Home


  • JE, TUJIFUNZE NINI KUTOKANA NA UZINDUZI WA CYBERTRUCK?

    Masomo matano ya kibiashara kutoka kwa Elon Musk na Kampuni yake ya Tesla

      Ni mwezi sasa umepita tangu Elon amezindua gari aina ya Cbyertruck ambayo imetegenezwa na kampuni yake ya Tesla. Cbertruck ni truck (pick up) ya kipekee tofauti na pickup za magari mengine ambazo umezoea kwa siku zote. Yaani Tesla wamekaa chini na kuja muundo  mpya kabisa .

    Siku ile ya uzinduzi watu walichanganyikiwa, maana aina ya gari waliloona linaingia ukumbini halikuwa sawa na lile ambalo wao walikuwa wanategemea kuona. Watu walidhani hiyo truck itakuwa ni sawa na pickup za makampuni mengine kama Ford na Toyota.
    Gari hilo ambalo halipitishi risasi (bulletproof) lilipigwa                      na nyundo siku ya maonesho na wala halikuonesha dalili zozote au alama yoyote  ya kukwanguliwa. Hata hivyo viooo vyake vilivunjika wakati wa maonesho baada ya kurushiwa chuma. Na hiki kilikuwa ni kinyume na watu walivyokuwa wanategemea.  Maana vioo vya gari pia ilitegemewa visikwanguliwe hata kidogo hata baada ya kurushiwa chuma.

    Baada ya uzinduzi w gari hilo kumekuwa na majadiliano makubwa kwenye mitandao ya kijamii. Sasa hivi ukiiiingia google na kuandika tesla cbyertruck unapata matokeo 46, 800,000. Hahah, milioni arobaini na sita laki nane!!!  Sasa leo hii ningependa tuongelee masomo muhimu ya kibiashara ambayo tunaweza kujifunza kutokana na uzinduzi huu wa gari hili la Tesla.

    MOJA, UKITENGENEZA KITU CHA KIPEKEE WATU WATAKIONGELEA TU
    Kama nilivyokwambia kwamba gari hili linaongelewa sana kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii.
    Wapo watu ambao wameonekana kupenda sana muundo huu mpya wa gari hili la Tesla, wakati wengine wakionekana kuwa hawajapenda. Mashirika mbali mbali yameonekana yakicchukua gari  hilo na kuweka logo zao na kuzitupia mtandaoni, kitu cha kipekee kinachofanya gari iongelewe zaidi ni swali ambalo watu wanajiuliza, kwanini vioo vya gari vilivunjika baada ya kurushiwa chuma?

    Somo kubwa la kibiashara ambalo napenda ujifunze kutokana na uzinduzi huu wa gari hili ni kuwa unapotengeneza kitu cha kipee basi watu lazima watakiongelea tu.

    Kwenye ulimwengu wa magari hakujatokea mabadiliko makubwa sana ya pickup tangu miaka ya Henry Ford. Karibia miundo inayotumika sasa hivi ni ile ile iliyokuwa inatumika miaka hiyo ya Henry Ford. Ila sasa Elon Musk amekuja na kitu cha kipekee. Na hivyo lazima watu wakiongelee.

    Elon Musk angeweza kutumia muundo ule ule kama wa pickup za kampuni megine kwa  kuweka mfumo wa umeme ndani yake tu. ila amekaa chini na kutengeneza kitu kipya kabisa ambacho ulimwengu haujawahi kuona.

    PILI, WATU WAKIONA KITU MARA YA KWANZA WATAKIKATAA, ILA WAKIJIHOJI TENA WATAONA NI KITU AMBACHO HAKIKWEPEKI
    Akili ya binadamu huwa inakuwa ngumu kupokea vitu vipya vinapotolewa. Na hili linaturudisha nyuma kidogo mpaka mwaka 2007, ilipozinduliwa iphone ya kwanza. Watu mwanzoni walionekana kuikataa maana ilikuwa imeenda kinyume na matarajio ya wengi. Wengi walikuwa tayari wamezoea simu zenye kibodi lakini sio hizo za ku pangusa na kidole.

    Lakini simu zilivyoingia sokoni kila mmoja akawa anahitaji moja ya wake.

    Sasa kitu hiki ndio nakiona kwa gari hii aina ya cybertruck ya Tesla. Siku ya uzinduzi ilionekana kama kituko kwa wengi ila sasa kila mmoja anakimbia kuweka oda yake ili awe miongoni mwa watu wa kwanza kupata hilo gari litakapotolewa.

    Elon musk mwenyewe anasema hilo ndilo gari ambalo litatumika siku zijazo.

    TATU, UNAPOAMUA KUFANYA KITU, USIIBE WATEJA. TENGENEZA SOKO JIPYA KABISA
    Kwa kitu alilchofanya Elon Musk sio kwamba anaenda kuiba wateja kidogo kutoka kwenye makampuni ya magari yaliyopo sasa hivi. Ila ametengeneza soko jipya kabisa ambalo halijawahi kuwepo.

