-
Vitabu Vitano Ambavyo Kila Muhitimu Wa Chuo Kikuu Anapaswa Kuanza Kusoma Mara Moja
Siku sio nyingi Sana, NILIANDIKA makala yenye kichwa cha WANAOSHEREHEKEA KUHITIMU CHUO TUWAAMBIE UKWELI? AU TUWAACHE KWANZA WAFUMUE NYWELE ZAO ZA GRADUATION?
Moja kati ya vitu ambavyo nilieleza kwenye makala hii ni wahitimu wa chuo kujenga tabia ya kusoma vitabu na kuwa tayari kujifunza.Kwenye maisha ya mtaani huwezi kuja na ile hali ya kusema kwamba mimi nilikuwa kipanga shuleni kwa hiyo na huku nitaendelea kuwa kipanga.
Maisha ya mtaani yanahitaji kujifunza kila siku. Kinachofanya kujifunza muhimu ni
Moja, kutokana na mabadiliko ambayo yanaendelea kutokea kila kukicha.
Pili kwa sababu unahitaji zaidi ya ujuzi mmoja. Yaani unahitaji kujua utunzaji wa hesabu, mauzo, masoko, utengenezaji wa bidhaa, ushawishi, uongozi, uandishi, elimu ya fedha, elimu ya malengo na mengineyo mengi.Sasa haya yote hujajifunza darasani kitu ambacho kinafanya kujifunza kuwe ni lazima. Kiukweli mtaani huwa hakuna kuhitimu.
Kwa sababu hiyo hapa ninaenda kukuelekeza vitabu vitano ambavyo utaanzia maisha. Vitabu ambavyo vitakupa mwongozo na kufanya uanze kuiona dunia kwa jicho la tofauti kabisa.
1. The Leader who had no title. Kitabu hiki kimeandikwa na mwandishi Robin Sharma. Kikiwa kimeleta kanuni za uongozi katika Zama hizi mpya.
Umetoka shuleni ukiwa umezoea kusukumwa. Yaani mpaka uambiwe kwamba unapaswa kufanya ya kitu fulani ndio unafanya.
Umezoea kusimawiwa ili kazi zifanyike. Ila sasa hivi msimamizi wako nambari moja ni wewe mwenyewe. Hii ndio kusema kuwa kitu cha kwanza kabisa unachohitaji kujifunza ni uongozi. UNAPASWA KUJIONGOZA MWENYEWE BILA YA KUHITAJI KUWA NA CHEO.Soma zaidi: Ukisikia Fulani Ni KIONGOZI, Basi Jua Anafanya Hivi
2. The Richest Man In Babylon
Kitabu hiki kimeandikwa na Clason. Kina masomo makubwa sana kuhusu fedha na kutengeneza utajiri. Ukishajifunza namna ya kuwa KIONGOZI wako mwenyewe. Sasa njoo na hizo mbinu za kiungozi kwenye masuala ya fedha.Kwenye kitabu hiki utakutana na dhana muhimu kuhusu fedha ambazo hukuwahi kuambiwa sehemu nyingine. Utakutana na dhana ya kujilipa mwenyewe.
Utakutana na dhana ya kuwekeza. Na vingine vingi.3. THINK AND GROW RICH
Hiki Ni kitabu kingine ambacho kwa mara ya kwanza litabadili fikra zako kabisa. Ngoja nikwambie kitu. Unahitaji kufikiri tofauti ili uanze kupata matokeo ya tofauti.Hiki nj kitabu ambacho mpaka sasa hivi kumetengeneza mamilionea wengi kuliko kitabu kingine. Kwenye kurasa za kitabu hiki utakutana na masomo 13 ambayo Kama utaanza kuyatumia mara mkja basi yatabadili fikra zako milele na milele.
4. RICH DAD POOR DAD
Kitabu hiki kimeandikwa na mwandishi Robert Kiyosaki ambaye pia ameandika vitabu vingine kama Cashflow Quadrant na Before you quit your job.Kitabu hiki kitakuonesha kuwa Mambo mengi ambayo umekuwa unajifunza kuhusu pesa sio sahihi.
Umekuwa unapokea fedha unakimbikia kununua runinga au kununua simu kubwa na ya kisasa. Lakini Sasa kwenye kitabu hiki utaelekezwa kwamba kitu bora cha kununua. Sio kwamba hujui kununua, bali umekuwa hufanyi manunuzi sahihi.
Kwenye manunuzi unaweza kununua RASILIMALI (ASSETS) au DHIMA (liability).
