Home


  • Niseme kitu kuhusu Elon Musk  Kununua Twitter Au Basi!👇🏿👇🏿

    Udhaifu wangu mkubwa Ni kwamba ninapokuwa na kitu kikubwa kinachoweza kukusaidia wewe kufanya makubwa siwezi kukaa nacho!

    Nashindwa kabisa  kujizuia,  Ndio maana leo nikaona nikujuze habari za Elon Musk

    Habari zilizotawala vyombo mbalimbali vya habari na hasa mtandao wa intaneti siku ya jana ni kuhusu bilionea Elon Musk kuwekeza kwenye kampuni ya Twitter. Ambapo amenunua asilimia 9.18%

    Kitu kinachomfanya yeye kuwa mwekezaji mkubwa kwenye hiyo kampuni.

    Kama ulikuwa hujui Ni kwamba: ukiwa mwekezaji mkubwaa kwenye kampuni maana yake unakuwa na nafasi ya kufanya maamumizi kwenye kampuni, unakuwa na uwezo wa kupush baadhi ya mambo kwa kutumia wingi wa hisa zako.

    Asilimia 9.18 haimfanyi Elon Musk kuwa na maamuzi kamili juu ya kampuni ya Twitter. Maana ili uwe na maamuzi kamili unapaswa kuwa na walau asilimia 51 ya kampuni ila inafanya usemi wake kwenye kampuni kuwa na uzito mkubwa.

    Kuna mambo mawili tu nataka ujifunze kutoka kwa Elon Musk siku ya leo kuhusiananna hiki kitu…

    1. Ukiamua kuwekeza wekeza
    Umeshafuatilia Elon Musk amewekeza kwenye kampuni gani na ana umiliki kiasi gani? Kwenye kampuni yake ya Tesla ana umiliki wa asilimia 17 na SpaceX ana umiliki wa asilimia 54.

    Hiki ni kiashiria kuwa huyu jamaa hawekezi kwenye kampuni yoyote kama underdog badala yake anafanya uwekezaji mkubwa haswa.

    Hiki kitu kikupe picha na wewe unapofanya uwekezaji. Usiwe mtu wa kufanya uwekezaji wa kudonoa, donoa badala yake amua kufanya uwekezaji mkubwa na wa viwango vya juu bila kuacha.

    Hata Kama utakuwa unaanza kidogo, wewe endelea tu kuwekeza kila mara bila ya kurudi nyuma hata kidogo.

    2. Ukiamua kufanya kitu kifanye vizuri

    Elon Musk amekuwa na historia ya kufanya vizuri kwenye makampuni yake, kitu ambacho kimewapa watu imani alipowekeza  twitter, na hapo watu wanaona kwamba  hata huku anaenda kuleta mabadiliko makubwa.

    Imani hiyo tu imefanya hisa za kampuni ya twitter kupanda.

  • Leo Na Mimi Nataka Niseme Kitu Kuhusu Gari Ya Masoud Kipanya

    Watu wenye kichaa cha kutosha kiasi cha kufikiri wanaweza kuibadili dunia, ndio ambao huibadili-Steve Jobs kwenye tangazo la THINK DIFFERENT la mwaka 1997-2002

    Takribani siku mbili zilizopita Masoud kipanya alizindua gari ya umeme ya kampuni ya Kaypee Motors. Kitu ambacho ni cha kipekee sana hasa kwenye mazingira yetu. Asubuhi ya leo nilipotazama hotuba yake wakati anazindua gari yake,ilikuwa ni kama naangalia hotuba ya Steve Jobs akizindua iphone ya kwanza kabisa mwaka 2007. Ilikuwa inahamaisha lakini pia inakufanya wewe uweze kufikiri kwa ukubwa zaidi na wakati huohuo unaona kwamba yajayo yanafurahisha.

