Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Niweke Fedha zangu benki Kama akiba au niwekeze kwenye CRDB Mzigo Flexi?

    Juzi kuna mtu alinipigia simu. Alikuwa ameniakiliza kupitia TEMINO YA CLOUDS FM. Swali lake lilikuwa moja tu na hakuwa na kitu kingine cha ziada

    Alitaka kujua kipi ni Bora, Kati ya kuweka fedha yake benki au kuwekeza kwenye CRDB Mzigo flexi!

    Unajiuliza kwani CRDB MZIGO FLEXI ni nini?

    Huu ni aina ya uwekezaji ambapo unaikopesha benki ya CRDB fedha, halafu yenyewe inawekeza kwenye miradi mbalimbali baadaye inakupa faida ya asilimia 9. Kwa mwezi, baada ya miezi mitatu, sita au kwa mwaka.

    Haya ni makubaliano ambayo mnaingia Kati yako wewe na CRDB, kwa hiyo fedha yako unapoiweka huku inakuwa salama na wanapaswa kukulipa wewe kiasi cha fedha mlichokubaliana.

    Kama umesoma kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE utagundua Kuwa Hii Ni aina ya HATIFUNGANI.

    Kama hujasoma kitabu changu hiki cha kipekee ngoja nukupitishe tu kwa haraka.

    Kuna aina mbili za hatifungani:

    Hatifungani za serikali (ambapo wewe unaweza kuikopesha serikali hela yako kwa makubaliano ya kuwa ikurudishie hela yako pamoja na hiyo faida ya kila baada ya muda fulani ambapo mara nyingi huwa ni kuanzia miezi sita, miaka mitatu, kumi na hata ishirini au ishirini na tano.

    Hatifungani za serikali huwa zinatolewa na benki kuu ya taifa (BOT).

    Pia Kuna hatifungani za makampuni ambapo unaweza kuikopesha kampuni fedha zako kwa makubaliano hayohayo Kama unayoyafanya kwa serikali.

    Sasa CRDB mzigo Flexi. Nadhani itakuwa flexible Ila wamefupisha 😂😂 ni hatifungani ila za kampuni.

    Tofauti kati ya hisa hatifungani

    Jamani jamani! Ambao hamjasoma kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE mnakosaa mengi. Niseme nisiseme!

    Tofauti kubwa iliyopo Kati ya hisa na hatifungani ni kwamba ukinunua hisa za kampuni fulani, wewe unakuwa ni sehemu ya mmiliki wa kampuni husika.

    Lakini ukinunua hatifungani, unaikopesha kampuni. Kuna tofauti kubwa hapo.

    Hiki kitu kinamaanisha kuwa endapo kampuni itafilisika Kama wewe ni mmiliki wa hisa kwenye Kampuni, hutapata chochote maana wewe mwenyewe ni mmiliki wa ile kampuni iliyopata hasara.

    Ila kama umeikopesha kampuni (umenunua hatifungani), hiyo ni stori nyingine kabisa.

    Yaani, kampuni itakazimika kuuza rasilimali zake zitakazokuwa zimebaki Kama majengo na uwekezaji mwingine ili kukulipa wewe.

    Any way, sasa baada ya kueleza hayo yote kwa kina ndio sasa nataka nikueleze nilivyomjibu yule mtu wangu wa juzi.

    Kumbuka aliuliza

    Niweke Fedha zangu benki Kama akiba au niwekeze kwenye CRDB Mzigo Flexi ?
    Yule mama aliendelea kuniambia kuwa alikuwa na milioni kama tatu hivi na ile fedha alikuwa anaiweka kwa ajili ya mwanae ambaye yupo darasa la saba sasa.

    Nilimwambia hivi, kulinganisha na riba inayotolewa kwenye akaunti za benki, hata kama ni akaunti ya mtoto, ni vigumu sana kupata riba ya asilimia 9 kwa mwaka. Ikizidi sana, sana, itakuwa asilimia nne. Hapo imezidi.

    Ila kwa riba ya asilimia 9 ukilinganisha na akaunti ya kawaida ya benki Ni Bora tu kuweka fedha zako huku utakapopata riba ya asilimia 9.