Rasilimali inakuingisia pesa mfukoni na dhima inatoa pesa mfukoni mwako. Sasa nikuulize. Runinga inakuingizia fedha? Simu je?
Kitabu hiki kinakuhusu sana.5. KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI.
Ninajua unahitaji kutengeneza kesho Bora. Tena kuanzia hapo ulipo. Kitabu Cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI kina mbinu kanuni za Kukuwezesha kutengeneza kesho Bora kuanzia hapo.Kwa maelezo zaidi kuhusu kitabu hiki SOMA HAPA
Rafiki yangu kama ambavyo unaona hapo juu. Hivyo ni vitabu muhimu ambavyo kama utaanza kuvisoma sasa hivi vutabadili maisha yak kwa kiwango kikubwa sana.
TAARIFA MUHIMU KWAKO. kila mara nimekuwa nikishirikisha watu vitabu. Na kila nikifanya hivyo lazima anajitokeza mtu ambaye anakuja kuomba atumiwe vitabu hivyo. Watu wengine wamekuwa wakipoteza vitabu hivi na hivyo kuniomba nitume vitabu hivi mara nyingine na nyingine.
Sasa ili kurahisisha maisha. Nimeamua vitabu vyote ambavyo nitakuwa nashauri watu wavisome, viwekwe kwenye kundi moja la telegram. Kwenye kundi hilo kutakuwa na uwezo wa kuomba vitabu na ukatumiwa. Lakini pia utakuwa unaruhusiwa kutuma vitabu kwa watu wengine. hivvo basi kama umesoma hapa na ungependa kupata vitabu ambavyo nimesema hapa, jiunge kwenye kundi hili la telegram HAPA ili uweze kupata vitabu hivi bure kabisa.
Nakutakia kila la kheri rafiki yangu
Godius Rweyongeza
0755848391 -
Kutana na mtu mwenye kumbukumbu kali kuliko wote
Kuna kipindi nilikuwa nasoma vitabu vya namna bora ya kuwa kumbukumbu ambavyo vimeandikwa na mwandishi Harry Lorrayne na waandishi wengine. Nilichojifunza kwenye vitabu hivi Ni kuwa unaweza kuwa mtu mwenye kumbukumbu kadri unavyotaka.
Una uwezo wa kukumbuka namba za simu za watu, una uwezo wa kukumbuka namba yenye urefu mpaka namba 21 na zaidi.
Una uwezo wa kukumbuka majina ya watu unaokutana nao. Una uwezo wa kukumbuka tarehe na bila kutembea na kalenda.Kwa mfano nikikuuliza tarehe 17 machi 2020 itakuwa siku gani? Kwa kutumia mbinu hizo una uwezo wa kusema siku hiyo lakini hata siku za miaka ya nyuma hata Kama ni mwaka 1901. Kuna kanuni ndogo tu za kutumia na ukafanikisha hili.
Hata hivyo lengo langu kwa siku ya leo halikuwa kutaka kukuonesha uwezo wako wa kumbukumbu ulionao. Nataka nikwambie mtu mwenye kumbukumbu kuliko wote. Huwezi amini mbali na uwezo ambao nimesema kwamba wewe unaweza kuwa nao Kama utaamua. Kuna mtu mmoja anakuzidi kwa uwezo wa kumbukumbu na huwa hasau hata kidogo. Mtu huyu ni yule anayekudai.
Kama unadaiwa usitegemee hata siku moja kwamba anayekudai atasahau. Nimekuja kugundua kuwa watu pekee wenye kumbukumbu za kimataifa ni wale ambao wanadai. Hata iweje lazima atakumbuka kwamba mtu fulani namdai kiasi fulani na inanipasa nimtafute anilipe.
Hivyo basi nipende kukusihi kwamba namna Bora ya kuwakwepa watu wa namna hii daima ni kuhakikisha kwamba hudaiwi. Au kiufupi ni kwamba usijikopeshe.
Ila UKIFANYA hivyo kwa mategemeo kwamba watawasahau. Nakuhakikishia kitu kimoja. Watu hawa hawasahau.
Hivyo njia ya kujipa wewe uhuru wa kutosumbuliwa ni kuachana na kukopa
Kwa Leo naishia hapo, naomba nikutakie wakati mwema.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Unaweza kuwasiliana naye kwa nambari ya simu 0755848391 -
WALE MNAOSEMA KILA KITU KINA FAIDA NA HASARA, EBU NIAMBIE FAIDA ZA KUWA MASIKINI!!!
Imezoeleka miongoni mwa watu kwamba kila kitu huwa kina pande mbili. Ukizungumzia kulia huwezi kusahau kushoto. Ukizungumzia mbele basi lazima kutakuwa na nyuma. Ukisikia mtu anasema juu Basi lazima kuna chini.
