-
Sababu yako ni ipi
Kila kitu huwa kinafanyika kwa sababu… Kuna mtu unayeweza kuwa unawona anafanya jambo fulani, ukafikri labda yeye ana kipaji na uwezo mkubwa kukliko wewe, ila baadaye ukija kufuatilia ukagundua kwamba suala kubwa siyo kwamba ana uwezo mkubwa kulliko wewe. Siyo kwamba ana konekisheni nyingi kuliko wewe, siyo kwamba amebarikiwa kuliko wewe, labda tu ni kwamba…
-
Jibu la kuwapa watu wanaokuja kukopa kwako
Rafiki yangu nadhani moja ya shida Kubwa ambazo zinawakumba watu wengi ni kushindwa kuwa na nidhamu ya fedha. Hivyo, kwa sababu hawana nidhamu ya na fedha. Wanatumia fedha zao hovyo na bado wanakuja kwako wakitaka uwakope. Ninachotaka kukwambia leo ni kuwa kama hawana nidhamu na fedha zao, usitegeemee kwamba ukiwakopa watakuwa na nidhamu Na fedha…
-
Dakika moja ya vitendo, ni bora kuliko maelfu ya dakika za maneno
Wakati tunasoma O-Level tulikuwa na jamaa mmoja hivi ambaye angeweza kukutisha kuwa atakupiga. Kwa vitisho vyake tu, ungeweza kudhani jamaa ana manguvu kama HAWAFU? Kwanza unamjua Hawafu kweli? HAHAH. Hii stori ya Hawafu mwenye nguvu tuiache kwa ajili ya siku nyingine. Ila kama umeikumbuka vizuri unaweza kunijuza kikashani kwa kujibu ujumbe huu. Ssasa tuendelee na…
-
KITABU: MAAJABU YA KUSOMA VITABU
Mwezi septemba mwaka 2019 niliandaa kitabu kifupi cha Maajabu Ya Vitabu. Kitabu hiki hapa nilikisambaza bure mtadaoni. Kimetokea kuwa moja ya kitabu cha Kiswahili ambacho kimesomwa na watu wengi sana. Mwanzoni sikutegemea kama kitabu hiki kingesomwa na watu wengi sana. Ila kilichotokea toleo la kwanza la kitabu hiki hapa kilisomwa na maelfu kwa maelfu ya…
-
Kwa nini huwa tunarudia kusoma vitabu
Rafiki yangu umewahi kujiuliza kwa nini huwa tunarudia kusoma vitbu ambavyo tulishavisoma siku za nyuma. Nimeanza mwaka huu kwa kurudia kusoma kitabu cha THINK AND GROW RICH. Na mwaka huu kuna vitabu vingi ambavyo nitakuwa narudia kusoma zaidi ya hiki. Unajua kwa nini huwa tunarudia kusoma vitabu. Huwa tunarudia kusoma vitabu kwa sababu kwenye kusoma…
-
Mambo Muhimu Utakayojifunza Kwenye Kitabu Cha JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO
Kitabu cha jinsi ya kuongeza thamani yako ni moja ya kitabu bora utakachosoma mwaka huu. Na leo nimetamani sana nikufungulie ndani ya hiki kitabu ili uweze kuona ni kitu gani hasa unaenda kupata kutoka kwenye hiki kitabu. Kipakue hapa chini
-
Ushauri Muhimu Kwa Mtu Yeyote Ambaye Ana Lengo La Kuweka Akiba 2023
Hivi ulivyo mwanzo wa mwaka najua kuna watu wengi ambao wameweka lengo la kuweka akiba. Watu wanataka waweke akiba ili waweze kupata uhuru wa kifedha. Sasa siku ya leo ningependa kukwambia kitu kimoja muhimu sana, wewe ambaye umeweka lengo la kuweka akiba KABLA sijakwambia hiki kitu naomba kujua ni wapi utakuwa unaweka fedha zako za…
-
Hii ndiyo aina pekee ya malengo ambayo hayatafanikiwa ndani ya mwaka 2023
Rafiki yangu, najua mwanzoni mwaka huu watu wengi wameweka malengo mengi ambayo watakuwa wakiyafanyia kazi. Ila leo hii nipo hapa kukwambia aina moja tu ya malengo ambayo watu wameweka na nina uhakika haya malengo hayatimia. Malengo haya ni yale malengo ambayo watu wameweka na hawajaanza kuchukua hatua kuyafanyia kazi Sifa moja kubwa ya malengo ni…
-
Viashiria vitano kuwa umeuanza mwaka mpya kwa kishindo
Rafiki yangu, naomba nichukue nafasi hii kuhakikisha kwamba nakutakia kheri ya mwaka mpya 2023. Kheri ya mwaka mpya rafiki yangu. Mwaka huu naamini, utakuwa ni mwaka wako wa kipeke na mwaka wako wa kufanya makubwa. mwaka huu nina hakika ni mwaka ambao hautaremb mwandiko. Na njia bora ya wewe kutoremba mwandiko ni kuhakikisha kwamba unaanza…
-
Nimepata kusoma kitabu cha THE YOUNG INVESTOR (Projects and activities for making your money grow)
Hiki ni kutabu cha uwekezaji ambacho kimeandaliwa maalumu kwa ajili ya watoto, kinalenga kuwafundisha watoto juu ya uwekezaji na namna gani wanaweza kuanza kufanya uwekezaji. Hata hivyo mtu mzima kama wewe unaweza (na unapaswa) kukisoma kitabu hiki pia. Na kwa kuwa lugha iliyotumika kwenye hiki kitabu ni lugha rahisi kwa ajili ya kuwafanya watoto waelewe,…
-
Njia Mpya Ya Kupakua Vitabu Mtandaoni
Kwa wale wanaopata shida kupakua vitabu Mtandaoni. leo nimekuja na suluhisho. hakikisha unaagalia video hii Mpaka mwisho. BONYEZA HAPA KUIANGALIA kila la kheri.
