-
USHAURI: Jinsi Ya Kutunza Fedha Itakayokusaidia Kuanzisha Biashara
Moja ya eneo muhimu sana kwenye maisha ya kila siku Ni fedha. Upende usipende fedha ni muhimu tena sana.
Maana hakuna hata siku inapita bila ya wewe kutumia fedha.
Ukiamka tu asubuhi, ujue kitanda ulichokuwa umelalia ni FEDHA.
Ukivaa nguo zako, ujue umevaa fedha.
Ukipata kifungua kunywa, ujue hizo ni fedha pia.
Ukipanda daladala, hiyo nayo ni nini….Sikiliza sasa, fedha ni muhimu sana, kiasi kwamba baada ya hewa ya oksijeni ambayo tunaipata bure, fedha ndio inafuata kwa umuhimu…
Sijui unanielewa hapo bwashehe….Sasa mbali na umuhimu wote huo wa fedha, bado kuna watu wanaifanyia masihala.
Lakini wengine wanapata changamoto wanapokuwa na fedha.
Fedha ni chanzo Cha furaha yote Na siku ya leo, nataka nitoe Ushauri kwa ndugu yangu na rafiki yangu Isack
Anasema hivi
Brother m n kijan delev bajaj nataman san kufug kuku ila kinacho nishind upend w kuifaz hela kutafut mtaj kilanikipat ela kidog matumiz yanaongezeka
Isack kutoka Mbeya
Ok vizuri sana ndugu yangu Isack. Kwanza nikupongeze kwa kuwa na ndoto na lengo la kufuga kuku.
Maisha yanaanza na malengo. Maana vijana wengi wanashindwa kufanya makubwa kwa sababu tu hawana ndoto wala malengo makubwaIli uvuke hiki kizungumkuti unapaswa kuwa na malengo au ndoto kubwa.
Labda ka ushauri kidogo tu kuhusu ndoto Yako. Usiishie tu kusema natamani kufuga kuku. Bali iweke sawa ndoto yako katika namna ambayo itakusuma zaidi
Kwa Mfano, ndoto Yako ikiwa ni kuwa mzalishaji na msambazaji nambari moja wa mayai kwa mbeya nzima.
Au mzalishaji nambari moja wa kuku wa nyama mkoa wa mbeya au hata nyanda za juu Kusini.
Yaani, kwamba ujenge jina kiasi kwamba yakizungumziwa mayai mkoa wa mbeya, au kuku wa nyama, basi jina Isack ndio liwe la kutajwa masikioni mwao.Ni kweli hii ni ndoto kubwa, Ila sasa ubora wake ni kwamba unaweza kuanza kuifanya hata kwa udogo. Lakini pia hii ndoto itakusukuma siyo tu, uanze kufuga kuku. Bali utaenda zaidi ya hapo. Ujue ukiwa na lengo la kufuga kuku, hata baadaye ukijenga bada na kufuga kuku kumi tu, utaona Ni sawa. Ila Unapokuwa unajua mkoa mzima wa mbeya unakutegemea wewe kwa ajili ya mayai, au nyama ya kuku. Hapo utaweka juhudi zaidi.
Sasa tuongelee upande wa fedha.
Ili uweze kufanikishaa ndoto yako hiyo, jua wazi kuwa fedha haikwepeki. Utahitaji fedha tu. Na sehemu ya kuanza kupata fedha ni hiyo kazi uliyonayo. Ngoja nikwambie kitu rafiki yangu, nataka wewe uvunje rekodi ya KUWA dereva wa Bajaji wa kwanza, kutoka kwenye udereva mpaka kujenga ngome kubwa.
Unajua utaendaje. Fuatilia kwa umakini hapa
Kila siku kwenye kazi yako, jiwekee kiwango ambacho utakuwa unaweka akiba kuanzia leo. Kwa mfano, labda unaweza kuniambia nitaweka akiba ya elfu kumi kila siku. Kwa hiyo, kwenye kazi yako utakayokuwa unafanya utapaswa ujitume kwanza upate pesa uliyokuwa unapata kawaida, lakini pia utapaswa ujisukume uweze kutengeneza fedha ya ziada ya akiba, ambayo ni elfu kumi.
