Home


  • Vitu Viwili Vya Kushangaza Kuhusu Warren Buffet. Angekuwa Tanzania Watu Wangesema Ametoa Kafara Au Basi Watu Wangesingizia Majini

    Katika bara la Afrika kuna tabia moja ya kipekee sana.
    Tabia hii imejengwa kwenye msingi kwamba, anayemiliki kitu cha bei ghali basi yeye ndiye, anachukuliwa kama tajiri. Kwa mfano, kama wewe unamiliki nyumba ya bei ghali sana basi wewe ndiye mtu tajiri sana kuliko wote. Hiyo ndio imani ya waafrika walio wengi.
    Kwa hiyo imani hiyo imepelekwa karbia kwenye kila kitu.  Anayemiliki simu ya bei ghali basi huyo ndiye tajiri. Anayevaa nguo za kisasa basi huyo ndiye tajiri na alipamba nyumba yake kwa maua ya kisasa basi huyo ndiye tajiri.
    Lakini matajiri wamedhihirisha kuwa hilo sio kweli. Sio tu kwa maneno bali kwa kuyaishi. Na leo hii nisingependa niongelee matajiri wengi sana. Bali nimwongelee bilionea Warren Buffet. Kwa utajiri wake basi Tanzania anafaa kuitwa Trilionea. Lakini kuna vitu viwili vya kushangaza sana kuhusu Bilionea huyu. Na nina uhakika kwa vitu hivi vya kushangaza angekuwa Tanzania basi watu wengi wangesema ametoa Kafara. Wengine wangesema majini ndiyo yanamtuma na kauli nyingine ambazo wewe mwenyewe utakuwa unazijua.
    Vitu hivi vya kushangaz akuhusu bilionea huyu ni kwamba

    SOMA ZAIDI: Je, Shule Na Maisha Yanaendana?

    1. ANAISHI KWENYE NYUMBA ALIYOIJENGA MWAKA 1958.
    Kiukweli kwa pesa alizonazo. Ni wazi kwamba kama angekuwa mtu mwingine basi angekuwa anaishi kwa nyumba moja matata sana. Lakini yeye anaishi tu kwenye nyumba ya kawaida aliyonunua zaidi ya miaka 60 iliyopita. na nyumba ile anaipa thamani kubwa sana. Warren Buffet anasema kwamba hiyo nyumba anayoishi ni uwekezaji nambari tatu mkubwa kwake kuwahi kufanya. Kwa hiyo unaweza kuona ni kwa namna gani anaiheshimu sana.
    Kuna funzo na somo kubwa sana hapa la kujifunza kwa kwake. usikimbizane na kila kila kitu. Kimbizana zaidi na vitu ambavyo vinaingiza fedha mfukoni mwako.
    Pia tunajifunza kwamba tunapaswa kuheshimu uwekezaji ambao tunaufanya siku hii ya leo. Kama unaona wazi kwamba unawekeza kwenye anasa basi mwisho wa siku utakuja kujutia uwekezaji wako huo.
    2. AMEANZA KUTUMIA IPHONE MWAKA HUU
    Huwezi amini kusikia kwamba bilionea huyu alikuwa bado hajamiliki simu nzuri na kali kama Iphone. Ila mwaka huu ndio ameanza kutumia iphone baada ya simu yake ya zamani kuharibika. Buffet amekuwa anatumia simu ya kawaida sana kutoka kwenye kampuni ya SAMSUNG.  Simu hiyo ilikuwa na thamani ya dola 20 tu. sawa na elfu 44 za kitanzania.
    Unaweza kushangaa, wakati watu wengine wanakimbizana kununua bei za bei kubwa sana mpaka milioni mbili na zaidi. Yeye ana simu ya elfu 44 tu.
    Wakati mwingine mtu akipoteza simu yake kwa siku moja tu ndio anajiona kama vile amepoteza maisha. Ila yeye mwaka huu tu ndio amekuja kununua simu ya aina hii.
    Kwenye hili tunajifunza kwamba
    Usiwe mtu wa kutaka kuonekana una viwango wakati viwango vyenyewe huna. Hata kama una viwango, usikimbilie kujionesha kwa watu. Kila mtu yuko bize na maisha yako.
    Tunajifunza pia kuwa na misimamo  na kutoendeshwa na hisia. Kuna vijana wengi wananunua simu bila kujua hata hizo simu wananunua za nini.  mtu ananuhnua simu ya milioni au zaidi, kisha anaitumia kwa kazi tatu tu. kupiga, kupoteza muda na kuchati. Wakati angeweza kufanya hayo yote kwa simu ya elfu 20 tu.

    SOMA ZAIDI; Uwekezaji Huu Utakufanya Kuwa Mtu Mkuu Kwenye Hii Dunia

    HITIMISHO
    Siku ya leo napenda nihitimishe kwa kukuelekeza kanuni mbili muhimu sana kutoka kwa bilionea huyu. Kanuni ya kwanza ni kwamba, kamwe usipoteze fedha
    Na kanuni ya pili ni kwamba usiisahau kanuni ya kwanza.
    Binafsi rafiki yangu napenda nihitimishe kwa kusema kwamba, anza kujenga nidhanu ya kutumia vizuri pesa kidogo.  Inawezekana kwa siku sasa umekuwa unaomba upate utajiri. Lakini sasa kama huwezi kutumia vizuri fedha kidogo zinazopita mikononi mwako, basi niseme tu waziwazi kwamba, miaka itazidi kupita. Na siku moja utakuja kushangaa utajiri haupati. Siku hiyo ukijihoji vizuri utagundua kwamba utajiri huu ulishapita mikononi mwako, ila tatizo lako ni kwamba hukuwa makini kwenye matumizi ya fedha kidogo ambayo ulikuwa unazipata.
    Nikutakie kila la kheri rafiki yangu.

  • Maendeleo Yetu Kama Taifa Yatatokea Hivi. Tofauti Na hapo Ni Uongo

    Maendeleo yetu kama taifa yanaanza na maendeleo ya mtu mmoja mmoja. Kama kila mtu atajitoa kuhakikisha anaongeza kipato chake. Kila mtu atajitoa kuhakikisha kwamba anakuwa bora kwenye kile anachofanya basi ni wazi kwamba taifa hili litaendelea kwa kasi sana.

