Category: A NOTE FROM SONGAMBELE

  • Zawadi Yako Kama Hutakata Tamaa

    Rafiki yangu, unapofanya  kitu kikaenda ndivyo sivyo, usikate tamaa. Kwa sababu kadiri unavyokosea ndivyo unazidi kuwa imara zaidi. Makosa ni mwalimu mzuri kama utayatumia vizuri.  Ndio maana wahenga wetu wanasema kufanya kosa siyo kosa. Kosa ni kurudia kosa. Ukirudia kosa maana yake hukukifunza chochote na wala hukupata funzo lolote kutokana na kosa la kwanza. Na…

  • Wazo Bora La Biashara

    Najua kila mtu anapenda kupata wazo zuri la biashara. Ukweli ni kwamba WAZO ZURI LA BIASHARA NI LILE AMBALO UNAWEZA KUFANYIA KAZI KWA SIKU 365 BILA KUCHOKA. Usipolifanyia kazi wazo lako, ujue utalinyima uhai. Ebu fikiria mtu ana wazo la kuchonga sanamu fulani, halafu hilo wazo akakaa nalo kichwani mwake. Unadhani wewe utaiona hiyo sanamu?…

  • Hivi Ndivyo Unaweza Kutenda Miujiza Maishani Mwako

    Ninaandika hii makala tukiwa kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa waislam. Kwa kawaida baada ya mfungo wa Ramadhan ndio huwa zinafuata sherehe za Idd. Hakuna mwaka hata mmoja nimewahi kusikia waislam wamesherehekea Idd bila ya kufunga kwanza. Haijawahi kutokea na wala haitakuja kutokea. Kwa kawaida siku ya Idd huwa ni sikukuu kubwa, ambayo…

  • Kwa Nini Unasherehekea Mabadiliko Yaliyo Nje Ya Uwezo Wako Pekee?

    Kuna watu vitu ambavyo huwa wanasherehekea kama mafanikio yao ni vile vitu vilivyo nje ya uwezo wao. Yaani, watu wanasherehekea sherehe kama pasaka, idi, siku za kuzaliwa,… Haya yote ni mabadiliko ambayo yanatokea kila mwaka, ila mabadiliko haya yapo nje ya uwezo wako. Wewe siyo unayesabisha mabadiliko haya, badala yake kalenda iko hivyo. Kwa mfano,…

  • Hii Ndiyo Kazi Rahisi Kuliko Zote Duniani

    Nakumbuka siku moja kwenye redio kulikuwa mjadala mzito. Mada mezani lilikuwa ni swali lililouliza ni kazi ipi ni rahisi hapa duniani. Kila mtu alijitahidi kuchangia mada kiundani kadiri alivyoweza. Nakumbuka vizuri jamaa mmoja alichangia mada kwa kusema kuwa hapa duniani hakuna kazi rahisi. Kila kazi ni ngumu. Aliendelea kusema kuwa ukiwa mwanasheria utaona kuwa Sheria…

  • Ni ushauri tu

    Mafanikio ya mwenzako yawe ni chachu kukusukuma na wewe kufanikiwa zaidi. Ni ushauri tu

  • Malengo Yako Yawe Na Ukomo

    Rafiki yangu, moja ya kosa ambalo watu wanafanya kwenye kuweka malengo ni kuyanyima ukomo wa muda. Wanaaweka kama vile wataishi milele na milele. Unapoweka malengo  yako hakikisha kwamba unayapa ukomo wa muda. Yaani kunakuwa na tarehe ya mwisho ya kuyafikia malengo haya. Na hili linapaswa kujionesha kwenye malengo yako unayoyaweka. Kwa mfano unaweza kuandika hivi,…

  • Sababu 10 kwa nini unapaswa kuanzia chini

    Habari ya leo rafiki yangu mpendwa. Siku ya leo tarehe 11 wakati nafikiria cha kuandika, nimekumbuka nukuu ya John D. Rockefeller. Kama ulikuwa hujui John D. Rockefeller alikuwa ni bilionea wa kwanza nchini marekani kufikia kiwango kikubwa. Kwa Afrika Mansa Munsa ndiye baba lao na utajiri wake haujafikiwa na yeyote mpaka leo duniani kote. Basi…

  • Ni ushauri tu-2

    Ule muda unaoutumia kufuatilia maisha ya watu wengine, utumie kufuatilia maisha yako. Jua nini unataka kufanya na kitu gani hutaki kufanya kwenye maiaha yako.. Jifuatilie uone kama bado unafanyia kazi malengo yako au la umeshaachana nayo. Ni ushauri tu.

