-
Jinsi ya kupunguza najuto yako utakapokuwa umezeeka
Moja ya changamoto kubwa ammbayo huwa inawakuta watu ambao wanakuwa hawafanyii kazi malengo na ndoto zao ni kwamba wanapofikia mwisho wa maisha yao basi wanakuwa na majuto mengi ambayo yanawaandama kutokana nay ale ambayo hawakuweza kufanyia kazi. Sasa wali kubwa ambalo unaweza kuwa unajiuliza ni kuwa je, kuna namna ambavyo naweza kupunguza haya majuto kwenye maisha yangu? Je, kuna namna ambavyo naweza nisije kuwa na majuto kabisa?
Ili kujibu haya maswali ni lazima kwanza tujue ni kitu gani ambacho huwa kinasababisha watu kuwa na majuto
Kwanza ni kufanya yale ambayo hawapendi.
Pili ni kutotumia uwezo wao
Tatu ni kutosimamia ukweli
Nne, ni kutochukua hatua na kujituma zaidi hasa wanapokuwa na uwezo wa kufanya hivyo.
Sasa kujua vitu ambavyo huwa vinasabahisha majuto miongoni mwa watu ni hatua moja kuwa, ila sasa baada ya kuijua hii hatua, kinachofuata ni kuchukua uamuzi wa wa kuahikisha kuwa mwisho wa siku unakuwa hauna majuto kwenye maisha yako. Fanya kinyume na hivyo vitu yaani
Fanya yale unayopenda kufanya
Fanya yale unayoona ni sahihi
Simamia ukweli
Tumia uwezo wako bila kuubana
Ukiweza kufanya hivyo, ni ukweli ulio wazi na usiopingika kuwa mwisho wa maisha yako hautakuwa na majuto, bali utakuwe umeweza kufanikisha makubwa pia
Kwa leo inatosha, nikutakie siku njema sana.
-
Kishiria kuwa umechelewa kufanya maamuzi
Rafiki yangu, kila siku kuna maamuzi ambayo tunatakiwa tufanye, yanaweza kuwa ni maamuzi ya nani uwe naye kwenye mahusiano, maamuzi ya biashara gani ufanye, maamuzi ya sehemu gani uende kutembelea. Maamuzi ya aina gani ya matangazo ufanye. Maamuzi ya nani umwajiri, nani umwondoe kazini au nani umpandishe cheo. Maamuzi ya shule gani mwanao asome au gari gani ununue na mengine mengi.
Kwa kuwa kuna maeneo mengi ya kufanyia maamuzi, siku ya leo ningependa tu kukwambia kuwa kama unafanya maamuzi hasa kwenye biashara ukiwa na uhakika wa asilimia 100 basi ni wazi kuwa unakuwa umechelewa. Yaani, umesubiri kila kitu kiwe sawa sawia.
-
Kuanguka ni kiashiria kuwa kuna kitu unafanya
Kuanguka siyo tatizo, kuanguka ni kishiria kwamba kuna kitu unafanya na ndiyo maana unakutana na vikwazo. Kumbe kuanguka kwako usikuone kama kigezo cha wewe kutoendelea mbele. Bali kuone kama sehemu ya wewe kuendelea kusonga mbele ili kuja kufanya makubwa zaidi.
Kadiri unavyokua, maanguko yako yanakuwa makubwa zaidi. Na yanajulikana kwa watu wengi zaidi kuliko pale unapokuwa chini, lakini hili lisikurudishe nyuma wala kukufanya ushindwe uweze kufanyia kazi malengo na ndoto zako. Bali hili liwe ni kama chachu ya wewe kuweza kufanya makubwa zaidi
Kwa sababu ukiendelea kubaki hapohapo ulipo, itakuwa ni vigumu kwako kuweza kufanya makubwa zaidi.
Wengine wanaogopa kuchukua hatua kwa sababu wanalinda heshima, labda ameajiriwa na anaogopa kwamba akianzisha biashara itafeli. Ukweli ni kuwa kulinda heshima ni sawa na timu inayolinda goli wakati wa mechi. Kama wachezaji hawatatoka kwenda kushambulia. Tena kushambilia kwa kiingereza kuna gumu kidogo to make an offense, . Kama wachezaji hawatatoka kwenda kushambulia, ujue wazi kuwa timu hiyo haitafunga.