Najua lengo hili linaweza kuwa kubwa, lakini sasa hakuna jinsi. Kwa sababu kwanza umeshakuwa na ndoto kubwa, wewe pia unapaswa ujitume kiasi cha kutosha, ili hii ndoto yako uweze kuifanikisha. La sivyo, itabaki KUWA ndoto ya Habunwasi.
Ndoto kubwa zinahitaji kujitoa. NDOTO KUBWA ZINAKUHITAJI ULIPE GHARAMA. Na hii ni gharama mojawapo.
Kwa hiyo basi, kwa mpango huu maana yake, Kuna wakati utalazimika kuamka mapema sana kwa ajili ya kuanza kazi. Utalazimika kuwasiliana na watu mbalimbali ambao unawajua huwa wanasafiri kutoka eneo moja kwenda jingine, ili uwachukue wewe wakupe fedha.
Utalazimika kuacha kuangalia mechi hata kama ulikuwa unaipenda ili upige kazi ya kukuingizia kipato.
Na hata mchepuko wako,…au basi, utajua mwenyewe unafanyaje na mchepuko wako.Bwana Isack nataka uanze kufanya hivi vitu kitalaam zaidi. Yaani, usiishie tu kutafuta hela na kuweka akiba chini ya godoro.
Hapa chini Kuna maeneo matatu ambayo napendekeza uweze kuweka akiba yako.
Nenda benki kafungue akaunti. Kisha weka utaratibu wa kuweka kiwango cha akiba ulichopanga.
Ubora siku hizi benki zimerahisisha. Unaweza kuweka fedha benki ukiwa hata mtaani kwako. Au pale kijiweni baada tu kumshusha abiria…
Sijui unanielewa….Kuna baadhi ya benki pia zinaruhusu wewe kufungua akaunti kwa mawakala. Hili nalo ni bao kisigino ndugu Isack. Kumbe haulazimiki tena kupanga foleni benki ili ufungue akaunti. UNACHOHITAJI NI KUDANDIA TEKNOLOJIA KIHIVYO.
Ukishafungua akaunti, hiyo hiyo kadi ya benki hiyo. Unaweza hata kuituma kwa bibi yako kijijini. Maana, kadiri unavyoendelea kuweka akiba najua utashawishika kwenda kuitoa fedha ukiwa na kadi. Ni Bora uitume Kijijini kwenu, au la unaweza kuiharibu kadi kabisa. Siriazi. Ujue hapa ninaongelea Mambo siriazi kwa ajili ya malengo na ndoto zako.
Ukikaa na hiyo kadi utashawishika kwenda kutoa fedha benki siku ukikutana na changamoto kidogo. Ila kama kadi huioni, itakusaidia usitoe pesa yako kwa haraka.
Kwa hiyo, unaweza kuiharibu kadi, ukifika wakati wa kutoa fedha benki utaomba kurenew kadi yako.
Ngoja ninywe maji kwanza, kabla sijaendelea…
Enhee, sasa bwana Isack, ukiachana na kungua akaunti benki. Unaweza kufungua akaunti UTT.
UTT, Ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja ulio chini ya serikali ambao unawawezesha watanzania wenye fedha kidogo kuzikusanya kwa pamoja. Ambapo hizo fedha baadaye zinawekezwa kitalaam. Kwa fedha yako unayoweka, baadaye ukija kuitoa, unaitoa na faida.Tena badala ya kufungua akaunti benki, Bora ufungue akaunti UTT mfuko wa Umoja. Au wewe unaonaje?

Huku fedha yako inakaa, Ila siku ukiihitaji, utajaza fomu, na itachukua siku saba tu kuipokea
Ukiona maelezo ya UTT huyaelewi vizuri hapa, unaweza kuwatwangia jamaa wa UTT wenyewe kwa namba hii 0754800455. Watakupa kizima. Halafu namba yenyewe unapiga bure bila hata kulipia . Yaani, hata kama hauna bando sasa hivi, ukipiga inaita na unaongea nao, labda ukipiga muda ambao siyo wa kazi mzee baba.
Sijui niendelee…au niishie hapa
Ngoja niendelee, kwanza…
Ukiona mizunguko yote hiyo mirefu basi kafungue laini ya simu maalumu kwa ajili ya kuweka akiba tu. Halafu unajua utafanyaje. Ukishafungua hii laini ya simu. Mfuate mtu wako wa karibu, labda mama, baba, mke, rafiki au yeyote unayemwamini. Utamwambia aweke namba ya siri.
