Home


  • Hili Ni Kundi Maalumu La Whatsapp Ambalo ulipaswa Kuwa Umejiunga Sasa Hivi

    Rafiki yangu hongera sana kwa siku hii ya kipeke sana. Siku ya leo napenda nikwambie juu ya kundi moja la whatsapp ambalo ulipaswa kuwa umejiunga mpaka sasa hivi. Kiukweli ulipaswa kuwa umejiunga na kundi hili hapa mwaka jana, ila kama hukukufanya hivyo, muda sahihi wa kufanya hivyo ni leo hiii.
    Kwanza hili  ni zaidi ya kundi la whtasapp. Ndani ya kundi hili hapa utakutana na masomo ya kila siku ambayo yanatolewa na masomo ya kipekee ambayo huwezi kuyapata sehemu nyingine. Masomo haya yamelenga kukuinua wewe na kukufanya utengeneze kesho bora kwa kuanzia hapo hapo ulipo.
    Ukiwa kwenye kundi  hili hapa utapata na kitabu kimoja cha Kiswahili ambacho huwa kinatolewa kila mwezi. Kitabu hiki huwezi kukipata sehemu nyingine.
    Kwenye kundi hili pia utakutanana na watu ambao wana mtazamo chanya na wenye kiu na kufikia mafanikio makubwa. Yaani ni watu ambao wanataka kupata mafanikio kama vile ambavyo wanataka kupumua.
    Utakutana na mijadala ya mara kwa mara na madarasa maalumu ambayo yanatolewa kila mwishoni mwa wiki.
    Lakini pia rafiki yangu ukiwa kwenye kundi  hili utakuwa na uwezo wa kuwa karibu na mimi Songambele karibu yako zaidi ya unavyoweza kuwa  nami. Hivyo ukiwa huku unaweza kuniuliza swali na nikakujibu
    Kama lilivyo kundi la tofauti. Hata kujiunga ni kwa namna ya tofauti ya kujiunga. Ili kujiuga na kundi hili hapa utapaswa kulipia ada ambayo ni sawa na  24 kwa mwaka mzima. Ambayo ni sawa na shilingi elfu mbili kwa mwezi mmoja.
    Je, unaweza kulipia kidogo aumpaka ikamilike. Ndio unaruhusiwa kulipa kidogo ila ada yako inapaswa kuanzia miezi mitano na zaidi. Yaani elfu 10 na kuendelea. Namba ya kulipia ni 0755848391 jina ni Godius Rweyongeza. Ukimaliza kulipia utanitumia ujumbe wa kunijulisha nikuunge kwenye kundi. Ujumbe huu utautuma kwa njia ya whatsapp. Na mimi nitakuunga bila kuchelewa ili uweze kujifunza mambo ya kipekee kutoka kwenye hili kundi.
    Karibu sana.
    Ni mimi anayejali mafanikio  yako
    GODIUS RWEYONGEZA.

  • Vitu Saba Vya Kujifunza Na Kuchukua Hatua Kutoka Kwenye Wimbo Wa Ben Paul Wa JIKUBALI

    Moja ya wimbo ambao huwa napenda kuusikiliza mara kwa mara ni wa mwanamziki Ben Paul unaoitwa JIKUBALI. Huwa napenda kuusikiliza mara kwa mara kwa sababu kuna mafunzo muhimu ambayo naona na wewe nikushirikishe baadhi ya hayo masomo siku ya leo.
    1. UNAWEZA
    Ben Paul anaanza kwa kusema kwamba,
    unaweza kuwa doctor,
    unaweza kuwa star,
     


    Ni ukweli usiopingika kwamba chochote kile ambacho utaamua kufikia maishani mwako, unaweza. Kila kitu kinaanza na maamuzi.
    kwa kutumia hicho kichwa chako. Kama utaiambia akili yako kwamba huwezi, jua kabisa kwamba hautaweza.Ila ukisema unaweza, utaweza tu.
    Napenda sana maneno yaliyoandikwa kwenye kitabu cha THINK AND GROW RICH sura ya tatu.
    mwandishi anasema.
    Kama unafikiria umepigwa, umepigwa
    Kama unafikiri umeshindwa, umeshindwa
    Kama unafikiri huwezi, huwezi
    Kama unataka kushinda lakini unafikiri huwezi, karbia huwezi.
    Kama unafikiri utapoteza, umepotea
    Kwa sababu katika dunia ushindi unaanza na msukumo wa ndani ya mtu,
    Hiyo inaitwa hali ya akili.(state of mind).
    Kama unafikiri umepitwa na wakati, umepitwa
    Inabidi ufikiri mbali
    Inabdi ujiamini mwenyewe kabla ya kushinda tuzo.
    Vita vya maisha hashindi mtu mweye nguvu au mwenye mbio za haraka
    Vita vya maisha anashinda mtu ANAYEFIKIRI ANAWEZA.
    kwa hiyo na mimi napenda kukwambia  kwba UNAWEZA.
    Sidhani kama mimi nina kitu cha zaidi cha kuongeza hapa tofauti na kusema tu kwamba, badili fikra zako sasa hivi na uanze kujiona kwamba unaweza. Kumbuka kwamba FIKRA ZAKO NDIZO HULETA HISIA UNAZOKUWA NAZONA HISIA NDIZO HUSABABISHA MATENDO AMBAYO UNACHUKUA, HUKU MATENDO YALILETA MATOKEO.