Moja ya kitu ambacho watu wamezoea kusambaza ni kwamba kila chenye faida basi lazima kitakuwa na hasara. Japo kitu hiki kinafanya kazi katika baadhi ya maeneo lakini kwenye suala la utajiri na umasikini basi sioni faida za kuwa masikini.
Inawezekana wewe ni mdau wa hiyo kauli ya kwamba kila chenye faida basi lazima kitakuwa na hasara. Sasa ebu niambie faida za kuwa masikini ni zipi?
Kitu kikubwa ninachoona ni kwamba,
👉ukiwa masikini utashindwa kulipa kodi muhimu👉utashindwa kupata huduma muhimu ambazo unastahili
👉utashindwa kupata huduma bora za kiafya
👉 Utashindwa hata kusomesha watoto wako au hata wewe mweyewe kujiendeleza kielimu..
👉utajificha ili usionekane hata kwa watu hasa kama unadaiwa.
soma zaidi; inawezekana kuondokana na madeni
👉utashindwa kutoa sadaka kadiri ya imani yako.👉👉na kuendelea na kuendelea
Orodha ya hasara za kuwa masikini ni nyingi sana.
Zikitajwa zote hapa Basi kitakuwa kitabu cha aina yake.Kiufupi faida za umasikini ni HAMNA labda Kama wewe unazijua niambie.
Hivyo basi kuanzia sasa jihakikishie unajifunza misingi ya fedha na kuiishi.
Hakikisha unakuwa na malengo ya kutafuata.
Fanya kazi na toa thamani ili upate fedha zaidi.
Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.
Godius Rweyongeza
0755848391 -
WANAOSHEREKEHEA KUHITIMU CHUO TUWAAMBIE UKWELI? AU TUWAACHE KWANZA WAFUMUE NYWELE ZAO ZA GRADUATION?
Siku zinaenda kweli. Mwaka jana kipindi kama hiki hapa kwenye mitandao ya kijamii kulikuwa na picha fulani iliyokuwa inasambaa sana. Picha hii ilikuwa na maneno yafuatayo. Wanaosherehekea kuhitimu chuo tuwaambie ukweli, au tuwaache kwanza wafumue nywele zao za graduation? Kisha lilikuwa linafuata cheko ka mtu anayeonekana kuujua ukweli wanaoenda kukutana nao wahitimu kwenye mtaa.
Mwanzoni nilipoiona picha hiyo sikuipa uzito sana, ila sasa nilikuja kushangaa profesa wa chuo kimoja hapa Tanzania ameiweka kwenye mtandao wake wake wa kijamii.
Hapo ndipo nilipojouliza, hivi huyu profesa anayefundisha wanafunzi wanahitimu chuo miaka mitatu, minne mpaka mitano. Kuna kitu gani ambacho hakuwahi kuwaambia wanafunzi wake darasani siku zote hizo mpaka anasubiri wanafunzi wafumue nywele zao za sherehe?
Ilibidi nifuatilie kwa umakini sana. Ndipo niligundua kwamba kuna vitu saba ambavyo shuleni huwezi kuambiwa ila mara tu baada ya kuingia mtaani. Vitu hivi utakutana navyo ana kwa ana. Sasa na mimi leo hii napenda niwaulize ndugu wasomaji. Wanaosherehekea kuhitimu chuo tuwaambie ukweli? Au tusubiri wafumue nywele zao za graduation?
Binafsi nasukumwa kuusema ukweli mapema ili kila mtu apate kuujua kabla mambo hayajawa mabaya. Hivyo naomba mnipe nafasi nijimwage na kuusema ukweli kabla mambo hayajawaendea vibaya wasomi wetu. Kitu kimoja ni kwamba ukweli huu sio kwa wasomi wa kike tu ambao wanasuka bali ni kwa wote.
UKWELI WA KWANZA: MUDA MZURI WA KUANZA MAISHA ILIKUWA KIPINDI UPO CHUO ILA MUDA MZURI ZAIDI WA KUANZA MAISHA NI SASA
Chuo ndio muda mzuri wa kuanza maisha. Huu ndio ulikuwa muda mzuri wa kuziona fursa na kuanza kuzichangamkia. Huu ndio ulikuwa muda wa kutengeneza mzunguko wa watu sahihi. Huu ndio ulikuwa wa kuanza kukutana na watu ambao ungekuja kuingia nao kwenye biashara, watu ambao wangekusaidia kutimiza vipaji vyako na ndoto zako. Huu ulikuwa ni muda mzuri wa wewe kutengeneza marafiki wa kudumu.Ila sasa kama umechelewa. Basi amua kwamba hiki kitu unaenda kujifanyia kazi sasa hivi. Muda wa kuwa chuo ulikuwa ni wakati mzuri wa wewe kuiangalia dunia inavyokwenda na kuangalia namna ambavyo ungeweza kutafuta au kupata wazo la biashara ambayo sasa hivi ungekuwa unaanza. Sasa kama hukufanya hivyo amua kufanya hivyo kuanzia sasa.