    NNE, UKITENGENEZA KITU BORA ZAIDI WATU WATAKUSAIDIA KUTANGZA.
    Mpaka sasa hivi Elon Musk hajatoa hata senti moja kulitangaza gari lake kwa watu, ila watu wengi wanakimbilia kuweka oda. Hii inatoa picha ni kwa namna gani watu wanavyoshirikiana kutangaza hilo gari lake kwa wengine.

    TANO, UNAPOWAACHIA WATU NAFASI YA KUONGEA, UNAPATA KUJUA MENGI
    Baada ya vioo vya dirisha kupasuka kwenye maonesho. Sasa kila mmoja anajaribu k utafuta kwa nini vilipasuka. Gazeti la Forbes limeandika sababu kumi za kwa nini vioo hivyo vilipasuka. Hii ni kuonesha ni kwa namna gani watu wapo tayari kujieleza na jinsi unavyoweza kujifunza zaidi kutoka kw hawa watu.

    Elon Musk amewaachia watu nafasi ya kujieleza nina hakika maelezo haya ya watu anaenda kuyafanyia watu ili kuja na kitu kingine ambacho kitakuwa ni bora zaidi ya hapa.

    Rafiki yangu hayo ndio masomo matano ya kibiashara ya kujifunza kutokana na uzinduzi wa gari hii mpya aina ya cybertruck ilizinduliwa na kampuni ya Tesla mwezi uliopita.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
    Unaweza kuwasiliana na mwandishi kupitia barua pepe ya songambele.smb@gmail.com
    Unaweza pia kuwasiliana naye kupitia wasapu namba 0755848391 karibu sana.

    JIUNGE NA KUNDI LA THINK BIG FOR AFRICA LEO ILI UWEZE UKUJIFUNZA ZAIDI KUPITIA KUNDI HILO
    Gharama ya kujiunga na kundi ni 2000 tu kwa kila mwezi ambapo utaendelea kupata masomo kila siku na kitabu kimoja cha kiswahli kila mwezi. Utalipia hiyo gharama kupitia nambari ya simu ambayo ni 0755848391 jina ni Godius Rweyongeza. Baada ya kufanya malipo utanitumia ujumbe mfupi kupitia hiyo hiyo namba ili niweze kukuunga kwenye kundi. Karibu sana

  • Kama Hauna Hata Mia Mbovu Jua Unakosea Hapa

    Kuna misemo ambayo imezoeleka kutolewa na watu siku hizi kiasi kwamba imekuwa ni sehemu ya pili ya maisha ya hawa watu. Unakuta mtu anasema “usawa huu wa Magufuri pesa imekuwa ngumu sana”. Utasikia mwingine anasema “vyuma vimekaza” wakati mwingine akitaka kukwambia kuwa hana pesa basi utasikia akisema, “sina hata mia mbovu”. Yaani kumaanisha kuwa hana kitu kabisa mfukoni mwake.

    Ukifuatilia kwa umakini. Yaani kwa jicho la tai anayeuangalia mchezo kutokea juu angani na kutoa tathimini, unaona wazi kabisa kuwa suala la vyuma kukaza sio jambo la leo au jana.  Historia inaonesha kuwa katika kila nyakati kumekuwa na mambo kadha wa kadha ambayo yamekuwa yakitokea na kusababisha vyuma kukaza. Hata hivyo kitu kimoja kimebaki uhakika siku zote. Wale wanaotengeneza pesa siku zote huwa hawaoni kukaza kwa vyuma Kama tatizo. Badala yake huwa wanaona fursa kwenye hilo.

    Ngoja nikueleze kiundani suala hili ili uweze kunielewa. Kukaza kwa vyuma kama wanavyosema wengine maana yake Ni kutokuwepo kwa pesa. Sasa tujiulize ni kitu gani kinakufanya wewe ukose pesa?  Unaweza kuwalalamikia watu wote duniani Ila mwisho wa siku mtu anayesababisha kukaza kwa vyuma ni mmoja tu. Na mtu huyu ni wewe.  Hii unatokana na ukweli kwamba pesa inafuata mkondo kwa wale wanaoiita. Kama wewe hauiiti ije kwako haiwezi kuja, utapishana nayo njiani tu.

    Leo hii nataka nikuoneshe namna utakavyoiita pesa ije kwako na uendelee kuwa ya kwako milele na milele. Siku nyingine kabla hujasema pesa ni ngumu hakikisha unarudi hapa kusoma andiko hili ili uone Kama umelitendea haki. Ila kama utasoma hapa na kuishia tu kusema kuwa huyu jamaa anaandika vizuri basi mimi nakuhakikishia utaendelea kusema kuwa pesa ni ngumu. Kama utasoma hapa na kufanyia kazi ulichojifunza hapa, basi tutakutana sehemu siku moja ukifurahi kwa sababu ya kile ukichojifunza hapa siku ya leo.

