Home


  • Zawadi Tano Nzuri Unazoweza Kutoa Kwa Uwapendao

    Mara kwa mara huwa tunapenda Kutoa zawadi za gharama kubwa ili kuwaonesha watu Kuwa tunawapenda. Zawadi kama gari ndio zinaonekana zawadi zenye maana kubwa Sana..

    Leo hii ningependa nikuoneshe zawadi Tano Nzuri ambazo unaweza kutoa kwa watu zikawa na maana kubwa Sana. Zinaweza zisionekane za thamani machoni pa watu ila aliyepewa zawadi husika akiichukua na kuitumia. Uhakika ni kuwa hii zawadi Ina uwezo wa kumfikisha mbali sana.

    Zawadi  ya kwanza ni zawadi ya kitabu.
    Ebu jiulize kwanza, wewe umewahi kupewa zawadi ya kitabu? Umewahi kuona MTU anatoa zawadi ya kitabu?
    Umewahi kufikiri kutoa zawadi ya kitabu?

    Zawadi ya kitabu siyo zawadi maarufu sana. Kwa Nini? Kwa sababu tumeambiwa kwamba ukitaka kumficha mwafrika kitu, basi niandike kwenye kitabu.

    Ila ukimpa mtu zawadi ya kitabu unakuwa umempa hazina kubwa sana. Kwenye kitabu kuna maarifa ambayo yanaweza kusaidia kumwinua mtu huyo

    Zawadi ya pili ni zawadi ya wazo
    Wazo moja linaweza kumwinua rafiki yako au MTU yeyote kutoka sehemu alipo kwenda sehemu nyingine.

    Kwa hiyo Kama mtu akikuomba msaada Basi mpe msaada wa wazo. Nasema Kama mtu akikuomba kwa sababu, watu huwa hawathamini mawazo. Watu wanathamini Sana fedha, hivyo usijitoe ufahamu tu wa kuwa unatoa zawadi ya mawazo yako bure kwa watu ambao hawayafurahii na hawatayatumia. Ila mtu akikuomba wazo, wewe mpe.

    Mimi mwenyewe kama una wazo lolote la kuniambia unaweza kuniambia. Napokea mawazo na Kuyafanyia kazi. Ebu nipe wazo/pendelezo lako Sasa Hivi
    Baruapepe:
    godiusrweyongeza1@gmail.com
    Simu/SMS/WhatsApp 0755848391
    Nitalipokea wazo lako.

    Zawadi ya tatu ni zawadi ya kumfundishaa mtu ujuzi
    Tunaishi kwenye ulimwengu ambapo ujuzi Ni kitu muhimu sana. Ukiwa na ujuzi wako na ukautumia vizuri. Huo ujuzi utakufikisha mbali.

    Ndio maana kwenye ulimwengu wa Leo tunapaswa pia kutoa zawadi za kufundisha watu ujuzi fulani…

    Ujuzi wa kufanya kitu fulani
    Ujasiriamali
    Uwekezaji
    Uchambuzi
    Kuna aina nyingi za ujuzi.

    Kuna soft skills na hard skills. Ila ujuzi wowote ule ni ujuzi tu, Kama unaweza kumfundisha mtu ujuzi, mfundishe.

    Na hapa naomba nieleweke kwa kitu Kimoja. Ujuzi aliokuwa anahitaji babu yako kuishi kwenye kipindi chake siyo ujuzi unaouhitaji wewe leo hii. Zama za sasa zimebadilika. Zamani walihitaji kuwa na ujuzi wa kuwinda, ujuzi wa kutengeneza moto, ujuzi wa kujua viashiria vya mazingira ya hatari n.k.

    Kwenye ulimwengu wa leo hali ni tofauti. Unaweza kuwa na ujuzi ambao watu wanauchukulia poa Ila ukakuingizia kipato kikubwa sana.

    Zawadi ya nne ni zawadi ya konekisheni.
    Kama kuna mtu anafanya kitu, zawadi pekee Unayoweza kumpa ni konekiaheni ili kitu chake kiweze kujulikana zaidi. Kama mtu ana mgahawa, mpe konekisheni ya watu zaidi wa kununua kwake.
    Kama mtu ni msusi, mpe konekisheni ya watu zaidi watakaosuka kwake.

    Kiufupi Kama Kuna MTU anafanya Jambo fulani zuri. Mpe konekisheni ya watu zaidi ambao wanaweza kupata bidhaa au huduma kwake. Hii Ni Zawadi kubwa Unayoweza kutoa. Maana ukimletea mtu mteja mmoja na akamhudumia huyo mteja mmoja vizuri. Ukweli ni kwamba huyo mteja mmoja Anaenda kununua kwake Mara nyingi zaidi na ataleta wengi zaidi

    Sasa hii si zawadi nzuri na ya kipekee?

    Zawadi ya tano ni zawadi ya kuwekeza kwenye HISA
    Mpe mtu zawadi ya hisa, hatifungani au VIPANDE. Hii Ni hazina kubwa sana.

    Ukimpa mtu zawadi ya hisa unakuwa unempa umililiki wa kampuni.

    Karibu sana kwenye semina ya uwekezaji kwenye HISA. Hili ni kundi la mapokezi.

    Semina hii itafanyika kwa njia ya mtandao (online) kupitia kundi maalumu la WhatsApp.

