe makala ya aina yako. Ila wale ambao wanapenda kuzama ndani na kujifunza vitu kwa kina vilivyotafitiwa na kutafitika, basi vuta kiti maana unachoenda kujifunza hapa ni kitu kikubwa sana.
Kwa siku nyingi sana nimekuwa nikipanga kuandika makala yenye kichwa hiki cha The Simba Mentality. Nadhani mara ya kwanza kupata wazo la aina hii, ilikuwa kipindi nasoma wasifu wa Kobe Bryant, unaoitwa The Mamba Mentality.
Kwenye wasifu huu, Kobe Brayant ameeleza safari yake kimichezo tokea akiwa shule ya upili (high school) mpaka anastaafu. Ni kitabu kizuri sana. na sote tunajua kwamba Kobe alishatangulia mbele ya haki, tangu mwaka 2020, hivyo, kitabu hiki, ndio kimebaki kama alama ya kumkumbuka na kujifunza kutoka kwake, sambamba na video na mafunzo kadhaa yanayozunguka mtandaoni. Unaweza kutazama video ya uchambuzi wa kitabu chake kwenye channel yangu ya youtube hapa chini. hakikisha umesubscribe pia.
Nakumbuka mwanzoni nilipanga kabisa niandike kitabu kinachoitwa The Simba Mentality, ila sasa leo nimeona kwanza nikudoletee makala hii. Kama utaipenda, unaweza kuniambia niiongezee nyama zaidi, ili pengine nitengeneze kitabu.
Siku siyo nyingi kwenye mtandao wa youtube nilikutana na video iliyokuwa ikiwaonesha simba waliokuwa njiani. Kilikuwa ni kikosi kikubwa cha Simba, ambao walilala katikati mwa barabara na hivyo, kusababisha magari yaliyokuwa yanatokea kila upande kukwama kwa muda, kila mwenye gari alijitahidi kupiga honi kadiri alivyoweza ili labda kuwaongopesha hawa wanyama na kuwafanya wasogee, ila hakuna mnayama hata mmoja ambaye alitoka.
Sote tumewahi walau kisikia stori za simba. maana nikisema, sote tumewahi kumwona simba ana kwa ana, hapa tutaanza kutafutana., labda kumwona kwenye royal tour tu
Simba ni mnyama wa mwituni ambaye pia anajulikana kama mfalme wa nyika. Anafahamika kwa ukali wake na uwezo wake maridadi wake kuwinda. Mpaka tulipokuwa wadogo tulikuwa tumamwimba,
Tulikuwa tunaimba hivi
KIONGOZI: Watoto wanguu ee…
WOTE: Ee
Kiongozi: Mimi mama yenu
WOTE: Ee
Kiongozi: Sina nguvu tena
WOTE: Ee
Kiongozi: Za kuua simba
WOTE: Ee
Kiongozi: Simba ni mkali
Wote: Eeh
Kiongozi: Aliua mama,
WOte: Ee
Kiongozi: Akaua mama
Wote: Ee
Kiongozi: Sasa kimbieni
Wote: Makelele ya shangwe……
Naam, nimekurudisha utotoni ee.
Huyu ndiye simba. Nakumbuka nyumbani jina maarufu la mbwa, ni simba. Mbwa wengi wa nyumbani ambao nimewahi kuwaona majina yao wanaitwa simba. Hii yote ni kwa sababu kila mtu anapenda mbwa wake awe na ukali kama simba. Na hata siku hizi kuna watu wanajiita majina ya wanyama.
Kama nilivyokudokeza tangu mwanzo kuhusu kitabu cha Kobe Brayant ambaye pia alikuwa anajiita Black MAMBA. Watu wengine wanajiita majina ya wanyama kama yeye, likiwemo jina la simba, chui,…
Nadhani kila mtu anajaribu kutafuta jina ambalo litamtambulisha vizuri, kulingana na tabia alizonazo. Ila jina SIMBA, nadhani wengi wanalipigania.
Sidhani kama kuna mtu ambaye anapenda aitwe panya, kunguru, au nguchiro. Hii yote ni kuonesha kwamba kila mtu anataka kuonekana kwamba ana ustadi wa hali juu kwenye kile anachofanya.
Sasa simba ana kitu gani cha kipekee ambacho kinamtofautisha na wanyama wengine.
Zifuatazo hapa chini ni sifa muhimu za simba ambazo zinamfanya kuwa mfalme wa nyika.
Rafiki yangu, kusoma andiko hili mpaka mwisho, hakikisha kwamba unajipatia ebook hii ya THE SIMBA MENTALITY kwa 5,000 tu. Au jiunge na kundi letu la mafunzo maalumu la THINK BIG FOR AFRICA. Kujiunga BONYEZA HAPA
Fedha ya kupata ebook yenye andiko lote la THE MAMBA MENTALITY utaituma kwa namba 0755848391 Jina ni GODIUS RWEYONGEZA
-
Je, Kuna Haja Ya Kuendelea Kusoma Wakati Ajira Hakuna?
Jana kupitia Temino ya Clouds FM niliongea na wanachuo wote hapa nchini, huku nikiwasisitiza juu ya umuhimu wa kutumia bumu lao la chuo vizuri maana kuna maisha baada ya chuo.