    Nikaweka kituo. Nikamwambia achukue kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Baada ya dakika tano tu, nikaona Mpesa inasoma hivi

    9ES67XC1Z imethibitishwa mnamo tarehe 27/5/22 1:23 PM, toa 30,000 kutoka kwa…

    Alikuwa ametuma fedha kwa ajili ya vitabu viwili. Kwanza ni kitabu Cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA na
    ebook ya MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE pamoja na nauli ya kumtumia kitabu.

    Sasa hivi anaendelea kusoma vitabu vyake.

    Ebu na wewe hakikisha unapata nakala laini ya kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE kwa 5,000/- tu. Tuma fedha kwa 0755858391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    Kumbuka hiki ni kitabu pekee kitakachokufundisha wewe uwekezaji kwenye HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE kwa namna ambayo hujawahi kujifunza.

    Naamimi sasa umeelewa CRDB mzigo Flexi ni Nini na tofauti take na akiba ya kawaida.

    Pata nakala yako, wasiliana na 0755848391

  • Tofauti Ya Thamani Ya Hisa Na Bei Ya Hisa

    Huyu ni msomaji wa kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE

    Habari ya leo. Siku ya leo ningependa kujibu swali la mtu mmoj amabye amesoma kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE.

    Anauliza swali hivi, samahani kuna kitu sijakikujua hapo, tofauti kati thamani yahisa na bei ya hisa

    Kwa hiyo hapa kitu cha kujibu ni je, thamani ni nini? na bei ni kitu gani?

    kwa kawaida thamani ya hisa huwa ni sawa ni bei ya ya hisa ya wakati  husika. Kwa hiyo, kama hisa zinauzwa kwa shilingi 500, hiyo ndiyo itakuwa thamani yake pia.

    Kitu hiki pia ndio kinatumika kupima utajiri wa watu. kwa mfano ukisikia wanasema bilionea fulani ana utajiri wa bilioni kadhaa ni kulingana na bei ya hisa kwenye soko la hisa, ambayo ndio inatuletea thamani ya utajiri wake.

    Kwa mfano, ukifuatilia orodha ya mtajiri hapa duniani. Utagundua kwamba utajiri wao unakuwa unapanda na kushuka kila mara. Kinachofanya utajiri wao ushuke au kupanda siyo kitu kingine bali ni kupanda na kushuka kwa hisa. Kadiri hisa zinavyopanda au kushuka bei, ndivyo utajiri wao unapanda na kushuka.

    Hili suala la kupanda na kushuka kwa bei ya hisa huwa linatokana na jinsi watu wanavyonunua na kuuza hisa zao.

    Ikumbukwe kuwa hisa ni bidhaa zilizo sokoni, kama zilizyo bidhaa nyingine.  Tuchukulie mfano wa kawaida tu wa nyanya sokoni. Kuna kipindi nyanya zinakuwa adimu na hivyo bei yake inakuwa juu. Na kuna kipindi nyanya zinakuwa nyingi sokoni na hivyo bei yake inakuwa chini. Hivyohivyo, kwenye suala zima la hisa.

    Kupanda na kushuka kwake huwa kunategemea na jinsi ambavyo watu wanauza na kununua. Wanunuaji wakiwa wengi, maana yake kuna uhitaji, hivyo ambavyo thamani ya hisa itapanda na kadiri wauzaji wanavyokuwa wengi maana yake uhitaji ni mdogo na thamani ya hisa inashuka.

    Thamani halisi ya hisa.

    Hizo thamani za hisa zote huwa zinatokana na mihemko ya wanunuaji. Maana yake, watu ndio wanaweza kufanya thamani ya hisa ipande au kushuka. Hata hivyo, ukitaka kujua thamani halisi kabisa ya hisa unapaswa kutumia taarifa za ndani ya biashara.

    Na yenyewe inapatikana kwa kuchukua rasilimali zote za kampuni kisha unatoa madeni yote ambayo kampuni inadaiwa, halafu unagawa kwa idadi ya hisa zote zilizo sokoni.

