Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Sababu Moja Kwa Nini unapaswa kuandika kitabu chako Leo

    Rafiki yangu wa ukweli Karibu kwenye makala ya jumapili ya leo. Leo ninataka nikwambie kwa nini unapaswa kuandika kitabu chako kuanzia leo hii.

    Ninachofanya leo ni kukuongezea nyama kwenye kile ambacho nimewahi kuandika.

    Na hapa ninasema kwamba, unapaswa kuandika kitabu chako kwa sababu kesho na kesho kutwa unaweza usiwe hapa duniani.  Sasa  kuandika kitabu kutakufanya uache ujumbe kwa watu wa Karibu yako ili wajue fikra zako, kile ulichokuwa unasimamia kwenye maisha, ulipotoka mpaka kufika ulipofika. Kwa hiyo, kwamwe usisite kuandika kitabu chako. Anza leo hii kuandika kitabu chako.

    Nina hakika wewe babu yako angekuwa ameandika kitabu, leo hii ungekuwa unaenda kukitafuta kukisoma. Kwa hiyo, kama ambavyo wewe unatamani kujua kitu kuhusu historia ya wazazi wako, hivyohivyo, andika kitu uwaachie wanao na wajukuu wako.

    Upo tayari kuandika kitabu chako? Karibu upate kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA. Kitakusaidia sana wewe kuanza kuandika kidogokidogo mpaka kukikamilisha hatuahatua. Kwa mfano kwenye kitabu nimeeleza kuwa unaweza kuandika kitabu chako Kama unavyoandika SMS.

    Ebu fikiria kwa siku unaandika na kujibu SMS ngapi? Kwa mwaka hizi SMS zikiuunganishwa ni sawa na kitabu chenye ukubwa kiasi gani?

    Ukiangalia hili, utagundua kuwa kitabu chako kinaweza kuwa kikubwa kama utatumia mbinu hii tu.

    Kitabu kimeeleza vitu vingine VIDOGO unavyoweza kutumia kwenye kuandika kitabu chako na kukiuza kwa mafanikio.

    Karibu upate nakala yako. Gharama yake ni 20,000/- na unatumiwa popote ulipo.

    Lakini pia nina kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30. Hiki nacho kinakuhusu pia. Kwa Sasa hiki kitabu kinapatikana kwa 5,000/- tu kwa mfumo wa softcopy. Karibu sana tuko pamoja.

    Kupata vitabu hivi wasiliana na 0755848391.

    Kila la kheri.

    kwa maoni, Ushauri na maswali: godiusrweyongeza1@gmail.com

    for booking: songambele.smb@gmail.com

  • Baadaye siku ya leo, nitakuwa CLOUDS FM nikiongelea Gharama za Kulipa ili kufikia ndoto zako

    Helo upande wa huko. Godius Rweyongeza hapa na leo nina taarifa fupi tu kwako.

    Taarifa hii ni kwamba baadaye siku ya leo nitakuwa CLOUDS FM, Kwenye kipindi Cha TEMINO.
    Mada nitakayozungumzia Ni GHARAMA ZA KULIPA ILI KUFIKIA NDOTO ZAKO

    Kipindi hiki kinaendeshwa na Harris KAPIGA pamoja na adv. Henry Mwinuka.

    Muda wa kipindi ni saa 9 mchana hadi saa 11 jioni.

    Hakikisha unafuatilia hiki kipindi. Kuna mengi ya kujifunza siku ya leo.

    Moja ya kitu ambacho nimejitoa kuhakikisha nakifanya kwa weredi ni kuambatana na watu wenye ndoto kubwa. Sipendi kabisa watu wenye ndoto ndogo. Na ndio maana nimeandika kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO kwa ajili watu wenye ndoto kubwa tu. Upo tayari kuzifikia ndoto zako kubwa kwa viwango vikubwa? Basi hakikisha unapata nakala ya kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO.

    Gharama ya nakala moja Ni 20,000/-. Tuwasiliane sasa kwa 0755848391 ili uweze kupata nakala yako leo.

