-
Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa
Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA
Simu: +255 (0) 684408755
Whatsap: +255 (0) 755848391
Email: songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)
-
Nitakuwa Kwenye Kipindi Cha Temino Ya Clouds FM Leo

👆🏿👆🏿Wakati unajipanga kwa ajili ya hiki kipindi Maalumu cha kufungua mwaka 2024. Hakikisha pia unajiandikisha kwa ajili ya semina ya kufungua mwaka 2024.
Taarifa kamili ya semina ya kufungua mwaka 2024 hii hapa👇🏿
www.songambele.co.tz/semina
Ni semina ya mwezi mzima.
Venue: WhatsappAda ya semina ni 30,000/-
Malipo yanafanyika kwa namba ya simu: 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA
Ukishalipia mapema TU tunawasiliana ili uweze kuungwa kwenye kundi la whatsap la semina .
Kwa Sasa unaweza kujiunga kwenye kundi la mapokezi hapa👇🏿
https://chat.whatsapp.com/CAdCnW82i8N0clD2fDvn7vMwaka 2024 ndiyo huu hapa, lengo lako kuu ni lipi? Au unamwachia Mungu?
Enewei tukutane kwenye TEMINO YA CLOUDS FM baadaye Leo kuanzia saa Tisa jioni mpaka saa Kumi na moja
Cheers!
Godius Rweyongeza
www.songambele.co.tz
Morogoro-Tz -
Code Ya Kukusaidia Kufanya Makubwa 2024 Hii Hapa
Unataka kufanya makubwa 2024. Code ya kufanya makubwa ndani ya 2024 imeelezwa kwenye hii video.
-
Kama una mpango wa kufunga Ndoa 2024, hakikisha unasoma hapa
Kama unamjuaa anayefunga ndoa mwaka huu mtumie ujumbe huu
Una mpango wa kufunga ndoa 2024 rafiki yangu.
Kwenye jamii zetu kumekuwa na utaratibu ambao unajirudia kila mwaka. Kila mwaka kuna maelfu ya watu wanaofunga ndoa na utaratibu ambao huwa unafanyika huwa ni uleule kila mwaka..
Mtu akitaka kufunga ndoa, anaandaa harusi kubwa, anaalika watu mbalimbali wamchangie, ili kuonesha ubabe anaweka vitu vya gharama kubwa.
Hela inapokuwa haitoshi anakopa na sherehe inafanyika.
Wengine wanafanya harusi wakiwa na matarajio kuwa ile fedha watakayopata siku ya harusi ndiyo iwasaidie kulipa mkopo au kuanzia maisha baada ya harusi.
sasa sipo hapa kusema kwamba usifanye harusi. Hilo utafanya au hutafanya kulingana na wewe mwenyewe au kulingana na ukubwa wa mfuko wako. lakini chonde chonde, usifanye harusi kwa kukopa hela. Usianze maisha ya mahusiano ukiwa na deni. Hii siyo sehemu nzuri ya kuanzia kimaisha.
Usikope fedha kwa ajili ya kufunga ndoa ukitegemea kuwa zawadi utakazopata zitaweza kurejesha ule mkopo. Mara nyingi huwa haiwi hivyo. Kumbuka sijasema mara zote, ila mara nyingi.
Najua kabla ya kufunga ndoa huwa kuna mafunzo ambayo huwa yanatolewa. Lakini kuna mafunzo ambayo huwa yanasahaulika. na mafunzo haya ni ya uwekezaji.
Kabla hujafunga ndoa mwaka huu hakikisha kwamba unajifunza uwekezaji. Siyo wewe tu, hata huyo mwenza wako, hakikisha anajifunza uwekezaji. Na hasa uwekezaji kwenye hisa, hatifungani na vipande. Nakwambia, utanishukuru kwa hili maisha yako yote.
