-
2024 badili mifumo yako ya kufikiri
Rafiki yangu, matokeo ambayo umepata ndani ya mwaka 2023, yanaweza yasibadilike kama hutabadilika. Unachohitaji kufanya mwaka 2024 ni kubadilika wewe. Kama hutabadilika au kubadili namna unavyofikiri, ukweli ni kuwa matokeo utapata matokeo yaleyale ambayo ambayo umepata 2023 au hata chini ya hapo.
Napenda sana nukuu ya Robert Pirsing kama ilivyonukuwa kwenye kitabu cha Thinking In Systems, anasema;
If a factory is torn down but the rationality which produced it is
left standing, then that rationality will simply produce another
factory. If a revolution destroys a government, but the systematic
patterns of thought that produced that government are left intact,
then those patterns will repeat themselves. . . . There’s so much talk
about the system. And so little understanding.
—Robert Pirsig, Zen and the Art of Motorcycle Maintenance
Akimaanisha
I’ll provide a translation of the given text into Kiswahili:
“Endapo kiwanda kitabomolewa lakini mantiki iliyosababisha kujengwa kwake ikabaki, basi mantiki hiyo itaunda tu kiwanda kingine. Endapo mapinduzi yanaharibu serikali, lakini muundo wa mawazo uliosababisha kuundwa kwa serikali hiyo unabaki salama, basi muundo huo utajirudia. … Kuna mazungumzo mengi kuhusu mfumo. Na uelewa ni mdogo sana.”
—Robert Pirsig, Zen and the Art of Motorcycle Maintenance
Hii maana yake nini, maana yake kitu kilicholeta matokeo ya kwanza, kama kitu hicho hakitaharibiwa au kubadilishwa, matokeo yataendelea kupatatikana.
Mfano wengi tumekuwa tunaongelea kuhusu serikali na namna ilivyo na mfumo mbovu. Na hivyo fikra za wengi zimekuwa kwamba ikibadilishwa serikali basi matokeo ya tofauti yanaweza kupatikana. Lakini mabadiliko ya serikali yamekuwa hayaji na matokeo ya tofauti. Na kitu ambacho kimekuwa kinasababisha hilo ni ile fikra iliyojenga serikali, au misimamo iliyojenga serikali, au misingi iliyojena serikali bado haijaharibiwa. Misingi bado ni ile ile, hivyo anapobadilishwa mtu mmoja juu, wengine wote wanaendelea kukaa vilevile hata wakibadilishwa. Kumbe, njia ya kupata matokeo ya tofauti ni kubadili ile misingi na kuweka mfumo mpya ambao utaleta matokeo.
Sasa achana na serikali. Hapa nakuongelea wewe, 2024 kama hutabadili mifumo ambayo umekuwa unaitumia utaendelea kupata matokeo yaleyale na hata chini ya hapo.
Sasa unajiuliza ni mfumo upi unapaswa kuwa nao.
KWANZA, anza kwa kuweka ratiba yako. Kuwa na ratiba yako ya kila siku, ambayo unaifuata.
Pili kwenye siku yako, fanya majukumu ya muhimu tu kwanza. Majukumu ambayo siyo ya muhimu kamwe usiyafanye. Fanya majukumu ambayo ni muhimu pekee.
Tatu,fanya majukumu machache, majuku mengine ambayo si ya muhimu zaidi wape wengine.
Soma zaidi: Lengo Lako Kuu La Mwaka 2024 Ni Lipi? Au Ndio Unamwachia Mungu🤔?
Karibu sana kwenye semina ya kufungua mwaka 2023. Kwenye hii semina nitaeleza hii mada kwa undani na kwa urefu kiasi kwamba utaweza kuilewa na kuitumia vyema sana.
Ni semina ya siku 30.
Itaanza tarehe 20 hadi tarehe 20 Februari, moja ya mada ambayo itafundishwa kwa kina ni hii.
Gharama za hii semina ni elfu thelathini.
Kujiunga na semina hii ni rahisi sana.
Lipia 30,000/- kwa namba 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA. Ukishalipia, basi utaniambia nili nikuunge kwenye kundi maalumu la semina.