    Kwenye semina hii utajifunza mengi kuhusu uwekezaji kwenye HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE

    Na baada ya semina utapata kitabu (Hardcopy/audiobook) Cha JINSI YA KUWEKA AKIBA NA KUANZA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE.

    Kitabu hiki utakipata bila kuongeza Gharama ya ziada.

    Gharama ya semina ni elfu ishirini na moja 21,000/- tu.

    Namba ya malipo kwa Ajili ya semina ni 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Karibu sana
    Ni Mimi Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • Mfuatilie huyu jamaa kwa mwezi mmoja tu, wewe mwenyewe utaniambia utakachoona

    Tunaishi katika dunia ambapo watu wanapenda kufuatilia sana maisha ya watu wengine. MTU anaweza kushinda mtandaoni akifuatilia maisha ya watu mbalimbali
    Wasanii
    Wachumba fulani
    Wachungaji n.k.

    Ila Kuna jamaa mmoja ambaye umekuwa unasahau kufuatilia. Na jamaa huyu siyo mwingine bali ni wewe mwenyewe.

    Rafiki yangu, kwa kitu chochote kile unachofanya. Penda Sana kujifuatilia wewe mwenyewe zaidi ya unavyofiatilia maisha ya watu wengine.

    Jijue maisha yako kwa uzuri.
    Jua wapi unapotezea muda wako mwingi zaidi ili uweze kuwekeza muda huo kwenye vitu vya maana.
    Jua ujuzi gani hauna sasa hivi, ili uanze kuujenga.
    Jua  konekisheni ambazo hauna ili uanze kuzijenga.
    Jua afya yako ikoje, ili uiboreshe.
    Jua maarifa unayohitaji sana sasa hivi, ili uweze kuyajenga.
    Jua changamoto zinazokukabili ili uweze kuzitatua.
    Jua ulivyofanya vizuri leo ili uweze kujipongeza
    Jua ulipokosea leo ili uweze kujirekebisha.

    Ukifuatilia maisha yako na kujiwekeaa nadhiri ya kuyaboresha maisha yako kila siku. Basi ni wazi kuwa baada ya muda maisha yako yatakuwa yanazidi kuboresheka na kuwa bora zaidi na zaidi.

    Rafiki yangu, jitahidi sana kufuatilia maisha yako na ili uweze kuyaboresha na Kuyafanya kuwa bora zaidi.

  • Vitu Vitano Unavyopaswa Kutembea Navyo Kila Mahali

    Ni vitu gani huwa unaambatana Navyo kila mahali unapoenda. Je, ni simu, kitabu au Nini? Leo hii ninakuletea orodha ya vitu Vitano Unavyopaswa kuambatana Navyo kila mahali na ubora Ni kuwa havina gharama ya ziada kuvifanya

    Kujiamini. Jiamini kwenye kila kitu unachofanya. Kama unafanya kitu ambacho hakikufanyi ujiamini, basi hapo kuna mawili.
    Achana nacho usikifanye kabisa ili uweze kufanya kitu kingine kitakachokufanya ujiamini. Au Anza kujiamini kuanzia leo hii.

    Upendo wa Kazi.

    Rafiki yangu, tembea na upendo wa Kazi kila mahali. Yaani, kazi unayoifanya ifanye kwa moyo wako wote bila kijibakiza.
    Kama huwezi Kuwa na upendo kwenye Kazi yako unayofanya sasa hivi una machaguo mawili moja Ni kuachana nayo na usiifanye kabisa ili uweze kutafuta kitu ambacho unakipenda au chagua kitu ambacho unakipenda na ufanye hicho.

    Tabasamu
    Haikugharinu kitu chochote kutabasamu popote pale utakapokuwa. Kama kuna kitu ambacho unapaswa kukifanya kila marra Basi Ni kutabasamu
    Anza leo hii

    Kuwaacha wengine zaidi ya ulivyowakuta

    Jitahidi sana kila mara Unapokutana na mtu kuhakikisha kwamba unamwongezea kitu cha ziada
    Kwenye mazingira yetu tumezungukwa na wakatisha tamaa wengi. Watu ambao wanarudisha maisha ya watu nyuma zaidi.

    Sasa unaonaje na wewe badala ya Kuwa mkatisha tamaa, ukiwa MTU wa kuwapa watu matumaini. Mara zote watie watu moyo na ONGEA maneno ya kuwainua ili waweze kufanya kazi na shughuli zao kwa ubora ZAIDI ya wanavyofanya.

    Kama hujapenda kitu badala ya kumkatisha tamaa anayekifanya, toa mbinu ya kukiboresha. Ila siyo kuishia tu kulalamika.

    Kila mtu anaweweza kulalamika. Kulalamika siyo Bei kubwa, ndiyo maana kila mtu anaweza kufanya hivyo, wewe jitofautishe kwa kuachana na kulalamika.

    Maneno yako.
    Mara zote tembea na maneno chanya. ONGEA kile unachomaanisha. Maneno yanaumba. Usijitamkie maneno mabaya na Wala usiseme maneno mabaya kwa wenzako. Weka nuvu kubwa kwenye kusema maneno chanya na kuwahamisha watu wengine ili waweze kufanya kile wanavyofanya kwa ubora ZAIDI.