    Thamani ya hisa =Rasilimali zote za kampuni (thamani kwa shilingi au dola)- madeni yote ya kampuni ÷ Idadi ya hisa zote zilizo sokoni

    Kama kampuni tayari imeshaingia kwenye soko la hisa, taarifa hizi unaweza kuzipata kwa kufuatilia taarifa zake za mwaka au mhura husika.

    Kama ndio inaingia mara ya kwanza kwenye soko la hisa utazipata kwenye ripoti yake inayotolewa kwa umma. Hata hivyo, utafiti binafsi unahitajika kwenye hili.

    Kama bado hujasoma kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE, nashauri sana usome kitabu hiki.

    Kitabu kingine cha nyongeza ni kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA

    Unaweza kupata vitabu hivi kwa kuwasiliana na 0755848391

    Fanya hivyo sasa hivi.

    Umekuwa nami

    Godius Rweyongeza

    0755848391

    Morogoro-Tz

    Kwa maswali, maoni au booking: songambele.smb@songambele

  • Kama Wewe Ni Shabiki Wa Yanga au Simba Hakikisha Umesoma Hapa

    Jana ilikuwa ni mechi ya simba na Yanga. Ni moja ya mechi zinagusa watu wengi kwa hapa Tanzania. Kuna watu hawashabikii timu yoyote ile hapa duniani, isipokuwa simba au Yanga.

    Sasa leo nilikuwa nikifikiri kuhusu hili nikawakumbuka rafiki zangu ambao wanahangaika kuandika vitabu. Wanahangaika na hawajui kitu gani wanaweza kuandikia. Nikasema ngoja leo niwaambie kitu.

    Kama wewe unajiuliza ni shabiki wa yanga au simba na unajiuliza ni aina gani ya kitabu unaweza kuandika. Ebu kuanzia leo hii tuandikie kitabu kuhusu ushabiki wako na timu yako.

    Ebu tuambie kwa nini unaipenda Simba au YANGA. Ilikuwaje mpaka ukaipenda simba au Yanga.

    Kwa nini mpaka leo hii wewe unaendelea kuishabiki hii timu

    Nini mpango wako kwa siku za mbeleni juu ya hii timu?

    Je, ushabiki wako nje ya hizi timu ukoje?

    Je, huwa unatumia kiasi gani kwa mwaka kwa ajili ya hii timu? Iwe ni kuangalia mechi, kutoa michango n.k

    Kuna mambo mengi san asana ya kuandika kuhusu simba na yanga tu, ambayo ni kitabu tosha.

    Nadhani kitabu chako unaweza kukiita. MIMI NI YANGA AU SIMBA DAMU.

    Au USHABIKI WANGU DHIDI YA SIMBA au YANGA NI MPAKA KIFO

    Au hata unaweza kusema NIMEFUNGA NDOA NA SIMBA au NIMEFUNGA NDOA NA YANGA. hahah

    Ni mapendekezo tu. lakini hii yote ni kutaka kukuonesha kwamba unaweza kuandika kitabu kuhusiana na hili nab ado tukasoma kitbu chako.

    Kwa hiyo kuanzia leo hii usije ukasema kwamba mimi sina cha kuandika na wala sijui nianzie wapi. Aznia hapohapo.

    Tukutane siku nyingine

    Kwa maswali, maoni au booking: songambele.smb@gmail.com

    Umeshapata nakala yako? Wasiliana na 0755848391

  • Mtaka cha uvunguni

    Leo nimemkumbuka jamaa mmoja niliyesoma naye shule ya msingi na baadaye sekondari. Huyu jamaa alikuwa anapenda maisha mazuri sana, ila alikuwa hataki kufanya kazi ili kuyapata hayo maisha mazuri.

    Alikuwa anapenda kufanya kazi kwenye ofisi nzuri ila alikuwa hapendi kupitia kwenye ule mchakato wa kumfikisha kwenye hiyo ngazi. Hivi kweli kitu kama hiki kinawezekana kweli

    Yaani, itokee tu siku moja upo kwenye gari unaendeshwa kwenda kazini. unafika ofisini watu wanakuita bosi, bosi, bosi. Unasaini tu na kuondoka bila kufanya kitu chochote…Linawezekana hili kweli…

    Sidhani hata kama mabosi wenyewe wanafanya hivi..

