Home


  • Hiki Ni kitu muhimu ambacho unapaswa kukitafuta kwenye kila kitabu

    Rafiki yangu usomaji wa vitabu ni kitu muhimu sana kwa ajili ya afya ya akili yako.

    Ukitaka kufurahia usomaji wa vitabu basi kwenye kila kitabu ambacho unasoma hakikisha unapata unapata vitu vitatu ambavyo unaweza kufanyia kazi Mara moja.

    Ukipata vitu hivi mwanzoni mwa kitabu, unaweza kuweka kitabu pembeni kwanza na kufanyia kazi kile ulichojifunza utakuja kuendelea nacho siku nyingine.

    Kwa hiyo rafiki yangu. Kama kwenye kila kitabu chako. Unachosoma tafadhali sana tafuta vitu vitatu vya kufanyia kazi Mara moja.

    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • Jinsi ya kuendeleza kipaji chako

    Habari ya leo rafiki yangu. Hongera sana kwa siku ya leo na siku ya kipekee sana.

    Leo nataka nikueleze namna ambavyo unaweza kuendeleza kipaji chako kwa viwango vikubwa mpaka kufikia hatua za kukifanya kikutoe. 

    Lakini kwanza tujiulize kipaji ni nini?
    Kujibu swali la kipaji ni nini naomba usome makala hii hapa ambayo imeeleza kwa kina kuhusu kipaji. Au pia unaweza kusoma Makala hii hapa.

    Sasa baada ya kujua kipaji ni nini tuone unawezaje kukiendeleza.

    Zipo njia kadhaa  Ila njia ya kwanza ni kutenga muda wa kukifanyia kazi kipaji chako kila siku.

    Unaweza kutenga hata nusu saa tu kwa ajili ya kunoa kipaji chako.

    Pili ni kufanya mazoezi endelevu. Ni kweli umetenga muda maalumu kwa ajili ya kipaji chako. Lakini fahamu kuwa hilo peke yake halitoshi. Na hapo ndipo wewe unahitaji kuwa na nidhamu ya kufanya kitu ulichopanga bila kukosa.

    Tatu, kwenye ulimwengu wa sasa mambo mengi ya yamehamia mtandaoni. Hivyo, na wewe kiweke kipaji chako mtandaoni.
    Fungua akaunti kwenye mojawapo ya mitandao ya kijamii.
    Tengeneza blogu
    Fungua akaunti Google my business.

    Yaani, kiufupi weka urahisi wa watu kukupata wanapokuwa wanaokihitaji uwasaidie na kipaji chako.

    Kila la kheri
    Godius Rweyongeza
    0754848391

  • Karibu Sana

    Hello! Tumekutumia kitabu kwenye barua pepe yako. Sasa hivi kitakuwa kimeshafika lakini kama hutajali, hapa nimekuwekea baadhi ya makala ambazo zimesomwa Sana

    Godius Rweyongeza

    0755848391

  • THINK BIG FOR AFRIKA

    Karibu kwenye kundi maalumu la whatsap la Think Big For Afrika! maelezo zaidi ya kina yanakuja hapa hapa baadaye. Au wasiliana na 0755848391 ili akupe maelekezo sasa.

  • WATU WANASEMAJE KUHUSU KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI?

    MIMI NAMFAHAMU GODIUS

    Ninamfahamu Godius si tu kwa kupitia maandishi yake bali kwa kupitia maisha yake. Jinsi anavyoishi ni darasa tosha la mtu yeyote mwenye nia ya kufanikiwa.

    Nilipoanza kusoma kitabu hiki sikukoma kuacha kwani kimegusa maisha yangu na baadhi ya mambo niliyoyapata humo nimeanza kuyafanyia kazi na nimeanza kuona maajabu makubwa.

    Unataka kuwa mbunifu? Soma kitabu hiki. Unataka kuwa kinara kwenye kipaji chako? soma kitabu hiki?

    Unataka kuwa kiongozi kwenye maisha yako? Soma kitabu hiki.Unataka maisha yenye furaha na ya kuacha alama? Majibu yote yanapatikana humu kwenye Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni.

    Imani yangu ni kwamba unaweza kuanzia hapo ulipo na kufika popote ili mradi akili yako umeipa ruhusa. Kila mtu amezaliwa mshindi, hakuna aliyekuja duniani kuwasindikiza wengine. Wewe ni wa tofauti, kuwa wewe, acha kujilinganisha na wengine, kujilinganisha kunabagua.

    Asante sana Godius Rweyongeza kwa kitabu hiki kinachotafakarishi, kinachotia hamasa na kinachotupa dira ya kuishi maisha kwa utimilifu.

    Edius Katamugora Mtunzi Yusufu Nina Ndoto


    MWANDISHI KATUMIA LUGHA NYEPESI KUONGEA MAMBO MAKUBWA YA KIMAFANIKIO

    Kila binadamu ndani kabisa ya moyo wake ana tamanio kubwa la kufanikiwa, yaani ikutoka ngazi ya chini kwenda ngazi ya juu katika Nyanja mbalimbali za Maisha. Kwa lugha nyepesi “Kutoka sifuri mpaka kileleni.