    Kwa hiyo ukitaka kubadili matokeo unayopata sasa hivi, basi anza kubadili hicho kitu ambacho unaweka kwenye akili yako sasa hivi. Anza kuona uwezekano. Ujue unapoiweka akili yako katika kutafuta uwezekano ujue kwamba lazima tu itatafuta muda wote kuhakikisha kwamba inatafuta suluhisho.
    2. KIPAJI CHAKO NDIO MTAJI WAKO WA KWANZA
    Ben Paul anaendelea kwenye wimbo wake kwa kusema kwamba;
    kipaji mali yako,
     


    Nadhani moja ya vitu ambavyo vimekuwa havipewi kipaumbele sana shuleni na hata nyumbani ni kipaji.  Lakini ukweli ni kwamba wewe unaweza kunoa kipaji chako kuamzia hapo hapo ulipo.
    kwenye kitabu changu cha  JINSI YA KUIBUA UBUNIFU ULIO NDANI YAKO nimeshauri kwa mtu yeyote kutenga dakika 30 tu kila siku kufanyia kazi kipaji chake.  ukiangalia kwa jicho la kipekee utaona kwamba dakika 30 kwa siku sio nyingi. Maana kwa siku moja tu una dakika 1440. Ukitoa dakika 30 unabaki na dakika 1440. Sasa unakwama kwa mfano unaweza kushindwa kupata dakika 30 kila siku za kufanyia kazi lengo lako?
    3. ELIMU NGAO YAKO, NGAO YAKO

    Ben Paul anaendelea kuimba kwa kusema ELIMU NGAO YAKO…
    Kama ulikuwa hujui, kamusi ya kiswahili sanifu inasema  NGAO NI KINGA. kwa hiyo ninaweza kusema kwamba elimu yako ndio kinga yako.
    Na hapa ninaposema elimu simaanishi tu elimu ya chuoni. Kuna aina nne za elimu
    ya kwanza ni ile ya kawaida ya nyumbani ambapo unafundishwa vitu vya hapa na pale.
    Ya pili ni ile ya shuleni ambayo unafundiswa kusoma na kuandika na kuhesabu. aina hii ya elimu inapimwa kwa kiwango ufaulu. Yaani A au B unazopata.
    Ya tatu ni elimu ya pesa (hii haifundishwi shuleni wala nyumbani) hii unajifunza kitaa. aina hii ya elimu haipimwi kwa kiwango cha elimu ulichonacho.  Na wala haipimwi kwa A au B ulizopata  Aina hii ya elimu inapimwa kwa pesa unazoingiza au pesa unazopoteza.
    kwa leo sitaingia ndani zaidi kuhusu aina hizi za elimu, nataka tu uzijue.  Na kamwe usije ukasema kwamba mimi siwezi kufanikiwa maishani kwa sababu tu sina elimu ya shule au chuoni. Wakati hiyo  ni mojawapo kati ya hizo elimu nyingine ambazo unaweza kuwa nazo.
    Aina ya nne ni elimu, ni elimu ya maendeleo binafsi. Wakati huleni unafundishwa kusoma na kuandika pamoja na kuhesabu, lakini maisha yanahitaji uandike, usome na kuhesabu. Na hapa ndipo elimu hii inaingilia katikati.
    Wakati mwalimu anakufundisha kusoma, lakini mwalimu huyohuyo anapokuja kwenye maisha ya kawaida hakuchagulii kitabu cha kusoma.
    Elimu hii ya maendeleo binafsi ndio itakuwezesha wewe kutumia vipaji vyako na uwezo wako ulionao.
    inawezekana wewe una kitabu hapo ambacho ningekuwa nasoma sasa hivi ila hujakiandika kwa sababu hupati elimu hii.
    Inawezekana wewe una wimbo wa kuniburudisha ila hujafanya hivyo kwa sababu hujiendelezi.
    inawezekana wewe una ujuzi mkubwa wa uongozi ila kwa sababu hupati elimu hii basi uongozi wako ndio hivyo hata hauutumii. Kiukweli kama utakufa na vitu hvivi, ujue kwamba utakuwa umefanya kosa kubwa.
    Naweza kuandika zaidi hapa. ila kwa leo napenda ukasoma makala yenye kichwa cha Kinachokukwaisha Ni Uoga HAPA
    Napenda kumalizia kipengele hiki cha Elimu kwa kusema kwamba mjinga wa karne ya 21 sio yule ambaye hajui kusoma na kuandika, bali mjinga wa karne ya 21 ni yule anayejua kusoma na kuandika ila hasomi. kiufupi kama unajua kusoma ila hujiendelezi kwa kusoma vitabu mbalimbali basi hauna tofauti kabisa na ambaye hajaenda shule.
    kumbuka elimu ni ngao yako. Na elimu itakuwa ngao yako kama kile unachojifunza utakiweka katika matendo.