    Binafsi naona kuna vikwazo vitatu vinazuia hili. Na tabia hizi zipo zaidi kwa vijana ambao ndio nguvu kazi ya nchi. Lakini athari yake ni kwa watu wote (wanaohusika na wasiohusika). 

    kwa mfano kuna vijana asipokuwepo mtu hawawezi kujituma, hawawezi kufanya kazi kwa bidii. hawawezi kwenda hatua ya ziada.Kwao mpaka awepo mtu wa kumwambia nenda huku, au usiende kule, mpaka awepo mtu wa kumwambia fanya hiki au achana na kile. ASIPOKUWEPO MTU WA AINA HII BASI KAZI INAKWAMA.

    unaweza kuona wazi kwamba tabia hizi sio za kuendeleza hata kidogo.

    basi kwa msingi huo nikualike ili uweze kusikiliza somo hili hapa mpaka mwisho.
    https://youtu.be/VbgeSLWDKzs

    usishau KUSUBSCRIBE.

  • Kitu Kimoja Cha Kishujaa Unachoweza Kufaya Kwa Dakika Moja Kikawa Na Manufaa Maisha Yako Yote

    Rafiki yangu, hongera sana kwa nafasi hii nyingine ya kipekee sana. Bila shaka siku ya leo ni siku yako ya kipekee sana.
    Ujue shujaa ni mtu ambaye anaheshimika sana kwenye jamii zetu. Lakini siku hizi jinsi ushujaa unavyopatikana ni tofauti kabisa na zamani. Wakati zamani ulihitajika tu uende vitani upigane na kulifanya taifa lako au eneo  lipate ushindi. Sasa hivi ushujaa hauna haja ya kuwa na hivyo.
    Tupo kwenye zama ambapo mtu mwenye maarifa sahihi ndiye anakuwa shujaa. Ukitaka kunielewa hapa tuseme kwamba kuna tetemeko linaenda kutokea sehemu. Na wewe una taarifa sahihi ila mwenzako hana taarifa za tetemeko. Kwa sababu una taarifa za tetemeko unaamua kuhairisha safari yako ya kwenda eneo hilo  mpaka wakati mwingine. Ila rafiki yako kwa sababu hana taarifa sahihi basi yeye anaenda kichwa kichwa.  Likitokea tetemeko basi kitakachomtapa hapa hatutaki kujua. Lakini wewe utakuwa tayari umekuwa shujaa kwa sababu uliweza kuzuia baya lolote kutokea kwako kwa sababu ulikuwa na taarifa sahihi.
    Sijui unanielewa hapo. Kwa hiyo shujaa wa karne ya 21 sio yule anayepigana vita na kurudi kidedea. Shujaa wa karne ya 21 ni mtu mwenye maarifa na taarifa sahihi kwa wakati.
    Moja ya watu ambao wamejitoa kuhakikisha kwamba unapata taarifa na maarifa sahihi wa kwa wakati kwenye karne hii basi ni mimi hapa rafiki yako GODIUS RWEYONGEZA.  Nimekuwa natoa maarifa haya kupitia mtandao huu wa songambele na nitaendelea kufanya hivyo kila siku.
    Lakini pia nitaendelea kuto maarifa zaidi kupitia channel yetu ya YOUTUBE ambayo unaweza kuitembelea kwa kubonyeza HAPA
    Wakati naendelea kutoa maarifa haya kuna kikundi cha watu wachache ambacho huwa kinapata maarifa zaidi kutoka kwangu kwa njia ya barua pepe. Kikundi hiki cha watu wachache sana binafsi nakipenda sana maana kinapata manufaa mengi zaidi. Leo hii nimeona nikushirikishe kitu hiki ili na wewe uweze kujiunga na kikundi hiki cha watu wachache kwa kujaza taarifa zako HAPA ili na wewe uwe miongoni mwa watakaopata maarifa haya kipekee bure kabisa.
    Kwa kufanya hivyo tu, utaweza kupata maarifa zaidi na mazuri zaidi kutoka kwangu kila mara.
    Rafiki fanya kitu hiki cha kipekee sana  leo ili uweze kupata maarifa ya kishujaa ambayo watu wengine hawapati kutoka kwangu. Na ubora ni kwamba hakichukui muda. Ni kitu cha dakika moja tu umemaliza.
    Bonyeza hapa kufanya hivyo sasa hivi rafiki yangu.
    Basi kwa leo napenda nikutakie kila la kheri.

  • UNATAKA KULA MEMA YA NCHI, BASI SOMA HAPA

    Rafiki yangu, habari ya jioni. Leo nimeona nikwambie aina tatu za ujuzi ambao ukiwa nao wewe hapo utakula mema ya dunia hii.
    Nadhani umewahi kusikia watu wanaosemekana kula mema ya nchi. Leo hii kuna vitu vitatu ambavyo ni uhakika ukiwa navyo basi utakuwa njiani kula mema ya nchi.

    Kwanza, ni ujuzi wa kuandika andiko lililotukuka.

    Hiki ni kitu ambacho nimekuwa nashauri mtu yeyote yule ambaye anaishi hapa duniani aweze kujifunza. Kwa chochote kile ambacho unafanya basi unahitaji kujifunza kuandika. Ila sio tu kuandika. KUANDIKA ANDIKO, LILILOTUKUKA.

    Andiko ambalo mtu akisoma, atataka asome tena na tena.
    kitu hiki kitakusaidia katika kuuza, katika kushawishi watu wanunue, wawekeze, au katika kazi yako yoyote n.k.

    kwahiyo weka utaratibu wa kujifunza ujuzi huu wa kipekee sana.

    Pili ni UJUZI WA KUUZA

    Huu ni ujuzi mwingine muhimu sana. Ujue kwa namna moja au nyingine katika maisha utalazikika kuuza. ukisimama mbele ya watu kuongea ujue unauza. ukiongea na mtu unakuwa unafanya mauzo, ukitaka mtu akubali falsafa au hoja yako basi ujue kwamba utakuwa unafanya mauzo, ukitaka kumpata mwenza lazima  utatakiwa kufanya mauzo, na hata kama unahubiri bado ni uuzaji.

    kwa hiyo jifunze namna bora ya kuuza ambayo itawafanya watu wanunue unachouza. Jua saikolijia ya watu ili ikusaidie katika aina ya mauzo unayofanya.

