Home


  • Ajionavyo Mtu Ndivyo Alivyo

    Miongoni mwa usemi maarufu sana Ni ule usemi wa Napoleon Hill ambapo anasema chochote ambacho akili yako inaweza kushikilia na kuamini, kinaweza kufikika.

    Ndio maana unashauriwa kujenga picha ya kile unachotaka kufikia. Ikikaa kichwani mwako kwa muda mrefu, huku ukiwa unaifanyia kazi. Ujue kwamba itafikia hatua utaifikia

    Sasa wewe picha yako kubwa unayoiona ni ipi?

  • Vitu Vitano Vya Kukusaidia Kuendelea Kuwasha Moto Wa Kufanikisha Malengo Yako.

    Lengo lilikuwa ni kukufungua na kukuonesha kuwa mwaka huu mpya umeuanzaje au ndio kwanza unazubaa zubaa.

    Nadhani ambao huwa hawasahau ni wenye lengo la kuoa/kuolewa tu!!
    Maana wakikupa kadi hata kama ni Januari na wanafunga ndoa mwezi wa tisa.  Halafu ukajichanganya ukatoa ahadi, watakudai ahadi yako mpaka utoe senti ya mwisho…

    Naona unacheka! Umekumbuka ule ujumbe unaokukumbusha kutimiza ahadi yako nini?

    Sasa leo nataka nikuulize kwa mara nyingine, hivi bado kweli unakumbuka lengo lako la mwaka huu? Bado kweli una motisha ya kulifanyia kazi?
    Bado unajisukuma kulifanyia kazi?

    Kwa hiyo, hakikisha kila siku asubuhi unajikukumbusha malengo yako, mchana unajikumbusha malengo yako, jioni unajikumbusha malengo pia.

    Jikumbushe malengo yako pia unapokwama au unapokuwa katika hali  ya sintofahamu.

    Kila siku jipe jukumu la kufikiria mawazo 10 ambayo unaweza kuanza kufanyia kazi mara moja ili yakusaidie kufanikisha lengo lako.
    Ushawahi kufanya hili zoezi.
    Lianze leo hii.
    Anza sasa hivi ni mawazobyapi 10 ambayo unaweza kufanyia kazi leo hii yakakusaidia kusogea karibu na lengo lako?
    Je, ni kuanza kusoma kitabu fulani…
    Je, ni kupiga simu..
    Je, ni kuonana na MTU fulani..
    Je, ni kuachana na tabia fulani…

    Ni nini sasa…ebu andika chini.

    Bado huamini tu, najua kuamini kwa mwafrika ni mpaka aguse 😂😂. Haya, pata nakala yako sasa hivi ili ujionee mwenyewe.
    Nakala ngumu ni elfu 20. Na nakala laini ni elfu 10. Tuwasiliane Sasa hivi kwa 0755848391.

    Niache kwanza niendelee mbele maana safari bado…

    Toa ripoti kila Mara kwake ili aweze kuona maendeleo yako. Ukikwama mshirikishe ili akuoneahe namna unavyoweza kuendelea mbele zaidi…

    Iko hivi, lengo huwa halitimii kwa siku moja mwishoni mwa mwaka. Kila siku Ni siku yako kufanyia kazi lengo lako.

    Huwezi kuweka lengo na kusubiri lengo Hilo lije kutimia mwishoni mwa mwaka. Lengo lako linapaswa kufanyiwa kazi kila siku. Jumatatu mpaka jumapili, siku saba za wiki.

    Pambana kila Mara kuhakikisha unalifanyia kazi.

    Bado unataka niendelee au umechoka?
    Umechoka eti!
    Kama bado una motisha na nguvu zaidi kama Mimi, weka jina lako na email yako ili niendelee kukupa mafunzo yalioenda shule kama hili kupitia email. Fanya hivyo Sasa hivi hapa chini 👇🏿👇🏿

  • Kitu kinachowakwamisha wengi ukiwemo wewe

    Wengi wanakwama kwenye maisha, siyo kwa sababu nyingine bali kwa sababu tu ya UJUAJI. Yaani, wanajua, na hata hii makala wataipitia juu juu kwa sababu tu wanajua.