    Wasomi wengi wana elimu nzuri na kubwa lakini hawaitumii kama ngao. Wao wenyewe haiwasaidii chochote. Ndio maana wengi wanakimbilia kuajiriwa.  Ila ukiwa na elimu ya kujiendeleza binafsi, basi watu watakutafuta tu kwa sababu utakuwa mtu wa viwango vingine.
    Angalia video hii hapa inayozungumzia Maeneo mawili ya kupata shahada mtandaoni bure kabisa HAPA
    4. USIISHIE NJIANI
    Tuendelee na wimbo wa Ben Paul. Hapa tunaaenda moja kwa moja mpaka kwenye mstari ambao anaimba hivi: “usiache jambo kati kwenye maisha yako
     


    Hapa ndipo vijana wengi wa Tanzania wanakwama. Kuna vijana wengi wa kitanzania wana mawazo mengi mazuri ya kujenga kweli kweli. Lakini tatizo lao ni kuishia njiani. Wanagusa gusa tu.  au kwa msemo maarufu ambao unatumika kwamba wanajaribu. Yaani unakuta mtu ana kipaji kizuri cha kuimba, ukiwambia kwamba aiseeh unaweza kuimba. Utasikia anakwambia kwamba najaribu jaribu tu.
    Watu wengi ambao huwa wanajaribu jaribu ndio watu ambao huwa wanaishia njiani. Kwa sababu huwa wanaanza kufanya kitu mguu mmoja ukiwa ndani na mwingine ukiwa nje. Yaani wanakuwa wanajua kama wataanza kufanya kitu hiki na kikawa hakijafanikiwa basi watarudi huko huko walipokuwa nyuma.
    Vijana wa kitanzania mnahitaji kujitoa. Au kiufupi naweza kusema kwamba KUCHOMA MELI MOTO.  
    Kwa kumalizia kipengele hiki hapa, nipende tu kukwambia kwamba, ukianza kitu kimalize. Usiishie njiani. Kuishia njiani kunafanywa na watu ambao hawana mwelekeo kwenye maisha. Kama kweli unataka kufanya mambo ya kipekee hapa duniani basi hakikisha kwamba kila unachomua kuanya basi unakikamilisha mpaka mwisho hata kama vinatokea vikwazo. Ndio maana Ben Paul anasema kwamba vikwazo lazima nawe usirudi nyuma.
    5. WAKATI WAKO NI LEO
    Tuendelee na wimbo wa wimbo wa Ben Paul.
    Na hapa tumefika kwenye mstari ambapo Ben anasema kwamba,
    Mi nakuasa, its your time
    Huwezi kuwa chini, you’ve got something special.

     