    Tunahitaji tutengeneze dunia ya tofauti na hii dunia hatuwezi kuitengeneza kwa Kuwa na watu ambao wanalalamikia kila kitu.

    Hivyo, Ni vitu Vitano ambavyo unapaswa kutembea mavyo kila mahali na kila siku.

    Kila la KHERI.

    Umekuwa nami,

    Godius Rweyongeza

    0755848391

    Morogoro-Tz

  • Je, bado na wewe ni mshamba wa fursa?

    Kila mara huwa wanakuja watu kwa kusema kwamba kitu fulani kinalipa ukilinganisha na kitu kingine. hiki kitu ndio kinanifanya leo hii intake kukuuliza, hivi na wewe bado ni mshamba wa fursa.

    Hkauna fursa moja ambayo unaweza kusema kwamba inalipa zaidi kuliko nyingine.

    Kila ulimwona mjomba amenunua gari kupitia fursa fulani, haimaanishi kwamba na wewe ukimbilioe huko.

    Moja ya stori ambayo imekuwa ikipagawisha watu kwenye kilimo ni stori KILIMO CHA TIKITI.

    Watu wengi wamekuwa wakikimbilia kulima tikiti kwa kujua kwamba tikiti linalipa sana. wapo ambao wamekuwa wanafanikiwa kwa viwango vikubwa huku wengine wakiangukia pua.

    Ujumbe wangu kwako siku ya leo ukiona mtu kafanikiwa kwenye fursa fulani, badala ya kukimbilia kuiga na kufanya kama alivyofanya, jiulize maswali yafuatayo.

    Je, amekuwa akiifanyia kazi hii fursa hii kwa miaka mingapi?

    Hiki kitu kitakusaidia kujua nje ndani kuhusiana na fursa husika na hivyo kujua  muda na nguvu utakazopaswa kuweka. Wengi  wanaposikia kuhusu fursa wanadhani kuwa ni kitu ambacho utafanya kwa siku moja na kitu hicho kikaleta matokeo makubwa. wengi unaowaona wamefanikiwa kwenye fursa fulani, wamekuwa wakizifanyia kazi hizo fursa kwa miaka mingi mpaka leo hii unaona tayari wamefanikiwa. Na hiki kitu kimewafanya waijue fursa husika nje ndani, kiasi kwamba inafikia hatua wanafanya maamuzi ambayo yanawasaidia kufika kule wanapotaka.

    Ni msimu gani zao hili linafanya vizuri?

    Kama umemwona mtu amefanikiwa kwenye kilimo. Na wewe unataka kuingia kwenye kilimo. Usiingie kichwa kichwa, la sivyo utakuja kuangukia pua. Kabisaaa. Badala yake jiulize ni  msimu gani zao lipi huwa linakuwa na bei ya juu. Hili lipo karibia kwenye kila zao. Hivyo, ni muhimu kwako kutambua hiki kitu, la sivyo utaingia kwenye kilimo kichwa kichwa halafu utaangukia pua.

  • Njia Nane Zitakazokuwezesha Wewe Kulipwa Mara Mbili Mpaka Mara Kumi Zaidi

    Moja ya tamanio la watu wengi ni kulipwa kiwango kikubwa kuliko ambavyo wanalipwa sasa hivi au  kupata kipato kikubwa zaidi ya wanavyopata sasa. Nina hakika hata wewe ungependa kulipwa zaidi ya unavyolipwa sasa, pengine ungependa kupata kipato mara mbili mpaka mara tatu zaidi ya unavyopata sasa hivi, si ndio? sasa kwenye andiko la siku ya leo tunaenda kuona mbinu ambazo zitakusaidia wewe kulipwa mara mbii mpaka mara kumi zaidi ya unavyolipwa sasa hivi. Mbinu hizi ambazo tunaenda kuona hapa, ni mbinu ambazo zimethibitishwa kufanya kazi na haziwezi kukuangusha endapo utazitumia kama zilivyoelezwa kwenye andiko la leo.

    NJIA YA KWANZA NI KUFANYA KAZI YA UNAVYOLIPWA

    Huu najua ni utamaduni ambao haujazoeleka kwa watu wengi. Kuna vijana wengi ambao siku hizi wanalia ajira mitaani ila wakishapata hizo ajira, wanarelax  na hivyo kushindwa kuchapa kazi kama inavyotakiwa. Moja ya kitu ambacho mimi mwenyewe kimekuwa kikinishangaza ni kuona kwamba vijana wengi wanaandika kwenye CV zao kwamba ni wachapakazi na wanaweza kufanya kazi kwenye hali yoyote, ila pale wanapopata kazi, wanakuwa wazembe kiasi kwamba wanashindwa kufanya kazi na kuleta matokeo ambayo wanaahidi wakati wa kuomba kazi.

    Sasa siku ya leo nataka nikwambie kwamba achana na uzembe wako, kama unataka kulipwa zaidi.  Fanya kazi kwa kujituma zaidi ya unavyolipwa, uhakika ni kwamba hiki kitu baadaye kitakufanya ulipwe zaidi ya unavyolipwa sasa.

