Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Unawezaje Kugundua Kitu Unachopaswa Kufanya Hapa Duniani?

    Mwishoni mwa mwezi uliopita nilikwenda Clouds Fm kwenye kipindi cha TEMINO. Kipindi kinachoendeshwa na Harris Kapiga pamoja na Adv. Henry Mwinuka. Sasa baada ya kipindi wakati nikiongea na Adv. Mwinuka kuna swali nilimwuliza, ndipo akawa ameniambia kwamba kipindi anaingia chuoni kuna vitu viwili alikuwa anapenda kufanya.

    Moja, ilikuwa ni utangazaji na pili ni sheria. Akawa anasema kwamba siku za kwanza kabisa za yeye kuingia chuoni alikuwa hajafikia uamuzi sahihi wa kitu gani anapaswa kusoma. Hivyo, alikuwa anajifunza kuhusiana na uandishi na wakati huo huo alikuwa anajifunza kuhusu sheria. Anasema kwamba kwa utaratibu wa chuo chao ulikuwa unaruhusiwa ndani ya wiki mbili kuhudhuria kozi yoyote unayotaka na mwishoni mwa hizo wiki ndio sasa ulipaswa kufanya uamuzi wa mwisho wa kozi ipi haswa unapaswa kusoma.

    Sasa kwa nini siku ya leo nimeanza kwa kuandika kitu kama hiki. Lengo langu ni moja tu, nataka nikusaidie wewe ambaye hujaua ni kitu gani ambacho unapaswa kufanya.

    Na wewe unaweza kutumia njia hii ambayo aliitumia Adv. Kwenye kuchagua kipi cha cha kufanya maishani mwako.

    Kama mpaka sasa hivi huelewi ni kitu gani ambacho unapaswa kufanya, basi unatakiwa kujaribu vitu mbalimbali. halafu kwenye hivyo vitu mbalimbali unavyojaribu, utagundua kitu kimoja ndio kinakuvuta na unakipenda zaidi hicho kuliko vingine.

    Basi hapo unaweza kuchana na vitu vingine vyote ambavyo unafanya na kuwekeza nguvu zako kwenye hicho kitu kimoja sasa ambacho unafanya.

    Kadiri unavyokuwa unajaribu vitu mbalimbali ndivyo unagundua vitu ambavyo unapenda na hivyo unaweza kuweka juhudi huko.

    Lakini pia, unaweza kugundua kile unachopaswa kufanya hapa duniani kupitia maswali ambayo watu wanapenda kukuuliza mara kwa mara. Au ushauri ambao watu wanaomba kwako mara kwa mara. Inawezekana watu wameshaona kwamba kuna kitu unweza. Hivyo, kwa kuagalia kitu ambacho  watu huwa wanakuja kwako kuomba ushauri mara kwa mara, ndio unaweza kugundua kitu ambacho unapaswa kufanya hapa duniani.

    Kuna kitu pia, unaweza kuwa unatumia nguvu na uwezo wa kawaida tu, ila ukawa unakifanya na watu wanapenda. Hiki nacho kinaweza kuwa ndio unapaswa kufanya hapa duniani.

    Pia, kama una kumbukumbu za vitu ulivyokuwa unapendelea kufanya utotoni. Hizi ni nzuri maana kipindi ulikuwa bado hujapitia mnyoosho kama uliopitia sasa hivi. Ninaposema mnyoosho, namaanisha kwamba sasa hivi jamii imekunyoosha na kukufinyanga kama inavyotaka, tofauti na ulivyokuwa mtoto. Ulipokuwa mtoto ungeweza kusema kwamba nitakuwa rubani, na watu wengekupongeza kwa kusema hivyo. Ila kuna umri uliofikia ambapo wewe mwenyewe ulikuwa unaogopa kusema kwamba unataka kuwa rubani. Si ndio?

    Hapo sasa fahamu kwamba ulishaanza kupitia kwenye mnyoosho. Na kama ungepata ujasiri wa kusema hivyo, basi ni wazi kuwa watu wangekucheka na kukuonesha kwamba haiwezekani. Huo ndio mnyoosho ninaouzungumzia leo hii.

    Kitu hiki kimekufanya umesahau ndoto na malengo yako na hata kusudi lako.

    Sasa leo hii rudi utotoni na ujiulize ni kitu gani ulichokuwa unapenda kufanya utotoni.

    Moja ya kitu ambacho nimeeleza kwa kina kwenye kitabu changu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO ni namna gani unaaweza kugundua ndoto zako.

    Kuna sura mbili maalumu kwa ajili ya hili suala. Nashauri uweze kusoma kitabu hiki hapa leo hii, maana kitakausaidia sana kwenye kugundua kitu unachopaswa kufanya hapa duniani. Lakini pia kitakupa mbinu za kuweza kukifanyia kazi.

    Siku ya leo una machaguo matatu:

    • Moja Ni Kuendelea na maisha yako Kama yalivyokuwa siku zote bila kusudi maalumu.
    • Pili kuendelea kuishi ambayo jamii imekuchagulia, ambayo pia hayana kusudi lolote la kufanyia Kazi na
    • Tatu, Kuchagua kusoma kitabu Cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO Ili uweze kukujua kusudi lako na kulitimiza.

    Gharama ya kitabu hiki ni 20,000 tu. Kupata kitabu hiki wasiliana nami kwa 0755848391 karibu

    Kitabu pia kina audiobook take ambayo kwa Bei ya ofa Leo tu. Utaipata kwa 15,000/- tu.