    Ujue kuna watu ambao wana vitu vya kipekee ambao haawajahi kuambiwa kwamba wanaweza. Hawajawahi kuambiwa kwamba una kitu cha kipekee. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwenye mazingira tumezungukwa na watu wengi ambao hi hasi.
    Ukijitahidi kufanya kitu chochote kile wanakwambia kwamba huwezi kufanya hicho kitu. Ukijitahidi kusonga mbele kidogo basi unaambia kwamba hicho kitu hakiwezekani. Na maneno mengine mengi.
    Kuna siku nilikuwa nasoma hadithi ya A BOY WHO HARNESSED THE WIND. Kwenye kitabu hiki mwandishi ambaye ni Kamkwamba akawa anasema kwamba aliweza kutengeneza umeme nchini kwao ila hakuwahi kushangiliwa wala kupigiwa makofi na mtu yeyote, isipokuwa watu waliokuwa wanataka kumuua kwa sababu eti kwa kutengeneza mtambo wa umeme amezuia mvua. Lakini kijana huyo alikuja kushangiliwa kwa kishindo sana katika nchi ya ugeni.
    Na hiki ndicho kinatokea kwa vijana walio wengi na wanaoanza. Kuna watu wengi ambao wanakukatisha tamaa kwenye hicho unachofanya.
    Kwa nini watu wanakukatisha tamaa? Watu wanakukatisha tamaa kwa sababu wao walishakujengea mazingira ambayo wanaona kwamba unafaa na hivyo hupaswi kwenda zaidi ya hapo. Yaani ni kama vile watu walishakuweka kwenye kopo. Kwa hiyo sasa unapoanza kufanya vitu vya tofauti na vile watu walivyokuwa wanategemea basi kila mmoja ataanza kusema maneno yake, kila mmoja ataanza kuongea na wengiine wataona kama umekeunga.
    Sasa nipende kukwambia kwamba usikubali kuwekwa kwenye kopo.
    Wakati ndio leo
    Kutimiza malengo
    Nakusihi uanze sasa
    Jishughulishe utapata.
    Kama anavyosema Ben Paul

    6. USIWE MCHOYO
    Ukitaka kufanya mambo ya tofauti kwenye hii dunia haupaswi kuwa mchoyo hata kidogo. Leo hii najaribu kufikiria kama Steve Jobs anegkuwa mchoyo wa kutengeneza hizi simu janja za kupangusa inawezekana wewe na mimi tusingefahamiana na hata hiki unachokisoma sidhani kama kingekufikia haraka kiasi hiki. Ila aliachana na uchoyo na kutengeneza kitu kizuri.
    Ebu fikiria pia kama huyu anayemiliki kiwanda cha nguo unazovaa angeamua kuacha kutengeneza nguo, kwa sababu ya uchoyo, bila shaka lolote lile usingekuwa umevaa hizo nguo. Au kiufupi ungekuwa uchi.
    Sasa na wewe uache uchoyo. Badala yake ongonzwa na upendo. Na hapa Ben Paula anasema hivi
    Tanzania ni yako, penda watu wako.
    Kuwa mfano bora kwenye jamii yako.
    Ujue watu wanaopenda jamii ndio wanafanya vitu vya kuisaidia jamii. Ni kwa sababu ya upendo ndio maana unaona watu wanaanzisha biashara. Ni kwa sababu ya upendo ndio maana unaona watanzania wanawekeza (japo wengi hawajui hili somo la kuwekeza)
    Ni kwa sababu ndio maana Ben Paul mwenyewe aliimba wimbo huu na kutumia kipaji chake.
    Sasa wewe upendo wako  unatumia kufanya nini? ebu na basi na wewe amua kutumia walau kipaji chako.
    Ebu na wewe amua basi kutumia uwezo wako wa uongozi. ebu na wewe amua basi kutumia kuchora hiyo michoro ambayo unayo kwenye kichwa chako.
    Ebu basi geuza hicho kipaji cha kubishana juu ya mpira ukitumie kwa manufaa zaidi.
    Kiukweli una vitu vizuri ila kama hutasukumwa na upendo basi inawezekana hivyo vitu tusivione kwa sababu ya kukosa upendo. Nakusihi uongozwe na upendo ili uweze kutumia kile ulichonacho kufanya makkubwa zaidi.
    7. FANYA KAZI KWA BIDII, HAKUNA NJIA RAHISI YA KUFANIKIWA

    Ni kweli mpaka hapa nimezungumzia mengi kwenye makala hii hapa. ila siwezi kuacha kuzungumzia suala zima la kufanya kazi kwa bidii. Kuna watu wengi utakuta kwamba wanakwambia wanataka kazi ambayo wataingia ofisini tu na kusaini. Kisha kuondoka. Kweli! Kiukweli kama unataka kufanikiwa basi huna budi kuhakikisha kwamba unafanya kazi kwa bidii sana.
    Ndio maana Ben Paula anasema hivi,
     inawezekana if  you work hard in it.
    Sio kwa sababu nimesema utumia kipaji chako basi unafanya hivyo mara moja tu.
    Au sio kwa sababu nimesema ujifunze na kuongeza maarifa basi unafanya hivyo mara moja tu.
    Inawezekana if you work hard on it,
    Unahitaji kuchapa kazi haswa, siku zote nyuma ya ushindi huwa kuna kazi kubwa ambazo huwa zinawekwa kabla ya kupata matokeo makubwa .
    Kuna mengi sana ya kujifunza ila kwa leo naishia hapahapa.
    Mpaka wakati mwingine. KWA HERI ni mimi anayejali mafanikio yako
    Umekuwa nami,
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA
    Hakikisha umesubscribe kwenye YouTube Channel Yangu Ya Youtube Kwa Kubonyeza Hapa

