-
Kitabu Muhimu Unachopaswa Kusoma Kuhusu Ubunifu
Ubunifu ni mbegu ambayo kila mtu anayo ndani yake. Mbegu hii inahitaji kuwekewa mazingira mazuri sana ili ikue na kutoa matunda.
Mbegu ya kawaida ambayo hupandwa shambani huhitaji maji, hewa, jotoridi na virutubisho ili kuota. Ila maji, hewa, jotoridi na virutubisho vya ubunifu ulio ndani yako ni tofauti na hivi vinavyohitajika na mbegu za kawaida. Mbegu za ubunifu ulio ndani yako zinahitaji vitu zaidi ya thelathini. Nimevieleza vitu hivi kwa undani kwenye kitabu cha JINSI YA KUIBUA UBUNIFU ULIO NDANI YAKO. Kinapatikana kwa sh, 7,000/-. Tuwasiliane.
Ila leo kuna kitabu cha ziada ambacho ninaenda kukutumia bure kabisa. Kitabu hiki sio kingine Bali ni kitabu IBA KAMA MSANII (STEAL LIKE AN ARTIST).
Unaruhusiwa kuiba. Ila sasa iba kama msanii.Kama wewe ni mfuatiliaji wa muziki utakuwa umewahi kusikia watu wanasema Diamond ameigizia wimbo fulani kutoka kwa msanii fulani.
Kitu hiki kwa lugha ya kisanii ndicho kinaitwa kuiba kisanii. Kinaruhusiwa.
Unajua wasanii wanaibaje?
Ngoja Sasa hapa nikwambie wanavyoiba
1. Wanasoma sana
2.wanawakubali wale waliowaibia
3. Wanaiba kutoka kwa wengi
4. Wanabuni kitu cha awali na kutengeneza kitu kingine kipya kabisaBila shaka unaifahamu treni. Treni imeibwa kutoka kwa jongoo, lakini ni wachache sana wanaweza kugundua hilo.
Huo ndio wizi wa kisanii na huo ndio wizi ambao unapaswa kuufanya.
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA -
Usitafute Kiki Kwa Kutengeneza Matatizo
Kama unataka kufanya mambo makubwa na kujulikana basi usitengeneze matatizo ili upate nafasi ya kujulikana.
Namna nzuri na inayodumu na ambayo imetumiwa na watu wote wa mfano kwenye dunia hii ni kutatua matatizo.Kwa hiyo wewe siku zote tafuta matatizo ambayo yanawakumba watu kwenye jamii. Tatua haya matatizo vizuri kabisa. Kumbuka kwamba matatizo ya jamii sio matatizo.
Matatizo ni biashara,
Matatizo ni fursa
Matatizo ni tuta katika barabara ambalo ukilivuka unaongeza mwendo.Hivyo usiogope kutatua matatizo. Kuwa sehemu ya suluhisho. Kama kweli unapenda kutafuta kiki, basi tafuta kiki kwa kuisaidia jamii.
-
NI MATATIZO YANAYOTANYA TUKUE, BILA MATATIZO TUSINGEKUA
Kama kuna misingi umeamua kuifuata kwenye maisha hakikisha unaifuata bila kujali upo katika hali gani. Uwe umekutana na changamoto au mambo yanaenda vizuri. Misingi ni misingi tu ifuate.
Kumbuka kwamba “ni matatizo yanayotufanya tukue, bila matatizo hakuna ukuaji”.
Tatizo la Steve Jobs kufukuzwa Apple ndilo lilimfanya aje kugundua zaidi na kuwa baba wa digitali.
Ila kipindi yuko nje ya apple hakuacha kufuata misingi yake. Aliifuata haswa.
Aliifuata pia baada ya kurudi apple.Kumbe kama kuna misingi umeiweka maishani, basi ifuate katika hali yoyote ile unayokutana nayo.
-
Chagua Kutoumizwa Na Kitu chochote
Choose not to be harmed and you won’t be harmed.
Don’t feel harmed and you haven’t been harmedMARCUS AURELIUS
Katika maisha huwa nyakati ambazo huwa zinaambatana na changamoto kubwa sana. Ni katika nyakati hizi watu wengi huwa wanakata tamaa ya maisha, kupoteza mwelekeo na kujihusisha na vitu vibaya.
Ila ukweli nyakati kama hizi zipo kutuimarisha. Kikubwa tunapaswa kuwa wasikivu na kutafuta kujua ujumbe unaotokana na kikwazo ambacho kimetokea kwa wakati husika.
Kuna watu wengi sana wamekuja kuwa wabunifu wakubwa baada ya kuwa wamepitia nyakati ngumu.Ukweli ni kwamba nyakati ngumu huwa haziishi. Ila ujumbe tunaopata baada ya kuwa tumepitia nyakati hizi unadumu milele.