Hii ni elimu ambayo haitolewi unapokuwa unataka kufunga ndoa ila ni elimu muhimu ambayo ukiipata itakuwa yenye manufaa kwako, kwa familia yako na kwa kizazi chako, hata miaka buku ijayo. hivyo basi, nikushauri kitu kimoja, jifunze uwekezaji kwenye hisa, hatifungani na vipande wewe na mwenzako kabla ya kuingia kweye ndoa mwaka huu.
Na sehemu nzuri ya kuanzia ni kusoma kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA kwenye hisa, hatifungani na vipande. Kitabu hiki unaweza kukipata kwa kuwasiliana na 0684408755 sasa.
Soma zaidi: Jiwe la uzito wa tani moja kwa wale ambao hawataki kuweka akiba
-
Tengeneza Pesa Kwa kuuza Unachojua (Maarifa + Taarifa)
Unaendeleaje, leo kwenye video fupi ambayo tumekuandalia, tumeandaa namna ambavyo unaweza kuanza kutengeneza fedha kwa kutumia kile ambacho tayari unajua sasa hivi.
Wewe ni kitu gani ambacho unajua? Je, umekuwa unaagiza mizigo nje ya nchi kwa muda? Huicho ni kitu unajua, kinaweza kuwasaidia wengine.
Umekuwa ukilima mahindi? Hicho ni kitu kingine muhimu sana ambacho unajua.Kwa chochote kile unachojua, kuna namna ambavyo unaweza kuanza kutengeneza hela kwa kutumia hicho kitu.
Nimeandaa video fupi ambayo unaweza kuitazama hapa
Kitabu kinachoeleza hii mada kwa undani zaidi kitakuwa tayari mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi. Unaweza kuweka oda 0755848391
Na usisahau kuhusu semina itakayofanyika tarehe 20.1.2024.
Soma zaidi kuhusu semina hapa
Uwe na siku njema sanaGodius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz -
Una Mpango wa Kuja Morogoro 2024
Rafiki yangu wa ukweli, una mpango wa kufika Morogoro, au kupita Morogoro mwaka huu?
Tupo Morogoro, Sabasaba ikitokea unapita Morogoro au unafika Morogoro mjini kutembea, basi usisite kufika ofisini kwetu.
Unaweza hata kujipatia nakala moja ya kitabu. Hahaha. Kama unapita MSAMVU, bado tunaweza kukuletea mpaka Msamvu bila wasiwasi wowote.
Mawasiliano ya ofisi yanafanyika kupitia 0684408755
Soma zaidi: GODIUS RWEYONGEZA Books
Maoni Ya Watu KuhusuVitabu Vya Godius Rweyongeza
Karibu sana
imeandikwa na Godius Rweyongeza
Morogoro-Tz
0755848391
-
Vitu 10 Vya Kijinga Ambavyo Unapaswa kufanya Walau Maram Moja Mwaka 2024
Leo nataka nikwambie vitu 10 tu vya kijinga ambavvyo unapaswa kujaribu kufanya walau mara moja ndani ya mwaka 2024
- Toa wiki moja ambayo utalala kwa saa tatu, halafu muda mwingine wote unafanya kazi. Fanya hivyo kwa siku mbili mpaka siku sita au wiki na siyo zaidi ya hapo.
- Weka akiba mshahara wako wote, halafu tafuta chanzo kingine ambacho kitakufanya ulipie bili na kuendesha maisha yako ya kila siku.
- Zima simu wiki nzima, halafu utumie muda huo kujifunza na kufanya kazi
- Ifanye siku moja kwa wiki kuwa takatifu kwako. Siku ambayo hutafanya kazi, bali itakuwa ni siku mapumziko na kupangilia ratiba zako za wiki inayofuata.
- Siku moja tembea kwa mguu au nenda na baiskeli sehemu ambayo ulikuwa umezoea kwenda kwa gari kama ofisini.
- Kwa dakika 15 tu kwa siku weka mziki wowote unaoupenda na cheza kama siyo wewe, kisha endelea na majukumu yako.
