Category: A NOTE FROM SONGAMBELE

 • Je, Kuna Haja Ya Kuendelea Kusoma Wakati Ajira Hakuna?

  Jana kupitia Temino ya Clouds FM niliongea na wanachuo wote hapa nchini, huku nikiwasisitiza juu ya umuhimu wa kutumia bumu lao la chuo vizuri maana kuna maisha baada ya chuo. Waendeshaji wa kipindi hicho ambao ni Harris Kapiga pamoja na Advovate Henry Mwinuka nao walisisitiza pointi muhimu sana kwa kusema kwamba kila mwaka kuna wahitimu…

 • Utafanyeje Unapokuwa Na Wazo La Kufanya Biashara Ila Huna Mtaji

  Rafiki yangu, leo nataka niongee na wewe na kwa namna ya kipekee sana. Najua kwamba kuna vijana wengi huko mitaani ambao wana ndoto za kufanya makubwa. Vijana ambao wana ndoto za kuanzisha biashara ila tatizo au kisingizio wanasema,ni kwamba hawana mtaji. Je, ni kweli kwamba tatizo lako ni mtaji. Je, ni kweli kwamba hauna mtaji…

 • Mwongozo kwa wapambanaji (Hustlers Guide)

  Leo nataka nitoe mwongozo maalumu kwa mtu yeyote ambaye anapambmana kufikia mafanikio makubwa sana. Kama unapambana kufikia mafanikio makubwa hakikisha kwamba 1. una malengo na unayafanyia kazi kila siku bila ya kuchoka 2. unajihusisha na watu sahihi, watu chanya na watu ambao wanaendana na wewe. Watu hasi watakuangusha 3. unaangalia namna ya kubadili ndoto yako…

 • Jinsi Ya Kubadili Mwelekeo Wa Kile Umachofanya Bila Kuathiri Matokeo (True Story)

  Leo nimeikumbuka stori ya Sixto Rodriguez. Huyu ni mwanamziki wa kimarekani ambaye mwaka 1967 alirekodi wimbo wake wa kwanza. Na miaka mitatu baadaye ilikuja kurekodi albamu ambayo ilikuwa inajulikana kwa jina la cold fact. Mwaka mmoja baadaye alirekodi albamu nyingine ambayo ilikuwa ikijulikana kama coming from reality. Hata hivyo, hizi albamu zake hazikufanya vizuri sana…

 • Usiishie tu kukaa kwenye kochi na huku ukisema, ONE DAY YES!

  Kwa jinsi hii hata kama una ndoto kubwa hazitaweza kutimia. Kitu kikubwa ni wewe kuchukua hatua ili uweze kufikia malengo na ndoto zako. Hakuna ndoto kubwa inatimia ukiwa umekaa kwenye kochi. Huwa napenda kusema hata watu ambao wanapata lift siyo wale waliokaa nyumbani wakiisubiri, bali wale wanaokupa barabarani wanaendelea na safari. Wakati unasema, ONE DAY…

 • Jinsi Teknolojia Kidogo Inavyoweza Kuleta Mabadiliko Makubwa Kwenye Biashara

  Siyo kwamba mara zote utahitaji kuwa wa kwanza kufanya kitu fulani ili ufanikiwe. Ukweli ni kwamba muda mwingine utahitaji ubunifu kidogo. Au utahitaji kuweka teknolojia kidogo tu na kubadili kila kitu. Mfano Amazon, ujue wazo lao la kuuza vitabu halikuwaa jipya au hata bidhaa nyingine walizokuja kuuza baadaye.Watu walikuwa wananua na kuuza vitabu kabla yao.…

 • Hii Ndio Gharama Halisi Ya Kufanikiwa. Upo tayari Kuilipa?