    Lakini changamoto kubwa inayowakabili watu wengi ni njia sahihi za kupita au kanuni za kufuata ili kufikia hatima hiyo.

    Mwandishi Godius Rweyongeza amejaribu, kwa kadri ya uwezo wake, kutumia lugha nyepesi na mifano halisi ya kumsaidia mtu kuweza kufuatana kutimiza azma ya mafanikio. Amezungumza kiundani jinsi ambavyo binadamu anaweza kutumia uwezo wa utashi aliopewa na Mwenyenzi Mungu katika kujiletea maendeleo binafsi katika Nyanja zote za Maisha.

    Ni matumaini yangu kuwau naposoma kitabu hiki utaweka katika matendo yale yote utakayojifunza ili uweze kupata matokeo bora yatakayokuwa chachu chanya kwa wengine pia.

    Nakutakia usomaji mwema na utekelezajiwa yale yote utakayojifunza.

    Anthony Luvanda

    Mjasiriamali na Mhamasishaji.

    Anzisha Biashara, Endesha Na Kuza Biashara Yako, Ufikie Ndoto Zako


    KAMA HUJUI NAMNA YA KUWEKA MALENGO, MWANDISHI AMEKUSAIDIA KUFANYA HIVYO KWENYE KITABU HIKI.

    “Usipowaambia watu kuhusu mafanikio yako bila shaka hakuna atakayekuja kuyajua” Donald Trump

    Acha Mimi nikuambie mafanikio yangu ili uyajue kupitia kitabu hiki cha kutoka sifuri hadi kileleni. Ukitaka kujua mafanikio yako anza kusoma kitabu hiki cha kutoka sifuri hadi kileleni. Kwani utagundua uwezo mkubwa wa kufanikiwa ulioko ndani yako, kwanini unajichelewesha kupata ushindi ambao uko ndani yako?

    Kama hujui kabisa namna ya kuweka malengo hatua kwa hatua ili yaweze kukusaidia kutoka sifuri hadi kileleni, basi mwandishi na mtaalamu wa kilimo cha bustani (Horticulture) Godius amekusaidia kufanya kazi hiyo kwenye kitabu chake cha kutoka sifuri hadi kileleni.

    Ukiona mtu amefanikiwa kutoka sifuri hadi kileleni jua kuna siri kubwa nyuma ya ushindi.

    Ninapendekeza kila anayetaka kufanikiwa, na hajawahi kusoma kitabu chochote kile basi kitabu hiki ni cha lazima kusoma kwa mtu makini anayeanzia chini kabisa na kutaka kufikia kileleni. Ni kitabu kinachokuonesha  mchakato wa mafanikio kutoka sifuri hadi kileleni.

    Kila la heri rafiki yangu katika usomaji wa kitabu hiki.

    Mwl. Deogratius Kessy

    Mwalimu, Mwandishi na Mjasiriamali.

    http://kessydeo.home.blog


    HIKI NI KITABU CHA KARNE YA 21

    Kujitoa bila kujibakisha, kusimamia jambo bila ya kurudi nyuma,  pamoja na kugundua uwezo wa ajabu aliouweka Mungu ndani yako, hivi vitakusaidia kufika hapo unapotaka kufika.

    Kitabu hiki kimeanza kwa kwanza kwa kumsukuma mwandishi ujiuliza kwa nini wengine wamefika walipokusudiwa na wengine hawafiki, majibu yake yakiwa ndani ya kitabu hiki, yanagusa kuhamasisha na kufundisha, hiki ni kitabu cha karne ya 21,hivyo kila mmoja anapaswa kukisoma.

    Mwalimu Adebert Chenche

    Mwenyekiti wa taasisi ya VIPAWA LINK ASSOCIATION


    NI KITABU CHENYE MAARIFA MENGI SANA.

    Ni kitabu chenye maarifa mengi sana. Kwa uhakika atakayekisoma na kuyafanyia kazi ataweza kupiga hatua kubwa katika kutimiza malengo yake

    NTANGEKI NSHALA


  • Jinsi Ya Kutengeneza Bahati Yako

    Dunia ina tabia ya kukupatia kitu kama utaonesha nia, kuwa wewe ungependa kupata hicho kitu. Huwa ninapenda kuwaambia watu kuwa, hata kama ni bahati itakukuta njiani unatembea wala sio chumbani kwako ukiwa umelala. Kwa hiyo, wewe kama unahitaji kupata bahati maishani mwako basi kuwa tayari kuweka kazi inayoendana na bahati unayotaka. Bahati unaitengeneza wewe mwenyewe na vitendo vyako ndivyo vinapaswa kuonesha hilo.

  • Vitu Vitano Kuhusu Fursa

    Leo nataka nikueleze vitu vitano muhimu unavyopaswa kufahamu kuhusu fursa. Watu wengi wamekuwa wanahadaiwa linapokuja suala zima la fursa.