- Jiwekee utaratibu wa kutoa kitu kila siku hata kama ni kidogo. Kwa kuanzia unaweza kununua mfuko wa pipi, kisha kila siku ukatoa zawadi ya pipi moja kwa mtu yeyote.
- Mara moja moja pika chakula mwenyewe. NB. Hii ni kwa wale ambao huwa hawapiki, au wana wapishi au wenza wao wanapika. mara moja moja hasa ile siku unayokuwa umepumzika (rejea namba 4) pika chakula mwenyewe.
- Washa moto bila ya kiberiti, wala kuomba kwa jirani. Washa kwa ulimbombo na ulindi
- Mara moja lala kwa saa 10 mfululizo
Siyo lazima ufanyie kazi haya yote, fanyia baadhi yale unayoona unaweza kwa sasa. Usiache kuja kutupa mrejesho hapa baada ya kuyafanyia kazi.
Soma Zaidi: Vitu vitano ambavyo hupaswi kuvipoteza kwenye safari yako ya mafanikio
Nakupenda
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz
NB: SEMINA YETU YA JANUARI, itafanyika kuanzia tarehe 20-20 Februari
*Karibu kwenye Semina ya Kipekee ya Kufungua Mwaka 2024!*
—Rafiki yangu mpendwa,
Karibu kwenye mwaka wa mabadiliko na mafanikio –Kila mwaka, tumekuwa tukijiwekea lengo la kuleta tofauti katika maisha yetu kupitia semina tatu muhimu.
Ambapo huwa tuna semina ya kufungua mwaka (Januari 15-30)
SEMINA ya ana kwa ana (Jumamosi ya mwisho ya mwezi Juni) na semina nyingine ya mtandaoni (Septemba 24-30)Kwa Leo ningependa kuongelea
*Semina ya Kufungua Mwaka 2024: Njia Mpya, Matokeo Makubwa!*Tofauti na miaka iliyopita, semina hii ya Januari itakuwa ya kipekee. Badala ya siku 15, safari yetu ya mabadiliko itadumu kwa mwezi mzima! Kutoka tarehe 20 Januari hadi 20 Februari,
Kwenye hii semina tutajifumza mengi baadhi yakiwa ni pamoja na:
*Siku ya Kwanza: Karibu kwenye semina ya kufanya makubwa kwa vitendo mwaka 2024*
*Siku ya Pili: Anza Leo na Siyo Kesho*
*Siku ya Nne: Jinsi ya kuishinda tabia ya kughairisha*-
*Siku ya Kumi na Mbili: Jinsi simu zinavyoharibu ufanisi wako na nini cha kufanya mwaka 2024*
Mada hizi zote zimeundwa kukuhamasisha na kukusukuma kufikia mafanikio makubwa ndani ya mwaka 2024.
Kila siku itakuletea changamoto mpya na ufahamu wa kipekee. Tutajifunza jinsi ya kujiondoa kwenye tabia zinazotuzuia, kukabiliana na changamoto za kila siku, na kuanza safari ya kujenga mfumo bora wa maisha.
*Ada Yako ya Ushiriki:*
Ada ya semina ni zaidi ya thamani utakayopata – Tsh 30,000/-. Pata nafasi yako sasa kwa kulipa kupitia namba 0684408755 (Godius Rweyongeza).
Hii ni fursa yako ya kuanza mwaka 2024 kwa nguvu mpya na mwongozo wa kufanikiwa.
*Jiunge Nasi:*
Tunakualika kwenye kikundi chetu cha WhatsApp kwa ajili ya semina. Jiunge na wenzako wanaotafuta mabadiliko na mafanikio:
(https://chat.whatsapp.com/CAdCnW82i8N0clD2fDvn7v)
*Fanya Uamuzi wa Kuleta Mabadiliko:*
Hatua ndogo ndiyo mwanzo wa safari kubwa. Hakikisha unathibitisha ushiriki wako mapema na kuwa tayari kubadilisha maisha yako.
Tunakusubiri kwenye Semina ya Kufungua Mwaka 2024 ili uianze safari Yako ya Mabadiliko na Mafanikio!