Lakini uwezekano wa timu hiyo kufungwa ni mkubwa sana.
Kama huchukui hatua yoyote ile kwa kuogopa kushindwa, unakuwa huna tofauti na mtu ambaye analinda lango. Kazi yako, siyo kulinda lango, bali kushambulia mara kwa mara kadiri unavyoweza. Kadiri unavyoshambulia ndivyo ambavyo unaongeza uwezekano wa wewe kuweza kufunga zaidi.
Siku ya leo nataka uondoke na vitu viwili vikubwa
Kwanza fahamu kuwa kushindwa siyo tatizo, bali kushindwa kuchukua hatua na kuogopa kushindwa ni kikwazo na tatizo pia.
Pili, nataka ufahamu kuwa mara zote unapaswa kuwa kwenye mwendo wa kushambulia. Usilinde lango, usilinde heshima. Wewe shambulia tu hata kama utashindwa, utapata heshima zaidi kwa kushambulia kuliko kulinda lango
Mpaka siku nyingine, uwe na siku njema sana.
By the way nimeandika vitabu viwili ambavyo kwa siku ya leo ni muhimu sana kwako uvipate. Kitabu cha kwanza ni kitabu cha NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA, na kitabu kingine ni kitaub cha NYUMA YA USHINDI: Kuna kushindwa, kushindwa, kushindwa. Kuapata nakala za vitabu hivi tuwasiliane kwa 0684408755 sasa
Mpaka kesho, mimi nakutakia siku njema kwako
-
TAARIFA KWA UMMA
Siku za karibuni whatsap zimepatwa na changamoto na changamoto ya kufungiwa, kitu ambacho kimenifanya nikawa siwezi kupata jumbe zenu moja kwa moja. Nimejaribu kufungua akaunti nyingine za whatsap ambazo nazo pia zimefungiwa pia.
Hivyo, kwa sasa nimeamua kuwa nitatulia kutumia whatsap kwanza. ila nitakuwa natumia telegram. Unaweza kunifikia kwa haraka telegram kwa namba hii ya +255755848391
Hata hivyo ifahamike kuwa namba hii hii ya +255755848391 bado inapatikana vizuri kwa simu ya kawaida ya kupiga na SMS.
Aidha, namba ya ofisi ambayo ni +255684408755 inafanya kazi vizuri whatsap, na unaweza kuitumia bila wasiwasi wowote.
Natumaini utakuwa umeweza kunielewa na asante kwa kuelewa mabadiliko haya.
Asanteni,
[Jina lako] -
Wewe unafahamika Kwa kitu Gani ?
Moja ya uamuzi unaohitaji kufanya ni Uamuzi wa namna unavyotaka ufahamike kwenye maisha Yako. Nimekuwa nikisisitiza hiki kitu mara Kwa mara, lakini cha kushangaza ni kuwa Watu wengi wamekuwa Bado wanarudia kufanya makosa yaleyale Kila mara.
Ngoja nikwambie KITU, watu wengi unaowafahamu, huwafahamu Kwa sababu wanafanya Kila kitu au walikuwa wanafanya Kila kitu, bali unawafahamu Kwa sababu walibobea sehemu Moja.
- Iwe ni viongozi wa kiroho kama Budha, Yesu na Mtume Muhammad
- Au wanasiasa kama Nyerere.
- Au wanamuziki
- Wanamichezo na hata waandishi
Nyerere anafahamika kama mwalimu, lakini impact yake haukuwa kwenye kufundisha, kwake ualimu umebaki kuwa cheo Cha heshima tu, ila impact yake ilikuwa kwenye siasa.
Ndiyo maana mwaka 1955 aliachana na ualimu Ili aingie kwenye siasa Kwa sababu huko ndiko alitaka kuacha alama.
Ualimu ulikuwa unamlipa. Kwa lugha ya Leo tunaweza kusema alikuwa anapata maokoto mazuri tu Kwa ajili ya kuendesha maisha yake, Tena kipindi hicho ambacho Ajira zilikuwa ni adimu.
Lakini aliamua kuachana na Ajira Ili na kuingia kwenye siasa, Kwa sababu aliona alama yake kubwa ataiacha kama atakuwa kwenye siasa kuliko akiwa mwalimu.