    Sasa kwanza lazima tukubaliane kwamba gari ya Masoud na kitu alichofanya kiujumla ni kitu ambacho kinawasha moto miongoni mwa vijana wengi wa kitanzania wenye ndoto kubwa. kitu hiki kinastahili pongezi na ndio maana nimeandika makala hii…

    Kwa kawaida vitu hivi huwa vinaonekana vigumu pale kunapokuwa hakuna mtu ambaye amewahi kuonekana akifanya vitu vya tofauti. Ila sasa anapotokea mtu katika jamii yenu akafanya kitu cha tofauti basi kinakuwa ni kiashiria kuwa wengine pia wanaweza na hivyo, watu wengine  watajitoa kuhakikisha kwamba wanafanyia kazi ndoto zao.

    Jamii nyingi za kitanzania na za kiafirika kiujumla zimeaminishwa kwamba kuna vitu ambavyo huwezi kufanya kwenye maisha yako bila ya kuwa msaada wa mtu yeyote nyuma yako. Na kiufupi inaaminika kwamba vitu vingine wanaweza kufanya wazungu tu na siyo waafrika au watanzania.

    Ndio maana ukizunguka mtaani utasikia watu wanasema maneno kama kazi ya mzungu, utasikia wengine wakisema kwamba mzungu noma.

    Nimekuwa nikisisitiza kwa watu kupitia makala zangu mbalimbali kuwa kila mtu ana uwezo mkubwa uliolala ndani yake ambao anaweza kuutumia kufanya makubwa. Ila watu wengi wamekuwa hawatumii uwezo huu na hii inatokana na sababu mbalimbali ikiwemo jamii zetu ambazo haziamini katika ndoto na vitu vikubwa,. Na hata mfumo wa shule.

    Lakini tafiti zimeonesha kuwa hata wale ambao wanaonekana wamefanya makubwa hapa duniani, siyo kwamba wanakuwa wametumia uwezo wao wote, bali wanakuwa wametumia chini ya asilimia kumi tu ya uwezo wao.  Sasa sijui wewe unatumia asilimia ngapi ya uwezo wako. Ila kikubwa ni kwamba ukikazana tu hata kutumia asilimia kumi ya uwezo wako, utaweza kufanya makubwa sana.

    Na unachopaswa kufahamu ni kwamba uwezo wako hauwezi kuutumia ukaisha. Kadiri unavyoutumia ndivyo unavyozidi kubarikiwa zaidi. Labda swali la uchokozi tu, umeshawahi kusikia kwamba Masoud ameacha kuchora kwa sababu kaishiwa na mawazo (ideas) za kuchora! Au kwamba hajaweza kuchora kwa sababu ametumia uwezo wake wote umeisha? Umewahi kusikia hilo..

    Unachopaswa kufahamu ni kwamba kadiri unavyotumia uwezo wako, ndivyo uwezo wako unavyozidi kuongezeka zaidi… hata kama ungekuwa unaishi miaka buku, bado tu uwezo wako ungekuwa unazidi kumeremeta! Ndio maana hautakaa usikie kwamba Masoud ameshindwa kuchora kwa sababu kaishiwa…

    Labda aamue tu.

    Sasa na wewe ungeweza kuutumia uwezo huu wala si ungefika mbali?

    Kwa maoni yangu kitu alichofanya Masoud ni mapinduzi makubwa na moto ambao ameuwasha kwa vijana wengi wa kitanzania. Siku siyo nyingi vijana wengine zaidi watakuwa wakizipambania ndoto zao siyo tu kwa kuanzisha vitu na kuishia njiani, bali kwa kuhakikisha kwamba wanazifanyia kazi ndoto zao mpaka zinatimia.

    Na kwa leo nimeona niandae mambo sita makubwa ya kujifunza kutoka MASOUD KIPANDA NA NDOTO YAKE YA GARI LA UMEME.

    KWANZA; KABISA NI KUWA NDOTO KUBWA.