Tafuta fursa ambazo unaweza kuchangamkia mara moja. Wasiliana na watu ambao unaona unaweza kujifunza kwao. Muda ndio huu.UKWELI WA PILI: KUHITIMU CHUO SIO MWISHO WA KUJIFUNZA BALI MWANZO WA KUJIFUNZA.
Mtu mmoja amewahi kunukuliwa akisema kwamba mjinga wa karne ya 21 sio yule ambaye hajui kusoma na kuandika. Mjinga wa karne ya 21 Ni yule ambaye anajua kusoma na kuandika ila hasomi wala kujifunza.
Ndugu mhitimu shuleni unafundishwa kusoma na kuandika ila huku mtaani unapaswa kusoma na kujifunza bila kuchoka. Nipende tu kukwambia kwamba dunia ya sasa hivi inabadilika sana. Kompyuta aliyokuwa anaitumia baba na mama miaka ya 90 sio ile ambayo mimi ninaitumia sasa hivi. Redio zenyewe zimebadilika sana tu. Simu zinabadilika kwa kasi, sekta ya afya inazidi kukua na usimamizi wa biashara kwenye zama hizi unabadilika kila kukicha. Ndugu mhitimu, ili uweze kuendana na kasi hii ya mabadiliko yanayoendelea kutokea kila siku basi utapaswa kukaa chini na kusoma vitabu na kujifunza. Sasa hivi husomi kwa ajili ya mtihani wala husomi ile usije ukaachishwa chuo (discontinuation). Sasa hivi unasoma ili kukabiliana na uhalisia.Sasa hivi hutasoma ili upate maksi za juu . Maana maksi za mtaani hazipimwi kwa viwango vya A, B+ na B. Maksi za mtaani zinapimwa kwa kiwango cha pesa unachoingiza au kupoteza. Nimeona nikudokeze hili kabla hujafumua nywele zako za graduation.
UKWELI WA TATU: MSIWAPE KAZI NZITO NDUGU NA JAMAA.
Inafahamika kwamba wanachuo wengi wanapohitimu chuo ndio unakuwa muda wao wa kuanza kuzurura kwa ndugu na jamaa. Wanaenda kwa mjomba na kukaa mwezi huku wakiwa wanakula na kunywa kwa kisingizio cha kwamba wanatafuta ajira. Baada ya hapo wanaenda kwa shangazi wanakaa mwezi. Kisha wanahamia kwa bibi wanakaa miezi miwili. Kote huko wanakula na kunywa bila kufanya kazi yoyote kwa kisingizio cha kutafuta ajira. Na kwa kuwa jamii zetu ziathamini sana wasomi basi wanapokelewa kwa mikono miwili. Ila sasa sisi tunaoujua ukweli tunaona wazi kwamba hapa hawa wanachuo wanakosea kula jasho la wengine huku wakiwa hawafanyi kazi yoyote ya maana.Ndugu mhitimu, Kuhitimu kwako kusiwe chanzo cha wewe kuwabebesha ndugu zako mzigo. Ninachoweza kukwambia ni kwamba chapa kazi. Huku mtaani ni kazi tu. Na wala sio tamthiliya tu. Wala sio facebook tu. Narudia tena huku mtaani ni kazi tu.
Mambo uliyokuwa unayafanya ukiwa chuoni unakaa mtandaoni siku nzima, Sasa yaweke pembeni. Masuala ya kuomba vocha achana nayo. Wewe sasa umekua na hakuna mtu mwingine ambaye unapaswa kumwomba vocha. Nimeona nikwambie ukweli huu mapema kabla hujafumua nywele zako za graduation.
UKWELI WA NNE: AJIRA HAZIPO ILA HAUTAKUFA NJAA.