Karibu sana!
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz -
Malengo Yako Ya Mwaka 2024 Usimwachie Mungu
Ni mwaka wa tatu sasa tarehe kama ya leo naandika makala inayosisitiza kuhusu malengo na kwa nini haupaswi kumwachia malengo yako mungu. Mwaka juzi niliandika makala hii hapa.
Makala hiyo hapo juu ina swali zuri sana ambalo nimekuwa napenda kuendelea kuwauliza watu kila mara.
Na hata juzi nilituma ujumbe kwa watu wa nguvu kupitia whatsap. Ujumbe huu ulikuwa na swali lililokuwa linauliza, umejiandaaje kwa ajili ya mwaka 2024? Lengo lako la mwaka 2024 ni lipi au unamwachia Mungu?
Cha kushangaza ni kwamba asilimia kubwa ya watu walisema kwamba wanamwachia Mungu. Kwa sababu ni mweza yote,
Ni alpha na omega.
anajua kesho yako
anachopanga yeye mwanadamu hawezi kupangua
na mengine mengi.
Ukweli ni kuwa malengo yako haupaswi kumwachia Mungu, japo ana sifa hizo ambazo watu wamekuwa wanatoa, ila ukweli ni kuwa Mungu mwenyewe anakuangalia wewe unavyofanya.
Mungu hawezi kukubariki ukiwa umebweteka, huna malengo, huna mwelekeo wowote, upo tu hapo. Kitendo cha wewe kukaa chini na kuweka malengo ni sawa na sala ya kumwambia Mungu kwamba sasa naomba baraka zako uzielekeze hapa.
Kitamfanya aachilie baraka zake kuelekea kwenye lengo lako, kuliko pale unapokuwa hauna lengo wala ndoto yoyote ile unayoifanyia kazi.
Umekuwa unaishi kwa miaka mingi bila ya kuwa lengo lolote. mwaka huu fuata mwongozo huu hapa kuweka malengo. Hata kama hujawahi kuweka malengo, ebu ufanye mwaka huu kuwa mwaka wako wa kwanza wa kuishi kwa kufuata malengo.
Kamwe usije kusema kwamba nimechelewa kuweka malengo. Muda bado, ndiyo kwanza kumekucha ndani ya 2024! Na kama unajua biashara mara zote ni asubuhi. Huu ndiyo muda wenyewe wa wwe kuutumia muda wako vizuri sasa.
Ukiwa na malengo, utakuwa na kusudi, utakuwa unajuwa wapi unaelekea na nini ufanye ili uweze kufika huko.
SOMA ZAIDI: Hatua Muhimu Katika Kuweka Malengo
Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu.
Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.
Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.
SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea.
Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga, +255 684 408 755
Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396
For Consultation only: +255 755 848 391 au godiusrweyongeza1@gmail.com
-
Salaam Za Kheri Ya Mwaka Mpya 2024 Kutoka Kwa Godius Rweyongeza
Rafiki yangu mpendwa, salaam. Nichukue nafasi hii kukutakia kheri ya mwaka mpya 2024. Ule mwaka uliokuwa umeusubiri sasa ndiyo huu hapa umefika. Yale mambo yote uliyokuwa umesema kwamba utayafanya ndani ya huu mwaka, sasa ndiyo muda muafaka wa kuyafanya.
Biashara uliyokuwa umesema kwamba utaanzisha mwaka 2024, hakikisha sasa unaianzisha. Akiba uliyokuwa umesema utaweka. Iweke.
Kiufupi lengo lako kuu la mwaka huu hakikisha kwamba unalifanyia kazi bila ya kuacha.
mwaka huu ufanye kuwa Baraka kwako. Na utaufanya hivyo kwa kufanyia kazi vile ulivyoopanga kufanya kuliko tu kuishia kusema kwamba utafanya.
Tumezoea kwamba watu huwa wanasherehekea sikukuu nyingi ambazo hawajasbabisha wao. Sikukuu ambazo huwa zinatokana na kalenda. Sikukuu hizi ni pamoja na mwaka mpya huu ambao unasherehehekea leo, siku za iddi, pasaka, sikukuu zote za kiserikali, krismasi na yinginezo. Mwaka huu usiishie tu kusherehehea sikukuu zinazotokana na kalenda. Sherehekea matokeo uliyopata kutokana na kufanyia kazi malengo na ndoto zako.
Kazi ya kufanya leo. Andika malengo yako makubwa ambayo utayafanyia kazi ndani ya mwaka 2024. Kila la kheri
Soma zaidi:Kheri ya mwaka mpya 2022
Kheri Ya Mwaka Mpya Na Mambo 12 Unayopaswa Kufanya Kuanzia Leo
-
Kwaheri 2023: Mambo 12 Ambayo Mwaka 2023 Umenifunza
Mwaka 2023 sasa unaisha.
Umekuwa ni mwaka bora sana kwangu, na umekuwani mwaka ambao nimeweza kufanya mengi, kuna mengi ambayo naweza kuandika kuhusu mwaka 2023 ila kwa leo nitaandika haya ambayo mwaka 2023 umenifundisha.
- mwaka 2023 umenifundisha kuwa kuwa mtandao wa intaneti una mkono mrefu. Najua wengi tumezoea kusikia kwamba serikali ina mkono mrefu. Lakini mwaka 2023 umenifundisha pia kuwa mtandao wa intaneti una mkono mrefu. Kuna makala nimekuwa naandika kwenye hii blogu tangu mwaka 2016 mpaka leo. Baadhi ya hizo makala hazikusomwa sana mwanzoni, ila kadiri siku zinavyokwenda watu wanazidi kuzisoma na kunufaika nazo. Japo nilishaandika hizi makala kwa muda mrefu ila mpaka leo hii kuna watu wanazidi kunufaika na hizo makala, na hii ni kwa sababu tu zipo mtandaoni. zingekuwa sehemu nyingine wasingeziona. Na ndio maana nimekuwa nashauri watu wengi wawe na blogu badala tu ya wewe kuwa unaandika vitu vyako vizuri na kuviweka whatsap ambapo baadaye vinapotea. Kama hauna blogu, mwaka 2024 hakikisha kwamba unaliweka hilo kama lengo lako la kuhakikisha unakuwa na blogu na hasa kama unashirikisha maarifa kwa njia ya mtandao. CHochote kile unachoandika hata kama ni kidogo, kiweke kwenye blogu, kuna siku kitakuwa na manufaa kwa watu wengine.
- Mwaka 2023 umenifundisha kuwa kufanya kazi kwa bidii kunalipa japo unaweza usione matokeo ya kwa muda mfupi muda mwingine. lakini unapaswa kuwa tayari kuwekeza kwenye kufanya kazi kwa bidii kama ambavyo wakimbiaji wa Marathoni huwa wapo tayari kuwekeza kwenye kufanya mazoezi kwa miaka minne kabla ya KUKIMBIA marathoni ya dakika kadhaa.
- mwaka 2023 umenifundisha kuwa tatizo la ajira nchini Tanzania ni kubwa, lakini pia vijana hawapendi kufanya kazi. Hili nimeligundua baada ya kuanza kuajiri. Mwanzoni nilifikiria kupata watu sahihi ni rahisi sana maana vijana wengi hawana ajira, ila kilichotokea ni tofauti. Vijana wengi kweli hawana ajira, ila pia hawako tayari kufanya kazi. Wanapenda pesa ila hawataki kazi.
- Mwaka 2023 umenifundisha kuwa kuchukua hatua ya kwanza ni muhimu sana. Lakini pia sambamba na hili mwaka huu umenifundisha kwamba unapopanga kufanya kitu kifanye. Mwaka huu tulipanga kufanya semina; kutokana na sababu kadha wa kadha kuna watu walidhani haitawezekana kufanyika. na wengine walisema huwezi kufanya semina bila ya kuwa na udhamini wa taasisi kubwa kama benki n.k. na hata wengine waliokuwa wameonesha nia ya kuhudhuria semina hawakufanya hivyo. Ila kwa kuwa tulikuwa tumepanga kufanya semina. Hatukurudi nyuma. Mwezi wa sita tarehe 24 tuliweza kufanya semina moja nzuri sana hapa Mjini Morogoro, ilihudhuriwa na watu wasiozidi 12, ila ilikuwa ni moja ya semina bora sana za mwaka 2023. Na hiki kimetupa mwanya wa kufanya semina nyingine zinazofuata, mfano mwaka 2024 mwezi wa sita tarehe 29 tutafanya semina ya ana kwa ana maeneo ya ubungo Dar. Unaweza kujiandikisha mapema, ada yake itakuwa ni laki moja kwa kila mshiriki. kujiandikisha tuma ujumbe kwenda namba ya simu 0755848391 sasa.
- Mwaka 2023 umenifundisha kwamba haupaswi kutegemea kitu kimoja au namba moja. Kama ni simu na unaitumia kwa kazi, usiitegemee moja. Kama ni kompyuta na unaitumia kwa kazi, usiitegemee moja, kuna siku hiyo unayoitegemea inaweza kugoma. Kama ni wafanyakazi usimtegemee mmoja, siku akiacha kazi utapasuka moyo, nadhani labda mwenza tu ndiyo unapaswa kuwa naye mmoja, ila vingine tafuta namna ya kuwa na ziada ili ikitokea moja imepata shida au dharula nyingine unaweza kuendelea mbele.
- Mwaka 2023 umenifundisha kuwa ukiajiri, lipa watu wako kwa wakati hata kama malipo unayowapa ni kidogo. Kamwe usimcheleweshee mfanyakazi wako mshahara wake..Hili somo nimejifunza kwa taabu sana baada ya kumcheleweshea mmoja wa wafanyakazi wangu maokoto yake, akaacha kazi na alikuwa ni mtu wa muhimu sana. Kwa lugha ya sasa hivi ni kwamba sikuzingatia maokoto. MWAKA 2024 ZINGATIA MAOKOTO.
- Mwaka 2023 umenifundisha kwamba, unapaswa kutangaza bidhaa au biashara yako au kitu chochote unachofanya kwa njia zote unazoweza kutumia. Mitandao, redio, runinga, viperushi kutaja ila vichache, mwaka huu kila njia niliyotumia kwenye kutangaza kwa namna moja au nyingine imeniletea wateja.
- Mwaka 2023 umenifundisha kuwa popote unapokuwa, itangaze biashara au bidhaa yako. Nilikuwa nasafiri kwenda Dar, kwenye gari nilisimama kwa ajili ya kuongea na wasafiri kuhusu umuhimu wa kusoma vitabu. Huwezi amini, miongoni mwa wale waliosikia kile nilichosema kuhusu usomaji wa vitabu, walihamasika, na sasa kuna watu wawili ambao wamekuwa wasomaji wazuri wa vitabu. Hii yote ni kutokana na mazungumzo yangu mafupi siku hiyo kwenye basi wakati tunatoka Morogoro kwenda Dar.
- Mwaka 2023, umenifundisha kuwa uwekezaji unanipa ridhiko la moyo sawa na kuandika kunavyonipa ridhiko la moyo. Huu umekuwa ni mwaka ambao nimekuwa nikifanya uwekezaji kwa nguvu zote, na mara zote ambazo nimekuwa nafanya uwekezaji, nimekuwa najisikia vizuri.