    PILI; ANZA KUFANYIA KAZI NDOTO ZAKO

    Uwepo wa mitandao ya kijamii umekuwa ni baraka na wakati huohuo umekuwa kama karaha vile. Mtu akifikiri kufanya kitu hata kama hajakiweka kwenye vitendo anaingia mtandaoni na kuanza kujitangaza.

    Ndio maana ukiingia kwenye mitandao ya kijamii kama facebook, twitter na instagram utakutana na vitu vya ajabu  kweli.

    Kuna watu ambao wanajiita wajasiriamali wakiwa hawajawahi kufanya biashara yoyote ile maishani mwao. Ila ukiangalia profie zao wanajiita maCEO wa kampuni.

    Kuna watu wanajiita waandishi wakiwa hawajawahi kuandika hata sentensi moja.

    Kuna watu wanajiita wachoraji wakiwa hawajawahi kuchora hata mchoro kimoja. Unajua kwa nini?

    Kwa sababu ni rahisi kuongea kuliko ilivyo rahisi kufanya.

    Sasa ninachotaka wewe ufanye siyo tu uwe muongeaji, bali uwe mtu wa vitendo. Na hili unaweza kulifanya.

    TATU IPE NDOTO YAKO MUDA

    Kuna mtu anapenda akiwa na ndoto kubwa leo hii, kesho yake awe ameifanikisha. Siyo kweli. Ndoto kubwa inachukua muda na inahitaji muda kuweza kuifikia.

    Kila mara nimekuwa nikiongea na vijana na kuwauliza una mipango gani miaka mitano au kumi ijayo. Ila cha kushanganza ni pale ambapo mtu anakushangaa. Utakuta mtu anasema yaani, wewe unaongelea mambo ya miaka 10 ijayo leo hii?

    Mwingine atakwambia “mimi nahangaika na leo, kesho itajipa yenyewe”.

    Ngoja nikwambie kitu.

    Kama unataka kufanya makubwa na kama unataka kufika mbali, kuwa na ndoto kubwa ambayo unaifanyia kazi.

    Inaweza kuchukua muda kufikiwa, ila ukweli ni kwamba inawezekana.

    jinsi ya kufikia ndoto zako
    Kupata kitabu hiki wasiliana nami kwa 0755848391

    NNE; KUBALI KUANZIA CHINI

    Ndio unapaswa kuwa na ndoto kubwa, ila unapaswa kuwa tayari kukaa chini na kuanza kuifanyia kazi ndoto yako hata kwa kuanzia chini.

    Ndoto kubwa haifanyiwi kazi kwa siku moja na kukamilika. Unahitaji kuanzia chini, unapaswa kuanza na kile ulichonacho na kukifanyia kazi na kisha kuendelea kukuza kile kidogo ulichonacho.

    Na sehemu nzuri ya wewe kuanzia ni kuanza kuitumia MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA sasa hivi.

    TANO;UKISIBURI MSAADA UFANYIE KAZI NDOTO YAKO, UTASUBIRI SANA

    Yaani, sijui ni nini huyu alikuja na hili suala la misaada. Unakuta mtu anataka akaombe msaada wa kufanyia kazi kila kitu ambacho anakifirikia kwenye maisha yake.

    Muda mwingine kuna vitu ambavyo unaweza kuanza kuvifanyia kazi bila hata ya kuhitaji msaada. Unaweza kudhani unahitaji msaada, kumbe huo msaada wenyewe utaishia tu kukuharibu na kukufanya ushindwe kufanikisha ndoto zako.

    Ujue hili suala la misaada linafanya watu wasifikiri nje ya boksi. Unakuta mtu ana vitu vya kumsaidia kufanikisha ndoto yake ila tu kwa sababu akili yake ameiaminisha kuwa bila msaada haiwezi, utakuta kwamba anaendelea kusubiri msaada.

    Nakumbuka niliwahi kukutana na kijana mmoja aliyekuwa na ndoto ya kufuga kuku. Nyumbani kwao kulikuwa na eneo kubwa tu la kumwezesha kufanya hivyo,ila unajua nini? Alikuwa amesubiri siku moja litokee zari la mentali ili aanze kufanyia kazi hiyo ndoto yake.