  • Hii Ndio Aina Bora Uwekezaji Unayoweza Kufanya. Hakuna Uwekezaji Wenye Manufaa Kama Huu

    Moja ya kitu ambacho watu wanatafuta na wangependa kupata maishani mwao ni uwekezaji mzuri. Najua na wewe unasoma hapa kwa sababu unataka uwekeze fedha zako sehemu ambayo itakupa faida kubwa. Sasa siku ya leo nataka nikwambie eneo zuri ambalo wewe mwenyewe unaweza kuwekeza na kupata faida.

    Kwa siku sasa nimekuwa nikikwambia maeneo ya kuwekeza na hasa kwenye hisa, hatifungani na VIPANDE.

    Huu Ni uwekezaji mzuri ambao hado nashauri uufanye, Tena kwa nguvu zako zote.

    Ikiwezekana tumia nguvu ya vitu vidogo kufanya uwekezaji huu. Yaani, anza kuwekeza kidogo kidogo, Kisha endelea kuwekeza kidogo kidogo bila kuacha kwa muda mrefu. Hiki kitu kidogo unachowekeza baada ya muda mrefu kitageuka kuwa kikubwa kwa kutumia kanuni ya riba mkusanyiko.

    Ila ukiachana na huu uwekezaji wa Hisa, hatifungani na vipande kuna uwekezaji mwingine mzuri ambao unaweza kuufanya na ukakupa faida kubwa pia. Na uwekezaji huu ni Kuwekeza kwenye matangazo ya BIASHARA yako.

    Huu ni uwekezaji mwingine ambao unaweza kuufanya, ukakupa faida na matokeo kwa muda mrefu ujao.

    Matangazo mara zote yanalenga kuleta wateja watakaonunua bidhaa fulani kwenye BIASHARA yako. Sasa matangazo yako yakifanyika vizuri, yana uwezo wa kuleta matokeo makubwa kuliko uwekezaji mwingine ambao tayari nimekwambia hapo mwanzoni.

    Kwa Nini?
    Kwa sababu, takwimu zinaoneshwa kuwa WAWEKEZAJI wakubwa kwenye soko la hisa, hatifungani, vipande na hata WAWEKEZAJI wa  fedha za kigeni huwa wanapata faida yenye ukomo.
    Mwekezaji Warren Buffet ndiye mwekezaji mwenye mafanikio ambaye huongelewa sana linapokuja suala zima la uwekezaji. Ila takwimu zinaoneshwa kuwa huwa anapata faida ya asilimia 20% ukuaji wa mwaka.

    Siyo Warren Buffet peke yake tu, hata WAWEKEZAJI wengine kama
    Carl Icahn anapata  31% ya ukuaji kwa mwaka.
    George Soros anapata 20% ukuaji wa mwaka.
    Peter Lynch anapata 29% ya ukuaji wa mwaka.

    Kwa hiyo nataka kusema tusiwekeze?
    Hapana. Ninapenda uwekezaji na Mara zote nimekuwa nikishauri uwekeze kwenye HISA, hatifungani na vipande. Kama Bado hujafungua akaunti yako ya uwekezaji, ujue wazo kuwa unajinyima fursa nzuri ya kupata faida kwa muda mrefu. Kafungue akaunti Leo hii na uanze kuweka fedha kidogo kidogo kama uwekezaji. Nimeandika mpaka kitabu cha uwekezaji kwenye hisa. Kinaitwa MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE.

    Ila sasa kikubwa ninachotaka ufanye pia ni Kuwekeza kwenye matangazo ya BIASHARA yako . Itangaze BIASHARA yako Mara kwa Mara na kila sehemu ambayo unajua inaweza kukuletea wateja. Huu ni uwekezaji ambao una faida kubwa sana.

    Ukifanya tangazo lako vizuri, utakuta kuwa tangazo Hilo linakuletea faida kubwa hata Mara 10 ya ule uwekezaji uliofanya mwanzoni.

    Unaweza kuwekeza laki moja ukapata mpaka faida ya milioni. Yaani, unatangaza kwa laki moja, unapata faida ya milioni moja. Faida ambayo ni ngumu kuipata kwenye uwekezaji wa kawaida wa hisa, hatifungani na vipande.