    Soma Zaidi: Usitafute Kiki Kwa Kutengeneza Matatizo

    3. Tatu ni KUNENA

    Huu ni ujuzi wa tatu muhimu sana. Kunena au kama kunavyofahamika kwa kiingereza ni public speaking.  Hiki ni kitu muhimu pia.
    kila siku tunakutana na watu na tukiwa na watu hawa tunaongea, tunawasilisha na kujadili mada, tunacheka na kufurahi.

    lakini unahitaji kujifunza kunena. Na kunena ni zaidi ya kuongea. Najua utauliza sasa kunena ni nini? Kwa haraka tu naweza kusema KUNENA ni KUONGEA NA WATU WAKASILIZA.

    Sasa kuongea na watu wakusikilize wewe ni kazi. Na sio kazi ndogo.
    Nadhani imewahi kukutokea  unaanza kumsikiliza mtu ila unagundua kuwa hana pointi za maana. Yaani amesimama mbele yako na wewe unaona wazi kwamba hakuna kitu cha maana anafanya.

    Omba isikutokee wewe. Na namna nzuri ya kuomba ni kuanza kufanya mazoezi leo.
    Rafiki, hizo ndizo aina tatu za ujuzi ambazo nimeona wazi nikwambie jioni ya leo.

    Nadhani kama utakuwa umefuatilia. Aina hizi tatu zinaendana sana. Yaani zote zinaelekea kuwa na lengo moja tu. Ukiwa na aina tatu za ujuzi, ni wazi kwamba utakuwa mtu anayetafutwa sana kwenye hii dunia. Au kiufupi ni kwamba utakula mema ya nchi.

    USHAURI WANGU: Chagua aina moja ya ujuzi ambao unaweza kuanza kufanyia kazi leo.

    Usianze na kila ujuzi. Anza na ujuzi mmoja, ufikishe kwenye viwango vikubwa. Kisha kuza ujuzi mwingine. Mwisho wa siku utajikuta umeweza kujenga kila ujuzi.

    SOMA ZAIDI: MAMBO MATATU AMBAYO VIJANA WA KITANZANIA WANAKOSEA ILA WANAYAFANYA KUWA HALALI

    Rafiki yangu binafsi nakupenda sana na nikutakie usiku mwema.
    Kila la Kheri.

  • Siri Muhimu Ya Mauzo Kutoka Kwa Tony Robins

    Naandika makala hii ikiwa ni usiku saa 2 kasoro dakika tatu sasa ya tarehe 21//2/2020. sijajua wewe makala hii unaisoma muda gani na siku gani. Nimeamua niandike makala hii baada ya kuwa nimetoka kufanya mauzo sehemu. Hivyo wakati narudi njiani ndio nikakumbuka kauli mojawapo ya Tony Robins. Hivyo nikaona wazi kwamba kuna somo kubwa sana la kujifunza hapa. na nimeamua nikushirikishe somo hili hapa, ili na wewe uweze kujifunza kitu na kuchukua hatua mara moja.
    Tony Robins alianza maisha yake  uhamasishaji kwa kuuza kazi za Jim Rohn. Alikuwa anauza CDs, vitabu na mafunzo mengine ya Jim Rohn. Sasa wakati anawazungukia watu na kuwauzia mafunzo hayo. Tony Robins alikuwa na kauli yake maarufu sana. Alipokuwa anaenda kwa mtu na yule mtu akawa haeleweki kwenye kununua, basi Tony Robins alikuwa anamwambia, NIKATALIE ILI NIKALIPWE. Sasa watu walikuwa wanashangaa, yaani wewe unalipwaje mimi nikikutalia. Tony Robins akawa anawaambia kwamba mnikatalia watu 10 anatokea mtu mmoja ambaye anafanya manunuzi makubwa. Wakikataaa wengine 10 anatokea mtu mwingine mmoja ambaye ananunua. Na anafanya manunuzi makubwa.
    Kitu kingine kikawa ni kwamba wakikataa watu mapema basi inakuwa ni nafasi yake kuwahi kuwaendea watu wengine ambao watanunua.
    Sasa leo ambacho ninataka tujifunze sio kwamba na wewe uende uanze kuwaambia watu hicho kitu. Bali kwamba ukienda kuuza kitu kwa mtu na akawa hajanunua basi sio kwamba  huo unapaswa kuwa mwisho wako. Wewe endelea mbele bila kukosa. Endelea mbele. Kadri utakavyokuwa unawafikia watu zaidi ndivyo unakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuuza. Kuliko pale unapokuwa umewafikia watu wachache tu.
    Rafiki yangu naomba uuchukue kitu hiki muhimu sana kwenye kazi zako ambazo unafanya. Kwenye biashara yako na hata kwenye mauzo. Jitahidi kwamba uwafikie watu wengi zaidi.
    Nilichogundua unapokuwa unauza kitu. Kuna watu ambao wakikuona tu watajenga fikra za kukitaa kitu chako kabla hata hawajakusikiliza.
    Kuna watu ambao watakusililiza ila hawatanunua.
    Kuna watu watakusililiza na hata kabla hujamaliza wataomba kununua.
    Na kuna watu watakusiliza ila kama hutawaambia wanunue, hawatanunua. Hivyo jitahidi unapoamua kufanya mauzo basi unamwangalia mtu wako uliyemlenga vizuri.
    Ukiona mtu ameshawishika na yupo tayari kununua, basi usiendelee kuweka maneo mengi zaidi. Badala yake, mpe bidhaa na yeye akupe fedha.
    Ukiona kwamba mtu mpaka anahitaji aambiwe kwamba nunua au chukua bidhaa hii. Basi mwambie hivyo. Rafiki yangu hayo ni mambo ya muhimu sana ambayo niliona nikwambie siku ya leo.
    Nashukuru sana. Na ninakutakia kila la kheri.
    Naweka kalamu chini ikiwa ni saa 8 dakika 13 sasa usiku.
    Kila la kheri.

