Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Kheri ya MWEZI WA SEPTEMBA

    Siku zinaenda balaa, ni kama jana tu nakumbuka watu walivyokesha wakiusubiri mwaka mpya. Watu walivyokuwa na mbwembwe za mwaka mpya na mambo mapya, hivi kwenu haya mambo yapo, au ni ushamba wa huku nilipo tu!

    Tafiti nyingi zinaonesha kwamba watu wengi ambao huwa wanaweka malengo. Huwa wanayasahau malengo yao kufikia januari 19, je, wewe malengo yako bado unayakumbuka?

    Katika ujumbe wangu wa kukutakia  kheri ya mwezi mpya siku ya leo,. Napenda pia kukumbusha kuwa tumebaki na siku 120 mwaka huu uishe.

    Hizi siku 120 usizichukulie poa na wala usianze kusema kwamba, ngoja mwaka huu uishe najipanga kwa ajili ya mwakani. Ukweli ni kwamba mwaka huu bado unapaswa kufanya makubwa. Siku 120 zilizobaki ni nyingi sana. Anza kujituma ndani ya hizi siku 120 kuhakikisha kwamba kila siku unafanya kitu cha tofauti.  Chagua kitu kimoja, kisha jisukume kufanya hiki kitu kwa siku 120 zijazo bila ya kurudi nyuma. Ukiweza kufanya kitu kimoja kwa siku 120 zijazo ni wazi kuwa kwanza utajijengea nidhamu, lakini pia kuna kitu ambacho utaweza kufanikisha ndani ya huu mwaka ambacho miakamingi ijayo utajivunia sana.

    Siku 120 ni sawa na mhura mmoja wa chuo kikuu. Ndani ya mhura mmoja mwanachuo anatarajiwa kuwa ameelewa mada ambazo zinafundishwa kwa undani.

    Na mhula mmoja ni kipimo kinachotumika kumpima mwanachuo kuona uelewa wake.

    Wewe pia jipe huu mhula mmoja wa chuo kupambana.

    Mhura wa kufanyia kazi malengo yako hata kama ulikuwa uliyaweka pembeni au ulitulia. Unataka kuandika kitabu, una mhura huu mmoja wa kufanya hivyo.

    Unataka kuongeza kipato chako, una mhura huu mmoja wa kufanya hivyo.

    Unataka kuweka akiba, utumie mhura huu kuweka akiba bila yakuacha

    Unataka kujiondoa kwenye dimbwi la mawazo na sonona inayokusumbnua, una siku 120 za kufanya hivyo.

    Ndani y a hii miezi minne zima kila kitu ambacho hakiendani na lengo lako kuu, kisha juhudi zako zote ziwekeze kwenye lango lako kuu. Kamwe rafiki yangu usikubali kurudi nyuma wala kuyumbandani ya hiki kipindi, huu ni muda wako wa kung’aa. Hakikisha unautumia kung’aa kweli.

    Kama unataka usimamizi wa karibu ndani ya hiki kipindi cha siku 120 zijazo, njoo kikashani nitakusaidia kukushika mkono ili ufanyie kazi lengo lakompaka lifanikiwe. Namba ya kuwasilialina nami ni 0755848391

  • Kazi inayolipa kuliko zote duniani. Jifunze kazi hii utaishi kama mfalme

    Rafiki yangu wa ukweli, bila shaka unaendele vizuri, siku ya leo ningependa kuleta kwako kazi ambayo inalipa kuliko zote hapa duniani. Na kazi hii siyo nyingine bali ni kazi ya kuuza.

    Ni kazi ambayo mtu yeyote ambaye yuko tayari kujifunza anaweza kujifunza. Haina ukomo wa kipato. Unaweza kupata zaidi kadiri unavyouza. Ukiuza zaidi unalipwa zaidi.

    Kitu kikubwa unachohitajhi ni kuwa na bidhaa sahihi na kuiuza kwa watu sahihi. Ni hilo tu. Hakuna zaidi ya hapo.

    Hata kama hauna bidhaa unaweza kuungana na watu wenye bidhaa na kuanza kuuza moja kwa moja. Je, na wewe ungependa kuwa supasta kwenye maisha yako. Basi anza kujifunza mauzo.

    Vitabu viwili unavyoweza kuanza navyo kwenye kujifunza mauzo ni

    Kitabu cha Pschology of selling cha Brian Tracy na

    How I raised myself from failure to success in selling.

