-
Mambo 20 Ya Kufanya Kwa Siku 340 Zilizobaki Kabla Mwaka Huu Kuisha
Siku ya leo sitaki niandike sana, ila hapa kuna mambo 20 ambayo unapaswa kufanya kwa siku 340 zilizobaki ili kuufanya mwaka huu kuwa mwaka wa mafanikio makubwa sana.
1. Hakikisha unakuwa na notebook ambapo kila siku utaangalia mwenendo wako. huku utaandika mambo yako unayofanya kila siku. Hii pia itakupa urahisi wa kujifanyia tathimini kila mwisho wa mwezi.
2. Walau mara moja kwa wiki fanya kitu ambacho unaogopa kufanya.
3. Anzisha biashara ambayo umekuwa unafikiri kwa siku nyingi sana kuanzisha ila hujawahi kuanzisha.
3. Soma kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI (hard copy)
4. Angalia video ya uzinduzi wa iphone mwaka 2007 ya Steve Jobs.
5. Washukuru watu ambao wanakusaidia kusonga mbele. Hata kama ni kwa hatua chache.
6. Tembelea Songambele blog kila siku. (www.songambeleblog.blogspot.com
7. Soma kitabu cha YUSUFU, NINA NDOTO cha Edius Katamugora.
8. Tembelea youtube channel ya GODIUS RWEYONGEZA kujifunza masomo mbalimbali. https://youtu.be/ZK5iBKkIdp0
9. Usipitishe siku bila kusikikiza muziki unaoupenda.
10. Tumia kanuni ya pomodoro kwenye kazi zako za kila siku.
11. Usianze siku yako kwa kutumia simu na wala usimalize siku yako kwa kutumia simu. Anza na malengo yako, maliza na malengo yako.
12. Nenda kwenye channel Ya LAZARO SAMWELI uangalie video zake kila siku.
13. Wafanye wengine wafanikiwe badala ya kutaka, ufanikiwe peke yako.
14. Angalia video ya STEVE JOBS akiwa chuo kikuu cha Stanford.
15. Weka biashara yako mtandaoni.
16. Tabasamu, tabasamu. Ebu tabasamu sasa hivi.
17. Usizuie vitu vinavyotokea kwa asili kutokea. Mfano usizuie kucheka pale unapopaswa kucheka.
18. Tembelea website ya Jacob Mushi.
19. Soma, kitabu cha Deo Kessy Cha Ongea Lugha Yako.
20. Jiandikie barua mara moja kwa mwezi kujipongeza kwa hatua ambazo umefanya ndani ya mwezi husika. Kwenye barua hiyo jiambie vitu ambavyo utapaswa kufanya ili ufanikiwe zaidi. Najua hujawahi kufanya hivi ila ukifanya hivi mwezi huu, utashangaa. Naomba kwenye hili hapa ukimaliza kulifanya nitafute kwa namba yangu uniambie umejisikiaje baada ya kujiandikie barua.
NA KUMBUKA HAPA NAMAANISHA BARUA YA KUANDIKA KWA MKONO!!
21. Hudhuria walau semina moja kila mwezi. Semina ambayo itakufundisha kitu ukichokuwa hujui.
22. Kuwa tayari kulipa gharama, kuna gharama saba utapaswa kulipa mwaka huu ili ufanikiwe. Gharama hizi zote utazikuta kwenye kitabu cha TIMIZA NDOTO ZAKO. (Kama tayari umesubscribe kwenye channel ya GODIUS RWEYONGEZA) nitumie screen shot ikionesha umefanya hivyo ili nikupe zawadi ya kitabu hiki bure badala ya 5,000 ambayo ni gharama yake ya kawaida. Hii zawadi inadumu kwa maasa 6 tu kutoka sasa. Mwisho ni saa tisa mchana.
Usisahau pia kushare na wengine walau wawili unaowapenda.
Ni mimi ninayejali mafanikio yako.
