Home


  • KITABU CHA DIAMOND: AKILI YA DIAMOND

    Habari ya upande wa huko rafiki yangu. Nimeandaa kitabu kizuri kinacjoitwa Akili Ya Diamond.

    Kitabu hiki Cha kipekee kimelenga kukuonesha wewe namna ambavyo unaweza kugundua kipaji chako, kukinoa na kukiendeleza huku tukipata masomo na mafunzo kutoka kwa Diamond Platnumz lwaa namna alivyofanyia kazi kipaji chake.

    Kitabu hiki kitaanza kupatikana kuanzia tarehe 1.8.2022

    Je, ungependa kupata nakala yako?
    Basi tuwasiliane sasa kwa 0755848391 ili utumiwe nakala yako. Bei ya kitabu ni 10,000/- tu.

  • Changamoto Ni Fursa

    Badala kuomba kuishi maisha ambayo hayana changamoto wala matatizo, omba uwezo wa kutatua changamoto unazokutana nazo.

    Changamoto ni fursa
    Changamoto ni biashara.
    Changamoto ni njia kufika mbali.
    Watu WALIOFANIKIWA siyo kwamba hawakuwa na matatizo wala changamoto.

    Bali walitumia changamoto na matatizo waliyonayo Kama fursa kwa ajili ya kusongambele zaidi. Mara zote jiulize Ni kwa namna gani naweza kunufaika na changamoto zilizopo sasa Hivi…?

    Angalia ni kwa namna gani unaweza kutumia changamoto kama fursa na ukasonga mbele. Je, changamoto au matatizo gani ambayo umekumbana nayo?

    Je, unaona fursa yoyote Ndani yake?

  • Uchambuzi Wa Kitabu Cha The Richest Man In Babylon

    Kitabu: The Richest Man in Babylon

    Mwandishi: Georges Clason

    Mchambuzi: Hillary Mrosso

    Simu: 255 683 862 481

    Utangulizi

    Zaidi ya miaka 8000 imepita, mji mkuu uliojengwa kwa ustadi wa juu sana huenda kuliko miji yote duniani ulijulikana kama Babiloni. Sifa za mji huu zilitapakaa duniani kote sio tu kutokana na ustadi na ufahari wa majengo au uzuri au uimara wa kuta za mji huu bali hekima waliyokuwa nayo watu wa Babiloni. Kwa sasa Babiloni haupo tena, historia ya uzuri, uimara, ufahari na umaarufu wake umepotea kwa karne nyingi sana. Licha ya kupotea kwa mji wa Babiloni kuna baadhi ya vitu havikupotea; vitu hivyo ni hekima ya wababiloni hasa hekima na kanuni za kupata utajiri na mali. Hekima hizo zilipatikana zimeandikwa katika vibao vya mawe, zikijulikana kama sharia za dhahabu. Ni sharia hizi ndizo walitumia kutafuta utajiri, kuutunza utajiri na kuendelea kuzalisha utajiri. Hekima hizi za wababiloni ndio zinaweza kutumika kuijenga Babiloni sehemu yoyote duniani. Karibu tujifunze hekima na sharia za wababiloni kuhusu fedha, utajiri na mali.