    Vitabu hivi vyote viwili unaweza kuvipata kwa njia ya mtandao na kuanza kujifunza kuhusu mauzo mara moja

    Makala hii imeandikwa na Godius Rwqeyongeza. Kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza

    Tafadhali Wasiliana naye kwa songambele.smb@gmail.com

    0755848391

    Morogoro-tz

  • AKILI YA MKULIMA: mambo 12 ya kujifunza kutoka kwa mkulima unayopaswa kuyatumia kwenye maisha yako ya kila siku

    Hata kama wewe siyo mkulima, hakikisha unasoma vizuri makala ya leo.

    MARA KWA MARA UTASIKIA watu mbalimbali wakisema kwamba ,mimi nimezaliwa kwenye familia ya wakulima. Mimi ni mtoto wa mkulima. Ila wanavyokuwa wanaishi maisha yao inakuwa ni kinyume na masomo ambayo tunajifunza kwa wakulima. Kama wewe ni mtoto wa mkulima, ni wazi kuwa kuna mengi ambayo unaweza kujifunza kutoka kwenye familia ya kikulima ambayo unaweza kuyatumia kwenye maisha ya kila siku.

    Kitu cha kwanza kabisa cha kujifunza kutoka kwa mkulima ni akili ya kutunza mbegu. Hakuna mkulima yeyote ambaye huwa anakula mbegu yote baada ya mavuno. Mkulima makini, baada ya mavuno, hata kama amepata mavuno ambayo hayatoshelezi, bado atatoa mbegu za kupanda mwakani. Anajua wazi kuwa akila mpaka mbegu, mwakani hatakuwa na kitu cha kupanda na kama hataweza kupanda basi maana yake kutakuwa hakuna mavuno.

    Hii ni akili makini sana ambayo na wewe mwenyewe unapaswa kuwa nayo na unapaswa kuitumia kwenye maisha yako.

    Inawezekana wewe siyo mkulima. Na inawezekana chanzo chako cha kipato hakitoki kwenye kilimo kama ilivyo kwa wakulima wengine, ila hii akili ya mkulima haupaswi kuiacha. Unapaswa kuambatana nayo popote pale utakapokuwa.

    Kwa kila kiasi cha fedha ambacho utapokea mkononi mwako, kitu cha kwanza kabisa ambacho unapaswa kufanyia kazi ni kutoa mbegu. Fedha yoyote ile ambayo unatoa na kuweka akiba ni mbegu ambayo unaiandaa kwa ajill ya kuja kuipanda mwaka unaofuata.

    Mkulima huwa anajua wazi kuwa mbegu hata kama ni kidogo, akiipanda mwisho wa siku atapata mavuno ambayo ni zaidi ya zile mbegu. Kama ameweka mbegu debe moja, akipanda hilo debe moja, hatapata tena tena debe moja. Badala yake atapata atapata magunia!

    Na wewe linapokuja kwenye suala la fedha yako, haupaswi kula mbegu, badala yake unapaswa kupanda mbegu, ili uweze kula mavuno yanayotokana na mbegu.kwenye kitabu cha tajiri wa babeli kuna somo moja kubwa sana ambalo binafsi niliondoka nalo. Ni baada ya jamaa mmoja kwenye kitabu ambaye anafahamika kama Bansir kuomba ushauri kwa tajiri aliyekuja Babeli kutoka mji mwingine. Tajiri alimwambia kitu kimoja tu, kuwa kwa kila kipato ambacho unaingiza kwenye mfuko wako, kitu cha kwanza kabisa ambacho unapaswa kufanya ni kuweka akiba.

    Bansir aliufuata huu ushauri, baaada ya mwaka mmoja alikuwa amepata kiasi cha kutosha kiasi kwamba litumia kiasi hicho kwenye kununua  punda. Tajiri alipokuja alimwambia kwamba, umekosea. Kitu cha kwanza kwako kufanya hakikupaswa kuwa kununua punda, maana kwa kufanya hivyo, maana yake unakuwa unakula mbegu za matunda yako. Wewe unachopaswa kufanya ni kutunza akiba yako na kuiwekeza ili uwekezaji huu uweze kukuletea mpaka wajukuu na vitukuu. Ni kutokea hapo sasa ndipo utakuwa unaruhusiwa kula wajukuu na vitukuu vyako. hii ni sawa na mkulima ambaye kwake

    Mbegu ya kupandwa kwa mkulima huwa ni kipaumbele na tena huwa inatolewa ikiwa ya kwanza kabla ya matumizi mengine. Tena huwa inatolewa mbegu ambayo ni bora kabisa kuliko nyingine zote. Hakuna mkulima ambaye huwa anatunza mbegu iliyoharibika. Mbegu ambayo huwa inatunzwa ni ile ambayo ni bora kabisa. Hili pia litufundishe kuwa AKIBA, inapaswa kuwa ni kipaumbele cha kwanza. Siyo upate fedha na utumie yote mpaka iishe halafu ndiyo uje ukumbuke kuweka akiba, badala yake ni kwamba unapaswa kuweka akiba kwanza  halafu mambo mengine yatafuata baadaye.

    uwe na siku njema.