    Hivyo kumbe, BIASHARA yako inapaswa kuwa sehemu ya kwanza kabisa ambapo utafanya uwekezaji. Kisha baada ya hapo wekeza maeneo mengine.

    Je, upo tayari kuwekeza kwenye BIASHARA yako na kuikuza kwa viwango vikubwa? Upo tayari?
    Kama upo tayari kuikuza BIASHARA yako kwa viwango vikubwa, nashauri usome kitabu changu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA.

    Ili uone hii nguvu inavyoweza kufanya kazi kwa ajili yako pia.

    Kila la kheri

    Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Dar-Tz
    Kwa maoni, Ushauri na maswali: godiusrweyongeza1@gmail.com

    For booking: songanbele.smb@gmail.com


  • Usifurahie kitu hiki kwenye maisha yako

    usifurahie kuitwa mnyonge. Hivi umewahi kujiuliza unyonge wako uko wapi? Sasa kwa nini watu wanakuita mnyonge na muda mwingine wanasema kwamba, wanakutetea wewe. Sikiliza, pambana kwa hali yoyote ile kuhakikisha kwamba wewe hauwi mnyonge. Kwa asili ni kwamba vitu vinyonge huwa havidumu. Sisi wenyewe hatupendi tukae na vitu vinyonge. Mfugaji wa ng’ombe hawezi kukaa na ng’ombe mnyonge mwaka mzima anamlisha tu. lazima atamuuza au atamchinja.

    Na kadiri ya sheria ya Darwin vitu vinyonge, havidumu. Huwa vinatoweka na kuisha kabisa, huku vitu ambavyo ni imara, vikizidi kudunda tu. sasa kazi ni kwako, kuhakikisha kwamba hauwi mnyonge kwenye kile unachofanya, badala yake unaamua kuwa ngangali.

    Kama ni fedha,pambana kuhakikisha kwamba unakuwa nayo. Kama ni kazi pambana kuhakikisha

    Rafiki yangu usikubali kuwa mnyonge.

    Umekuwa nami,

    Godius Rweyongeza

    0755848391

    Morogoro-Tz

    Kwa maswali, maoni au ushauri: godiusrweyongeza1@gmail.com

    For bookings: songambele.smb@gmail.com

  • Leo ndiyo siku ya mwisho ya kupata kitabu cha jinsi ya kufikia ndoto zako kwa bei ya ODA

    Habari ya upande wa huko rafiki yangu. bila shaka unaendelea vyema kabisa. Nimekuwa nikikutaarifu kuwa leo ni siku ya uzinduzi wa kitabu cha jinsi ya kufikia ndoto zako. kitabu hiki cha kipekee kimeeleza kwa kina, jinsi gani unaweza kugundua ndoto zako na kuzifanyia kazi mpaka zikatimia.

    Hivi umeshajiuliza swali ee! Kwa nini natumia neno ndoto zako? Ukweli ni kwamba hauwezi kuwa na ndoto moja tu. ni lazima utakuwa nazo nyingi, kwenye kitabu nimeeleza kwamba ni haki yako kuwa na ndoto nyingi, lakini sasa linapokuja suala zima la kuzifanyia kazi ndio unapaswa kuzifanyia kazi moja baada ya nyingine.

    Kitabu hiki cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO, kinazinduliwa rasmi leo kwenye kundi maalumu la kuweka oda. Kama wewe hauko kwenye hili kundi unapaswa kufanya hivi. Weka oda yako hapa. Baada ya kuweka oda utatumiwa kiunzi maalumu cha kuingia kwenye kundi la kuweka oda.

    Gharama ya kitabu hiki ni 20,000/- ila ukilipia leo nakala yako utaipata kwa 15,000’- tu. leo ni siku ya mwisho ya kupata nakalayako kwa bei ya oda.

    Rafiki yangu kiukweli nisingependa wewe ukose nakala hii ya kipekee kwenye maktaba yako. Kitu kikubwa cha kufanya sasa hivi. ni kuweka oda yako kupitia kiunzi hiki hapa. Baada ya hapo utapewa utaratibu wakulipia na nakala yako, itatumwa bila kuchelewa.

    Rafiki yangu karibu sana uweze kujipatia nakala ya kitabu hiki cha kipekee sana.

    Umekuwa nami,

    Godius Rweyongeza

    0755848391

    Morogoro-Tz

  • KUHUSU KITABU: NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA

    Hivi umewahi kujiuliza kuwa vitu vidogo vinaweza kukusaidia kitu gani maishani mwako?

    Mara nyingi sana watu huwa wana ndoto kubwa na malengo makubwa ya kufikia kifedha, kimahusiano, kibiashara au kikazi. Lakini cha kushangaza ni kwamba huwa hawafanyii kazi hizo ndoto kubwa walizonazo bali huwa wanasubiri itokee siku moja ya muujiza ambapo ndoto yao itatimia kwa asilimia zote.

    Kwenye kitabu hiki unaenda kujifunza nguvu ya vitu vidogo na namna ambavyo unaweza kutumia nguvu hii kwenye maisha yako ya kila siku, kufanya makubwa.

    Kupata kitabu hiki, wasiliana na 0755848391. Nakala unatumia popote ulipo. Gharama ya kitabu hiki ni 20,000/-

    Umekuwa nami,

    Godius Rweyongeza

    0755848391

    kwa maoni, ushauri au maswali: godiusrweyongeza1@gmail.com

    For bookings: songambele.smb@gmail.com

  • JINSI YA KUANZA UPYA BAADA YA KUANGUKA

    Huwa inatokea mtu anaanza kitu unakikuza lakini inafikia hatua ambapo unapata anguko na kurudi chini. Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha kuanguka, ikiwa ni pamoja na kupumzika kwa nguvu baada ya kuwa umefika juu. Au inaweza kutokana na sababu kuwa mwanzoni ulikuwa na lengo kubwa, ila baada ya kuwa umefikia juu au baada ya kuwa umefikia hilo lengo, sasa umekosa lengo kubwa zaidi.

    Unakuta labda mtu ana lengo la kujenga nyumba, na kuitunza familia yake. Anapambana, anafikia hatua ambapo anapata hela ya kutosha kumwezesha yeye kujenga na kuitunza, sasa mtu huyu unakuta analala na kujisahau, sasa kitu hiki, na mwingine ni ile hali ya kupokea fedha nyingi kwa wakati mmoja. Anakuwa hajui namna ya kuzitunza na kuzitumia vizuri, anazitumia hovyo, mwisho wa siku, anaingia mkenge.

    Sasa leo nataka nikueleze ni kwa namna gani unaweza kuanza upya baada ya kuanguka.

    Lakini kabla sijakwambia hiyo, nataka nikwambie hauko peke yako. Kiuhalisia ni kwamba watu wengi huwa wanaanguka. Hakuna mtu ambaye huwa anaanzisha kitu na kukifanikisha moja kwa moja bila kupitia anguko lolote. Laiti kama maisha yangekuwa hivi, basi ni wazi kuwa kila mmoja angekuwa amefanikiwa sana.

    Maisha ni kama huwa yana tabia ya kumjaribu mtu kuona kweli huyo mtu yuko siriazi na mafanikio anayoyataka? Yupo siriazi kweli.  Na hapo ndipo kushindwa hutokea, ila kushindwa kwa kawaida siyo kushindwa, kushindwa ni fursa.

    Leo hii nataka nikuoneshe namna gani unaweza kuanza upya baada ya kuwa umeanguka.