    Kanuni ya asili ni kwamba, ili upate vinono, sharti ukubali kuvilipia gharama.

    Mtaka cha uvunguni sharti ainame.

    Huwezi kutaka kuishi maisha mazuri, wakati wewe mwenyewe  Kwa hiyo, ondoa huo mtazamo wako uliokuwa nao.

    • jua kitu unachotaka kwenye maisha, ila sasa kuwa tayari kulipa gharama ili uweze kukifikia.
    • fanya kazi kwa bidii. Waru wanaweza kukushind kwenye vitu vingine vyote. Wanaweza kukushinda kwenye kipaji, watu wanaweza kukushinda kwenye kujituma, ila wasikushinde kwenye kuchapa kazi kwa bidii. Chapa kazi kwa bidii mpaka kieleweke
    • Onesha kazi yako Haitoshi tu wewe kusema kwamba u mbunifu. Au kusema kwamba una kipaji, bila kuonesha kazi yako. Onesha kazi zako kwa watu. Watu wataziona hizo kazi, na hapo sasa ndipo wataamua kuwa wazichukue hizo kazi au la. Ila usichoke kuonesha kazi zako. Onesha kazi zako mara zote
    • na kutokea hapo sasa, ndio siku moja utajikuta upo kwenye gari unaendeshwa, upo kwenye ofisi wenye kiyoyozi na mengine mengi.

    Mimi nakuamini sana ila unapaswa pia kufanya kazi, ili hayo yote unayoyatamani yaje kwenye uhalisia.

    Umeshapata nakala zako. Kama bado wasiliana na 0755848391 ili utumiwe nakala zako popote pale ulipo duniani.

  • Hii ni kazi anbayo huwezi kuajiri mtu kuifanya kwa niaba yako

    Unaendeleaje rafiki yangu wa ukweli. bila shaka kila kitu kinaenda vizuri upande wa huko. Siku ya leo ningependa nikujuze kazi mbili ambazo huwezi kumwajiri mtu kuzifanya kwa niaba yako. Na kazi hizi siyo nyingine bali ni

    Moja kufikiri. Hiki ni kitu ambacho huwezi kumwajiri mtu ili akifanye kwa niaba yako. Badala yake ni kwamba unapaswa ukifanye wewe mwenyewe bila kujali unapitia hali gani. kufikiri kwa ajili ya kesho yako, ni jukumu lako na hakuna mtu ambaye anaweza kufanya hilo kwa niaba yako.

    Kufikiri kwa ajili ya kesho ya kampuni au biashara yako, ni jukumu lako na hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kufanya hicho kitu kwa niaba yako.

    Kwa hiyo kuanzia leo hii, fahamu kuwa huu ni wajibu wako, na hakikisha kwamba unaufanyia kazi..

    Pili ni kupanga ratiba yako. Hili ni jukumu lako jingine ambalo huwezi kumwajiri mtu kulifanya kwa niaba yako. Wewe mwenyewe unapaswa kuwa tayari kulifanya. Kila mwishoni mwa wiki unapaswa kutenga muda maalumu ambapo utaipangilia wiki yako. Muda ambapo utafanya na kukamilisha majukumu ya wiki ijayo. Na kila siku jioni unapaswa kupanga ratiba ya kesho yako. Kiasi kwamba ukiamka tu asubuhi, basi unaanza kuifanyia kazi hiyo ratiba kama ambavyo umeipangilia.

    Sikiliza kitu kimoja, kama huwezi kupangilia ratiba yako kwa ufanisi na ubora unaotakiwa, unapaswa kujua kwamba majukumu yako utayafanya hovyohovyo. Sasa kazi ni kwako. je, upo tayari kufanya majukumu yako hovyohovyo au utaanza kupangilia ratiba yako kiufanisi?

  • Mapambano yanaendelea!

    Kwenye Moira wa MIGUU, timu huwa haishindi wa kufunga goli dakika ya kwanza. Hata timu ukifunga goli dakika ya kwanza. Bado huwa haitangazwi Kuwa imeshinda.