    Naomba unisikilize wewe mwenye ndoto kubwa. ni kweli maishani kuna bahati, ila sasa bahati haimfuati mtu ambaye amelala kitandani na kuisburi. Bahati wanakutana nayo watembeaji…

    Kama na wewe unataka bahati ya kukusaidia kufanikisha ndoto yako, basi utapaswa kuanza kufanyia kazi ndoto yako, ndipo utajiweka kwenye nafasi ya kukutana na bahati. Sijui unanielewa hapo, au niongeze sauti….

    Basi bana, niache kwanza niendelee…

    SITA; UNAWEZA KUTENGENEZA NJIA PASIPO NA NJIA

    Njia pekee ya wewe kutengeneza njia pasipo na njia ni wewe kuhakikisha kwamba unapita eneo hilo kila siku bila kuacha. Siku ya kwanza hakuna kitu kitaonekana. Kadhalika siku ya pili mpaka hata ya 100 ila uhakika ni kwamba baada ya siku 365, eneo ambalo unapita kila siku. Kuna njia ambayo itakuwa imeshaanza kuonekana kuwa ipo.

    Sasa hivyohivyo kwenye ndoto yako. Ukianza leo hii kuifanyia kazi ndoto yako, utaanza kuonekana kichaa kwa kufanyia kazi kitu ambacho hakiwezekani kabisa. ila ukweli ni kwamba kama hautakata tamaa, miaka kadhaa mbeleni, basi na wewe utakuwa na kitu ambacho unaweza kuongelea mbele ya watu na kuonesha kuwa kweli nimeweza kufanya kitu cha maana.

    Nakuamini wewe

    Naamini unaweza

    Usiniangushe

    Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio

    Ni mimi

    Godius Rweyongeza

    0755848391

    Morogoro-Tz

  • Njia Mpya Ya Kujenga Tabia Kwa Haraka

    Leo nataka nikwambie kitu kikubwa ambacho kitakusaidia wewe kuweza kujenga tabia mpya kwa haraka. Ebu fikiria tabia yoyote ile ambayo ungegependa kujenga miashani mwako. Ni tabia gani nzuri ambayo kwa siku umekuwa unatamani kuwa nayo?

    Je, ni kusoma vitabu?

    Je, ni kuandika

    Je, ni kufanya mazoezi?

    Au kuweka akiba?

    Ni kitu gani haswa unataka uwe nacho ila sasa umekuwa unashindwa?

    Je, ni kuboresha na kujenga mahusiano mazuri na mwenza wako?

    Leo nataka nikwambie hivi. unaweza kujenga tabia mpya au kufanya kitu chochote kile ulichokuwa unatamani kufanya maishani mwako kwa kutumia kanuni ndogo tu ya dakika mbili.

    Na dakika mbili siyo dakika nyingi sana rafiki yangu.

    Ebu kwa mfano sasa hivi unavyosoma hapa. chagua kitu kimoja ambacho ungependa kufanyia kazi kisha kifanyie kazi sasa hivi unavyosoma hapa. acha kwanza kusoma hapa kifanyie kazi kisha urudi kumalizia.

    Unaona eeh.

    Badala ya kubaki na ndoto kubwa ya kuwa mwandishi na kuendelea kutamani kuwa mwandishi, kaa chini uandike ndani ya dakika mbili. ukiandika sentensi mbili. zinatosha na ni za kwako. Kesho utaongeza nyingine mbili na kesho kutwa utaongeza nyingine mbili. ukiweza kuandika kwa mwaka mzima, siyo siri hizi dakika mbili zitakusaidia hata kuandika kitabu kikubwa tu.

    Bado unabisha tu. Ebu fanyia kazi hii kanuni ya dakika mbili kwa mwezi huu mmoja tu halafu utanipa mrejesho.