    Kitu cha kwanza kabisa kama umeanguka ni wewe kujua kwa nini umeanguka. Jiulize, hivi imekuwaje mpaka nimeanguka wakati nilikuwa juu kabisa. halafu hizo sababu zitunze vizuri ili zisije zikakuangusha tena baadaye, maana ukifuatilia, vitu ambavyo huwa vinawaangusha watu ni vile vile. Hivyo, ukijua kilichokuangusha  wewe, hata ukianza upya utakiepuka.

    pili, kama umeanguka, hakikisha sasa unaweka mipango mipya ya kule unapotaka kwenda. Anzia palepale ulipo. Kisha endelea kusonga mbele. Unaweza kufika unapotaka na hata zaidi ya hapo. ubora ni kwamba kama ulishawahi kufika juu ukaanguka, unajua mchakato wote wa kufika huko. Na zamu hii itakuchukua muda kidogo zaidi maana mbali ya kuwa unaanzia chini, ila kuna baadhi ya vitu ulishavijenga tanagu mwanzoni ambavyo utavitumia sasa. mfano, vitu kama konekisheni, hata kama ulianguka, haimaanishi kuwa na konekisheni zako zote zilianguka. Kuna konekisheni ulizonazo sasa hivi, ambazo unaweza kuanza kutumia ili kusonga mbele.

    Tatu penda kujifunza. unapaswa kuzama zaidi kwenye kujifunza ili upate maarifa yatakayokusaidia wewe kuinuka na kusongambele. Kama ambavyo nilikudokeza ni kuwa makosa ambayo watu wanafanya na kuwaangusha siyo kwamba ni mapya, ni makosa ambayo yamekuwa yakifanyika enzi na enzi, tokea enzi za mababu zetu. Ila tatizo ni kwamba watu hatujifunzi.

    Mfano kama mahusiano yako yanaenda vibaya, haimaanishi kwamba, hilo tatizo linalokukumba wewe ni la kipekee na halijawahi kutokea hapa duniani, unachopaswa kujua ni kuwa limewahi kutokea na kuna watu wengine wamewahi kupitia kwenye hali mbaya zaidi ya kimahusiano kuliko hata wewe hapo. ila waliweza kutatua hiyo changamoto.

    Tatizo lako ni kwamba hujifunzi na hupendi kusoma vitabu. na ndio maana unaendelea kurudia makosa yaleyale waliyofanya wengine, na kitu hiki kitakufanya uendelee kuanguka zaidi. Penda sana kujifunza.

    Jifunze kuhusu biashara

    Jifunze kuhusu mahusiano

    Jifunze kuhusu fedha na mambo mengine ambayo unaweza kujifunza.

    Kuanguka chini siyo tiketi ya wewe kutojifunza au kuwekeza kwenye vitabu. kuanguka chini kunapaswa kuwa ni tiketi yako ya kuanza upya, na tena zamu hii ukianza upya unapaswa ukue bila kurudi nyuma mpaka watu washangae.

    Nne, jenga utaratibu wa kujifanyia tathimini kila mwezi , kila wiki na kila siku. Jiulize, hivi kweli nazidi kusongambele au ndio narudi nyuma. Kutojifanyia tathimini kunaweza kukufanya uanguke chini, kwa sababu kila mara utakuwa unajiona kama uanafanya vitu vinaenda sawa, ila kumbe kuna sehemu unakosea. Unaona ee. Hivyo, kila mara jiulize hivi kweli nipo kwenye njia sahihi? Hivi ni kweli nazidi kusongambele kama ninavyostahili au ndio narudi nyuma?

    Jifanyie tathimini mara kwa mara.

    Hii itakusaidia kwanza kuwekeza vitu na nguvu zako kwenye vitu vichache unavyoweza kufanya kwa ustadi.

    NB. Tumeanza kusambaza vitabu vya jinsi ya kufikia ndoto zako. nakala ngumu (hardcopy). Kitabu hiki kinatumwa popote pale ulipo Afrika Mashariki. Hakikisha unapata nakala yako leo hii kwa bei ya punguzo. Yaani badala ya 20,000/- unapata nakala yako kwa 15,000/- tu. Mwisho wa kupata kitabu kwa bei ya oda ni tarehe 20. Jionee mwenyewe chini hapa muda uliobaki kupata nakala kwa bei hiyo hapo chini

    [wpcdt-countdown id=”5798″]

    Umekuwa nami,

    Godius Rweyongeza

    0755848391

    Kwa maoni, ushauri au maswali: godiusrweyongeza1@gmail.com au info@songambele.co.tz