    Umewahi kuona watu wa aina hiyo ee. Ukianza kuongea naye jambo anakwambia na hilo nalijua.

    Mkianza kuongelea mada fulani, anajijua. Yaani, anajua kila kitu, 

    Kwenye mahusiano, yeye ndiye nyota.

    Mkiongelea michezo anajua kila kitu.

    Mkiongelea kuhusu siasa, anajua kila kitu.

    Mkiongelea usomaji wa vitabu, anajua kila kitabu,

    Mkiongelea wasanii, anajua kila kitu mpaka chakula waichokula leo…..

    UJUAJI, UJUAJI, UJUAJI.

    Muda mwingine wewe unapaswa kuwa msikivu. Wasikilieze wengine wanasemaje, utapata kujifunza mengi, na utapata mengi ya kufanyia kazi kwenye maisha kuliko ukiwa mjuaji zaidi.

    Wengi wanakwama maishani kwa sababu ya ujuaji mwingi. Mtu anasoma makalaunayoandika kwa juu kwa kusema kwamba ANAJUA.

    Au mwingine anasoma ila hafanyi kazi, kwa kusema kwamba anajua.

    Mwisho wa siku hapati matokeo. Anaendelea kuwa na maisha yaleyale.

    Labda nikuulize, ni kwa kiwango gani ujuaji umekukwamisha wewe kufika mbali maishani. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

  • Mbinu za kutimiza malengo yako

    Habari ya leo rafiki yangu. Moja ya mada ambayo nimeiandikia sana kuliko mada nyingine, Ni mada ya malengo.
    Kuanzia namna ya kuweka malengo
    Namna ya kuyafanyia kazi malengo yako
    Namna ya kuyafanikisha na Mambo mengine yanayouhusiana na malengo

    Nimeandika makala nyingi zinazohusiana na hii mada.

    Leo hii kuna mtu kaniuliza mbinuza kutimiza malengo yake. Nimeona nimrudishe nyuma kwenye hizi makala za kitambo ili aweze kufaidika na uhondo uliopo humu; maana ya kale ni dhahabu.

    ujumbe kutoka kwa mmoja wa wasomaji wangu.

    Makala nyingine hizi hapa

    Ninaweza kuendelea zaidi ya hapa. Kwenye tovuti hii Kuna makala nyingi kuhusu malengo Kuliko unavyoweza kusoma kwa wiki moja au mwezi. Anza na hizi nilizokutumia.

    Hizi makala kwa umoja wake ni zaidi ya kitabu. Siriazi! Ebu zisome, Kisha utaniambia.

    mpaka wakati mwingine. Kama umependa Makala hizi, tafadhali usisite kujiunga na mfumo wetu wa kupata mafunzo zaidi hapa chini. Ebu weka jina lako na barua pepe yako, na sisi tutakusuprise kwa mafunzo zaidi.

  • Njia Rasmi Ya Mkato Itakayokupa Mafanikio Makubwa

    Chagua kitu kimoja, Kisha hakikisha kwamba unakijua kitu hicho nje ndani

    Kama ni biashara basi amua kuijua nje ndani.
    Kama ni kipaji chako basi zama na ubobee kwelikweli.

    Kama ni njia ya mkato, basi hii ndio njia pekee ya mkato unavyoweza kutumia kufikia kule unapotaka.

    Ukiwa mtu wa kugusa vitu kwa juu juu. Hutakaa ubobee na mara zote utakuwa unaona kama unachelewa kufanikiwa.

    Kumbe tatizo ni lako.

    Jipe miaka mitano mpaka kumi ya kuzama kwenye kufanya kitu ulichochagua bila kuacha.

    Kama umenielewa, jiunge na mfumo wetu wa kupokea mafunzo kwa barua pepe. Jiunge hapa chini

  • Uwezo mkubwa ulio ndani yako

    Leo nimeikumbuka sana siku nilipoenda kumtembelea rafiki  yangu. Kama ulivyo utaratibu wetu waafrika. Alinikaribisha kwa kuleta vinywaji pale mezani.