Waendeshaji wa kipindi hicho ambao ni Harris Kapiga pamoja na Advovate Henry Mwinuka nao walisisitiza pointi muhimu sana kwa kusema kwamba kila mwaka kuna wahitimu zaidi ya laki nane ambao wanahitimu na miongoni mwao, ni wahitimu elfu themanini tu ambao wanapata ajira. Huku wahitimu laki saba na elfu ishirini wakibaki bila ajira. Na hizi usifikiri ni takwimu za kubahatisha. Hapana, ebu angalia screenshot hizi hapa chini

Hii nimeitoa kwenye tovuti ya bunge la Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania. Kama hujaweza kuona vizuri, ebu yasome hayo maneno hapa chini Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa taarifa ya Serikali, kila mwaka takribani Wahitimu laki nane, kwa mwaka, na wanaoajiriwa ni elfu arobaini peke yake, kwa hiyo laki saba na sitini wanabaki mtaani. Ningependa kujua Serikali ina Mkakati gani wa ziada, kwa sababu Mkakati uliopo umeshindwa kukidhi vigezo vya kuweza kuwaajiri vijana wengi ambao wamehitimu? Ni Mkakati gani wa ziada ambao Serikali inao kwa ajili ya kuwasaidia Vijana hawa ambao wengi wako mtaani?
Screenshot nyingine hii hapa

hii nimeitoa kwenye tovuti ya gazeti la habari leo. Iliandikwa tarehe 28.12.2021 Sasa swali la mmoja aliyesikia huo ujumbe lilikuwa ni hili hapa

Habari bro mm naitwa mtima nimekusikia kwenye kipindi cha chimbo clouds FM mm nilikua naomba ushauli kama ajira ni chache je kunahaja ya kusoma maana unaweza kusoma na usipate ajira alafu ukawa umepoteza mda mm ni mwanafunzi naelekea kujiunga na kidato cha tano
Kama unavyoona hapo. Leo ninaenda kuwa najibu swali la je, kuna umuhimu wowote ule wa mtu kuendelea kusoma wakati ajira hamna? Kuna umuhimu wowote kweli, au ndio bora ukaanze biashara kabla hata ya kupoteza fedha na muda?
Eti kwa mfano wewe kwa maoni yako unasemaje?
Kwenye hili siendi kuongea sana, badala yake napenda kwanza nikupe stori.
Mwaka 2017 nikiwa chuoni, nilitaka kuacha chuo. Siriazi, nilitaka niache chuo, ili niende nikaanzishe biashara.
Niliongea na rafiki zangu na kuwapa taarifa kuwa ninaenda kuacha chuo, na baadaye nikaongea na wazazi ambao hawakupenda uamuzi huo kabisa. Wazazi wangu walikuwa wachungu kwenye hili kuliko hata mwimba.
Baadaye nikaongea na mshauri mmoja ambaye alinipa ushauri, ambao ningependa niutoe kwako pia.
Aliniambia hivi, Godius huna haja ya kuacha chuo na kwenda kuanzisha biashara. Badala yake pambana na vyote viwili. Anzisha biashara na soma chuo. Ukifanikisha kufanya vyote viwili ukiwa chuoni, utakuwa shujaa.
Kwangu huu ushauri niliupokea kwa mikono miwili, hivyo niliamua kukomaa na chuo na wakati huohuo nilianzisha biashara na kukomaa nayo.
SOMA ZAIDI: Kama upo chuoni na una mpango wa kujiariri; fanya hivi. Mwongozo kujiajiri baada ya kumaliza chuo
Hivi Ndivyo Unaweza Kupata Mtaji Wa Biashara Ukiwa Bado chuo
Kwa hiyo kwanza kabisa ningependa kukwambia kwamba, USIACHE KUSOMA. SOMA KWA BIDII NA UFAULU. ILA SASA FIKIRI NJE YA MASOMO. Na hapa sasa ndipo nataka nikupe mbinu na vitu ambavyo huwezi kuvipata sehemu nyingine.
Labda tujiulize ni nini lengo la shule? Je, ni kukaririsha watu vitu wasivyovielewa? Ukiniuliza mimi nitakwambia hivi

#1. LENGO LA ELIMU NI KUTENGENEZA WATU AMBAO WANAWEZA KUTAFSIRI KILE WANACHOJIFUNZA KWENYE MAISHA YA KAWAIDA
Nakumbuka siku moja niliwahi kumsikia mkuu wa chuo cha SUA akihoji watafiti kuwa je, hizo tafiti mnazofanya zinawasaidiaje wananchi wa kawaida? Unaone ee.
lengo la elimu siyo kwamba ukariri kile unachojifunza darasani. Badala yake ni kwamba, uweze kutafsiri kile unachojifunza na kukileta kwenye maisha ya kawaida.
Nakumbuka tukiwa mwaka wa pili pale chuoni. Tulisoma kozi moja inaitwa SPICE PRODUCTION (uzalishaji wa viungo) Viungo si unavijua? Mambo ya iriki, tangawizi, karafuu…Mambo ya Pemba hayo yahe…
Hii kwangu ndio ilikuwa ni kozi ya kipekee iliyokuwa na vitu vingi ambavyo nilikuwa napenda. Niliona kuna vitu vingi ndani yake ambavyo ningeweza kuvitumia kwenye maisha ya kawaida ya kila siku. Na hivyo, nikawa nimeamua kwamba baada ya chuo, nitakuwa nashughulika na uzalishaji na usindikaji wa viungo. Kwa hiyo, nikawa nimeona fursa kutokana na kile nilichokuwa nimejifunza na sasa hivi nimefungua kampuni inayohusika na uzalishaji wa viungo.