Kwa hiyo ukikutana na nyakati ngumu, basi chagua kutoumia. Jua kwamba ni hali ambayo unapaswa kuipitia kwa wakati husika ili uwe bora zaidi.Chuma hupitia kwenye moto mkali, (ambao tunaweza kusema ni wakati mgumu).
Ila kikitoka kinakuwa imara zaidi kuliko awali.Kwa hiyo na wewe ukikutana na changamoto kwenye maisha chagua kutoumia maana hiyo ni sehemu ya kukuimarisha wewe zaidi.
Asante sana,
Umekuwa nami,Godius Rweyongeza0755848391KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA -
Hii Ndio Idadi Kamili ya Vitabu Unavyopaswa Kuwa Umesoma Kuhusu Pesa Tu
Moja kati ya somo ambalo wengi huwa hawapendi kuliongelea sana ni pesa. Hata wale ambao huwa wanaiongelea basi huwa wanaiongelea kwa namna ambayo si sahihi.
Leo hii katika suala zima la pesa napenda ujue idadi ya vitabu unavyopaswa kuwa umesoma mpaka Sasa hivi. Maana kiwango cha pesa ulichonacho kinaendana na maarifa uliyonayo. Huwezi kupata pesa zaidi ya kiwango cha maarifa yako.
Na kwa kuwa maarifa yanapatikana kwenye vitabu basi leo hii napenda nikwambie idadi kamili ya vitabu unavyopaswa kuwa umesoma mpaka sasa hivi.
Idadi ya vitabu hukusu pesa tu. Ninasema kuhusu pesa tu. Unavyopaswa kuwa umesoma mpaka sasa hivi inapaswa kuendana na umri wako. Yaani idadi ya vitabu vya pesa inapaswa kuwa ni (MIAKA YAKO MARA KUMI NA MBILI)
Kama una miaka 20 basi idadi ya vitabu vyako inapaswa kuwa (20 mara 12) sawa na vitabu 240.Kwa lugha rahisi ni sawa na kusema, unapaswa kusoma kitabu kimoja tu kwa mwezi kuhusu pesa. Idadi hii haihusishi vitabu vya malengo, vipaji, uongozi na vitabu vinginevyo. Hii ni idadi ya vitabu vya pesa tu.
Umekuwa nami,Godius Rweyongeza0755848391KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA -
TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA tatizo unamwibia Petro Kumlipa Paulo
Kuna misemo mingi sana ya wahenga na kila usemi huwa unakuta umebeba ujumbe fulani. Sasa leo hii tunakutana na usemi unaosema, “unamwibia Petro kumlipa Paulo”.
Katika maisha kuna vitu unafanya ambavyo kwa hakika ni vya kumwibia Petro ili Kumlipa Paulo.
Mfano umeishiwa na hela na unachokimbilia kufanya ni kukopa. Hapa unakuwa unakimbilia kuzima moto kwa haraka haraka (sawa na wizi). Ila madhara yake yanakuja kuwa makubwa kwako.Au umekutana na changamoto. Usikimbilie kunywa pombe au kilevi ili uondokane na tatizo hilo. Hapo unakuwa unatengeneza tatizo zaidi. Huwezi kutatua tatizo kwa kuongeza tatizo, hiyo ni sawa na kumwibia Petro kumlipa Paulo.
Jiepushe sana kumwibia Petro kwenye maisha yako ili umlipe Paulo.
Siku zote inapotokea tatizo, tafuta chanzo chake. Litatue na songa mbele. Asante sana.
-
Tafakari ya Kufikirisha Kutoka Kwa Waziri Mkuu Wa Ufaransa
“Tone la wino linaweza kufanya mamilioni ya watu kufikiri”, alisema Gordon Bryon Noel (1788-1824) ambaye alikuwa mtunga mashairi wa uingereza. Na matone haya ya wino ambayo yanafikirisha yamejaa sana kwenye vitabu. Matokeo yake ni kwamba matone haya huweza kumfanya mtu kufikiri kwa kuweka mipango mikubwa, au matone haya pia huweza kumfanya mtu achukue hatua kubwa.
Kwa sasa nipo nasoma kitabu cha THE PARABLE OF DOLLARS. Kwenye kitabu hiki nimekutana na kauli ya kutafakarisha kutoka kwa waziri mkuu wa ufaransa. Kauli hii inasema hivi, “Tengeneza mipango mikubwa. Usiweke mipango midogo. Mipango mikubwa huvutia watu wakubwa. Mipango midogo huvutia watu wadogo na watu wadogo husababisha matatizo makubwa”.