    Soma Zaidi: Vitu Vitano Vinavyoharibu Ubunifu Wa Watanzania 

    kijana usidanganyike, wakati unazidi kusogea


  • Mambo Saba (07) Ya Kufanya Pale Unapokuwa Hauna Cha Kufanya

    Huwa inatokea kwa watu wengi mara nyingi, ambapo wanajikuta kwamba hawana kitu cha kufanya. Kitu hiki huwa kinawafanya watu wengi kuanza kuzunguka huku na kule wakisema kwamba wanapoteza muda. Sasa siku ya leo napenda nikwambie vitu vitano ambavyo utapaswa kufaya pale ambapo utakuwa unaona kwamba hauna kitu cha kufanya.
    KWANZA, SOMA KITABU
    Ukijikkuta katika mazingira ambayo unaona kwamba hauna kitu cha kufanya, basi chukua kitabu na anza kusoma. Akili yako yote iweke kwenye kitabu hicho ambacho umeamua kusoma. Tena hakikisha kwamba una daftari na karatasi ambapo utapata kuandika vitu vya kipekee sana kutoka kwenye kitabu hicho.
    Kwa kufanya hivi utakuwa umeutumia muda wako vizuri badala ya kusema kwamba, uzunguke huku na kule UKIPOTEZA MUDA
    PILI, PITIA MALENGO YAKO
    Mara nyingi ukiona kwamba mtu anasema kwamba anapoteza muda, basi ujue kwamba hiyo ni ishara tosha ya kwamba hajapangilia vizuri malengo yake. Hivyo ukijiona kwamba upo kwenye hali kama hii ambayo huelewi ni kitu gani ambacho unapaswa kufanya basi chukua malengo yako na uyapitie. Kitu hiki hapa kitakusaidia kujua ni kitu gani haswa unapaswa kufanya. Kitu hiki pia kitakusaidia kuweka nguvu yako kubwa kwenye kutimiza malengo yako ambayo yako mkononi mwako.
    ANGALIA SOMO HILI YOUTUBE:  Jinsi Ya Kutengeneza Fedha Mtandaoni
    TATU, ITUMIE NAFASI HII KUONGEZA WATEJA WAWILI KWENYE BIASHARA YAKO
    Ukiona kwamba hauna kitu cha kufanya basi utumie muda huu kwa ajili ya kutafuta wateja wawili wa biashara yako au huduma yako ambayo unatoa. Hivyo unaweza kutumia muda  huu kuwapigia watu ambao wanaweza kununua bidhaa zako au unaweza kwenda ofisi/ nyumba zao ili uongee nao kuhusu biashara yako au huduma yako. Kwa kufanya hivi utakuwa umeutumia vizuri muda wako kwa kuhakikisha kwamba umeongeza wateja na mauzo kwenye bidhaa yako.
    Kama hauna biashara basi unaweza kuutumia muda huu kuangalia ni biashara gani unaweza kuanza kufanya mara moja.
    NNE, UTUMIE MUDA HUU KUMSHUKKURU  MTU MMOJA
    Kila siku kwako inakuwa ni nafasi yako wewe hapo kukutana na watu wengine. Sasa unapokutana na watu, kuna wale watu ambao mnabadilishana namba, kuna wale ambao wanakusaidia kufanya na kutimiza kazi fulani, kuna wale ambao wanashiriki kuinua kipaji au ndoto yako. Hivyo utumie muda huu katika kuandika ujumbe mfupi wa kumshukuru mtu wa aina hii. Au kupiga simu na pengine kuandika barua kwa ajili ya mtu huyu. Mshukuru kwa kitu cha kipekee ambacho amekufanyia.
    Haya ni matumizi mazuri ya muda wako  ambao unao siku ya leo.
    TANO, SIKILIZA VITABU VILIVYOSOMWA
    Kama wewe unapenda kuzunguka na hupendi kukaa eneo moja, basi cha kufanya hakikisha kwamba unakuwa na vitabu vilivyosomwa. Unaweza kusikiliza vitabu hivi hapa ukiwa unatembea. Unaweza kusikiliza vitabu hivi hapa ukiwa umekaa chini. Lakini pia unaweza kusikiliza vitabu hivi hapa ukiwa unaendelea na shughuli nyingine kama hii hapa tunayoenda kuona kwenye namba sita chini.
    SITA, TENGENEZA CHAKULA AMBACHO UMEKUWA UNAPENDA KWA SIKU SASA
    Inawezekana kuna aina ya chakula umekuwa unapenda kula kwa siku sasa, ila kutokana na kwamba hukuwa na muda wa kukitengeneza basi ulikwama kwenye kufanya hiki kitu. Hivyo, kwa muda huu ambao unaona kwamba hauna kitu cha kufanya unaweza kuutumia kutengeneza chakula cha kipekee ambacho kwa siku umekuwa unapenda kula.
    Au kinywaji cha kipekee ambacho umekuwa unapenda kunywa kwa siku sasa hivi.
    Haya yatakuwa ni matumizi mazuri ya muda wako katika kujenga afya yako.
    SABA, ONGEA NA WATOTO WAKO KUHUSU MAMBO MBALIMBALI YA KISHULE NA MAISHA
    Unaweza ukawa ni mtu ambaye umekuwa unabanwa sana na kazi za hapa na pale, kiasi kwamba watoto wako hawapati nafasi ya kuwa karibu na wewe. Na pengine hata mwenza wako hapati muda mzuri wa kuwa karibu na wewe. Unaweza kuutumia muda huu kukaa na familia na kuongea mambo mbalimbali.
    Unaweza kuutumia muda huu kufuatilia maendeleo ya watoto wako shuleni. Lakini pia unaweza kuutumia muda huu kuwasaidia watoto wako kufanya kazi za shuleni.
    Rafiki yangu haya ndio mambo saba ya kufanya pale unapojiona kwamba hauna kitu cha kufanya. Nina hakika sana kwamba mambo haya yatakusaidia sana pale utakapojikukta kwenye hali hii hapa.
    Kitu hiki kitakufanya usiwe mtu wa kusema kwamba ninapoteza muda tu hapa. badala yake utakuwa na kila kitu ambacho kimepangiliwa  vizuri sana.
    Nashukuru sana nikutakie kila la kheri
    Ni mimi anayejali mafanikio yako
    GODIUS RWEYONGEZA

    KUWA MIONGONI MWA WATU AMBAO WANAPOKEA MAKALA MAALUMU KWA WATU MAALUMU KWA KUBONYEZA HAPA

    SUBSCRIBE KWENYE CHANNEL YANGU YA YOUTUBE HAPA


    JIUNGE NAMI KWENYE NURU ANGAZA

  • Hivi Ndivyo Unaweza Kufanya Mishale Inayolenga KukuangamizaKuwa Baraka

    Maisha hayatakuja kuwa rahisi kwako hata kidogo. Maisha yataendelea kukurushia mawe na mishale. Na kadri utakavyokuwa  na ndoto kubwa sana, ndivyo mishale itakavyokuwa mingi zaidi.

    habari njema ni kwamba ukiwa mgumu, mishale hii itakuumiza kwa muda tu lakini bado utaendelea.