Wakati mwingine inaonekana vigumu kuweka nguvu sehemu moja hasa pale ambapo vitu vyako vidogo vidogo unavyofanya vinapokuwa vinakuingizia maokoto kidogokidogo. Ila ukweli ni kuwa hiki kitu ndicho kitakupoteza pia. Maana haya maokoto kidogo ndiyo yatakunyina pesa za maana laiti kama ungewekeza muda na nguvu zako sehemu Moja na kuikuza. Ni ukweli kuwa ungeweza kupata matokeo makubwa zaidi.
Jipe muda wa kuwekeza kwenye ndoto Yako kuu na kuachana na vitu vingine vyote unavyofanya Kwa Sasa.
Inaweza isikulipe Kwa Sasa ila itakulipa baadaye.
Makala ya Leo imeandikwa na Godius Rweyongeza
Whatsap: 0687848391
Calls & SMS: 0755848391Jifunze zaidi Kwa Godius Rweyongeza Kwa kutembelea www.songambele.co.tz
Mpaka wakati mwingine. Tchao.
-
Kufa Leo, uishi milele
Ikiwa inamaanisha pambana Leo Ili juhudi zako ziendelee kukusaidia Mpaka kesho. WEKEZA Leo ule vinono kesho.
Kubali kupoteza Leo, Ili kesho kesho kutwa upate Kila kitu.
Ukweli ni kuwa maisha Yana trade off. Huwezi kupata Kila kitu unapokihitaji. Kuna baadhi ya vitu unahitaji uvipoteze Leo, Ili ufanye vingine lakini ukiwa Unajua kesho Utapata zaidi.
Na hili litawezekana kama tu utakuwa na ndoto kubwa. Kitu kinachonishangaza ni kuwa Watu wengi wanafanya vitu wakiwa hawana ndoto kubwa.
MTU anafanya BIASHARA, lakini hajui anataka BIASHARA hiyo impeleke wapi miaka mitano au Kumi ijayo.
MTU anafanya KAZI, au anaajiriwa lakini ukimuuliza, Nini malengo Yako na hii ajira Yako, Hana malengo Wala ndoto zozote.
Sasa haishangazi kuona MTU huyu anaanza Kufanya KAZI bila Kuweka juhudi Wala kujituma Kwa sababu hajui wapi hasa anaelekea.
Haishangazi kuona kwamba MTU anapopata mafanikio ya muda mfupi anaridhika na kuona kuwa amekwishafika, kumbe Bado sana.
Je, wewe ndoto zako kubwa ni zipi?
Kama Bado Hauna ndoto kubwa, kinachofuata hapa ni wewe kuhakikisha kwamba unapata kitabu Cha jinsi ya kufikia ndoto zako. Hiki Kitabu kina MWONGOZO mzuri WA kukusaidia wewe kufanikisha makubwa ambayo umekuwa unatamani kufanikisha Kwenye maisha Yako.
Watu wengi waliosona kitabu Hiki, nawaona wakipiga hatua kiasi kwamba ninaendelea kuwa na uhakika zaidi kuwa na wewe ukipata nakala Yako utaweza kupata matokeo makubwa kama haya na zaidi.
Kama Hawa wameweza, wewe unaweza pia.
Sasa, sikiliza kupata nakala Yako ni rahisi sana.
Lipia 20,000/- kwenda Airtel money 0684408755 Jina ni GODIUS RWEYONGEZA.
Ukishalipia, utanitumia ujumbe nikutumie Kitabu chako. Nauli ni juu Yako.
Asante sana
Makala hii imeqndikwa na Godius Rweyongeza
Whatsapp: 0687848391
Calls & SMS: 0755848391
MOROGORO-TZTembelea:www.songambele.co.tz
Kujifunza zaidi kutoka Kwa Godius Rweyongeza
-
Wiki Hii Nipo Nasoma Kitabu Cha Elon Musk. Kitu Kimoja Unachopaswa Kufahamu Kwanza

Wiki hii nipo nasoma kitabu kizuri sana Cha ELON MUSK: Kilichoandikwa na Walter Isaacson mtalaam wa kuandika vitabu vya wasifu (biographies).