    Kama ni mazoezi badala ya kusubiri upate masaa mawili ya kufanya mazoezi. Amka sasa hivi nenda hapo mbele ya uwanj na ufanye mazoezi ndani ya dakika mbili tu. au unaweza kufanyia hata hapo chumbani kwako kwa dakika mbili tu. dakika mbili siyo nyingi na wewe huwezi kushindwa kufanyia kazi kitu kwa dakika mbili tu.

    Kama ni kuboreshamahusiano yako, tumia kanuni hii hii ya dakika mbili. tumia dakika mbili kuandika vitu viwili unavyopenda kwa mwenza wako. Kushukuru kwa kizuri alichokufanyia na hata kuongea naye.

    Unaona eeh. Dakika mbii siyo nyingi sana, na zinaweza kukusadia wewe kufanya makubwa.

    Ikitokea umepanga kufanyia kazi kitu fulani ila mzuka ukapanda ukakifanya kwa dakika zaidi ya hapo, basi. Ila hata mzuka usipopanda ukitumia hizo dakika mbili tu. inatosha.

    Nadhani hata hii makala umeisoma kwa dakika mbili. kama siyo basi, maana mwenyewe nilidhamiria uisome kwa dakika mbili tu.

    Tukutane wakati mwingine

    Ni mimi

    Morogoro-Tz

    0755848391

  • Kwa nini wazazi wanawalazimisha watoto kusoma kozi wanazopenda wao

    Kila mwaka kikifika kipindi cha wahitimu wa kidato cha sita kuomba vyuo, huwa napokea simu za vijana ambao wanalazimishwa na wazazi kwenda kusomea kozi wasizopenda.

    Unakuta kijana anataka akasomee uhandisi, mzazi anataka akasomee human resources.

    Sasa leo kwa ufupi tu nataka niseme kwa nini, wazazi wanakuwa hivyo:

    Moja ni kwa sababu ilikuwa ndoto ya mzazi, ikamshinda sasa anaisukuma kwa mwanae.
    Unakuta mzazi wako alikuwa na ndoto ya kuwa daktari ila udaktari ukamshinda, akaapa kuwa nitahakikisha mwanangu anakuwa daktari. Sasa bila kujali wewe unaupenda au huupendi, utakuta anakulazimisha ukausome.

    Kitu hiki siyo sahihi. Kama wewe ni mzazi unapaswa kufahamu kuwa jukumu lako siyo kumchagulia mwanao kozi ya kusoma Bali kumwongoza na kumwacha achague mwenyewe.

    Wazazi wengi huwa wanatumia nguvu waliyonayo kama wazazi kuwalazimiaha watoto kuchagua kozi wanazotaka waaome. Na muda mwingine kuwatishia watoto kuwa endapo wataenda kinyume watawaadhibu kwa kuwanyima ada.

    Mzazi kama mzazi unapaswa kuwa shabiki kwa kile anachofanya mwanao na anachopenda kufanya.

    Kama wewe ulikuwa na ndoto za kusomea kitu fulani Ila ilashindikana, basi. Hiyo imepita, mwache na mwanao apambane na hali yake.

    Pili ni kwa sababu, ya walivyowaona ndugu wengine.
    Unakuta mzazi kamwona ndugu au rafiki yake amesomea kitu fulani na anatamani hicho kitu, basi analazimisha na mwanae asomee hicho kitu.

    Unachopaswa kufahamu mzazi ni kuwa ukiona ndugu au rafiki amesomea kazi fulani na anaifanya inamlipa, jua kasomea kitu anachopenda. Na wewe mwache mwanao akasomee anachopenda.

    Kitu kingine Ni kwamba, ajira inayolipa leo, haitakuwa inalipa kesho. Hivyo, Leo unaweza kumwambia mwanao kasomee kozi fulani inalipa Sana. Ila kesho kozi hiyohiyo ikawa haina dili kwenye soko la ajira….

    Ndio maana nawashauri vijana wengi waaomee kile wanachopenda wenyewe.


  • Kozi gani nzuri ya Kusoma chuo inayolipa

    Sikumbuki ni mara ngapi watu wamekuwa wakinitafuta kwa ajili tu kuniuliza kozi gani ambayo mtu akisoma itamlipa. Nimejitajidi kujibu swali hili kadiri ninavyoweza kwa kila mtu, Sasa leo nataka nijibu swali hili mwanzo na mwisho.

    ujumbe niliopokea kutoka kwa mmoja wa wafuatiliaji wa kazi zangu

    Jibu la swali hili halina exception. Haijalishi umehitimu kidato Cha nne na unataka kwenda chuo au umehitimu kidato Cha sita na unatakiwa kwenda chuo. Kama swali lako unajiuliza ni kozi gani inayolipa basi soma hapa uone.

    Zamani ulikuwa hivi, ulitakiwa kwenda shuleni, kusoma kwa bidii ili baadaye yje uajiriwe serikalini! Serikalini ndipo kulikuwa na uhakika wa ajira maana ulipoajiriwa huko kulikuwa na uhakika kuwa utafanya kazi mpaka unastaafu na hatimaye ungepata kiiunua mgongo na kwenda zako kifurahia maisha. Siku hizi Mambo YAMEBADILIKA.

    Kuna kipindi udkaktari ulikuwa dili sana. Hivyo, kusoma tu udkatari kulikufanya wewe uwe kwenye nafasi nzuri ya kutoboa.
    Wanafunzi wengi walikimbizana na kusoma udkaktari na masomo yanayohausiana na udaktari, hata kama hawakuwa na ule moyo wa kutibu.  Nadhani ndio maana kulitokea madkatari waliokuwa wanapasua kichwa badala ya mguu…Natania tu!!
    Lakini siku hizi madkatari nao wapo mtaani wanasugua benchi.

    chanzo: Jamii Forums

    Baadaye uanasheria ulivuma. Kama ulitaka kuajiriwa ulipaswa kuwa mwanasheria. Siku hizi wanasheria nao wanasugua benchi mtaani, hawana ajira.

    Ualimu nao kuna kipindi ulitamba sana. Kama ulitaka kuajiriwa ulipaswa kusoma ualimu. Juzi kuna mtu nilikuwa naongea naye akaniambia amesomea ualimu Ila sasa ajira ameamua kwebda kusomea umeme…..

    Sasa sijui huko kwenye umeme atapata AJIRA….

    Ebu kwanza niache ninywe maji….au niagize soda utalipia wewe 😂😂.

    Sasa Kwa nini Ushauri Huu Haufanyi Tena Kazi?

    Jibu Ni moja tu. Zama Zimebadilika…

    Kabisa. Ushauri wa nenda shuleni, kasome kwa bidii utaajiriwa serikalini umepitwa na wakati. Ulikuwa Ni ushauri wa Zama za viwanda. Mtu yeyote ambaye aliutumia ushauri huu kipindi hicho alitoboa Ila kwa ukiutumia ushauri huohuo, unatoboka mwenyewe…

    Nifanyeje Sasa? Nisome kozi gani itakayonipa ajira. Ukweli ni kwamba kozi inayolipa kwa sasa ipo moja tu ila yenyewe haupaswi kuisoma kwa mkumbo wa kuajiriwa.  Nakuomba sasa uangalie video hii hapa chini ambapo nimeeleza kwa kina kozi inayolipa zaidi kwenye zama hizi

  • Mjasiriamali ni nani

    Siku hizi kumekuwepo na wimbi kubwa la vijana wanaojiajiri. Hiki ni kitu kizuri, hata hivyo wengi wamekuwa wanadhani kujiajiri tu kunakufanya uwe mjasiriamali.

    Kwa wengine ujasiriamali umekuwa unahusishwa na kutengeneza bidhaa kama vile sabuni, vitenge, viatu vya kimasai…..

    Ukiwa unatengeneza hivyo vitu, wewe ni mjasiriamali. Kama hutengenezi hivyo vitu wewe siyo mjasiriamali. Kitu ambacho siyo kweli?

    Ujasiriamali unaanza kwa kutatua tatizo lililopo kwenye jamii. Lakini haushii hapo…
    Kutengeneza bidhaa ni sehemu moja. Unaweza kutengeneza bidhaa Ila bidhaa hizo kuuzwa unakuwa bado hujafaulu.

    Wengi wamekuwa wanategeneza bidhaa Ila sasa wanashindwa kuziuza. Ujasiriamali wa kweli upo kwenye vitu viwili.

    Kutengeneza bidhaa ya kweli au kutoa thamani kubwa na
    Kuuza.

    Unaweza kutengeneza bidhaa Ila kama hujui kuiuza utabaki unaijua mwenyewe.

    Kwa hiyo kama wewe unatengeneza vitenge, viatu vya kimasai au sabuni, usiishie tu kujiita mjasiriamali kwa sababu umejua kutengeneza hizo bidhaa. Nenda kaziuze kwa watu

    Ukienda kuuza bidhaa zako ndio utagundua kuwa kazi kubwa haipo kwenye kutengeneza bidhaa bali kuuza.

    Kwa hiyo mjasiriamali Ni mtu AMBAYE anatatua changamoto za watu na kuwauzia watu suluhisho.

  • Siri Mbili Za kuwa Kiongozi Bora Kutoka Kwenye Kitabu Cha My Story Cha Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum

    1.Siri ya kuwa Kiongozi Bora kuwasikiliza watu wako na kuwa karibu na watu wako.

    Mwandishi anasema kwamba hiki Ni kitu ambacho alijifunza kutoka kwa babu yake na alikuja kukifanyia kazi yeye mwenyewe kwenye maisha yake.

    Ukiwa karibu na watu wako ni rahisi kujua matatizo yao na hivyo kujua wanataka Nini?

    2. Unapaswa kubadilika la sivyo mabadiliko yatakubadilisha. Huu ni usemi ambao aliusema kwenye hotuba yake mwaka 2004 wakati akihutubia viongozi wa nchi za kiarabu.

    Miaka 60 na 70 nchi nyingi za kiarabu zilifanya mapinduzi ya kivita. Na wote waliokuwa wanafanya mapinduzi kuna aina  fulani ya maisha walikuwa wanataka. Wengi walikuwa wanaona viongozi hawatendi haki na wananchi wanaonewa. Lakini baada ya wao kuingia madarakani walisahau hilo na kuanza kufanya yaleyale ambayo wao walikuwa hawataki.

    Na hapo ndipo aliwaambia kuwa BADILIKA au la sivyo mtabadilishwa.

    Hapa Kuna somo kubwa sana kwetu. Watu wengi huwa wanapenda kuhubiri mabadiliko Ila wao wenyewe huwa hawapo tayari kubadilika.

    Ngoja nikwambie kama unataka mabadiliko, basi anza wewe kubadilika la sivyo utabadilishwa.

    Kama ungependa kupata kitabu hiki jaza taarifa zako hapa chini, nitakutumia kwako bila kuchelewa

    Kila la kheri
    Umekuwa nami
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • [eBOOK MPYA] NGUVU YA KUTOA (THE MAGIC OF GIVING)

    Utangulizi

    Rafiki yangu kuna nguvu kubwa sana katika kutoa. Hii ni tabia ambayo unapaswa kujifunza na kuifanyia kazi kila siku. Nadhani utakuwa umewahi kusikia kuwa matajiri wana hadi mashirika ambayo yanahusika na utoaji. Kwa mfano, Bill Gates ana shirika la GATES AND MELINDA FOUNDATION. Elon Musk ana shirika la MUSK FOUNDATION na mabilionea wengine pia wana mashirika au tasisi zinahousika na utoaji au la wamejiunga moja kwa moja na shirika la Bill Gates au shirika jingine ambalo wao wameona linawafaa. Hii ni kwa sababu kutoa kuna nguvu kubwa sana kwenye maisha.

    Kwa asili ni kwamba, kadiri unavyotoa ndivyo unapokea zaidi. haupungukiwi chochote kile unapotoa. Ndio maana unaona kwamba mabilionea wanaotoa, wanazidi kuwa mabilionea zaidi na zaidi. Kutoa kwao hakuwafanyi washindwe kuendelea kukua zaidi. kwa hiyo kama ulikuwa unaamini kuwa ukitoa labda utaishiwa, siyo kweli.

    Hivyo na wewe anza kujenga utaratibu wa kutoa. Hakikisha kwamba kwako haipiti siku bila ya wewe kuwa umetoa kitu chochote kile hata kama kitu hicho ni kidogo. unaweza kununua hata mfuko wa pipi na kila siku ukawa unatoa pipi moja tu kwa mtu mmoja kwa mwezi mzima. Na siyo kwamba utoe kwa mtu huyo huyo huyo kila siku. Bali kila siku toa kwa mtu yeyote kitu. Hii itaimarisha misuli yako ya kutoa. Mwanzoni unapoanza utaratibu wa kutoa kwa watu, kinakuwa ni kitu kigumu lakini kadiri unavyoendelea misuli yako inazidi kuimarika na hivyo unajikuta kwamba unaweza kutoa vizuri tu bila shida yoyote.

    Sasa hili suala la kutoa linaweza kuwa linakuchanganya kidogo. wewe unaweza kuwa unaona kwamba hauna kitu cha kutoa. Au pengine unasubiri mpaka pale utakapokuwa milionea au bilionea ili utoea. Ila ukweli ni kwamba hakuna binadamu ambaye ni masikini kiasi cha kukosa kitu cha kutoa. Hivyo, katika ngazi yoyote ile ulipo, una uwezo wa KUTOA

    Ninatoa nini sasa wakati sina fedha?

    Na hapa ninapozungumzia kutoa simaanishi kwamba, utoe fedha peke yake. Fedha ni kipengele kimojawapo cha kutoa kwa watu. Ila kuna vitu vingine ambavyo unaweza kutoa ikiwa ni pamoja na muda wako, nguvu zako, furaha yako, kuwasaidia watu kutengeneza maisha bora na utajiri, kuwaburudisha watu kwa kipaji chako, kuwashirikisha wengine maarifa, makala na vitabu n.k

  • 1. UCHAMBUZI WA KITABU CHA THE 5 SECOND RULE

    Una sekunde tano tu za kuanza kufanya kitu. Kitabu cha the 5 second rule kinakuonesha nguvu ya sekunde tano katika kufanya majukumu yako na kuepuka kughairisha.

    Kama umelala kitandai na alarm ya kuamka ikalia. Hesabu tano, nne, tatu, mbili, moja, kisha toka kitandani..

    Kwenye kitabu hiki Mel Robbins anaenda kukuonesha namna ambavyo utaepuka kughairisha majukumu yako ya kila siku. Ebu BONYEZA hapa chini kufuatilia uchambuzi mpaka mwisho

  • Kitu Ambacho Hakuna Mtu Yeyote Anaweza Kufanya Kwa Ajili Yako

    Pigana kwa ajili ya ndoto zako maana hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kufanya hivyo kwa ajili yako. Hakuna mtu wa aina hiyo.

    unajua kwa nini?

    Kwa sababu hakuna mtu AMBAYE anaweza kuiona ndoto yako kwa usahihi Kama ambavyo wewe mwenyewe unaiona. Wewe ndiwe unaona ndoto yako kwa usahihi.

    Pili, kama wewe mwenyewe tu utashindwa kupambana kwa ajili ya ndoto zako, usitegemee kwamba kutakuwa na mtu mwingine ambaye anaweza kupambana kwa ajili yako.

X