    Kuna watu wamekuwa wanatumia mlango wa kuita haadhi ya vitu fursa ili wakupate.

    Kuna watu unakuta wanataka fedha zako, wanaangalia namna nzuri ya kuzipata, wanaona wanaweza kukupata kwa kukwambia kuwa kuna fursa ambayo unaweza kuifanyia kazi. Unahadaika, kumbe kitu chenyewe siyo fursa. Bali wewe mwenyewe ndiyo ulikuwa fursa.

    Ndio maana nimekuandalia vitu vitano unavyopaswa kujua kuhusu fursa. Hivi hapa

  • Jinsi ya Kuipangilia Ratiba Yako Vizuri Kuanzia Leo

    Njia bora ya Kuipangilia Ratiba Yako Vizuri ni kujiuliza ni

    1. vitu gani vya muhimu ambavyo napaswa kufanya.

    2. Vitu gani vya kufanya japo siyo muhimu sana.

    3. vitu gani ambavyo wanaweza kufanya wengine.

    4. Na ni vitu gani ambavyo wengine wananitaka nifanye.

    Mara zote weka nguvu zako kwenye namba 1 na namba 2.

    Kwa vitu ambavyo wanaweza kufanya wengine; wape wavifanye.

    Achana na vile ambavyo wengine wanakutaka uvifanye.

    Maisha ni mafupi kuyaporeza kwenye shughuli ambazo siyo muhimu.

  • Naomba ushauri Nifanyeje?

    Bila shaka wamewahi kutokea watu wa kukuomba ushauri maishani mwako.

    Na pengine wewe ulitoa huo, ushauri. Ila sasa una hakika kuwa wewe ulikuwa hauhitaji huo ushauri?

    Kama huwa inatokea kuwa unatoa ushauri kwa watu ambao wewe mwenyewe unauhitaji. Hakikisha unaanza kuutumia mwenyewe.

    Ukimshauri mtu kuweka AKIBA, wewe mwenyewe weka akiba.
    Ukimshauri mtu kufanya mazoezi wewe mwenyewe fanya mazoezi

    Ukimshauri mtu kula vizuri, kama profeda jay alivyomshauri ferooz kwenye wimbo wa starehe, hakikisha na wewe unafanya hivyo.

    Ni hivyo tu?

    Umekuwa nami
    Godius Rweyongeza
    0755848391

  • Kitu kingine kimoja cha ziada kuhusu Masoud Kipanya

    Au wewe hukupenda….

    Nashukuru wengi waliipokea vizuri mkala ya Jana, hata hivyo leo nimeona nitaongeza kitu kimoja.

    Unachopaswa kufahamu ni kuwa sijalipwa na mtu yeyote kuandika ninayoandika. Ninaamdika mwenyewe tu kwa mapenzi yangu. Ni hivyo tu….

    Kitu chenyewe ninachotaka ujue ni kuedesha BIASHARA kitalaam tangu siku ya ya kwanza (day one)

    Umeelewa hapo au nirudie.

    Ukiangalia hapo utagundua kwamba japo ndio kwanza kampuni yake inaanza, ila tayari ana timu ya mauzo, ana timu ya uzalishaji, mkurugenzi msaidizi,
    Logo n.k.

    Hapo unagundua kitu kikubwa ambacho BIASHARA nyingi zinakosa. Mfumo sahihi wa kuendesha Biashara.

    Ebu niambie, wewe kwenye BIASHARA yako una mkurugenzi wa uzalishaji.
    Mkurugenzi wa masoko na mauzo
    Mkurugenzi mkuu na msaidizi wake
    Biashara yako ina logo?

    Najua unaweza kujitetea kwa kusema kuwa biashara yako ni ndogo, ila unachopaswa kufahamu ni kuwa kama una ndoto na mpango wa kuipeleka mbali biashara yako, utapaswa kuipangilia kihivyo.
    Utapaswa kuwa na meneja wa uzalishaji hata kama unafanya biashara ya rejareja.
    Utapaswa kuwa na meneja wa masoko hata kama uko peke yako kwenye biashara!

    Unaona eeh!

    Najua utaanza kuniambia, ooh unajua BIASHARA yangu siyo kama ya Masoud. Shauri yako…

    BIASHARA yotote unahitaji hivyo vitu.

    Tatizo lalo wewe unafanya vitu kienyeji halafu ukiambiwa, unakuwa mhishi kweli….

    Ka uko peke yako utapaswa kugawa majukumu yako na kila Mara ujue ni lini unafanya majukumu kwenye idara gani.
    Ukienda kununua bidhaa, ujue kabisa kwamba hapo upo kwenye uzalishaji kwa biashara za rejareja na jumla.

    Ukiwashawishi wateja waje kwenye biashara yako, hayo ni masoko.

    Ukiuza hayo ni mauzo

    Fahamu hivi vitu, vitakusaidia weww kuendesha biashara yako kitalaamu.

X