  • Jinsi ya kununua ndinga yako mpya

    Ndoto ya kumiliki gari ni ndoto ya vijana wengi. Siyo tu vijana na hata wazee. Lakini inawezekana hujawahi kukaa chini na kuona ni kwa namna inavyowezekana. Sasa leo nataka nikuoneshe ni kwa namna gani unaweza kufanikisha ndoto kubwa kama hii.

    Kabla sijakwambia ufanyeje, Ningependa ujifunze kutoka kwa Rafiki yetu Sanga. Ambaye alikuwa na ndoto ya kumiliki gari lake na sasa kilichobaki ni yeye kwenda kuchukua gari yake.

    Juzi alinitumia ujumbe unaosomeka hivi.

    Nguvu ya Vitu Vidogo Soon Inanipa Nissan Dualis very Soon.

    Hii nguvu ya vitu vidogo anayoongelea ni kitu gani? Ni uwezo wa kufanyia kazi ndoto kubwa kidogo kidogo. Nguvu hii imeelezwa kwenye kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA ambacho alikisoma takribani mwaka mmoja uliopita.

    Baada ya kusoma hiki kitabu aliamua kuchukua hatua na kuanza kuifanyia kazi ndoto yake ya kumiliki gari. hii ndiyo nguvu ya vitu vidogo kuelekea mafanikio makubwa kwa vitendo.

    Akaanza kulipia kwa installment na sasa anakamilisha malipo.

    Wewe pia unaweza kumiliki gari yako kwa kutumia NGUVU hii YA VITU VIDOGO.

    Siyo lazima ulipe kwa installment. Unaweza hata kufungua akaunti maalumu UTT. Kisha kwenye hii akaunti, ukaanza kuweka akiba. Hatua kwa hatua baada ya muda ukaweza kumiliki gari yako mubashara.

    Jifunze nguvu hii ya vitu vidogo kwa kupata nakala yako ya kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA.

    Kitabu kinapatikana kwa 25,000/-. Utasikiaje kama utatoa elfu 25,000/- tu kwa ajili ya kupata kitabu ambacho kitakuwezesha wewe kumiliki gari?

    Changamka sasa. Lipia 25,000/-. Namba ya malipo ni 0684408755 jina GODIUS RWEYONGEZA
    Kisha nitumie ujumbe wa sehemu ulipo ili nikutumie kitabu chako poppte pale ulipo duniani.

  • Habari Njema Kwa Wewe Utakayehudhuria Semina

    Habari njema kwako rafiki yangu ni kuwa ukifanya malipo ya semina mapema kabla ya tarehe 1.9.2023, unaenda kupewa audiobook ya kitabu cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA bure. Sample ya Audiobook hii hapa
    https://youtu.be/On0sNI94FXA?si=0OZ_ddwBCuwMe1hz

    Sambamba na hilo, unaenda kupata mafunzo kamili ya semina.
    Utapata ufuatiliaji wa karibu kwa miezi tisa baada ya semina.
    Utaungana na wengine ambao wanafanyia kazi kwa vitendo yale waliyojifunza.

    Na hilo litakupa nguvu ya tofauti, ukilinganisha na wengine.

    Kutokana na upekee huu wa semina, kama wewe upo tayari kupata matokeo ya tofauti. Kama upo tayari kujituma na kwenda hatua ya ziada basi hii semina ni ya kwako ma haya hapa ndiyo tutakayojifunza.

    https://chat.whatsapp.com/CAdCnW82i8N0clD2fDvn7v

    SIKU YA KWANZA:
    KARIBU KWENYE SEMINA YA KUONGEZA KIPATO MARA 2
    Katika hii siku tutaona
    Utangulizi
    Kwa nini unahitaji kuongeza kipato chako mara 2
    Hatua sita Muhimu za kufuata ili uongeze kipato chako mara 2 ndani ya mwaka mmoja
    Jinsi ya kuweka yatakayokupelekea kuongeza kipato chako mara 2

    SIKU YA 2
    Vyanzo muhimu vitakavyokuwezesha kuongeza kipato chako mara mbili NDANI YA MWAKA MMOJA
    Kamuni ya 80/20

    Siku ya tatu: JINSI YA KUTENGENEZA MSHAHARA NJE YA MSHAHARA

    Ndani ya hii siku tutazama ndani zaidi na kuona….

    Kwa nini unahitaji kutengeneza mshahara wako mwenyewe (nje ya mshahara ya mshahara wa kawaida)

    Namna ya kutengeneza mshahara nje ya mshahara

    Uwekezaji. Msingi mkuu wa kutengeneza mshahara nje ya mshahara.