    Kuna usemi mzuri wa kiingereza ambao unasema kuwa safari inapokuwa ngumu, wagumu ndio huwa wanaendelea na safari yao ( When the going gets tough, the tough get going) Sio wanarudi nyuma.
    Sio wanakata tamaa, bali wanaendelea. Mpaka kinaeleweka (mpaka kileleni)

    Sasa hapa nataka nikwambie vitu ambavyo vitakufanya wewe uweze kuendelea hata mambo yanapokuwa magumu.

    KWANZA HAKIKISHA KUWA UNA MAONO MAKUBWA
    Rafiki yangu, bila maono makubwa utapoteza mwelekeo hata ukisukumwa kidogo tu. Yaani utaanza kusema hiki kitu sio kwa ajili yangu (sio type yangu).
    Ndio maana, Dale Carnegie anatuasa kwa kusema kwamba, vitu vingi katila dunia hii vimeweza kukamilishwa na watu ambao waliweza kuendelea pale ambapo kulionekana kwamba hakuna matumaini. Kilichowafanya watu waliofikia makubwa  waweze kuendelea ni kuwa na maono makubwa.

    Kuna siku nilikuwa nasoma Tawasifu ya Thomas Edison. Niligundua kwamba Thomas Edison alishindwa sana, sana.  Ila alikuwa anaendeleka kila baada ya kushindwa. Kwake kushindwa kukikuwa kama msukumo wake wa kusongambele. Bila shaka lolote Thomas Edison alikuwa anafahamu kwamba Nyuma Ya Ushindi kuna kushindwa, kushindwa, Kushindwa. Aliendelea kusongambele kuelekea maono na ndoto yake kubwa. Hivi wewe nikikuuliza unataka kufika wapi baada ya mwaka mmoja au miaka mitatu ijayo? unataka kuwa umeifikisha wapi biashara yako miaka 10 ijayo. ukiweza kujibu maswali haya, basi nina hakika. Utakuwa na Uwezo wa kuendelea mbele hata mambo yatakapokuwa magumu.

    PILI, FAHAMU KUWA VIKWAZO NI KIPIMO SAHIHI CHA BINADAMU
    Hatuwezi kujua kama unaweza kufanya makubwa kama hujapitia kwenye vikwazo, changamoto, kurushiwa mawe na mishale. Chuma huwa kinakuwa imara baada ya kupitia kwenye moto.
    Matatizo huwa yanaimarisha kitu nankukifanya kiwe ma nguvu zaidi. Nakubaliana na Robin Sharma aliyandika kuwa “ukitoa jasho jingi wakati wa mazoezi, utatoa damu kidogo wakati wa vita”.

    Mtu anakuwa shujaa baada ya kuwa amepitia katika vikwazo na kushinda. Kwenye hili Martin Luther King Jr anasisitiza kwa kusema hivi, “kipimo sahihi cha mtu sio pale anapokuwa amesimama wakati wa utulivu, bali pale anapokuwa amesimama baada ya changamoto na vikwazo”

    ANGALIA VIDEO HII YOUTUBE: Chuma Hunoa Chuma

    TATU, FAHAMU KUWA FURAHA YETU SIO KUTOSHINDWA
    Furaha yetu kubwa sana sio kutoshindwa, bali kuamka pale tunapoanguka. kwa hiyo mishale na mawe yanayokujia sio vitu vibaya. Bali vitu ambavyo vitakuongezea furaha pale utakapokuwa umeweza kuvivuka.

    leo ili uweze kuvijua. 



    Ni mimi anayejali mafanikio yako,
    GODIUS RWEYONGEZA

  • Kitu Kimoja Kitakachotokea Endapo Utakuwa Mlalamikaji

    Rafiki yangu hongera sana kwa siku hii ya leo na ya kipekee sana. Kama umekuwa mtu wa kulalamika leo kuna vitu viwili ambavyo huwa vinatokea pale mtu anapolalamika.
    Kwanza kabisa unapolalamika unakuwa unawaonesha watu wengine fursa ambazo wewe mwenyewe umeshindwa kuzitatua. Hivyo watu wengine wanaweza kutatua kurekebisha hicho kitu ambacho wewe mwenyewe unalalamikia. Ni wazi kwamba matatizo na changamoto ambazo mtu unakuwa unalalamikia ni fursa za watu wengine.
    Hata ukiiangalia historia yote. Ugunduzi wote ambao umefanyika, umefanyika ili kutatua matatizo ambayo yalikuwepo hapo awali.
    Biashara zote ambazo zimeanzishwa,  zimeanzishwa ili kutatua changamoto ambazo zilikuwpo hapo awali.
    Wajasiliamali wote na wafanyabiashara wote unaowafahamu, kazi iyao ni moja tu. kutatua matatizo.
    Kwa hiyo wewe unapolalamika ni wazi kwamba watu wa aina hii wataichukua hiyo changamoto na kuangalia namna ambavyo wanaweza kuitatua na ili waisaidie jamii. Ikumbukwe kwamba ujasiliamali ni kutatua matatizo ya watu.
    Kuanzia leo hii kitu chochote kile ambacho unaona unataka kulalamikia, nenda hatua ya ziada ili uweze kukibadili. kama huwezi kukibadili achana nacho.

    SOMA ZAIDI: Kama Tatizo Ni Nyota; Ya Kwako Imeenda Wapi?

