Category: A NOTE FROM SONGAMBELE

  • MAAJABU YA KUAMKA ASUBUHI NA MAPEMA

    Benjamin Franklin ambaye anafahamika kama mwananchi wa kwanza Marekani alikwahi kuandika kwamba kulala mapema na kuamka asubuhi na mapema kunamfanya mtu awe na afya njema, tajiri na mwenye busara. Haya maneno aliyaandika zaidi ya miaka 200 iliyopita kwenye moja ya barua aliyokuwa anaandika kwa mwanae. Pengine Franklin angekuwa anarudi leo hii angeshangaa kwa jinsi maneno…

  • Kama unafikiri elimu Ni ghali, jaribu ujinga

    Siku Kama mbili zilizopita hivi, nilikuwa naongea na mama mmoja ambaye anamiliki salooon kubwa mkoani Mwanza. Katika kuongea aliniambia kitu ambacho nilikidaka vizuri. Alisema, Mimi nimetumia gharama kubwa kujifunza mambo ya saloon. Gharama ambayo nimewekeza Ni kubwa sana. Hiki kitu kilikumbusha Ile stori ya kwamba Kama unafikiri elimu Ni ghali jaribu ujinga. Na kitu ambacho…

  • Kiwango Cha Elimu Unachopaswa Kuwa nacho ili uandike kitabu

    Leo nimepokea ujumbe wa MTU anateniuliza, kiwango gani Cha Elimu unapaswa kuwa nacho ili uandike kitabu? Swali hili limenivutia sana kiasi kwamba nimeona niandike Makala na kuileta kwako. Kwenye ulimwengu wa uandishi kuna waandishi wa kila aina. Kuna waandishi wenye PHD,Kuna waandishi wenye shahada mojaKuna waandishi ambao wameishia darasa la saba n.k. Kwa hiyo, hakuna…

  • Tuna saa 24 tu kwa siku

    Kila siku tuna saa 24 tu. Hakuna siku ambayo utakuwa na saa zaidi ya hizo, hivyo, unatakiwa kuutumia vizuri muda wako. Watu waliofanya makubwa, na watu wanaofanya vitu vya kawaida wote Wana saa 24. Sasa kwa Nini wewe usitumie muda wako vizuri?

  • Baadaye Siku Ya Leo Nitasikika Kwenye Temino Ya Clouds Fm

    Hello upande wa huko Nimeshaamka mapema siku ya leo kama ilivyo kawaida yangu. Na kama kawaida hapa nipo nyuma ya PC yangu nikiwa naandika kitu. Leo sina kitu kikubwa sana cha kukwambia labda taarifa fupi tu kuwa Baadaye siku ya leo Nitakuwa kwenye Temino ya Clouds Fm, kipindi kinachoendeshwa na Harris Kapiga, tukipiga stori kuanzia…

  • Ajionavyo Mtu Ndivyo Alivyo

    Miongoni mwa usemi maarufu sana Ni ule usemi wa Napoleon Hill ambapo anasema chochote ambacho akili yako inaweza kushikilia na kuamini, kinaweza kufikika. Ndio maana unashauriwa kujenga picha ya kile unachotaka kufikia. Ikikaa kichwani mwako kwa muda mrefu, huku ukiwa unaifanyia kazi. Ujue kwamba itafikia hatua utaifikia Sasa wewe picha yako kubwa unayoiona ni ipi?

  • Vitu Vitano Vya Kukusaidia Kuendelea Kuwasha Moto Wa Kufanikisha Malengo Yako.

    Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka huu niliandika makala ambapo ndani yake nilikuwa nikikukuuliza kuwa Lengo Lako Kuu La Mwaka 2022 Ni Lipi? Au Ndio Unamwachia Mungu🤔? Lengo lilikuwa ni kukufungua na kukuonesha kuwa mwaka huu mpya umeuanzaje au ndio kwanza unazubaa zubaa. Baadaye tarehe 19 Januari nilikukumbusha kwa kukwambia kuwa hiyo ndio tarehe ambayo watu wengi…

  • Kitu kinachowakwamisha wengi ukiwemo wewe

    Wengi wanakwama kwenye maisha, siyo kwa sababu nyingine bali kwa sababu tu ya UJUAJI. Yaani, wanajua, na hata hii makala wataipitia juu juu kwa sababu tu wanajua. Umewahi kuona watu wa aina hiyo ee. Ukianza kuongea naye jambo anakwambia na hilo nalijua. Mkianza kuongelea mada fulani, anajijua. Yaani, anajua kila kitu,  Kwenye mahusiano, yeye ndiye…

  • Mbinu za kutimiza malengo yako

    Habari ya leo rafiki yangu. Moja ya mada ambayo nimeiandikia sana kuliko mada nyingine, Ni mada ya malengo.Kuanzia namna ya kuweka malengoNamna ya kuyafanyia kazi malengo yakoNamna ya kuyafanikisha na Mambo mengine yanayouhusiana na malengo Nimeandika makala nyingi zinazohusiana na hii mada. Leo hii kuna mtu kaniuliza mbinuza kutimiza malengo yake. Nimeona nimrudishe nyuma kwenye…

  • Njia Rasmi Ya Mkato Itakayokupa Mafanikio Makubwa

    Chagua kitu kimoja, Kisha hakikisha kwamba unakijua kitu hicho nje ndani Kama ni biashara basi amua kuijua nje ndani.Kama ni kipaji chako basi zama na ubobee kwelikweli. Kama ni njia ya mkato, basi hii ndio njia pekee ya mkato unavyoweza kutumia kufikia kule unapotaka. Ukiwa mtu wa kugusa vitu kwa juu juu. Hutakaa ubobee na…

  • Uwezo mkubwa ulio ndani yako

    Leo nimeikumbuka sana siku nilipoenda kumtembelea rafiki  yangu. Kama ulivyo utaratibu wetu waafrika. Alinikaribisha kwa kuleta vinywaji pale mezani. Lilikuwa Jambo la furaha sana kukutana na hiyo rafiki yangu na stori zilianza bila kuchelewa, huku tukikumbushana baadhi ya mambo yaliyowahi kutokea siku za nyuma na hata kutaniana. Wakati stori zinazidi kukolea, glasi mojawapo pale mezani…

  • UAMINIFU NI MTAJI

    Mwaka 2018, nilisafiri kwenda Arusha na baadaye nikaenda Bukoba kwa wazee kusalimia. Ilikuwa ni safari ya zaidi ya mwezi… Nikiwa Arusha kuna jamaa alinitafuta. Alikuwa mshikaji ninayemfahamu. Au basi niseme tulikuwa tunasoma wote pale SUA. Aliniambia anataka nimkope fedha kama laki tano hivi, na angenirudishia hiyo fedha ndani ya wiki…Kuna fedha alikuwa anaisikilizia…. Nilimwambia wiki…

  • Anza wewe kubadilika.

    Unazikumbuka kampeni za mwaka 2015!!! Unazikumbuka? Ni miongoni mwa kampeni zilizokuwa motomoto. Kila mgombea alikuwa na hoja zake kubwa ambazo alikuwa akitoa kwa wapiga kura ili waweze kumchagua. Kitu kikubwa kwenye kampeni hizi yakikuwa mabadiliko. Kila mgombea alikuwa akiongelea namna ambavyo ataleta mabadiliko endapo atapewa madaraka.Magufuri alikuwa anasema Tanzania ya viwanda.Lowassa alikuwa anasema Movement For…