    1. Siku zote kama unataka ushauri wa kukusaidia kuvuka au kufanya jambo lolote kwenye maisha jaribu kutafuta watu sahihi. Kama vile mfalme na watu wa Babiloni walivyomtafuta Arkadi ili awashauri na kuwapa siri za kupata utajiri na mafanikio.
    2. Kupata mwalimu au mtu sahihi wa kukushauri sio tu atakwambia cha kufanya, bali atakuelekeza namna ya kufanya jambo kwa ufasaha zaidi. Mfano mzuri ni Arkadi sio tu alikuwa mshauri mzuri lakini pia aliwafundisha wengine kwa mifano yake mwenyewe na maisha yake yalikuwa mfano mzuri.
    3. Ni ujinga kuamini kuwa utajiri wa mtu upo katika mifuko ya pesa alizonazo, utajiri wa kweli ni kuwa na mirija inayoingiza fedha katika mifuko yako bila kukoma.
    4. Kuwa na mapesa mengi au dhahabu mifukoni sio ishara ya utajiri au mafanikio, wababiloni wanasema utajiri na ishara zake ni kuwa na mirija isiyokauka inayokuingizia fedha, mirija ya dhahabu golden streams.
    5. Haijalishi matumizi yako ni makubwa kiasi gani, kama una mirija ya uhakika ya kukuingizia kipato katika mifuko au hazina zako bado unaweza kuishi kwa uhuru sana.
    6. Kama hauna utajiri au mali kwenye maisha yako sababu kubwa inaweza kuwa ni kushindwa kujifunza kanuni za kupata utajiri au ulizipuuzia kanuni za kupata au kujenga utajiri. Mfano, Wababiloni wengi walikuwa masikini kwa kutokujua kanuni na sharia za kupata utajiri.
    7. Utajiri hauji tu kwa bahati nzuri au mbaya, utajiri na mafanikio ni matokea ya kujifunza na kufanyia kazi sharia za kupata utajiri. Mfano mzuri ni kutoka wa Nomasir, amabaye alipoteza kila kitu baadaye akakaa chini akajifunza tena kanuni za kupata utajiri alizopewa na baba yake na akafanikiwa kufikia utajiri.
    8. Ili usipoteze muda ukizengea zengea jangwani, jifunze kwa moyo wako wote na kwa akili zako zote kanuni na sharia za kupata utajiri, kutunza utajiri ambazo ziliasisiwa na kutumika na watu wengi maarufu waliofanikiwa hapa duniani.
    9. Mafanikio ya kudumu hayaji tu kwa kufanya kazi kwa bidii pekee, unahitaji kupata maarifa na hekima katika kazi na namna ya kuyatunza mafanikio utakayoyapata.
    10. Njia ya kwenda kwenye utajiri ni kuhakikisha katika mapato yako yote unayopata tenga asilimia kumi pembeni kama akiba yako binafsi.
    11. Haijalishi unaingiza mapato kidogo kiasi gani kwenye shughuli zako, hakikisha unatenga asilimia kumi ya mapato yako kama malipo yako.
    12. Wababiloni wanatufundisha kuwa, tujilipe wenyewe kwanza, na hapa kwenye kujilipa isiwe chini ya asilimia kumi (10%) ya mapato yako.
    13. Wababiloni wanashangaa sana, tunaweza kumlipa kila mtu lakini tunashindwa kujilipa wenyewe, hii ni moja ya sharia ya dhahabu waliyojifuza watu wengi waliofanikwa ikiwamo wababiloni wenyewe.
    14. Kila kiasi kidogo unachoweka kama akiba kwa ajili ya uwekezaji ni mtumwa wako wa baadaye kukufanyia kazi ufanikiwe.
    15. Kila fedha au dhahabu unayoipata na kuweka akiba, iwe kwa lengo la kukufanyia kazi ili ufanikiwe zaidi.
    16. Kama unataka kuwa na utajri endelevu, kila mapato unayopata yanatakiwa yaendelee kukuzalishia mapato zaidi, hasa sehemu ya mali ulizowekeza au kuweka akiba.
    17. Kama umeamua kujilipa mwenyewe kama wanavyoshauri wababiloni, haitakiwi kuwa chini ya asilimia kumi ya mapato yako. JILIPE WEWE MWENYEWE KWANZA.
    18. Wababiloni wanasisitiza sana, hatakama mapato yako ni kidogo kiasi gani, jambo la kwanza kufanya kwenye mapato yako ni kujilipa kwanza, iwe asilimia kumi ya mapato yote.
    19. Ukipata fedha zako, usinunue nguo kwanza, usinunue viatu, usinunue gari, usinunue simu, usinunue mabati, usikimbilie kulipa madeni kwanza, jilipe mwenyewe kwanza.
    20. Baada ya kujilipa mwenyewe asilimia kumi ya mapato yako, hapo ndio uanze kufikiria matumizi mengine jinsi ikupendezavyo.
    21. Kama unataka ukweli kuhusu kodi nenda kwa watu wa kodi, kama unataka ukweli kuhusu ng’ombe nenda kwa wafugaji wa ng’ombe, ukienda kwa watu tofauti itakugharimu sana muda na rasilimali nyingine kama fedha.
    22. Tamaa, hisia, uchoyo ni mambo ya kuyazuia sana katika safari ya kwenda kwenye mafanikio na utajiri.
    23. Endelea kufanyia kazi bajeti yako ili ikufae na ikusaidie katika safari yako ya mafanikio na utajiri.