Laiti ningeacha chuo nikiwa mwaka wa kwanza, hiki kitu nisingekaa nikakisoma mwaka wa pili. Na sijui sasa hivi kampuni yangu ingekuwa inahusika na nini
Kwa hiyo, endelea kusoma, ila sasa jiulize kwenye kile ambacho unajifunza darasani, unawezaje kukitumia kwenye maisha ya kwaida ya kila siku. Huku mtaani, kuna watu wana shida na wanategemea wasomi wazitatue, siyo kwamba wasomi watatatua hizi shida kwa kuwapa hela. Hapana, bali kwa kuwaletea suluhisho sahihi.
Wewe hujawahi hata kumsaidia bibi kizee huko kijijini ambaye simu yake imejifunga tu, labda watoto walikuwa wanaichezea, ila kwa sababu hajui kiingerereza haelewi wapi pa kubonyeza. Mara paap akaileta kwako, ukasoma soma vitu viwili vitatu, ukaifungua akafurahi? Hujawahi? Mimi huwa inanitokea sana, na hiyo huwa inanipa picha kwamba hata matatizo mengine yanayokumba watu huku mtaani, ukiyatatua, watu watafurahi hivi hivi….
Kwa hiyo, kila mara unapaswa kuwa unajiuliza nasoma chuoni. Lakini, hawa uliowaacha nyumbani kwenu. Wanawezaje kunufaika na hiki ninachosoma. Je, kuna namna ambavyo wanaweza kunilipa kutokana hiki ninachosoma kama ipo. Basi zama ndani, ukijue hicho kitu. Ili baadaye uje ukigeuze hicho kitu kuwa biashara.
Nakumbuka siku moja nilikuwa nasoma wasifu wa Ben Carson. Ndani yake akawa amemtaja kaka yake. Aanasema kaka yake alikuwa anapenda Geometry..
Hivi Geometry ndio elimu ya maumbo ee…
Au basi siyo lazima uelewe kila kitu, vingine utaelewa siku ya mtihani…Hahaha
Ila ninachotaka kukwambia ni kwamba, Ben Carson anasema kaka yake aliona fursa kwenye hiyo elimu ya maumbo na akaamua kuitumia kwenye maisha ya kawaida ya mtaani.
Hiki ni kitu ambacho shuleni walimu wako hawakwambii, ila ukweli ni kwamba, kwa kila unachojifunza unapaswa kuangalia namna ambavyo unaweza kukitumia kwenye maisha ya kawaida ya huku mtaani. Maana huku, ndio kuna maisha yenyewe…
Siyo kila kitu kitakufaa wewe, na haipaswi kuwa hivyo, unahitaji kitu kimoja tu ambacho unaweza kutumia huku mtaani, vingine waachie wengine.
Sijui unanielewa….
Kama umenielewa basi, vuta pumzi kidogo wakati mimi nakunywa maji hapa….
SOMA ZAIDI: · WANAOSHEREKEHEA KUHITIMU CHUO TUWAAMBIE UKWELI? AU TUWAACHE KWANZA WAFUMUE NYWELE ZAO ZA GRADUATION?
Usiende Chuo Kusomea Uandishi Wa Vitabu; Badala Yake Fanya Hivi

Kafanyaje huyu? #2. Imani ni yangu kuhusu chuo ni kwamba, chuo kipo kwa ajili ya kuandaa watu ambao watakuja kuajiri baadaye
Hii ni imani yangu na ni msimamo wangu, hata ukiniamsha saa nane usiku, na kuniuliza ebu niambie kazi za shule na vyuo ni vipi.
Nitakwambia vyuo vinapaswa kuandaa watu ambao watakuja kutengeneza ajira baadaye.
Kwa nini? Na kwa jinsi gani?
Kwa sababu elimu wanayoitoa shuleni, inapaswa kutafsiriwa kwenye maisha ya kawaida ya huku mtaani. Kwa hiyo kama kila mwanachuo, akitoka chuoni na kitu kimoja amnacho anaweza kupambana nacho huku mtaani, ataweza kuwasaidia hata wale aliowaacha nyumbani.
Sasa kinachotokea sasa hivi ni kwamba wale waliosoma, wanarudi tena nyumbani na wanaanza kuwategemea wale waliowaaacha.
Hiki kitu unaweza usiambiwe na walimu wako, lakini unapaswa ukijue. Jua kabisa kwamba unaposoma, hata kama mwalimu wako anakwambia soma bidii ili uje upate ajira. WEWE badili hilo liwe kwamba nasoma kwa bidii ili nije niajiri.
#3. Lengo la elimu ni kukusaidia kutengeneza konekisheni.
Iko hivi, unapokuwa unasoma kwanza unakutana na watu wengi. na kila mtu ana kipaji chake na uwezo wake. sasa hili ndilo lengo la shule. Kwamba liwakutanishe watu wenye vipaji vyenu, halafu muone namna ambavyo mnaweza kuunganisha vipaji vyenu kwa manufaa makubwa.
Ila sasa hili halitokei kwa sababu, vipaji na uwezo havipewi kipaumbele kwenye mfumo wa elimu uliopo. Ndio maana mtu anasoma mpaka chuo kikuu, lakini ukiumuuliza kipaji chake hajui.
Lakini, ukiweza kukutana na watu ambao wana vipaji na mkaweza kuunganisha nguvu kwa pamoja. YAANI, kiufupi mkaendana au mkaivana, basi ujue mtaweza kufika mbali.