    Usije ukachukukulia kuwa juhudi zako ambazo unaweka kwa sasa hivi, zinapotea bure. Unaweza kusema kwamba bosi wako hazioni ila ukweli ni kwamba anaziona hata kama hatakuwa hasemi. Na pengine kuna kitu cha kipekee ambacho atakuwa anakiandaa kwa ajli yako. Au hata kama bosi wako hazioni wala kujali juhudi zako ambazo unaweka. Fahamu kuwa kuna watu wengine ambao wanajali na wanapenda sana juhudi zako, hivyo, kuna siku katika mazingira na namna ambayo wewe mwenyewe hutegemei watu hao watakutafuta ili uende kufanya nao kazi.

    Hamna juhudi zako zinapotea bure. Kiufupi ni kwamba asili, ilivyo ni kwamba, hakuna kitu chochote ambacho huwa unafanya unafanya ambacho huwa kinapotea bure. Ndiyo maana wahenga wetu walituasa vizuri waliposema kwamba unavuna ulichopanda. Ukipanda mbegu nzuri, utapata mavuno mazuri, lakini wakati huohuo ukipanda mbegu mbaya utavuna mavuno mabaya.

    Ukipanda mbegu ya uchapakazi, utpata mavuno yake.

    Ukipanda mbegu ya uzembe, maavuno yake utayapata pia.

    Kwa hiyo, kwenye maisha unapaswa kuchagua, unapaswa kuchagua mbegu nzuri ya uchapakazi dhidi ya mbegu ya uzembe. Maana uchapakazi na kufanya kazi kwa bidii na kujituma zaidi ya unavyolipwa kunalipa zaidi ya kitu kinginecho chochote.

    Sikiliza, kama wewe kwenye maisha yako, unafanya kazi kwa kusukumwa. Yaani, kama ni mpaka usukumwe na kufuatiliwa ili uweze kufanya kazi. basi achana na hiyo tabia kuanzia siku ya leo. Badala yake anza kujituma na kufanya kazi hata kama hakuna mtu yeyote yule wa kukusukuma nyuma ya pazia. Kwanza sifa ya kufanya kazi bila ya kusukumwa wala kufuatliliw na mtu yeyote ndiyo sifa ya pekee ambayo watu wanaoingiza kipato kkubwa wanayo, wewe pia unapaswa kuwa nayo.

    Tena anza kuwa nayo kuanzia leo hii.

    Nakukmbuka kuna kipindi nilikuwa nafanya kazi na kijana mmoja hivi ambaye alikuwa anafanya kazi kwa bidii na kujituma sana. kiukweli nilikuwa napenda kazi zake ambazo alikuwa anafanya na siku zote hakuwahi kuniangusha. Mara nyingi sana nilipokuwa nikimpa kazi ya kufanya kwa siku husika, yeye alikuwa anaweza kuifanya ndani ya saa tatu mpaka nne, na kuimaliza kisha kuendelea na mambo mengine. Hivi union hicho kitu ee. Yaano, kwake kazi ya siku nzima anaifanya ndani ya masaa matatu na kuimalizaa.a

    Alikuwa haitaji usimamizi wangu muda wote.

    Alikuwa anajongeza snaa kwenye kazi yake na kufanya zida.

    Mara zote nilikuwa nikiona juhudi zake, nilizipenda kweli.

    Lakini kumbe kuna watu wengine ambao walikuwa wakiona juhudi zake pia. Siku moja, niliona ananifuata na kuniambia kwamba anaachan kazi kwangu. Kitu hiki kwangu kilikuw akama mwiba maana nilikuwa nikipenda kuwa na kijana kama yule anayechapa kazi na kujituma badala ya kijana anayesimamiwa na kufuatiliwa nyuma muda wote.

    Nilijaribu kumwongezea mshahara mara mbili ii tuendelee kufanya kazi kwa pamoja, lakini alikuwa ameshafikia uamuzi wa kuondoka. Mpkaka leo hii huwa anakutana naye mara kwa mara, ana furaha muda wote na anapenda kazi anayofanya huku akiendeleza juhudi zake za kuchapa kazi zaidi ya anavyolipwa.

    Hiki kitu kimenifunza sana, mbali na kwamba kufanya kazi kwa bidii kunakufanya unalipwa zaidi. lakini pia naona kwamba wanaofanya kazi kwa bidii wana furaha kuliko ambao wanzembe.

    Wanaozembea ndio wenye majungu muda mwingi, maneno mengi ambayo hayana tija, ndio wanalalamika, ndio ambao wanapenda kuonewa huruma, wanapenda kuongezwa mishahara huku wakiwa hawaweki juhudi. Naomba unisikilize kwa kitu kimoja. Weka juhudi kwenye kazi zako unafanya. Juhudi zako unawezoweka zitakufikisha mbali zaidi ya ulipo sasa hivi.

    Penda sana kufanya kazi zaidi ya unavyolipwa

    SOMA ZAIDI: JITUME KWA FAIDA YAKO

    FANYA KAZI KWA BIDII

    NJIA YA PILI NI KUSOMA VITABU

    Kusoma vitabu kuna uwezo wa kukufanya ulipwe mara mbili mpaka mara tatu au hata mara kumi zaidi ya unavyolipwa sasa hivi. kama kuna kitu ambacho unapaswa kukipa kipaumbele kwenye maisha yako nbasi ni kusoma vitabu na kupenda kujifunza mara kwa mara.