  • NGUVU YA WAZO: (THE POWER OF AN IDEA):Jinsi Wazo Linavyoweza Kuiongoza Dunia

    NGUVU YA WAZO: (THE POWER OF AN IDEA) How An Idea Can Rule The World Jinsi Wazo Linavyoweza Kuiongoza Dunia Utangulizi Ebu ngoja kwanza. Ukiingia kwenye mtandao wa google na kuandika neno idea utapata majibu 4,270,000,000 Ujue sijakosea ni bilioni nne na milioni mia mbili sabini. Haya tuachane hilo, ukitafuta neno business idea utapata matokeo…

  • Una Uwezo Mkubwa Ndani Yako

    Kwenye Biblia kuna hadithi ya watu watatu waliopewa talanta. Mmoja alipewa tano, wa pili alipewa mbili na mwingine alipewa talanta moja. Aliyepewa talanta moja hakuithamini, na wala hakuitumia kufanya kitu chochote cha maana. Binafsi sipo hapa kukwambia hiyo stori, naamimi kuwa utakuwa unaijua vizuri tu, au la utaenda kuisoma baada ya hapa. Kitu kikubwa ninachotaka…

  • Njia Bora Ya Kukusaidia Kuishi Maisha Yako Kikamilifu

    Unaendeleaje upande wa huko.  Mimi naendelea vyema kabisa.Leo ni jumapili ya tarehe 10.  Siku 100 za kwanza za mwaka huu zimeisha. Na Sasa zimebaki siku 265. Najua tangu mwaka huu umeanza lazima Kuna kitu uliazimia kuwa utakifanyia kazi. Sasa swali langu kwako, ni je, bado hiki kitu unakifanyia kazi, au ndio tayari umekata tamaa? Ninachotaka…

  • Hiki Ni kitu muhimu ambacho unapaswa kukitafuta kwenye kila kitabu

    Rafiki yangu usomaji wa vitabu ni kitu muhimu sana kwa ajili ya afya ya akili yako. Ukitaka kufurahia usomaji wa vitabu basi kwenye kila kitabu ambacho unasoma hakikisha unapata unapata vitu vitatu ambavyo unaweza kufanyia kazi Mara moja. Ukipata vitu hivi mwanzoni mwa kitabu, unaweza kuweka kitabu pembeni kwanza na kufanyia kazi kile ulichojifunza utakuja…

  • Jinsi ya kuendeleza kipaji chako

    Habari ya leo rafiki yangu. Hongera sana kwa siku ya leo na siku ya kipekee sana. Leo nataka nikueleze namna ambavyo unaweza kuendeleza kipaji chako kwa viwango vikubwa mpaka kufikia hatua za kukifanya kikutoe.  Lakini kwanza tujiulize kipaji ni nini?Kujibu swali la kipaji ni nini naomba usome makala hii hapa ambayo imeeleza kwa kina kuhusu…

  • Karibu Sana

    Hello! Tumekutumia kitabu kwenye barua pepe yako. Sasa hivi kitakuwa kimeshafika lakini kama hutajali, hapa nimekuwekea baadhi ya makala ambazo zimesomwa Sana Kwa Nini Wanafunzi Wanaopata “A” Wanawafanyia Kazi Wanafunzi Wanaopata ‘C’, Na kwa Nini Wanafunzi Wanaopata “B” Wanaifanyia Kazi Serikali Jinsi ya kuendeleza kipaji chako KAMA UNAFIKIRI KILA KITU KILISHAANDIKWA, FIKIRI TENA (SABABU 18…

  • THINK BIG FOR AFRIKA

    Karibu kwenye kundi maalumu la whatsap la Think Big For Afrika! maelezo zaidi ya kina yanakuja hapa hapa baadaye. Au wasiliana na 0755848391 ili akupe maelekezo sasa.

  • WATU WANASEMAJE KUHUSU KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI?

    MIMI NAMFAHAMU GODIUS Ninamfahamu Godius si tu kwa kupitia maandishi yake bali kwa kupitia maisha yake. Jinsi anavyoishi ni darasa tosha la mtu yeyote mwenye nia ya kufanikiwa. Nilipoanza kusoma kitabu hiki sikukoma kuacha kwani kimegusa maisha yangu na baadhi ya mambo niliyoyapata humo nimeanza kuyafanyia kazi na nimeanza kuona maajabu makubwa. Unataka kuwa mbunifu?…

  • Jinsi Ya Kutengeneza Bahati Yako

    Dunia ina tabia ya kukupatia kitu kama utaonesha nia, kuwa wewe ungependa kupata hicho kitu. Huwa ninapenda kuwaambia watu kuwa, hata kama ni bahati itakukuta njiani unatembea wala sio chumbani kwako ukiwa umelala. Kwa hiyo, wewe kama unahitaji kupata bahati maishani mwako basi kuwa tayari kuweka kazi inayoendana na bahati unayotaka. Bahati unaitengeneza wewe mwenyewe…

  • Vitu Vitano Kuhusu Fursa

    Leo nataka nikueleze vitu vitano muhimu unavyopaswa kufahamu kuhusu fursa. Watu wengi wamekuwa wanahadaiwa linapokuja suala zima la fursa. Kuna watu wamekuwa wanatumia mlango wa kuita haadhi ya vitu fursa ili wakupate. Kuna watu unakuta wanataka fedha zako, wanaangalia namna nzuri ya kuzipata, wanaona wanaweza kukupata kwa kukwambia kuwa kuna fursa ambayo unaweza kuifanyia kazi.…

  • Jinsi ya Kuipangilia Ratiba Yako Vizuri Kuanzia Leo

    Njia bora ya Kuipangilia Ratiba Yako Vizuri ni kujiuliza ni 1. vitu gani vya muhimu ambavyo napaswa kufanya. 2. Vitu gani vya kufanya japo siyo muhimu sana. 3. vitu gani ambavyo wanaweza kufanya wengine. 4. Na ni vitu gani ambavyo wengine wananitaka nifanye. Mara zote weka nguvu zako kwenye namba 1 na namba 2. Kwa…

X