  • Epuka Haya Makosa Matano (05) Wakati Unaanzisha Biashara

    kitabu hiki kipo kwa ajili yako. kinapatikana kwa shilingi elfu tano tu
    tuwasiliane kwa 0755848391


    Rafiki yangu, hongera sana kwa siku hii ya kipekee sana. Karibu sana kwenye makala ya leo ambapo ninaenda kukuonesha makosa matano ambayo unapaswa kuepuka kama kweli una mpango wa kuanzisha biashara, yenye mafanikio makubwa. ni vizuri uyafahamu haya makosa mapema, ili usije ukaanzisha biashara huku ukiona kwamba  hakuna mafanikio. Epuka makosa haya matano wakati unaanzisha biashara, ili uweze kuanzisha biashara yenye mafanikio makubwa.
    KOSA LA KWANZA; EPUKA KUKOPA ILI UANZISHE BIASHARA
    Hili ni kosa kubwa ambalo watu wengi wamekuwa wanafanya wakati wa kuanzisha biashara, watu wanakopesha pesa ili kuanzisha biashara. Nipende kukwambia ukweli rafiki yangu kwamba haupaswi kukopa ili uanzishe biashara. Badala yake unapaswa kuanza kujijengea utaratibu wa  kuweka akiba kwa kila pesa ambayo inapita mkononi mwako. Ujue pesa ambayo inapita mkononi mwako ni nyingi ila sasa wewe umekuwa hauweki nguvu katika kuhakikisha kwamba unatoa akiba yako na kuiweka pembeni ili akiba hii iweze kukusaidia katika kuja kuanzisha kitu cha tofauti hapo baadae.
    Siku hizi imekuwa ni rahisi sana kupata mkopo kutoka kwenye taasisi ambazo zinakopesha. Taasisi nyingine zitakufuata,  na kukuomba wewe uchukue fedha ya mkopo, ili uweze kuanzisha biashara. Usitumie kigezo cha kwamba unakopesheka kuchukua mkopo benki. Hata kama wewe ni mfanyakazi wa benki.
    Unapoanza biashara, kuna vitu vingi ambavyo unakuwa hujui mpaka pale utakapoingia kwenye biashara. Na biashara nyingi huwa hazisimami ndani ya siku moja. kwa hiyo utaanza kuhangaika katika kuhakikisha kwamba unaijenga biashara yako mwanzo, mwanzoni kabisa. na pengine utakuta kwamba fedha zaidi itakuwa inahitajika kwa ajili ya kuendesha biashara. Ambayo inakuwa ni fedha zaidi ya ile ya mwanzo.
    Sasa katika kipindi hiki hapa, ambapo wewe mwenyewe utakuwa unapigana katika kuhakikisha kwamba biashara yako imekaa vizuri, benki itakuwa inahitaji pesa ambayo walikukopesha. Unaweza kuanza kuona kwamba biashara ni chungu mwanzo, mwanzoni ila kumbe tatizo utakuwa umelisababisha wewe mwenyewe kwa kupuuzia maarifa haya muhimu.
    Hivyo kama ambavyo nimekwambia hapo awali. Anza. kuweka akiba sasa hivi ili akiba hiyo ije kukusaidia kuanzisha biashara kubwa.
    Au anzisha biashara ndogo kwanza ambayo haihitaji mtaji mkubwa kwanza, ili upate fedha kutoka huko ambayo itakusaidia kuanzisha biashara kubwa
    Au anza biashara kubwa kwa kuanza kidogo kidogo.
    Hivyo ndivyo unaweza kuepuka kosa la kwanza kabisa ambalo watu wanafanya kwenye biashara rafiki yangu mpendwa.
    KOSA LA PILI NI KUKOSA JINA LA BIASHARA
    Hili ni kosa jingine ambalo watu wanafanya wanapoanzisha biashara. Yaani, unaanzisha biashara yako bila ya kuipa jina. Kiukweli rafiki yangu naomba usije ukafanya kosa hili hapa. ujue vitu vyote hapa duniani vinapewa majina.
    Mtoto akizaliwa tu anapewa jina. Nchi zote zina majina, ndege zina majina, hadi pikipiki zina majina. Sasa kwa nini wewe ukose jina la biashara yako? Tena kibaya zaidi ni pale ambapo unakuta kwamba wewe una mbwa ambaye ana jina, ila biashara yako haina jina. Kwa hiyo nakuomba sana ujitahidi katika kuhakikisha kwamba biashara yako inakuwa na jina kabisa. jina la biashara linapaswa kuendana na aina ya biashara ambayo unafanya. Kwa maelezo zaidi kuhusu jina la biashara, basi usisite kusoma kitabu changu cha MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA  WA KUANZISHA BIASHARA. Kitakufaa sana. Tuwasiliane kwa simu 0755848391
    TATU, EPUKA KUANZISHA BIASHARA KWA SABABU KILA MTU AMEANZISHA HIYO BIASHARA
    Usianzishe biashara kwa sababu kila mmoja unaona anakimbizana na hiyo biashara. Au kwa sababu kila mtu anasema  kwamba inalipa basi na wewe unakimbia kufanya biashara hiyo hiyo. Ni wazi kwamba hii biashara, haitakuwa biashara yako.
    Kitu hiki kitakuepusha wazi wazi na makosa ambayo watu huwa wanafanya kwa kujirundika sehemu moja na aina moja ya biashara. Kiukweli wewe hapo haupaswi kutengeneza ushidani usio wa lazima. Yaani, kama unaona biashara imeanzishwa, na wewe huoni kama unaweza kufanya kitu cha tofauti ambacho kitakupa upenyo basi usitengeneze ushindani usio wa lazima.
    Ila kama unaona kwamba unaweza kutengeneza upenyo wako wa kipekee sana, kwa kujitofautisha, basi unaweza kuendelea mbele na kufanya hivyo.
    NNE, USIANZISHE BIASHARA NA KUJISHIKIZA KWENYE HIYO BIASHARA
    Rafiki yangu, kunapaswa kuwa na utofauti kati yako wewe hapo na biashara. Na hapa ndipo watu wengi wamekuwa wanakosea sana.  Yaani yeye na biashara wanakuwa kitu kimoja. Pesa yake na pesa ya biashara havieleweki. Yeye anatoa pesa  hapa na kutumia kwa kisingizio kwamba biashara ni yake. Na wakati huo huo akitaka kufanya kufanya manunuzi ya biashara anatoa pesa humohumo.
    Hili ni kosa kubwa. Kunapaswa kuwepo na mtari kati yako wewe na bishara. Wewe ujue ukomo wako na biashara iwe na sehemu yake ya kujtawala.  Naomba ufahamu kwamba wewe sio biashara. Ndio maana biashara tayari umeipa jina lake la tofauti kabisa. wewe hapo una mahitaji yako ya msingi ambayo kama utayapata basi utaendelea kuishi na ukiyakosa utakufa. Biashara pia ina mahitaji yake ya msingi, ambayo kama itayapata basi itaendelea kukua, na yakikosa basi itakufa.
    Biashara ina mzunguko wake kama wewe ulivyo na mzunguko wa damu. Kwa hiyo  wewe ukijitofautisha na biashara itapendeza.
    TANO, KUKOSA MAONO MAKUBWA,
    Rafiki yangu, biashara inahitaji maono makubwa wakati inaanza. Yaani, unapaswa kujua kwamba unafanya hiyo biashara ukiwa unaelekea wapi. Na unataka kufika wapi. Kitu hiki hapa kitakusaidia sana hata kwa maamuzi unayofanya, maana yatakuwa ni maamuzi ya msingi na ambayo yanajulikana yanaenda wapi. Ila kama unafanya biashara tu kwa sababu unataka upate pesa kesho au kesho kutwa. Basi utajikuta kwamba unafanya makosa makubwa kwenye maamuzi, ambayo kwa muda mrefu yatakugharimu sana.
    Rafiki yangu, hayo ndio makosa makubwa matano ambayo leo nilipenda uyafahamu na kuhakikisha kwamba umeyaepuka. Kiukweli kama utaepuka makosa haya utaweza kuanzisha biashara yenye mafanikio makubwa sana. Napenda sana usemi wa Robert Kiyosaki anayesema kwamba, biashara yenye mafikio inaanza kabla ya biashara yenyewe kabisa. hii ndio kusema kwamba kabla biashara haijaanza basi kwenye akili yako tayari unakuwa umetengeneza biashara yenye mafanikio makubwa sana.
    Basi, basi rafiki yangu, nenda kaweke katika matendo haya ammbayo umejifunza hapa ili uweze kupata matokeo mazuri sana.
    ASANTE SANA, TUKUTANE KWENYE JUKWAA LA WANAMFANIKIO.
    NI MIMI ANAYEJALI MAFANIKIO YAKO,
    GODIUS RWEYONGEZA
    075584839, lakini pia napenda nikwambie kitu kimoja cha mwisho. Ebu jiunge na mfumo wetu wa kupokea makala kwenye barua pepe leo kwa kubonyeza HAPA