    MOJA, KAMA PESA NI NGUMU MAANA YAKE HUJATOA HUDUMA KWA JAMII
    Zig Ziglar amewahi kusema kuwa utapata kitu chochote unachotaka kama utawasaidia watu kiasi cha kutosha kupata kile wanachokitaka. Kitu ambacho unapaswa kuelewa hapa ni kuwa kuna watu wananpesa zako mkononi mwao. Ila hizo pesa hazitakuja kwako kirahisi. Labda uwakabe (na ukifanya hivyo jela itakuwa rafiki yako). Ila njia pekee ya kuzitoa hizo pesa kwa watu na kuzileta kwako ni kuhakikisha kuwa una bidhaa ambayo unaweza kuwauzia hao watu. Hiki kitu ndicho Zig Ziglar anakiita kuwasaidia watu kupata WANACHOTAKA.
    Kuna watu wanahangaika kwa sababu huduma fulani hawaipati vizuri. Lakini wewe ukiweza kuwafikishia hiyo huduma kwa ustadi watakuwa tayari kukulipa na hiki ndicho Zig Ziglar anakiita kuwasaidia watu kupata WANACHOTAKA.
    Kuna watu hawajui kwamba wewe ni mtaalamu na umesomea ujuzi fulani chuoni. Sasa huo ujuzi ulilojifunza chuoni ukiweza kuutafsiri na kuuleta kwenye maisha yabm kawaida hapa mtaani. Ukautumia ujuzi huo kuwasaidia watu kupata kitu fulani ambacho unaona kitaalamu hakifanyiki vizuri. Hapo utakuwa umewasaidia watu kupata kitu wanachokitaka.

    Nikukumbushe kuwa pesa hazitakuja kwako Kama wewe utakuwa tu umelala afu unaishia kusema pesa ni ngumu au vyuma vimekaza. Pesa itakuja kwako pale ambapo utaamua kutatua matatizo ambayo jamii inakumbana nayo.
    Muuza maji hapati pesa kwa kuuza maji bali kwa kutatua tatizo lako la kiu.
    Mtu daladala hapati pesa kusafirisha abiria, bali kwa kutatua tatizo lako la kusafiri na kufika eneo husika mapema.
    Mitandao ya simu haipati pesa kwa kuuza vocha bali kwa kuunganisha na watu walio mbali na wewe.
    Wewe unatatua tatizo gani?

    Shida yako wewe imelala kwenye  haya maeneo mawili.
    Kwanza unaamini kuwa hakuna kitu kingine kipya unaweza kufanya kuondokana na hali hiyo uliyonayo. Yaani umejikatia tamaa mwenyewe. Nan kama umekata tamaa mwenyewe hata akitokea mtu akakupa mamilioni ya pesa hayatakusaidia. Cha kufanya inuka tena anza tena kupambana.

    Tatizo lako la pili, unaona kuwa haya ninavyoongea hapa yanawafaa wengine na sio wewe. Huchukui hata hatua ya kuanza, unabaki kusema tu haya yanawafaa watu wenye hela zao bana. Hivi unadhami hao unaosema wana hela zao walizaliwa nazo? Kuna wengine walikuwa na maisha mabaya pengine zaidi ya wewe. Kuna wengine walikuwa na madeni makubwa kuliko hata wewe hapo. Ila walisimama wabeba majukumu yao na Sasa unawaonea gere. Usipochukua hatua UTAJIJU.

    2. KAMA PESA NI NGUMU MAANA YAKE UNAWAHUDUMIA WATU KIDOGO
    Kiasi cha pesa unachoingiza kinaweza kuniambia ni idadi gani ya watu unaowahudumia. Kama unaingiza pesa kidogo maana yake UNAWAHUDUMIA WATU KIDOGO. Kama Kuna kiasi kikubwa unaingiza maana yake unawahudumia watu wengi. Hii wala hata sio hesabu ngumu kama unavyofikiria.

    Ebu tuseme wewe na Paulo mnauza maji. Paulo anawauzia watu 1000 na wewe unawauzia watu 100 kila siku na kipimo mnachitumia kuuza Ni kile kile unadahami atapata pesa zaidi?

    Ukiona pesa ni ngumu unapaswa kujua kuwa unawahudumia watu kidogo. Kama umeajiriwa ujue unafanya biashara na mteja mmoja tu ambaye Ni bosi wako. Sasa usitegemee ulipwe kwa viwango sawa na mtu ambaye anatoa huduma kwa wateja mia, elfu au laki moja.

    3. KAMA PESA NI NGUMU UJUE KUWA HUJAJUA MISINGI NA MIIKO YA PESA.
    Ni kawaida kuwa mwanasheria akienda chuoni lazima atafundishwa misingi ya sheria na miiko kwenye sheria. Daktari pia anafundushwa misingi na miiko. Mwajiriwa kazini ataambiwa Mambo anayopaswa kufanya kazini na yale anayopaswa kuepuka. Pesa pia ina misingi yake na miiko yake. Ukiona ni ngumu kwako basi ujue hii misingi hujaijua.
    Hujajua kuwa unapaswa kuweka akiba kwa kila kiasi unachopata
    Hujajua pia kuwa unapaswa kupunguza matumizi yako na kubaki na mtumizi ya lazima tu.
    Hujajua kuwa unapaswa kuanza kuwekeza ili pesa yako ikuzalie pesa zaidi.
    Hujajua kuwa haupaswi kutumia zaidi ya kipato chako.
    Hujajua pia kuwa haupaswi kukopa pesa ili utumie ili uje ulipe.
    Hujajua pia kuwa mtu akikuahidi pesa, haupaswi kuiweka kwenye hesabu zako mpaka utakapokuwa umeipokea mikononi mwako.