    Unaweza kuwa unajuliza, kwani kusoma vitabu kunawezaje kunifanya mimi  niongeze kipato changu mara mbili mpaka mara tatu zaidi ya ninavyoingiza sasa hivi.

    Kwanza ni kwamba kusoma vitabu na kupenda kujifunza kunakufanya unakuwa na maarifa ambayo wengine wanakuwa hawana. Hivyo, hayo maarifa yanakuwezesha wewe kufanya uamuzi ambao wengine wanakuwa hawana.

    Ebu tuchukulie mfano, umesoma na kujifunza kuhusu uwekezaji kwenye hisa. Umeuelewa vizuri na na kutumia maarifa haya mauzri uliyoyapata ukaanza kuwekeza kwenye hisa, hatifungani pamoja na vipande. Baada ya siku kadhaa, utaanza kupata gawio linatokana na uwekzaji wako kwenye hisa. Hicho ni kipato zaidi rafiki yangu ambacho ulikuwa huingizi mwanzoni rafiki yangu.  Na tena unakipata bila kuweka juhudi zaidi.

    Au tuseme unasoma kitabu kama JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEBVU. Baaada ya siku chache unajifunza ujuzi wa uandishi, ujuzi ambao unalipa na ujuzi mzuri kwenye zama hizi tunazoishi. Baada ya siku si nyingi utakuwa umeweza kuwa mwandishi mzuri ambaye anaweza kuandika andiko linaloeleweka. Unaweza kukuta unapata tenda z kuandika maeneo mbalimbali ambayo hata hukutegemea kama magazetini, hicho ni kipato cha ziada rafiki yangu hapo kinakuwa kinagonga mlango.

    Lakini pia kusoma na kujifunza kunakusaidia wewe kuweza kupangilia ratiba yako na hivyo, kujua majukumu yapi uyafanye lini na majukumu yapi usiyafanye kwa wakati gani. wakati hali ni tofauti kwa mtu ambaye hasomi.

    Kusoma vitabu na kupenda kujifunza kunakufanya unakuwa mmbunifu. Kitu hikitu kinaweza kukufanya wewe ulipwe mpaka mara tano au mara kumi zaidi.

    Nakumbuka kuna mzee mmoja ambaye alikuwa anapenda sana kujifunza kupitia semina na mafunzo mbalimbali. HUYU MZEE alikuwa daktari. Kuna siku alihudhuria semina inayohusiana na upasuaji wa macho. Semina hii ilikuwa ya gharama kubwa, ila mzee huyu alilipia. Kwenye semina hii alijifunza ujuzi ambao ulikuja kumtofautisha yeye na madajtari wengine maisha yake yote.

    Kumbe, kitu kimoja ambacho unasoma kwenye kitabu kinaweza kubadili maisha yako na kukufanya kuwa mtu wa tofauti kabisa.

    NJIA YA TATU NI KUWAFIKIA WATU WENGI ZAIDI

    Kama unamhudumia mteja mmoja, unachopaswa kufahamu ni kuwa siku huyo mteja akiacha kununua kwako basi wewe utakuwa huna kipato tena. Kama umeajiriwa maana yake unamhudumia mteja mmoja ambaye ni mwajiri wako. Kwa hiyo kipato chako kitakuwa na ukomo kwa sababu mteja unayemhudumia ni mmoja.

    Sasa ebu fikiria mtu menye ujuzi kama wewe, elimu kama wewe na kila kitu kingine chochote kama wewe akiwahudumia wateja watano, unadhani atalipwa kiasi gani? maana yake atalipwa mara tano zaidi ya unavyolipwa wewe.

    Kumbe basi, mara zote angalia ni kwa namna gani ambavyo unaweza kuwahudumia wateja zaidi na kupanua masoko yako.

    Kama umeajiriwa, unaweza kuanza kuagalia namna ya kutumia ujuzi wako nje ya ajira, ili ule muda baada ya kutoka kazini uweze kuuwekeza kwenye biashara au kuwahudumia wengine zaidi. Kwa jinsi hii utakuwa untengeneza mifereji ya kulipwa zaidi hapo baadaye.

    NJIA YA NNE NI UAMINIFU

    Katika uliwngu tunaoishi sasa hivi, uaminifu ni kitu kimoja muhimu sna ambacho unahitaji. Bila uaminifu rafiki yangu takwama sana. Iwe umeajiriw au unafanya kazi kwa kujiajiri, unahitaji uaminifu  wa hali ya juu sana.

    Watu wanapenda kufanya kazi na waaminifu.

    SOMA ZAIDI: UAMINIFU NI MTAJI

    NJIA YA TANO NI KUONGEZA THMANI KWENYE BIDHAA UNAZOTOA

    Watu wanapenda kupata vitu vyenye thamani nzuri. Hakikisha kwamba kazi yoyote ile ambayo mkono wako unagusa, unaifanya kwa viwango vya juu. Kwa jinsi hii nakuhakikishia kwamba muda si mrefu, watu watamiminika ili wapate kazi zako zaidi.

    NJIA YA SITA NI KUWA NA BIDHAA ZAIDI YA MOJA.

    Ukiwa na bidhaa moja maana yake mteja akija kununua wako hiyo akiondoka ndiyo ameondoka. Yaani, hatarudi tena kununua tena. Ebu tuchukulie unauza redio tu. Mtu akinunnua kwako hawezi tena kuna kununua kwako redio maana tayari anayo.