    24. Bajeti yako inatakiwa ikusaidie kulinda fedha zako, mali zako na kukufanya uendelee kuwa tajiri, idhibiti na kuizingatia sana bajiti yako hasa ya matumizi.
    25. Hakikisha hekima na maarifa uliyojifunza katika kitabu hiki yanakusaidia, hasa katika kupata, na kulinda hazina na uwekezaji wako ili uwe salama.
    26. Tunatakiwa kuwa na uwezo wa kulipa madeni yetu kwa wakati, na pia kujizuia kununua kitu ambacho hutaweza kukilipia.
    27. Madeni ni mabaya yanaweza kukutenga na familia yako, marafiki na yanakufanya kuwa mtumwa. Mfano mzuri ni Dabasir wa Babiloni, aliyekuwa mtumwa na kufanya kazi za kutunza farasi kipindi kile.
    28. Unapolipa madeni ya watu kwa muda unaheshimika sana katika jamii, na pia utapata watu wazuri wa kushirikiana nao.
    29. Tunatakiwa kuwa na huruma kwa wote ambao hawakuweza kufanikiwa na kuwa matajiri kama sisi, tunatakiwa kuwa na kiasi katika jambo hili la huruma na misaada.
    30. Kila wakati tuanatakiwa kujiongeza na kujifunza zaidi ili tuongeze uwezo wetu wa kuzalisha na kupata utajiri zaidi.
    31. Unapojifunza na kujipatia hekima maarifa, ujuzi unaongeza nguvu ya ushawishi na kuheshimika na kukubalika katika jamii. Mfano, watu wa babiloni waliheshimika kwa hekima zao zilizowasaidia kuwa matajiri na kuwasaidia wengine pia.
    32. Bahati nzuri inamsubiri mtu ambaye yupo tayari kupokea fursa zinazojitokeza.
    33. Kinacho tufanya kushindwa kutumia fursa zinazojitokeza mbele yetu ni roho ya kughairisha mambo iliyopo ndani yetu inayotufanya kuiona hatupo tayari au tuna muda mwingi.
    34. Kama tunataka kuwa sehemu ya kuvuna utajiri na hazina kama ilivyokuwa Babiloni tunatakiwa kuifukuzia mbali roho ya kughairisha mambo isiwepo karibu na sisi kabisa.
    35. Hazina na uatajiri wa Babiloni unapatikana na kuwafikia wote ambao wameachana kabisa na roho ya kughairisha mambo. Usighairishe kabisa mambo muhimu kwenye maisha yako, yafanye kwa nguvu zako zote, hata kama unajisikia hovyo kiasi gani.
    36. Hatua unazochukua kila wakati ndio zitakufikisha kwenye mafanikio na sio matamanio uliyonayo, matamanio yaendanie na matendo.
    37. Dhahabu au fedha zimehifadhiwa kwa wote ambao wanazifahamu sharia na kanuni zake na kuzifuata.
    38. Epuka mihemuko na hisia za tamaa katika kutafuta utajiri, fuata kanuni na hekima za waliofanikiwa katika kutafuta utajiri utafika ukiwa imara na utajiri wako ukiwa salama.
    39. Fedha na dhahabu zitawapotea kwa haraka sana watu wasio na hekima, zitakimbilia kwa walio na hekima. Soma sharia saba za dhahabu zilizowasaidia wababiloni, zinaweza kutusaidia sisi pia.
    40. Kama unatamani kumsaidia rafiki yako msaidie kwa namna ambayo matatizo yake hayatakuwa mzigo kwako mwenyewe.
    41. Kama mtu ana roho ya utumwa, ataendelea na hiyo roho ya utumwa hata akiwa hayupo utumwani. Siku zote maji yanafuata mkondo wake.
    42. Madeni yanaweza kukufanya ukawa mtumwa bila wewe kujua.
    43. Mtu yeyote anayejali maisha yake na nafsi yake lazima atoke kwenye madeni, madeni yanakuondolea heshima na utulivu.
    44. Wafalme wakuu wanatumia nguvu kubwa na kila kitu walichonacho kupambana na maadui zao. Wewe adui yako ni madeni yako.
    45. Madni yatakufukuza mbali na uwapendao, mbali na mahali ulipopapenda, mbali na nchi yako, yatakufanya ujione mpweke. Mfano mzuri ni kama ilivyomtokea Dabasir wa Babiloni.
    46. Waliokukopesha sio maadui, unaowadai sio maadui, ni watu mlioaminiana na kupendana ndio maana mkakopeshana, madeni ndio maadui wenyewe. Ukitaka kurudi Babiloni nchi ya uhuru na utajiri lazima ulipe madeni yako yote.
    47. Dhamiria kulipa madeni yako ili urejeshe uhuru wako na furaha yako. Penye nia pana njia. Amua kwa dhati kupata uhuru wako wa kifedha, uhuru ni bora kuliko utumwa. Toka utumwani na urudi Babiloni nchi ya washindi na walio huru.
    48. Kama unadhamira ya kweli ya kurudi babiloni, jua kuwa elimu na mafunzo uliyopata kuhusu fedha na dhahabu umeyaelewa na kuyatekeleza.
    49. Simama tena, jisikie mtu huru, fanya na ishi kama mtu huru na aliyefanikiwa. Rudi tena Babiloni.
    50. My debts were my enemies, but the men I owed were my friends for they had trusted me and believed in me.