    Badala yake Ni mchezo huwa unaendelea mpaka dakika ya 90.

    Na wewe fahamu kuwa mapambano yanaendelea. Hujafaulu kwa sababu ushindi wa muda mfupi uliopata. Huu ushindi huo wa muda ukupe NGUVU ya kuendelea mbele ila siyo kukufanya ubweteke.

    Mapambano yanaendelea.

    Imeandikwa na Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

    For booking: songambele.smb@gmail.com

  • Kiongozi ni mtu wa aina gani?

    Kwa watu wengi akitajwa kiongozi au mtu yeyote yule anayeitwa kiongozi basi wanafikiria kwamba kiongozi ni mtu mwenye cheo. Kama rais, waziri, mkurugenzi au cheo chochote kikubwa.

    Kama hauna cheo wewe siyo kiongozi. Ninachoweza kusema hapa ni kwamba watu wanachanganya kati ya cheo na uongozi. unaweza ukawa na cheo ila ukawa siyo kiongozi. Na unaweza ukawa usiwe na cheo ila ukawa ni kiongozi.

    Kwa hiyo sasa kiongozi ni nani?

    Kiufupi ni kwamba kila mtu anapaswa kuwa kiongozi. Kiongozi wa maisha yake mwenyewe. Na sifa moja kubwa ya kiongozi ni kujisimamia. Hivyo, kama wewe unaweza kujisimamia na kufanya majukumu yako bila ya kuhitaji kusimamiwa basi ujue kwamba wewe ni kiongozi.

    Kama hujaweza kujisimamia kwenye baadhi ya majukumu ambayo unafanya, basi ujue kwamba unapaswa kubadilika ili uanze kujijengea sifa za kuwa kiongozi.

    Kuna vitu unaweza kuanza kukjisimamia kuanzia leo hii na vikakufanya kuwa kiongozi.

    Kwa mfano huhitaji kuwa kiongozi ili kuamka asubuhi na mapema.

    Huhitaji kuwa kiongozi ili uweze kusema ukweli na kuwa mwaminifu.

    Huhitaji kuwa kiongozi ili uweke akiba

    Huhitaji kuwa kiongozi ili ufanye kazi kwa bidii

    Na hizo ni baadhi ya sifa ambazo kiongozi anapaswa kuwa nazo, na wewe huhitaji kuwa hata kiongozi ili uwe na hizo sifa.

    umeshapata kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO?

    kama bado, basi jipatie nakala yako sasa hivi, wasiliana na 0755848391

  • Uchambuzi wa kitabu cha Think And Grow Rich (Mambo 50 Ya Kujifunza)

    Kitabu: THINK AND GROW RICH
    Mwandishi: Napoleon Hill
    Mchambuzi: Hillary Mrosso

    Kupata kitabu cha THINK AND GROW RICH BONYEZA HAPA

    Whatever your mind can conceive and believe it can achieve.