  Unaweza ukawa unajilinganisha na watu wengine na pengine kuona kama unachelewa  kufanikiwa ukilinganisha na wengine. Ila sasa usichokijua ni nguvu na juhudi lakini pia miaka ambayo hao watu wamekuwa wakifanya kitu ambacho wanafanya. Unawajua imewachukua miaka mingapi kufikia walipofikia? Ebu kwa mfano tuseme wewe ni kijana amayependa utangazaji, na  Salim Kikeke ni mtu unayetamani mafanikio…

 • Maisha Ni Wajibu Wako

  Nataka, ifahamike kuwa maisha ni wajibu wako. Ukishinda au ukishindwa ni juu yako. Kama kila mtu akijenga utaratibu wa kuona maisha Kama wajibu wake tutafika mbali unajua kwa nini? Kwa sababu, ukianza kuona maisha kama wajibu wako utapambana kwa hali na mali kuweka kila Kitu sawa. Hutakuwa tena na muda wa kumlalamikia mtu KUWA Kitu…

 • Mimi Nakuamini Sana

  Kama kuna mtu namwamini Basi, Ni wewe…Naamimi haukati tamaaNaamimi hauko tayari kurudi nyuma hata ukikutana na kikwazoNa hicho kitu ukiendeleze kila siku.Usikate tamaa na wala usirudi nyuma.Endelea kupambana. Kikubwa ujue malengo yako.Uyafanyie kazi kila siku hata kama ni kwa udogo Unaweza usione matokeo kwa muda mfupi, Ila Hilo kisikukatishe tamaa. Maana yajayo yanafurahisha. Ni MimiGodius…

 • USHAURI: Jinsi Ya Kutunza Fedha Itakayokusaidia Kuanzisha Biashara

  Moja ya eneo muhimu sana kwenye maisha ya kila siku Ni fedha. Upende usipende fedha ni muhimu tena sana. Maana hakuna hata siku inapita bila ya wewe kutumia fedha. Ukiamka tu asubuhi, ujue kitanda ulichokuwa umelalia ni FEDHA.Ukivaa nguo zako, ujue umevaa fedha.Ukipata kifungua kunywa, ujue hizo ni fedha pia.Ukipanda daladala, hiyo nayo ni nini….…

 • MAISHA NI KAMA KUENDESHA BAISKELI..

  Leo nimeukumbuka usemi wa Albert Einstein. Anasema maisha Ni Kama kuendesha baiskeli, ili usianguke unapaswa kuendelea kunyonga. Ukiacha tu, unaanguka Hivi ndivyo ilivyo hata kwenye maisha ya kutafuta… Ili uendelee kusongambele haupaswi kuacha kuweka juhudi, haupaswi kuacha kupiga kazi kwa bidii, kujituma, kufanyia kazi malengo yako kila siku. Hivi ndivyo maisha yalivyo. Ukikata tamaa, Basi…hutoboi..…

 • Jinsi Mafanikio Makubwa Yanavyojengwa

  Picha hapo chini ni picha ya jengo la Taj Mahal. Jengo hili lipo kwenye Maajabu Saba ya dunia.Hili jengo lilichukua miaka 22 kujengwa Mpaka kukamilika. Hiki kitu kikupe picha ya kuwa vitu vizuri kwenye maisha huwa haviji kirahisj. Najua unapenda sana kupata vitu vizuri, lakini vitu vizuri huwa haviji kirahisi. Ni mchakato. Ndio maana wahenga…

 • Ufanyeje unapokuwa unasoma vitabu huku unasahau?