Halafu konekisheni haiishii kwa wanafunzi wenzako tu, hata kukuunganisha na walimu wako na hata watu wenye fikra za tofauti kabisa na wewe. Hii yote inakusaidia wewe kuuona ulimwengu katika namna ya kipekee na kuchukua maamuzi sahihi.
Kuna konekisheni ambazo unaweza kuzitengeneza wakati wa kusoma zikaja kukusaidia baadaye. Pengine wewe kwenye kusoma umependa kuzama zaidi kwenye mambo ya uzalishaji wa viungo (spices) kama mimi. Na mwezako amependa kuzama kwenye sheria. Baadaye huyu mwanasheria anaweza kukusaidia wewe wakati unaajiri kwenye kuweka mikataba.
Hata kama utamlipa, lakini kwa kuwa ni miongoni kwa konekisheni ambayo uliwahi kuitengeneza wakati unasoma, basi utakuwa na uhakika kwamba hapa nasaidiwa na mtu sahihi. Na siyo magumashi, anaweza pia kukusaidia kupooza bei kidogo…
Hiki kitu ninachosema hapa unaweza usikielewe vizuri, lakini ulimwengu wa sasa umeanza kuonesha kuwa kweli hiki kitu kinafanya kazi kweli.
Mfano mzuri tu, siku hizi mtandaoni kuna hivi vitu tunvyoviita aplikesheni.
Unaweza kukuta kuna aplikesheni labda inayohusika na masuala ya uhasibu. Kama THL (watu wa THL mkisoma hapa, mnitumie vocha maana nimewarusha hewani leo)
Sasa kutengeneza aplikesheni kama hii ya THL inayohusika na utunzaji wa kumbukumbu za kihasibu, kunahitaji walau muunganiko wa watu wa aina mbili.
Kwanza ni wahasibu
Na pili ni watalaamu wa teknlojia.
Hizi ndizo konekisheni zenyewe, ambazo unaweza kuzipata ukiwa shuleni. Kwa hiyo wewe wakati unasoma, unaweza kugundua kwamba mtu fulani yuko vizuri kwenye kitu fulani, na mimi niko vizuri kwenye hiki kitu, basi tukiungana na kuunganisha haya maujuzi yetu, tunaweza kutengeneza kitu fulani ambacho kitakuwa na manufaa kwenye jamii.
Mimi ni daktari, na jamaa mwingine ni mtalaamu wa teknolojia, tunaweza kuunganisha udaktari na teknojia tukawasaidia watu wengi zaidi.
Daah, hapa nimemkumbuka jamaa mmoja. Ofcourse kinyozi. Hivi anaitwa kinyozi au fundi kinyozi, au basi…
Huyu jamaa alikuwa anataka kuunganisha utalaamu wake wa kunyoa na teknoljia. Yaani, kwamba ukienda saloon kwake anachukua namba yako, ukishaondoka tu kuna mfumo wa kiteknolojia unakutumia ujumbe wa kukushukuru kwa kuweza kufika ofisini kwake kunyoa, baada ya wiki mbili mfumo huo unakukumbusha urudi kunyoa maana zimepita siku tangu unyoe…
Sasa mtu kama huyu anahitaji konekisheni. Anahitaji kuunganishwa na mtu mwenye uelewa wa haya mambo ili amwezeshe kutengeneza mfumo wa aina hii…
Sijui unanielewa? Kama umenielewa mpaka hapo, gonga cheers!
SOMA ZAIDI: · Kama upo chuoni na una mpango wa kujiariri; fanya hivi. Mwongozo kujiajiri baada ya kumaliza chuo
Vitabu Vitano Ambavyo Kila Muhitimu Wa Chuo Kikuu Anapaswa Kuanza Kusoma Mara Moja
#4. naamini kwamba chuo kipo kwa ajili ya kukupa maarifa sahihi unayoyahitaji kwenye maisha ya baada ya chuo.
#5. shuleni na chuo ni kwa ajili ya kukufundisha wewe kusoma na kuandika, sasa jukumu lako baada ya kumaliza shule ni kujiendeleza kwenye kusoma na kuandika.
Shuleni unafundishwa kusoma na kuandika. Si ndio? Tatizo la watu wengi wanapomaliza shule, ndio wanaona kwamba hakuna haja ya kusoma tena. Hawajifunzi kitu chochote kipya.
Kitu hiki kinawafanya waendelee kuwa na maarifa yaliyopitwa na wakati. Sikiliza. Shuleni unafundishwa kusoma na kuandika. Ila sasa kwenye maisha ya kawaida ya huku mtaani unapaswa kusoma na unapaswa kuandika pia.
Ebu fikiri amtu aliyesomea kompyuta mwaka 2010. Kama mtu huyu hajajiendeleza kuongeza maarifa na kujifunza zaidi, lazima tu ameshapitwa na wakati. unajua kwa nini? kwa sababu kompyuta zinabadilika kwa kasi, na na kuna vitu vingine vinazidi kugunduliwa sasa hivi.
Mtu aliyosoma kompyuta 2010 atakuwa hakujifunza mambo ya roboti kama yalivyo sasa hivi. lakini kama wewe ukiwa ni mtu wa kujiupdate na kujifunza zaidi kila siku. Hata baada ya chuo, hutahangaika, maana utakuwa unapata ujuzi na kuelewa kinachoendelea. Na utakuwa unaweza kutumia hiki kitu unachojifunza kwenye maisha ya kawaida.