    1. Mafanikio yote yanaanzia kwenye mawazo, na ukiyaamini mawazo yako na kuyafanyia kazi utayaona mafanikio yako.
    2. Mafanikio mara zote yanakuja kwa wale wanaofikiria mafanikio kwenye fikra zao au mawazo yao.
    3. Mwandishi wa kitabu hiki ni Napoleon, ambaye inasemekana ndie mtu mwenye ushawishi zaidi kuwahi kutokea duniani, hasa kwenye masuala ya fedha, utajiri na biashara.
    4. Utajiri sio mara zote utapimwa kwa wingi wa fedha. Utajiri unajumuisha, afya njema, mahusiano mazuri, na mwenendo mzuri wa maisha.
    5. Ili kupata unachokitaka katika maisha unahitaji kuwa na matamanio dhabiti ndani yako, matamanio na tamaa kali ya kufanikiwa ndio itakusaidia kuchukua hatua.
    6. Unahitaji dhamira ya dhati kabisa na uvumilivu mkubwa ili kufikia na kuyaona mafanikio yako.
    7. Hakuna mafanikio yatakuja bila gharama za kuumia, kupoteza, kushindwa, kukataliwa au kuchukiwa.
    8. Unahitaji kuwa kinganganizi kweli ili kufikia malengo na mafanikio unayotaka, kifedha, kiuchumi, kifamilia nk.
    9. Katika safari yako ya mafanikio, unahitaji sana imani, mani itakusukuma na kukupa matumaini ya kuendelea mbele pale mambo yanapoonekana magumu.
    10. Imani ni muhimu sana katika safari ya mafanikio maana itakufanya uendelee kuamini ndoto zako na kuzipigania kwa uvumilivu.
    11. Katika kanuni na fomula za kufanikiwa kwenye maisha ya kifedha na kiuchumi ni kutokata tamaa, kamwe usikate tamaa kuufikia mafanikio yako.
    12. Kuwa na tamaa ya kupata mafanikio, penda kupata mafanikio unayoyataka na utayafikia licha ya changamoto zitakazojitokeza.
    13. Inawezakana kushindwa na kuambiwa haiwezekani mara moja au zaidi ya mara moja, kama ndani yako kuna ule moto na matamanio ya kufikia ndoto zako, endelea kuzifanyia kazi na kuzipigania.
    14. Kushindwa kwako jambo hakutafsiri kushindwa kwa wengine, au ndivyo itakavyokuwa kwa wengine.
    15. Kama umeshindwa wewe umeshindwa wewe, usitengeneze iwe sheria kuwa kwa kuwa wewe umeshindwa iwe hivyo kwa wengine kushindwa pia.
    16. Kumbuka siku zote wewe ndio mwamuzi wa hatima yako, maisha yako ya sasa na baadaye yanaathiriwa zaidi na wewe mwenyewe.
    17. Chukua hatua juu ya maisha yako, jipe jukumu la asilimia 100 la kuwajibika na maisha yako. Usimwachie mwingine maisha yako kama vile hayakuhusu.
    18. Tengeneza maisha bora unayoyataka na unayoyafurahia kuyaishi. Kuwa na mpango wa kila siku wa kuboresha maisha yako.
    19. Hakuna atakayeishi maisha yako badala yako, hakuna anayeweza kuyabadili maisha yako bila wewe mwenyewe kuamua, imiliki hatima yako.
    20. Amua mawazo yako yatawaliwe na hisia nzuri za mafanikio, utajiri, fedha na haki. Hayo yote yapo ndani ya uwezo wako kuyaruhusu na kuyatawala.
    21. Kumbuka pia unaweza kuruhusu mambo hasi na hisia za hofu, kushindwa, magonjwa na kukata tamaa vikatawala mawazo yako. Amua kwa dhati ni mambo gani unataka yatawale na yachukue sehemu kubwa ya fikra zako na mawazo yako.
    22. Chochote kitakachotawala mawazo, hisia na fikra zako kwa kiasi kikubwa hicho ndio kitakuwa rahisi kufanyiwa kazi na kutokea kwenye maisha yako, mfano kama ni fedha, utajiri, afya, Imani, upendo, chuki, hasira, vyote hivyo vinaweza kukaa ndani ya mawazo ya mtu na vina athiri mwenendo wake wote.
    23. Kama umeamua kulivalia njuga suala la mafanikio yako, basi fanya hivyo na jiweke kwenye msitari wa mbele kabisa wa mapambano ama ufanikiwe ama ukufe, kusiwe na uwezekano wowote wa kurudi nyuma au kukata tamaa. DO or DIE.
    24. Ukiamua kuingia kwenye njia ya mafanikio na kupata utajiri, akili, mwili, roho, nafsi na kila kitu ndani yako kinatakiwa kutambua jambo moja tu, ni kupambana hadi kufikia mafanikio hayo.