Kwa hiyo, wewe utakuwa na laini, labda tuseme yenye Mpesa. Ila hujui namba ya siri. Utakuwa unaweka akiba kila Mara, Ila siku ukija kutoa fedha, utapaswa kuomba namba ya siri kwa mtu aliyekusaidia kuweka namba ya siri.
Mtu huyu unapaswa kumshirikish lengo na umwambie asikupe namba ya siri mpaka utakapokuwa umefikisha kiwango fulani Cha pesa.
ONGEA naye, kuwa mimi nataka niweke akiba ya milioni tatu kwenye hii laini. Tafadhali usiniambie namba ya siri mpaka nitakapokuwa nimeweka kiasi Cha milioni tatu kama akiba.
Siku nikikuonesha kuwa nimeweka milioni tatu kama akiba. Basi hapo ndipo utapaswa kuniambia namba ya siri.
Naona maji yangu ya kunywa yameisha, na Mimi naacha kuandika, ngoja nikatafute maji ya kunywa kwanza.
Halafu sikiliza kwanza
Hapa nina orodha, ya vitabu vitakavyokusaidia wewe Kufanikisha haya yote niliyoandika leo.1. MAAJABU YA KUWEKA AKIBA
2. MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE
3. JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKOKupata vitabu hivi, wasiliana nami kwa 0755838391.
Mimi ni Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE CONSULTANCY
0755848391
Morogoro-TzUna swali, maoni au ushauri? Kuna jambo linakutatiza, unataka ushauriwe?
Basi sikiliza, tuandikie chini
.
Nenda benki ufungue akaunti.
Kisha Anza kuweka fedhaFungua laini ya simu ya kuweka AKIBA tu
Thibutu matumizi yako
Kusanya kiasi Cha kutosha kuanza kuwekeza.
-
MAISHA NI KAMA KUENDESHA BAISKELI..

Leo nimeukumbuka usemi wa Albert Einstein. Anasema maisha Ni Kama kuendesha baiskeli, ili usianguke unapaswa kuendelea kunyonga.
Ukiacha tu, unaanguka
Hivi ndivyo ilivyo hata kwenye maisha ya kutafuta…
Ili uendelee kusongambele haupaswi kuacha kuweka juhudi, haupaswi kuacha kupiga kazi kwa bidii, kujituma, kufanyia kazi malengo yako kila siku.
Hivi ndivyo maisha yalivyo.
Ukikata tamaa, Basi…hutoboi..
Kama umependa Makala hii, utapenda Makala zaidi nikazotuma kwa njia ya barua pepe… Jaza taarifa zako zote hapa chini
-
Jinsi Mafanikio Makubwa Yanavyojengwa
Picha hapo chini ni picha ya jengo la Taj Mahal. Jengo hili lipo kwenye Maajabu Saba ya dunia.
Hili jengo lilichukua miaka 22 kujengwa Mpaka kukamilika.
Jengo la Taj Mahal Hiki kitu kikupe picha ya kuwa vitu vizuri kwenye maisha huwa haviji kirahisj. Najua unapenda sana kupata vitu vizuri, lakini vitu vizuri huwa haviji kirahisi. Ni mchakato.
Ndio maana wahenga wetu wanasema kwamba hata mbuyu ulianza kama mchicha. Hii ni kuonesha kuwa vitu vizuri, vipo, lakini vinajengeka kidogokidogo.
Tena wakati mwingine vinaweza kuonekama vinaanza kimasihala vile.
Ebu fikiria kama wajenzi wa ghorofa. Ukikuta wanaanza kujenga ghorofa, wewe mwenyewe unaweza kufikiri wamechanganyikiwa. Eti wanajenga ghorofa Ila wanaanza kwa kushuka chini. Hahaha
Wanachimba shimo reeefu kwenda chini…Hivi ndivyo mazuri yanavyoanza, siyo kwamba mara zote mazuri yataanza kwa uzuri wake. Muda mwingine msingi unajengwa kwanza, halafu ndio Mambo mengine yanafuata.
Rafiki yangu, labda nisisitize tu. Ni kitu gani unapenda kufikia au kupata maishani mwako?
Basi kipe muda. Anza kukifanyia kazi taratibu bila kuchoka. Kumbuka kwamba inawezekana kama hautarudi nyuma.