    Many things do I enjoy but nothing takes the place of work.

    Ahsanteni sana!

  • Vitu vitano vya kujiepusha navyo ili ufike mbali

    1. Jiepushe na vileo
    Hivi vitachukua muda wako mwingina fedha lakini havitakufanya upige hatua yoyote kubwa kimaisha.

    2. Jiepushe  Kuwa bize na kila kitu.
    Yaani, hiki unafanya. Kile unafanya. Unapambana na kila kitu. Hapana, sililiza rafiki yangu, wekeza nguvu yako kwenye vitu vichache ambavyo unaweza kufanya kwa ubora wa hali ya juu sana. Kisha vifanye kwa ubora wa hali ya juu. Ikiwezekana fanya hata kitu Kimoja na ujulikame kwa hicho.

    Kuna usemi wa kiingereza unaosema kuwa the jack of all trades is a master for none.
    Wekeza nguvu zako kwenye vitu vichache na uvifanye vizuri, Tena ikiwezekana kitu kimoja tu.
    Kwa mfano, ukisikia majina kama Mbwana Samatta unajua wazi kuwa Huyu ni MTU wa mpira.
    Ukisikia Diamond, unajua kabisa kuwa konachoongelewa ni muziki.
    Wewe pia weka nguvu zako sehemu ambapo utafahamika. Eneo moja ambalo utabobea na kulielewa vizuri.

    3. Jiepushe kujua kila kitu
    Ugonjwa unaoua watu wengi hapa duniani ni ugonjwa wa kujua kila kitu.
    Jitahidi sana kujiepusha na ugonjwa huu. Kuwa mtu wa kujifunza kila mara.

    Kadiri unavyojifunza kila mara Ndivyo unavyoweza kuelewa mambo mengi ambayo hapo awali ulikuwa huelewi.

    Ila usipokuwa MTU wa kujifunza, unakuwa unatimiza ule usemi wa kuwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.

    4. Epuka kuishi maisha bila mpango. Maisha bila mpango siyo maisha mazuri unayopaswa kuishi. Jitahidi mara zote kuwa na mpango malengo ambayo unayafanyia kazi.

    Usipokuwa na malengo, daah rafiki yangu. Utajiona kama vile unapiga hatua wakati hakuna hatua yoyote kubwa unayopiga. Malengo, yanakuweka kwenye njia.
    Malengo mara zote yanakukumbusha kuwa bado hujafika. Hivyo, weka juhudi zaidi ili uweze kufika. Malengo yanakwambia kuwa endelea kupambana na KUWEKA juhudi zaidi.
    Malengo yanakupa motisha.
    Penda mara zote kuweka malengo makubwa, kuyafanyia kazi na ukishayafikia weka malengo makubwa zaidi Kisha yafanyie kazi.

    5. Epuka kuishi maisha ya kujilinganishana watu wengine
    Mara zote jitahidi uweze kuishi maisha yako kama maisha yako bila ya kujilinganisha na watu wengine.
    MTU pekee unayopaswa kujilinganisha naye Ni wewe wa jana.
    Na wewe mwaka Jana.