Kutokana na kauli hii kuna mengi sana ya kujifunza.
1. Unapaswa kuwa na mipango mikubwa sana kwenye maisha yako.2. Mipango mikubwa huvutia watu wakubwa. Wawekezaji wakubwa wanapenda kuwekeza kwenye mipango mikubwa. Kama wewe una mpango mdogo utavutia watu wadogo kama mpango wako ulivyo.
Lakini mwisho wa maneno haya yenye busara kutoka kwa waziri huyu mkuu kuna onyo. Tena hili ni onyo kali.
Anasema hivi, “mipango midogo huvutia watu wadogo NA WATU WADOGO HUSABABISHA MATATIZO MAKUBWA. Hili ni onyo kali.
Kama unataka matatizo kwenye maisha basi weka mipango midogo. Na matatizo utakayoyapata yatakuwa ni makubwa zaidi.
Ngoja nikuoneshe mfano wa mpango mdogo na madhara yake yalivyo makubwaChukulia umeishiwa hela . Sasa unaweka mpango mdogo wa kukopa. Unakopa ili ule. Baada ya hapo siku za kulipa deni zinafika ila bado hujawa na hela. Unaamua kukopa kwa mwingine ili kulipa deni. Wahenga wanasema unamuibia Petro kumlipa Paulo.
Kwa hiyo unajikuta mchezo unaendelea bila kikomo. Hayo ndiyo madhara ya mipango midogo. Ila kama ungekuwa na mipango mikubwa.
Ungejiuliza nini chanzo cha mimi kukosa hela! Je, nifanye nini ili kupata hela kuondoa huu uhaba nilionao.
Mwisho wa siku ungejikuta umekuja na wazo kubwa ambalo lingetatua tatizo mwanzo mwisho.Kuanzia leo. Sema kwamba mipango midogo mwisho.
Karibu mipango mikubwa. Maisha yanajegwa kwenye nguzo za mipango mikubwa.Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.
MIPANGO MIKUBWA + HATUA KUBWA=MATOKEO MAKUBWA kinyume chake
MIPANGO MIDOGO +HATUA NDOGO =MATATIZO MAKUBWA.Soma Zaidi: TAFAKARI YA WIKI: Kipaji Ni Bei Rahisi Sana Kuliko Chumvi
Chagua kuwa na mipango mikubwa.
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA -
Badili Fikra zako Ili Ubadili Maisha Yako
Mwandishi nguli wa vitabu anayejulikana kama Napoleon Hill, alikiita kitabu chake THINK AND GROW RICH. Ikiwa na maana kwamba fikiri na uwe tajiri. Najiuliza “hivi kwa nini mwandishi huyu hakuiita kitabu hiki, FANYA KAZI KWA BIDII ILI UWE TAJIRI.
au kwa nini hakukiita, jitume sana ili uwe tajiri.
Au pengine kukiita pambana uwe tajiri.Alitumia tu neno fikiri. Neno ambalo linahitaji ubadili fikra zetu ili kwenda hatua ya ziada. Au kiufupi neno ambao linatutaka tubadilike kwa ndani kwanza kabla ya kubadilika kwa nje.
Kumbe kinachombadilisha mtu au kinachofanya mtu tajiri sio kufanya kazi kwa bidii, kujituma na kupambana.
Kitu nambari moja kitakachofanya maisha yako yawe ya kipekee sana ni wewe kubadili fikra zako (kubadili mwonekano wa ndani kabla ya mwoneoano wa nje). Mwandishi Brian Tracy, alikazia juu ya hili alipoandika kitabu chake na kukipa kichwa cha Badili fikra zako ili ubadili maisha yako.
Ni kutokana na kubadili fikra unaweza kujikuta unapaswa kuweka juhudi zaidi sehemu fulani ili uweze kusonga mbele zaidi.
Fikra ndizo huwatifautisha masikini na matajiri.
Watu wawili wanaweza kuingia kwenye mji mmoja na kukuta kwamba usafiri ni shida.Mmoja akasema, “huu mji haufai kabisa, yaani usafiri wa shida na unasumbua kweli kutoka eneo moja kwenda jingine”
Ila mwingine akasema, “watu wa mji huu hawana usafiri, hii ni fursa kwangu kuwaletea usafiri ili niwarahisishie maisha. Watanilipa kwa kupanda usafiri na mimi nitakuwa tajiri”
Unaweza kuona kutokana na mifano huo hapo, mmoja ana fikra chanya, wakati mwingine anaona tatizo na anaendela kulalamika.
Siku zote ukikutana na tatizo, basi kuwa tayari kulibadili maana siku zote matatizo si tatizo bali ni daraja.