Hatua moja moja itakufikisha mbali tu.
Inawezekana. Kila la KHERI
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-TzNB: Kama umependa makala hii utapenda pia mafunzo ninayotuma kwa baruapepe. Jaza taarifa zako hapa chini ili uwe miongoni mwa watu wanaopokea mafunzo haya
-
Ufanyeje unapokuwa unasoma vitabu huku unasahau?

Unaendeleaje rafiki yangu, juzi kuna mtu aliniambia kwamba anapenda kusoma vitabu, ila sasa tatizo lake ni kwamba akisoma anasahau alichosoma kwenye kitabu na hata kabla ya kumaliza kusoma kitabu husika.
Kitu hiki ndicho kimeniweka hewani siku ya leo nili niweze kukiandikia maana najua kuna watu wengi pia ambao wanapata shida hii.
Kwanza ninachopenda kusema ni kwamba kama unasoma na unasahau, usiache kusoma vitabu. Endelea hivyo hivyo bila kuacha.
Usitake kuona matokeo kwa siku moja. kuna kitu kinaitwa riba mkusanyiko. Yaani, vitu vidogovidogo vinakusanyika kutengeneza kitu kimoja kikubwa. Unaweza leo hii usione matokeo ya kile unachosoma, ila kumbe yanakusanyika na siku moja katika hali ambayo hutegemei, ukapata matokeo ya tofauti.
Kwa hiyo, kama unasoma vitabu na unasahau, usiache kusoma endelea kusoma.
Kitu cha pili, baada ya kuwa umesoma kitabu, jiulize ni kitu gani kimoja ambacho nimetoka nacho kwenye hiki kitabu? Ni kitu gani kimoja? Usitaka kuondoka na kila kitu kwenye kitabu. Wewe ukipata kitu kimoja tu kutoka kwenye kitabu na hicho kitu ukakifanyia kazi. inatosha.
Kwa mfano, ukisoma kitabu kuhusu fedha na uwekezaji. Toka na kitu kimoja kama kuweka akiba kila unapopokea mshahara wako. Hicho kitu kifanyie kazi. raha ya vitabu ipo kwenye kufanyia kazi kile ulichojifunza na siyo kwenye kusoma tu.
Huo ndio ujumbe wangu kwako wewe msomaji wa vitabu siku ya leo. Kwa msomaji yeyote yule ambaye ni makini, ahakikishe amesoma kitabu changu cha MAAJABU YA KUSOMA VITABU. kina mambo mengi ndani yake ya kukusaidia wewe kuweza kupiga hatua na kufika mbali.
Kwa sasa hivi sina la ziada
Mimi naitwa Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE
Tuwasiliane kwa 0755848391
Baruapepe yangu ni GodiusRweyongeza1@gmail.com
NB. Kama umependa makala hii, utapenda makala zangu za kipekee ninazotuma kwa njia ya barua pepe. WEKA JINA LAKO Na BARUA PEPE YAKO hapa chini ili niweze kukutumia taarifa zako.
-
JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA MTANDAONI-2

Umewahi kujiuliza ni kwa namna gani unaweza kutengeneza kipato kwa njia mtandao wa intaneti? Umewahi kujiuliza kitu kama hiki?
Hiki kitu ndicho kilinifanya mimi niweze kuingia mtandaoni, na hiki kitu ndicho kimenifanya niweze kuendelea kuutumia mtandao huu wa intaneti mpaka leo hii. Niliwahi kuandika makala kama hii siku za Nyuma, hivyo hakikisha unaisoma hiyo makala HAPA
SOMA ZAIDI: Jinsi Ya Kutengeneza Fedha Mtandaoni-1
Kuna kipindi nilikuwa nikisikia stori za watu kama Millard Ayo, kwamba hawa watu wanatengeneza fedha kwa njia ya mtandao. Sasa wali langu lilikuwa hivi hawa watu wanawezaje kutengeneza fedha kwa njia ya mtandao? Wanawezaje, hilo swali tu mpaka sasa hivi limenifungulia dunia na kunifanya niweze kuona vitu vingi sana ambavyo kiuhalisia nisingeweza kuviona bila ya kujiuliza swali la alina hiyo.
Najua kuna watu wengine wengi wanajiuliza swali la aina hii? Pengine na wewe utakuwa unajuliza swali la aina hii. Sasa swali langu kwako ni je, unawezaje kutengeneza fedha kwa njia ya mtandao? Unawezaje?