    Jiulize hivi nikijilinganisha na jana, je, leo niko bora zaidi ya jana.
    Ukigundua kuwa leo hii upo bora zaidi ya jana. Basi weka nguvu zaidi kwenye kufanyia malengo ili uzidi kuwa bora zaidi.
    Ukigundua Leo uneyumba na kurudi nyuma, Basi weka nguvu zaidi ili uweze kuwa Bora.

    Ni hivyo tu.

    Makala hii imeandaliwa na rafiki yako
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • Mwaka Huu Ni Wangu Kufanya Makubwa

    Mwaka Huu Ni Wangu Kufanya Makubwa

    Kila mwanzoni mwa mwaka watu wengi huwa wanaweka malengo makubwa ya kufanyia kazi. utasikia mtu anasema kwamba mwaka huu ni mwaka wangu wa kufanya makubwa. utasikia mwingine anasema kwamba mwaka huu lazima tu nifanye makubwa. ila sasa cha kushangaza

    Unakuta kwamba siku zinakuwa zinazidi kupita kiasi kwamba inafikia hatua huyo mtu anashindwa kufanyia kazi lengo lake la mwaka.

    Kinachokwamisha watu wengi ni kwamba wengi wanaweka mipango na malengo makubwa ila wanakuwa hawachukui hatua kuhakikisha kwamba wameweza kufikia malengo na ndoto zao.

    Hivi wewe ni miongoni mwa hawa watu rafiki yangu?

    Ninachotaka kukwambia ni kwamba mafaniko makubwa huwa hatatokei mara moja tu yaani, mwishoni mwa mwaka. Badala yake ni mchakato wa vitu vidogovidogo unavyokuwa unafanya kila siku.

    Hivi vitu vidogo vidogo unavyofanya kila siku, baadaye vinaunganika na kutengeneza kitu kikubwa.

    Ebu fikiria kila siku ukiwekea utaratibu wa kufanya kitu hata kama ni kidogo, ni uhakika kuwa mpaka mwisho wa mwaka lengo lako lililokuwa kubwa utakuwa umelisogeza mbali pangine hata kulifikisha na kupita makadirio yako.

    Hiki kitu hakiwezi kukushinda.

    Kwa siku zilizobaki kumaliza mwaka huu. anza kufanya kitu hata kama ni kidogo tu kila siku kuelekea kwenye lengo lako kuu. Kila siku fanya kitu hata kama ni kimoja tu. uhakika ni kuwa baada ya mwaka utakuwa umeweza kufanya siyo hicho kitu kimoja, badala yake utakuwa umeweza kufanya makubwa.

    Haijalishi umeajiriwa

    Uko bize sana au

    Bosi wako anakubana.

    Huwezi kukosa hata dakika kumi na tano tu kwa siku za kufanya kitu cha kwako hata kama ni kidogo. rafiki yangu, endelea kuipambania ndoto yako mpaka kieleweke. Usikubali kurudi nyuma kwa namna yoyote ile.

    Bila kuongeza la ziada, naomba niishie hapo……..

    Kitu kimoja cha ziada kuhusu kitabu cha nguvu ya vitu vidogo kuelekea mafanikio makubwa.

    Najua hapa kwa vile nimeongelea kitabu unaishia hapa na kucha kusoma zaidi. hahahaha

    Unaanza kufikiria huyu jamaa hapa anaongelea pesaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    Enewei, hiki kitabu ni muhimu kwako rafiki yangu…..

    Ni muhimu mno.

    Kama kuna kitabu kimoja unachopaswa kusoma mwaka 2022 basi ni hiki. Sikisifii kwa sababu nimekiandika mimi bali kwa sababu waliokisoma wengine wamethibitisha hilo.

    Ebu ona maoni haya hapa chini

    Umeona ee….

    Sasa, kitabu hiki ni 20,000 tu za kitanzania au dola kumi (10) kama upo nje ya nchi.

    Utaongeza gharama kidogo za usafiri kulingana na sehemu ulipo nami nitakutumia hiki kitabu. Ninatuma popote pale duniani.

