Home


  • Shukrani Zangu Na Taarifa Rasmi Ya Upatikanaji Wa Kitabu Cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni

    Jana tarehe 02.02.2020 ilikuwa ndio siku rasmi ya uzinduzi wa kitabu cha kutoka sifuri mpaka kileleni. Kitabu hiki ambacho kwa sasa kinapatikana katika mfumo wa nakala ngumu (hard copy) kilizinduliwa jana kwenye ukumbi wa Morogoro Hotel hapa Morogoro.
    Kwanza kabisa nichukue nafasi hii kuwapongeza sana watu waliohudhuria huu uzinduzi wa kipekee sana. Kiukweli nimefurahi sana kuwa nanyi na kujumuika nanyi kwenye hiyo siku ya kipekee sana, jana. Tarehe 02.02.2020 itabaki kuwa ni historia  kuwa kitabu hiki kilizinduliwa. na watu wote waliokuwepo walichukua nakala zao.


    Siku ya leo nimekuja na taarifa kwako wewe ambaye hukuweza kupata nafasi ya kuhudhuria uzinduzi huu wa kitabu.  Taarifa hii ni kwamba kitabu hiki sasa hivi kipo sokoni na unaweza kukipata popote pale ulipo Tanzania. Nakala moja ya kitabu hiki hapa inapatikana kwa shilingi 10,000 tu. na wewe hapo unaweza kuipata popote pale ulipo katika hii nchi.
    Kikubwa ni kwamba utaniambia uko wapi na mimi nitakupa utaratibu. Unaweza kuwasiliana na namba hii 0755848391 sasa hivi ili utaratibu wa kukuletea kitabu hiki hapa ufanyike.
    Mwaka huu ni mwaka wako wa mafanikio makubwa, hivyo jipange kuhakikisha kwamba kweli unafanyia kazi kile ambacho umeamua kufanya. Kitabu hiki hapa kitaweza kukufikisha kwenya malengo yako makubwa uliyojiwekea.
    Kumbuka kwamba gharama ya kitabu hiki hapa ni elfu 10,000/- ila kama utakuwa mkoani utaongeza 5,000/- ikiwa ni pamoja na gharama ya kutuma. Namba ya kufanya malipo ni 0755848391 karibu sana

    SOMA ZAIDI: KITABU; kutoka sifuri mpaka kileleni

    Ni mimi anayejali mafanikio yako,
    Godius Rweyongeza
    0766848391
    MOROGORO

  • JIFUNZE MATUMIZI SAHIHI YA NOTEBOOK: Ufanye Mwaka Huu Uwe Wa Mafanikio Kwa kutumia Maajabu Ya Notebook Tu