    Ukiwa na bidhaa zaidi ya moja maana yake mteja mmoja anaweza kununua kwako zaidi ya mara moja. na hata akinunua mara moja maana yake atanunua vitu vingi kwa wakati mmoja. Mfano ni simu, earphone, chaja, memory card, n.k

    Lakini pia unamfanya mteja aweze kurudi kununua kwako mara kwa mara.

    Endapo ukiwa na bidhaa moja walau iwe ni bidhaa ambayo wateja watakuwa wanakuja kununua mar kwa mara. Mfano chumvi au sukari. Hizi ni bidhaa ambazo wateja lazima watakuja kunua mara kwa mara hata baada ya kuwa wamenunua mara ya kwanza. Kwa jinsi hii kadiri watakavyokuwa wanaunua zaidi ndivyo na kipato chako kitaongezeka. Na siyo wanunue tu wenyewe kwa kurudi. Bali warudi na wateja wengine zaidi.

    NJIA YA SABA NI KULIPWA KWA KAMISHENI

    Kama unachapa kazi kwa bidii, badala ya kukubaliana na bosi wako akulipe kwa mshahara mwisho wa mwezi, amua kwamba unaenda kulipwa kwa kamisheni. Unajiuliza hivi kulipwa kwa kamisheni ndio nini?  Kulipwa kwa kamisheni maana yake unalipwa kulingana na matokeo unayozalisha. Yaani, kwa mfano kama unafanya kazi mgahawani. Ukiuza sahani 10 na kila sahani unalipwa elfu moja maana yake siku hiyo, utalipwa elfu kumi. Lakini, ukijisukuma zaidi ukauza sahani thelathini maana yake siku hiyo utalipwa elfu thelathini. Huku ndiyo kulipwa kwa kamisheni.

    Yaani, juhudi zako zinakuwa ziaendana na bidii unavyoweka. Kadiri unavyoweka bidii zaidi kwenye kazi ndivyo ambavyo unalipwa zaidi.

    Mbinu hii unaweza kuitumia kama umeajiriwa au umejiajiri.

    Kwa mfano, kama unaona unaweza kuajiriwa kwenye biashara fulani na kumsaidia bosi wako kupata matokeo makubwa zaidi ya anavyopata sasa hivi. unaweza kuongea naye, mwambie kwamba  wewe unaweza kuwa na mbinu ya kusamsaidia kuongeza kipato kwenye biashara yako, lakini sharti akulipe kwa kamisheni. Hii ni nzuri sana maana hakuna anayepujwa. Unalipwa kwa jasho lako. Kadiri unavyoweka juhudi zaidi, ndivyo ambavyo unalipwa zaidi.

    Kama umeajirajiri unaweza kujiwekea lengo. Labda lengo la kufanya mauzo na laki tano kila siku. Na ukajiambia kwamba nikifikisha mauzo laki tano kwa siku basi mimi mmweywe nitajilipa asilimia labda kumi. Kwa hiyo, siku ambayo unakuwa hujafikisha hiyo laki tano, utajilipa kulingana na kiwango ulichoingiza

    Kama umeingiza laki moja basi utajilipa elfu kumi tu.

    Hii ni njia nzuri, japo watu wengi hawaipendi kwa sababu haijazoeleka kwenye mazingira mengi. Lakini pia siyo njia rafiki kwa watu ambao hawapendi kufanya kazi kwa bidii na kujituma zaidi.

    SOMA ZAIDI: Njia Tano Za Kuingiza Fedha Mtaani Kwako Kuanzia Leo

    Je, Kuna Namna Na Kutengeneza Fedha Kupitia Affiliate Marketing Ukiwa Nchini Tanzania?

     

    NJIA YA NANE, ACHANA NA ANASA

    Unaweza kuwa unajiuliza, kwani anasa zangu zina uhusiano  gani na kulipwa zaidi. Tena, unaweza kuhitimisha kwa kusema kwamba, mimi nitaendelea na starehe zangu ila nitafania kazi hayo mengine ambayo umeeleza hapo juu.

    Ninachotaka ni nikwambie ni kwamba, anasa zinapoteza muda wako mwingi ambao ungutumia kwa ajili ya kufanya kazi ya kukuongezea kipato. Anasa zitakufanya upoteze muda kwa wingi. Na muda ni mali.

    Kwa hiyo, achana na kupambana na mambo ya anasa kuanzia leo hii. badala yake pambana na ndoto pamoja na malengo yako. Kila siku hakikisha kwamba unafanya kitu na unakfanyia kazi kila siku. Siku siyo nyingi wa

    Lakini pia ni muhmu cha kufahamu ni kuwa kwanza anasa zinachukua fedha zako.

    pili, anasa zinakupunguzia ufanisi

    Na tatu unapokuwa unapambana na anasa, maana yake unakuwa na pambana na lengo ambalo siyo sahihi. Na hivyo, lengo la kuongeza kipato chako zaidi litakushinda.

    Rafiki yangu, hizo ndizo njia nane za kulipwa mara nane mpaka mara kumi zaidi ya unavyolipwa sasa.

