Home


  • NJE YA KUMI NA NANE: fikiri, Hoji Na Uliza Maswali Katika Ulimwengu Ambao Hautaki Uwe Hivyo.

    Rafiki yangu, kama kwenye maisha yako bado hujafikia hatua ambapo wewe unaweza kufikiri nakuhoji na kuuliza maswali vitu. Basi bado hujaianza safari yako ya maisha. Hii ni hatua muhimu sana ambayo unapaswa kuifikia.

    Tuli[pokuwa wadogo tulikuwa tunapenda sana kuuliza maswali. Kuanzia maswali ya Mungu ni nani? Mpaka maswali ya watoto wanatoka wapi? Ila baada ya kukua inaonekana kuna ustaarabu ambao unakuja ghafla. Na ile shauku ya kujua vitu ambayo unakuwa nayo tangu utotoni inapotea. Leo hii nipo hapa kukwambia kuwa unapaswa kuendelea

    Kufikiri

    Kuuliza maswali

    Kuhoji

    Na kufanya maamuzi yako mwenyewe.

    Hakuna mtu ambaye anaweza kufikiri kwa niaba yako. Usimwongope yeyote.

    Watu wengi, viongozi wengi hawapendi kabisa uulize maswali au uhoji au ufikiri kwa namna yako. Ukionekana unafikiri, unahoji na kuuliza maswali na kufanya maamuzi yako mwenyewe unaonekana wewe ni tishio kwao na kwa uongozi wao!

    Ndiyo maana hata mfumo wa elimu ulipokuja hapa barani kwetu Afrika uliletwa katika mfumo huuhuu. Kwamba wapokeaji wa elimu wasiwe watu wa kufikiri, bali wawe watu wa kupokea maagizo na kuyafanyia kazi.

    Unaweza kudhani ni utani, unaweza kusema haka ka jamaa kanapata wapi ujasiri wa kusema haya, kama huniamini mimi basi iamini hata hii barua aliyoiandika Mfalme Leopord wa Pili kwa ajili ya wamisionari waliokuwa wanaeneza injili Afrika.

    Kwenye barua yake ameandika hivi; wafundishe hawa watu kusoma lakini siyo kufikiri.

    Hii dhana ya kufikiri, kuhoji na kuuliza maswali inaleta utata miongoni mwa watu wengi.

    Kwenye dini ukionekana unauliza maswali sana, watakwambia kwamba umeanza kuasi. Hivyo ili usionekane kama mtukutu unapaswa kufuata kila kitu kinachoelezwa au unachoambiwa. Kama una swali kafie nalo mbele huko…

    Kwenye elimu mpaka vyuo vikuu hivyohivyo, ukionekana unauliza sana, inaonekana unataka kuwa *challenge* maprofesa. Wanaweza mpaka wakakufelisha hivihivi..

    Wanafunzi wenzako wakiona unauliza sana maswali, wataanza kudhani ni utukutu tu au unajionesha.

    Sasa nataka nikwambie kitu kimoja tu, hoji kila kitu kwenye maisha yako. Uliza kila kitu, hata hili andiko unaruhusiwa kulihoji  na kuuliza. Ni kwa jinsi hii ndiyo utaweza kuupata ukweli kamili wa kile ambacho kineongelewa au ambacho unaanmbiwa. Na hivyo utaishi maisha yenye uhuru sana.

    NB: Hiyo barua ya mfalme Leopord wa pili wa wabeljiji unaweza kuipata mtandaoni. Andika, King Leopords letter to African Missionaries.

    Utakachosoma huko siri yako.

    Uwe na siku njema sana

    SOMA ZAIDI: Vitu viwili vinavyokufanya ushindwe kufikia ndoto zao

    Makala ya hii imeandikwa na Godius Rweyongeza

    0755848391

    Morogoro-Tz

  • Hiki ni kitu ambacho kinaenda kukupa matokeo makubwa kama utakifanyia kazi

    Rafiki yangu mpendwa salaam,

    Bila shaka unaendelea vyema na kazi zako. Hongera sana kwa kazi. Siku ya leo ningependa nikwambie kitu kimoja ambacho kinaenda kukupa matokeo makubwa.

    Kitu hiki siyo kingine bali ni kufanya kazi ambayo unapenda. Kama unahairisha sana kufanyia kazi majukumu yako, kuna uwezekano mkubwa kuwa unafanya kazi ambayo wewe mwenyewe hupendi. Kama utaanza kufanya kazi ambayo unapenda, ni wazi kuwa utajikuta kwamba unaifanya kwa bidii na kwa muda mrerfu na hata bila kuhairisha.