Kabla sijajibu hili swali, nataka kwanza tujue kwenye maisha watu wanatengenezaje fedha? Kwa mfano, wewe unatengezaje fedha? Kama umeajiriwa, maana yake unaenda kazini unafanya kazi na mwisho wa mwezi unalipwa, unatoa thamani kwanza ndipo unakuja kulipwa.
Kama unafanya biashara, maana yake unapaswa kuwa na bidhaa ambazo watu wanazihitaji, na unapaswa kuzileta bidhaa hizo kwa watu sahihi ili wakupe fedha. Bado tunarudi palepale kwamba unapaswa kutanguliza thamani kwanza.
Kwa chochote kile unachofanya na kinakuingizia fedha halali, ni wazi kuwa utakuwa unafanya kitu kwanza, kisha kitu hicho ndipo unakuja kulipwa.
Nimeona niliweke hili wazi, maana vijana wengi wanapofikiri kutengeneza fedha mtandaoni, basi kitu cha kwanza kabisa wanachofikiri ni kukaa bure bila kufanya kazi yoyote na kulipwa fedha ndefu. Hakuna kitu kama hicho.
Mtandao wa intaneti haumaanishi kwamba ulale na utengeneze fedha ya bure bila kufanya kitu chochote. Badala yake mtandao wa intaneti, upo kurahisisha huduma unauyoitoa au kuifanya bishara yako iweze kuwafikia watu wengi zaidi kwa haraka na kwa gharama kidogo.
Kiufupi kwenye ulimwengu wa leo kila mtu anapaswa kujitahidi kudandia teknolojia.
Kwa biashara au kitu chochote kile ambacho unafanya unapaswa kukiweka mtandaoni, ili kiweze kuonekana ka watu wengi zaidi. kitu ambacho kitakusaidia wewe kukutana na wateja sahihi wa biashara yako.
Kwa hiyo nifanyeje ili niweze kutengeneza fedha mtandaoni.
ANZA KWA KUTOA THAMANI
Ngoja nikwambie kitu, watu wanapenda fedha zao. Hakuna mtu ambaye ametafuta fedha kwa shida, atapenda kuona kwamba fedha alizozitafuta kwa shida zinapotea bila manufaa yoyote yale, badala yake kila mtu anapenda kuona kwamba fedha zake alizozitafuta kwa shida anazitumia vyema. Kwa hiyo, kitu cha kwanza kabisa unachopaswa kufahamu kama unataka kutengeneza fedha mtandaoni ni kwamba unapaswa kutoa thamani kwa watu.
Wasaidie watu kupata wanachotaka
USIINGIE MTANDAONI KWA KUFIKIRI KUTAPELI WATU
Kama nilivyokwambia ni kwamba watu wanapenda fedha zao, hivyo usije ukaingia mtandaoni kwa kufikiri kwamba unaweza kuwatapeli watu fedha zao na kutokomea. Hizo ni fikra za kimasikini sana na hicho kitu ndicho kimefanya vijana wengi washindwe kuendelea wala kufanya kitu chochote kikubwa maishani.
Mara zote kuwa na fikra za namna gani ambavyo unaweza kuwasaidia watu kwanza. Watangulize watu mbele, maana watu wakinufaika na wewe ndio unakuwa unanufaika. Sijui unanielewa…
SOMA ZAIDI: JINSI YA KUANZISHA BLOG
BADILI KITU UNACHOFANYA NA KUWA CHA KITEKNOLOJIA
Ukiangalia biashara kubwa za sasa hivi, hakuna kitu kikubwa ambacho wanafanya tofauti na kwamba biashara hizo nyingi zilikuwepo kwa miaka mingi sana iliyopita.
Biahsara ya kuuza vitabu ni biashara ambayo imekuwepo kwa miaka mingi sana, ila sasa kijana mmoja alifikiria kwamba badala ya kuwa tunazunguka na kutoka huku kwenda kule tukitafuta vitabu kwenye maduka ya vitabu, kwa nini vitabu visiwe vinauzwa mtandaoni na watu wanaweza kuvinunua mtandaoni, hapo ndipo ulipokuja mtandao wa Amazon.