Nimejaribu kutafuta namna ya kuusema ukweli huu ila nimekosa. Hivyo nausema kama ulivyo. Ajira hamna. Ila ukweli mwingine ni kwamba hutakufa njaa. Inawezekana wakati unaanza chuo walikuambia kwamba kasome kozi fulani maana ina ajira sana. Lakini sasa uhalisia unaokutana nao baada ya chuo ni tofauti.Ndugu mhitimu, chuo kimekuandaa na sasa kimekutunuku shahada, stashahada au astashahada. Hii ni hazina. Ukijua kuitumia vizuri hii inawezekana kabisa usikimbilie kutafuta ajira nyingine tena.
Tafuta tatizo ambalo unaona watu wanalo kwenye jamii kutokana na kile ambacho wewe umesomea chuo. Kuanzia hapo anza kuwasaidia watu kutatua tatizo lao.Inasikitisha kukuta mtu kasoma kilimo miaka mitatu ila anahangaika kutafuta ajira. Sasa unabaki kujiuliza huyu mtu alikuwa anasoma nini darasani. Kama alichosoma hakiwezi kumsaidia yeye kwanza? Na hali kama hii wanayo wahitimu kutoka sekta zote.
Ebu tafuta namna ya kuanza kuitumia taaluma yako kuisaidia jamii. Ukiweza kufanya hivyo jamii nayo pia itakulipa.
UKWELI WA TANO: USIOGOPE KUCHAFUKA
Sasa hapa ndipo kazi ilipo. Wahitimu wengi hawapendi kufanya kazi za viwango vya chini. Kila mtu anahitaji akae ofisini kwenye kiti kinachonesa na kiyoyozi.Ndugu mhitimu, najua wazi kwamba wewe ni msomi. Ila usomi bila pesa hauna maana. Hi hivyo mimi nakwambia hivi, usiogope kuchafuka.
Kama kuna kazi ya chini ambayo unaona unaweza kuifanya ifanye badala ya kukaa ukisubiri ajira ya kuweka sahihi tu kwenye kiti kinachonesa. Anzia popote ilimradi panaweza kuanza kukuingia kipato mfukoni mwako.
Ndugu mhitimu, najua wazi kwamba hupendi kilimo na wala hupendi kushikwa na matope. Ukianza kufikiria juu ya wanja yako ya gharama, unaona sio vizuri kuipeleka kwenye kilimo.
Naheshimu hili sana ila sasa kama hauna pesa, hiyo wanja yenyewe siitaisha? Bora ukachafuke kwa kulima mchicha ila uwe unaingiza fedha mfukoni kuliko kukaa unazurura mtaani bila mwelekeo.
UKWELI WA SITA:USIPOKUWA MWAMINIFU BASI MAISHA YAKO YATAKUWA MAGUMU SANA
Kuna hiki kijitabia ambacho watanzania wengi wamekibeba. Mtu akipata kazi sehemu basi anaanza kufikiria namna ya kukwepesha baadhi ya vitu kutoka kwenye hiyo kazi yake. Kama ni kijana kapewa duka basi anatafuta kila namna aibe kitu kutoka humo dukani. Kama ni mwajiriwa kaajiriwa sehemu basi anatafuta fursa ili abebe vitu vya huko. Jamani hii hali itaendelea mpaka lini?
Ndugu mhitimu. Uaminifu ni hazina kubwa sana ambayo unaweza kujenga kwenye maisha yako. Hivyo basi popote pale utakapokuwa anza kwa kujenga msingi wa uaminifu.
Hata kama utaajiriwa sehemu na ukawa unalipwa mshahara kidogo. Usikimbikie kuiba eti kwa sababu hulipwi vizuri. Na wala usikwepeshe kitu Cha kazini au ofisini.
Kama mtu akikuamini kufanya kazi yake, kiukweli ifanye kwa moyo wako wote, nguvu zako zote na pia khwa mwaminifu.
Ndugu mhitimu. Uaminifu unalipa zaidi ya kitu kingine ambacho unaweza kufikiria.
UKWELI WA SABA: ZAMA ZIMEBADILIKA
Kazi ambayo zamani ilikuwa inafanywa na watu 40. Sasa hivi inafanywa na mashine moja tu.Hali hii imesababisha watu ambao wao hawajiongezei maarifa kutoweka kwenye soko la ajira.
Ndugu mhitimu, bado kuna mabadiliko makubwa sana yanazidi kutokea. Inawezekana sasa hivi ukapata kazi ila kesho hiyo kazi ikasitishwa baada ya kuletwa mashine moja tu. Ninachojua mimi kuhusu wewe ni kwamba, unapaswa kujiweka katika namna ambapo kazi unayofanya wewe. Hakuna mashine yoyote duniani yenye uwezo wa kufanya hiyo kazi. Nakuhakikishia ukiweza hicho kitu. Hutakosa kazi ya kufanya na wala hautakosa pesa za kukufanya uishi na utengeneze utajiri.