    Habari siku hii njema sana rafiki yangu. Bila shaka siku hii njema sana ya leo umeianza vyema kabisa bila shida yoyote ile. Kama utakuwa makini, utagundua kwamba kuna kitu ambacho tayari kimeshatokea kwenye mwaka huu wa kipekee 2020. Unajua kitu hicho ni kitu gani? Kitu hiki sio kingine, bali ni kuwa, mwezi mmoja wa mwaka huu umeisha kabisa.
    Huwezi amini yaani ule uliokuwa unaitwa mwaka mpya 2020, sasa hivi upya wake ushapotea. Na kama bado upya bado upo, basi upo ukingoni kabisa.
    Binafsi najua wazi kwamba mwaka huu ulijiwekea malengo. Hivi nikuulize haya malengo uliyaandika au uliweka tu kwenye kichwa, basi.  Mimi sijui wewe umefanyaje, ila kama hujaandika malengo yako sehemu, basi naona wazi kwamba unafeli mapema.
    Naomba nikuulize kitu kingine, hivi malengo yako hayo bado unayafanyia kazi? Kama huyafanyii kazi, sasa hapo ndio kabisaa. Mimi nichojua kuna watu ambao tayari wameshaanza kusahau malengo yao ya mwaka huu. Inawezekana sio wewe, ila watu hao wapo. Omba usiwe wewe hapo.
    Binafsi siku hii ya leo, kuna kitu kimoja muhimu sana ambacho ningependa nikushirikishe ili kiweze kukuepusha kuupoteza mwaka 2020 hata chembe. Yaani sitaki uupoteze huu mwaka 2020, kwa sababu nakujali. Na kwa kuwa mimi nakujali, hivyo basi jitahidi sana kuepuka vitu hivi ndani ya mwaka huu ili uweze kuwa na mwaka wenye baraka kubwa sana.
    Kitu hiki muhimu ambacho ningependa ukiepuke ndani ya mwaka huu ni kupita ndani ya mwaka bila notebook. Ujue hiki ni kitu kidogo sana ila kina maana kubwa. Notebook inakusaidia wewe hapo kujua maendeleo yako binafsi kwa kila siku inayopita. Tena kwa mwaka huu sitaki tu ununue notebook ilimradi umenunua. Nunua kabisa notebook yenye kalenda ya mwaka kuanzia januari mpaka disemba. Na kila siku hakikisha kwamba unarekodi kitu kwenye notebook yako hii mhimu. Yaani kila siku andika kitu kimoja ulichojifunza kwenye hii notebook yako, andika hatua ulizochukua na watu uliokutana nao au kuwasiliana  nao. Hivi ni vitu vidogo sana ila vyenye maana kubwa sana.
    Pia kwenye hii notebook hakikisha kwamba unaandika kipato chako ambacho umeingiza kwa siku na matumizi uliyofanya kila siku. Ukiwa na notebook yako na ukawa unafuatilia maendeleo yako kila siku, kila wiki na kila mwezi inakuwa ni rahisi sana kujua ni wapi unakwama ili uweze kujirekebisha na kusongambele zaidi katika kufanya kazi zako za kila siku. Lakini kitu hiki kitaifanya kila siku yako inakuwa ni bora zaidi ya ile ambayo ilitangulia na kitu kingine ni kwamba kitafanya kila mwezi uliotanulia unakuwa ni mwezi wewe kuchukua somo kubwa ulilojifunza ndani huo mwezi hiyo kutorudia kosa ambalo ulifanya kwa mwezi uliopita. Narudia tena. Mwaka huu usikubali kuuishi bila ya kuwa na notebook hata kidogo.
    Unaweza kuona kwamba kutoa kiasi cha pesa kizichozizdi elfu kumi kuwa ni kikubwa sana, ila kiuhalisia ni kwamba, kwa kutotoa hiki kiasi unajikuta kwamba unapoteza zaidi ya vile ambavyo wewe mwenyewe unategemea. Hivyo basi, hakikisha kwamba ndani ya mwaka huu 2020 unaamua kwa dhati kuwa na notebook. Hii siisemi kwa ajili ya manufaa yangu. Kama unaona hiki kitu ninachoandika hapa ni propaganda bora usiendelee kusoma, maana unapoteza muda wako. Ila kama unaamua kwa dhati kabisa kuhakikisha kwamba unakifanyia kazi, binafsi nina uhakika kwamba kitu hiki kinaenda kukusaidia sana kupiga hatua kubwa sana ndani ya mwaka huu 2020.
    Sasa napenda nimalizie na vitu vya muhimu ambavyo utapaswa kufanya na notebook yako ndani ya mwaka huu
    Kwanza kabisa andika jina la kitabu ambacho utasoma au utasikiliza ndani ya siku husika. Mwishoni mwa mwaka watu wengi huwa wanashirikisha ni vitabu vingapi wamesoma. Sasa kuna watu wengi huwa wanapata shida kujua ni vitabu vingapi walisoma kwa mwaka mzima ambao umepita just kwa sababu tu walikuwa hawaweki kumbukumbu. Kwa hiyo wanaanza kubahatisha na kubahatisha. Epuka kitu hiki kwa kuhakikisha kwamba  unaandika jina la kitabu ambacho unasoma kila siku kwenye notebook  yako. Just andika kichwa cha kitabu tu.
    Pili, andika kitu kikubwa ambacho umejifunza kwenye siku husika. Kitu hiki unaweza kuwa umekisoma kwenye kitabu,pia kitu hiki unaweza kuwa umekutana nacho kwenye uhalilsia wa kila sikku katika majukumu yako au mambo ambayo unafanyia kazi.  Kiandike kitu hiki ni muhimu sana.
    Tatu, andika pia mapato na matumizi yako kwa siku husika.
    Nne, andika majina ya watu muhimu unaokutana nao ndani ya siku husika au kuongea nao ndani ya siku husika.kama umekutana na mtu kwa mara ya kwanza, andika jina lake na namba yake ya simu baada ya jina lake.
    Tano,fanya tathimini kila unapofikia katikati ya mwezi wako na kila unapofikia mwishoni mwa mwezi. Jiulize hivi ni kweli bado nipo njia kuu ya kuelekea malengo yangu, au ndio kwanza napotea.
    Sijui kama umeweza kunielewa kwa hivi vitu ambavyo nimekueleza. Kitu kimoja tu ambacho najua umechanganyikiwa hapa unaweza ukawa unajiuliza hivi vitu vyote nawezaje kuviweka kwenye notebook moja? Mbona nafasi kwenye notebook huwa ni ndotgo na haitoshi kwa ajili ya hivi vitu vyote? Jibu langu hapa ni moja tu, inawezekana. Kama hujui ni namna gani ya kufanya na umesoma mpaka hapa basi nitafute kwenye hii namba 0755848391 kwa kutumia wasapu tu, kisha uniambie tatizo lako, nitakuwa tayari kukusaidia kwa hicho kitu chako ambacho unakwama.
    Sitaki uupoteze mwaka huu. Kama umeipoteza januari hakikisha kwamba huo unakuwa mwezi wako wa mwisho kupoteza. Hakuna muda wa kupoteza  tena ndani ya 2020. Jikwamue wewe mwenyewe kuanzia sasa hivi. Kanunue notebook leo, na ufanye yale niliyokushauri. Maajabu yake utakutana nayo huko mbeleni.
    Ni mimi anayejali mafanikio yako
    Godius Rweyongeza.
    Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.

  • YAH: MABADILIKO YA JALADA LA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI

    Rafiki yangu, hongera sana kwa siku hii ya kipekee sana.
    Ni siku sasa zimepita tangu uzinduzi wa kitabu cha  KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI.

    Nakumbuka ilikuwa ni tarehe 25 mwezi wa 9 2017, mtu wa kwanza aliposoma hicho kitabu.

    mmoja wa watu waliosoma hicho kitabu alikuwa ni Octavian, yeye alikuwa na haya ya kusema siku chache baada ya kuanza kukisoma

    Nimesoma kitabu cha kutoka sifuri mpaka kileleni. Cha ajabu nikiwa bado ukurasa wa utangulizi,  nimesoma sentensi, nikaona malengo niliyoyaweka ndani ya miaka miaka minane yanaenda kukedamilika  ndani ya miaka minne. Sasa sijui nikija kufika ukurasa wa mwisho itakuwaje. Big up sana ndugu yangu Godius

    Kitu kikubwa nikichonacho kwako siku ya leo ni juu mabadiliko yabjalada la kitabu. Kama unavyofahamu jalada la awali lilikuwa hili hapa.