    *Mpaka hapo ada yako ya semina itakuwa imeisha, ila semina itakuwa inaendelea*

    SIKU YA NNE: BIASHARA: NYENZO MUHIMU YA KUONGEZA KIPATO CHAKO MARA MBILI ZAIDI NDANI YA MWAKA MMOJA

    Kuanzisha biashara yako – wazo na mkakati

    Usimamizi wa biashara na ukuaji wa kipato

    Mbinu za kujiongezea mauzo na mapato

    Kutambua fursa za kukua na kupanua biashara yako

    Kupima mafanikio na kutengeneza mkakati wa baadaye

    SIKU YA TANO: MTANDAO WAKO NDIYO UTAJIRI WAKO:

    Jinsi ya kujenga mtandao utakaokupa fedha

    Mbinu za kuwafikia wateja au watu watakaokuwa tayari kutoa fedha mfukoni kukulipa au kununua bidhaa zako

    Biashara ni mahusiano na namna ya kuyajenga

    Siku ya SITA: ELIMU YA KIFEDHA: KUDHIBITI NA KUKUZA FEDHA ZAKO

    Uelewa wa msingi wa fedha na bajeti
    Kupunguza matumizi yasiyo ya lazima
    Kuweka akiba na kuwekeza kwa ufanisi
    Kudhibiti madeni na mikopo

    SIKU YA SABA: UTAJIRI: MISINGI MIKUU YA KUJENGA UTAJIRI ISIYOYUMBA

    Jinsi ya kuandaa utajiri utakaorishwa mpaka kwa watoto na wajukuu zako

    SIKU YA NANE: HITIMISHO

    Haya ndiyo makubwa niliyoandaa kwa ajili yako. Kinachofuata baada ha hapa ni wewe kuthibitisha kushiriki kwenye hii semina.

    Sasa kabla hujathibitisha, ningependa tu kukutaarifu kuwa ukithibitisha ushiriki wako kwenye hii semina kabla ya tarehe 1.9.2023 unaenda kupokea zawadi ya kitabu sauti (audiobook) moja bure.

    Na kitabu hiki utakachopewa bure ni kitabu cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA (audiobook)

    Unachotakiwa sasa ni kuthibitisha ushiriki wako kwenye hii semina. Kuthibitisha ushiriki wako.
    Lipia ada ya semina ambayo ni 20,000/-
    Namba ya malipo ni 0684408755

    Unaruhusiwa pia kulipia kidogokidogo.
    Unaweza kulipia kila siku (1,000)
    Au unaweza kulipia kila wiki (5,000/-)

    Unachotakiwa kufanya, chagua mpango wako wa kulipia

    Kisha tuma ujumbe wenye jina lako
    Mfano.
    SEMINA; GODIUS RWEYONGEZA; NITALIPIA KIASI CHOTE TAREHE 30.8

    Au

    SEMINA JOHN MSEMAKWELI. Nitalipia KILA WIKI 5,000/-

    Chagua mpango wako, ili kuthibitisha kushiriki semina.

    NB: Ukikamilisha malipo yote kabla ya tarehe moja. Utapata bonus ya audiobook ya kitabu cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA.

    Kumbuka, semina inafanyika tarehe 24-30
    Na ada ha semina ni 20,000/-
    Namba ya malipo ni 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Imeandikwa na
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • Jinsi Ya Kufikia Ndoto Kubwa Hatua Kwa Hatua

    Pata picha una ndoto ya kujenga hoteli kubwa ya kifahari…Yenye nyota saba. Mhh kama unaguna au kujiuliza kama hoteli ya aina hiyo ipo au haipo…
    Ukweli mi kwamba ipo moja huko Uarabuni panaitwa Burj Al Arab iko Dubai.

    Sasa kumbe moja tayari ipo, basi hiki ni kiashiria kingine kuwa na wewe unaweza kujenga hoteli yako ya aina ya hii….

    By the way huu ni mfano, usije ukaacha kufanyia kazi ndoto eti kisa hapa nimeandika hoteli. Kuna kitu nataka nikwambie leo.. hivyo, kaa mkao wa kula.

    Swali ni je unajengaje hoteli kubwa na kifahari hivyo?
    Hela unaitoa wapi?
    Nyenzo nyingine za kukuwezesha kujenga hoteli yako unazitoa wapi?

    Hapa sasa ndipo nataka nikazie. Kuna vtu Vitano amnavyo unaweza kufanya ili kufanikisha ndoto yako hii.