    Muda mwingine unaharishisha majukumu ambayo unapasw akuwa unayafanyia kazi kwa sababu huyapendi. Fanya kile unachopenda na ukweli ni kuwa hutajihisi kama unafanya kazi. Na hili litakufanya uweze kupata matokeo makubwa huku ukiwa unajisikia vizuri kwa kile unachofanya.

    Ujumbe wangu wa leo kwako ni mmoja tu; kama unataka kupata matokeo makubwa fanya kazi ambayo unapenda.

    Thomas Edison ni mmoja wa watu waliokuw awanafnaya kazi sana na kwa muda mrefu. Siku moja aliulizwa ni kwa nini anafanya kazi muda mrefu sana. Alijibu kwa kutoa jibu la kushangaza sana. Alisema, sijawahi kufanya kazi; inashangaza sana.

    Unajua kwa nini alisema kwamba sijawahi kufanya kazi. Alisema hivyo kwa sababu, alikuwa anafanya kazi anayoipenda na hivyo alikuwa hajisikii kama anafanya kazi japo alikuwa anafanya kazi kwa muda mrefu kuliko watu wote wlaiokuwa wamemzunguka.

    Kama huwezi kunisikiliza mimi, basi msikilize vizuri Thomas Edison.

    Kila la kheri.

    Makala imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Unaweza kuwasiliana na mwandishi kwa 0755848391 au baruapepe ya godiusrweyongeza1@gmail.com

    Kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza, jiunge na mfumo wake wa kupokea mafunzo kwa baruapepe. hapa chini

    Je, na wewe ungependa kujifunza uandishi? BONYEZA HAPA

  • Muda Ni Dhahabu

    Muda ni kitu pekee ambacho watu wote tunacho Kwa usawa. Ni muhimu sana kwangu kuhakikisha kuwa nakutumia vizuri muda wangu Kwa Manufaa. Hata kama Sina utajiri wa fedha ninaweza kubadili utajiri wa muda kuwa wa fedha.

    Muda ni DHAHABU, ninapaswa mara zote kuhakikisha nakutumia vizuri.

    Asante.

  • Utajiri ni hatima ambayo Kila Mmoja anapaswa kuipambania

    Kujenga utajiri ni mtazamo. Napaswa kubadili mtazamo wangu na kuona kuwa inawezekana kujenga utajiri mkubwa.

    Watu wengi wanakuwa na imani mbalimbali Kuhusu utajiri, wanaona utajiri ni mbaya na matajiri ni wabaya. Mtazamo huu huu unawafanya wengi washindwe kujenga utajiri Kwa sababu huwezi kupata kitu ambacho wewe Mwenyewe unaona ni kibaya.

    Ili kujenga utajiri unapaswa kuwa na mtazamo chanya kuwa utajiri ni mzuri na unapaswa kuupenda utajiri.

    Utajiri ni baraka. Ukiwa nao unakuwa msaada Kwa wengine usipokuwa nao unakuwa karaha Kwa wengine