  • SIku ya leo (valentine) napenda nimtambulishe kwako….. (sijawahi kufanya utambulisho mkubwa kama huu, ila leo imebidi tu nifanye hivyo)

    Kheri ya sikukuu ya wapendanao, rafiki yangu. Siku kama hii hujitokeza mara moja tu kwa mwaka, hivyo huna budi kuhakikishakwamba unafurahi na kuitumia kwako. Siku ya leo binafsi kuna mtu mmoja tu ambaye ningependa nimtambulishe kwako. na mtu huyu si mwingine bali ni wewe mwenyewe. Kwa nini ninafanya hivi? Ninafanya hivi kwa sababu katika dunia ya sasa unakuta kwamba inakuwa ni rahisi sana kufuatilia maisha ya watu wengine zaidi ya unavyofuatilia maisha yako. Hivyo unaweza kukuta kwamba unajua kiudani kwamba mtu fulani akifanya hiki, au akiepuka hiki lazima tu atafanikiwa maishani mwake. Lakini ukawa hujijui wewe mwenyewe. Yaani ukawa hujui ni kitu gani unapaswa kufanya au kuepuka ili uweze kuwa na maisha mazuri sana. Ndio maana siku ya leo nimeona waziwazi kwamba nikutambulishe wewe kwako wewe mweyewe.
    Kama kuna upendo unapaswa kuwa nao basi ni upendo wa kujijua wewe mwenyewe. Jua wapi unatoka na wapi unaelekea maishani mwako. Ni zawadi ya kipekee ya upendo ambayo unaweza kujipa maishani mwako.
    Kwa hiyo napenda kuanzia leo hii ujifuatilie wewe mwenyewe kuliko mtu mwingine. Najua wewe ulidhani nitambulisha mtu mwingine na ulitaka umjue. Lakini unaonaje ukijijua wewe kiundani kabla ya kumjua mtu mwingine.
    Ujue unaweza  kukuta kwamba kila siku kunafuatilia maisha ya watu ya watu wengiine. Ila ukashidwa kujifuatilia wewe mwenyewe. Hivi kwa mfano nikikuuliza jana ulitumia kiasi gani unakumbuka?
    Je, ulitumia muda gani mtandaoni? Je, ulitumia muda gani kusoma kitabu?
    Je, ulitumia muda kiasi gani kuongea kwenye simu?
    Uliingiza shilingi ngapi?
    Je, baada ya hayo yote ambayo yametokea jana upo tayari kufanya marekebisho ili kuhakikisha kwamba unakuwa mtu bora zaidi siku ya leo zaidi ya ulivyokuwa siku ya jana?
    Kama hujijui mwenyewe, sasa kwa nini uwekeze nguvu kwenye kuwajua watu wengine? Kwa hiyo kuanzia leo hakikisha kwamba unawekeza kwanza katika kujijua wewe mwenyewe zaidi ya unavyowafuatilai wengine na kuwajua watu wengine.
    Ukiweza kujijua wewe mwenyewe unaweaza kuboresha maisha yako kutokana na kile ambacho unaona kwamba haufanyi vizuri sana. Nakutakia kila lakheri.
    Unaweza kukuta kwamba mtu anamfahamu msanii fulani au mtu fulani maarufu zaidi ya anavyojifahamu yeye mweyewe. Sasa naomba kujua kama kweli wewe unajifahamu kweli au la!
    Kwa kusema hayo rafiki yangu, naomba kwa leo niishiei hapo

  • Habari njema kwako Rafiki yangu.

    Rafiki bila shaka uaendelea vyema kabisa.
    Binafsi jioni ya leo nimekuja kwako na habari njema sana. Habari hii ni kwamba unaweza kuwa wakala wa kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI mkoani kwako. Kwa hiyo popote pale ulipo (bara na visiwani) naomba uwasiliane na mimi ili tufanye utaratibu wa wewe kupata nakala za vitabu.

    Hii ni habari njema sana ambayo nimeona nikupe jioni ya leo. Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nami kwa simu 0755848391

    Karibu sana.