-
Nani anapaswa kusoma vitabu na kwa nini
Kuna MTU kaniuliza swali hili, Nani anapaswa kusoma vitabu na kwa nini Jana kwa upande wangu imekuwa Ni moja ya siku moja bize Sana. niliamka saa nane usiku, nililala saa sita usiku. Na hapa nipo ikiwa Ni saa kumi alfajiri nimeahaamka. Ninachotaka kukwambia siku ya leo siyo kuamka mapema, Bali kusoma vitabu. Ninaamka mapema hivi…
-
Ushauri Huu Haufanyi Kazi Kwenye Uwekezaji
Mara kwa mara utasikia watu wanakwambia Kuwa unapaswa kuanza kwanza, mambo mengine utayajua wakati unaendelea na safari. Hicho kitu kinafanya kazi vizuri sana na nimekuwa nikikitumia kwa siku nyingi . Ila Sasa siku ya leo ningependa nikuongezee ushauri muhimu hasa kwa upande wa uwekezaji. Kwenye uwekezaji Ni muhimu kwako kufanya utafiti wa kina Kabla hujaamua…
-
App Itakayokusaidia Kutuma SMS baadaye, kupiga simu kwa wakati na kudai hela zako😂😂
Katika makala ya leo tunaenda kuona namna ya kuandaa ujumbe leo na ukautuma siku ya krismasi au mwaka mpya. HutahItajika kuuandika tena au kuutuma tenaTutaona namna ya kupanga kumpigia siku za mbeleni na ukampigia kwa uhakika bila kukosa hata dakika 1Tutaona namna ya kupangilia watu wa kuwasiliana nao.Tutaona njia nzuri ya kukukumbusha kufanyia kazi majukumu…
-
STRIVE MASIYIWA
STRIVE MASIYIWA Strive Masiyiwa ni bilionea wa Zimbambwe ambaye alizaliwa mwaka 1961 huko nchini Zimbambwe. Alikulia nchini Zimvambwe na baadaye alienda kusoma masomo ya chuo kikuu nchini Uingereza akisomea uhandisi. Baada ya masomo Strive Masiyiwa kama walivyokuwa watu wengine wazalendo wa kipindi kile alirudi nchini mwake kwa ajili na kuanza kufanya kazi na shirika la…
-
Makosa ambayo watu hufanya wanapotaka KUONGEZA chanzo kingine Cha kipato
Utakuwa umegundua kuwa wiki hii nimekuwa nikikushirikiaha nakala zinazoeleza ni kwa namna gani unaweza KUONGEZA chanzo kipato Cha ziada. Sasa Leo napenda kukwambia kuwa bado sijamaliza nilichokusudia kukwambia. Kwenye hii makala ya leo ningependa ujue makosa ambayo watu hufanya wanapotaka KUONGEZA chanzo kingine Cha kipato. Makosa yenyewe ni Kosa la kwanza wanaanzisha chanzo kwenye eneo…
-
Siri Hii Wanayoijua Matajiri Unapaswa Kuijua Pia
Tujifunze kwa bahari Kila mwaka huwa kuna mito na vijito ambavyo huwa huwa vina maji na baadaye hukauka. Wakati mito hivi na vijito, vikikauka, bahari huwa haikauki hata siku moja. Unajua kwa nini bahari huwa haikauki, moja ya kitu ambacho huwa kinafanya bahari isikauke ni kwa sababu huwa inapokea maji kutoka kwenye vyanzo vingi. Kadiri…
-
Baadhi Ya Vyanzo Vya Kipato Ambavyo Unaweza Kuwa Navyo
1. AjiraHiki ni chanzo maarufu ambacho wengi huwa wanakuwa nacho. Chanzo hiki huwa kinaingiza kipato (ujira) kila baada ya muda fulani (siku,wiki au mwezi). Kwa MTU yeyote ambaye hana sehemu ya kuanzia hakikisha walau unaanzia kwenye ajira. Ukipata ajira hakikisha unaifanya kwa uaminifu na kwa kujituma. Maana ajira inaweza kukupelekea wewe kupata vyanzo vingine zaidi.…
-
Viashiria Vinne Vya Uhuru wa kweli. Kama hauna hivi vitu jua huna Uhuru..
Leo Ni tarehe 9 Disemba, ni siku uhuru hapa nchini Tanzania. Sikupanga kuandika chochote kuhusiana na uhuru, ila ngoja niandike haya machache kuhusiana na uhuru wako binafsi. Watu wengi huwa wanachanganya kuwa kwa kuwa nchi iko huru Basi na wao wako huru. Siyo kweli, Kuna viashiria ambavyo vinaweza kuonesha kuwa wewe uko huru au hauko…
-
Kwa Nini Unahitaji Kuwa Na Vyanzo Vingi Vya Kipato
Unahitaji Kuwa na vyanzo vingi vya kipato Moja ya Kitu Cha muhimu ambacho unahitaji kuhakikisha umekizingatia ni kuwa na vyanzo vingi vya kipato. Labda swali la kwanza la kujiuliza ni je, vyanzo vingi vya kipato maana yake nini? Vyanzo vingi vya kipato, Ni pale unapokuwa unaingiza kipato kwa njia zaidi ya moja. Yaani, siyo tu…