Godius RweyongezaWhatsapp namba yangu ni hii hapa; 0755848391
Barua pepe; songambele.smb@gmail.com -
SHUKRANI ZANGU ZA KIPEKEE KWA MTU HUYU HAPA
Rafiki yangu, nitakuwa sio mtu mzuri sana kama sitatoa shukrani kwa watu ambao wananijali maishani mwangu. na leo hii mtu wa pekee ambaye ningependa kutoa shukrani hizi za kipekee kwake mi WEWE.Kiukweli napenda sana kukushukuru kwa sapoti yako kubwa. Bila shaka kama wewe usingekuwa unasoma makala hizi kwenye hii blogu na mitandao mingine ambayo ninaweka makala basi kazi yangu ingekosa maana. Hivyo nipende kukushuru sana.Pamoja na shukrani zangu, siku ya leo nina taarifa MOJA muhimu kwako.TAARIFA HII ni kwamba kuanzia leo nitakuwa nakuwekea video nzuri sana kwenye mtandao wa you tube. Video hizi zitakuwa zinakujia kila siku.
kwa mwezi wa pili nategema kukuweka mpaka video 25 kwenye channel yangu. Video hizi hazitakuwa na urefu maalumu, ila ni ukweli kwamba zitakuwa na somo muhimu na hatua za kuchukua kwako. Hivyo kaa mkao wa kula.Cha kufanya sasa hivi, ingia youtube, uangalie video hii hapa, https://youtu.be/ZK5iBKkIdp0
kisha uhakikishe UNASUBSCRIBE na kuobonyeza kitufe cha kengele. Kitu hiki kitakuwezesha kupata taarifa za video mpya tunazotoa ili uwe unazipata mapema. -
Pesa zako zimelala hapa tu! Fanya Haraka Uzichukue Kabla Hazijachuliwa
Kwa kila sekunde inayopita, mtandao wa google unapokea maombi 40,000. Hawa ni watu mbalimbali wanaotafuta majibu ya maswali yao kwenye mtandao huu.
KWA NINI WATU WANATAFUTA MAJIBU GOOGLE?Moja ni kwa sababu majibu waliyonayo hayatoshelezi hivyo wanatafuta suluhisho jipya.Pili, kwa sababu hawajawahi kupata suluhisho la swali hilo kabisa maishani mwao. Hivyo njia pekee ni kukimbilia Google kuona kama kuna mtu ambaye anweza kutoa suluhisho.SASA HILI LINA MAA GANI KWAKO?
Hii maana yake kwamba, ukiweza kujibu swali moja tu kati ya hayo 40,000 ambayo yanaulizwa kila sekunde basi utakuwa umeweza kuwasaidia watu kupata kile WANACHOTAKA.Na kumbuka kwamba, unaweza kupata kitu chochote unachotaka kama utawasaidia watu kupata kile WANACHOTAKA.Wewe, hapo ulipo umebeba majibu ya maswali ya baadhi ya watu. Kwa nini hutaki kuyatoa ili uwasaidie.Ebu chukua hatua leo uanze kujibu walau swali la mtu mmoja kuanzia siku hii ya leo.USIBANIE HAYO MAJIBU UMEPEWA WEWE KWA AJILI YANGU. Nisaidie mimi kujibu maswali yangu ili nikulipe.Asante Sana.Kitabu hicho unachokiona kwenye picha ni nakala tete (soft copy), na kinapatikana kwa 5,000 tu. Kichukue leo ili kikupe msingi wa kuanzisha kitu kitakachotoa majibu ya maswali ya watu.Lipia kwa nambari 0755848391 jina Godius Rweyongeza Kisha nitumie ujumbe wenye neno BIASHARA ili nikutumie kitabuUsisahau pia kuingia YouTube Leo na kuangalia video hii yenye masomo matatu ya kibiashara. https://youtu.be/GuLZ97G34bQKaribu sana -
HIVI NDIVYO UNAWEZA KUTENGENEZA BAHATI YAKO MILELE NA MILELE
(utashangaa kwa nini ulichelewa kujua hiki kitu)
Rafiki yangu hongera sana kwa siku hii ya kipekee sana. Leo hii naenda kukufundisha namna ya kutengeneza bahati maishani mwako.
Na njia hii ya kutengeneza bahati ni kuwasaidia watu zaidi kupata bahati. Ukiwasaidia watu kupata wanachotaka utakuwa umewawezesha kupata bahati. Na kwa kuwa hili utakuwa umefanya jambo jema sana basi watu hao baadae watakuwa tayari kukulipa kwa kile unachofanya.