    Utajiri ni mzuri.
    Utajiri ni hatima ambayo Kila Mmoja anapaswa kuipambania

    Asante
    Godius Rweyongeza
    www.songambele.co.tz

  • Mambo kumi yatakayokusaidia kulianza juma hili ukiwa mbele ya watu wengine

    1. Kwenye kila hatua unayofikia, bado kunakuwepo na hatua nyingine kubwa mbele yako ambazo unaweza kupiga, kwa hiyo usijizuie kupiga hatua kwenye Maisha yako kwa sababu ya mafanikio ya muda mfupi ambayo unapata. Badala yake kila mara jiulize ni kwa namna gani naweza kutumia matokeo ya sasa kwenda mbele zaidi.
    2. Unachohitaji wewe ni kuendelea mbele hata kama unapitia kwenye changamoto. Kitendo cha wewe kuendelea mbele kitaonesha kuwa wewe ni shujaa
    3. Watu wanaofanya vitu vya tofauti siyo kwamba wana muda mwingi wa kutosha kama unavyofikiri, nilichogundua ni kwamba mtu yeyote wa kawaida anayeweza kupangilia ratiba yake ya kila siku na akaifuata hiyo ratiba, anaweza kufanya makubwa kuliko mtu  anayesubiri kuwa na muda wa kutosha ili afaie kazi anachotamani.
    4. Kuwa na ndoto kubwa ni kitu kmoja, ila kufanyia kazi ndoto zako kubwa ni kitu kingine. Wewe kuwa upande wa kufanyia kazi ndoto zako.
    5. Ndoto yako kubwa kwa vyovyote vile inahitaji fedha, kuwa mtumiaji mzuri wa fedha, wekeza, na kila fedha inayoingia mfukoni mwako itumie vizuri kwa manufaa yako ya sasa na baadaye.
    6. Kama unataka kuishi Maisha ya kawaida, fanya vitu vya kawaida, kama unataka kufanya mambo ya tofauti, fanya vitu vya kawaida katika namna ambayo siyo ya kawaida.
    7. Mambo mengine yote yanaweza kusubiri, ila usisubirishe ndoto zako anza kuzifanyia kazi ndoto zako. anza kuzifanyia kazi ndoto zako hata kwa udogo.
    8. Kuna vitu viwili ambavyo kama bado hujavifanikisha basi unapaswa kuendelea kupambana mpaka kieleweke, endelea kupambana bila ya kurudia nyuma. Kitu cha kwanza ni kuwa na uwekezaji ambao unakuingizia fedha hata kama umelala na hapa siongelei fedha za kawaida, bali naongelea fedha za kuishia Maisha unayotaka , kama bado hujafikia hiki kiwango, basi usilale Rafiki yangu, endelea kupambana mpaka kieleweke.
    9. Kitu cha pili ambacho kama hujakifikia ni kuwa biashara ambayo inaweza kujiendwesha yenyewe bila ya kukuhitaji wewe. Kama bado hujafikia kwenye hivi viwango, basi unapaswa pia kuendelea kupambana bila ya kurudi nyuma mpaka kieleweke.
    10. Ishi Maisha yako, usiige Maisha ya watu wengine, unapoanza kuishi Maisha ya watu wengine, moja kwa moja unakuwa unajinyima fursa ya kuwa wewe halisi na kuonesha kile ambacho wewe mwenywewe unaweza kufanya..

    Hayo kwa leo yanatosha. Nikutakie mwanzo mwema wa juma hili hapa.

    Kila la kheri na waslimia sana Rafiki zako walio karibu na wewe.

  • Weka akiba kwa manufaa yako

    Ni vigumu sana kupata suluhisho la kudumu kwa njia za mkato. Suluhisho la kudumu, linahitaji njia ya uhakika ambayo utaifuata mpaka kufikia suluhisho.

    Kama una changamoto ya akiba, kukopa siyo suluhisho. Ila kuthibiti matumizi yako, kuongeza kipato na kuwa na vyanzo vingi vinayokuingizia kipato ndiyo suluhisho.

    Anza kuweka akiba leo, maana akiba ni mbegu ambayo unaitunza siyo kwa ajili ya leo tu bali kwa ajili ya siku nyingi zijazo. Weka akiba leo kwa manufaa yako ya siku nyingi zijazo.

    Kupata kitabu cha maajabu ya kuweka akiba ni rahisi sana. Wasiliana na 0684408755

    Fanya hivyo sasa ili kujipatia nakala yako sasa.

  • Hili Ndilo Suluhisho la Kudumu Kwa Tatizo La Ajira Linaloendelea

    Rafiki yangu mpendwa, bila shaka unaendelea vizuri, changamoto kubwa kwenye zama tunazoishi sasa hivi ni ajira. Kuna vijana wengi ambao wamehitimu chuo ila hawana ajira, kila siku wanahangaika kuomba kazi kwenye taasisi moja baada ya nyingine. Ukweli ni kuwa kwenye zama tunazoishi sasa hivi hakuna ajira kama ilivyokuwa kwenye zama za viwanda. Hata hivyo kazi za kufanya zipo nyingi na mahitaji ya msingi kabisa ya kila siku ya mtu yapo palepale. Kila siku kuna watu ambao wanahitaji kula, kila siku na watu ambao wanaendelea kutafuta elimu, watu wanaendelea kujenga kila siku…

    Kumbe tatizo siyo kazi maana zimejaa ila watu wa kufanya hizo kazi ndiyo hawapo.