SOMA ZAIDI: · Hii Ni Maana Mbaya Ya Mwanachuo Kuwahi Kutolewa
VITU AMBAVYO WAHITIMU WA CHUO HAWAPENDI KUFANYA INGAWA VINALIPA SANA
Hayo ndiyo nilivyokuwa nayo moyoni kuhusu chuo na wqnachuo kwa leo. Nina mengi Ila sasa nikiyabwaga hapa tote, hayataleta maana. Nadhani siku nyingine jamaa akinichokoza kwabkuniuliza swali kamablanleo nitaandikia ena Kitu kingine.
Ila jamani nisitize. Endelea kusoma, soma kwa bidii ila fikiria nje ya ajira. Kama umenielewa share makala hii na watu wengine ili nao wanufaike.
Mpaka wakati mwingine
Mimi ni Godius Rweyongeza kutoka SONGEMBELE CONSULTANTANCY
-
Utafanyeje Unapokuwa Na Wazo La Kufanya Biashara Ila Huna Mtaji
Rafiki yangu, leo nataka niongee na wewe na kwa namna ya kipekee sana. Najua kwamba kuna vijana wengi huko mitaani ambao wana ndoto za kufanya makubwa. Vijana ambao wana ndoto za kuanzisha biashara ila tatizo au kisingizio wanasema,ni kwamba hawana mtaji.
Je, ni kweli kwamba tatizo lako ni mtaji. Je, ni kweli kwamba hauna mtaji wa kukutosha kuanzisha biasahra?
Siku ya leo nataka nikupe mfano kidogo tu wa mnyororo wa chakula. Hiki kitu tulijifunza shule ya msingi

Kwenye mnyororo wa chakula ni kwamba mnyama aliye juu kwenye myororo wa chakula anakula mnyama aliye chini yake.
Mahindi yanaliwa na panya na panya analiwa na Bundi
Karoti zinaliwa na Sungura na sungura analiwa na mbwa mwitu na mbwa mwitu wanaliwa na simba
Sasa nataka kusema nini kwa kuonesha hivi vitu. Nataka nikwambie kwamba, kama una wazo la biashara au la kufanya kitu chochote kile ila huna mtaji, maana yake una NDOTO KUBWA.
Kitu hiki siyo kibaya maana mara zote nimekuwa nakusisitiza wewe uwe na NDOTO KUBWA kweli.
Ila sasa unataka uwe Simba wakati hujafikia hivyo viwango Unapokuwa na ndoto kubwa unapaswa kuwa tayari kuanzia chini na kupanda juu. Siyo utake kuanzia juu kwa juu.
Yaani, ni sawa na kwamba uwe SUNGURA kwenye mnyororo wa chakula halafu eti utake kumla MBWAMWITU.
Kubali kwamba kwa sasa wewe ni SUNGURA na kula majani. Baadaye ukifikia hatua ya USIMBA utakula hao mbwa mwitu bila tatizo lolote.
Hiki ni kitu ambacho unapaswa kukipokea, kwa sababu pia vijana wengi hawapendi kuanzia chini. wengi wanapenda kuanzia juu kwa juu. Unakuta kijana ana ndoto ya kuanzisha biashara na anakwambia kwamba yeye anataka kufanya biashara ya mtaji wa milioni 200. Sasa wewe unafanyaje biasahra ya mtaji wa milioni mia mbili wakati hata mtaji wa milioni moja unakushinda kuuendesha vizuri? Unafanyaje?
Kiukweli kubali kuanzia chini.kisha kubali kukua kidogokidogo, mpaka mwisho.
- SOMA ZAIDI Jinsi Ya Kuanzisha Biashara Bila Mtaji Tanzania
- Wazo Bora La Biashara
- Unawezaje Kupata Wazo La Biashara La Kipekee?
KILA LA KHERI
Umekuwa nami
Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE CONSULTANCY
Tuwasiliane kwa 0755848391
Morogoro-Tz
NB: Hakikisha kwamba umepata kitabu changu cha NGUVU YA WAZO NA KITABU CHA MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA. Vitabu hivi viwili vitakusaidia sana wewe kuweza kufika mbali kwenye kufanyia kazi wazo lako na hata kupata mtaji wa kuanzia kwenye kufanya biashara. Upo tayari nikutumie vitabu hivi viwili? Upo tayari?
TUma elfu kumi leo nikutumie ebooks zote mbili. Wahi sasa hivi.
Tuma kwa 0755848391 jina ni Godius Rweyongeza. Akhsante
-
Mwongozo kwa wapambanaji (Hustlers Guide)
Leo nataka nitoe mwongozo maalumu kwa mtu yeyote ambaye anapambmana kufikia mafanikio makubwa sana.
Kama unapambana kufikia mafanikio makubwa hakikisha kwamba
1. una malengo na unayafanyia kazi kila siku bila ya kuchoka
2. unajihusisha na watu sahihi, watu chanya na watu ambao wanaendana na wewe. Watu hasi watakuangusha
3. unaangalia namna ya kubadili ndoto yako kuwa huduma. Angalia namna ambavyo unaweza kuwasaidia watu kutatua matatizo yao kwa kujenga huduma nzuri kwenye ndoto yako. Kumbuka usemi wa Zig Ziglar unaosema kuwa “unaweza kupata chochote unachotaka kwa kuwaswaidia watu kupata kitu wanachotaka.”