Magari na usafiri wa taxi umekuwepo kwa siku nyingi sana. ila kilichofanyika kwenye ulimwengu wa leo ni kuweka vitu hivi kwenye mtandao wa intaneti. Kwa hiyo, unaweza kununua gari mtandaoni, unaweza kukodisha gari mtandaoni, unaweza kuwasiliana na boda akusafirishe kwa njia mtandao
Nakwambia hivi vitu ili ujue kwamba, unapozungumziwa mtandao, usianze kufikiria kitu cha ajabu cha kufanya kwa njia ya mtandao wa intaneti. Badala yake uanze kutumia vitu hivyo vhiyo ulivyonavyo sasa hivi na kuviweka mtandaoni.
Biashara hiyo hiyo uliyonayo sasa hivi, unapaswa kuiweka mtandaoni na kunufaika na uwepo wa mtandao
Kipaji chako hichicho ulichonacho, unapaswa kukiweka mtandaoni na kunufaika na uwepo wa intaneti.
Mgahawa wako huohuo, utengenezee ukurasa mtandaoni au hata tovuti, kisha sasa ndio uje kunufaika na uwepo wa mtandao.
Rafiki yangu, kwa kitu chochote na kwa vyovyote vile, hakikisha kwamba,
WEKA BIASHARA YAKO MTANDAONI
Kwa biashara yako yoyote ile ambayo unafanya, hakikisha kwamba biashara hii unaiweka mtandaoni. Hata kama ni kipaji chako.
Kuna njia nyingi za kuweka biashara yako mtandaoni kama kufungua tovuti au blog, kutengeneza ukurasa kwenye mitandao ya kijamii, kutengeneza
Anza kuwaonesha watu bidhaa zako, kama utahitaji kuwafundisha watu kuhusu bidhaa zako wafundishe ili waweze kuzielewa kiundani
Jibu maswali na maoni ya watu
Kusanya mawasilino ya watu wanaohitaji bidhaa zao na wasiliane nao
Wauzie bidhaa zako
Hakikisha pia umeangalia video hii hapa chini ambayo ina mafunzo ziaidi kuhusu namna unavyoweza kutengeneza fedha mtandani.
Umekuwa nami
Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE
kama umependa makala hii, nakuhakikishia kuwa utapenda na mafunzo yetu mengine tunayotoa kwa njia ya barua pepe. Jiunge na mafunzo hayo kwa kujaza taarifa zako hapa chini,
-
MAAJABU YA KUAMKA ASUBUHI NA MAPEMA
Benjamin Franklin ambaye anafahamika kama mwananchi wa kwanza Marekani alikwahi kuandika kwamba kulala mapema na kuamka asubuhi na mapema kunamfanya mtu awe na afya njema, tajiri na mwenye busara. Haya maneno aliyaandika zaidi ya miaka 200 iliyopita kwenye moja ya barua aliyokuwa anaandika kwa mwanae. Pengine Franklin angekuwa anarudi leo hii angeshangaa kwa jinsi maneno hayo machache yalivyopata umaarufu hasa kwenye ulimwengu maendeleo binafsi na hamasa. Maneno yake sasa yanatumika kama sehemu ya kuwahamasisha ili wajenge tabia ya kuamka mapema.
Leo hii ukiingia kwenye mtandao wa Google, na kuandika neno early to bed, early to rise utapata matoke zaidi ya laki mbili na elfu sabini. Hii ndio kusema kwamba huu usemi ni miongoni mwa semi zinazotumika sana.
Kipindi Benjamin Fraklin anasema hivyo hakukuwa na maendeleo makubwa kwenye teknolojia na sayansi kama ilivyo sasa hivi. Tafiti za kisayansi zimethibitisha kwa asilimia 100 kuwa maneno ya Benjamin Franklin ni ya ukweli na uhakika. Hivyo, kulala mapema na kuamka mapema kuna uwezo wa kukufanya uwe na afya njema, uwe tajiri na mwenye busara.
Pengine unaweza kujiuliza nawezaje kuwa na afya njema kwa kulala na kuamka mapema tu? Unaweza kuendelea kujiuliza pia kuwa nawezaje kuwa na utajiri kwa sababu ya kulala na kuamka mapema? Na mwisho unaweza kujiuliza nawezaje kuwa na busara kwa kulala na kuamka mapema?
Sasa hapo naomba uvute kiti chako ili nikuoneshe jinsi kulala mapema kulivyo na nguvu hizo zote na zaidi ya hapo.