    Wasiliana nami sasa ili uweze kupata nakala yako Sasa. Namba ya mawasiliano ni 0755848391

  • Uchambuzi Wa Kitabu Cha UNFAIR ADVANTAGE

    Kitabu: UNFAIR ADVANTAGE
    Mwandishi: Robert Kiyosaki
    Mchambuzi: Hillary Mrosso
    Mawasiliano: 255 683 862 481

    UTANGULIZI

    Kama jina la kitabu hiki lilivyo, Unfair Adavantage, mwandishi anaeleza kwa undani namna alivyotoka kwenye ajira, namna alivyo anzisha biashara, namna alivyojifunza kwa undani masula ya kodi, hati fungani, mifuko ya pensheni, mifuko ya hifadhi ya jamii, mabenki na mifumo mingine ya kifedha, kuanzia marekani hadi sehemu nyingine duniani, pia ameeleza mifumo ya elimu jinsi ilivyofeli kutoa elimu ya kifedha wa wanafunzi. Maarifa yaliyopo kwenye kitabu hiki yatakufanya upate faida kwenye kila eneo ambalo unataka kuwekeza fedha zako, na hii ndio dhana kuu ya Unfair Adavantege.

    Karibu tujifunze mambo 70, niliyoyaona ndani ya kitabu hiki;