    KWANZA NI KUANZA KUIFANYIA KAZI MDOTO YAKO KWA UDOGO

    Hapa ndipo watu wengi huwa wanashindwa kufanyia ndoto zao. Unakuta mtu ana ndoto kubwa ila haangalii ni kwa namna gani anaweza kuifanyia kazi kwa udogo. Ukweli ni kuwa mtu yeyote anatetaka kuhamisha mlima, sharti aanze kuhamisha mawe kidogokidogo.

    Jiwe likitoka linakuwa limetoka. Halirudi. Hivyohivyo kwako mwenye ndoto kubwa. Kama una hii ndoto kubwa sana, anza kuifanyia kazi hata kama ni kwa udogo.

    Kuthibitisha kuwa hili jambo ninalokwambia hapa, mimi mwenyewe nimekuwa nikilitumia kwenye uandishi wa vitabu. Watu wengi wanashangaa ni kwa namna gani nimeweza kuandika vitabu vingi kiasi hicho, ila ukweli mi kuwa sijaandika vitabu 20 vyote kwa wakati mmoja badala yake nikiandika vitabu hivi kidogokidogo, mwisho wa siku hiki kidogokidogo kimegeuka kuwa vitabu vikubwa na vingi.

    Juzi mmoja wa watu ambao walisoma kitabu changu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA alinitumia ujumbe. Alisema,

    Nguvu ya Vitu Vidogo Soon Inanipa Nissan Dualis very Soon..

    Hii nataka nikuoneshe kuwa ukiwa na lengo kubwa lolote, unaweza kukifanyia kazi hatua kwa hatua kwa kutumia NGUVU YA VITU VIDOGO ndiyo maana na wewe nakushauri usome kitabu hiki.

    Kitabu hiki kinaenda kukupa Mwongozo wa hatua kwa hatua wa kifanyia kazi ndoto kuvwa sana. Kupata nakala ya kitabu hiki wasiliana na 0684408755 sasa ili utumiwe nakala hako. Nakala moja 20,000/-.

    😊😊. Mara paap unaona bei, unaanza kujisema kitabu chenyewe bei kubwa😊😊. Sasa jamani ndoto yako si kubwa eti… Enewei tuachane na kitabu kwanza tuendelee..

    PILI ni kuwa na juhudi kwenye kazi na shughuli zako zaidi. Yaani, ufanye kazi kwa juhudi na kukituma zaidi ya mtu yeyote yule. Mambo unayoyafanya kuelekea ndoto yako yawe mara kumi zaidi ya mtu wa kawaida

    Kwenye kitabu chake cha THE 10X RULE; Mwandishi anasema kila kitu unachofanya kinapaswa kuwa na viwango vikubwa mara kumi zaidi ya wengine waliokuzunguka.

    Uwe na ndoto kubwa zaidi ya mtu yeyote aliyekuzunguka (ndio maana tumeanza na mfano wa ndoto ya hoteli ya nyota saba)

    Ufanye kazi kwa bidii na kwa juhudi mara 10 zaidi ya wengine. Na ukae na watu wanaofanya kazi kwa bidii na kujituma. Kama wewe unakaa kwenye chumba ambacho kuna watu wengine wanafanya kazi kwa bidii zaidi yako basi anza kupambana na kuanza kufanya kazi kwa bidii.

    Tatu, weka akiba. Kwa kila kiasi unachopata usiache kuweka akiba kwa ajili ya ndoto na malengo yako. Akiba ni muhimu sana maana itakuja kukuinua na kukusaidia kufanikisha ndoto zako.

    Hayo ni mambo matatu makubwa ambayo yatakusaidia wewe kufanikisha NDOTO ZAKO KUBWA.

    Anza leo kuyafanyia kazi bila kurudi nyuma.
    Kupata kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA wasiliana na 0684408755. Utatumiwa kitabu chako popote pale ulipo.

    Makala hii imeqndikwa na GODIUS RWEYONGEZA
    0755848391
    www.songambele.co.tz

  • Ujiajiri Au Uajiriwe? Ukweli Mchungu….

    Suala la kuajiriwa na kujiajiri limekuwa linapata mjadala mkubwa sehemu mbalimbali. Kwenye vyombo Vya habari, Kwa wahamasishaji, wanasiasa, viongozi wa Serikali ma dini pia.

    Hata hivyo wengi ambao Huwa wanahamasisha kujiajiri, wenyewe hawajawahi kujiajiri😊😊.

    Hiki kitu a uta wa siutata Kwa wale wanaofanya KAZI huu ushauri. Yaani, wanaufanyia KAZI, lakini wanaokwama wanakuwa hawana mtu sahihi wa kuwashika mkono.