4. Kila siku piga hatua haka ni hatu ndogo, kuelekea kwenye mafanikio yako.
5. Usiache kusoma kitabu kila iitwayo leo. Tena anza na hiki hapa chaMAAJABU YA KUSOMA VITABU. kinapatikana bure tu.
6. Jifunze kutoka kwenye makosa ambayo umewahi kufanya siku za nyuma. Usirudie makosa yaleyale kila mara.
7. Zijue amri kumi za maisha na uziishi. Zisome Hapa
8. Usitake kujionesha kwamba wewe ni mtu wa aina fulani. Acha vitendo tu vikuoneshe
9. Fanya mazoezi ya kutosha nyuma ya pazia kabala hujatokea kuonekana mbele ya watu. Yes, fanya mazoezi ya kutosha rafiki yangu.
10. Fanya mazoezi kiasi kwamba ukionekana mbele ya watu, watu wafikri kuwa wewe kipaji chako cha asili, kumbe nyuma ya pazia wewe unapiga kazi kwa namna ambavyo hakuna mtu anajua.
Hiki siyo kitu cha ajabu, akina Ronaldo hawa unaowaona wanafanya vizuri uwanjani nyuma ya pazia wanafanya mazoezi ya kufa mtu. Akina Diamond hawa unaowaona wanatoa nyimbo mara kwa mara, nyuma ya pazia wanarekodi nyimbo nyingi kuliko unavyoweza kutazamia. Ila chache unazoziona ni hizo. Wanafanya mazoezi kwelikweli. Na wewe fanya hivyo.
-
Jinsi Ya Kubadili Mwelekeo Wa Kile Umachofanya Bila Kuathiri Matokeo (True Story)
Leo nimeikumbuka stori ya Sixto Rodriguez. Huyu ni mwanamziki wa kimarekani ambaye mwaka 1967 alirekodi wimbo wake wa kwanza. Na miaka mitatu baadaye ilikuja kurekodi albamu ambayo ilikuwa inajulikana kwa jina la cold fact.
Mwaka mmoja baadaye alirekodi albamu nyingine ambayo ilikuwa ikijulikana kama coming from reality. Hata hivyo, hizi albamu zake hazikufanya vizuri sana kiasi kwamba ile label yake iliyokuwa imemsajiri iliamua kuachana naye. Kipindi hicho alikuwa katika harakati za kurekodi albamu nyingine na alikuwa tayari amerekodi nyimbo tatu.
Kwa hiyo hicho kitu kilimfanya aachane na muziki huku akianza kujishughulisha na kazi nyingine za kawaida nyumbani kwao. Taratibu alipotea kwenye chati ya mziki wa Marekani.
Ilitokea kwamba kulikuwa na binti ambaye alienda kumwona mchumba wake Afrika kusini. Akawa ameenda na albamu ya Rodriguez AFRKA KUSINI

Akiwa huko wakawa wanacheza nyimbo za Rodriguez na watu wakaanza kuzikubali. Ghafla albamu yake ilikuwa miongoni mwa albamu zenye uhitaji mkubwa zaidi Afrika kusini. Hii ilitokana na ukweli kuwa miongoni mwa nyimbo zilizokuwa kwenye albamu ya Rodriguez zilikuwa za kiharakati, halafu kipindi hicho nchi ya Afrika kusini ndio ilikuwa kwenye harakati za ukombozi wa mtu mweusi.
Hivyo ilibidi shirika moja lianze kuchapa na kusambaza nyimbo zake kulingana na uhitaji wake. Kutokana na umaarufu wa nyimbo zake watu waliamua kumtafuta mwanamziki huyo ili aweze kuja Afrika kusini kufanya show kwa mashabiki wake wa muziki. Hata hivyo hakuna mtu aliyekuwa anajua habari zake. Baadaye ilikuja kusambaa miongoni mwa watu kwamba mwanamziki huyu alijiua baada ya albamu zake kutofanya vizuri.
Lakini mwanahabari mmoja hakuamua kuchulia kitu hiki kama kilivyokuwa kinasambazwa na watu. Hivyo aliamua kuanzisha tovuti ambayo lengo lake lilikuwa ni kumtafuta mwanamziki huyu tu. Siku moja mtoto wa Rodriguez akiwa anapita mtandaoni aliona hiyo tovuti ambayo ilikuwa imelenga kumtafuta mwanamziki huyo. Aliandika pale kwenye ile tovuti kwamba Rodriguez ni baba yangu, na ninamaanisha hilo. Akawa ameacha mawasiliano yake. Baadaye alipigiwa simu na mipango ya Rodriguez kwenda Afrika kusini ilifanyika.
Habari zilisambaa sana kwamba legendari wa mziki alikuwa hai na alikuwa anakuja Afrika kusini. Watoto wa Rodriguez walikuja na baba yao ila hakuna mtu hata mmoja aliyekuwa anatazamia kukutana na watu wengi kwenye hiyo show. Sio hata Rodriguez mwenyewe.
Ila cha kushangaza walipofika Afrika kusini walishangaa kukuta watu 5000 na tiketi zilikuwa zimeuzwa zote na kuisha. Rodriguez aliposimama kwenye jukwaa alishangiliwa na watu waliokuwepo kwa dakika 10 mfululizo (10 minutes standing ovation).
Kumbe umaarufu wake Afriks Kusini ulikuwa ni mkubwa sana kuliko mtu msanii mwingine nchini Marekani. Na alikuwa tayari ameuza nakala za albamu yake kuliko wasanii maarufu wa kipindi hicho kama Bob Dylan na Cat Stevens.