    1. Watu wengi wanatumia maisha yao kuwa watumwa wa mishahara ya waajiri wao na kuwa watumwa wa kodi kwa serikali.
    2. Watu wengi bado hawajui kati ya chakula na chakula ambacho ni mtego ndio maana ni rahisi sana kukatatika.
    3. Wengi wanaingia kwenye ajira na hapo ndio inakuwa mtego kwao, kutoka inakuwa ngumu sana, kwasababu ya dhana ya usalama iliyopo.
    4. Kama unataka kuwa muwekezaji basi, jua kuwa hutakiwi kuwa mtu wa kawaida (average), unatakiwa kuwa mwekezaji mwerevu na mwenye busara zaidi.
    5. Wawekezaji wa kawaida ndio huwafanya wawekezaji werevu au wenye busara kuwa matajiri.
    6. Mwandishi anasisitiza sana kuwa uwekezaji ulio bora sio kwenye majumba, hisa, hati fungani, mifuko ya pensheni, dhamana, au kwenye mali zisizo hamishika, uwekezaji bora ni kuwekeza kwako mwenyewe.
    7. Kam usipokuwa mwerevu na mwenye busara katika kuwekeza, kila utakachowekeza kitapotea na utapata hasara, Kama wewe ni mjinga, hata uwekeze kwenye vitu gani, kwa kiasi kikubwa utaishia kushindwa vibaya.
    8. Siku zote, kama hujui cha kufanya na fedha zako, kitu bora cha kufanya ni kutomwambia mtu yeyote.
    9. Upeo ulionao kuhusu elimu ya fedha ndio huamua nini ufanye na fedha zako na ni sehemu gani sahihi zaidi ya kuwekeza fedha zako.
    10. Kama huna elimu ya fedha hatari zinakuwa nyingi, kodi zitakuandama, na faida zitaendelea kupungua. Elimu ya fedha ni muhimu sana katika uwekezaji na biashara.
    11. Watu wasio na elimu ya fedha huishia kuwekeza katika vitu visivyo na faida na vyenye hasara. Mfano kununua sana Liabilities.
    12. Haina maana kabisa kufanya kazi kwa nguvu zako zote kisha serikali ikachukua fedha zako, bila wewe kunufaika nazo.
    13. Fedha nyingi za waajiriwa zinakwenda serikalini kwa majina tofauti tofauti kama vile kodi, pensheni, nk
    14. Kama usipokua mwerevu serikali itazichukua fedha zako ulizozipata kwa damu na jasho baada ya wewe kufariki. Kuwa na mpango madhubuti wa kuondokana na hali hiyo, kwa kuwa mwekezaji mjanja.
    15. Usipokuwa mwerevu na mjanja magonjwa na madalali watanufaika zaidi na fedha zako kuliko wewe.
    16. Usipokuwa mjanja hata wanasheria nao watakuwa karibu ili kunufaika na fedha zako zaidi ya wewe mwenyewe ambaye umezitafuta kwa kufanya kazi ngumu usiku na chana
    17. Kabla ya kutafuta na kutengeneza fedha, jifunze namna ya kuzilinda fedha zako maana wanaozihitaji ni wengi sana.
    18. Hali ya kukosa Imani na usalama wa fedha zako ndio husababisha wengi kufikiria kuwa uwekezaji na kuingia kwenye biashara ni gumu na kuna hatari nyingi.
    19. Kumbuka siku zote kuwa chochote ambacho ni hatari ni kwasababu hakijadhibitiwa, kama ukiwa na udhibiti au usimamizi mzuri wa fedha na mali zako, hatari zinapungua au zinaweza zisiwepo kabisa.
    20. Elimu ya fedha inayofundishwa mashuleni na vyuoni inawafundisha watu kuwekeza fedha zao serikalini, banki, benk za uwekezaji, mifuko ya hifadhi ya jamii nk.
    21. Elimu ya kweli na nzuri kuhusu fedha ni ile inayokufundisha namna ya kuwafanya watu wakuletee wewe fedha zao, na sio wewe uchukue fedha zako upeleke serikalini, au uwape watu wengine wanufaike nazo.
    22. Mwekezaji mjanja na mwenye maarifa ni yule anayetumia fedha za watu wengine kupata utajiri, kama vile kukopa benk, serikalini na kwa watu wengine.
    23. Usiwape fedha zako matajiri, au kuhifadhi fedha zako benki, feha inashuka na kupanda thamani kila wakati, ukiweka fedha benki kama uwekezaji jua kuwa huo sio uwekezaji wa busara.
    24. Jinsi unavyoifanyia kazi fedha, ndivyo unavyokatwa kodi kubwa kwenye mapato yako.
    25. Jinsi fedha inavyokufanyia wewe kazi kwa nguvu, ndivyo unavyolipa kodi kidogo,
    26. Ndio maana waajiriwa wengi wanaandamwa na makato makubwa ya kodi, na jinsi wanavyojitahidi kuongeza kufanya kazi kwa bidi ndivyo na makato yanakuwa makubwa.
    27. Ukitumia fedha za watu wengine ndio zikufanyie kazi kwa bidi, uwezekano ni mkubwa sana wa kulipa kiasi kidogo cha kodi, na wakati mwingine unaweza usilipe kodi kabisa.
    28. Kama unataka kupata fedha zaidi na ulipe kodi kidogo, unahitaji kubadili aina ya mapato yako, yani sehemu mapato yako au fedha zako zinakotoka.
    29. Njia nzuri ya kubadili chanzo cha mapato yako ni kuwa na biashara au uwekezaji ambao unakuingizia fedha na kuacha kutegemea ajira pekee maana mapato yanayotoka kwenye ajira ndio hukatwa kodi kubwa.
    30. Katika ulimwengu wa kifedha na uzalishaji wanapenda sana wakopaji kuliko watunzaji wa fedha.
    31. Kama unakopa fedha benki kwa lengo la kuzalisha, mabenki yanapenda sana watu wa aina hiyo, maana ndio wanaoleta faida na kufanya benki ziwe na fedha zaidi.
    32. Wengi tunafahamu ilivyo rahisi kuingia kwenye madeni, ishu sio kuingia kwenye madeni, ishu ni unayabebaje hayo madeni, unayasimamia vipi hayo madeni, hapo ndipo ugumu ulipo.
    33. Kama wewe ni mjinga hakuna uwekezaji utakao kufaa, hata kama utawekeza kwenye dhahabu na silva, bado unaweza kupata hasara.
    34. Sehemu zote duniani, serikali huwa zinawalinda wazalishaji kuliko walaji wa mwisho ambao wanaifanyia kazi fedha, hasa waajiriwa wanaotegemea ajira.
    35. Wanaoifanyia kazi fedha mara nyingi ndio huwa wahanga wa kupata hasara na huishia kuwa masikini.
    36. Cha kushangaza zaidi huku duniani ni kwamba wengi wenye elimu nzuri ya darasani wanaheshimu sana maswala yao ya kitaaluma lakini wanashuindwa kuheshimu elimu ya kifedha ambayo ni muhimu sana kwenye maisha.
    37. Wengi wanataka fedha na wanataka kuwa matajiri, lakini wanataka utajiri na fedha bila kulipa ghrama au kujitoa sadaka kufikia malengo hayo.