    For bookings: songambele.smb@gmail.com au songambele@songambele.co.tz

  • Unafanyaje ili kupata mbia sahihi wa biashara

    Leo nataka tuongeelee kuhusu ubia wa biashara. Ikiwa ni moja ya kitu muhimu sana kwenye biashara ambacho unakihitaji hasa kama umelenga kufika mbali. Ubia kwenye biashara unakutanisha watu wenye ujuzi, elimu na hata fedha ambapo wanaungana kutengeneza kitu kimoja. Kwenye biashara ubia ni muhimu sana hasa kama unataka kufika mbali.

    Kitu kikubwa unachohitaji kujua kuhusu biashara ni kwamba biashara ni mchezo. Na kama mchezo, una kanuni na taratibu zake, hivyo unapaswa kuzifuata hizi kanuni na taratibu za biashara au kwa manufaa yako, au la unapaswa kuzivunja kwa hasara yako pia.

    Sasa vifuatavyo ni vitu muhimu unavyohitaji kujua kuhusu mbia wako.

    Kwanza unahitaji kumjua mbia wako vizuri.  Hiki kitu ni muhimu sana kwenye biashara kutokana na ukweli kuwa huyu mtu unaenda kufanya naye kazi kwa muda mrefu.Ni mtu ambaye ambaye mnaenda kujenga kitu kikubwa, hivyo, unahitaji kumjua vizuri huyu mtu wako

    Pili fahamu kuwa mbia wako siyo lazima awe mtu mwenye fedha nyingi sana, siyo mtu mwenye ushawishi mkubwa, siyo mwanasiasa, mwenye jina kubwa au mtu wa aina hiyo. Mbia wako ni mtu kama wewe ambaye mnaweza kuendana kwenye kufanyia kazi kile unachofanya. Kikubwa awe ni mtu ambaye mnaweza kuendana kwenye biashara yenu.

    Tatu, Mbia wako awe na ujuzi ambao unaweza kujazilia kwenye kile ulichonacho wewe na yupoo tayari kufanya kazi kwa bidii, naam bidii sana.

    Nne, Usivunje makubaliano uliyowekeana na mbia wako hata kama utagudua kuwa ule ubia mlioweka, kuna hila fulani zilifanyiaka wakati mnaweka huo ubia. Badala ya kwenda kinyume na makubaliano, utapaswa kumwita ili mkae chini na kuweka sawa kile ambacho unaona kwamba hakijakaa sawa.

    Kwa leo nimeona nikushirikishe hayo mambo machache kuhusu ubia na namna ambavyo unaweza kuutumia ubia kwa manufaa.

    NB. Tumeanza kusambaza vitabu vya jinsi ya kufikia ndoto zako. nakala ngumu (hardcopy). Kitabu hiki kinatumwa popote pale ulipo Afrika Mashariki. Hakikisha unapata nakala yako leo hii kwa bei ya punguzo. Yaani badala ya 20,000/- unapata nakala yako kwa 15,000/- tu. Mwisho wa kupata kitabu kwa bei ya oda ni tarehe 20. Jionee mwenyewe chini hapa muda uliobaki kupata nakala kwa bei hiyo hapo chini

    [wpcdt-countdown id=”5798″]

  • Ukifanya kitu unachopenda Ubunifu unakuwa mwingi.

    …….muda si mrefu nimetoka kuongea na mteja wetu mmoja ambaye yuko mkoani Mara (Msoma mjini).
    Ambaye amepokea kitabu Cha jinsi ya kufikia NDOTO ZAKO na kuanza kukisoma.

    Kitu cha pekee nilichopenda kutoka kwake ni usemi wake anaosema kuwa ukifanya kitu unachopenda, Ubunifu unakuwa mwingi.

    Na hiki kitu nimeona nikushirikishe na wewe pia.

    Kuna utafiti unaonesha kuwa watu wengi wanakufa siku ya jumatatu baada ya kula Bata wikendi halafu jumatatu wanaamka na kwenda kufanya kazi wasiyopenda. Hicho kitu tu, kinawakatisha tamaa.