  • BADILI MAJI KUWA DIVAI: Jinsi Ya Kuona Fursa Katika Changamoto Unazokutana Nazo Masihani

    Nimeona niseme hiki kitu, ili usije kusema kwamba sikusema.
    Usije kusema kwamba sikusema kwamba fikra zako ndizo zinazalisha matokeo unayopata.
    Watu wawili wanaweza kuwa wanapitia katika hali  ileile, ila mmoja akawa ameiona kama fursa ya yeye kusonga mbele. Wakati mwingine akaona kwamba ni kikwazo. Mmoja akaona kwamba ni upenyo wake wa kufanya makubwa mwingine akaona kwamba huo ndio mwisho wake na hapo hataweza kutoboa.
    Ujue matatizo huwa yanafanya baadhi ya watu wanavunje rekodi na wengine kuvunjika. Sasa wewe upo upande gani? Upande wa kuvunja rekodi au kuvunjika?
    Iko hivi watu wawili wanaweza kuwa wanapitia katika hali moja ila mmoja akawa amepata funzo na kulifanyia kazi na kupata matokeo makubwa na mwingiine anaweza kuona kwamba huo ndio mwisho wake wa kufanya  hicho kitu, hivyo kuishia hapo. Ndio maana nikasema kwamba matatizo huwa yanawafanya baadhi ya watu wanavunja rekodi na wengine wanavunjika.

    Kuna vijana wawili ambao walilelewa baba mmoja ambaye alikuwa mlevi. Vijana hawa walikuwa wanateswa na baba yao kila alipokuwa anarudi kutoka kunywa pombe.  Walipokuwa watu wazima kijana mmoja akawa mfanyabiashara na mwingine akawa mlevi. Siku moja mwandishi wa habari alitaka kujua ni kitu gani kilimsukuma kila mmoja kuwa jinsi alivyo.
    Mwandishi wa habari, alimfuata kijana yule mfanyabiashara na kumwuliza, “hivi ni kitu gani ambacho kimekusukuma na kuwa mfanyabiashara” kijana yule mfanyabiashara alijibu na kusema, “ NI BABA YANGU”. Kijana yule alijibu kwa kuendelea kusema kwamba, “nilipoona kwamba baba yangu analewa nikaona kwamba hayo sio maisha ambayo binafsi ninapaswa kuishi, niliona kwamba ninapaswa kubadili maisha ambayo ninasihi. Na hivyo nikaona kwamba ni vyema niihudumie jamii kwa kufanya kitu ambacho kitaongeza thamani kwa jamii”
    Kijana yule aliendelea kwa kusema kwamba, “ nilipokuwa mdogo niliona baba yangu akipeleka pesa nyingi kwenye baa kwa ajili ya kunywa pombe, na wale wamiliki wa baa walikuwa wafanyabiashara ambao kipato chao kilikuwa kinaongezeka kila siku, kila  mwezi, na kila mwaka. Wakati sisi nyumbani tulikuwa tunakosa hata pesa ya kula, hivyo nikaona kwamba katika maisha nitapaswa kuwa mfanyabiashara ili niweze kukusanya pesa za watu wngine na kuzivuta kwangu” hivyo ndivyo alimalizia maongezi yake kijana mfanyabiashara.
    Baada ya maongezi hayo mwandishi alimfuata kijana ambaye mwingine ambaye alikuwa mlevi. Mwandishi alimuuliza swali kama lile ambalo alimuuliza kiijana wa kwanza. Alimuuliza hivi, “ ni kitu gani kilikusukuma wewe kuwa mlevi”?
    Kijana yule mlevi alijibu na kusema kwamba, “ NI BABA YANGU” . alisema kwamba nilipokuwa mdogo nilimwona baba yangu akiwa analewa na hivyo mpaka leo ninajua kwamba maisha ni juu ya ulevi tu hakuna kitu kingine. Alimalizia hivyo kijana mlevi.
    Kwa hiyo unaweza kuona kwamba mazingira ya aina hiyo hiyo yanavyoweza kuzalisha watu wa aina tofauti tofauti. Mazingira yale yale yanaweza kumfanya mtu mmoja avunje rekodi na mwingine kuvunjika. Je, wewe upo upande gani?
    Siku zote unapaswa kuwa upande wa kuvunja rekodi. Na hapa ninaenda kukupa mbinu za kukusaidia wewe kuvunja rekodi badala ya kuvunjika kwa sababu ya hicho kitu ambacho kinatokea kwenye maisha  yako.
    KWANZA; KABISA KUWA MTU WAKUONA CHANYA KWENYE HASI