JINSI KULALA MAPEMA NA KUAMKA ASUBUHI NA MAPENDA KUNAVYOWEZA KUKUFANYA UWE NA AFYA NJEMA
Imethibitishwa kuwa muda wa kulala kwa mwanadamu yeyote unapaswa kuwa kati ya saa sita mpaka nane. Suala la nani analala masaa sita au saba au nane linategemea na mtu mmoja mmoja. Kuna wale ambao mwili wao unawahitaji kulala saa saba, kuna wale ambao mwili wao unawaruhusu kulala saa nane. Mwili ukiunyima usingizi wa kutosha utakuwa unajichosha na itafikia hatua ambapo wewe mwenyewe utapoteza nguvu na uwezo wako wa kufanya kazi kwa weredi.
Nimewahi kusikia hadithi ya mzee mmoja aliyekuwa bahiri na hakutaka kupanga chumba cha kulala. Hivyo, akawa anajibana na kulala kwenye jiko la kazini kwake. Kadiri siku zilizyokuwa zinasogea mzee huyo akawa kama anaumwa. Ila hospitali walipokuwa wanapima ugonjwa wakawa hawaoni chochote. Ndipo watu walimshauri apange chumba na apate muda wa kutosha wa kulala. Alipopanga chumba ndani ya wiki moja ya kupata usingizi unaoeleweka, afya yake ikawa imerudi kwenye hali ya kawaida.
Kumbe usingizi ni muhimu sana kwa afya yako. Kitu kingine kuhusu kulala mapema ni kwamba, saa moja unalola kabla ya saa sita usiku ni bora zaidi kuliko masaa matatu unayolala baada ya saa sita za usiku. Yaani, mwili huwa una mpangilio wake wa kibaiolojia (biological rythm) ambapo katika masaa fulani kuna shughuli zainafanyika. Muda wa kuanzia saa nane mpaka saa 10 ni mida ambayo mwili unakuwa unajitengeneza, hivyo ni muda ambao mtu ananufaika kama ameshalala kwa muda na kuwa kwenye usingizi mzito. Hivyo, kulala mapema kunaufanya mwili kukamilisha zoezi hilo vizuri. Pia mtu anapowahi kulala anapata muda mzuri wa kuwa kwenye usingizi mzito (REM SLEEP) kuliko anayechelewa kulala. Usingizi mzito ndiyo wenye manufaa zaidi kwenye mwili
Kama huamini, toa siku moja ulale saa nne usiku na uamka saa kumi na moja ambayo hayo yatakuwa ni masaa nane kamili. Kisha toa siku nyingine ulale saa saba usiku na uamke saa moja asubuhi. Utagundua kwamba siku uliyolala saa saba usiku na kuamka saa moja asubuhi ni siku ambayo unaamka umechoka huku ukiwa hauna nguvu ila siku uliyoamka saa kumi na moja ni siku ambayo unaamka mwili ukiwa umetulia kwa asilimia zote. Hii ndio maana napenda kukwambia kwamba kulala mapema na kuamka mapena kunamfanya mtu awe mwenye afya njema.
JINSI KULALA MAPEMA NA KUAMKA MAPEMA KUNAVYOWEZA KUKUFANYA UWE TAJIRI
-
Kama unafikiri elimu Ni ghali, jaribu ujinga
Siku Kama mbili zilizopita hivi, nilikuwa naongea na mama mmoja ambaye anamiliki salooon kubwa mkoani Mwanza. Katika kuongea aliniambia kitu ambacho nilikidaka vizuri. Alisema, Mimi nimetumia gharama kubwa kujifunza mambo ya saloon. Gharama ambayo nimewekeza Ni kubwa sana.
Hiki kitu kilikumbusha Ile stori ya kwamba Kama unafikiri elimu Ni ghali jaribu ujinga.
Na kitu ambacho kinaonekana kwa mtu yeyote ambaye amebobea. Hakuna MBOBEVU yeyote ambaye amebobea ndani ya siku moja. Wote wamewekeza gharama tena kwa muda mrefu, kabla ya kufikia hapo unapowaona sasa hivi.
Katika ulimwengu wa leo wengi wanapenda matokeo ya haraka bila kulipa gharama. Unaweza kuyapata ila fahamu kuwa hayatakuwa ya kudumu.