  • Hii Ndiyo Sheri Ambayo Itakusaidia Wewe Kupata Chochote Kile Unchotaka

    Profesa mmoja alifanya kijiutafiti chake binafsi. Zilikuwa ni nyakati za krismasi, hivyo alichofanya ilikuwa ni kuandika kadi za krismasi kwa watu ambao walikuw hawamjui huku akiwatakia kheri ya krismasi.

    Profesa akakaa huku akisubiria majibu. Baadaye alikuja kugundua kuwa asilimia kubwa ya watu walijinu kwa kushukuru kwa kadi ile ya krismasi ambayo alitoa na , ila wengi sana hata hawakumuuliza kuwa alikuwa nani na mawasiliano yao aliyapataje.

    Hiki kitu ndiyo ninataka kianze kutupa mwanga kwa ajili ya somo letu la leo

    Leo tunaizungumzia kamnuni ya RECIPROCAL. Kulingana na kanuni hii ni kwamba, ukifanyia mtu kizuri. mtu huyo anahisi kama ana deni na anapaswa kukulipa kulingana na kile ulichomfanyia.

    Ukimpa mtu labda msaada, anajiona kwamba kuna deni ambalo anapaswa kukulipa kulingana na msaada ambao umempa.

    Hivyo, unaweza kuitumia kanuni hii kwenye biashara yako pia au kwenye kitu ambacho unafanya pia. Kadiri unavyotoa kitu chenye thamani kubwa, ndivyo watu wataona kwamba kama wana deni vile ambalo wanapaswa kukulipa na hivyo utajenga timu ya watu ambao wanakuamini kwenye kile unachofanya na hata wateja wa kudumu.

    Kila la kheri.

  • Nguvu ya uvumilivu

    Kuna ndugu mmoja alianzisha biashara huku akitegemea kwamba watu wangemiminika kwenye biashara yake siku ya kwanza. Ila watu hawakumiminika kama alivyokuwa anatarajia. Siku ya kwanza alitokea mtu mmoja wa kuuliza kuhusiana na biashara yake na kile ambacho anafanya. siku ya pili watu kadha wa kadha pia walipitia na kuangalia kuuliza uliza ila hawakununua.

    Siku ya tatu ndipo alikuja kufanya mauzo ya kwanza.

    Kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusoge ambele ndivyo watu walikuwa wanazidi kuongezeka kwenye kununua kwake.

    Kumbe siyo kwamba kila ukianzisha kitu watu watamiminika kwako na kujipanga ili wapate kitu chako. Hapana, itachukua muda, maana kadiri watu watakavyokuwa wakiona ukiendelea kufanya hicho kitu ndivyo ambavyo hao watu watakuwa wakivutiwa kuja kwako.

    Ukimhudumia vizuri yule mteja wako wa kwanza, atarudi kwako tena siku nyingine. nap engine hatarudi peke yake. Bali atarudi pamoja na rafiki zake na hivyo kuongeza idadi ya watu ambao wanapata huduma kwako.

    Usidharau hizi hatua ndogo ndogo unazopiga. Na usiwe na haraka. Vumilia pale unapokuwa hupati matokeo makubwa mwanzoni huku ukiendelea kuweka juhudi zaidi ili uweze kufikia mafanikio unayoyataka.

    Kila la kheri

  • Vitu Vitano Vitakvyokuwezesha Kupata  Maisha Ambayo Umekuwa Unatamani

    Siku ya leo kuna vitu vitano ambavyo naamini kwamba ukivifanyia kazi, unaenda kuwa na maisha ambayo umekuwa ukiyatamani kwa siku nyingi. Kilichokukwamisha wewe kuweza kupata maisha unayoyataka ni kwa sababu hujafanyia kazi hivi vitu vitano hapa.

     

    Kitu Cha Kwanza Ni Kujua Watu Wanataka Nini. Ukijua watu wanataka nini, wewe pia utaweza kupata kitu chochote kile ambacho unataka. Kivipi unajiuliza, iko hivi, kama kuna kitu ambacho watu wanataka na wewe ukawaletea hicho kitu, ni wazi kuwa hawa watu wantakuwa tayari kukulipia na kwa jinsi hiyo utaweza kutengeneza kipato chako kizuri tu.

     

    Lakini je, unajuaje kitu ambacho watu wanataka.

    Hapa utaangalia vitu ambavyo watu wanapenda kufuatilia

    Vitu ambavyo watu wanapenda kuongelea mara kwa mara

    Matatizo ya watu pia yanaweza kukuonesha vitu ambavyo watu wanataka

    Lakini pia kuna vitu ambavyo kwa asili tunataka. Chakula, mavazi na malazi. Na havitabadilika. Kwa hiyo, angalia ni kwa namna gani ambavyo unaweza

    Kwa hiyo kazi yako ya kwanza kabisa rafiki yangu ni kuangalia watu walio kuzunguka wanataka nini. Ukishajua kitu ambacho watu wanataka, basi wape hicho kitu, na hao watu watakuwa tayari kukulipa.

    Pili Ni Kufanya Hicho Kitu Kwa Ubora Na Ubunifu

    Kuna kanuni ambayo unaweza ukawa hujawahi kuisikia. Inaitwa copy-cut principle. Kulingana na kanuni hii ni kwamba kwa kitu chochote kile ambacho unafanya. , hata kama umeanza kufanya hicho kitu kikiwa kipya, ndani ya miezi sita, kuna watu watakuwa nao wameanza kufanya hicho kitu. Watakopi unachofanya na wataanza kukifanya wao pia.