NB: Ofa ya Krismasi bado inaendelea. Mwisho ni siku ya tarehe 1.1.2024 saa sita usiku
*Bado siku mbili TU ya wewe kupata ofa hizi mbili*
*Ofa ya kwanza*
*Unapata vitabu 6 (softcopy kwa 20,000/- au vitatu kwa 10,000/-* 🤭Chagua hapa, nipe taarifa👇🏿
1: JINSI YA KUTENGENEZA MSHAHARA NJE YA MSHAHARA
2: NGUVU YA WAZO
3: NGUVU YA KUWEKA MALENGO
4: MWONGOZO WA WAPAMBANAJI
5: MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BIASHARA
6: VYANZO VINGI VYA KIPATOLipia 10,000 upate vitabu VITATU, LIPIA 20000 Upate vyote SITA. ( Softcopy)
Namba ya MALIPO ni. 0684408755 GODIUS RWEYONGEZA
*Ofa ya pili*
Unapata audiobook 6 kwa 15,000/- TU. Audiobooks zenyewe ni.
1. NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA
2. JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO
3. MAISHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE
4. JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO
5. MAAJABU YA KUWEKA AKIBA
6. KIPAJI NI DHAHABU
Gharama ya hizi audiobooks ni zaidi ya ~100,000/~ ila kwa Sasa lipia 15,000/- TU upate zote sita.Namba ya malipo ni 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA
*Hii ndiyo Ile ofa ushindwe mwenyewe*
Wewe ofa Yako msimu huu ni ipi? -
Ushauri Muhimu Ambao Kila Kijana Anapaswa Kufanyia Kazi
Huu ni ushauri ambao kila kijana anapaswa kuupata.Toka nyumbani anza kupambana na hali yako.
-
Usisubiri Mtu Yeyote Kuanza Kufanyia Kazi Ndoto Zako
- USISUBIRI YA MTU YEYOTE KUANZA KUFANYIA KAZI NDOTO NA MALENGO YAKO. Ndiyo unapawa kuwa na ndoto kubwa bila ya kusubiri mtu yeyote, ila ukweli ni kuwa ndoto kubwa na malengo makubwa bila ya kufanyia kazi, hayatakaa yatimie. Ndiyo maana unapaswa kuanza kufanyia kazi malengo na ndoto zako bila ya kusubiri ruhusa.
Kwenye andiko langu la Jana ee mtu mkubwa….niliandika kuhusu kuwa na ndoto kubwa. Ndiyo unapawa kuwa na ndoto kubwa bila ya kusubiri ruhusa ya mtu yeyote, ila ukwlei ni kuwa ndoto kubwa na malengo makubwa bila ya kufanyia kazi, hayatakaa yatimie. Ndiyo maana unapaswa kuanza kufanyia kazi malengo na ndoto zako bila ya kusubiri ruhusa.Kuifanyia Kazi ndoto Yako ndiyo habari mjini.
Huu ni upande wa pili wa shillingi. Upande wa kwanza ni KUWA NA NDOTO Kubwa upande wa pili unaosema baada ya kuwa na ndoto kubwa Sasa unapaswa kuzifanyia kazi.
Ebu pata picha kama Dunia yote ikibadilika Leo hii unaposoma hapa na Kila mmoja akaanza kuwa bize na ndoto zake.
Aliyekuwa anapiga umbea ukakuta ndiye Yuko bize na ndoto zake kubwa. Hataki utani, hataki umbea ila kipaumbele kwake ni kazi TU. Na kazi hiyo ni ndoto zake.
Baada ya kuwa umeonana na huyo mtu pata picha ukatoka hapo ukaenda kukutana na mwingine ambaye siku za nyuma alikuwa anakaa kaa tu bila kufanya kitu chochote, lakini leo hii ukakuta jamaa huyu anapambana na kazi za ndoto zake….
Mara Kila mmoja akawa amebadilika.
Na hata lugha ikabadilika. Ukakuta watu hawaongei Tena lugha za kukatishana tamaa. Ukakuta watu wanaongea maneno ya kutiana moyo. Kila mmoja anapenda mafanikio ya mwingine.
Dunia hii utakuwa nzuri sana, si ndiyo ee? Bila shaka…
Nakuhakikishia kuanzia siku hiyo, hapa duniania hakutakuwa na vita. Hakutakuwa na marumbano..