  Unaendeleaje rafiki yangu, juzi kuna mtu aliniambia kwamba anapenda kusoma vitabu, ila sasa tatizo lake ni kwamba akisoma anasahau alichosoma kwenye kitabu na hata kabla ya kumaliza kusoma kitabu husika. Kitu hiki ndicho kimeniweka hewani siku ya leo nili niweze kukiandikia maana najua kuna watu wengi pia ambao wanapata shida hii. Kwanza ninachopenda kusema ni…

 • JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA MTANDAONI-2

  Umewahi kujiuliza ni kwa namna gani unaweza kutengeneza kipato kwa njia mtandao wa intaneti? Umewahi kujiuliza kitu kama hiki? Hiki kitu ndicho kilinifanya mimi niweze kuingia mtandaoni, na hiki kitu ndicho kimenifanya niweze kuendelea kuutumia mtandao huu wa intaneti mpaka leo hii. Niliwahi kuandika makala kama hii siku za Nyuma, hivyo hakikisha unaisoma hiyo makala…

 • MAAJABU YA KUAMKA ASUBUHI NA MAPEMA

  Benjamin Franklin ambaye anafahamika kama mwananchi wa kwanza Marekani alikwahi kuandika kwamba kulala mapema na kuamka asubuhi na mapema kunamfanya mtu awe na afya njema, tajiri na mwenye busara. Haya maneno aliyaandika zaidi ya miaka 200 iliyopita kwenye moja ya barua aliyokuwa anaandika kwa mwanae. Pengine Franklin angekuwa anarudi leo hii angeshangaa kwa jinsi maneno…

 • Kama unafikiri elimu Ni ghali, jaribu ujinga

  Siku Kama mbili zilizopita hivi, nilikuwa naongea na mama mmoja ambaye anamiliki salooon kubwa mkoani Mwanza. Katika kuongea aliniambia kitu ambacho nilikidaka vizuri. Alisema, Mimi nimetumia gharama kubwa kujifunza mambo ya saloon. Gharama ambayo nimewekeza Ni kubwa sana. Hiki kitu kilikumbusha Ile stori ya kwamba Kama unafikiri elimu Ni ghali jaribu ujinga. Na kitu ambacho…

 • Kiwango Cha Elimu Unachopaswa Kuwa nacho ili uandike kitabu

  Leo nimepokea ujumbe wa MTU anateniuliza, kiwango gani Cha Elimu unapaswa kuwa nacho ili uandike kitabu? Swali hili limenivutia sana kiasi kwamba nimeona niandike Makala na kuileta kwako. Kwenye ulimwengu wa uandishi kuna waandishi wa kila aina. Kuna waandishi wenye PHD,Kuna waandishi wenye shahada mojaKuna waandishi ambao wameishia darasa la saba n.k. Kwa hiyo, hakuna…

 • Tuna saa 24 tu kwa siku

  Kila siku tuna saa 24 tu. Hakuna siku ambayo utakuwa na saa zaidi ya hizo, hivyo, unatakiwa kuutumia vizuri muda wako. Watu waliofanya makubwa, na watu wanaofanya vitu vya kawaida wote Wana saa 24. Sasa kwa Nini wewe usitumie muda wako vizuri?

 • Baadaye Siku Ya Leo Nitasikika Kwenye Temino Ya Clouds Fm

  Hello upande wa huko Nimeshaamka mapema siku ya leo kama ilivyo kawaida yangu. Na kama kawaida hapa nipo nyuma ya PC yangu nikiwa naandika kitu. Leo sina kitu kikubwa sana cha kukwambia labda taarifa fupi tu kuwa Baadaye siku ya leo Nitakuwa kwenye Temino ya Clouds Fm, kipindi kinachoendeshwa na Harris Kapiga, tukipiga stori kuanzia…

 • Ajionavyo Mtu Ndivyo Alivyo

  Miongoni mwa usemi maarufu sana Ni ule usemi wa Napoleon Hill ambapo anasema chochote ambacho akili yako inaweza kushikilia na kuamini, kinaweza kufikika. Ndio maana unashauriwa kujenga picha ya kile unachotaka kufikia. Ikikaa kichwani mwako kwa muda mrefu, huku ukiwa unaifanyia kazi. Ujue kwamba itafikia hatua utaifikia Sasa wewe picha yako kubwa unayoiona ni ipi?

X