Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • KITABU:MAAJABU YA KUWEKA AKIBA: Jinsi Tabia ya Kuweka Akiba Inaweza Kukufanya Uwe Tajiri

    Mwaka juzi (2020) niliandika kitabu cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA. Kwenye kitabu hiki niliandikabutangulizi huu hapq chini ambao Leo hii bado una nguvu kubwa aawa na nilipouandika.

    “Tangu umezaliwa mpaka leo hii, ni unaposhika kitabu hiki mikononi mwako ni wazi kuwa fedha nyingi tayari zimepita mikononi mwako. Hivi laiti ungekuwa umeweka utaratibu wa kuwa unatoa kiasi kidogo kwenye kile ambacho unapokea na kukiweka kama akiba, unadhani leo hii ungekuwa na kiasi gani?

    Niliwahi kumwuliza dada mmoja swali hili hapa, akawa amefikiri kwa muda, kisha akaniambia, “Loo! Ningekuwa na fedha nyingi sana”. Bila shaka na wewe utakuwa na majibu kama hayo ambayo huyo dada alikuwa nayo.

    Kila mtu huwa anapokea fedha kwa viwango tofauti, japo kiasi ambacho unapokea sasa hivi kinaweza kuonekana kidogo. Lakini ukiweka utaratibu wa kuweka akiba kutoka kwenye hicho kidogo, ni wazi kuwa itafikia hatua ambapo hicho kidogo kitakuwa kikubwa.

    Ni imani yangu kuwa baada ya kuwa umesoma kitabu hiki hapa, utachukuka hatua na kuanza kuweka akiba bila ya kuchelewa. Nipo nafikiri tu kuwa kwa mfano, ukimfundisha mtoto wako misingi ambayo utajifunza humu ni wazi kuwa mpaka anakuja kufikisha miaka 18 au 20 basi atakuwa ameweka akiba ya kutosha kumfanya hata aweze kujilipia ada ya chuo kikuu bila kuhitaji mkopo wa chuo. Na kwa sababu atakuwa amejenga msingi imara basi ni wazi kuwa bado kiasi zaidi kitakuwa kinazidi kuingia kwake.”

    Rafiki yangu hayo ndiyo maneno kuntu niliyoandika mwaka 2022. Leo hii nimeguswa na umuhimu wa maneno haya kiasi kwamba, nikaona nitalete kwako. Yasome na uyaweke kwenye vitendo. Kikubwa zaidi hakikisha UMESOMA KITABU CHA MAAJABU YA KUWEKA AKIBA. Kinapatikana kwa elfu 5 tu na Ni softcopy.

    Tuma fedha kwa namba 0755848391 jina Ni GODIUS RWEYONGEZA

  • Hakuna mwenye kipaji cha kila kitu

    Hakuna mwenye kipaji cha kila kitu na wala hakuna anayeweza kila kitu.

    Usitake kujihangaisha na kuonesha kuwa wewe ndiye wewe kwenye kila kitu. Kuna vitu vichache unaweza kuvifanya vizuri

    Weka juhudi zako hapo.

    Vingine waachie wengine.

    kupata ebook ya KIPAJI NI DHAHABU tuma elfu tano kwenda 0755848391 ili utumiwe ndani ya dakika tano bila kuchelewa.

  • Jinsi ya kupata chochote unachotaka

    Rafiki yangu habari ya leo. Bila shaka unaendelea vyema kabisa. Zig Ziglar aliwahi kunukuliwa akisema kuwa unaweza kupata chochote unachotaka kama utawasaidia watu kupata kile wanachotaka. Yaani, kauli hii fupi laiti ingefahamika kwa watu vizuri basi kila mtu alipaswa kufurahi maana kauli hii imebeba siri kubwa.

    Kama hujajua siri iliyobebwa kwenye kauli hii naomba utulie ili mimi leo hii nifanye tu kukudavulia na kikuwekea mezani kila kitu.