Watu hawatajiua wala kuwaua wengine…Naamini wasiwasi kuwa Moja ya kitu kinachofanya watu wajiue ni kwa sababu hawana ndoto, au kama wanazo basi hawazifanyii kazi, au kama wanazifanyia kazi basi wameanza TU kidogo na wamekatishwa tamaa.
Lakini hicho nilichokiandika hapo ni kama stori ya Habunwasi. Haliwezi skutokea…
Haliwezi kutoka kwa sababu watu wote duniania hawawezi kubadilika ndani ya siku Moja. Wanaohitaji kubadilika kwanza ni mimi na Wewe. Na baadaye watafuata watu wa karibu waliotuzunguka mimi na wewe.
Ebu baada ya hapa Anza kujiambia MIMI ndiye ninapaswa kubadilika.
Mimi mdiye ninapaswa kuwa na ndoto kubwa. Kuna stori kwenye Biblia kuwa Yesu (Nabii Issa) aliulizwa kuwa marafiki zako ni akina nani? Alisema marafiki zangu ni wale wanaolifuata neno la Mungu na kuliishi…
Sasa na Mimi ukiniuliza kutoka moyoni kuwa marafiki zangu ni akina nani?
Nitakujibu kwa kukwambia kuwa
Marafiki zangu ni wenye ndoto kubwa na ambao wanaziishi hizo ndoto zao. (kama mpaka Sasa hivi hauna ndoto kubwa, fanya kitu uwe Nayo, ili uendelee kuwa miongoni mwa marafiki zangu.
Na njia zuri ya kuigundua ndoto Yako kubwa na kuanza kukifanyia kazi ni kuanza kusoma kitabu changu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. MARAFIKI zangu wa kweli pia ni wale ambao wamesoma vitabu vyangu na wanajua vinaongelea Nini.
Sikiliza, huwezi kukaa unasubiri upewe ruhusa ya kufanyia kazi ndoto yako ukaipata. Kila utakayemshirikisha ndoto yako kubwa atakuwa nay a kwake ya kusema, yupo atakayekwambia kwamba haijawahi kufanyika, mwingine atakwambia kuwa jambo kama hili haliwezekani, mwingine atakwambia kwamba halijawahi kufanyika, mwingine atakwambia kwamba, kama ingekuwa rahisi kila mmoja angekuwa anafanya na mengine…
Ruhusa ya kufanyia kazi ndoto yako kubwa unapaswa kujipa wewe mwenyewe na siyo mwenza wako, serikali, mjomba au mtu yeyote unayemfikiria wewe…
Nadhan na mimi naweza kukupa ruhusa pia, ebu fumba macho kisha jiambie kwamba, kuanzia leo liwe jua au mvua, kiangazi au masika, nitafanyia kazi ndoto zangu…
Kisha toka hapa nenda kafanyie kazi ndoto zako
kwa leo inatosha.
Kuna ofa ya krimasi. Unapata vitabu sita kwa elfu ishirini tu (softcopy)
kama bado hujapata hii ofa changamka. Wasiliana nami kwa 0684408755
Vitabu vilivyo kwenye ofa ni
1: VYANZO VINGI VYA KIPATO
2: JINSI YA KUTENGENEZA MSHAHARA NJE YA MSHAHARA
3: MWONGOZO WA WAPAMBANAJI
4: NGUVU YA KUWEKA MALENGO
5: NGUVU YA WAZO
6: MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BIASHARA
Ukitaka vitatu kati ya hivyo, utavipata kwa 10,000/- tu.
Kumbuka hii ni ofa ya muda mfupi tu. Ni au unalipia sasa hivi ili kupata hii -
Sababu Kumi Kwa Nini Haupaswi Kuongea Sana
Unapokuwa unaongea au unawasilisha jambo lako kwa watu, usiwe mtu wa KUONGEA sana mpaka ukapitiliza.
.jua lini unapaswa KUONGEA
Lini unapaswa kusikiliza au kujenga hoja
Lini unapaswa kuuliza MASWALI n.kWewe kwenye mazungumzo Yako, usiongee sana. Sikiliza sana. Na hata pale unapoongea, ukigundua point unayoongea tayari watu wameshaielewa, usilazimishe kuendelea KUONGEA.