    Hata hivyo sasa hivi jalada letu ndio hili hapa

    Kwa hiyo hili jalada ambalo leo ndio kwanza unaliona, ndio linaenda kuonekana kwenye kitabu.

    Mabadiliko ya jalada ni ishara ya mabadiliko makubwa ndani ya kitabu. Ninaenda kusa nakujulisha zaidi juu ya mabadiliko haya siku zijazo.

    kwa leo nilitaka nikujuze haya mabadiliko ya jalada. Hata hivyo unapaswa kufahamu kwamba, mabadiliko ya jalada ni ishara ya mabadiliko ya kilicho ndani ya kitabu.

    kwa maelezo zaidi soma zaidi: KITABU; KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI

    Ni mimi anayejali mafanikio yako,
    Godius Rweyo geza
    0755848391

  • Tabia Saba (07) Zinazoleta Umasikini Na Jinsi Ya Kuziepuka Ili Kutengeneza Utajiri

    Rafiki yangu, hongera sana kwa siku hii nyingine ya kipekee sana. Leo ikiwa ni februari 29 2020. siku zinazidi kusogea kwelikweli. Mwezi wa pili wa mwaka uliokuwa mpya, sasa unaelekea ukingoni. Siku chache zijazo tu utashangaa mwezi wa tatu huo umefika.
    Nina hakika moja ya lengo lako kubwa maishani ni kutokomeza umasikini na kujenga utajiri utakokunufaisha wewe, familia yako, watoto mpaka wajukuu. Yaani tuseme kuondoa laana ambayo imekuwepo sasa kwenye familia yenu (umasikini).
    Kuna tabia ambazo zitakuzuia kutengeneza utajiri ambao  umepanga. Na tabia hizi leo ndizo nataka uvunje moja kwa moja. Kama utaendelea na tabia hizi basi utaagana na utajiri maisha yako yote.
    TABIA YA KWANZA NI TABIA YA KULALAMIKA
    Hii ni tabia ambayo umekuwa nayo kwa siku sasa. Unalalamika juu ya hali ya hewa. unalalamika juu ya maisha ya watu wengine.
    Unalalamika juu ya matatixo ambayo unakutana nayo kila siku kwenye maisha.
    Hii hapa sio tabia ya matajiri hata kidogo. Matajiti wanajua kwamba kwenye maisha kuna vitu vya aina mbili.
    kwanza ni vile ambavyo wanaweza kuvibadili, pili ni vile ambavyo vipo nje ya uwezo wao na hivyo hawawezi kuvibadili kabisa.
    kwa hiyo matajiri wanachofanya ni kubadili vile wanavyoweza na kuachana na vile ambavyo hawawezi kubadili kabisa kwenye maisha yao.
    Hivyo ambavyo wao hawawezi kubadili wanawaachia watu wengine ili nao wafanye kazi yao.
    Na wewe ukiona kwamba kuna kuna kitu huwezi kubadili basi achana nacho, waachie wengine wanaoweza kubadili hicho kitu. Mwisho wa siku kama kila mtu atatimiza wajibu wake. Basi dunia itakuwa sehemu nzuri sana.
    Kwa hiyo kitu cha kufanya siku ya leo. gawa vile vitu ambavyo umekuwa unalalamilia kwa siku sasa kwenye vipengele viwili. kipengele cha kwanza ni kile ambacho unaweza kubadili.
    Na kipengele cha pili ni vile ambavyo huwezi kabisa kubadili.
    Kwa vile vitu ambavyo huwezi kubadili, basi waachie wengine. Wewe kazana na vile tu ambavyo unaweza kubadili tu.
    TABIA YA PILI, NI KUWA NA MATUMIZI MAKUNWA ZAIDI YA KIPATO CHAKO
    Hili ni kosa ambalo sidhani anahitajika nabii kukwambia ukweli huu. Ni wazi kwamba kama unatumia kiasi kikubwa zaidi ya kipato chako basi umasikini unakunyemelea kwa kasi kubwa.
    kwa hiyo basi, napenda ufahamu kwamba kuanzia leo hii, kiasi cha fedha ambacho unatumia, hakikisha kinakuwa ni kidogo kuliko pesa unayoingiza.
     kama unaona kiasi cha fedha unachoingiza  ni kidogo basi fanya utaratibu kuanzia leo wa kuongeza kipato chako. Anzisha hata biashara ambayo inaweza kuanza kukuongezea kipato cha ziada.
    Kamwe, kamwe,usitumie fedha zaidi ya kiasi unachoingiza.
    TABIA YA TATU,USINUNUE VITU AMBAVYO HAVIONGIZI FEDHA
    Kanuni muhimu ya fedha ni kwamba, unapaswa kuwa na rasilimali nyingi zinayoingiza fedha kuliko dhima (liabilitiy). rasilimali zinaingiza fedha zaidi na dhima zinatoa pesa mfukoni. kama una tabia ya kununua dhima zaidi ujue kwamba umasikini utakuwa unakunyemelea zaidi. wakati kama una tabia ya kununua rasilimali basi ujue kwamba utajiri utakuwa unakunyemelea pia. rafiki yangu nipende kukushauri kuwa unapaswa kujenga tabia ya kuwa na tabia ya kununua rasilimali zaidi ya unavyonunua dhima.
    TABIA YA NNE NI KUNUNUA VITU BILA MPANGILIO
    Hivi ushawahi kuona mtu akiwa na pesa ndio anawashwa kufanya matumizi kiasi kwamba anakuta kwamba pesa yote amenunua vitu ambavyo sio vya msingi. Ndio unakuta kwamba mtu ananunua  beseni, sinia au vitu vingie ambavyo vinaoenekana mbele ya macho yake bila mpangilio.
    Kama wewe una tabia hii hapa basi niseme kwamba hii ni dalili ya umasikini. Yaani umasikini unakunyemelea kwa kasi. Jenga tabia moja muhimu sana ya kitajiri, tabia hii ni ya kukaa na pesa na kuituliza kwanza kila unapoishika mkononi mwako. Kwa  hiyo unapopata pesa usipoteze akili yako. Yaani ukawa kama umelogwa, ukawa hushikiki nyumbani, ukaanza kutumia kwa kisingizio kwamba unatumia kidogo tu.
    Hapa ninaenda kukupa mbinu mbili ambazo zitakusaidia wewe hapo usiwe unatumia fedha zako hovyo hovyo.
    Jenga utaratibu wa kuwa unaandika  vitu ambavyo unaenda kununua kila unapoamua kwenda kufanya manunuzi. Usiende kununua kwa sababu una fedha, utajikukuta kwamba umenunua na vitu vingine ambavyo sio. Utanunua vitu vingine kwa sababu tu umevipenda kwenye macho yako tu. ila baadae utakuja kugundua kwamba ulikuwa huvihitaji.
    Pili, jenga utaratibu wa kufanya matumizi makubwa kwa wakati mmoja. Yaani yale matumizi ya muhimu unaweza kuyanunua kwa pamoja na kwa wingi. Kitu hiki hapa kitakusaidia wewe kutofanya matumizi ya hovyohovyo, lakini pia kitakufanya uwe unanunua vitu kwa bei ya kawaida sana.