    Ndiyo maana nimeupenda huu usemi, kiasi cha kuwa tayari kukushirikisha huu usemi na wewe.

    Ujumbe mkubwa nilio nao kwako siku ya leo ni kwamba ufanye kazi au kitu unachopenda.

    Ukifanya kitu unachopenda hutachoka
    Ukifanya kitu unachopenda ubunifu unakuwa mwingi.

    Thomas Edison alikuwa analala saa tatu kwenye maisha yake na kuamka mapema kwenda kazini. Siku moja aliulizwa kwa nini unafanya sana kazi.

    Aliwajibu watu kwa kuwaambia kuwa sijawahi kufanya kazi.

    Umeona ee! Alikuwa anafanya kitu anachopenda. Hivyo, kwake hakuona kama hiyo ilikuwa kazi.

    Hivi wewe unafanya unachopenda kweli? Unafanya unachopenda?

    Ngoja nikukumbushe, “ukifanya kitu unachopenda, ubunifu unakuwa mwingi”.

    Kwa jioni ya leo naishia hapa.

    Halafu ujue kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO kipo tayari. Na watu wanapokea nakala zao popote pale walipo. Wewe pia unaweza kupata nakala yako kwa Bei ya oda. Ujue gharama ya kitabu hiki ni 20,000/- Ila habari njema ni kuwa ukilipia kitabu hiki kabla ya tarehe 20 Mei. Utakipata kwa 15,000/- unaanzaje Sasa kwa mfano kukosa nakala yako.

    Ebu nitumie ujumbe wako sasa hivi

    Tuma ujumbe kwa
    0755848391
    Au WhatsApp
    https://wa.me/message/3PMZSAFONLHAP1

    Ili utumiwe kitabu chako.

    Umewkuwa nami
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

    Ukifanya kitu unachopenda ubunifu unakuwa mwingi.

  • Tumebaki Na Siku 3 Tu Za Kupata Kitabu Cha Jinsi Ya Kufikia Ndoto Zako Kwa Bei Ya Oda

    [wpcdt-countdown id=”5798″]

    Hello, habari ya leo. Bila sahaka unaendelea vyema.

    Kwa siku sasa nimekuwa nikikwambia kuhusiana na kitabu cha jinsi ya kufikia ndoto na jinsi ambavyo unaweza kupata nakala yako. Kitabu hiki kinazinduliwa tarehe 20 Mei, hata hivyo, oda zimeshaanza kuwekwa.

    Nikieleza Jambo kuhusu kitabu

    Na ubora ni kuwa nakala za kitabu zimetoka mapema. Hivyo, nimeona badala ya kusubiri mpaka tarehe 20 Mei ndio nitume vitabu. NI bora nianze kutuma nakala sasa hivi, maadam zipo. Kwa hiyo, kila aliyeweka oda ya kitabu na kulipia. Tayari ametumiwa kitabu chake au la anatumiwa leo na wengine vitabu vyao vipo njiani.

    Sasa leo wakati naagalia kwenye tarehe hapa, nikaona kwamba, zimebaki siku chache tu kabla ya tarehe ya mwisho ya wewe kupata kitabu hiki kwa bei ya oda.

    IPO HIVI, kitabu hiki gharama yake ni 20,000/- ila ukiweka oda siku ya leo unaenda kupata kitabu hiki kwa gharama ya 15,000/- tu.

    Sasa kilichobaki rafiki yangu ni wewe kuchangamka ili uweze kupata kitabu hiki.

    Cha kufanya sasa hivi, weka oda yako kwa kutuma ujumbe kwenda namba 0755848391

    Tuma ujumbe wenye jina lako

    Namba yako na mahali ulipo.

    Mfano: Godius Rweyongeza 0755848391 (Morogoro mjini-Morogoro)

    Ukishatuma huo ujumbe utapewa maelekezo ya kulipia, ili uweze kupata nakala yako mapema.

    Karibu sana rafiki yangu, tuko pamoja.

    Audiobook ya kitabu pia ipo

X