Chagua kubadili fikra kwanza, ili ubadili maisha yako
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA -
Makala Maalum Kwa Watu Wenye Mpango Wa Kuomba Kazi Au Wanaoomba Kazi Sasa Hivi
Moja ya mbinu ambayo imezoeleka kwenye kuomba ni kuandika CV na kuituma kwa mwajiri mtarajiwa huku ukisubiri majibu. Kadri siku zinavyozidi kusogea njia hii inazidi kuwa ya kizamani kidogo na hivyo lazima kuwe na njia bora kabisa ya kuomba kazi tofauti na wengi walivyozoea lakini yenye uhakika.
Njia hii mpya ni kuomba kukutana na mwajiri wako mtarajiwa ana kwa ana. Unaweza kuomba kukutana naye kwa ajili ya mlo wa jioni au unaweza kumfuatilia kwa umakini na kujua huwa anapendelea kula wapi chakula cha jioni. unaweza pia kufuatilia maeneo ambapo huwa anapenda kutumia wikendi yake.
Ukishajua hilo unaenda eneo hilo na kuhakikisha unakutana naye.
Hapa unaweza kuongea naye mambo mengi ila mwisho wa siku ukaanza kuonesha ujuzi wako kwako.Hakikisha unaeleza nini unaweza kufanya kwa ubora zaidi ya wengine.
Kama kuna video ya yako ukifanya jambo la kipekee ioneshe.
Njia hii inakuongezea uwezekano wa kupata kazi mara 10 mpaka 100 zaidi ya yule ambaye anayetuma CV na kutulia.
Je, una mpango wa kuomba kazi?
Hakikisha unafanya kama nilivyoelekeza hapo.
Karibu sanaUmekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA -
Hivi Ndivyo Huwa Napata Mawazo Kuandika Ya Makala Kila Siku
Moja kati ya swali ambalo ninakutana nalo kila siku, ni swali la “Je, ninapata wapi vitu vya kuandika kila siku”?
Huwa napenda kujibu swali kirahisi sana kama swali lenyewe lilivyo rahisi? Huwa nauliza watu unapata wapi cha kuongea kila siku?
Wengine huwa wanasema, unajua kuongea sio sawa na kuandika. Sasa hapa nataka kukuonesha wapi huwa napata mawazo ya kuandika. Utashangaa sana.
Kumbuka haya ni baadhi tu ya maeneo sio yote1. Maongezi yangu na watu wengine. Hapa huwa napata mambo mengi sana ya kuandika. Huwa natumia kanuni kwamba unaweza kujifunza kitu kutoka kwa kila mtu. Hivyo nikikutana na mtu siwezi kukosa kitu cha kujifunza kutoka kwake, kitakachopelekea Mimi kuandika. Hata kama tutakutana kwa sekunde mbili.
Wanasema unapokuwa nyundo kila kitu hugeuka kuwa msumari, Sasa hicho ndio nafanya. Kwangu kila ninachokiona najiuliza ni nini naweza kuandika kutoka hapa?
2. Nasikiliza zaidi ya kuongea. Kuna kanuni inaitwa kanuni ya 60-40. Kanuni hii inasema hivi “tumia asilimia 60 kusikiliza na asilimia 40 kuongea”. Kwa kufanya utajifunza mengi sana na utapata mengi sana ya kuandika. Njia hii naitumia na wewe unaweza kuitumia
Sasa labda unajiuliza nisikilize nini?
Anza kuwasikiliza watu waliokuzunguka. Watu wanapenda kusikilizwa sana. Unapoongea na watu jitahidi kuweka simu pembeni ili upate kusikikiza zaidi.Sikiliza sauti za vifaa mbalimbali kama pikipiki zinazopita, magari, ndege n.k
3. Nasoma vitabu. Hapa ndipo pazuri sana. Na nimekuwa nikiandika sana huu ya kusoma Vitabu. Kifupi ni kwamba unapaswa kuwa na kiu na kusoma kila siku.
4. Napenda kutembelea mazingira ya asili. Yaani huku ndipo penyewe sasa. Asili huwa haidanganyi utapata kujifunza mengi sana. Asili inahusisha vitu kama misitu, milima n.k kile ninachojifunza huku ndio nakuja kuandika
5. Napenda kujifunza kwa waliopiga hatua na ambao hawajapiga hatua.
Kwa aliyepiga hatua najifunza kitu gani napaswa kufanya kwenda ninapotaka kwenda.Kwa ambaye hajafanikiwa najifunza nini cha kuepuka.
Kwa jinsi hii sitakuja kukosa cha kuandika hata siku moja.
Karibu sana
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA




