-
Siri Hii Wanayoijua Matajiri Unapaswa Kuijua Pia
Tujifunze kwa bahari Kila mwaka huwa kuna mito na vijito ambavyo huwa huwa vina maji na baadaye hukauka. Wakati mito hivi na vijito, vikikauka, bahari huwa haikauki hata siku moja. Unajua kwa nini bahari huwa haikauki, moja ya kitu ambacho huwa kinafanya bahari isikauke ni kwa sababu huwa inapokea maji kutoka kwenye vyanzo vingi. Kadiri…
-
Baadhi Ya Vyanzo Vya Kipato Ambavyo Unaweza Kuwa Navyo
1. AjiraHiki ni chanzo maarufu ambacho wengi huwa wanakuwa nacho. Chanzo hiki huwa kinaingiza kipato (ujira) kila baada ya muda fulani (siku,wiki au mwezi). Kwa MTU yeyote ambaye hana sehemu ya kuanzia hakikisha walau unaanzia kwenye ajira. Ukipata ajira hakikisha unaifanya kwa uaminifu na kwa kujituma. Maana ajira inaweza kukupelekea wewe kupata vyanzo vingine zaidi.…
-
Viashiria Vinne Vya Uhuru wa kweli. Kama hauna hivi vitu jua huna Uhuru..
Leo Ni tarehe 9 Disemba, ni siku uhuru hapa nchini Tanzania. Sikupanga kuandika chochote kuhusiana na uhuru, ila ngoja niandike haya machache kuhusiana na uhuru wako binafsi. Watu wengi huwa wanachanganya kuwa kwa kuwa nchi iko huru Basi na wao wako huru. Siyo kweli, Kuna viashiria ambavyo vinaweza kuonesha kuwa wewe uko huru au hauko…
-
Kwa Nini Unahitaji Kuwa Na Vyanzo Vingi Vya Kipato
Unahitaji Kuwa na vyanzo vingi vya kipato Moja ya Kitu Cha muhimu ambacho unahitaji kuhakikisha umekizingatia ni kuwa na vyanzo vingi vya kipato. Labda swali la kwanza la kujiuliza ni je, vyanzo vingi vya kipato maana yake nini? Vyanzo vingi vya kipato, Ni pale unapokuwa unaingiza kipato kwa njia zaidi ya moja. Yaani, siyo tu…
-
Jinsi Ya Kufungua akaunti ya mfuko wa FAIDA (FAIDA FUND)
Juzi niliandika makala kuhusu mfuko wa FAIDA (FAIDA FUND). Swali ambalo nilipokea kutoka kwa wengi waliosoma makala hii lilikuwa ni kwa namna gani naweza KUFUNGUA akaunti kweye mfuko huu wa FAIDA. KITU hiki kimenisukuma nikuandalie Makala nyingine kukuonesha ni kwa namna gani unaweza KUFUNGUA akaunti kwenye mfuko huu wa FAIDA. Unajua unawezaje kufungua akaunti. Fanya…
-
Kitu Kimoja Kinachopaswa Kukufanya Usome Vitabu Vya Hardcopy badala ya Softcopy
Rafiki yangu, linapokuja suala la softcopy au hardcopy watu wamekuwa wanakuwa na mtazamo tofauti. Wapo wanaopendelea hardcopy na wapo wanaopendelea softcopy na wengine wanapendelea audiobook kama huyu hapa Kwa upendeleo wowote atakaokuwa nao mtu, hakuna ambaye anakuwa sahihi wakati mwingine akiwa hayuko sahihi. Kitu kikubwa sana ni kupata maarifa yaliyo kwenye kitabu na kuyafanyia kazi.…
-
Jinsi ya kupata matokeo ya tofauti mwaka 2023
Kuna kitu kimoja nakijua kuhusu wewe rafiki yangu. Na kitu hiki ni kwamba mwaka 2023, ungependa kupata matokeo ya tofauti. Matokeo ya tofauti kwenye kila eneo ambalo utakuwa ukilifanyia kazi. Kama unataka kupata matokeo ya tofauti mwaka 2023, basi hakikisha kwamba unakuwa tayari kufanya vitu vya tofauti. Yaani, vitu ambavyo hujawahi kufanya siku za nyuma.…
-
Faida Tatu KUBWA unazopata pale unapowekeza kwenye hisa
Rafiki yangu, umewahi kuwaza kwamba ukiwekeza kwenye hisa utanufaika na kitu gani? Kuna faida nyingi za kuwekeza kwenye hisa, ila kwenye hii makala ya siku ya leo ningependa kuongelea faida mbili kubwa kwa haraka Faida ya kwanza ya kuwekeza kwenye hisa ni kupata ongezeko la thamani. Ongezeko la thamani ni pale unaponunua hisa kwa bei…
-
Njoo Uongeze Kipato Chako Mara Mbili Zaidi Mwaka 2023
Kuna kitu kimoja nilicho na uhakika nacho juu yako rafiki yangu…Kitu hiki ni kwamba, ungependa kuongeza kipato chako walau mara mbili zaidi ndani ya mwaka 2023! Na hiki ni kitu ambacho ningependa kukusaidia ukifanikishe ndani ya mwaka 2023! Kuanzia tarehe 15 januari 2023, tutakuwa na semina ya kufungua mwaka mpya 2023, lengo kubwa la semina…
-
Mfuko wa FAIDA (FAIDA FUND): Unawekeza au Huwekezi?
Watumishi Housing Investment (WHI) wameanzisha mfuko wa uwekezaji wa pamoja ambao wanauita MFUKO WA FAIDA au kama unaielewa vizuri lugha ya kigeni basi unasema FAIDA FUND. Mfuko wao ni mfuko ulio wazi (open-endend). Kama bado hujasoma kitabu changu cha maajabu ya kuwekeza kwenye hisa, hatifunagni na vipande lazima tu utakuwa unajiuliza mfuko ulio wazi maana…
-
SEMINA YA KUFUNGUA MWAKA: Karibu kwenye Semina ya kufungua mwaka 2023
Kila mwanzo mwa mwaka na katikati mwa mwaka huwa Kuna semina ambayo huwa naiendesha. Mwakani wakati wa kufungua mwaka mpya tunatarajia kuwa na semina ya kufungua mwaka ambayo itafanyika kuanzia tarehe 15. Na itadumu kwa siku 15 mfululizo. Semina hii ya kipekee ambayo itafanyika kwa njia ya mtandao, inalenga kukupa maelezo ya kina yatakayokusaidia kuuanza…
-
Maisha ndiyo hayahaya rafiki yangu
Rafiki yangu wa ukweli, moja ya kitu ambacho watu huwa wanafanya kwenye maisha yao ni kusubiri kila kitu kiwe sawa ili waweze kufanyia kazi malengo na ndoto zao. Ila ninachotaka kukwambia rafiki yangu ni kwamba, hakuna hata siku moja ambayo kila kitu kitakaa sawa kwa ajili ya kukusubiri wewe ufanyie kazi malengo yako. Maisha ni…
-
Bei kisiwe kigezo cha wewe kuuza
Moja ya dhana ambayo watu huwa wanatumia kwenye kuuza ni kuuza kwa bei ya chini. rafiki yangu, nataka kukwambia kitu kimoja muhimu sana, kwamba mara zote usishindane kwa bei. Maana kadiri unavyopunguza bei, mara zote utakuta kwamba kuna mtu anawezakupunguza bei zaidi yako. Hivyo, bei kisiwe ndiyo kigezo pekee cha wewe kuuza.