Na ili uweze kufikia kwenye viwango ambavyo wewe utakuwa na ujuzi ambao hakuna mashine yenye uwezo wa kufanya kazi yako basi utapaswa kufanya kitu kimoja muhimu. Utapaswa kuunganisha ujuzi au taaluma yako ya sasa na kitu kingine cha ziada. Kwa mfano ukiunganisha uhandisi na ubunifu. Sheria na uandishi. Kilimo na utafiti. Kwa jinsi hiyo hakuna hata siku moja itakuja kupatikana mashine yenye uwezo na ujuzi wa kufanya kazi ambayo wewe unaifanya.
Ndugu mhitimu, nimeona niseme ukweli huu mapema kabla hujafumua nywele zako za graduation. Ili yakija kukupata ya kukupata. Usije kusema sikusema.
Nakutakia kila la kheri.
Godius Rweyongeza
0755848391
MOROGORO TZ🔥🔥LEO NIMEONA NITOE ZAWADI YA VITABU VYANGU KWA WAHTIMU WOTE WA CHUO TANZANIA.
Nimeandika vitabu vitano. Na Gharama ya vitabu vyote kwa pamoja ni 37,000/- tu.Sasa kwa mhitimu au mtu ambaye atapenda kumunulia vitabu hivi ndugu yake mhitimu siku ya leo. Basi atalipia 20,000/- tu ili avipate vitabu hivi vyote vitano.
Vitabu hivi ni pamoja na
1. Kutoka sifuri mpaka kileleni (10,000/-)2. Tatizo si Rasilimali zilizopotea (10,000/-)
3. Nyuma ya ushindi (5,000/-)
4. Mambo 55 ya KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BIASHARA (5,000/-)
5. JINSI YA KUIBUA UBUNIFU ULIO NDANI YAKO (7,000/-).
Ila kwa wahitimu na watu ambao watawanunulia ndugu zao wahitimu vitabu vyote kwa pamoja, gharama take itakuwa 20,000/- ni kwa leo tu.
Lipia kwa namba 0755848391 jina Godius Rweyongeza Kisha nitumie ujumbe mfupi wenye neno VITABU. Karibu sana
-
KUTANA NA KAULI AMBAYO IMEUA UBUNIFU WA WAAFRIKA WENGI NA JINSI YA KUIEPUKA.
Afrika yetu ina mambo mengi ambayo yanachukuliwa kawaida na watu ila ukiyaangalia kwa jicho la kusongambele, unaona wazi kwamba watu wanalazimisha kujweka vikwazo kwenye safari ya kutoka sifuri mpaka kileleni.
Moja ya vitu huvyo ni kauli ambazo zinazuia ubunifu na watu kusongambele. Kauli hizo ni pamoja na
1. Hakuna haraka barani Afrika
2. Ukitaka kumficha mwafrika kitu basi kiandike kwenye kitabu.
3. Mababu zetu hawakuwahi kufanya hivyo.Japo kila kauli Kati ya hizo zote tatu ina madhara makubwa kwa maendeleo ya mtu binafsi. Kwa Leo napenda kuiongelea kiundani zaidi hiyo kauli ya tatu.
MABABU ZETU HAWAKUWAHI KUFANYA HIVYO.
Unakuta mtu ana wazo la kuboresha na kufanya kitu kwa namna ya tofauti, ila utasikia watu wanasema kwamba. Mababu zetu hawakuwahi kufanya hivyo. Yaani maana yake kitu kiendelee kufanyika kwa namna ile ile kilivyokuwa kinafanyika miaka 30 iliyopita. Hata Kama mtu atakuja na njia ya kuboresha na kufanya vizuri zaidi ila kama mbinu hiyo haikuwahi kutumiwa na mababu zetu Basi haifai.Kama unavyoona kauli hii sio kauli ambayo inawafanya watu wachangamke. Hivyo basi sio kauli ya kuendekeza.
Kama ulikuwa unatumia kauli hii achana nayo mara moja, maana mambo yanabadilika. Kitu kilichowapa matokeo ya mazuri mababu zetu sio kitakacholeta matokeo makubwa sasa hivi. Zama zimebadilika.
Kauli hii pia inaua ubunifu. Watu wenye vipaji vyao wanakwama kuvitumia kwa sababu tu wanaambiwa mababu zetu hawakuwahi kufanya hivyo.
Kuanzia leo hii achana na kauli hii mbovu kabisa. Unachopaswa kufahamu ni kuwa, kama mababu zetu hawakuwahi kufanya hivyo basi wewe unaweza kuja na njia bora zaidi hata ya ile wakiyokuwa wanaitumia.