Inatosha. Kama watu wameshaielewa pointi Yako, basi inatosha usiongee sana.
Kamwe usiwe mtu wa KUONGEA sana kwenye mazungumzo Yako yoyote. Hizi hapa ni sababu Kumi Kwa Nini haupaswi kuwa mtu wa KUONGEA sana
1. Kusikiliza ni muhimu: Kusikiliza kunaweza kutoa ufahamu mzuri wa mazingira na watu wanaokuzunguka.
2. Kuepuka kutoa habari zisizo muhimu: Kuongea sana kunaweza kufichua mambo yasiyo ya lazima au yasiyo muhimu.
3. Kuzuia kutokueleweka: Kuongea sana kunaweza kuchangia kutoeleweka vyema na kuchanganya mawazo yako.
4. Kuheshimu muda wa wengine: Watu wengine wanaweza kuwa na majukumu mengine, hivyo ni vyema kuheshimu muda wao.
5. **Kuepuka kuchoka wengine:** Kuongea sana kunaweza kuwachosha wengine na kusababisha kukosa hamu ya kusikiliza.
6. Kujilinda kijamii: Mara nyingine, kutoa maelezo mengi kunaweza kusababisha kutoeleweka vizuri au hata kujionyesha sana.
7. Kudumisha siri: Kuzungumza sana kunaweza kusababisha kutoa siri zisizo muhimu au za kibinafsi.
8. Kujenga heshima: Kuongea kidogo mara nyingine kunaweza kuimarisha heshima yako mbele ya wengine.
9. Kujifunza kutoka kwa wengine: Kusikiliza wengine kunaweza kutoa fursa ya kujifunza na kuboresha uelewa wako.
10. Kusitisha ubishani usio na maana: Kuongea sana kunaweza kusababisha ubishani usio na tija au kuleta mfarakano.
kAMA UMEIPENDA MAKALA HII, BASI UTAPENDA MAFUNZO MENGINE AMBAYO INATOA.
Jiunge hapa
-
Ya Ngoswe Mwachie Ngoswe
Moja ya ushauri maarufu sana ambao umekuwa unatolewa kwa watu ni ushauri wa kuwa mind your own business. Kwa lugha yetu sisi vijana wa siku hizi ni saawa na kusema kwamba pambana na hali yako.
Yaani, kwamba achana na mabo mengine ya watu wengine halafu
Nguvu zako
Muda wako
Akili yako
Fedha zako na
RASILIMALI ZAKO zote ziweke kwenye mambo yanayokuhusu wewe.
Mambo ya wengine waachie na wao wapambana na mambo yao.
Ya Ngoswe mwachie ngoswe
Ya Kaisari mwachie Kaisari…
Ni mara ngapi wewe umekuwa unavunja ushauri huu? Badala ya kupambana na hali yako unapambana na hali za watu wengine.
Unaanza kufuatilia maisha ya watu wengine,
Wanaishije
Wanatoka na nani
Hali ya mahusiano yao ikoje
AU MUDA MWINGINE UNAjiingiza kwenye mijadala isiyokuwa na ulazima wowote…
Unaanza kujadili kati ya mtu A na B nani ana hela.
Au kati ya fulani na fulani nani ana kipaji zaidi..
Nani ana wafuasi zaidi kwenye mitandao ya kijamii.
Wew haya hata uyafuatilie kiasi gani, hayakusaidii.
Leo nataka nikurahisie tu.
Kama kitu hakikuiuingizii pesa leo, au kama hakitakuja kukuingizia pesa siku zijazo. Usikifuatilie.
Kama kitu siyo lengo lako kuu, usikipe muda wako
Kama kitu siyo biashara au kazi yako, usikifanye kuwa biashara yako.
Mimi kwa leo naishia hapo
Kama bado hujapata ofay a vitabu sita kwa elfu 20 tu. Jua unajikwamisha. Hii ni ofa ya muda mfupi ambayo tumejadiliana na wasaidizi wangu kuwa itapaswa kuisha muda si mrefu. Kama bado hujapata hii ofa, sikiliza.
Wasiliana na 0684408755 (whatsap/sms/simu). Kisha mwambie akupe ofa ya vitabu sita.
Fanya hivyo haraka iwekezakavyo kabla ofa haijafungwa.
Niliyekuandikia makala ya leo naitwa Godius Rweyongeza
Nipo Morogoro nchini Tanzania
-
Vitu Vikubwa Vitano nilivyojifunza kuhusu MAISHA na biashara
Rafiki yangu siku ya Leo Nina ujumbe mmoja TU kwako. Kama una kitu ambacho Wewe mwenyewe unafanya, na unajua kitu hicho kitaleta mabadiliko, mapinduzi au kitasaidia watu basi.
- Kifanye kwa moyo wako wote
- Jitume na kifanye kwa bidii sana kiasi kwamba hakuna mwingine anayeweza kukifanya kama Wewe
- Kifanye Kila siku bila kuacha na kwa muda mrefu bila kuacha.
- Usikifanye mara Moja TU, kisha ukasema sioni matokeo. Kifanye mara kwa mara na kwa muda mrefu bila kuacha.
- Jitahidi Kila mara kuhakikisha unawafilia watu wapya ambao mwanzoni ulikuwa hujawafikia.
Nakuhakikishia ukifanya haya mambo matano, kwa uhakika, kwa msimamo na bila kuacha. Sharti utaona TU matokeo.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza
Kujifunza zaidi kutoka kwake jipatie nakala za vitabu vyake. Unaweza kupata nakala hizi kwa kuwasiliana naye kwa 0684408755.karibu sana
-
Kosa Kubwa Ambalo Watu Wengi Hufanya
Kwenye maisha kuna makosa ambayo watu huwa wanafanya. Ila hupaswi kufanya makosa ya nanma hii mengi, maana kadiri unavyofanya makosa haya mengi, maana yake unakuwa unajiuzuia ile nafasi yaw ewe kusonga mbele na kuweza kfuanya makubwa zaidi. Sasa unajua ni kosa gani kubwa ambalo watu hufanya?
Kutojifunza baada ya kumaliza chuo.
Ile baada ya mtu kuhitimu na kurusha kofia juu, ndiyo anakuwa amerusha kila kitu. Yaani, hataki tena masuala ya kusikia sijui kuna vitabu au kitu gani. Ukweli ni kuwa kama unataka kufika mbali kwenye maisha kusoma kunapaswa kuwa sehemu ya maisha yako.
Nani amekwambia kwamba, ukijifunza kitu kimoja tu mara moja tu ndiyo unakuwa umebobea. Unapaswa kuendelea kujifunza kila siku bila ya kuacha. Kila siku, ya maisha yako iwe ni siku ya kujifunza.
Kiukweli ili ufanikiwe kwenye maisha unahitaji zaidi ya elimu ya darasani. Unahitaji kujifunza vitu vingi. Unahitaji kujifunza biashara, unahitaji kujifunza mauzo, unahitaji kujifunza kuongea mbele ya watu, unahitaji kujifunza uandishi na mengine mengi.
Soma na jifunze mara kwa mara. Iwe ni kupitia vitabuni, iwe ni kupitia kozi ambazo unaweza kusoma mtandaoni, kozi za kwenda sehemu na njia nyinginezo.
Ningependa nimalizie makala ya leo kwa nukuu inayosema kuwa, mtu ambaye hasomi, ni mzee hata kama bado ana miaka 20 na mtu ambaye anasoma na kujifunza ni kijana hata kama ana miaka 80.
Uwe na siku njema.
-
Kitu muhimu unachopaswa kukifanya unapokuwa unakutana na mtu
Niwe mkweli, hiki kitu mwenyewe kimekuwa kinanipa shida sana. Watu wengi wanaomba kuonana namimi halafu muda mwingine wanakuwa hawajajipanga. Na muda mwingine wanaomba tu kuonana na mimi ilimradi…. Lakini pia mimi siwaambii muda ambao nitaweza kuwa nao.
Nimejifanyia tafakari kwa watu wengi ambao wameomba kuonana na mimi ndani ya mwaka 2023, nimegundua kitu hiki kimejirudia sana. Hivyo, nimeamua mwaka 2024, ninaenda kufuata utaratibu wangu kama ifuatavyo.