    Lilikuwa Jambo la furaha sana kukutana na hiyo rafiki yangu na stori zilianza bila kuchelewa, huku tukikumbushana baadhi ya mambo yaliyowahi kutokea siku za nyuma na hata kutaniana.

    Wakati stori zinazidi kukolea, glasi mojawapo pale mezani ilidondoka chini na kupasuka.

    Hili hambo lilinifanya nitafakari sana, ukizingatia zile glasi zilikuwa bado mpya kabisa.

    Nilibaki najisemea kimoyomoyo kwamba hii glasi imeharibika ikiwa bado na uwezo makubwa ndani yake ambao ulikuwa haujatumika.

    Hiki kitu kunatokea kwa watu wengi pia..
    Kuna watu wengi wenye uwezo mkubwa ila huwa hawautumii hata kidogo. Uwezo huu wa kipekee ungeweza kuinufaisha dunia…

    Pengine hata wewe uko kwenye hili kundi.

    Labda swali la kujiuliza hapa ni kwamba unautumia KWELI uwezo wako? Unautumia?

    Kama hautumii uwezo wako ipasavyo, unadhani kitu gani kinakuzuia wewe kuweza kufanya hivyo?

    Amua kuanzia leo hii kuwa nitakutumia uwezo wangu.
    Nitakutumia kipaji changu, nitatumia ubunifu wangu au chochote kile nilichonacho.

    Kitumie tafadhali, manufaa siyo kwa ajili yako tu. Bali yanakuwa kwa watu wote

    Mpaka hapo umenielewa?

    Kama umenielewa, weka email yako hapa chini, ili niendelee kukuelewesha zaidi kupitia jumbe zangu za kipekee nikazotuma kwa njia ya email kila siku.

    Jaza taarifa zako hapa👇🏿👇🏿

  • UAMINIFU NI MTAJI

    Mwaka 2018, nilisafiri kwenda Arusha na baadaye nikaenda Bukoba kwa wazee kusalimia. Ilikuwa ni safari ya zaidi ya mwezi…

    Nikiwa Arusha kuna jamaa alinitafuta. Alikuwa mshikaji ninayemfahamu. Au basi niseme tulikuwa tunasoma wote pale SUA.

    Aliniambia anataka nimkope fedha kama laki tano hivi, na angenirudishia hiyo fedha ndani ya wiki…
    Kuna fedha alikuwa anaisikilizia….

    Nilimwambia wiki moja siyo kubwa sana, subiri wiki ipite, utapata hiyo fedha unayoisikilizia na utaendelea na kazi zako.

    Alivyo niganda sana, nikamwambia nipo safarini (of course na mwenyewe alikuwa anajua hili) na nimewacha mtu kwenye biashara yangu. Fedha isingeweza kutolewa bila ya mimi kuwepo kuweka sahihi (kitu ambacho kilikuwa kweli pia).

    Akatulia…

    Sasa ngoja nifupishe stori. Mwaka mmoja baadaye nilikuja kupata taarifa kuwa kumbe kipindi kile anakopa kwangu, alikuwa akikopa kwa wengine pia.

    Kuna ambao tulikuwa wagumu na hatukutoa fedha zetu na wengine walimpa. Kitu ambacho siyo kibaya…

    Ila sasa huyu jamaa hakuwarudishia fedha zao….kitu ambacho ni kibaya.

    Sasa ninachotaka niseme leo ni nini?

    Kwanza, nataka niseme kwamba uaminifu ni mtaji. Ukiaminiwa aminika.

    Pili, nataka niseme kwamba, upende hela zako. Hakuna mtu mwingine anayeweza kupenda fedha zako kama wewe. Hakuna.

    Tatu, usipende kukopa kama hauedeshi microfinance ya kukopesha. Si unajua kukopa harusi….au umesahau..