    38. Njia nzuri ya kuisaidia na kuiokoa dunia ni kujiokoa na kujisaidia wewe mwenyewe kwanza. Kama huwezi kujisaidia na kujiokoa wewe mwenyewe, na utawezaji kuisaidia dunia?
    39. Mwandishi wa kitabu hiki ameandika haya ili kututia moyo tuwe wanafunzi wa elimu ya fedha, ili tujue namna ya kushughulika vizuri na maswala yetu ya kifedha na kuwa wakarimu kwa vipawa tulivyopewa na Mungu.
    40. Ni kama vile alivyowahi kusema Dr. Fuller kuwa ni kwa kuwa wakarimu ndio tunaweza kujua vipawa tulivyopewa na Mungu na uwezo wetu wa kipekee.
    41. Hii ina maana unapofanikiwa kifedha, uwe mkarimu zaidi kwa kuwasaidia wengine kufikisha malengo yao kifedha, usiwe mchoyo.
    42. Hali mbaya ya kifedha tunayopitia imesababishwa na matumizi mabaya ya fedha na rushwa katika ngazi za juu serikalini.
    43. Rushwa imeangusha mambo mengi mazuri na yenye tija kwa jamii. Imeaharibu misingi ya haki na usawa.
    44. Ni kweli kabisa kuna wengi wana tamaa ya madaraka kiasi cha kuuza hata nafsi zao, kuumiza maisha ya wengine, kumwaga damu ili kutimiza adhima yao ya kutaka madaraka.
    45. Dunia inashughudia kuwa na watu wa aina hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa wamesababisha kukua kwa umasikini na kuwa matumizi mabaya tya fedha kama vile kutawala kwa rushwa.
    46. Siku zote kumbuka, ajira yako sio asset, huwezi kumrithisha watoto wako ajira uliyonayo.
    47. Fedha sio asset, siku hizi fedha inazidi kupungua thamani yake kwa jinsi deni la taifa linapovyongezeka.
    48. Proleteriat, ni watu wasiomiliki vitu vya uzalishaji, kama mashamba, walichonacho watu hawa ni mshahara wa ujira kutokana na kazi ngumu wanazozifanya.
    49. Mfumo wetu wa elimu na mitaala yake inawandaa wanafunzi kuwa waajiriwa, watu watakaotegemea mishahara na ujira wa mwezi baada ya kuwafanyia wengine kazi.
    50. Badala ya wanafunzi kuondoka shuleni na kuanza kutafuta ajira zenye mishahara mikubwa, inatakiwa wakitoka shuleni wafikirie namna ya kutengeneza ajira na kazi zenye mishahara mikubwa.
    51. Mfumo wetu wa elimu unatakiwa kuwa andaa wanafunzi waje kutengeneza ajira kwa ajili ya kuajiri wengine na sio kutegemea kuajiriwa pekee.
    52. Wengi wanaotoka vyuoni wanataka walipwe zaidi kwa kufanya kazi kidogo, jambo hili ni gumu, maana kwa jinsi kulivyo na uhaba wa ajira hakuna mwajiri atakayevumilia hilo.
    53. Badala ya kutoka vyuoni na kuanza kutafua ajira zenye mikataba mizuri na zenye usalama, inatakiwa wanafunzi wakitoka vyuoni, watengeneze ajira au kazi zenye mapato endelevu.
    54. Wengi wanakimbilia ajira maana zinaweza kuwa na mishahara, mikataba, na marupurupu mengine, lakini ukweli ni kwamba wanatafuta usalama, na sio fedha kiivyo,
    55. Kwa kiasi fulani mfumo wetu wa elimu unawaaminisha wanafunzi kuwa matajiri ni watu wenye tamaa na watu wabaya, wanafunzi wanatakiwa wajue kuwa tajiri ni jambo zuri na wanatakiwa kuwa wakarimu.
    56. Duniani kwa sasa kuna shule za sharia, shule za udaktari, mwandishi anahoji, kwanini kusiwe na shule kwa ajili ya kufundisha ujasiriamali na ubepari?
    57. Mwandishi anatamani kila mtu apate elimu ya fedha na uwekezaji, hii itaokoa muda na kukuondolea hatari za kupoteza fedha katika uwekezaji au biashara.
    58. Mwandishi hapendezewi sana na kuwapa fedha zetu watu wa mipango fedha au watalamu wa masuala ya kifedha, anaamini wengi wa watu hao sio wazuri na wanaweza wasikushauri vizuri kuhusu namna ya kuzalisha fedha zaidi.
    59. Kuna watu wanafikiri kuwekeza fedha benki ni ujanja, nasema, sio ujanja maana hata wasio na akili wanaweza kufanya hivyo. Pata elimu ya kifedha uwekeze kwenye faida.
    60. Kichwa chako au ubongo wako ndio asseti yako kubwa, lakini pia inaweza kuwa ni liability yako kubwa. Haya yote yameandikwa ili tupate unfair advantage ya kutumia na kugeuza akili zetu kuwa asseti yetu kubwa.
    61. Hutajua ladha ya uhuru wa kweli kama hujafanikiwa kuwa huru kiefdha, au kuwa na uhuru wa kifedha.
    62. Hivyo basi wekeza katika kupata uhuru wa kweli ambao ni kupata uhuru wa kiefha. Kupata elimu ya fedha ni muhimu kuliko kujifunza utalaamu au profession.
    63. Linapokuja suala la fedha kila mtu atatamani kukwambia lake, hivyo kamwe usiende kuuliza kwa mtu anayeuza bima kama unahitaji bima.
    64. Wawekezaji werevu na wajanja wanazingatia sana suala la kodi kabla ya kuingia kwenye uwekezaji.
    65. Wawekezaji halisi hawahifadhi fedha zao, huwa wanaziachia ziingie kwenye mzunguko ili kuzalisha zaidi kuna neno wanapenda kulitumia “velocity of money.”
    66. Kikubwa cha kujua siku zote, haijalishi unawekeza kwenye kitu gani, unatakiwa ujifunze kitu hicho jifunze na elewa mambo yote muhimu kuhusu uwekezaji wako.
    67. Ukiwa mwekezaji mzuri unaweza kuzalisha fedha katika hali zote bila kuangalia soko lipoje, hata kama uchumi ni mbaya bado unaweza kutengeneza fedha.
    68. Ukishajua unataka kufanya nini kwenye maisha yako, tafuta kocha, mtu ambaye atakusimamia hadi umalize jambo lako.
    69. Katika maswala ya kifedha, kuna hisia sana na kama huwezi kudhibiti hisia zako, basi jua hutaweza kudhibiti fedha zako
    70. Unaweza kusema kuwa huna fedha mara nyingi uwezavyo, lakini itakuwa haina tija kwenye maisha yako. Shauku ina nguvu kuliko elimu, tumia shauku uliyonayo kuingia kwenye utajiri kwa kuzingatia elimu ya fedha uliyoipata. Hata haya yote tuliyojifunza hapa, kama huna shauku ya kuyafanyia kazi hayatakuwa na maana sana kwenye maisha yako.