    25. Ondoa uwezekano wowote wa kurudi nyuma na kukata tamaa, kushindwa kunaweza kutokea lakini kukata tamaa hakutakiwi kutokea, pambana ufikie ndoto zako au ufe ukizipambania lakini sio kukata tamaa.
    26. Usitoe ruhusa kwa mawazo au akili yako kuleta hisia za kukata tamaa kwenye mapambano ya kufikia mafanikio yako ya kifedha, kielimu, kiuchumi au kiafya, pambana mpaka pumzi yako ya mwisho.
    27. Choma madaraja yote, ziba njia zote zitakazokufanya ufikirie kutoroka uwanja wa vita, salia uwanja wa vita ukipambania ndoto zako, hatima yako na uhai wako kwa nguvu zako zote.
    28. Weka mipango imara na madhubuti ya kufikia mafanikio yako ambayo haitajali utashindwa mara ngapi ili kufikia ndoto zako.
    29. Panga na weka mipango ya kuvumilia na kuendelea kung’ang’ania kubakia katika njia ya mafanikio yako.
    30. Kutamani tu hakutakuletea matokeo, panga, weka mikakati na fanyia kazi mipango hiyo hadi ilete matokeo uliyotamani, fanyia kazi matamanio yako.
    31. Matamanio yako ni vizuri yakachanganyika na imani na hisia kali za kukufanya uchukue hatua hata kama mazingira ni magumu, hata kama hakuna hamasa yoyote.
    32. Imani ina mchango mkubwa sana katika kutuletea utajiri, usipuuze imani katika safari yako ya mafanikio.
    33. Unajua hakuna ukomo kwenye fahamu zetu, isipokuwa ukomo tuliojiwekea wenyewe. Jipe ruhusa na ruhusu ufahamu wako kufikiri makubwa ili uchukue hatua kubwa zitakazo kuletea mafanikio makubwa.
    34. Utajiri na umasikini vyote vinaanzia au vinazalishwa na mawazo. Chagua mawazo unayotaka kazalisha katika fikra zako.
    35. Hakuna kinachoingia kwenye mawazo yetu bila sisi wenyewe kutoa ruhusa hiyo, toa ruhusa kwa mawazo chanya ya mafanikio kuingia katika fikra zako nafahamu zako.
    36. Maarifa pekee hayaleti utajiri wala fedha, kinacholeta utajiri na fedha ni matumizi ya maarifa uliyojifunza au kusikia. Fanyia kazi maarifa au elimu uliyoipata ili ilete matokeo.
    37. Onyesha maarifa yako kwa njia ya matendo, matendo yana nguvu na ushawishi zaidi, tekeleza unachojifunza.
    38. Maarifa bora hayataleta maisha bora kama huyatatekeleza. Uwe mtendaji wa neno usiwe msikiaji tu.
    39. Panga kabisa tena kwa kumaanisha kuwa utakachojifunza utakifanyia kazi, utaweka kwenye matendo unachojifunza, au maarifa unayopata.
    40. Thamani ya maarifa ipo pale unapoamua kuiweka kwenye matendo au kutekeleza. Jiahidi nafsi yako kuwa utaanza kufanyia kazi maarifa, ujuzi na elimu uliyoipata.
    41. Utofauti kwenye maisha unakuja pale unapoamua kufanyia kazi maarifa au elimu uliyoipata. Jitofautishe na wengine kwa kuwa mtendaji zaidi.
    42. Jifunze kila siku kuboresha ujuzi wako, pata maarifa ya kutosha kuhusu utalamu wako, itakufanikisha sana.
    43. Nidhamu ni muhimu sana katika safari ya mafanikio. Kama huna nidhamu huwezi kufika kwenye mafanikio yako.
    44. Nidhamu binafsi ndio kazi kubwa ambayo itakugharimu sana kuifanya.
    45. Tunahitaji nidhamu kwenye kila eneo la maisha yetu, nidhamu ya fedha, nidhamu ya muda, nidhamu ya kuendelea kufanyia kazi malengo yetu.
    46. Moja ya kazi kubwa unatakiwa kuifanya kwenye maisha yako ni kujizuia, kujidhibiti, kujitawala na kujiweza. Kama utafanikiwa kujitawala na kujiweza, basi umefanikiwa.
    47. Sio vizuri kuwapa wengine jukumu la kukusimamia, kukudhibiti ili uwe na nidhamu, jipe wewe mwenyewe hili jukumu liwe ndio jukumu la maisha yako yote.
    48. Kabla hujaanza kusimamia na kuwaongoza watu wengine, jisimamie, jimiliki, na jiongoze wewe mwenyewe kwa mafanikio kwanza.
    49. Uhuru wa kweli upo pale unapoweza kujidhibiti, kujizuia na kujitawala. Utumwa ni pale unapokosa utawala na udhibiti kwenye maisha yako binafsi.
    50. Dhibiti na tawala kila eneo la maisha yako, kifedha, afya, hisia, mapenzi, kazi, chakula, nk. Ukiweza kudhibiti mambo hayo utakuwa na maisha huru yenye afya na furaha.

    Kitabu hiki kina mambo mengi sana ya msingi kwa ajili ya kuboroesha maisha yetu, hakifai hata kuchambua maana kila kilichoandikwa ni mafunzo muhimu sana. Nashauri kila mtu akisome kitabu hiki ili aboreshe maisha yake na ya watu wengine. .

  • Jinsi Ya Kufanikisha Ndoto Zinazohitaji Fedha Nyingi

    Kwenye video ya leo kupitia channel yetu ya YouTube nimeeleza kwa kina ni namna gani unaweza unaweza kupata na kutunza fedha ya kukusaidia Kufanikisha ndoto yako kubwa. Je, upo tayari kwa ajili ya hiki? Ebu tazama video yenyewe hapa

    Hakikisha umejiunga na mfumo wetu wa kupokea makala maalumu kikashani mwako kwa kujaza taarifa zako hapa chini.

    usisite kuagiza nakala ya kitabu chako cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO ili uweze kutumiwa popote pale ulipo. Kupata nakala ya kitabu hiki, wasiliana nami kwa 0755848391

    For bookings: songambele.smb@gmail.com

  • Huu ndio utaratibu mzuri ambao unapaswa kuujenga kuanzia mwezi huu

    Moja ya sifa ya watu wanaofanya makubwa kwenye hii dunia ni tabia ya kujifunza. Hii ni tabia moja muhimu ambayo inaweza kukusaidia wewe kufanikisha mambo makubwa kwenye hii dunia. Kama bado unajiuliza ni kwa jinsi gani kusoma kunaweza kukusaidia wewe, chukua hatua. Utoe mwaka mmoja ambapo utajifunza kila siku. Kisha linganisha huo mwaka na miaka mingine ya nyuma ili uweze kuona utofauti.

    Baada ya mwaka mmoja, linganisha mwaka wako huo mmoja ambao ulikuwa unasoma vitabu na ile miaka ambayo ulikuwa husomi. Kusoma ni jambo la muhimu sana kwenye maisha yako ya kila siku, kama kula kulivyo muhimu kwenye maisha yako ya kila siku.

    Kwa hiyo, anza kujijengea utaratibu wa kusoma vitabu kuanzia leo hii. Lakini, haupaswi kuishia hapo tu. Badala yake unapaswa pia, kujenga utaratibu mzuri wa kununua walau kitabu kimoja kila mwezi. Kila unapopokea mshahara, hakikisha kwamba, unatoa kiasi fulani kwa ajili ya tu ya kununua vitabu au kitabu. Hiki kitu kidogo tu, kinaweza kukusukuma na kukufikisha mbali.

    Fedha yako ya kununua kitabu, inaweza kuwa ni fedha hiyohiyo ambayo wewe unatumia kufanya mambo ambayo si ya muhimu kwa sasa.Ila sasa kwa kuwa umejijengea utaratibu huu wa kusoma vitabu. Unaamua kuanza kuiwekeza hii fedha kwa ajli ya baadaye yako.

    Rafiki yangu, anzisha huu utaratibu. Nina hakika mwaka mmoja baadaye utanishukuru kwa ajili ya huu utaratibu wa kipekee ambao utakuwa umeuanzisha. Je, upo tayari kwa ajili ya hiki kitu.

    Kama upo tayari, anza kuwa kuchukua kitabu cha JINSI YA KUFIKI ANDOTO ZAKO Toleo la 2.

    Kwenye hiki kitabu unaenda kujifunza namna ambavyo utaweza kufanikisha ndoto zako kubwa za kimaisha. Je, upo  tayari?

X