    Ni mimi anayejali mafanikio yako,
    Godius Rweyongeza
    0755848391

  • Uwekezaji Huu Utakufanya Kuwa Mtu Mkuu Kwenye Hii dunia

                       
    Rafiki yangu, hongera sana kwa siku hii ya kipekee sana. Siku hii ya leo napenda nikwambie uwekezaji ambao kama utaufanya na utakuja kukufanya mtu mkuu kwenye hii dunia. Kwanza kabla sijakwambia ni uwekezaji gani. Nataka nikwambie kwamba kuna watu ambao unaweza kuwa unawaona wanafanya vitu vikubwa, wewe ukawa unawaona kwamba wao wamezaliwa na Baraka za kipekee ambazo wewe hauna. Ukweli ni kwamba kila mtu kazaliwa na baraka zake.
    Ila linapokuja suala la kutumia baraka hizi hapa unakuwa na uhuru wa kuzitumia au kutozitumia. Ukiamua kuzitumia Baraka hizi za kuzaliwa nazo basi kuna kitu muhimu sana ambacho unapaswa kufanya. Kitu hiki ni kuwekeza katika wewe.  
    Kuwekeza katika wewe kutakufanya kuwa mtu  mkuu sana. Na watu ambao wamekuwa wanawekeza katika wao wamekuwa wanafikia mambo makubwa sana maishani. Ni kwa msingi huu huu Warren Buffet amewahi kumwambia kijana mmoja kwamba       ‘kama unataka kuwa bilionea unapaswa kusoma kurasa 500 za kitabu kila siku’. Hii ndio kusema kwamba alikuwa anamsisitiza kijana kuwekeza katika yeye.
    Je, wewe unawekeza katika wewe?  Hivi mara yako ya mwisho kuwekeza katika wewe ni mwaka gani? Sasa leo hii kuna kitabu kimoja ambacho utafanya uwekezaji mdogo kukipata ila kitabu hiki kitakuafanya uweze kuufikia ukuu wako. Kwa kusoma kitabu hiki hapa utakuwa umewekeza katika wewe. Na kitabu hiki sio kingine bali ni kitabu cha kutoka sifuri mpaka kileleni.
    Kwenye kurasa za kitabu hiki utakutana na mambo mengi sana ila kwa leo ningependa tu kusema kuhusu  malengo. Kwenye kurasa za kitabu utajifunza nje ndani kila kitu unachohitaji kujua kuhusu malengo. Kuanzia jinsi ya kuweka malengo, kuyafanyia kazi mpaka kuyafikia. Utapata kujua makosa ambayo watu wengi huwa wanafanya kwenye kuweka malengo na jinsi ya kuyaepuka. Hii ndio kusema kwamba mpaka kufikia mwisho wa kitabu hiki hapa utakuwa tayari umepangilia katika namna ambayo asilimia 99 ya watu hawafanyi hapa duniani.
    Kitabu hiki hapa ni 10,000 tu. lipia kupitia 0755848391 ili niweze kukutumia kitabu hiki popote pale ulipo Tanzania.

  • Ukiweka Juhudi Kubwa Sana Kuelekea Malengo Yako, Malengo Yako Pia Yataweka Juhudi Kubwa Kukuelekea Wewe

    Moja ya kanuni za fizikia ni hii kanuni inayosema kwamba, to every action there is equal and opposite reaction. Ikimaanisha kwa kila kitu ambacho unafanya kuna kuwa na nguvu ya aina hiyo hiyo ambao inakujwa kwako.
    Kwa hiyo ukifanya kazi kwa bidii kubwa ili uweze kupata matokeo makubwa, mwisho wa siku matokeo makubwa yataanza kuja kuelekea kwako na mtakutana katikati.
    Hii ndio kusema kwa malengo yako uliyonayo. Matokeo ya malengo ambayo unayapata kwenye maisha yanategemea na kiwango cha juhudi ambacho unaweka. Kama unaweka juhudi kubwa katika kuhakikisha kwamba unatimiza malengo yako. Malengo yako yenywe yatakuja kwako kwa kasi kubwa na mtakutana sehemu.
    Lakini kama unayakimbia malengo na unaogopa kuyafanyia kazi, basi badala yake malengo yako hayo yatakukukimbia na wewe na malengo hamtakuja kukutana kamwe. Kwa hiyo basi kuanzia siku hii ya leo, anza kuweka juhudi kuelekea malengo yako kila iitwayo leo. Hakikisha kwamba haulazi damu. Weka juhudi mara nyingi zaidi kiasi kwamba malengo nayo yaanze kukusogelea hapo ulipo. Nikutakie kila la kheri katika kile ambacho unafanya
    Ni mimi ninayejali mafanikio yako
    Godius Rweyongeza