    Kwenye makala ya Leo tunaenda kuona mbichi na mbuvuvkuhusu kujiajiri na kuajiriwa na mwisho wa siku tutaina ni hatua Gani unaweza kuchukua. Makala ya leo ni jibu kwa swali ambalo aliniuliza rafiki yangu mmoja. kabla hatujaebdelea zaidi tuone swali lake.

    Habari yangu ni njema kabisa ESTA.

    1. Kwanza nikupongeze Kwa ujasiri huu WA kujifanyia tathmini na kuona NGUVU na kile ulichonacho na unachoweza kufanya.
    2. Pili ni ukweli Kuwa tumekuwa tunahamasisha watu kujiajiri, ila ukweli mwingine ni kuwa siyo rahisi SANA. kujiajiri Kuna mengi. Hakuna uhakika WA kipato. Kuna wakati unaweza kupitisha Muda hujapata kipato na Kuna wakati unaweza kupata Hela nyingi ndani ya Muda mchache kuzidi hata mishahara kadhaa ya mwajiriwa. Yote hayo yapo, ila ukweli Bado unabaki Kuwa kujiajiri siyo rahisi
    3. Kwa upande wako, nakushauri utafute KAZI kwanza. Kujiajiri kunaweza Kuwa rahisi ukiwa na chanzo kingine Cha kipato ambacho ni Ajira. Lakini pia kujiajiri kunaweza Kuwa kugumu ukiwa na Ajira. Ugumu wake unakuwa hivi, kwanza unakuwa na uhakika WA kipato Kila mwezi. AKILI yako inalemaa na inakuwa haitaki kujihangaisha Zaidi na Zaidi. Hivyo, utegemezi wako wote unauweka kwenye mshahara.

    Lakini pia KUANZISHA BIASHARA ukiwa umeajiriwa maana yake ni kwamba unapaswa kugawa Muda wako vizuri. Kati ya muda wako na muda WA mwajiri. Na unapaswa kujituma haswa Ili utimize majukumu yako na ya mwajiri. Unapaswa kuwa SIKU mbili ndani ya simu Moja, SIKU ya kazi za mwajiri na siku ya BIASHARA yako na hatimaye muda na familia. Siyo rahisi.

    1. Lakini sambamba na hayo yote Bado nakushauri ESTA katafute KAZI kwanza uajiriwe. Ukishapata KAZI sasa ndiyo tutapanga mpango mzuri WA KUANZISHA BIASHARA. Hii Kwa upande wako itakuwa na faida ya kupata mtaji ambao itakusaidia KUANZISHA BIASHARA. Tafadhali naomba ufahamu kuwa unavyoajiriwa, ajiriwa ukiwa na PLAN B kichwani. Plan ya SIKU Moja kutengeneza Kitu cha kwako.

    Sasa swali kinakuja unapataje Ajira?

    Binafsi sijawahi kuomba KAZI. Sijawahi kutuma CV sehemu yotote Ile. Ila kama ningekuwa naomba KAZI Leo hii. Ningefanya yafuatayo.

    Kwanza, ningeandaa vyeti vyangu vyote va msingi.
    Pili, ningechagua kampuni ambazo nataka kufanya nazo KAZI. Ningetafuta hata kampuni 50 za kuanza nazo.

    Tatu, ningetuma maombi yangu kwa wanaohusika kuajiri kwenye hizi kampuni nilizochagua, ningeendelea kuwafuatilia Kwa ukaribu hata Kwa kuwapigia simu Ili nijue kama wana mpango wao.

    VITU vingine viwili vya ziada ambavyo ningefanya vingekuwa ni
    Kujiunga na mtandao WA LINKELDN. Huu ni mtandao WA watalaam. Waajiri wengi wako huku. Huu mtandao siyo kama Instagram ambapo Kila MTU anajiunga. Wanaojiunga huku ni watu makini sana. Huku Sasa ningefuatilia fursa za ajira zilipo. Lakini pia ningeanza kujenga ukaribu na watu ambao ningependa kufanya KAZI kwenye taasisi zao. Na hata kuwauliza kama Wana nafasi au wanafahamu sehemu yenye nafasi ambapo naweza kuajiriwa.

    Sambamba na Hilo ningetembelea ofisi mbalimbali ambazo ninataka kufanya nazo KAZI. Hapa ningezitembelea ana Kwa ana na kuomba kuonana na bosi wao. Kitendo Cha kuonana na bosi TU, kingenifanya nimweleze Mimi ni nani na ninaweza Nini. Ningemweleza ni Kwa namna Gani nitakuwa MTU WA msaada kwake.

    Hiki kipengele ndiyo kugumu kuliko Vyote ambavyo nimetaja hapo juu. Wengi wanakiogopa hiki, ila kama ningekuwa Mimi ninayetafuta KAZI. Hiki ndiyo ningekipa kipaumbele Zaidi.