Nyimbo za Rodriguez zinatupa picha ya jinsi kitu kinaweza kukataliwa nyumbani, lakini kikaja kukubalika ugenini, kisipokubalika leo hii basi kinakuja kukubalika kesho. Lakini ili kiweze kukubaliwa utapaswa kuhakikisha umekifanya na kukimaliza.
Lakini pia ni funzo kubwa kwamba usikate tamaa mapema. Kuna wakati unapaswa kubadili mwelekeo kwa sababu kule ulipokuwa umeleekeza mwanzoni siyo sehemu sahihi.

Naipenda sana hii picha ya mvuvi. Huyu jamaa, baadaye anaweza kukata tamaa, lakini kumbe issue hapa siyo kukata tamaa, issue ni kubadili mwelekeo kidogo tu na mambo mengine yote yakakaa sawa.
Kwa Rodriguez muziki wake haukubalika nchini mwake. Lakini, kumbe kuna sehemu muziki wake ulikuwa unahitajika. Kazi yako kubwa ni wewe kujua wapi watu wanahitaji kazi zangu.
Kazi yako ni kusoma mazingira ili ukiweka chambo, samaki wanase.
Anyway, leo vipi? Angalia hii video yangu hapa youtube kisha usubscribe.
Mpaka wakati mwingine. Mimi ni Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE
0755848391
Morogoro-Tz
-
Usiishie tu kukaa kwenye kochi na huku ukisema, ONE DAY YES!
Kwa jinsi hii hata kama una ndoto kubwa hazitaweza kutimia. Kitu kikubwa ni wewe kuchukua hatua ili uweze kufikia malengo na ndoto zako. Hakuna ndoto kubwa inatimia ukiwa umekaa kwenye kochi. Huwa napenda kusema hata watu ambao wanapata lift siyo wale waliokaa nyumbani wakiisubiri, bali wale wanaokupa barabarani wanaendelea na safari.
Wakati unasema, ONE DAY YES vitendo vyako pia vioneshe hilo
#FANYA #onedayyes #inawezekana #songambele #usirudinyuma #hainakufeli #godiusrweyongeza -
Jinsi Teknolojia Kidogo Inavyoweza Kuleta Mabadiliko Makubwa Kwenye Biashara

Siyo kwamba mara zote utahitaji kuwa wa kwanza kufanya kitu fulani ili ufanikiwe.
Ukweli ni kwamba muda mwingine utahitaji ubunifu kidogo. Au utahitaji kuweka teknolojia kidogo tu na kubadili kila kitu.
Mfano Amazon, ujue wazo lao la kuuza vitabu halikuwaa jipya au hata bidhaa nyingine walizokuja kuuza baadaye.
Watu walikuwa wananua na kuuza vitabu kabla yao. Kampuni ya WARMART ulikuwa unafanya hiyo biashara.Wenyewe walichofanya ilikuwa ni kuongeza teknolojia kidogo tu kwenye kitu kilichokuwepo.
Waliona kweli watu wanahitaki kusoma vitabu, ngoja niongeze teknolojia kidogo tu niwasaidie watu kupata vitabu mtandaoni.
Kitu kilichokuwepo kikapewa teknolojia na watu wakakipenda sana.
Wewe pia huhitaji kuwa wa kwanza ili ufanye makubwa. Kwanza ukiwa wa kwanza kabisa watu wanaweza hata wasinunue bidhaa ZAKO.
Matatizo ya watu ni yaleyale unachohitaji wewe Ni
Kuongeza teknolojia kidogo kwenye kitu ambacho watu wamekizoea.
Watu wamezoea kusoma vitabu, unawawekea mtandaoni. GETVALUE, AMAZON.Watu wamezoea kutafuta taarifa, warahisishie upatikanaji. GOOGLE, BING
Watu wanapenda kuwasiliana wape nAmna ya kuwasiliana. APPLE, SAMSUNG, AMAZON, TECHNO
Watu wanapenda kuwatumia ndugu zao fedha, Ila sasa utumaji siyo wa kuamininika. Hivyo, watengenezee teknolojia nzuri ya kutuma na kupokea fedha. M-PESA
Watu wanapenda kuangalia tamthiliya, ongeza teknolojia kidogo, Kisha wape movie za kutosha. NETFLIX.
Watu wanasafiri, na teksi ni kitu muhimu kwenye usafiri. Wasaidie kupata teksi kwa haraka popote walipo. UBER
Kwa hiyo nisikilize. Huhitaji hata kuwa wa kwanza kufanya kitu cha kipekee ambacho hakijawahi kifanyika. Angalia Vitu vilivyopo Sasa hivi. Kisha jiulize ni teknolojia gani kidogo naweza kuongeza hapa ikaleta matokeo ya tofauti.
Na kwenye biashara yako hiyohiyo. Jiulize ni teknolojia gani unaweza kuongeza sasa hivi ikarahisisha upatikanaji wa huduma na kuongeza mauzo?
Kama ipo, itumie.
SOMA ZAIDI: Jinsi Ya Kudandia Teknolojia Mpya
-
Hii Ndio Gharama Halisi Ya Kufanikiwa. Upo tayari Kuilipa?

Unaweza ukawa unajilinganisha na watu wengine na pengine kuona kama unachelewa kufanikiwa ukilinganisha na wengine.
Ila sasa usichokijua ni nguvu na juhudi lakini pia miaka ambayo hao watu wamekuwa wakifanya kitu ambacho wanafanya.
Unawajua imewachukua miaka mingapi kufikia walipofikia?