    Hiyo ndio misingi ya pesa miiko ya pesa.

    HITIMISHO.
    Naamini baada ya kuwa umesoma hapa, hutakuja kukosa mia mbovu kuanzia leo. Maana tayari unajua jinsi pesa inavyopatikana mpaka inavyotumika. Nikutakie kila la kheri.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza
    Unaweza kuwasiliana naye kupitia 075584891

  • Hivi Ndivyo Utaweza Kujifunza Lugha Mpya 2020 (Ukiamua kuitumia vizuri njia hii, mwakani watakusikia ukinena kwa lugha nyingine)

    Inawezekana umekuwa na mpango wa kujifunza lugha mpya kwa siku sasa, ila Kuna vitu vinakuzuia.
    1). Pengine unaona gharama za kuingia darasani ni kubwa.
    2). Majukumu yako ni mengi kiasi kwamba unaona huwezi kuyaacha kuanza kuhudhuria darasa jipya.
    3). Hujui wapi unapaswa kwenda kujifunza lugha mpya.
    Sasa leo hii napenda nikwambie wapi utaweza kujifunza lugha mpya 2020.  Njia hii ni kutumia app inayoitwa DUOLINGO.
    •   Njia hii haihitahitaji muda mwingi kutoka kwako. Yaani utahitaji dakika tano mpaka 15 kila siku.

    Na huu Ni muda ambao naamini kabisa huwezi kuukosa. Najua huu ndio muda ambao huwa unautumia ukiwa mitandaoni. Najua huu ndio muda ambao huwa unautumia kuangalia tamthiliya. Ila zamu hii tutaufanya uwe wenye manufaa kwako. Kwa muda huu utajifunza lugha mpya

    •   Njia hii pia haitahitaji gharama. Gharama kubwa utakayotumia ni kuhakikisha una kifurushi.

    Hiki najua sio shida kwako Kama umeweza kusoma hapa leo.

    • Kwa njia hii utaweza kujifunza   ukiwa nyumbani kwako, ofisini au hata safarini.

    Ninaamini kwa mwaka ujao, hutakosa hata siku moja ya kujifunza maana unaweza kujifunza ukiwa popote.
    TUONGEE KIDOGO KUHUSU DUOLINGO.
    Hii app unaweza kuipakua kwenye simu yako kutoka kwenye playstore au appstore. Ukishaipakua utaamua ni lugha gani unapenda kujifunza na utaanza Mara moja bila kuchelewa.
    Bila shaka unaona jinsi ilivyo rahisi.
    KITU KIMOJA KINACHOHUTAJIKA KUTOKA KWAKO KABLA HUJAPAKUA DUOLINGO.
    Ukiwa na Duolingo utaweza kuchagua lugha yoyote unavyopenda kujifunza. Lakini utapaswa kuwa unajua walau lugha ya KIINGEREZA.
    Hiki ni kitu kimoja na pekee kinachohitajika kutoka kwako.
    Naamini baada ya hapa utaenda kupakua app hii ya DUOLINGO kwenye simu yako
    Nitafurahi Kama utaniambia wewe unaenda kujifunza lugha gani 2020. Asante sana,
    Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.
    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
    Unaweza kuwasiliana na mwandishi kupitia namba 0755848391
     

  • Nakukumbusha Jukumu Lako Hiki Usije Ukasahau

    Kwenye dunia hii kila mmoja ana jukurmu lake. Kuna watu ambao jukumu lao ni kukosoa, kukatisha tamaa, na kukukwamisha.  Hawa watu utakutana nao katika safari yako. Ila kumbuka kwamba wao kazi yao waliyoichagua ni kukosoa.

    Ukiona mtu anakukosoa na kusema vibaya juu ya kile unachofanya, Jua kwamba yeye amechagua hiyo kazi. Hivyo wewe endelea na shughuli zako bila kujali anachosema.

    Kikubwa wewe kila mmoja atimiza majukumu take vizuri. Na wewe jukumu lako kubwa ni kuweka njia ili wengine waweze kufuata.

    Nakutakia siku njema sana.