Bila shaka utakuwa unaona jinsi kauli hii inapaswa kuondolewa kwenye kamusi ya maongezi barani. Na wewe ndiwe unapaswa kuwa mstari wa mbele kufanya hivyo.
Makala hii imeandaliwa na
Godius Rweyongeza.Godius Rweyongeza ni mwanzilishi wa mtandao wa SONGAMBELE (www.songambeleblog.blogspot.com) na programu ya THINK BIG FOR AFRICA.
Ukijiunga na programu hii utapata kitabu kimoja cha kiswahili kila mwezi pamoja na masomo ambayo huwezi kuyapata popote kila siku. Gharama ya kujiunga ni elfu 2 kila mwezi ambapo kwa kuanzia utalipia 10,000 ambayo ni gharama ya miezi mitano. Utalipia kwa namba 0755848391 jina Godius Rweyongeza Kisha utatuma ujumbe ili uungwe kwenye kundi la WhatsApp programu inapoendelea.Karibu sana.
Kupata makala maalum kila wiki BONYEZA HAPA
-
Hivi Ndivyo Nilivyopata Bahati Ya Kukutana Na Donald Trump Na Mambo Matano Aliyoniambia
(kama unataka kuchomoka kwenye maisha basi utapaswa kuzingatia haya aliyosema)Siku chache zilizopita nilikaa meza moja na raisi wa marekani katika maongezi mazito sana. Na katika maongezi haya alinishauri vitu vitano ambavyo ninaenda kuvidadavua hapa chini. Labda utakuwa unajiuliza huyu jamaa aliwezaje kukutana na raisi mkubwa hivyo. Ni rahisi sana na connection hii nimeitengeneza mwenyewe. Na wewe kama unataka nitakutengenezea connection hii ya kukutana naye bila kkuchelewa.Nimekutana naye kwa kusoma kitabu chake cha How TO GET RICH. Katika kitabu ameniambia mambo yafuatayo.Moja anasema kwamba unapaswa kuwa unasukumwa na kitu zaidi ya pesa kwenye kufanya kazi zako za kila siku. Hiki ni kitu ambacho kitakufanya uweze kuongeza thamani zaidi na kuwafikiria wateja wako. Ila kama utasukumwa na pesa maana yake utakuwa unajifikiria wewe mwenyewe na namna ya kutengeneza faida muda wote. Hutaweka nguvu katika kutoa vitu ambavyo ni boraPili anasema kwamba wakati wa maongezi yako au hat akama unaandika barua au ujumbe. Hakikisha kwamba ujumbe wako unakuwa ni mfupi na unaoeleweka. Usiwe mtu wa maneno mengi sana.Tatu anasema kwamba unapaswa kuwa mkurugenzi wa maisha yako. Hivyo unapaswa kujua kwamba maisha ni wajibu wako, ukishinda ni juu yako lakini pia ukishindwa ni juu yako.Nne, unapaswa kuhakikisha kamba unazungukwa na watu wanaoju. Kama unaajiri basi ajiri ambao wanajua. Usiajili tu ilimradi umeajiri. Kuwa na watu ambao muda wote ukitaka kujua kitu Fulani unaweza kuwauliza na wakakupa jibu sahihi.Tano, usipoteze mwelekeo wakona wala usidanganywe na mafanikio ya muda mfupi. Trump anasema kwamba moja kati ya vitu ambavyo vilimwangusha sana ni yeye kupoteza mwelekeo kwa kile anachofanya. Hivyo anashauri kwamba unapaswa kuwa mtu wa kutopoteza mwelekeo wa maisha yake ili uweze kufikia hatua kubwa. -
KITENDO KIMOJA, KIDOGO NA CHA UHAKIKA KITAKACHOKUWEKEZESHA KUWEKA AKIBA KWA VIWANGO VYA JUU SANA
Kuna utafiti nimewahi kusoma kwamba mwajiriwa mmoja kwa nchi za ulaya akiachishwa kazi siku hii ya leo anaweza kuendelea kuishi kwa siku nyingine zijazo 18 tu. yaani kwamba akiba yake aliyonayo kwa siku hii ya leo inaweza kumfanya aendelee kuishi kwa siku 18. Huu ni utafiti unaonesha hali ya nchi za ulaya, sasa sijui hali ikoje kwako rafiki yangu. Je, wewe kama leo hii ungekuwa unaacha kazi au kama biashara yako ingekwama leo hii una uhakika wa kuendelea kuishi kwa siku ngapi zijazo? HIILI NI JIBU AMBALO NAJUA UNALO WEWE MWENYEWE TU.Lengo langu leo hii nikukuonesha