  • Njia pekee ya itakayokuhakikishia wewe kupata matokeo ya tofauti

    Siku za nyuma niliandika makala niliyoipa kichwa cha Kama Unataka Mali: Maeneo Matano Unapoweza Kupata Mali Halali…

    Kwenye makala hii nilieleza mbinu mpya za kupata Mali. Najua kwamba wengi tulisoma shairi la kama mnataka Mali mtazipata shambani, Ila sasa je, siku hizi na zama hizi tunazoishi,  bado tunapaswa kutegemea Mali kutoka shambani? Hapo ndipo nilikueleza hizo mbinu za kukuaidia kupata Mali kwenye hizi zama.

    Sasa siku ya leo nina kitu Kimoja. Leo nataka nikwambie Kuwa kama unataka kupata matokeo ya tofauti. Rafiki yangu sharti unapaswa kukubali kufanya vitu vya tofauti.

    Huwezi kuendelea kufanya vitu vilevile kila siku huku ukitegemea kupata matokeo ya tofauti.

    Matokeo ya tofauti hayapo kwenye kufanya vitu vilevile kila siku. Kama unataka kupata matokeo ya tofauti, sharti ukubali kufanya vitu vya tofauti kwanza.

    Kama unafanya kile ambacho kila mtu anafanya, utapata matokeo ambayo kila mtu anapata. Njia pekee ya wewe kupata matokeo ambayo hujawahi kupata Ni kufanya vitu ambavyo hujawahi kufanya.

    Kama umeajiriwa, unaenda kazini muda ambao kila mtu anaenda kazini na muda wa kutoka unakukuta getini. Ujue wazi kuwa hutapata matokeo ya tofauti maishani mwako. Fanya kitu Cha tofauti, wahi kazini, fanya kazi kwa bidii, chelewa kidogo kutoka, pangilia ratiba zako.

    Kama umejiajiri unafungua biashara au unaenda kazini unapotaka na kutoka unapojisikia, jua wazi kuwa hutakuja kupata matokeo ya tofauti. Sikiliza, Anza kwenda tofauti. Jitume kufanya kazi zaidi ya saa 15 kila siku. Kumbuka siyo saa 15 za kuwa macho na kuperuzi mtandaoni. Ni saa 15 za kazi siriazi.

    Rafiki yangu, popote pale ulipo. Pambana kufanya kazi kitofauti na vile ulivyozoea.

    Ukiendelea kufanya kazi kwa namna ulivyozoea nakuhakikishia kuwa hakuna MUUJIZA wowote utakaouona maishani mwako.

    Kila la kheri.

  • Endelea Kupambania Ndoto Na Lengo Lako

    Kama una lengo na ndoto kubwa ambayo unaifanyia kazi. Endelea kupambania ndoto yako na lengo lako kila siku. Usirudi nyuma kwa kuanza kujilinganisha na watu wengine.

    Sikiliza kila siku jiboreshe wewe mwenyewe.
    Jifanyie tathimini kila mara kuangalia umatoka wapi, uko waapi unaelekea wapi.

    Jisukume kila mara kufanya zaidi. Ila usijilinganishe na MTU mwingine.

    Hakuna mtu mwingine mwenye lengo na ndoto Kama zako.

    Kabisa….

    Kila mtu anapambana na hali yake…

    Kitu pekee ambacho unapaswa kuchukua kutoka kwa Watu Ni mbinu na namna ambavyo wanainuka kutoka eneo moja kwenda jingine na kusongambele.

    Ila siyo kujilinganisha nao.

    Kisa eti fulani kanunua gari Basi na wewe ukimbizane na gari

    Kisa eti fulani kajenga NYUMBA Basi na wewe ukajenge.

    Sikiliza, tulia na ndoto yako na vipaumbele.
    Ukifuata kile ambacho wengine wanafanya Hutakata uishi maisha yako kama wewe. Utaishi maisha ya kuiga tu siku zote na sehemu zote. Hakuna haja ya wewe kuiga maisha.

    Ishi maisha yako
    Jitathimini kila mara
    Fanyia kazi uliyopata kutoka kwenye tathimini yako.
    Songambele.
    Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.

  • Hiki kitu ndicho kinafanya watu wanakuchukulia poa

    Umewahi kujiuliza kwa Nini watu wengi wanakuchukulia poa.