Wanaweza wasikulipe leo. Ila kadri utakavyokuwa unaendelea kuwasaidia watu wengi zaidi basi ujue kwamba watu hao pia watakuwa tayari kukulipa kwa kazi ambayo utakuwa unafanya
Hivyo kuanzia sasa hivi ninapoongea na wewe, anza kutengeneza bahati kwa kuwasaidia watu zaidi waweze kupata kitu ambacho wanataka. Sasa nikuulize, unaenda kuwasaidiaje watu? Utawapa nini?
Naomba uchukue muda kutafakari. Kama Unaweza kunishirikisha kile ambacho unaenda kuwasaidia watu kwa kutuma ujumbe wako hapa. https://wa.me/255755848391
kama pia hujajua namnanunavyoweza kutengeneza bahati za watu wengine basi na wewe nitumie ujumbe wako hapa
https://wa.me/255755848391Nikutakie siku njema
Ni mimi Rafiki wako wa Ukweli Godius Rweyongeza
-
Hiki Ni Kioo Kitakachokuonesha Kiuhalisia Wapi Utakuwa Miaka Mitano Ijayo. KIOO HAKIDANGANYI
Miaka mitano ijayo utakuwa jinsi ulivyo isipokuwa kwa vitu viwili tu! watu unaokutana nao pamoja na vitabu unavyosoma.
Sasa swali langu kwako ni je, leo hii unasoma vitabu gani? Je, leo hii unaambatana na watu gani?
vitabu unavyosoma vina uwezo wa kubadilisha maisha yako kwa kukupa aina mpya ya maarifa ambayo hukutegemea. vina uwezo wa kukuinua na kukufanya uzidi kusonga mbele kwa hiyo unapaswa kuamua haswa kusoma vitabu ambavyo vitakujenga haswa wewe na kukufanya uzidi kusonga mbele.
pia amua kuambatana na watu ambao watakupa motisha ya kusongambele. sio wale wanaokukatisha tamaa na kuona haiwezekani kwenye kila kitu unachofanya.
kuna video nzuri nimekuandalia kwenye mtandao wa Yourube. unaweza kuendelea kujifunza zaidi kuhusu saikolojia hii ya kipekee sana.
https://youtu.be/LrBROehGr64
👆usisahau KUSUBSCRIBE ili uendelee kuwa wa kwanza kupata video nzuri zaidi kutoka kwangu
haya twende👇
https://youtu.be/LrBROehGr64
-
Ukiona unavutwa nyuma zaidi basi jua kwamba ukiachiwa ndio utakimbia kam upepo
Changamoto na vikwazo huwa havikosi kujitokez kwenye maisha. Tofauti ni ukubwa wa changamoto ambayo mtu huwa anakutana nayo. Sasa changamoto yako inapokuwa kubwa usikate tamaa na kuacha kufanya kile kitu ambacho unapasawa kkuwa unafanya. Unapasawa kujua kwamba kadri unavyokutana na changamoto kubwa kwenye maisha yako basi ujue kwamba ukishaitatua hiyo changamoto utasongambele kwa kasi kubwa sana. Na kadri unavyokuwa na changamoto kubwa ndivyo utaweza kusonga mbele zaidi.
Kadri changamoto zinavyokuvuta nyuma zaidi fahamu kwamba ukianza kutoka huko nyuma na kuchomoka. Basi utakimbia kama upepo. Hivyo endelea kushikilia hapo hapo uliposhikilia kila siku. Weka juhudi. Ila fahamu ukitoka huko nyuma, watu wengine watakuona ukivuka ng,ambo.
Zimebaki siku 2 tu ambapo utaweza kupata vitabu vyangu vyote kwa 20,000. Ikiwa ni zawadi yangu kwako ndani ya mwaka huu 2020. Lipia sasa hivi kupitia 0755848391 jina Godius Rweyongeza kisha nitumie ujumbe wenye jina lako.
Kama una kitabu kimoja kati hivyo utalipia elfu 16 tu. kama una zaidi ya kimoja na ungependa kupata vilivyobaki wasiliana namikupitia 0755848391
-
masomo matatu ya kibiashara ambayo hujawahi kufundishwa sehemu nyingine
habari ya siku hii njema sana rafiki yangu. katika maisha huwa ni rahisi sana kukutana na changamoto ya kuchekwa na kususiwa na watu, hasa pale ambapo wewe utaamua kutumia vipaji vyako na kutimiza ndoto zako.