    Hiki kitu ndiyo kinaitwa copy-cut. Unaweza kuanzisha mgahawa eneo fulani. Ndani ya miezi sita, ukakuta kuna watu watatu au wanne nao wameanzisha migahawa kama wa kwako halafu eneo hilohilo.

    Sasa ili kujitofautisha kwenye kile unachofanya unahitaji kuwa mbunifu na kuhakikisha kwamba unafanya unafanya kile unacahofanya kwa ubora

     

    Lakini ubunifuni ni nini? na utauwekaje kwenye biashara? Hii ni mada ndefu ambayo siwezi kuiongelea yote kwenye hii makala ila kwa leo itoshe kusema kwamba ubunifu ni kufanya vitu kwa namna ta tofauti na vile ulivyofanya jana. Na hapa huhitaji kufanya mapinduzi makubwa kwa wakati mmoja. Badala yake unaweza kufanya marekebisho ya kitu kimoja baada ya kingine, baada ya muda biashara yako ikawa inazidi kuboresheka zaidi.

    Mfano leo hii unaweza kujiweka kwenye viatu vya mteja wako na kuangalia kama ungekuwa mteja kwenye biashara yako, je, ungependa kupata huduma ambayo inatolewa kwenye biashara yako? Kama huduma hiyo hujaipenda basi unaangalia wapi pa kuboresha ili uweze kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wako.

    Lakini pia kesho unaweza kuboresha kipengele cha huduma kwa wateja na kukifanya kuwa bora zaidi.

    Kwa vyovyote vile unakuwa hutulii kwenye hali ileile kila siku. Badala yake unakuwa unazidi kukua na kufanya kitu kwa ubora na ufanisi zaidi.

     

    Tatu Ni Kuwa Na Mwendelezo Wa Kile Unchofanya

    Watu wengi huwa wanapenda kuanzisha vitu ila wanaishia njiani. Sasa naomba unisikilize kwenye hili, bila kujali kwa sasa unapitia kwenye hali gani. kwa vyovyote vile jitahidi kuendeleza ulichoanzisha bila ya kukoma. Kuna watu wengi huwa wanapenda kuanzisha vitu ila huwa wanaishia njiani. Sikiliza, kitu kimoja cha uhakika ni kwamba ukiweza kuwa na mwendelezo wa kile ulichoanzisha, utaweza kufika mbali.

     

    Haijalishi umeanzia wapi, haijalishi umeanzia kwenye hali ya chini kiasi  gani. Bado utaweza kufika mbali na kuona makubwa endapo tu utakuwa na mwendelezo wa kile unachofanya bila ya kuacha.

    Nne Ni Kujifanyia Tathimini

    Ni muhimu sana uwe unajifanyia tathimini kila mara kuona vitu gani ambavyo umefanya na vimefanya vizuri na vitu gani unafanya ambavyo havijaenda vizuri. Na kwa jinsi hii utaweza kuona wapi labda kuna mwanya ili uweze kuuziba, au labda utaona kwamba kuna vitu ambavyo umekuwa unafanya kwa mazoea, na sasa unahitaji kuviboresha na kuvifanya kwa uzuri zaidi.

    Tano, Ukifanya Makosa, Usijishikize Kwenye Makosa Yako. Inuka endelea mbele. Ni kweli huwa tunafanya makosa kwenye vitu ambavyo tunafanya, ila sasa usijishike kwenye makosa yako. Badala yake ukifanya makosa, imuka, kisha songambele ili uweze kufanya makubwa zaidi.

    Kwa leo naishia hapa

    Nakutakia kila la kheri

    Godius Rweyongeza

    0755848391

  • Fanya vitu vichache kwanza

    Kuku anapoatamia mayai anasahau mpaka kula ili tu hakikishe lengo lake la kuatamia na kupata vifaranga linatimia.

    Wewe pia kuna vitu unapaswa kuachana navyo sasa hivi li uweze kufika kule unapotaka kwenda

    Siyo lazima ukimbizane na kila kitu sasa hivi.

    Fanya vitu vichache ambavyo vitekupelekea kwenye lengo na ndoto yako badala ya kukimbizana na kila kitu.

    Kila la kheri

  • Hatua Nane Za Kuwa Mwandishi Mbobevu

    Leo nataka nikupe hatua nane za kuwa mwandish mbobevu.

    1. Andika

    2.  Kila

    3. Siku

    3. Hata

    4. Kama

    5. Ni

    6. Sentensi

    7. Moja

    8. Tu.

    Rafiki yangu unakwama wapi kwenye kuandika. Naamini kwa siku huwezi kukosa hata dakika tano tu za kuanadika hata kama unaandika kitu kidogo.

    Unahitaji kuandika kila siku kwa sababu kadiri unavyoandika kila siku ndivyo unavyozidi kubobea zaidi kwenye uandishi wako.

    Je, upo  tayari kuanza marathon ya uandishi? Basi anza leo hii kwa kuandika hata utambulisho wako kwa kifupi na kitu ambacho utakuwa unaandika.

    Unaweza kunishirikisha kwenye whatsap  0755848391

    Godius Rweyongeza

X