kitendo kidogo ambacho kinaweza kukufanya uweke akiba kubwa kwa viwango ambavyo hukuktegemea. Na kitendo hiki si kingine bali ni kitendo cha wewe kufungua akaunti yako benki kwa ajili ya kuweka akiba. Hivyo tu.Ujue nini kitatokea pale ambapo wewe utafungua akunti yako benki. Ni kwamba akili yako itajua kila mara inapopokea pesa inapaswa kutoa akiba kwanza kabla ya kitu kiingine. Na hivyo utalazimika kuweka pesa yako benki. Kwenye hiyo akaunti.Kuna mataifa mawili ambayo kwa muda sasa yamekuwa yakitumia hii kanuni ya kufungua akaunti benki na kuweka akiba na yameweza kupiga hatua kubwa sana kiuchumi. Mataifa haya ni China na Israel. Wewe mwenyewe unaweza kuona ni kwa namna gani yanapamba moto kwenye sekta nyingi nyingi tu. sasa rafiki yangu, naomba nikusihi uchukue hatua mara moja na kwenda benki kufungua akaunti ya kuweka akiba. Rafiki yangu huo ndio ushauri muhimu nilionao kwako kwa siku hii ya leo.Umekuwa nami,Godius Rweyongeza0755848391 -
Kama Unashindwa Kutendea Madogo haki, Makubwa Yatakushinda
Kama unashindwa kutendea madogo haki. Hata makubwa yatakushinda(jifunze kitu hiki hapa ambacho ulikuwa hukijui)Kunaa watu wanasema kwamba watakapokuwa na mamilioni ya pesa ndipo wataanza kuweka akiba, na ndipo wataanza kutumia pesa zao vizuri. Ukweli ni kwamba kama unaweza kutumia vizuri kile kidogo ulichonacho leo hii na kukifanya kiweze kuongezeka zaidi basi hata kikubwa ukikipata hakitakupa shinda kuweza kukuza zaidi.Usiseme kwamba nasubiri mpaka niwe na mamilioni ya pesa ndio nianze kufanya matumizi mazuri ya pesa. anza na hiyo mia tano ambayo umeipata leo. Ifanyea hiyo mia tano iweze kukuongezea pesa zaidi na zaidi. Je, hiyo pesa kidogo sasa hivi ikiiingia mkononi mwako inasababisha kuongezeka au kupungua? -
Inalipa kutumia muda wako vizuri
Muda wako haupaswi kuutumia katika kufanya mambo ambayo haya kufai kabisa. Utumie muda wako kufanya kazi ambazo zinakuinua wewe na kuweza kukufikisha kwenye kilele cha mafanikio.Pia jiwekee utaratibu wa kujikamata kila siku kuona kama leo umetumia muda wako vizuri zaidi. Unaweza kufanya hivyo kwa kupata muda wa kuitafakari siku yako kila siku kabla ya kulala.Jiulize ni vitu gani umefanya vyema ndani ya siku ya leo. Je, ni vitu gani umefanya vibaya? Je, ni masomo gani ambayo umejifunza siku ya leo. Kama utaaweza kufanya hivi kila siku, ninahkuhakikishia hautaendelea kuwa mtu Yule Yule. Utaondokana na ule usemi ambao watu wengi wanautumia kwanba bora ya jana maana kwako kila siku mpya kwako itakuwa ni bora zaidi ya jana. Asante na nikutakie siku njema -
KANUNI ZA KUWEKEZA HAZIJABADILIKA
“For me, nothing has really changed in terms of those basic principles:
you start with what you have, you do what you can, you invest what you
get, so that you can do bigger and bigger thingsjapo kumekuwa kunatokea mapinduzi makubwa sana kwenye sekta za teknolojia na sekta nyinginezo. Ila linapokuja kwenye suala zima la kuwekeza pesa na kutengeneza utajiri. Kanuni bado ni zile zile. BILIONEA STRIVE MASIYIWA ANASEMA KWAMBA kwa miaka yote ambayo yeye amekuwa akifanya uwekezaji kanuni za uwekezaji hazijabadilika.
Na kanuni zenyewe ni kwamba
1.Unapaswa kuanza na kile ulichonacho
2. unafanya unachoweza
3. unawekeza unachopata ili uweze kupata kikubwa zaidi na kufanya makubwa zaidi.Tuzichukue kanuni hizi kutoka kwa bilionea mkubwa barani afrika na tuzifanyie kazi.