  • NDUGU MZAZI; barua ya wazi kwa wazazi na walezi wote

    Ndugu mzazi: barua ya wazi kwa wazazi na walezi wote

    Unaweza kumpenda mtoto anayepata A darasani na kumchukia anayepata C au F. Lakini anayepata A darasani inawezekana asipate A maishani.
    Tujifunze kupenda watoto wote na kuwajali watoto wote kwa usawa.
    Ndugu wazazi A ya darasani haimaanishi maisha yatakuwa mazuri. Na maisha mtaani yalivyo hayapimwi kwa viwango vya A za darasani.
    Mwanao akienda benki hataulizwa kuonesha alipata A ngapi darasani. Benki wanachohitaji kuona ni je, ana pesa mkononi?
    Ndugu mzazi, mwanao akianzisha biashara au kufungua kampuni, hatatakiwa kuonesha A za darasani.
    Na hata akienda kukata tiketi ya ndege hawaulizi “tuoneshe A ya darasani ili tukukatie tiketi”. Wanachojali na WANACHOTAKA kuona ni Je mfuko unasoma?
    Ndugu mzazi kama kuna kitu cha muhimu unapaswa kumfundisha mtoto wako basi mfundishe umuhimu fedha. Mfundishe namna ya kutafuta fedha na namna ya kuzitumia.
    Mfundishe namna ya kuwekeza akiwa bado mdogo ni hazina kubwa ambayo ukimpa hatakusahau.
    Ndugu mzazi, sio kwamba nimesema usimpeleke mtoto wako shuleni. Na wala sijasema mtoto wako asisome ila napenda ufahamu kwamba maisha ni zaidi ya A za shuleni.
    Napenda ufahamu kwamba shuleni unafundishwa kusoma na kuandika. Ila maisha yanahitaji usome kweli na kuandika kweli kweli.

    ……………………………………………………………..Ndugu mzazi, usibaki tu kumwambia mtoto wako kwamba Kuna shetani. Ukiishia kusema hivyo utakuwa unalea kilaza. Mwambie kabisa kwamba anapokuwa amepanga kufanya majukumu yake ya siku na akawa hayajayafanya huyo ndiyo SHETANI mwenyewe.
    Mwambie akipokea elfu kumi na akaitumia yote ikaisha huyo ndiye SHETANI mwenyewe
    Mwambie akiishi maisha bila ya kuwa ndoto, kusudi wala malengo shetani anakuwa amemtawala.
    Mwambie akiamini kila kitu anachoambiwa bila kufikiri na kufikia uamuzi wake mwenyewe na huyo ni shetani pia.
    Mwambie akiishi chini ya viwango vyake huyo pia ni shetani anakuwa amemtawala.
    Mwambie akianza kitu na akaishia njiani huyo ndiye shetani mwenyewe.
    ………………………………………………………………Ndugu mzazi, kama umeajiri wafanyakazi wa ndani basi mwanao asibweteke tu na kukaa bila kufanya kazi. Itakuwa ni Jambo la ajabu mfanyakazi wa ndani akawa anafanya usafi wa ndani na mwanao yupo tu kwenye kochi ananyanyua miguu ili mfanyakazi afanye usafi.
    MAKALA ni ni sehemu ndogo sana ya kitabu. Kupata kitabu hiki hapa utalipia kiasi cha shinfi elfu mbilil tu. ukilipia elfu 2 utaunganisha na kundi la think big for Africa ikiwa ni pamoja na kupata kitabu hiki hapa cha kipekee sana.
    Lipia kwa namba 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA. Karibus sana

  • WHO MOVED MY CHEESE?

    🍕🍕🍕🍕🍕

    Huwa inatokea mara nyingi maishani kwamba watu wanashabikia na kupenda mabadiliko yatokee maishani Ila wao huwa  kusababisha mabadiliko hayo ni vuta nikuvute

    Huwa inaonekana vizuri kumshangilia KIONGOZI wa siasa ambaye  anahaidi kuwa mara tu baada ya kuingia madarakani atafanya mabadiliko moja, mbili na tatu

    Kitabu Cha WHO MOVED MY CHEESE kimezungumzia sana kuhusu mabadiliko ambayo huwa yanatokea kwenye jamii. Kwenye kitabu hiki ninaweza kusema kwamba watu wamewekwa kwenye makundi matatu linapoja suala la mabadiliko.

    Kundi la kwanza, Ni lile ambalo linajua kwamba lazima tu mabadiliko yatatokea na hivyo linajiandaa. Linajua tu ikitokea kuna mabadiliko yoyote yametokea basi na lenyewe litabadilika Mara moja na kuchukua hatua. Hili ni kundi la wale ambao wanajua kuwa maisha ni wajibu wao. Linajua kuwa kushinda na kushindwa ni wajibu wao .

    Watu walio kwenye kundi hili, kila mara huwa wanaofuatilia kujua Kama mabadiliko ambayo yameshaanza kutokea ili wasije kushangazwa na mabadiliko yoyote ambayo yametokea.

    Kundi la pili, ni la wale watu ambao huwa wanastukia mabadiliko yametokea ila hawajui mabadiliko haya yametokeaje. Wanashangaa tu kuona kitu fulani kinaendelea. Japo kundi hili huwa linabadilika baadae, lakini huwa linafanya hivyo kwa kuchelewa sana.