    TABIA YA TANO NI KILA MMOJA KUJUA KWAMBA UNA PESA
    Hii ni tabia moja mbaya ambayo ukiendelea nayo basi itakukwamisha kwelikweli.  Hakuna mtu anapaswa kujua ni lini umeingiza kiasi kikubwa cha pesa au  lini haukuwa na pesa kabisa. usiwe unabadilika kulingana na pale unapopata pesa au unapokosa pesa. Tabia zako zinapaswa kuwa ni zilezile muda wote.
    Moja ya hasara kubwa ya wewe kujionesha kwa watu kwamba una pesa ni kwamba utakauwa unapata marafiki “feki”ambao wananuia kutumia pesa zako tu. lakini pesa zako zinapoisha na wao wanapotea.
    Na mchezo huu unaweza ukawa unaendelea miaka nenda, miaka rudi bila ya wewe kujua. Unaweza kufikia hatua ya kujiuliza, kwanini huwa ninapata marafiki ambao huwa wanakuja na kupotea? Jibu ni kwamba wanaona pesa wanakuja. Ukifulia tu, na wao wanaenda sehemu nyingine.
    Kuanzia leo hii, mtu yeyote asijue kwamba una pesa au hauna pesa. ishi maisha yaleyale bila kujali kwamba kwa sasa upo kwenye hali gani.
    TABIA YA SITA,  KUGAWA PESA BILA MPANGILIO
    Najua utakuwa na marafki, ndugu, na watu wengine ambao huwa wanakuomba pesa ya kula au pesa ya kutatua tatizo fulani ambalo limewakumba. Watu hawa wanajenga utaratibu kwamba upo muda wote. Hivyo wakipatwa na tatizo, muda wowote tu wanakimbilia kwako kuomba pesa. hata kama tatizo ni dogo na wao wanaweza kulitatua lakini bado wanakimbilia kwako ili uwasaidie pesa. kuanzia leo anza kujenga utaratibu wa tofauti. Watu wanapokuomba pesa wape ushauri wa namna wanavyoweza kutatua matatizo yao wenyewe.  Kiufupi ni kwamba usijenge utaratibu wa kuwapa watu samaki. Wakati unaweza kuwafundisha kumiliki bwawa la samaki. Hivyo wafundishe namna ya kumiliki bwawa la samaki badala ya kuwa unawapa samaki kila siku.
    Wafundishe kutatua matatizo yao ya kipesa wenyewe.
    TABIA YA SABA, KUKOPA NA KUKOPESHA
    Kama una tabia ya kukopa, basi leo iwe mwisho. Usikope teana. Kukopa ni tabia ya kimasikini ambayo watu masikini wanayo na wanaibeba kwenye maisha yao ya kila siku. Madeni sio kitu kizuri ambacho unawezakujizoeza. Badala ya kuiweka akili yako kwenye kuomba mikopo basi
    Pia usikopeshe fedha yako. Nadhani umewahi kusikia watu wanasema kwamba kukopa harusi kulipa matanga. Huu usemi sio kwamba ni wa kubahatisha. Ni wa ukweli. na asilimia kubwa ya watu ambao utawakopesha hawatajitokeza kulipa kwa muda walipanga. Na hata wakilipa watakulipa kwa kuchelewa nap engine baada ya mikwaruzano mingi sana. Sasa kwa nini ujiingize kwenye shida zote hizo.
    Kuna watu wanafanya  biashara ya kukopesha. Kama wewe hufanyi hii biashara basi usikopeshe.
    Rafiki yangu, nimeona kwamba nikwambiae vitu hivi vya kipekee sana leo ili uweze kuvijua. 