    Ahsante sana!

  • Kitu kimoja kitakachokusukuma wewe kuweza kufanya makubwa

    Habari ya upande wa huko rafki yangu wa ukweli, siku ya leo ningependa kukwambia kitu kimoja ambacho kitakusukuma wewe kuweza kufanya makubwa. na kitu hiki siyo kingine bali ni upendo. Upendo unapaswa kukusukuma wewe kufanya kitu kwenye maisha yako. Bila upendo sidhani kama kuna kitu cha maana ambacho utafanya hapa duniani.

    Upendo wa kazi

    Upendo wa kazi ndio unapaswa kukusukuma wewe katika kufanya kazi, yaani, ufanye kile ambacho wewe mwenyewe unapenda na uhakikishe kwamba umekifanya kwa ubora wa hali lya juu sana. Ukiwa na upendo kwenye kazi hakuna kitakachoshindikana, utahakikisha unajisukuma kufanikisha kazi yako kuliko ambavyo mtu mwingine amewahi kuifanya hiyo kazi na hivyo kupiga hatua kubwa kuliko mtu wa kawaida.

    Upendo kwa familia yako.

    Upendo kwa familia ayako ndio utakusuma wewe kuihudumia familia yako.

    Upendo kwa jamii yako

    Upendo kwa jamii yako ndio utakusukuma wewe kutatua matatizo yanayoikumba jamii yako. Ni kwa sababu unapenda kuona watu wa jamii yako wakipata huduma mbalimbali karibu yako, ndio maana umeanzisha biashara.

     Ni kwa sababu hupendi kuona jamii yako inahangaika kwa sababu ya maji, ndio maana, umeanzisha kisima cha maji karibu yako.

    Upendo kwa taifa lako

    Ni kwa sababu ya upendo kwa taifa lako ndio maana unawekeza kwa ajili ya kesho. Ni kwa sababu ya upendo kwa taifa lako ndio maana unaanda kizazi kijacho vizuri kwa kuhakikisha unakifundisha misingi ya maisha na misingi ya kazi.

    Upendo wa jina lako

    Ni kwa sababu ya upendo wa jina lako ndio maana unahakikisha kwamba, kila kazi ambayo unafanya inafanyika kwa ubora wa hali ya juu. Hakuna kugushi wala kufanya kazi chini ya viwango.

    Kama bado hujasoma kitabu changu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA nashauri sana usome kitabu hiki.

    Unaweza kupata vitabu hivi kwa kuwasiliana na 0755848391

    Fanya hivyo sasa hivi.

    Umekuwa nami

    Godius Rweyongeza

    0755848391

    Morogoro-Tz

    Kwa maswali, maoni au booking: songambele.smb@gmail.com

  • Vitabu Vitano Ambavyo Kila Mfanyabiashara Makini Anapaswa Kusoma

    Kwanza kabla sijaandika mambo mengi sana siku leo. Ningependa kukwambia kwamba baadhi ya vitabu ambavyo ninaenda kukueleza hapa vinapatikana bure kabisa mtdanoni, hivyo, unaweza kupakua hivi vitabu bure. Labda unajiuliza unawezaje kupakua hivi vitabu bure mtandaoni?

    Hakikisha kwamba umeangalia hii video hapa, itakusaidia wewe kupakua vitabu hivi bure. Ila pia kuna vitabu vya kulipia ili uvipate, kwa vitabu ambavyo unapaswa ulipie ili uvipte, basi utatkiwa kutoa kisi kidogo mfukoni li uvipate.

    Pili ni kwamba, kuna kitabu cha bure ambacho napenda kila rafiki yangu akisome.

    Kupata kitabu hiki, jaza taarifa zako hapa chini, kisha bonyeza nitumie hiki kitabu.

    Sasa tuendelee na vitabu vitano ambavyo kila mfanyabiashara makini anapaswa kuhakikisha kwamba amesoma. Ni vitabu ambavyo hupaswi kuchukulia kimzaha badala yake unapaswa kuvisoma na kuviweka kwenye matendo.

    Mimi sijui wewe kwa sasa una miaka mingapi. Ila ninataka ujipe changamoto leo. Ebu jiulize umeishi hapa duniani kwa miaka mingapi? Halafu jiulize ni kitu gani cha kipekee umeweza kufanikisha ndani ya hiyo miaka ambayo umekuwa ukifanya kazi bila ya kusoma vitabu au bila kufufuata mwongozo wowote ule kutoka kwenye vitabu? Sasa kwa nini usijipe changamoto ya kuchukua vitabu vichache ambavyo utasoma na kufuata kwa kipindi hata cha miaka mitatu minne ijayo. Yaani, kama umekuwa unafuata mwongozo wako kwa hiyo miaka yote kwani ukitoa miaka mitatu au mitano tu ambayo utafuata mwongozo wa vitabu fulani na kuuishi unadhani utapoteza nini?

    Kama kuna mwongozo wa vitabu ambao utapaswa kuufuata basi ni vitabu vifuatavyo.

    Kwanza ni kitabu cha THINK AND GROW RICH

    Hiki ni kitabu chako cha kwanza ambacho unapaswa kusoma kama unataka kuwa mfanyabiashara makini kwenye maisha yako. Kwenye kitabu hiki unaenda kujifunza mbinu ya kwanza kabisa ya mafanikio kwamba ni kuanza na wazo. Hakuna kitu chochote kile ambacho unaweza kufanikisha bila ya kuwa na wazo kwanza. Na wazo ukilifanyia kazi, na kulileta kwenye uhalisia hilo wazo linawezekana kukamikilika na kuja kwenye uhalisia.