Kabla ya kuonana utaniambia tunataka tuongee nini.
Kama kuna gharama ambazo utakuwa unapaswa kulipia utalipia mapema.
Halafu tutapanga muda wa kuonana na kikao hicho kitadumu kwa muda gani.
Ukichelewa, imekula kwako. Muda wako umeenda.
Usipofika kwa wakati na hakukuwa na taarifa mapema, basi muda wangu wa kuondoka ukifika nitaodnoka. Hili litanisaiaidia kuonana na watu wachache, ila ambao wako siriazi na ambao tutafanya mambo ya maana.
Nimejieleza mwenyewe leo hii, lakini pia na wewe angalia kwenye ratiba zako. Hivi kwa mfano, mwaka huu umekutana na watu wangapi? Je, ni muda kiasi gani umepoteza kwa vikao ambavyo havikuwa na tija?
Hilo liondoe kwenye ratiba zako. Mwaka 2024, usirudie kosa hilohilo, la sivyo litakukwamisha kusonga mbele.
Kama umenielewa gonga cheers, kisha mshirikishe rafiki yako makala hii aweze kusoma.
Kila la kheri.
-
Je, kuna ulazima wowote ule wa kuandika majukumu yangu chini naweza kuyakumbuka?
Kwenye makala ya jana nilikwambia kwamba unapaswa kuandika majukumu yako yak la siku. Unapaswa kuhakikisha kwamba umeyaandika chini. Lakini., Inawezekana wewe ukawa na kumbukumbu nzuri, hivyo ukajiambia kwamba sipaswi kuwa naandika vitu vyangu chini.
Siku ya leo nipo hapa kukwambia kuwa hata kama una kumbukumbu nzuri. Hata kama unayesoma hapa ni profesa. Bado unapaswa kuandika chini majukumu yako utakayoyafanya ndani ya siku husika. Huandiki chini m ajukumu yako ya siku husika kwa sababu utasahau, bali unaandika chini ili uweze kuipa akili na kichwa chako nafasi ya kufikiria mambo mengine ya maana zaidi.
Hivyo, ile nguvu ambayo ungeitumia kwenye kukumbuka ratiba yako ya siku, unaitumia kwenye kwenye mambo mengine yatakayokupa matokeo makubwa zaidi.
Sijui umenielewa hapo? Ee, usije kusema ooh, unajua mimi nina kumbukumbu kubwa bwana sihitaji ratiba. Hapana, andika chini, ratiba yako.
-
Kitu kimoja unachopaswa kuanza kufanyia kazi mara moja

Rafiki yangu mpendwa salaam, bila shaka unaendelea vizuri.
Hivi umewahi kujiuliza ni kwa nini unakuwa unapoteza muda kwenye siku yako? Unajua kwa nini hili linatokea? Moja ya kitu kinachokufanya upoteze sana muda wako ni kwa sababu, hujapangilia vizuri siku yako. Yaani, chochotfe kile kinachokuja mbele yako wewe unafanya. Ukweli ni kuwa unapoianza siku yako, unapaswa kuutumia muda wako kwenye kuipangilia siku yako.
Ndiyo, andika saa kwa saa kitu ambacho unaenda kufanyia kazi ndani ya siku husika.
Kisha fuata hiyo ratiba yako.
Hiki kitakusaidia kuepukana na muda mwingi ambao ungeupoteza ndani ya siku yako. Lakini pia kitakusaidia kuiendea siku yako katika namna ambayo itakuzalishia matokeo.
Kwenye ratiba yako weka vitu ambavyo utafanya na vitakuletea matokeo. Kama kitu hakitaleta matokeo sasa au siku zijazo, kiondoe. Kipaumbele chako kiwe ni yale majukumu yako ya muhimu tu.
Sijui umenielewa.
Ebu anza leo. Ni kwa namna gani unaenda kupangilia ratiba yako siku ya leo? Ni vitu gani ambavyo unaenda kuondoa kwenye maisha yako ambavyo umekuwa unafanya ila havina manufaa?
Nitumie ujumbe whatsap kwa 0755848391
Emai: godiusrweyongeza1@gmail.com
Kila la kheri
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Kujifunza kuhusu uandishi wa makala. BONYEZA HAPA