    Labda kwanza nikuulize ni kitu gani unataka? Ni vigumu kupata kitu ambacho wewe mwenyewe hujui. Unapaswa kwanza kufahamu kitu unachotaka kwanza, ndio ukipate.

    Kinachowafanya watu wengi waishi maisha ya kawaida Ni kwa sababu tu wanaishi maisha hovyo have hovyo tu bila ya kuwa mpangilio.

    Kama kuna njia ya wewe kupoteza maisha yako bila kupata chochote cha maana, Ni wewe kuishi bila hata kujua kitu gani unataka.

    Unawezaje Sasa kupata chochote unachotaka?
    Kwa hiyo kwanza kabisa jua kitu chenyewe unachotaka. Na hiki linawezekana kupitia kuweka malengo. Kuweka malengo ni hatua ya kwanza ya kubadili yasiyoonekana kuwa yanayoonekana.

    Anza leo kwa kuweka malengo? Unajiuliza namna gani unaweza kuweka malengo?

    Pili ni kutoa thamani kwa watu.
    Watu wanatafuta na kupata fedha kwa taabu . Na hawapo tayari kuitumia hiyo fedha yao kwa mambo ambayo siyo ya muhimu sana. Au yale ambayo wanaona wazi kuwa hayawezi kuwa na thamani kwao.

    Kwa hiyo unapaswa kuwa tayari kutengeneza vitu ambavyo vina thamani na ambavyo watu wakinunua kwa hela yao, hasi waone wazi kuwa kweli fedha yao haikwenda bure.

    Tatu, tatua matatizo yao.

    Hakuna mtu AMBAYE anapenda kukaa na kusumbuliwa na matatizo. Hiki ni kitu kingine ambacho unapaswa kukifahamu. Ukiweza kutatua matatizo ya watu, watu watakuwa tayari kukulipa. Ni hivyo utakuwa na uwezo wa kupata chochote unachotaka.

    Je, una maswali au maoni?
    Tuandikie: godiusrweyongeza1@gmail.com
    Au WhatsApp: 0755848391

    Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • Kipaji ni dhahabu-4: Kipaji Hakifanyiwi Kazi Kwa Siku Moja

    Najua kuna wengi wangependa wagundue kipaji chao Leo hii na kesho yake wawe tayari wamekuwa mabingwa.

    Hapana. Inachukua muda. Unahitaji muda kukinoa kipaji chako.

    Kifanyie kazi kipaji chako kila siku.

    Wewe wa leo hapaswi kuwa sawa na wewe wa jana na wiki ijayo. Kila wiki iwe wiki ya tofauti kidogo.

    SOMA ZAIDI: Kipaji ni dhahabu-3 njia ya kuwa gwiji

  • Jinsi Ya Kutengeneza Fedha Mtandaoni

    Moja ya swali ambalo niliwahi kujiuliza miaka mingi iliyopita, lilikuwa ni namna gani naweza kutengenwza fedha mtandaoni?

    Kiukweli swali hili lilipa shauku ya kutaka kujua mengi.

    Kipindi hicho nilikuwa nasikia habari kuwa akina Millard Ayo wanalipwa kupitia mtandao.
    Sasa swali langu lilibaki, na mimi nawezaje kulipwa mtandaoni.

    Swali hili lilinifanya niianze kujifunza kupitia kusoma maandiko mengi mtandaoni pamoja na vitabu. Baada ya miaka kadhaa ya kufanyia kazi yote niliyojifunza. Sasa ningependa kukupa na wewe mwongozo ili usihangaike tena kwa kujiuliza unawezaje kutengeneza fedha mtandaoni?

    jinsi kutengeneza fedha mtandaoni

  • Vyeti Vya Hisa Vinaenda Kusitishwa Kutolewa

    Unaendeleaje rafiki yangu. Leo nina taarifa muhimu kwako ambayo unapaswa kuifahamu kama mwekezaji.

    Hata hivyo, utaratibu mpya unaenda kuanza tarehe 1 mwezi ujao (April) Ni kwamba utakuwa hutumiwi cheti cha hisa kama ilivyokuwa mwanzo. Badala yake utakuwa uwekezaji wako kiujumla.

    Wewe unasemaje kuhusu hili?

    Binafsi nimeipenda hili maana kila utakapokuwa ukiwekeza utakuwa unapata taarifa ya sehemu ulipofikia kwenye uwekezaji na hivyo kukupa Moto wa kujituma zaidi ili ukuze uwekezaji wako.

    Anza kuwekeza Leo kwa kusoma ebook ya MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Rusha elfu tano tu kwa 0755848391 ili nikutumie ebook hii.

  • Mafanikio yanachukua njia ndefu

    Ndio inachukua muda, lakini sasa hakuna jinsi. Hii ndio njia nzuri ya kufika kule tunapotaka. Njia nyingine fupi zipo ila sasa siyo za kuaminika na wala hazikupi matokeo ya kudumu.

    Kwa hiyo njia pekee ya kufika mbali ni kuhakikisha unachagua njia sahihi na kuifuata hata kama inachukua muda. Njia fupi zina matokeo ya haraka yasiyodumu.

  • Kipaji ni dhahabu-3 njia ya kuwa gwiji

    Njia pekee ya wewe kuwa gwiji kwenye kufanyia kazi kipaji chako ni kufanya mazoezi mara kwa mara bila kuacha.

    Kadiri unavyofabya mazoezi ndivyo unavyozidi kuwa imara zaidi na kubobea.

    Usichoke kukifanyia kazi kipaji chako.

  • Kafanyaje nini huyu?-2

    Mwaka wa tatu jamaa yupo mtaani Hana ajira

    Ebu fikiria hili. Unaenda shule, unasoma kwa bidii huku ukiwa unategemea upate ajira ya maana, mara unamaliza chuo na ajira haipo!

    Unasubiri mwaka wa kwanza unapita huku ukiwa umetuma maombi ya kutosha.

    Unataka kuanzisha biashara, unakuta kwamba mtaji huna! Hiki kitu tu, lazima kitakupa pressure.

    Ione mitaji yenyewe hapa

  • Kafanyaje huyu?

    Kapata pressure baada ya biashara yake kutofanya vizuri!

    Tafiti zinaonesha kuwa Kati ya biashara 10  zinazoanzishwa biashara tano hufa ndani ya mwaka mmoja na nyingine ambazo hubaki huwa hazifikishi miaka 10.

    Hili wewe mwenyewe lifuatilie mtaani kwako. Utakuta kwamba kuna biashara nyingi zinazoanzishwa  baada ya muda kidogo zinapotea.

    Hii ndio kusema kwamba usipokuwa makini wakati unaanzisha biashara, utajikuta kwamba na wewe unakuwa miongoni mwa hizo takwimu za biashara kufa ndani ya mwaka.

    Sasa yafutayo ni mambo muhimu ya KUZINGATIA Unapokuwa unafanya biashara.

    Hakikisha biashara yako inakuwa kipaumbele kwako. Yaani, biashara yako itunze kama unavyomtunza mtoto mchanga.

    Kila mwezi mtoto anapelekwa kliniki ili kupimwa baadhi ya vipimo.

    Wewe pia kila mwezi ipime biashara yako. Pima mauzo yako. Mtaji unaozunguka. Pima mauzo yaliyofanyika na wateja walionunua pamoja na masoko yaliyofanyika ikiwa ni pamoja na matokeo ya masoko.

    Kitu hiki kidogo kitakupa mwongozo wa biashara ilipotoka na inapoelekea. Na utaepuka biashara yako kufa ndani ya mwaka mmoja.

    Pata kitabu changu cha MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA KUANZISHA BIASHARA. Utajifunza mengi ya kukusaidia kuanzisha na kukuza biashara yako. Kitabu hiki ni ebook na kinapatikana kwa elfu 5 tu. Rusha elfu 5 kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

X