  • Kama Sio Wewe Nani? Kama Sasa Lini? INAWEZEKANA

    Rafiki yangu hongera sana kwa nafasi ya siku hii ya kipekee sana. Siku ya leo napenda nikwambie kwamba inawezekana, ndio kama una lengo ambalo unataka kulifanyia kazi katika maisha yako unapaswa kufahamu  kwamba inawezekana kulifanikisha lengo hili hapa.
    Kama kuna ndoto ambayo unayo maishani mwako basi fahamu kwamba inawezekana. Watu unawaona sasa hivi wakiwa wamefanya makubwa kwenye hii dunia ni walikuwa ni watu wa kawaida kama wewe hapo. Sasa kuna kitu ambacho kiliwatofautisha watu hawa na kuwafanya watu hawa waweze  kusongambele na kufanya makubwa zaidi maishani.
    Kitu hiki ni kuwa na malengo. Walikuwa na malengo ambayo waliyafanyia kazi. Ukiwa na lengo ambalo unalifanyia na kazi na ukaweka nguvu na akili yako hapo, huwezi kushindwa kulifikia. Tatizo la watu walio wengi ni kwamba wanaweka malengo makubwa ila hawayafanyii kazi. Au hawaweki nguvu zao kwenye kufanyia kazi hayo malengo. Hakikisha kwamba unajiepusha na hicho kitu. Jitoe kuhakikisha kwamba unatimiza na kufanikisha lengo lako kwa namna yoyote ile. 
    Ujue  Brian Tracy amewahi kusema kwamba, ukiwa na malengo unayafanyia kazi na hayo malengo yanakuwa yanafanya kazi kuhakikisha kwamba yanakuelekea wewe hapo. Mwisho wa siku wewe  pamoja na malengo yako mnafikia hatua ambapo mnakutana.
    Sasa swali langu kwako, ni je una malengo gani mwezi huu? Je, una malaengo gani kwa mwaka huu 2020.
    Chukua hatua uweke malengo leo hii na uanze kuyafanyia kazi moja kwa moja bila kuchelewa. nakutakia kila la kheri.
    Godius Rweyongeza.

  • ACHANA NA TABIA HIYO

    Kuna tabia hiyo ambayo unifanya japo haikupeleki kwenye mafanikio, achana nayo.

    Anza kushugulika tabia ambazo zinakufanya wewe uweze kusongambele kwenye mafanikio makubwa.

    Kama unataka kufanikiwa na bado kuna tabia ambazo zinakuvuta ila hutaki kuziacha, utajiangusha.

    Yaani hapo ni sawa na wewe umekuwa baba/mama ila hutaki kuachaa na utoto. Hivyo ukitaka kufanikiwa achana na tabia zinazokukwamisha (utoto) ili ukumbatie tabia za mafanikio.

    Mafanikio ni haki yako ya kuzaliwa kama utakumbatia tabia za kimafanikio.

    Ni mimi anayejali mafanikio yako
    Godius Rweyongeza

  • Kinachokukwamisha Ni Uoga

    Ujue kuna watu ambao wewe unawazidi kwa kipaji cha kuimba ila wanazunguka dunia nzima wanaimba.

    Kuna watu  ambao wewe unawazidi kwa viwango vya kucheza mpira, ila leo hii watu wanakaa kwenye runinga kuwatazama dakika 90.

    Wengine wewe unawazidi viwango vya kuchekesha, ila leo hii watu wanaingia YouTube kuwatazama ili wacheke na wewe upo hapo umejificha.

    Kuna watu wana viwango vya kawaida sana vya uongozi, ila leo hii wanazunguka dunia kama viongozi na kushangiliwa. Na wewe mwenye viwango vikubwa vya uongozi upo hapo!

    Kuna watu hawajui kuchambua mpira kama wewe hapo! Ila leo hii wakichambua tu, hata kama wanasema vitu vya kawaida wanasikilizwa sana. Wewe mwenye uwezo mkubwa upo hapo!

    Kuna watu uwezo wa kuandika vitabu ni mdogo sana, ila leo hii vitabu vyao vinasomwa kila kona ya dunia.

    Yaani wewe kinachokukwamisha ni uoga. Kwenye kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI ukurasa wa 87 nimezungumzia vitu ambavyo vinazuia watu kufikia mafanikio yao.  Moja ya kikwazo hiki ni UOGA.

    Ebu fungua ukurasa huu hapa uone uoga unavyokukwamisha.

    Kama hauna kitabu tuwasiliane kwa namba 0755848391 ili wewe upate kitabu hiki uanze kutengeneza kesho bora sasa hivi.