    Ni mimi anayejali mafanikio yako,
    GODIUS RWEYONGEZA

    KUWA MIONGONI MWA WATU AMBAO WANAPOKEA MAKALA MAALUMU KWA WATU MAALUMU KWA KUBONYEZA HAPA

    SUBSCRIBE KWENYE CHANNEL YANGU YA YOUTUBE HAPA


    JIUNGE NAMI KWENYE NURU ANGAZA

  • Maswali sahihi yatakupa matokeo sahihi

    Moja ya ujuzi ambao unauhitaji maishani mwako ni ujuzi wa kuuliza maswali sahihi. Watu wengi huwa wanaogopa kuuliza maswali maishani mwao kwa kuogopa kwamba wataonekana kwamba hawajui. Hata hivyo kama wahenga walivyosema, ni kwamba kuuliza sio ujinga. Lakini kikubwa zaidi ni kwamba kuuliza kunakufanya unakuwa mjanja zaidi. Yaani kunakufanya ujue kile kitu ambacho ulikuwa hujawahi kujua kama kipo au la.
    Kitu ambacho hukifahamu. Moja ya kitu ambacho unapaswa kukiuli sana ni VITAB. Ni ukweli usiopingika kuwa vitabu sahihi  hukupa  majibu sahihi. Na majibu sahihi husababisha uchukue hatua sahihi kitu ambacho kinaleta matokeo sahihi.
    Kiufupi tunaweza kusema kwamba,
    MASWALI SAHIHI=MAJIBU SAHIHI=HATUA SAHIHI=MATOKEO MAKUBWA.
    Kwa hiyo ukitaka kubadili  matokeo yako ya sasa hivi, anza kuuliza maswali sahihi. Ukiona kwamba kwa sasa hivi upo kwenye hali mbaya basi jua kwamba unapaswa kuuliza maswali sahihi ambayo  yatakupelekea wewe kuchukuka hatua sahihi ambazo zitakuletea matokeo sahihi.
    Ebu tuseme kwamba sasa hivi hujui jinsi ya kulima mapapai. Ukaamua tu kumpgia mtaalamu wa kilimo akusaidie kwenye hili. Ukamwuliza mtaalamu maswali sahihi juu ya kilimo cha mapapai. Mtaalamu wa kilimo atakupa majibu sahihi. Ukishapata majibu ya mtaalamu unakuwa hauna kitu kinginie cha kusubiri badala yake unachukua hatua sahihi. 

    Ukichukua hatua sahihi, utapata matokeo sahihi. Ambayo ndiyo matokeo makubwa. matokeo ambayo watu wengine hawawezi kabisa kuyapata kamwebkwa sababu hawana majibu yake. Na majibu wewe uliyapata kwa kuuliza maswali sahihi.

    SOMA ZAIDI; AKILI NENE vs MWILI MNENE

    Rafiki yangu hayo ndiyo mambo muhimu ambayo nilipenda uyafahamu ndani ya siku hii ya leo.

     Hivyo nikutakie kila la kheri kwenye kazi zako na katika utekelezaji wa majukumu yako. Leo kwenye mtandao wa youtube nimekuandalia video nzuri sana. Unaweza kuendelea mbele kuiangalia hapa ili uweze kujifunza zaidi na kuchukua hatua. https://youtu.be/TjMSSwdHWIk
    Tafadhali sana naomba usisahau kusbscribe ili uweze kupata video nyingine kwenye mtandao huo wa youtube. https://youtu.be/TjMSSwdHWIk

  • Jiepushe Na Vitu Hivi Viwili Ili Uweze Kupata Matokeo Mazuri Maishani Mwako

    Kuna makosa mawili ambayo umekuwa unafanya kwenye maisha yako ya kila siku ambayo kiukweli unapaswa kuyaepuka mara moja. La sivyo kama utaendelea kuyafanya makosa haya yatakufanya upoteze rasilimali hizi mbili muhimu. Utapoteza rasilimali muda lakini pia utapoteza rasilimali nguvu. Ukiyaepuka utaweza kukutumia muda wako vizuri kufanya mambo ya maana, lakini pia uwekeza nguvu hiyo kwenye kufanya mambo ambayo yanakujenga au kukuongezea kipato kwenye maisha yako.
    MOJA EPUKA KABISA KULALAMIKA
    Moja ya kitu ambacho watu wengi wanapenda kufanya kwenye maisha ni kulalamika. Kitu kidogo tu utakuta kwamba mtu analalamika. Wanailalamikia serikali, wanawalalamikia wazazi au kuwalalamikia watu. Katika maisha na katika hali yoyote ile ambayo wewe utakuwa nayo, huwezi kukosa mtu ambaye unaweza kumlalamikia.
    Hata ukijikwaa njiani unatembea peke yako lazima mtu wa kulalamikia tu utampata. Hata ukichelewa kazini lazima tu utapata wa kulalamikia. Unaweza kukuta unamlalamikia mtoto kwamba alichelewa kuamka, au unalalamikia daladala kwamba walichelewa kufikisha gari ulipokuwa umekusudia, au pengine utalalamikia barabara kwamba ni mbovu na hivyo zimekufanya wewe uchelewe. Kwa vyovyote vile mtu wa kulalamikia hajawahi kukosa hata siku moja.
    Ila ukifuatilia kwa umakini utagundua kwamba hivi vitu unasababisha wewe mwenyewe. Na ili uweze kugundua hili, wewe kila likitokea tatizo hakikisha kwamba unajiuliza hivi, imeukwaje mimi nikasababisha hili tatizo. Lazima utagundua kwamba kuna sehemu ambayo wewe umechangia kusababisha hilo tatizo.
    Kwa mfano tuseme kwamba umechelewa kazini.
    Ukijihoji kwa umakini utagundua kwamba wewe hapo kuna namna ambavyo umesababisha kuchelewa kazini . pengine ulichelewa kuamka au ulijizungusha sana nyumbani kiasi umechelewa au hukupangilia siku yako tangu jana hivyo leo umekurupuka tu ukawa unafanya kila kitu. Au umeanza kupiga stori na mshikaji au shoga wako. Kwa vyovyote vile ukifuatilia utagundua kwamba wewe hapo ndiye msababishaji wa hili tatizo na hakuna mtu mwingine ambaye amesababisha tatizo hili hapa.
    Kwa  hiyo basi badala ya kuanza kuwalalamikia watu wengine wewe tafuta kujua ni kwa jinsi gani wewe umesababisha hilo tatizo ili uweze kuliepuka hilo tatizo siku nyingine.