Ebu kwa mfano tuseme wewe ni kijana amayependa utangazaji, na Salim Kikeke ni mtu unayetamani mafanikio yake! Unajua miaka mingapi amekuwa kwenye industry ya utangazaji? Unajua?
Ukifuatilia utagundua kuwa amekuwa akifanya anachofanya kwa miaka mingi.
Sasa swali langu kwako, upo tayari kulipa gharama unayotakiwa ili uweze kufikia kule unapotaka! Upo tayari? Upo tayari kukifanya kwa miaka yote kama ambavyo yeye amefanya
Hapo Sasa ndio ujue kuwa mafanikio makubwa siyo rahisi, yanachukua muda.
Na hili siyo kukuogopesha bali kukuonesha uhalisia wa kile unachotakiwa kufanya mpaka ufike kule unapotaka.
Sasa leo nataka uangalie video hii niliyorekodi miaka Kama kumi iliyopita😂😂. Halafu, ukishaiangalia. Subscribe kwenye channel yangu pia.
Mpaka wakati mwingine, mimini GODIUS RWEYONGEZA
0755848391
Morogoro-TzNB: LEO nataka ufanye kitu kimoja tu, uangalie video ya gu yotote YouTube. Kisha usubscribe na kuwashirikisha wengine.
BONYEZA HAPA kuingia kwenye YouTube channel yangu.
-
Maisha Ni Wajibu Wako
Nataka, ifahamike kuwa maisha ni wajibu wako. Ukishinda au ukishindwa ni juu yako.
Kama kila mtu akijenga utaratibu wa kuona maisha Kama wajibu wake tutafika mbali unajua kwa nini? Kwa sababu, ukianza kuona maisha kama wajibu wako utapambana kwa hali na mali kuweka kila Kitu sawa. Hutakuwa tena na muda wa kumlalamikia mtu KUWA Kitu fulani hakijakaa sawa au hakijafanyika.
Kwa mfano ukilalamika KUWA hakuna ajira. Hausaidii chochote, ila ukiona kwamba kweli hakuna ajira. Ngoja sasa na Mimi nipambane nitumie mitaji niyopewa bure kama kipaji, nguvu ZAKO, ujuzi, muda wako, na mitaji mingine uliyonayo.
Soma zaidi: MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA
Unatumia mitaji hii kupata fedha, ambayo baadaye unaweza kuitumia kufanya kitu Cha maana.
Napenda sana ule usemi wa Martin Luther King Jr. Anaosema kuwa kama kila mtu akifangia barabara dunia hii itakuwa safi Sana. Yaani, ebu fikiria hivi, kama kila mtu mtaani mwake akifagia mazingira yanayozunguka ya nyumba yake tu. Si mtaa wote utapendeza ndani ya siku moja? Si ndio?.
Sasa na kwenye hili suala zima la ajira. Kama kila mtu akisema ngoja kwanza nipambane na hali yangu. Nifanye kile kinachoweza tu. Niamini mimi, ndani ya miaka mitano mpaka kumi tuna uwezo wa kutatua tatizo hili la ajira.
SOMA ZAIDI: HUWEZI KUMKODISHA MTU WA KUKUPIGIA PUSH UP
Bado huamini tu? Sikiliza, kama kwa mfano wewe ulisema kwamba kuanzia leo, nitapambana nipate elfu mbili, elfu tatu, nne au tano na kuiweka akiba. Kila siku. Naamimi, kuwa baada ya miaka mitano, akiba yako hii ya elfu 2 kila siku. Itakuwa imekufikisha mbali. Tena siyo mbali kidogo, mbali sana tu.
Hii ndio Dhana nzima ya kuona maisha Kama wajibu wako. Na siyo wajibu wa MTU mwingine. Siyo wajibu wa mjomba au babu!
unahusika wewe mwenyewe bila kumtulia mtu lawama au kumtegemea mtu.
Sikiliza, kuanzia leo hii, Anza kujitegemea.
Usilalamike wala kumtupia mtu yeyote yule lawama. Kukitokea tukio. Jiulize ninahusikaje hapa kulitatua. Kama lipo nje ya uwezo wako achana nalo. Pambana na kile kilicho ndani ya uwezo wako.
SOMA ZAIDI: Hivi Ndivyo Unaweza Kufanya Mishale Inayolenga Kukuangamiza Kuwa Baraka
Mpaka wakati mwingine, mimini GODIUS RWEYONGEZA
0755848391
Morogoro-TzKama umependa makala hii, utapenda pia Makala ninazotuma kwa njia ya baruapepe. Jiunge na mfumo wetu wa kupokea Makala kwa njia ya baruapepe kwa kujaza taarifa zako hapa chini
-
Mimi Nakuamini Sana
Kama kuna mtu namwamini Basi, Ni wewe…
Naamimi haukati tamaa
Naamimi hauko tayari kurudi nyuma hata ukikutana na kikwazo
Na hicho kitu ukiendeleze kila siku.
Usikate tamaa na wala usirudi nyuma.
Endelea kupambana.Kikubwa ujue malengo yako.
Uyafanyie kazi kila siku hata kama ni kwa udogoUnaweza usione matokeo kwa muda mfupi, Ila Hilo kisikukatishe tamaa.
Maana yajayo yanafurahisha.
Ni Mimi
Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE CONSULTANCY.
Tukutane kesho
0755848391Rafiki yangu, Kama umependa makala hii, utapenda pia mafunzo ninayotoa kwa njia ya baruapepe. Weka taarifa zako hapa chini, ili uwe miongoni mwa watu wanaopokea mafunzo yangu kwa baruapepe.