    Ngoja nikwambie kitu rafiki yangu, nyakati ngumu kwenye maisha huwa haziishi. Ila sasa ni juu yako wewe kuona ni namna gani unazitumia nyakati hizi katika kuhakikisha kwamba unasonga mbele.
    Kwa kila baya au gumu ambalo litakutokea maishani mwako, angalia ni kwa namna gani utaweza kuona fursa kwenye hilo baya ambalo unaona au kukutana nalo maishani.  Usiliangalie tatizo kama tatizo. Badala yake angalia fursa ambazo unaweza kuziona kutokana na hilo tatizo ambalo unakkutana nalo kwa wakati husika.
    Hivi kwa mfano wewe mvua ikinyesha unaona. Unaona kwamba imekukwamisha kufanya mambo yako, au ndio unaona kwamba ni fursa ya wewe kufanya kitu kikubwa zaidi.

    Naipenda sana hadithi ya mwalimu mmoja ambaye alikuwa anafundisha chuo. Huyu mwalimu alizoea kuona chanya kwenye kila kitu ambacho kilikuwa kinatokea maishani mwake. Sasa siku hii mvua kubwa kweli ilikuwa inayesha huku ikiwa imeammbatana na radi, ngurumo  na upepo mkali. Wanafunzi wote darasani walikuwa wamekaa kimya na wengine walidhani kwa sababu ya hali ya hewa basi inawezekana huyo mwalimu asitokee kabisa darasani. Lakini mwalimu alitokea kwa wakati na kila mwanafunzi alikuwa na shauku ya kusikia huyo mwalimu siku hiyo atasemaje? Maana walizoea kwamba kila jambo baya kwake huwa lina uzuri au ya kufanyia kazi. Lakini leo angesemaje? Maana mvua kali iliyoambatana na radi na ngurumo pamoja na upepo mkali vilikuwa vinaendelea kwa wakati huho. Hivyo kila mwanafunzi alikaa chini kwa shauku kubwa sana akitaka kusikia maneno ya mwalimu wake.
    Mwalimu alipongia darasani alitabasamu sana na kisha akasema, “ tumshukuru Mungu, maana siku kama hii huwa hazijitokezi maishani”.
    Mwalimu huyu hapa alikuwa ni mtu ambaye anaona chanya katika jambo ambalo ni hasi maishani. Alikuwa anaona chanya hata ambapo watu wengine wote walikuwa wanaona kwamba haiwezekani.
    Je, wewe huwa unaona nini katika changamoto ambazo unakutana nazo maishani mwako?
    PILI; FANYIA KAZI KILE AMBACHO UNAONA KWAMBA UNAWEZA KUBADILI KWA SASA HIVI

    Kuna magumu au mambo mabaya ambayo yanaweza kuwa yanakukumba wewe au jamii. Lakini yanaaweza kuanza kupatiwa suluhisho mara moja. Na mtu wa kufanya hivyo ni wewe mwenyewe wala sio mtu mwingine.
    Ebu tuseme kwamba jamii yako inapata shida ya maji. Wewe utafanyaje? Utalalamika au utasubiri serikali ije ilete maji?  Ukiangalia kwa jicho la kipekee unaweza kuona kwamba kuna kitu ambacho unaweza kubadili hapa. unaweza kutatua tatizo la watu kwa kutafuta namna ya kuwaletea maji karibu lakini pia wewe mwenyewe ukapata maji karibu. hivyo kwa kufaya hivyo ukakutakwamba umetatua tatizo na umetengeneza biashara ambayo inakuingizia kipato.
    Lakini ukiona tatizo la namna hii na wewe ukawa mtu wa kulalamika, basi ni wazi kwamba tatizo hili litakuvunja badala ya kukufanya uvunje rekodi.
    TATU, KUBALI KUBEBA MAJUMUKU YAKO

    Ujue kitu ambacho huwa kinafanya matatizo kuwa makubwa ni kwa sababu ya watu kutokubali kubeba majukumu yao. Watuwengi huwa wanapenda kuwabebesha watu wengine majukum. Watu wanakaa sehemu wakiwa wanaamini kwamba kuna mtu ambaye yupo sehemu fulani na huyo ndiye anahusika na kuwafanya wao waweze kuwa watu wenye furaha. Huyo ndiye anahusika kuwapa afya njema na kuwapatia kila kitu.
    Kuanzia leo hii, wewe ukikutana na hali au jambo ambalo unaona kwamba linakukwamisha, basi ona ni kwa namna gani wewe umesababisha hilo tatizo . ona ni kwa jinsi gani wewe umeweza kujiingiza kwenye hilo tatizo. Anza kutafuta namna ya kukutoa kwenye hilo tatizo.
    Ukigundua kwamba unaangamia basia kinachofuata inakuwa ni kwamba
    NNE; ANZA KUFANYIA KAZI FURSA UNAYOIONA KWENYE TATIZO

    Haitoshi tu kwako kuona fursa kwenye kitu. Au kuona kitu chanya. Bali hicho kitu chanya unapaswa kukiweka katika vitendo na kuhakikisha kwamba unakifanyia kazi katika kuleta matokeo chanya.
    Rafiki yangu, siku ya leo nimeona wazi kwamba ninapaswa kukushirikisha haya nilyojifunza ili na wewe uweze kunufaika na matatizo badala ya kukaa ukilalamika kwa changamoto au matatizo ambayo unakutana nayo kila siku.
    Endelea kutembelea blogu hii hapa kila siku. Lakini pia
    Usikose kujiunga na mfumo wetu wa makala MAALUMU KWA WATU MAALUMU ambazo huwa zinatumwa kwa baru pepe. Bonyeza hapa ili kujiunga.
    Umekuwa name anayejali mafanikio yako,
    Godius Rweyongeza
    Unaweza kuwasiliana nami kwa 0755848391
    JIUNGE NA KUNDI LA THINK BIG FOR AFRICA ili uweze kupata mafunzo zaidi ya kukufanya usonge mbele.

    Soma Zaidi Hapa THINK BIG FOR AFRICA

X