    Changamoto inakuja kwenye kuonana na bosi hasa unapoenda kwenye kampuni husika. Wasaidizi WA mabosi Huwa wanakuwa wagumu sana kukukutanisha na mabosi zao.
    Wanataka wajue Nini hasa unachofuata Kwa bosi na ukiwaambia wanakukatisha tamaa na kukwambia Hilo haliwezekani. Ila kumbe kama ungekutana na bosi ingekuwa ni rahisi sana kwako kumwambia unachotaka akakubali.

    Sasa basi, ambacho ningefanya. Kiuhalisia hiki ndicho Huwa nafanya. Mbali na kuwa sijawahi kuomba KAZI kama nilivyokwambia, ila Huwa ninaonana na wakurugenzi wa kampuni mbalimbali Kwa ajili ya shughuli zangu. Wiki hii TU nimeshatembelea kampuni na taasisi 14 na Leo nitaendelea kutembelea kampuni na taasisi zaidi. Kati ya hizo kampuni na taasisi 14. Ni kampuni 4 tu ambazo nimeona na bosi Moja Kwa Moja. Nyingine Kumi nimeishia Kwa wasaidizi ambao wameniblock nisionane na bosi wao na kampuni nyingine bosi alikuwa amesafiri au hayupo ofisini Kwa wakati huo.

    Kati ya hao wanne, ni mmoja tu ambaye tumekubaliana Kitu cha maana na Leo saa SITA mchana ninaenda kuongea na wafanyakazi wa taasisi yake kuwafundiaha Kuhusu UMUHIMU WA KUSOMA VITABU na Kuweka AKIBA.

    Mwingine ameniambia niende mwisho wa mwezi.

    Nataka kusema njni, ninachotaka kukuonesha hapa ni kwamba hiki Kitu siyo rahisi ila kinawezekana.

    Naomba nimalizie Kwa kusema kwamba chagua mpango wako ambao utaufanyia KAZI. Ufanyie KAZI Kwa uhakika bila kuacha. Nina hakika hili utalifanikisha.

    Unafanyaje Sasa baada ya kupata KAZI?
    Wengi Huwa wanajisahau sana bada ga kupata Ajira. MTU anapta Ajira anasahau kuwa ana ndoto na malengo ya kujiajiri. MTU anasahau Kuweka akiba. MTU anasahau kuwekeza.

    Hiki ni kitu kibaya, kwani Kwa muda unapokuwa na Ajira utaona kuwa maisha umeyapatia, maana hata ukiutumia mshahara mwisho wa mwezi mshahara mwingine utakuwepo tu. Ila ambacho Haupaswi kusahau ni kuwa unapaswa KUAJIRIWA na PLAN B Kichwani. Plan ya kutengeneza kipato kingine nje ya Ajira.

    Ndiyo maana unapaswa kuweka akiba, kuwekeza n.k.

    Kwa Leo nadhani inatosha.
    Mwisho kabisa uliniomba vitabu vizuri kutoka kwangu Vya kusoma. Naomba usome vitabu hivi Kwa mpangilio wake kama ninavyovitaja hapa JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO, NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA na JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO.

    Lakini pia mwezi wa Tisa tutakuwa na SEMINA ya mtandaoni (online). Hii ni SEMINA ya KUONGEZA KIPATO CHAKO mara mbili ndani ya mwaka mmoja. Kwenye hii semina moja ya mada tutakazoongelea ni JINSI YA KUTENGENEZA MSHAHARA NJE YA MSHAHARA. Tutaongelea vitu vingine Vingi ambavyo vitakufaa wewe kama mpambanaji Makini. Hivyo, nashauri usiache kuhudhuria semina hii ya mtandaoni ambayo itaanza tarehe 24 na kumalizika tarehe 30.

    Semina itafanyika Kwenye kundi maalumu la whatsap na gharama ya SEMINA itakuwa ni 20,000/-
    Tafadhali hakikisha unahudhuria semina hii. Unaweza kuwasiliana na msaidizi wangu 0684408755 na Kuweka mpango wako WA kulipia. Unaweza kulipia hata buku au jero. Unaweza kulipia Kila siku kiasi kidogo, unaweza kulipia Kila wiki kiasi Fulani au Kila mwezi. Unaweza pia kulipia mara moja.

    Nimekupa taarifa mapema Ili usije kukosa mambo mazuri.