    Kundi la mwisho kabisa ni kundi la watu ambao wanaendelea kushikilia mila na na desturi na hawapo tayari kubadilika. Kiafrika afrika hawa ndio wale huwa wanasema mababu walikuwa wanafanya hivi na hivyo hatuwezi kubadili namna walivyokuwa wanafanya. Hawa ndio wale ambao huwa wanasema, haikuwahi kufanyika hivyo kabla. Yaani Hawa huwaambii kitu, wanashikilia kile kitu cha zamani kama msahafu.

    Kati ya hizo aina tatu zote, bila shaka kwa haraka unaweza kujua ni aina gani inafurahia sana maisha. Ni aina ya kwanza. Ila sasa kuwa kwenye kundi hili la kwanza ni vigumu sana.

       Ni vigumu kwa sababu watu watakusema ukiwa kwenye kundi hili.
       Ni Ni vigumu pia kwa sababu ya uoga.
        Ni vigumu kwa sababu ya marafiki ambao wanapenda tuendelee kufanya mambo kama yalivyokuwa yakifanyika hapo zamani.

     Hivyo inahitaji kujitoa ili uweze kuingia kwenye kundi la kwanza.

    Mwandishi Spencer kwenye kitabu chake cha WHO MOVED MY CHEESE? ametuahirikisha hadithi yenye funzo kubwa sana maishani mwetu.
    Hadithi hii inaanza kwa kuwakutanisha vijana waliokuwa marafiki wa ukweli chuoni. Sasa nu miaka michache baadae wamekutana kujadili juu ya mabadiliko na mmoja wa wale vijana anatoa hiyo hadithi ya WHO MOVED MY CHEESE? Hadithi hii imejaa mafunzo mwanzo mpaka mwisho Ila kikubwa zaidi kikiwa ni juu ya MABADILIKO.

    1. Kitu cha kwanza kutoka kwenye hiyo hadithi ni aina hizo tatu za watu, naomba wewe ujiulize upo kwenye kundi gani?

    2. Hivi ni kitu gani ungefanya kama usingekuwa na uwoga? Hili ni swali ambalo mmoja wa wahusika kwenye hadithi alijiuliza mara kwa mara, hasa pale alipokuwa anaogopa na kutaka kurudi nyuma.
    Kwa kujiuliza swali hilo aliamua kusongambele bila kuogopa na kufikia kuleta mabadiliko.

    3. Ukiogopa kubadilika unazuia majibu ya maswali yakiyojificha mbali kidogo tu.

    4.  Ukiwa mtu wa kuangalia mabadiliko madogo kunakufanya usije kustuka yametokea mabadiliko makubwa sana. Maana utakuwa unaendana na hayo mabadiliko mabadiliko madogo madogo yanayotokea kila siku.

    5. Kuna nyakati utapaswa kujicheka mwenyewe kutokana na makosa ambayo unafanya na kisha uamue kusongambele.

    6. Mambo yanapobadilika na wewe badilika mara moja. Usianze kukaa kwenye eneo hilo hilo na kulalamika.
    Kwenye hadithi ya kitabu kuna kajamaa kalikataa kubadilika baada ya mabadiliko makubwa kuwa yametokea.

    SOMA ZAIDI: ZAMA ZIMEBADILIKA, maisha yamebadilika, ajira hatarini na wewe badilika.

    7  Unapaswa kujua jibini zako ni zipi. Kwa mwingine jibini zake Zinaweza kuwa ni nyumva nzuri, kwa mwingine gari, kwa mwingine biasharabyenye mafanikio wakati mwingine ni familia yenye furaha. Je, wewe jibini zako ni zipi?

    8. Siku zote Kuna jibini (cheese) mpya huko? Ni wewe tu kuamua kuzitafuta

     Kiukweli kitabu hiki cha WHO MOVED MY CHEESE. Kimejaa mafunzo mengi sana ambayo yatakuinua wewe binafsi.

    Kitabu hiki hapa kimetolewa kama audiobook jumatatu ya leo kwenye kundi letu la telegram la AUDIOBOOKS TU. Nikukaribishe uianze wiki yako kwa kujipatia kitabu hiki kwa mfumo wa audiobook.
    Ndani ya kundi hili hapa tunapata audiobooks mbili kila wiki. Yaani kila jumatatu na alhamisi.

    Kujiunga unalipia 3,000 kwa mwezi.  Ambayo ni sawa na 18,000 kwa miezi sita. Sawa na 32,000 kwa mwaka. Ila ukilipia kwa mwaka mzima utalipa elfu 30 tu.

    Ebu chukua hatua uwe miongoni mwa watu ambao wanaenda kuwa wanajipatia vitabu kwa mfumo huu wa audiobooks na kusikiliza popote pale bila usumbufu.
    Unalipia kwa namba 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA Kisha unatuma ujumbe wenye kwa telegram ili kukutaarifu baada ya hapo nitakuunga na utaanza kufurahia vitabu hivi.

    WHO MOVED MY CHEESE?? Audio hii si ya kukosa aiseeh!!!