    Gharama ya kitabu ni 10,00/- tu.
    na utakipata popote pale ulipo tanzania.

    pia nafasi za kuwa wakala wa kitabu hiki mkoani kwako ziko wazi. Niandikie ujumbe kwa 0755848391 ili nikupe utaratibu. Karibu sana

  • Ebu fanya kitu hiki hapa siku ya leo kuongeza mtadao wako

    Siku ya leo ningependa iwe siku yako kuongeza mtandao wako wa watu ambao unawafahamu. Na hapa tunaenda kutumia tu mbinu za kawaida ambazo wewe mwenyewe unaweza kuzitumia kukongeza idadi ya mtandao wako.
    Siku ya leo nataka umpgie mtu ambaye hujawahi kumpgia maishani mwako.
    Anaweza akawa mtu ambaye umekuwa unamfuatilia kwa kazi anazofanya kila siku. Au anaweza kuwa ni mtu ambaye umekuwa ukijifunza kwake kwa namna yoyote ile. Au anaweza kuwa mtu maarufu, anaweza kuwa ni mtu ambaye unaona kwamba huyu kuna siku anaweza kunisaidia kukutana na mtu mwingine au anaweza kunisaidia kufanikisha kitu fulani. Anaweza pia akawa mtu ambaye unajua ana tatizo ila suluhisho la tatizo hilo ni wewe hapo.
    Kwa vyovyote vile hakikisha unatafuta jina la mtu mmoja tu ambaye hujawahi kuwasiliana naye maishani  mwako.
    Sasa ukishakuwa na jina la huyu mtu anza kujiuliza unaendaje kupata namba ya huyu mtu. Je, utaipata kwa kutumia mzunguko ambao unao sasa hivi. Jiulize ni watu gani kati ya hawa ambao mimi nawafahamu sasa hivi wanaweza kuwa msaaada kwenye kuipata namba ya huyu mtu? Kama hakuna hata mmoja usihofu. Nenda mbele kwa kuitafuta google. Andika google jina la mtu huyo kisha tafuta namba yake.
    Kama haipatikani google basi ulizia hata kama unaweza kupata namba ya mtu wa karibu yake ili uanze kuwasiliana na huyo mtu.
    Bila shaka kwa njia hizi nina hakika hutakosa namba yake. Kama ulikuwa nayo ila hujawahi kuitumia basi leo ndio leo, asemaye kesho ni mwongo. Baada ya hapo weka vocha kisha piga. 
    KUMBUKA: Kama ni mara yako ya kwanza kabisa unawasiliana na mtu usianze kwa kumtumia ujumbe (hii ni kanuni yangu na ninaitumia sana) hasa mtu huyo anapokuwa mkubwa au anapokuwa ni mtu ambaye unapenda kujifunza kwake zaidi. Mimi kwenye hili huwa naendeshwa na falsafa ya kwamba,
    Kama ninaweza kuonana na  mtu ana kwa ana basi sipigi. Kama ninaweza kupiga siandiki ujumbe. Hii ndio kusema kwamba kwangu ujumbe mfupi huwa ni jambo la mwisho kabisa baada ya kuona njia zote zimeshidwa.
    Ukipiga hakikisha kwamba unazingatia yafuatayo;
    KWANZA,   Hakikisha kwamba kabla ya kupiga unamjua huyu mtu nje ndani. Jua anafanya nini, ili unapoanza kuongea naye unaongea naye vitu vinavyoeleweka. Kwa hiyo fanya utafiti wa kutosha kabla ya kupiga simu
    PILI, Mpongezea kwa kazi anayofanya. Au mshukuru kwa jinsi kazi zake zilivyoweza kukusaidia wewe.
    TATU, Muulize maswali mahsusi ambayo ungependa kujifunza kutoka kwake. Kisha msikilize anavyoyajibu hayo maswali. Muulize tena maswali mengine ili upate majibu zaidi
    NNE, Kama kuna tatizo kwenye biashara yake na wewe unaweza kulitatua, basi mwambie kwamba unaweza kulitatua hilo tatizo.
    MWISHO, kama kuna kitu ambacho ungependa huyu mtu akusaidie mwambie bila kusita. Hiki kitu sio kwamba nimekiweka mwisho kwa bahati mbaya ila nimekiweka mwisho maksudi kwa sababu kinaenda hivyo tu. kwa hiyo basi, nikusihi ufuate hizi hatua  ili uweze kufikia hatua kunwa kwenye kile ambacho unafanya.

    Hayo ndiyo mambo ya muhimu ammbayo naamini kama kwa siku ya leo utayafanyia kazi basi utaongeza mzunguko wako wa watu ambao unawafahamu. Usisite kuhakikisha kwamba unawasiliana nam ili kunipa mrejesho wa kile kilichotokea. Wasiliana name kwa whatsap tu, 0755848391
    Nikuktakie kila la kheri
    Ni mimi anayejali mafanikio yako
    GODIUS RWEYONGEZA

X