    Nne, jiongezee kipato chako katika namna ambayo hutahitaji kukopa tena maishani mwako.

    Ni hayo tu.

    Mpaka wakati mwingine
    Mimi ni Godius Rweyongeza

    Hakikisha umejiunga na mfumo wetu wa kupata mafunzo zaidi kwa kujaza taarifa zako hapa chini.👇🏿👇🏿

  • Anza wewe kubadilika.

    Unazikumbuka kampeni za mwaka 2015!!! Unazikumbuka? Ni miongoni mwa kampeni zilizokuwa motomoto. Kila mgombea alikuwa na hoja zake kubwa ambazo alikuwa akitoa kwa wapiga kura ili waweze kumchagua.

    Kitu kikubwa kwenye kampeni hizi yakikuwa mabadiliko.

    Kila mgombea alikuwa akiongelea namna ambavyo ataleta mabadiliko endapo atapewa madaraka.
    Magufuri alikuwa anasema Tanzania ya viwanda.
    Lowassa alikuwa anasema Movement For Change.

    Wote walikuwa wanazungumzia mabadiliko Ila kwa namna tofauti.

    Na maelfu kwa maelefu walikuwa wanakuaanyika kuwasikiliza.

    Kila mtu alikuwa anapenda mabadiliko…..

    Kiufupi hakuna mtu asiyependa mabadiliko…

    Wote wanapenda mabadiliko. Au wewe hutaki?

    Lakini changamoto kubwa ni kwamba unataka mabadiliko pasipo kutaka kubadilika wewe.

    Wewe mwenyewe ndiwe unapaswa kuwa chachu ya mabadiliko kabla ya mtu mwingine yeyote yule.

    Kama kuna mabadiliko unataka, Anza wewe kubadilika.

    Ukisubiri mabadiliko yatokee juu, halafu wewe uyapokee, utasubiri sana.

    Kama unataka mabadiliko ya kiuchumi, Anza kubadili uchumi wako kwanza.

    Napenda Sana usemi wa Martin Luther King Jr. Anasema kila mtu akifangia mbele ya nyumba yake, dunia yote itakuwa Safi.

    Au kwa lugha rahisi sana kwamba kila mtu akifanikisha majukumu yake, mambo mengine yote yataenda sawa.

    Kuna hii nukuu ambayo niliwahi kuambiwa kuwa ni ya mwalimu Nyerere. Inasema kwamba play your part.

    Yaani, timiza wajibu wako. Ukitimiza wajibu wako na mwenzako akatimiza wajibu wake, Basi hakuna kitakachokwama.

    Sijui naeleweka….

    Kama umenielewa jiunge na mfumo wetu wa kupokea mafunzo zaidi, ili niendelee kukuelewesha zaidi kila siku kwa baruapepe. Jaza taarifa zako hapa chini👇🏿👇🏿

  • Kitabu Ambacho Utatamani Kuwa Ungekuwa Umekisoma Miaka Mitano Iliyopita

    Kuna mwaka nilikutanana mzee mmoja ambaye alikuwa anatamaani sana kuwekeza kwenye kilimo cha miti ila hakuweza.

    Kilichomkwamisha ilikuwa ni kukosa mwongozo sahihi.

    Labda niseme kwamba watu wengi wamekwama maishani mwao kwa kukosa mwongozo.

    Leo hii nataka nikupe kitabu kimoja tu ambacho wewe mwenyewe utashangaa kwa nini hukukipata miaka mitano iyopita

    Kipate hapa Ni bure, halafu kinapatikana kwa lugha adhimu ya Kiswahili

    Hiki hapa

  • Ilikuwaje Mpaka Nikaandika Vitabu 10 Na zaidi

    Ilikuwaje?

    Kwa wasionijua, basi wanafikiri kwamba Godius Rweyongeza ni jitu fulani hivi la miraba minne. Lenye miaka zaidi 60+ na mabusara kama yote…

    Hahaha!