    KITU CHA PILI NI KUFUATAILIA MAISHA YA WATU WENGINE
    Kama umekuwa na tabia hiii hapa unahitaji kuiepuka mara moja. kwenye maisha  mtu pekee ambaye unahitaji kuhakikisha kwamba unamfuatilia kila siku ni wewe mwenyewe. Usihangaiike kumfuatilia mtu mwingine, maana maisha ya mtu mwingine hayawezi kukusaidia kitu chohcote kile. Hivyoo jifuatilie wewe mwenyewe uweze kujijua kiundani zaidi.
    Kwa mfano, jifuatilie ujue kwamba kwa siku unaingiza shilingi ngapi. Jifuatilie ujue kwamba unatumia muda gani mtandaoni na huo muda unakuwa unafuatilia vitu gani. Jifuatilie ili ujue kwamba unaongea na watu gani kwenye simu na hao watu mnaongea kitu gani kwa pamoja. Jifuatilie ujue kwamba chakula gani unakula na je, hicho chakula ni chakula bora kwa ajili ya afya yako. Jifuatilie ili uweze kujua kama unafanyia kazi malengo au au bado uko nyuma sana katika kuyafikia.
    Kiukweli kama hutajifuatilia wewe mwenywe ujue kwamba utakuwa unajipoteza na mwisho wa siku utabaki nyuma na utahidwa kukamiliha mambo muhimu sana kwenye maisha.

    Rafiki yangu hayo ndiyo mambo muhimu ambayo nilipenda uyafahamu ndani ya siku hii ya leo. Hivyo nikutakie kila la kheri kwenye kazi zako na katika utekelezaji wa majukumu yako. Leo kwenye mtandao wa youtube nimekuandalia video nzuri sana. Unaweza kuendelea mbele kuiangalia hapa ili uweze kujifunza zaidi na kuchukua hatua. https://youtu.be/TjMSSwdHWIk
    Tafadhali sana naomba usisahau kusbscribe ili uweze kupata video nyingine kwenye mtandao huo wa youtube. https://youtu.be/TjMSSwdHWIk

    KUPATA MAKALA MAALUMU KWA WATU MAALUMU BONYEZA HAPA
    KUPATA VITABU BONYEZA HAPA

  • Hili hapa ndio wazo bora la Kibiashara Kwa Mwaka 2020. Fanyia Kazi Wazo Hili Hapa Tu, Utakuwa Na Mwaka Wenye Mafanikio Makubwa Sana

    Kama mpaka sasa hivi umekuwa unajiuliza ni wazo gani bora la mwaka 2020 ambalo unaweza kufanyia  kazi na kupata mafanikio makubwa basi leo nimekuja na suluhisho. Na suluhisho iko wazi kabisa. yaani hadi mwenyewe utashanga kwa nini hukujua suluhisho hili mapema. Ila uhakika ni kwamba ukilifanyia kazi wazo hili ndani ya mwaka huu mmohja tu, basi nina uhakika  mwishoni mwa mwaka huu utakuwa tayari umekuwa mtu mwingine kabisa.
    Kwa hiyo kama mwaka huu bado hujapatwa wazo bora la biashara basi wewe tulia tu maana leo nina suluhisho. Lakini hata kama bado una biashara, wazo hili linakufaa pia.