    Kuna sababu nyingi zinaweza kuwa zinasababisha hiki ila sababu ya kuu unaweza kuwa Ni wewe umewafanya wakuchukulie poa.

    Inawezekana kuna kipindi ulitakiwa kutoa huduma fulani kwao ila hiyo huduma hukuitoa vizuri.

    Inawezekana ulijishusha viwango kwa kutaka kupata kitu fulani wakati hukupaswa kujishusha

    Na pengine inawezekana ni kwa sababu ya mtazamo  wa MTU tu. Yaani, akiaakuangalia anakuchukulia poa.

    Unachopaswa kujua ni kuwa siyo kazi yako kuanza kuwaambia watu kuwa msinichukulie poa.

    Badala yake nenda kafanye kazi. Acha matendo yako yaongee kiasi kwamba hata wale wanaokuchukulia poa waanze kuona thamani yako.

    Anza leo.
    Chukua hatua hata Kama ni ndogo kwa ajili ya kuongeza thamani yako.

    Kazi utakayofanya, ifanye kwa ubora.
    Ongeza kipato chako
    Kuwa bize na maisha yako badala ya kufuatilia maisha ya watu wengine.
    Acha kutuatilia maneno wanayosema wengine.
    Nguvu zako zote ziweke kwenye kazi.

    Kwa jinsi hii itakuwa umekataa kuchukuliwa poa kwa vitendo na siyo kwa maneno. Endelea kupambana, watakuona ukivuka ng’ambo.

  • Vitu vizuri huchukua muda

    Mfano hupandi mti wa mwembe leo naa kuvuna kesho. Hapana.
    Unachukua muda.

    Utamwagilia mbegu
    Utapalilia kuondoa majani ili mhegu iweze kuendelea kukua.

    Ila walau haitachukua siku moja wala siku mbili. Itachukua muda. Kwa miembe ya kisasa inachukua siyo chini ya miaka mitatu na nusu.

    Kwa miembe ya kawaida inachukua miaka Saba na zaidi.

    Inashangaza kuona watu wako tayari kuvumilia miaka saba kabla ya kuvuna maembe lakini hawako tayari kuvumilia miaka saba kabla ya kufikia ndoto au lengo kubwa walilojiwekea.

    Watu wapo tayari kusoma shuleni kwa miaka 16-20 au zaidi kabla ya kuanza kufurahia matunda ya elimu. Lakini hawako tayari kuvumilia miaka saba mpaka kumi kabla biashara yao haijaleta matunda makubwa.

    Hiki kitu kinapelekea watu kukimbilia fursa zisizokuwepo.
    Leo hii wakiambiwa kuna fursa ya kuweka laki moja kesho kuvuna laki mbili wanaikimbilia.

    Rafiki yangu nisikilize kwa kitu kimoja tu.
    Kwa lengo lako au ndoto yako uliyonayo. Utaweza kuifikia iwapo tu utaifanyia kazi hatua kwa hatua.

    Tumia nguvu ya vitu vidogo Kwenye kufanyia kazi ndoto zako.

    Ndiyo maana nimekuandalia mwongozo wa kitabu hiki Cha kipekee.

    NGUVU ya VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA.
    Kitabu hiki Cha kipekee kinapatikana kwa 20,000/- tu.

    Unatumiwa popote pale ulipo. Sasa cha kufanya leo hii unapaswa kufanya hivi
    Wasiliana na 0755848391 ili uweze kupata kitabu chako. Utatumiwa popote pale ulipo

  • Fanya Hiki Unapokuwa Huna Kitu

    Kama huna kitu chochote kile Cha kupoteza basi pambana. Pambania ndoto na malengo yako kila siku na kila Mara bila kurudi nyuma.

    Maana huna kitu chochote cha kupoteza.
    Huna hela
    Huna ujuzi
    Huna konekisheni

    Hivyo njia pekee ya wewe kutoboa ni Kuendelea kupambana bila ya kurudi nyuma hata kidogo.

    Ipambanie ndoto yako mpaaka uifikie.

    Nakushauri Sana usome hiki kitabu Cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA
    Nitakuonesha Ni kwa namna gani unaweza kuanza kidogo mpaka ikafikia hatua ukafanya makubwa.

    Karibu sana

X