    Makala hii imeandaliwa na Godius Rweyongeza.
    Unaweza kuwasiliana naye kwa 0755848391
    Au tembelea www.songambeleblog.blogspot.com kujifunza zaidi.

  • Huu Ndio Upekee Wa Vitabu Hivi Viwili

    Siku chache zilizopita Kuna mtu alikuwa anaangalia kava za vitabu vyangu viwili vya KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA. Alipomaliza kuziangalia alisema maneno yafuatayo.
    Kiukweli unajitahidi sana kuhakikisha unatengeneza kava nzuri za vitabu.
    Bila kuchelewa ilibidi nimwambie ukweli huu ambao niliona alikuwa haujui. Nilisema, “kama unavyoona kava za vitabu vyangu zilivyo vizuri, ndivyo na kile kilichondani kilivyo kizuri zaidi”.

    Huu Ni ukweli ambao hakuujua. Inawezekana na wewe hukuujua pia.
    Sasa kama wanavyosema wahenga kuwa utamu wa ngoma sharti uingie ucheze. Vivyo hivyo ukitaka kujua ubora wa vitabu hivi vichukue uvisome na ufanyie kile kilichomo humu
    Kitabu cha kutoka sifuri mpaka kileleni kimekuandalia masomo mazuri kukutoa hapo ulipo na kwenda hatua ya ziada. Unaweza kusoma maelezo zaidi hapa kuhusu kitabu hiki.
    Kitabu cha TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA kimebeba mafundisho mazito ambayo yatakufanya uache kulalamika na uanze kuchukua hatua, ubebe majukumu ya maisha yako na kuacha kufikiria kwamba wengine ndio wanaohusika.
    Uanze kutumia uwezo wako kipkee ulionao. 

    Katika kitabu hiki pia nimezungumzia juu ya kitu ambacho huwa husikii Mara kwa mara watu wakikwambia. Kitu hiki ni kulipa gharama.

    Nikushauri tu ujipatie nakala za vitabu hivi viwili leo hii ili uweze kujifunza mengi zaidi.
    Gharama ya vitabu vyote viwili ni elfu 20. Na vitabu vyote vipo katika mfumo wa nakala tete.
    Ngoja nikwambie kitu. Kupata vitabu hivi viwili kwa gharama hiyo ni sawa na kupewa bure kabisa. Maana kilichonadikwa kwenye kurasa za vitabu hivi ni kitu ambacho kitabadili maisha yako kabisa. 
    Ukishasoma vitabu mpaka mwisho utagundua gharama uliyotoa kwa ajili ya vitabu hivi Ni sawa na bure kabisa ulilinganisha na kile ulichotoa.
    Lipia hiyo elfu 20 kwa namba 0755848391 jina Godius Rweyongeza
    Ukishalipia utanitumia ujumbe wenye neno vitabu ili nikutumie vitabu bila kuchelewa.
    NIKUHAKIKISHIE KITU KIMOJA: Ukichukua vitabu na ukasoma ila ukaona kama umepoteza pesa yako bure. Hapo hapo utapaswa kunitumie ujumbe au kunipigia simu ili nikurudishie pesa yako bila kuchelewa. Na Cha ajabu zaidi ni kwamba utaendelea kubaki na vitabu, lakini pia pesa yako nitairudisha.
    Karibu sana ujipatie nakala hizi mbili muhimu kwako sasa hivi na kwa mafanikio yako ya baadae.

  • Habari Njema Sana Kwa Wapenzi Wa Kusoma Vitabu

    Habari ya muda huu rafiki yangu. Kama ulikuwa hujui basi leo naomba nikupe habari njema.

    Kuna idadi kubwa ya watu ambao huwa wananiomba vitabu mbalimbali vya kusoma mara kwa mara.
    Ambacho huwa nafanya mtu akiniomba vitabu ninamtumia. Kwa hali ilivyo unaweza kukuta siku moja unatumia watu 3-5 na idadi hii inajirudia kwa nyakati tofauti na unakuta kila mtu anahitaji vitabu  tofauti na vile ulivyotuma kwa mwingine.

    Sasa nimeona nirahisishe maisha kwa kuwawekea vitabu hivi sehemu ambapo mtaweza kuvipata. Lakini pia nimeona niweke vitabu ambapo kila mtu anaweza kuomba huko. Na kila mtu anaweza kutuma au kutumiwa vitabu huko.

    Kitu kingine ni kwamba hapa nilipoweka vitabu, nitakuwa silazimiki kuvituma mara mara kwa watu tofauti. Nikituma mara moja tu, ndio nitakuwa nimetuma. Mtu anaweza kuvipakua na kuvisoma baadae mwingine anaweza kupakua na kusoma. Lakini nitakuwa navituma mara moja tu na maelfu ya watu wanapata kuvipakua na kusoma.

    Na vitabu hivyo vitakuwa vinawekwa hapa kwa ajili ya kila mtu mwenye uhitaji. Jiunge ili upate vitabu hivyo. Lakini pia washirikishe wengine juu ya habari hii njema.