-
Wafanyakazi na mfumuko wa Bei
Kila tarehe 1 mwezi Mei. Macho na masikio yote ya wafanyakazi huwa yapo kwa kiongozi mkuu wa nchi kuona kama atawaongezea mshahara. Unajua kwa nini huwa wanataka ongezeko la mshahara? Ni kwa sababu kile kipato wanachokuwa nacho mwanzoni kinakuwa hakitoshi kuwafanya wamudu mahitaji ya kila siku. Hivyo, ongezeko la mshahara likiwepo kweli, linaweza kuwa suluhisho,…
-
USIFANYE kosa hili unapotaka kufanya uwekezaji
Rafiki yangu, bila shaka uko vizuri. Leo nataka nikwambie kosa moja unalopaswa kuepuka unalofanya uwekezaji. Na kosa hili ni kuwekeza kwa sababu rafiki zako wanawekeza. Ni muhimu Sana kabla wewe hujawekeza, uhakikishe kwamba unefanya ufuatiliaji wa kina, Kisha uwekeze. Rafiki yangu, USIFANYE kosa la kuwekeza kwa mkumbo.
-
Mfumuko wa bei ni nini?
Kila mwaka serikali kupitia benki kuu ya Tanzania huwa inatoa takwimu za mfumuko wa bei. Unakuta ripoti inasema kwamba mwaka huu mfumuko wa bei ni asilimia 4, 5,au 3.5,7 au vyovyote vile kulingana na ripoti inavyokuwa inasema. Wengi huwa hawajui mfumuko wa bei ni kitu gani na una madhara gani kwao. Leo hii ningependa kukueleza…
-
Aina tano za uwekezaji ambazo kila kila kijana anapaswa kufanya
Habari ya siku hii ya kipekee rafiki yangu. Bila shaka unaendelea vyema kabisa,Siku ya leo ningependa nikwambie Aina Tano za uwekezaji ambao unapaswa kuhakikisha umezifanya. Huu ni uwekezaji ambao ukiufanya sasa hivi ukiwa kijana. Kadiri siku zinavyoenda wewe utavuna matokeo yake tu. Hakikisha unazitumia aina zote hizi za uwekezaji ukiwa bado kijana, maana ujana ni…
-
Kiashiria kuwa uwekezaji uliolfanya Siyo sawa
Juzi Kuna mtu alinipigia simu na kuniambia kuwa Kuna uwekezaji ameufanya. Ila hawezi kuniambia uwekezaji huo kwenye simu mpaka tuonane. Nilipomuuliza kwa Nini, alisema hataki watu wawepo maana uwekezaji wenyewe ni siri. Rafiki yangu, kama uwekezaji uliofanya wewe mwenyewe unaogopa kuusema mbele ya watu basi jua tayari umeshaliwa😂😂. Simaanishi kwamba ufanye uwekezaji halafu uende mbele…
-
Uchambuzi wa Kitabu: Atomic Habits; Tiny Changes, Remarkable Results
Mwandishi: James Clear Mchambuzi: Hillary Mrosso Simu: +255 683 862 481 UTANGULIZI Tabia hujenga maisha tuliyonayo, tabia huamua mafanikio kwenye maisha yetu. Ubora wa maisha yetu ya sasa na ya baadaye yanategemea sana tabia tunazoziishi kila siku. Mara zote tumejikuta kwenye jamii ambayo inaishi na kuamini kwenye tabia fulani ambazo kwa kiasi kikubwa ndio tabia…
-
Ni nani anaruhusiwa kununua hisa na kwa Nini?
Mwaka juzi nilikuwa naongea na ndugu mmoja kuhusiana na hali yake ya kiuchumi. Alikuwa katika hali mbaya kiuchumi. Nilimwuliza kama huwa ana tabia ya kuweka akiba. Akaniambia huwa anaweka akiba Ila huwa anaitumia siku chache mbeleni. Nikamwambia kuwa kwa Hali hiyo utapaswa kufungua akaunti benki ili uwe unaweka fedha zako huko. Lakini kikubwa zaidi nikamwambia…