Leo nimeakuandalia video yenye masomo matatu makkubwa ya kibiashara ambayo unaweza kujifunza na kukyafanyia kazi mara moja. sikilize hapa chini. usishau kusubsceibe ba kukomenti kwenye hiyo video. karibu sana.
-
Hii Makala Ni Kwa Watu Wenye Kiu Ya Kufikia Mafanikio Makubwa Tu
Habari ya siku hii njema sana rafiki yangu. Nichukuke nafasi hii kukupongeza kwa siku kuuu ya krismasi, jana. Nichukue tena nafasi hii kukutakia siku kuu njema sana kufungua vifurushi leo.Sasa leo hii nimekuandalia makala wewe tu mwenye kiu kubwa ya mafanikio.Rafiki yangu kama wewe ni mtu mwenye kiu kkubwa sana ya kufikia mafanikio makubwa basi siku ya leo ningependa ujiunga na mfumo wangu huu wa kupokea makala maalumu kwa watu maalumu ili niwe nakutumia makala ambzo ni za kipekee na ambazo zitakufanya uweze kufikia mafanikio makubwa sana maishani mwako. Hivyo basi kitu cha kufanya sasa hivi bonyeza hapa
https://blogspot.us14.list-manage.com/subscribe?u=35d404174ee6b730531b8d920&id=7ff0bfcfcaHapa nitakuwa nakutumia makala maalumu ambazo huwezi kuzipata sehemu nyingine rafiki yangu. Kwa kusema hayo naomba nikutakie siku njema sana ya kufungua vifurushi,Kila la kheriMakala hii imeandikwa na Godius RweyongezaUnaweza kuwasiliana naye kupitia nambari ya simu 0755848391,Unaweza pia kunitumia barua pepe kupitia songambele.smb@gmail.com -
Salamu Za Krismasi Kutoka Kwa Godius Rweyongeza
Habari ya leo. Nichukue nafasi kukutakia kheri ya sikukuu za Krismasi na mwaka mpya.
Kwa mwaka mpya 2020. Kuna Mambo haya nisingependa uyakose.
1. Kwanza kabisa nisingependa ukose kupata kitabu kimoja cha kiswahili kila mwezi kwa njia ya (PDF).
Kwa sababu nathamini mafanikio yako, basi nitahakaikisha nakuandalia kimoja na kukupa kila mwezi. Wewe mwenyewe utakipenda na ukifanyia kazi unachosoma. Basi utazidi kusongambele2. Sipendi ukose kutapata masomo mapya ambayo huwezi kuyapata sehemu nyingine, pamoja na chambuzi za vitabu kila siku.
Hivyo inaenda kukuandalia pia hivi vitu. Labda ushindwe wewe tu.
3. Nisingependa ukose mjadala mzuri wa kila siku jioni. Ambapo mimi nitakuwa naanzisha huo mjadala kwa kutoa mambo niliyojifunza ndani ya siku husika.
Haya yatakuwa ni Mambo mawili au zaidi ambayo na wewe unaweza kuyafanyia kazi na kuboresha maisha yako kuanzia unapoyasoma au kesho yake.
Na wewe utatushirikisha ya kwako uliyojifunza ndani ya siku husika na wengine watafanya hivyo.
4. Pia nisingependa ukose darasa moja maalumu ambalo linatolewa kila wiki.
Ili uweze kupata hayo yote utapaswa kuwa kwenye kundi la think big for Africa. Na utalipia ada kidogo tu ya 2000/- kwa mwezi mmoja.
Ambayo ni sawa na 10,000 kwa miezi mitano. Je, ni kweli utaamua kujikwamisha mwenyewe?
Ebu amua kulipia hiyo gharama Leo kupitia 0755848391 jina Godius Rweyongeza Kisha nitumie ujumbe mfupi ili nikuunge kwenye kundi.JIUNGE NA THINK BIG FOR AFRICA ndani ya mwaka 2020. Utaona kwa nini 2020 haitakuwa sawa na 2020.