    Kama unaweza kuchagua kazi yoyote ile na kujikita kwenye hiyo, ukaifanya kwa ubora na kutoa thamani kubwa kwa watu, maana yake mwisho wa siku utapata fedha kutoka kwa hao watu.

  • Nguvu Ya Vitu Vidogo Kuelekea Mafanikio Makubwa katika Vitendo…

    Huwa kuna kichekesho mtandaoni ambacho huwa kinasema ibada ilianza hivi, mpaka inaisha ilikuwa hivi..

    Au ibada ilianza vizuri, ila mambo yalibadilila pale mchungaji aliposema atakayeimba vizuri ataondoka na sadaka…

    Vichekesho vya aina hii huwa vinakuja kwa mfumo tofauti, ila lengo la hivi vichekesho huwa ni kitu kimoja tu, kusisitiza nguvu ya KUCHUKUA HATUA YA KWANZA ambayo ikiunganishwa na VITU VODOGO huwa inaleta matokeo makubwa.

    Na hiki ndicho ninataka kukwambia leo. Mwanzo wako hauwezi kuwa sawa na mwisho wako kana utaamua kufanya kile ulichochagua kweli bila kurudi NYUMA.

    Kumbuka, unahitaji ufanyie kazi ulichoamua kwa nguvu na kwa juhudi zako bila kurudi nyuma, mwisho wa siku, zile juhudi kidogo, zitaleta matokeo makubwa.

    Mambo yatakuwa mazuri kama utaendeleea kukomaa. Yatakuwa magumu pale uakapoishia njiani. Na mimi sitaki wewe uishie njiani…

    Endelea kupambana hata kama leo itaonekana ngumu..

    Jack Ma anasema leo itakuwa ngumu, kesho itakuwa ngumu zaidi, lakini siku baada ya kesho mambo yatakuwa marahisi ila ukweli mchungu ni kuwa watu wengi huwa wanakufa kesho jioni.

    Wewe usife kesho jioni…
    Unajua kufa kesho jioni maana yake ni nini?
    Maana yake ni kuacha kufanyia kazi ndoto zako.
    Maana yake ni kurudi nyuma baada ya kuwa umeanza
    Maana yake ni kuacha kufanyia kazi malengo yako kabla riba mkusanyiko haijaanza kuleta mabadiliko.

    Endelea mbele, hata kama leo mambo ni magumu, kesho mambo yatakuwa mazuri zaidi.

    Vitabu vitatu unavyopaswa kusoma leo ni

    1. NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA
    2. NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA
    3. NYUMA YA USHINDI: Kuna Kushindwa, Kushindwa, Kushindwa,….

    Kupata nakala zako wasiliana na 0684408755

    Asante sana

  • Vitu viwili vinavyokufanya ushindwe kufikia ndoto zao

    Ukiingia kwenye mitandao ya kijamii utakuta vijana mbalimbali wameandika kwenye mitandao yao mambo kadha wa kadha, unaweza kukuta mtu ameandika mfanyabiashsra, CEO, mjasiriamali na vungine vingi.

    Kati ya hayo matamanio mengi wanayokuwa nayo, ni wachache sana sana ambao huwa wanafikia na ndoto hizo. Kwa nini?

    Ninaenda kutoa sababu kuu mbili lakini kwanza, angalia video hiyo hapo juu👆🏿

    Sababu ya kwanza kwa Nini vijana wengi hawafikii ndoto zao kuwa na mambo mengi.

    Naam, huu ndiyo sababu ya kwanza kwa nini wengi hawafikii ndoto zao. Tena utakuta mtu anasema kuwa mambo ni mengi muda ni mchache. Ukweli ni kuwa unapokuwa na ndoto, akili yako na muda wako mwingi unapaswa kuuweka kwenye ndoto yako, sahau mambo mengine yasiyohusiana na ndoto zako na weka umakini wako wote kwenye ndoto zako.

    Ukiweza kuachana na mambo mengi unayopambana nayo na kuweka nguvu zaidi kwenye ndoto zako, ni wazi kuwa hii ndoto yako kubwa lazima tu utaifikia. Sasa swali ambalo unapaswa kujiuliza ni mambo gani ambayo umekuwa unafanya nje ya ndoto yako kuu? Je, ni vijitabia gani hasa ambavyo vinakupotezea muda ambao ungeweza kuuweka kwenye ndoto yako kubwa? Hivi vijitabia unapaswa kuachana navyo ili ujenge ndoto yako kubwa au la achana na ndoto yako kubwa ili ujenge vijitabia…..