    JIUNGE HAPA

    👉ukiwa humu utaruhusiwa kuomba vitabu.

    👉utaruhusiwa kutuma vitabu ulivyosoma na kuona ni vizuri wengine wasome.

    👉utaruhusiwa kutuma kitabu ambacho utaona kinafaa kisomwe na wengine.

    👉HAUTARUHUSIWA kutuma tangazo, link, makala, video au audio yoyote ambayo SI kitabu. UKIFANYA hivyo utaondolewa kwenye kundi mara moja.

    Wewe ingia kwa ajili ya vitabu tu. Ukiona huwezi kukaa pakua vitabu unavyopenda kisha uondoke upaache pakiwa salama.

    JIUNGE HAPA

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
    Unaweza kuwasiliana naye kwa namba hii hapa 0755848391

  • UKIAMBATANA NA MASIKINI WATANO, WEWE NI MASIKINI WA SITA

    UKIAMBATANA NA MASIKINI WATANO, WEWE NI MASIKINI WA SITA



    Ukiambatana na masikini watano, wewe ni masikini wa sita. Ukiambatana na matajiri watano, wewe ni tajiri wa sita.  Hii ni kutokana na ukweli kwamba watu waliokuzunguka wanakuwa na mchango mkubwa kwa kile unachokuwa.

    Jim Rohn aliwahi kusema kuwa wale watu waliokuzunguka  wanakuwa na mchango mkubwa sana kwa kile ambacho unakuwa. Ukitafuta wastani wa kipato cha watu watano waliokuzunguka utagundua kwamba hamjazidiana  sana.
    Ukifuatilia mahusiano ya wale watu ambao wamekuzunguka, utagundua kuwa hamjatofautiana sana kimahusiano. Yaani nyote mna mahusiano yanayoendana endana.
    Hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa unakuwa na timu nzuri ya marafiki wako watano wa karibu sana. Maana Hawa Wana mchango mkubwa sana kwa kile kitu ambacho unakuwa maishani mwako.
    Kama maishani mwako utaamua kufanya uamuzi wa maana sana. Basi hakikisha kwamba unafanya uamuzi wa marafiki wachache wa kuambatana nao. Hawa wanapaswa kuwa wale ambao wanakupa nguvu, sio wale ambao muda wote wanakuambia mkapige stori.
    Hawa wanapaswa kuwa watu wanaofikiri nje ya boksi, sio wale ambao muda wote wanalalamika kwamba maisha mabaya.
    Hawa wanapaswa kuwa wale ambao ukikosea wanakuwa tayari kukwambia ukweli, sio wale wanaokwambia wewe Ni jembe wakati wewe hauna lolote la maana.
    Hawa wanapaswa kuwa wale ambao ulifanikiwa wanaturahi, sio wale ambao ukipata fedha tu wanaanza kusema siku hizi unajidai.
    Hawa wanapaswa kuwa wale wenye kiu ya maarifa na mafanikio. Sio wale ambao wakikuta unasoma wanaanza kusema waliosoma walikuwa wa zamani.
    Hawa wanapaswa kuwa wale ambao penye tatizo wanaona fursa, sio kwenye tatizo wanaona tatizo zaidi.
    Hawa wanapaswa kuwa wale ambao ukikaa nao unajiona Kama hujui(sio kwamba wanakushusha hadhi ila kwa jinsi wanavyojifunza na kuwa na ufahamu mkubwa) sio wewe unaonekana ni gwiji kwenye kundi lako.
    Sasa nikuulize marafiki zako ni wa aina gani?
    Tafakari, chukua hatua

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza
    Unaweza kuwasiliana naye kwa namba hii hapa 0755848391

  • PESA YAKO WEWE IKO HAPA (Na wala sio sehemu nyingine)

    Kama kwa siku sasa umekuwa unatafuta pesa ila huipati. Kama umekuwa unajiuliza hivi nitapataje pesa na  kutengeneza utajiri.

    Leo hii napenda nikwambie pesa yako haiko mbali sana. Pesa yako iko kwenye biashara unayoogopa kufanya. Kama utaamua leo hii kuanza kuanza biashara hiyo unayoogopa kuanza basi pesa yako itakuja na wewe  utaanza kuikusanya.

    Kwa hiyo kazi yako leo hii ni hii. Kuanza biashara uliyokuwa unaogopa kuanza ili upate ukusanye pesa yako.

    Asante Sana, tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.

    Makala hii imeandaliwa na Godius Rweyongeza
    Unaweza kuwasiliana na mwandishi kupitia wasapu kwa namba hii 0755848391

    Unaweza pia kupata vitabu vyake kwa kuwasiliana naye kwa namba hiyohiyo.

    Endelea kutembelea blogu hii kila siku kujifunza zaidi.

    Jiunge kwenye maktaba ya Songambele ili uendelee kupata vitabu zaidi vya kiswahili kwa kiingereza. BONYEZA HAPA kujiunga

X