  • Kitabu Ambacho Utatamani Kuwa Ungekuwa Umekisoma Miaka Mitano Iliyopita

    Kuna mwaka nilikutanana mzee mmoja ambaye alikuwa anatamaani sana kuwekeza kwenye kilimo cha miti ila hakuweza. Kilichomkwamisha ilikuwa ni kukosa mwongozo sahihi. Labda niseme kwamba watu wengi wamekwama maishani mwao kwa kukosa mwongozo. Leo hii nataka nikupe kitabu kimoja tu ambacho wewe mwenyewe utashangaa kwa nini hukukipata miaka mitano iyopita Kipate hapa Ni bure, halafu…

  • Ilikuwaje Mpaka Nikaandika Vitabu 10 Na zaidi

    Ilikuwaje? Kwa wasionijua, basi wanafikiri kwamba Godius Rweyongeza ni jitu fulani hivi la miraba minne. Lenye miaka zaidi 60+ na mabusara kama yote… Hahaha! Miaka sina mingi kiviiile, labda mabusara nadhani nitakuwa nayo. Ila mama yangu alinifundisha nisiwe najisifia… Binafsi nilikuwa na ndoto ya kuandika kwa siku nyingi sana, tangu nasoma. Nakumbuka nikiwa kidato cha…

  • NGUVU YA KUWEKA MALENGO

    Umewahi kujiuliza malengo yanaweza kuwa na nguvu gani kwenye maisha yako. Kama ulikuwa hujui ni kwamba malengo ni kama petroli kwenye moto. unajua ukiweka moto kwenye petroli ni kitu gani ambacho kinaenda kutokea…Moto utawaka zaidi, si ndio… malengo na yenyewe yako hivyohivyo. Ukiweka malengo, yatakusukuma kufanya makubwa zaidi karibu sana ujipatie ebook ya kipekee ya…

  • Mipango yangu ya miaka 100 ijayo

    Nilipokuwa mdogo, nilikuwa napenda sana kusikiliza redio. Kila siku SAA kumi na mbili asubuhi ilikuwa lazima  nisikilize DW habari za ulimwengu. Mchana na jioni ilikuwa hivyo hivyo, yaani, ilikuwa kama dozi . Siku moja wakati nasikiliza habari, walitangaza kwamba kufikia mwaka 2050 kuna viumbe watakuwa wamepotea na kutoweka kwenye uso wa dunia. Watu niliokuwa nao walianza…

  • Email List Ni Nini?

    Jana niliandika hapa JINSI YA KUANZISHA BLOG. Kuna watu tayari wamesoma hiyo Makala na kuifanyia kaI. Sasa leo nilikuwa nikiwaambia wafungue email list kupitia MailChimp.com Ila swali lilikuwa email list nini? Kujibu Hilo swali naomba usome hapa chini Email list ni mfumo wa kukusanya mawasiliano ya watu wanaofuatilia kazi zako. Ambapo kila anayesoma na kupenda…

  • Jinsi Nilivyoandika Kitabu Kilichosomwa Sana Kuliko Vitabu Vyote Tanzania

    Nakumbuka mwaka 2019 kulikuwa na kijitabu kidogo hivi kilikuwa kinazunguka mtandaoni. Kijitabu hiki kilikuwa kinajulikana kama Baharia. Kilikuwa kinazungumzia mambo kadha wa kadha ambayo baharia anafanya. Kijitabu hiki kilizunguka sana, sana. Binafsi sikukisoma, Ila watu wengi ninaowafahamu mimi walikisoma hicho kijitabu. Kwa hiyo mada yao kubwa kwenye mazungumzo ikawa imekuwa BAHARIA. Yaani, ulikuwa huwezi kupitisha…

  • JINSI YA KUANZISHA BLOG

    Habari ya leo rafiki yangu. Siku ya leo ningependa kukuelezea ni kwa namna gani unaweza kufungua blog. Kwanza labda nianze kwa kusema kwamba ulimwengu wa sasa hivi umebadilika. Kwenye ulimwengu wa leo mtu anapokuwa na wazo, au dukuduku sehemu ya kwanza kabisa anapokimbilia ni mtandaoni kutafuta kitu hicho. Hiki kitu kimejenga utagemezi kwa watu, maana…

X