    Ukweli ndio huo …
    Hakikisha umepata kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO utanishukuru kwa kukisoma, hiki mtandaoni hapa

    Au piga 0684408755 sasa uletewe nakala yako

    Sababu ya pili ni kuiga maisha ya watu wengine

    Kwenye clip fupi ambayo nimekushirikisha hapo juu nimekuonesha mhusika ambaye kila anapotembea kidogo anawaona wengine wanavyotembea anaanza kuiga mwenenedo wao wa kutembea. Sasa naomba unisikilize vizuri ili tuweze kuelewana; kuna vijana wengi wanapokuwa wanafanyia kazi ndoto zao wanakuwa hivi.

    Wanakuwa kama bebdera na kila wakati wanafuata upepo. Ukivuma kwa kasi kutoka kaskazini kuelekea kusini, wanaanza kuelekea kusini, baadaye ukibadili mwelekeo na wao wanabadili mwelekeo. Sikiliza, ukishajua ndoto yako kubwa ni ipi, kinachofuata ni wewe kukomaa nayo, haijalishi upepo unatokea wapi kuelekea wapi. Wewe komaa kwanza na ndoto yako moja mpaka kieleweke

    Usiwe mtu wa kuiga rafiki zako wanafanya nini. Ukweli ni kuwa ukienda kwa staili hiyo huwezi kufanikisha ndoto zako. Kwa sababu kila mara utakuta kuna mtu ambaye anafanya kitu fulani au ambaye amekuzidi.

    Lakini ukweli mwingine mchungu ni kuwa kadiri unavyobadili mwelekeo wako, ndivyo ambavyo utakosa kutumia UBUNIFU mkubwa ulionao. Nimeandika kitabu kizima kinachozungumzia namna unavyoweza kuibua ubunifu ulio ndani yako, unaweza kukipata mtandaoni ndani dakika mbili tu hapa.

    Kwa kumalizia Ningependa kusema kuwa ndoto uliyonayo, inawezekana kabisa kuitimiza. Unaweza kuitimiza kwa asilimia 100. Ila inahitaji ujitoe, ufanye kazi kwa bidii na ujitume mpaka kieleweke.

    Nakukumbusha kuhakikisha umepata kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO utanishukuru kwa kukisoma, hiki mtandaoni hapa

    Au piga 0684408755 sasa uletewe nakala yako

    Kuwa wewe mwenyewe.

    Makala hii imeqndikwa na Godius Rweyongeza
    Kujifunza zaidi kutoka Kwa Godius Rweyongeza tembelea www.songambele.co.tz
    Wasiliana naye Kwa 0755848391
    Morogoro-Tz

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza wasiliana na 0684408755

    Kujifunza UANDISHI na kupata usimamizi wa Moja Kwa Moja kutoka Kwa Godius Rweyongeza wasiliana na 0678848396

    Karibu sana

  • Unachohitaji wewe siyo hamasa zaidi bali ni matendo zaidi

    Mara kwa mara watu wamekuwa wanatafuta hamasa ya kufanya kitu. Ukweli ni kuwa huhitaji hamasa pekee ili kufanikisha lengo na ndoto yako kubwa. Bali unahitaji matendo ili uweze kufanyia kazi malengo na ndoto zako ziweze kufanikiwa.

    Nakwambia hivi kwa sababu hamasa huwa haidumu, hamasa ni kitu cha muda mfupi ambacho kinapotea. Hivyo ili ufanikishe malengo na ndoto zako kubwa ulizonazo unahitaji zaidi ya hamasa. Unahitaji matendo

    Wakati mwingine hujisikii kama kufanya kitu chochote kile. Lakini unapaswa kujisukuma kwa sababu ukisubiri hamasa pekee ili ufanyie kazi ndoto zako, ukweli ni kuwa hamasa hiyo itachelewa sana.

    Leo hujisikii kama una hamasa. Sikiliza, fanya kitu kimoja tu. Fanya kile kitu unachopaswa kufanya hata kama huna hamasa. Hamasa itakuja njiani, na hata kama hamasa haitakuja, utakuwa umeweza kukifanya hicho kitu.

    Kwa leo nadhani ujumbe umetosha sana.

    Kikubwa ni wewe kuufanyia kazi

    Kupata nakala za vitabu vyangu, basi wasiliana na 0684408755 karibu sana.

X