    Mwandishi anasema kwamba moja ya kitu ambacho huwa kinawafanya watu wengi wanashindawa kufanikiwa, iwe ni kwenye biashara au kwenye maisha ya kawaida ni kukosa uendelevu kwenye kufanyia kazi wazo ambalo wanakuwa nalo. Unakuta kwamba mtu ana wazo zuri, lakini mtu huyu anaanza kulifanyia kazi wazo lake na baada ya muda mfupi  unakuta amekata tamaa na hivyo anakuwa halifanyii wazo lake kama ambavyo inapaswa na mwisho wa siku anakata tamaa na kuachana nalo.

    Tena siku hizi tafiti mbalimbali zinaonesha vizuri. Ambapo zinaonesha kwamba kati ya biashara mia moja ambazo huwa zinaanzishwa kila mwaka karibia biashara kumi zinakufa. Moja ya kitu ambacho huwa kinafanya hizi biashara kufa ni kukosa mwendelezo au mtu wa kuendelea kufanyia kazi wazo la awali la biashara.

    Kwenye kitabu hiki utakutana na mwanadishia ambaye atakupa mbinu kumi na tatu, ambazo zitakusaidia wewe kuweza kuinua biashara yako kutoka sifuri mpaka kuifikisha kwenye viwango vikubwa .

    Je, upo tayari kwa ajili ya kusoma hiki kitabu na kufuata mwongozo wake.

    ANZA KWA KUSOMA UCHAMBUZI WAKE HAPA

    PILI NI KITABU CHA THE RICHEST MAN IN IBABYLON

    Hiki ni kitabu kingine cha kipekee ambacho haswa kinazungumzia kuhusu fedha. Fedha ni kitu cha muhimu sana kwenye maisha ya kawaida na kwenye biashara. Maisha yetu ya kila siku hayawezi kwenda bila ya kuwa na fedha. Fedha ni kitu muhimu kwenye maisha ya kawaida na kwenye biashara. Ukikosa fedha unaweza kushindwa mpaka kuanzisha biashara na ukiwa na fedha ni wazi kuwa utaweza kuanzisha biashara yako kwa uzuri tu.

    Sasa unahitaji kujua misingi ya kutafuta pesa, kuitumia na kuitunza. Na kitabu hiki hapa kimefunza kwa kina hasa namna ambavyo unaweza kufanyia kazi hayo yote matatu bila ya shida yoyote ile.

    KITABU CHA TATU NI RICH DADA POOR DAD

    Hiki ni kitabu kingine ambacho unaweza kuanza nacho. Hiki kitakusaidia zaidi kwenye utunzaji wa pesa zako. utajua ni wapi kabisa ambapo unaweza kuwekeza pesa zako kwa manufaa ya muda wa sasa na muda ujao. Utajua kwamba kuna baadhi ya vitu ambavyo watu huwa wanaunua kwa kuona kwamba vina thamani kubwa na thamani ambayo inaweza kuwafikisha mbali, ila vitu hivyo kwenye uhalisia siyo kwamba vinapanda thamani na kuwafikisha kwenye utajiri, badala yake ukweli ni kwamba vitu hivyo vinakuwa vinashuka thamani na kuzidi kuwashusha hao watu. kwa hiyo, kwenye hiki kitabu utajifunza mbinu mbalimbali za kifedha ambazo zitakusaidia kuwa NINJA linapokuja suala zima la fedha na hasa uwekezaji.

    Sasa baada ya kuwa umesoma hivyo vitabu vyote na umeingia kwenye biashara. Vitabu viwili vya mwisho kwa siku ya leo vina mwongozo ambao unapaswa kuufuata na kuuishi. Ni vitabu ambavyo nashauri usome tu siyo mara moja au mara mbili ni vitabu ambavyo nashauri usome na kusoma tena.

    Hivi ni vitabu ambavyo vitakusaidia wewe kuanzia sifuri na mwisho wa siku ukaishia kuwa na kila kitu kwenye maisha yako. Upo tayari kwa ajili ya kuvijua vitabu hivi

    4. NI WINNING cha JACK WELCH

    Hapa sasa tunaongea biashara. hiki ni kitabu kuhusu usimamizi wa biashara. Yaani, namna ambavtyo unaweza kusimamia biashara yako kitalaam mpaka ikaweza kukua. kama ulikuwa hujui ni kwamba, Jack Welch alikuwa mkurugenzi mkuu wa kampuni ya GM. Aliikuza hii kampuni kwa viwango vikubwa na alikuwa mkurugenzi mkuu kwa miaka zaidi ya 20.

    kwa kipindi chote ambacho alikuwa kwenye uongozi wa juu, alijifunza mengi sana alipitia kwenye mambo mengi ambayo ametushirikisha kwenye kitabu chake hiki. Lakini siyo hilo tu, baada ya kuwa amestaafu kazi alikuwa akizunguka maeneo mbalimbali hapa duniani kwa ajili ya kuongea na vijana mbalimbali kuhusiana na masuala ya kibiashara na namna ambavyo wanaweza kukuza biashara zao.

    Sasa wakati anafanya hivyo, ndivyo alikutana na maswali mengi ambayo watu walikuwa wakiuliza. Katika kuyaunganisha haya maswali ndipo alikuja kugundua kwamba hayo maswali yote yalikuwa yanatosha kuwa kitabu. Hivyo akawa ameandika maswali kujibu hayo maswali kwa kutumia uzoefu wake. Maswali haya nina uhakika kwamba wewe mwenyewe utakuwa ukijiuliza, haya maswali. Sasa kazi ni kwako siku ya leo kuhakikisha kwamba umepata kitabu hiki na kukisoma.