    Wazo bora la mwaka 2020 ni LILE AMBALO UTAWEZA KULIFANYIA KAZI kila siku kwa siku 365. Hili ndilo wazo bora kabisa.
    Ngoja mikwambie kitu. Wazo huwa haliwi zuri kabla ya kulifanyiwa kazi. Wazo huwa linakuwa bora wakati linafanyiwa kazi au baada ya kufanyiwa kazi.
    Kuna siku Chinua Achebe aliulizwa, hivi ulikuwa unajua kuwa kitabu chako kitakuwa kitabu bora cha nyakati zote? alisema sikujua ila kwa wakati huo hicho ndicho kilikuwa kitu ambacho nilipaswa kufanya.
    Mwaka 2008 Kelvi Kelly aliandika makala ambayo ilisambaa mtandaoni na kuwa maarufu sana. Baadae alikuja kuandika kitabu kutokana na hiyo makala kilichouza sana. Baadae alikuja kuulizwa, hivi ulijua kuwa andiko lako hilo lingekuwa andiko bora sana. Alisema, sikujua, ila kwa wakati huo hicho kilikuwa ni kitu cha kipekee ambacho ningeweza kufanya.
    Kwa hiyo tunaweza kusema kwamba wazo bora huwa haliwi bora mpaka pale unapokuwa umelifanyia kazi na kulikamilisha. Ni wazi kwamba kitabu cha Chinua Achebe kisingekuwa maarufu kama asingekuwa ameweza kufanyia kazi wazo lake na kulikamilisha.
    Hakuna aliyejua kwamba iPhone ingekuwa wazo bora. ila baada ya Steve Jobs kulifanyia kazi na kulikamilisha lilikuwa wazo bora. Hakuna aliyejua kuwa magari ya Tesla yatakuwa bora ila baada ya kufanyiwa kazi na kukamilishwa ndio yakawa maarufu.
    Hakuna aliyejua kwamba google itakuwa kampuni  bora sana. ila wazo la Google lilipofanyiwa kazi likawa wazo bora sana.
    Kwa hiyo kama unataka kujua wazo bora mwaka huu 2020 basi lifanyie kazi wazo lako hilo kazi kwa siku 365. Nina uhakika ndani ya kipiindi hiki tutakuwa tayari na uhakika wa kwamba wazo lako ni bora sana.
    Nimeona niseme kitu hiki mapema leo, maana kuna watu wanakuwa na mawazo ya kuanzisha vitu vikubwa ila hawachukui hata hatua ya kwanza. Kuna watu wanakuwa na mawazo ya kuanzisba biashara kubwa kila siku wanasema kwamba ninataka nifanye kitu fulani ila bado hawachukui hatua. Na hata wewe unayesoma hapa, endapo hutafanyia kazi wazo ambalo unalo leo hii. Nina hakika mwakani tarehe kama hii uutakuwa bado hivyo hivyo ulivyo hapo. Ila ukiamua kulifanyia kazi leo hii, basi nina hakika kufikia mwakani tarehe kama hii utakuwa umeweza kufika hatua kubwa sana ambayo ulikuwa hujafikiria wewe mwenyewe.
    Kwa hili nakubaliana na Dr. Myles Munroe ambaye aliwahi kusema kwamba, sehemu tajiri sana hapa duniani  sio kwenye machimbo ya dhahabu kule Afrika Kusini. Wala sio kwenye kwenye visima vya mafuta kwenye nchi za uarabu, na wala sio kwamba utajiri upo kwenye nchi zenye gesi. Ila utajiri mkubwa sana umelala makaburini. Huko ndiko kuna watu wengi ambao walikuwa na vipaji na mawazo makubwa ila hawakuyafanyia kazi. Huko ndipo kulikuwa na watu waliokuwa na mawazo mazuri ya muziki ila hawakuwahi kuimba, huko ndiko kulikuwa na watu ambao walikuwa na ndoto za kuwa viongozi wakubwa wa nchi ila hawakuwahi hata kuthubutu kuchukua fomu za kugombea. 
    Sasa hiki ndicho kitu ambacho kitatokea kwako endapo hutafanyia kazi wazo lako mwaka huu. Endapo hutafanyia kazi wazo lako mwaka huu basi mwaka huu utaisha   na wewe bado utakuwa bado hivyo hivyo na utaendelea kuishi maisha yale yale uliyokuwa unaishai kila siku.
    Je, una wazo gani ndani ya mwaka huu? Ebu nenda sasa hivi ukalifanyie kazi sasa hivi ninapoongea  na wewe ili uweze kunufaika na wazo hili hapa
    Katika makala ijayo nitakueleza sababu za kwa nini unapaswa kufanyia kazi wazo lako mwaka huu na sio wakati mwingine.
    Tafadhali, usikose kutembelea blogu ya songembele kwa ajili ya kujifunza kila siku.
    Kama bado hujajiunga na kundi la think big for Africa unaaweza kunitumia ujumbe wasapu kwa nambari hii 0755848391 ili nikupe utaratibu wa kujiunga huku.

    KAMA BADO HUJASUBSCRIBE UJAJIUNGA KWENYE CHANNEL YANGU YA YOU TUBE BONYEZA HAPA
    https://www.youtube.com/channel/UCRGDR3d_Pt-TeRxSlF3ORzQ kisha USUBSCRIBE kwa ajili ya video mpya za kila siku.

    SOMA ZAIDI:  TOO BUSY TO WATCH YOUR DREAM; Hatua Sita Za Kutana na Watu Maarufu,  Wafanyabiashara Wakubwa Na Wanamziki Nguri Bila Kutumia Nguvu Kubwa

  • AKILI NENE vs MWILI MNENE

    Kuna kitu ambacho  watu wamekuwa wanakiona kama sifa. Na pengine kama ishara ya kuwa ya pesa. Kitu hiki ni mtu kunenepa. Kwa hiyo watu wanawekeza pesa kwenye kunenepa mwili ila wanasahau kitu muhimu zaidi ambacho kinapaswa kunenepa kwa mtu sio mwili. ila akili. Yaani hata iweje, fanya ufanyavyo ila hakikisha kwamba kila siku unanenepesha akili yako kwanza, kisha unakuja kunenepesha vitu vingine.

    Hivi kwa mfano tungekuwa tupo kwenye jamii ambapo kila mtu amenenepa akili unadhani jamii hii ingekuwaje! Bila shaka tungekuwa na magwiji, wabunifu, watu wanaothubutu na watu wanaochukua hatua za tofauti.

    Sasa je, tukibadilika sasa hivi si inawezekana? Ndio ni kweli inawezekana.

    Basi, kuanzia leo wewe hapo anza kuweka mpango wa kunenepesha akili yako kwanza kabla hujafiria kunenepesha kitu kitu kingine.

    Ninachofahamu kwamba
    AKILI NENE=HATUA NENE=MATOKEO MANENE😊.

    2020 ni mwaka wa kunenepesha akili.

    2020 ni mwaka kuwa na akili kubwa.

    kumbuka AKILI NENE=HATUA NENE=MATOKEO MANENE. Iila sasa hapa kuna kitu cha ziada nataka niongeze kwenye mlinganyo wetu.

    kitu hiki ni kwamba.
    VITABU SAHIHI=AKILI NENE=HATUA NENE=MATOKEO MANENE.

    Umeona ee! Vitabu sahihi huleta akili nene, akili nene husababisha tuchukue hatua kubwa, hatua kubwa huleta matokeo makubwa.

    Soma zaidi: Hili ni Jambo Linalowafanya Watu Washindwe Maishani

  • Kitu Hiki Kimoja Huwezi Kujifunza Kwenye Vitabu

    Rafiki yangu kwa siku sasa nimekuwa nakusisitiza juu ya usomaji wa vitabu. Na kitu hiki ni muhimu sana kwako ili uweze kusoga mbele kimaisha. Hata hivyo kwenye kusoma vitabu kuna kitu kimoja ambacho inaonekana kabisa bado hujakifahamu. Kitu hiki ni kwamba hutakikuta kwenye vitabu. Na kitu hiki ni KUCHUKUA HATUA.

    Ujue unaweza kuwa unasoma vitabu lakini bado ukawa huchukui vitabu. Vitabu vinaweza kukwambia kwamba unapaswa kuchukua hatua za hatari lakini wewe hata ukawa kabisa huchukui hatua hizi hapa. kitu hiki kitakufanya ukwame bila kujali kwamba wewe unasoma vitabu vingapi kila siku.

    Kazi kubwa inayofanywa na vitabu ni kukuweka kwenye njia sahihi. Lakini vitabu havikufanyi uitembee hiyo njia. Hivyo jukumu la kuitembea hiyo njia ya mafanikio lipo juu yako.

    Kama bado hujanielewa vizuri hapa naomba uchukulie mfano wa mama na mtoto wake anayeumwa. Ni ukwelil kwamba mtoto anayeumwa anakuwa anahitaji huduma kutoka kwa mama. Kitu kikukbwa ambacho mama yake anaweza kufanya ni kuhakikisha kamba anampa mtoto wake kidonge.

    Ila sasa unakuta kwamba mtoto mwenyewe anakuwa kabisa hataki hicho kidonge. Hivyo mama anamshika pua huyo mtoto na kumlazimisha kunywa dawa (pengine baada ya kuikoroga). Lakini mama akiachia pua, basi huyo mtoto anatema, hiyo dawa.

    Hii ndio kusema kwamba huyu  mtoto ataendelea kuumwa hata kwama ameonja dawa kidogo. Maana suluhisho la ugonjwa sio kuweka dawa mdomoni bali ni kunywa dawa kabisa.

    Sasa hiki ndicho kitu ambacho kinatokea kwako kama utasoma vitabu bila kuchukua hatua kila siku. Unakuwa sawa na mtoto anayeonja dawa na kuitema baada ya kuwa ameachiwa mdomo wake. NIKUOMBE KITU KIMOJA MUHIMU SANA KUANZIA LEO. Na kitu hiki ni KUCHUKUA HATUA JUU YA KILE UNACHOJIFUNZA KWENYE VITABU.

    Nikukumbushe tu kuwa vitabu vinaweza kukuweka kwenye njia sahihi, lakini vitabu hivi havitahusika na wewe kuweza kutembea njia hii ambayo ni sahihi.
    Rafiki yangu siku hiii ya leo umekuwa na mimi ambaye ninajali mafanikio yako.
    Godius Rweyongeza
    0755848391

  • Kitu Hiki Kitakupa Mafanikio Mara 10 Zaidi Mwaka Huu

    Napenda nikwambie kitu kimoja ambacho kitakusaidia kuinuka mwaka huu ili uweze kutengeneza mafanikio makubwa zaidi. Najua Laiti ungekuwa umeamgiwa Kitu Hiki tangu mwaka huu unaanza basi sasa hivi ungekuwa mbali kabisa.
    Tayari ungekuwa umefanya vitu ambavyo watu wengine hawajafanya.
    Ila sasa hujachelewa kujua kitu hiki, maana wanasema muda mzuri wa kupanda mti ulikuwa ni miaka kumi iliyopita. Na muda mzuri zaidi wa kupanda miti ni sasa hivi.
    KITU CHENYEWE NI KUANZA.
    Ujue Zig Ziglar, amewahi  kusema kuwa huhitaji kuwa mkubwa ili kuanza. Badala yake unahitaji kuanza ili uwe mkubwa.
    sasa watu wengi sana wamekuwa hawaanzi kwa kusubiri kila kitu kikae sawa. Hawaanzi kwa kusubiri labda watengenezewe mazingira mazuri.
    nipende tu kukwambia kwamba hakuna wakati ambapo unaweza kusubiri kikae sawa na wakati huo ukatokea. Mara nyingi watu huwa wanaanza wakiea hawajawa tayari lakini wanaendelea.
    Thomas Edison alikuwa na wazo la kutengeneza taa, ila ukweli ni kwamba alikuwa hajui ni vitu gani haswa anapaswa kutumia kwenye kutengeneza taa. Hivyo yeye alianza. Alijaribu mara nyingi zaidi kuliko mtu mwingine. Alijaribu kila vitu vya kila aina.  kitu hiki ndicho kilipelekea Thomas Edison Kushindwa maea elfu kumi. 
    kiukweli kama unasubiri kila kitu kikae sawa. Mimi naona waziwazi junsi unavyojichelewesha.  kwenye mtandao wa Youtube nimekuandalia video nzuri sana ambayo itakusaidia wewe hapo uweze kuanza. 
    kamilisha somo letu la leo 
    kwa kuangalia video hii hapa.
    Ukimaliza kuangalia video, tafadhali sana usisahau KUSUBSCRIBE ili uendelee kupata videos nyingine zaidi. Kila la kheri

    Umekuwa nami ninayejali mafanikio yako,
    Godius Rweyongeza.
    0755848391

X