    Asante sana

    Karibu sana na Kila la kheri

  • Uwekezaji Kwenye Hisa vs Uwekezaji Kwenye Maeneo Mengine

    Pata hiki kitabu kwa 20,000 hardcopy na 10,000 softcopy

    Ukilinganisha uwekezaji kwenye hisa na vipande na uwekezaji maeneo mengine kama ardhi, Vito vya thamani….n.k ukweli ni kwamba, uwekezaji kwenye hisa ni rahisi Kwa MTU yeyote kuanza.

    Unaweza hata kuanza kumiliki kampuni Kwa mtaji mdogo.
    Unaweza kuwekeza kidogo kidogo.

    Ili ufanye uwekezaji kwenye nyumba, unahitaji mamilioni ya pesa ila kuwekeza kwenye hisa, unaweza KUANZA na hisa kumi tu,

    Swali linabaki kuwa je, hisa kumi ni sawa na shilingi ngapi?

    Nikiiangalia kwenye soko la HISA, bei za Jana zinaonesha kuwa hisa zilizouzwa Kwa bei kubwa sana ni hisa za TCC ambazo bei yake ni 16,200

    Na hisa za bei ya chini ni za TTP ambazo bei yake ni 120

    Hisa za kampuni nyingine zipo katikati hapa

    Mfano hizo hisa 10 za TCC unaweza kuzimilili Kwa 162,000. NA hisa kumi za TTP ni 1200

    Lakini huwezi kumiliki nyumba kiasi hichohicho.

    Hivyohivyo kwenye vipande. Kwa Sasa mfuko Wenye vipande vya bei ya juu ni mfuko wa UMOJA ambapo kipande kimoja bei yake ni 937.7959

    Na kipande chenye bei ya chini ni kipande Cha mfuko wa FAIDA. Ambapo kipande kimoja bei yake ni 106.3648

    Mifuko mingine bei zake zipo katikati hapo.

    Na kwenye mifuko hiyo mwili niliyoongelea hapo, unaweza KUANZA kuwekeza kwenye hiyo mifuko Kwa elfu Kumi TU.

    Ili uwekeze kwenye soko la hisa kwa mafanikio unapaswa kuwa na maarifa sahihi.

    Anza Kwa kununua kitabu HIki Cha MAAJABU GA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI na VIPANDE.
    Gharama yake ni 20,000/- tu kwa hardcopy.
    Na 10,000 kwa softcocpy

    Kupata kitabu hiki lipia. 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Utatumiwa kitabu hiki tu ounde baada ya kufanya malipo.

  • Mara moja siyo mbaya

    Mara kwa mara utasikia watu wanasema mara moja siyo mbaya. Yaani, kwamba kufanya jambo mara moja halafu ukaacha siyo kitu kibaya.

    Kwenye ulimwengu wa mafanikio, mara moja ni mbaya sana.

    Unahitaji ufanye vitu kwa mwendelezo na mara kwa mara, bila kuacha kwa kuda mrefu ili upate matokeo.

    Kama ni akiba unapaswa kuweka akiba kila siku hata kama ni kidogo, ufanye hivyo kwa mwendelezo bila kuacha. Baada ya muda vitu vidogo utakavyokuwa unafanya vitakuletea matokeo.

    Kama ni kujitlfunza. Fanya hivyo kila siku bila kuacha.

    Kama ni kuamka asubuhi na mapema, fanya hivyo kila siku.

    Ukifanya mara moja ni mbaya sana. Nakubaliana na Bruce Lee aliyesema kuwa
    “Sina hofu na yule aliyejaribu mishale elfu moja mara moja, lakini nina hofu na yule aliyejaribu mshale mmoja mara elfu kumi.”

    Akiwa anaamaanisha kwamba kufanya mara mwendelezo Kuna nguvu kubwa sana kuliko kufanya kwa kustukiza mara moja.

    Hatua ya kuchukua leo.

    1. Chagua kitu kimoja cha kufanyia kazi (kuweka akiba, kuwekeza, kujifunza n.k)
    2. Kifanye hicho kitu kwa mwendelezo kila siku bila kuacha.
    3. Pima matokeo yake baada ya siku 100.

    Kila la kheri

  • USISUBIRI mpaka uwe na Kila kitu Ili uanze.

    Anza na kile ulichonacho. Fanya unachoweza Sasa. Ili ufanikishe MAKUBWA.

    Miaka kumi ijayo, utajishukuru Kwa kuchukua HATUA na kufanya kitu kuliko kukaa bila kufanya kitu.

    Ukianza kuweka akiba Leo. Miaka kumi ijayo, utajishukuru Sana Kwa HATUA uliyochukua Leo hii.

    Kumbuka. Muda mzuri WA kupanda mti ulikuwa ni miaka kumi iliyopita, ila muda mwingine mzuri zaidi ni Sasa.

    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

    Kupata Vitabu vizuri Kwa Ajili Yako wasiliana na 0684408755

X