    5. NVUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA.

    Naam, hiki ni kitabu ambacho nimendika mwenyewe. Ndani yake utajifunza namna ambavyo unaweza kuikuza biashara yako kwa kutumia nguvu ya vitu vidogo mpaka kuifanya hiyo biashara yako iweze kukua.

    watu wengi wanashindwa kukua kwa sababu wanataka waaanzishe kitu le hii na kesho yake wawe wameza kufanya makubwa. ila kwenye hiki kitabu unaenda kujifunz kwamba kwa kutumia nguvu ya vitu vidogo unaweza kufanya makubwa kwenye maisha. je, upo tayari kwa ajili ya kuhakikisha kwamba unaitumia nguvu hii ya vitu vidogo kwenye kufanya makubwa?

    sasa pata nakala ya kitabu chako kwa shilingi 20,000/-. Kupata kitabu hiki wasiliana nami kwa 0755848391

    BONASI KITABU CHA SITA: HOW TO BUILD A MULTI-BILLION DOLLAR BUSINESS IN AFRICA

    Hiki kitabu ameandika Strive Masiyiwa. Mmoja wa mabilionea wakubwa hapa barani Afrika. Kwenye kitabu hiki bilionea huyu katushirkisha mbinu halisi ambazo ametumia yeye kwenye kujenga biashara na kampuni zake.

    hiki kitabu huwa nakisoma kila mara. Siwezi kusema mengi juu ya hiki kitabu, zaidi ya kusema kwamba kisome.

    KUPATA VITABU HIVI YOTE BURE BONYEZA HAPA

    Umeshajiunga na kundi letu la THINK BIG FOR AFRIKA? KAMA BADO BONYEZA HAPA

    Kama bado hujasoma NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA nashauri sana uweze kusoma kitabu hiki.

    Cha kufanya wasiliana nami kupitia 0755848391

    Fanya hivyo sasa hivi.

    Umekuwa nami

    Godius Rweyongeza

    0755848391

    Morogoro-Tz

    Kwa maswali, maoni au booking: songambele.smb@gmail.com

  • Sababu 18 Kwa Nini Tunaandika Vitabu Na Kwa Nini Wewe Unapaswa Kuandika Cha Kwako

    Kuna watu wanafikiri kwamba wao hawawezi kuandika vitabu. na wengine wanafikrii kwamba ili uweze kuandika kitabu basi unapaswa kuwa na aina fulani hivi ya ugenius. Sasa siku ya leo nimeona siyo vibaya ngoja nikwambie sababu 18 kwa nini tunaandika vitabu na kwa nini wewe unapaswa kuandika kitabu chako.

    Je, upo tayari kuzijua hizi sababu.

    Kama umekuwa unaandika na watu wanakukatisha tamaa, hakikisha unasikiliza hizi sababu 18 kwa nini tunaandika vitabu na kwa nini wewe unapaswa kuandika kitabu chako leo hii.

  • Sala Muhimu Unayopaswa Kusali Kila Siku. Inaleta Matokeo Ya Haraka

    Kupata vitabu hivi wasiliana na 0755848391

    Unaendeleaje rafiki yangu wa ukweli. Najua umekuwa ukisali sala mbalimbali kwa siku nyingi.

    Ila leo ninataka kukwambia sala moja tu ambayo hujawahi kusali, na sala hii siyo nyingine bali kumwomba Mungu akupe usikivu.

    Uwe msikilizaji mzuri kuliko kuwa muongeaji mzuri.

    Tuna mdomo na masikio mawili. Ikimaanishabkuwa tunapaswa kuwa wasikilizaji wazuri kuliko kuwa waongeaji. Ila kinachotokea Ni kinyume chake. Unakuta MTU Ni muongeaji mzuri halafu hasikilizi.

    Sasa kuwa kinyume. Kuwa msikilizaji. Hii itakupa faida nyingi sana, maana kwanza watu wanapenda kusikilizwa.
    Lakini pia unaposikiliza unampa mtu nafasi ya kujieleza zaidi na hivyo kumfahamu au kufahamu tatizo lake kiundani.

    Kuanzia leo, jipe jukumu la kuwa msikilizaji mzuri. Utajua mengi kupitia kusikiliza kuliko kuongea.

    Kwa hiyo sala yako iwe hivi: Ee Mungu naomba unifanye niwe msikilizaji mzuri kuliko kuwa muongeaji. Amina


    Kila la kheri
    Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli
    Godius Rweyongeza
    0755848391

  • Kwa nini unajipunja hivyo?

    Wahaya wana usemi unaosema hivi, “endirira ekagaba emikira yayeyebwa”. Ukiniuliza tafsiri yake sijui ila nitakupa stori😂😂.

    Inasemekana hapo zamani za kale kulikuwa na mkutano wa wanyama. Kitu kikubwa kwenye mkutano huo ulikuwa ni ugawaji wa mikia.

    Mnyama aliyepewaa jukumu la kuwagawia wanyama wengine mikia ni mnyama mmoja ambaye kwa kihaya anaitwa NDIRIRA. Kiswahili chake sikijui aisee😂😂. Anayejua ataniambia baadaye nirekebishe🙈🙈.