    Miaka sina mingi kiviiile, labda mabusara nadhani nitakuwa nayo. Ila mama yangu alinifundisha nisiwe najisifia…

    Binafsi nilikuwa na ndoto ya kuandika kwa siku nyingi sana, tangu nasoma. Nakumbuka nikiwa kidato cha tatu au cha nne, niliongea na mama yangu nikamwambia kwamba nikihitimu kidato cha nne nitaandika riwaya (novel).

    Baada ya kuhitimu kidato cha nne nilirudi nyumbani na kukaa miezi kama nane hivi, ila sikuwahi kuandika ile novel ya ndoto zangu…

    Mama yangu alikuwa ananiuliza mara kwa mara, wewe si ulisema kwamba utaandika novel baada ya kuhitimu kidato cha nne… Nikawa namwambia ndio ila nitaandika..

    Siku zikazidi kusogea… mara likizo yangu ikaisha na nikatakiwa kuanza kidato cha tano..

    Hiyo nazungumzia ilikuwa ni mwaka 2013 /2014….

    Kama umezaliwa miaka ya 1960… 2014 siyo mbali hata kidogo.. maana una mastori ya kuanzia uhuru mpaka leo..

    Ila kama umezaliwa 2000, basi 2014 utaona ni mbali kiviile. Na hata ukipiga stori za kitambo unapiga za 2014 au 2015 wakati wazee wanajua mpaka ya vita vya Kagera… Wewe vita vya Kagera unavisoma tu vitabuni….

    Basi wacha niendelee…

    Baada ya kuingia kidato cha tano, nilisahau kidogo kuhusu ndoto yangu mpaka baada ya kuhitimu kidato cha sita.

    Sitaki nikuchose,

    Baada ya kuingia chuo, niliweka lengo kuwa mpaka nahitimu chuo napaswa kuwa nimeandika vitabu 11.

    Nakumbuka nilimshirikisha rafiki yangu mmoja hilo akakuna kichwa, akaniambia ungeweza kuandika hivyo vitabu,ila siyo kwa maisha ya chuo na hasa Chuo cha SUA.

    Nikamwambia hicho wacha nikifanyie kazi, nikifeli, nifeli nikiwa kazini..

    Nikifupisha stori zaidi ni kwamba, mpaka nahitimu chuo nilikuwa nimeandika vitabu 8. Sikuweza kuandika vitabu 11, ila walau nilikuwa nimeweza kuandika vitabu 8…

    Kitu gani kilinisaidia kuweza kuandika hivyo vitabu, na kuandika vitabu zaidi baada ya maisha ya chuo..

    Kitu kimoja kikubwa ni kwamba nilikuwa na lengo ambalo nilikuwa nalifanyia kazi.

    Usipokuwa na lengo au malengo ambayo unayafanyia kazi maishani mwako, ujue kabisa kwamba unaenda kukwama. Kikwazo kidogo tu, kitakukwamisha wewe na kukurudisha nyuma.

    Malengo yatakuonesha wapi uwekeze nguvu zako na vitu gani unapaswa kuachana navyo ili uweze kufika mbali.. ni uhakika kuwa mpaka sasa hivi utakuwa umeshaweka malengo ya kufanyia kazi maishani mwako.

    Kama mpaka leo hii hauna malengo, maana yake unaishi tu. Yaani, kunakucha na kuchwa huku wewe ukiwa unazunguka bila mwelekeo.

    Acha kila kitu unahofanya sasa hivi uweke malengo.

    Lakini pia hakikisha kwamba umesoma kitabu cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni. Hiki kitabu kina mwongozo mzuri wa kukusaidia wewe kufikia malengo yako. Sura ya pili nzima ya kitabu hiki imeingia kiudani kueleza malengo na jinsi ambavyo yanafanya kazi. Kisome kitabu hiki, kitakusaidia sana.

    Kinapatikana kwa 20,000/- nakala ngumu. softcopt utaipata kwa 10,000.

    Wasiliana nami sasa kwa 0755848391 ili nikutumie kitabu.

    Umekuwa nami rafiki  yako wa ukweli

    Tuwasiliane kwa 0755848391

    Ji

X