Imeandikwa na Godius Rweyongeza
-
JAMANI NIACHENI NISEME KITU HIKI KIMOJA SIKU YA LEO. YATAKAYOBAKI TUTAONGEA KESHO
Leo hii ni siku njema sana. Kwanza nichukue muda huu kukutakia kheri sikuu ya krismasi na mwaka mpya. Baada ya kusema hayo naomba uniache sasa niseme kitu kimoja tu yatakayobaki tutaongea kesho.Najua tangu asubuhi umesikia mengi kutoka kwa watu ila kitu kimoja kitabadili maisha yako kabisa. Hivyo basi niache kabisa niseme hiki kitu kimoja tu, yatakayobaki tutaongea kesho.Kitu hiki sio kingine bali ni juu ya kitabu hiki ambacho naona kinaenda kubadili maisha yako kabisa. kitabu kitakachokupa mwongozo juu ya ndoto zako. Na kitabu hiki sio kingine bali ni kitabu cha YUSUFU, NINA NDOTONaomba uniache niendelee kidogo. Kuna kitu nataka kusema hapa. yatakayobaki tutaongea kesho.Kama ambavyo mwalimu anakuwa na kiongozi cha mwalimu wakati anafundisha wanafunzi naKama ambavyo mchungaji anakuwa na roho mtakatifu kumwongoza kwenye kazi zake za kichungaji naKama ambavyo mchezaji anakuwa na kocha wake wa kumfundisha mpiraKama ambavyo nyumba inakuwa na mhandisi wa kuijengaVivyo hivyo ndoto yako inahitaji kitabu hiki. Ndio ni kitabu cha YUSUFU NINA NDOTO.Ukiwa na kitabu hiki utapata kuona kwamba ndoto yako inawezekana kutimia bila kujali ukubwa wake. Bila kujali watu wanaikubali au wanaikataa, bila kujali kuwa una connection na watu wengine au la! Bila kujali umewahi kufanya makubwa au la! Ndio maana leo hii nilitaka nikwambie hiki kitu kimoja ili yatakayobaki tuongee kesho.’Kitabu hiki hapa kimeandikwa na mwandishi mahiri ambaye ni Edius Katamugora. Mwandishi huyu ambaye tayari alishatuandikia kitabu cha BARABARA YA MFANIKIO pamoja NA kitabu cha NMANA YA KUWA MTAALAMU UKIWA BADO UNASOMA. Sasa zamu hii tunapoanza mwaka mpya 2020 ameamua kutupa kitabu cha kipekee ambacho ni YUSUFU NINA NDOTO. Kitabu hiki ni kwa ajili yako wewe mwenye ndoto.SOMA ZAIDI: Hii Ni Barabara Ambayo Unaweza KuichukuaKikubwa zaidi ni kwamba kitabu hiki hapa kitaanza kupatikana kuanzia tarehe 11 januari 2020. Na hivyo ndivyo tutaufungua mwaka mpya. Kitabu hiki kitapatikana kwa shilingi 10,000 tu.Hii ni kweli ni zawadi ya mwaka mpya 2020. Na ndio maana niliona nikwambie kitu hiki kimoja tu ili mambo mengine yote yanayobaki tuje tuyaongee kesho.Rafiki yangu utapaswa kuweka koda ya kitabu hiki mapema iwezekanavyo.Cha kufanya sasa hivi1. chukua simu yako.2. mtafute mwenye namba hii hapa 0764145476. Ambaye ni Edius Katamugora.3. kisha lipia 10,000 tu. ili uweze kuwa miongoni mwa watu watakaopokea kitabu siku hiyo ya tarehe 11 saa 11 kabla jogoo hajawika.Soma Zaidi; Maajabu Ya kitabu Cha Barabara ya MafanikioWahaya wanasema anayekusaidia usiku huwa unamshukuru kukicha. Sasa ninachokwambia sasa hivi ni kitu ambacho najua wazi kitakuja kusaidia maisha yako. Ila shukrani pekee ninyotaka kutoka kwako ni kufanyia kazi utakayojifunza kwenye hicho kitabu. Ukishasoma mwambie na rafiki yako asome na kufanyia kazi.Nataka siku moja tukutane kwenye meza ya wanamafanikio kwa pamoja. Naamini siku hiyo tutaongea sana. Siku hiyo utaniambia ulivyosoma kitabu hiki kikabadili maisha yako.Hivyo weka oda yako leo hii ili tuje tukutane mwaka huo kwenye mzunguko wa wanamafanikio.Makala hii imeandikwa na GODIUS RWEYONGEZA