- Mwaka 2023 umenifundisha kuwa unapofanya kazi, unapaswa kuifanya kwa ubora wa hali ya juu sana. Maana hiyo kazi itadumu, lakini pia itawafikia wengi. Kuna baadhi ya vitabu nimeandika zaidi ya miaka sita iliyopita. Ila watu wamevisoma mwaka huu na vimekuwa vitabu vyenye msaada mkubwa kwao. Laiti ningekuwa nimeviandika hovyo visingeweza kuwa vyenye msaada kihivyo. Vitabu hivyo ni pamoja na kitabu cha TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA ambacho ndani ya huu mwaka kimepata mpaka nafasi ya kuongelewa kwenye bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hii ilikuwa ni baada ya mbunge, mh. Shamsi Vuai Nahodha kuwa amekisoma na kukipenda. Kitu hiki kilifanya watu wengi wapende kujipatia nakala zao, na kweli kila aliyepata nakala alitaka na rafiki yake aipate. Hii yote ilikuwa ni kwa sababu, niliandika kitabu hiki vizuri mwaka 2018, na sasa watu ndiyo wanatambua uwepo wake na wanakisoma kwa nguvu zao zote. Na wewe pia usisite kujipatia nakala ya kitabu hiki cha TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA: tatizo ni rasilimali watu tunaowapoteza. Kupata nakala yako wasiliana na 0684408755 sasa.
- Mwaka 2023 umenifundisha kukaa na watu sahihi. Nikijaribu kuangalia mambo yote makubwa ambayo nimeyafanya mwaka 2023 ni kwa sababu nyuma yangu nilikuwa na watu sahihi walionizunguka, la sivyo mengi yasingewezekana.
- Mwaka 2023 umenifundisha kuwa hakuna elimu au kitu chochote unachojifunza kinachopotea. Unaposoma kitabu siyo kwamba unapoteza, na kama kuna baadhi ya vitu ambavyo hujatumia siyo kwamba ndiyo umepoteza. Ila kuna siku, saa na dakika kitu hicho utakitumia na kitakuwa chenye manufaa kwako.
kuna mengi ambayo mwaka 2023 umenifundisha, ila kwa leo itoshe tu kusema kwamba hayo ndiyo masomo makubwa ambayo binafsi nimejifunza 2023.
Wwewe mwaka 2023 umekufunza kitu gani? Mjadala huu unaendelea kwenye kundi la whatsap, hapa
Au kwa email ambapo unaweza kunijibu kwa kunitumia ujumbe kwenda godiusrweyongeza1@gmail.com
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye ni kocha, mjasiriamali na mkufunzi. Unaweza kujifunza zaidi kwake kwa kujiunga na mafunzo ambayo huwa anatoa kwa njia ya barua pepe hapa.
Kupata makala maalum ambazo huwa anaandika kwa watu maalum. Bonyeza hapa
KUMBUKA:
Ofa ya msimu wa sikukuu inaelekea kuisha. Mwisho ni tarehe 1.1.2024 saa sita usiku
*Ofa ya kwanza*
*Unapata vitabu 6 (softcopy kwa 20,000/- au vitatu kwa 10,000/-* 🤭Chagua hapa, nipe taarifa👇🏿
1: JINSI YA KUTENGENEZA MSHAHARA NJE YA MSHAHARA
2: NGUVU YA WAZO
3: NGUVU YA KUWEKA MALENGO
4: MWONGOZO WA WAPAMBANAJI
5: MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BIASHARA
6: VYANZO VINGI VYA KIPATOLipia 10,000 upate vitabu VITATU, LIPIA 20000 Upate vyote SITA. ( Softcopy)
Namba ya MALIPO ni. 0684408755 GODIUS RWEYONGEZA
*Ofa ya pili*
Unapata audiobook 6 kwa 15,000/- TU. Audiobooks zenyewe ni.
1. NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA
2. JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO
3. MAISHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE
4. JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO
5. MAAJABU YA KUWEKA AKIBA
6. KIPAJI NI DHAHABUGharama ya hizi audiobooks ni zaidi ya ~100,000/~ ila kwa Sasa lipia 15,000/- TU upate zote sita.
Namba ya malipo ni 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA
*Hii ndiyo Ile ofa ushindwe mwenyewe*
Wewe ofa Yako msimu huu ni ipi?