Kuna watu wengi ambao wanapenda wapate elimu nzuri bila kulipia, rafiki yangu mpendwa, elimu ni gharama. Tena siyo gharama kidogo, gharama kubwa.
Wakati mwingine unakuta gharama unayilipia haiendani na thamani kubwa utakayoipata kwenye kitu husika. Huwa napenda kutokea mfano wa vitabu vyangu. Labda kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO au KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI. Hivi vitabu thamani yake ni kubwa kuliko unacholipia.
Kama na wewe upo tayari kulipia kidogo, rusha elfu ishirini nikutumie vyote viwili. Kila kimoja ni elfu elfu kumi. Hizo Ni soft copy.
Kila hardcocopy ni elfu 20.
-
Kiwango Cha Elimu Unachopaswa Kuwa nacho ili uandike kitabu
Leo nimepokea ujumbe wa MTU anateniuliza, kiwango gani Cha Elimu unapaswa kuwa nacho ili uandike kitabu?
Swali hili limenivutia sana kiasi kwamba nimeona niandike Makala na kuileta kwako.
Kwenye ulimwengu wa uandishi kuna waandishi wa kila aina.
Kuna waandishi wenye PHD,
Kuna waandishi wenye shahada moja
Kuna waandishi ambao wameishia darasa la saba n.k.Kwa hiyo, hakuna kiwango maalumu cha elimu ambacho MTU anatakiwa kuwa nacho.
Kitu kikubwa kwenye uandishi ni mwandishi kuhakikisha ameijua mada anayoiandikia kiundani. Ameitafiti na kuifuatilia nje ndani.
Hicho ndiyo kitu muhimu sana.
Kiufupi ni kwamba kama unajua kusoma na kuandika Basi unapaswa kuandika.
-
Tuna saa 24 tu kwa siku
Kila siku tuna saa 24 tu. Hakuna siku ambayo utakuwa na saa zaidi ya hizo, hivyo, unatakiwa kuutumia vizuri muda wako.
Watu waliofanya makubwa, na watu wanaofanya vitu vya kawaida wote Wana saa 24.
Sasa kwa Nini wewe usitumie muda wako vizuri?
-
Baadaye Siku Ya Leo Nitasikika Kwenye Temino Ya Clouds Fm
Hello upande wa huko
Nimeshaamka mapema siku ya leo kama ilivyo kawaida yangu. Na kama kawaida hapa nipo nyuma ya PC yangu nikiwa naandika kitu.
Leo sina kitu kikubwa sana cha kukwambia labda taarifa fupi tu kuwa
Baadaye siku ya leo Nitakuwa kwenye Temino ya Clouds Fm, kipindi kinachoendeshwa na Harris Kapiga, tukipiga stori kuanzia saa tisa mpaka saa 11.
Najua wengi mmekuwa mkisoma makala zangu kupitia mtandao na hasa mtandao wangu wa SONGAMBELE. Sasa leo unapaswa kutenge muda upate kunisikiliza kabisa pengine kwa mara ya kwanza.
Lakini na wewe hupaswi kusubiri kabisa mpaka huo ndio uje kunisikiliza,. Unaweza kunisikiliza na hata kuniona kabla ya hapo kwenye youtube yangu kwa kufuatilia baadhi ya mafunzo yangu na hata kusubscribe.
Sasa kuna kitu nataka nikwambie. Leo kabla sijaingia kwenye kipindi hicho mchana saa tisa. Nataka nihakikishe kwamba nimekusainia wewe kopi moja ya kitabu cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni au la hata nimekutumia nakala laini ya kitabu changu cha MAISHA NI FURSA, MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA na KIPAJI NI DHAHABU
Nakala ngumu ya kitabu cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni ni 20,000/- tu. na ninaweza kukutumia popote pale ulipo Afrika Mashariki.
Nakala laini ya kitabu cha kutoka Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni ni 10,000/- tu.
Lipia leo hii nakala yako kwa
Ni mimi rafiki yako,
Godius Rweyongeza
075584831
Morogoro-Tz
NB. Saa tisa mchana mpaka saa 11 leo usisahau kufungulia redio yako ili kumsikiliza Godius Rweyongeza. Lakini kabla ya hapo hakikisha umepata ya kitabu changu cha kutoka SIFURI MPAKA KILELENI au VINGINE HIVI HAPA