    Sasa mnyama NDIRIRA aligawa mikia kwa wanyama wote. Wengine akawapa mikia mirefu, wengine akawapa mikia ya saizi ya kati na wengine mikia mifupi.

    Halafu, mikia ikaisha….

    Mwisho wa siku yule mnyama alijisahau, akawa amebaki na kitu kilichokuwa hakieleweki ni mkia au siyo mkia….

    Akaambulia hicho tu…

    Sasa kwa nini nimeandika hivi leo.
    Nataka nikwambie kuwa usijipunje. Una ndoto kubwa, zifanyie kazi na kitakachokuwezesha wewe kufikia hizi ndoto kubwa ni mwongozo sahihi.

    Mwongozo huu ndio nimeuandika kwenye kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO.

    Hakikisha unapata mwongozo huu wa kipekee sana, utakaokusaidia wewe kuzifanyia kazi ndoto mpaka kuzifikia. Usipopata mwongozo utakuwa unajipunja.

    Mwongozo huu unapatikana kwa 20,000/-.

    Utatuma fedha kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA halafu utaniambia uko wapi ili uweze kutumiwa kitabu hiki.

    Gharama kidogo za usafiri zitaongezeka kulingana na eneo ulipo.

    Umekuwa nami
    Godius Rweyongeza
    www.songambele.co.tz
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • Vitu Vinne Ambavyo Hakuna Mtu Anaweza Kufanya Kwa Niaba Yako

    Kwanza hakuna mtu ambaye anaweza kupenda familia yako kwa ajili yako. Ni jukumu lako kuhakikisha unaijali na kuipenda familia yako.

    Pili hakuna mtu mtu anaweza kutunza afya yako kwa ajili yako, jukumu la kutunza afya yako ni la kwako.

    Tatu ni juu yako kuhakikisha kuwa unatunza fedha zako vizuri. Hakuna mtu ambaye anaweza kufanya hili kwa niaba yako.

    Nne, ni kuongeza maarifa. hakuna mtu anaweza kusoma na kujifunza kwa niaba yako. Ni wewe ambaye unapaswa kufanya hivyo.

    soma zaidi: Hii ni kazi anbayo huwezi kuajiri mtu kuifanya kwa niaba yako

  • Audiobook ni nini?

    Audiobook ni kitabu kilichosomwa. Yaani, kitabu kilekile ambacho ungekaa chini na kukisoma kwa siku au wiki. Zamu hii kinakuwa kimesomwa na kuwekwa kwenye mfumo wa sauti.

    Hivyo, unaweza kukisikiliza popote pale ulipo.

    Muda mwingine unaweza kukuta majukumu yamekubana, hivyo ukasikiliza audiobook vizuri tu bila ya shida yoyote wakati unaendelea na majukumu yako mengine kama kufua, kupika, au majukumu mengine yanayoruhusu usikilize audiobook.

    Muda mwingine wakati unasafiri kwenye gari yako unaweza kusikiliza audiobook yako vizuri tu.

    Audiobook ni kitabu ila kwa mfumo wa sauti.

    Kinakusaidia kupata mengi ndani ya muda kidogo. Na unaweza kukisikiliza mara nyingi kadiri uwezavyo.

    Sasa hapa tunayo audiobook ya kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. Unaweza kuipata hii kwa  kwa elfu kumi tu (10,000/-)

    Kupata audiobook ya kitabu Cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO lipia 10,000/- kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA. Utapata audiobook bila kuchelewa.

  • Huu Ndio Ulevi Pekee Ambao Unapaswa Kuwa Nao

    Rafiki yangu mpendwa, najua umekuwa unasikia kuwa ulevi ni noma! Ulevi ni hatari. Mimi mwenyewe siyo kwamba napinga hili. Hapana, nakubaliana nalo kwa asilimia zote, ukweli ni wamba ulevi ni hatari kwa afya yako.

    Watu wanajiiingiza kwenye aina mbalimbali za ulevi. Kuna ambao wanaingia kwenye ulevi wa pombe, wengine madawa ya kulevya, wengine mitandao ya kijamii na hata wengine umalaya.

    Sasa siku ya leo napenda nikwambie aina mpya ya ulevi ambao unapaswa kujihusisha nao. Na ulevi huu ni ulevi wa kufanya kazi kwa bidii.

    Hii ndi oaina pekee ya ulevi ambayo inaweza kukusogeze mbele na kukufanya wewe uweze kufika mbali maishani mwako. Hakuna aina nyingine ya ulevi ambayo inaweza kukuletea maendeleo tofauti na aina hii tu ya ulevi. Kwa hiyo, kama unataka kufanya makubwa rafiki yangu, zama kwenye ulevi wa kufanya kazi kwa  bidii.

    Hii ndio aina pekee ya ulevi ambayo ninaweza kukushauri ujihusishe nayo rafiki yangu. aina pekee ya ulevi ambayo inaweza kukuletea maendeleo.

    umeshasoma kitabu changu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO? Hiki ni kitabu ambacho kitakufanya ufikiri kwa ukubwa lakini pia uanze kuzifanyia kazi ndoto zko kwa bidii kubwa,

    Kkupata kitabu hiki wasiliana na 0755848391

    Fanya hivyo sasa hivi.

    Umekuwa nami

    Godius Rweyongeza

    0755848391

    Morogoro-Tz

    Kwa maswali, maoni au booking: songambele.smb@gmail.com

X