Kwa Kuwa Bado naendelea kukisoma Kwa Sasa sitasema mengi zaidi ya kusema kuwa bila kujali unezaliwa wapi, Bado unaweza kuweka alama kwenye hii Dunia
Huhitaji ruhusa ya watu wengine zaidi ya ruhusa Yako tu kufanya hivyo.
Labda siku ya Leo Ningependa kuuliza swali Moja tu. Ndoto Yako kubwa ni ipi?
Iandike chini, Kisha chukua Hatua Ili uanze kuifanyia KAZIKupata kitabu Cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. Bonyeza hapa
Je, na wewe ungependa kupata Kitabu hiki Cha Elon Musk kilichoandikwa na Walter Isaacson. Utalipia vocha tu, tukutumie kitabu chako. Lipia Kwa 0684408755
Karibu sana
-
Je, ni kwa namna gani wewe unaitumia simu yako kwa manufaa?

Wakati mwingine ukiambiwa kwamba simu yako ina uwezo mkubwa, unaweza kudhani ni masihala vile. Leo nimechapa mawasiliano (namba za simu) yaliyo kwenye moja ya email yangu. Nimepata karatasi zenye kurasa 131
Na kila ukurasa umejaa juu mpaka chini.
Nilipobeba karatasi zenye haya mawasiliano mkononi ndiyo nikagundua ni kwa namna gani simu yangu imebebeba vitu vingi sana.
Nikajaribu kufikiria kama hivi vitu vyote vikiwekwa kwenye karatasi au kwenye mfumo wa kushika mkononi, pengine vinaweza visitoshe kwenye nyumba nzima (naweza kuwa nimetia chumvi kidogo hapa).
Mfano email yangu moja ina zaidi ya email elfu ishirini na tatu!
Vitabu zaidi ya elfu moja ambavyo vipo kwenye simu.
Sms za whatsap hata sijui ni ngapi
Sms za kawaida kama zote.
Hivi kama hivi vitu vyote vikichapwa kwenye karatasi kama nilivyofanya kwa namba za simu nitakuwa na karatasi zenye kurasa ngapi?
Hapo sijazungumzia screenshots ambazo huwa nachukua hapa na pale.
Picha za kawaida
Video na ……..
Hiki kitu nataka kikuoneshe thamani ya kifaa kidogo unachobeba mkononi mwako na kwenye mfuko wako leo hii.
Ukihitajika utoe kila kilicho kwenye simu ukibebe, huwezi kubeba vyote, (labda kama wewe ni hawafu mweye nguvu)
Miaka kama mitatu au minne hivi ya nyuma nilikutana na nukuu ambayo imekuwa ikinifanya nijitahidi kuitumia simu yangu kwa uzuri kila mara. Na nukuu hii ilikuwa inasema kwamba simu tunazotumia leo hii, zina uwezo mkubwa kuliko hata kompyuta iliyopeleka mtu mwezini.
Ebu pata picha ya kifaa ulichonacho leo hii. Yaani, kwa kifaa ulichonacho leo hii. Kina uwezo kuliko mtu kompyuta ya mwaka 1969 iliyopeleka mtu mwezini. Kinadharia ni kwamba, ukitaka kutumia kifaa chako hichohicho, unaweza kupeleka watu mwezini.
KUNA WATU WAMEONA FURSA YA KUTUMIA hiki kifaa (simu) vizuri. Na kuna watu ambao wanatumiwa na hiki kifaa.
Wewe uko upande gani?
Siku za nyuma niliwahi kushirikisha kuhusu vijana wa KiNigeria waliotengeneza kwa kutumia simu yao ya iliyoharibika haribika.Je, wewe ni kama hawa vijana wa kiNigeria waliotengeneza tamthiliya kwa kutumia simu? Au wewe ni kijana ambaye muda wote anafuatilia umbea kwenye simu yake.
Una app za umbea kwenye simu yako kuliko ulivyo na app za kujifunza vitu vya maana. Kama wewe ni mmoja wao, badilika.
Tena futa hizo app kabla sijafika hapo sasa hivi, hahaha,
Usiwe na wasiwasi, hapo siji, ila kama unazo kweli, FUTA
Niliwahi pia kushikirisha habari za kijana Khaby Lame ambaye aliachishwa kazi mwaka 2020. Je, wewe ni kama huyu kijana ambaye aliachishwa kazi wakati wa kipindi cha UVIKO-19 akaamua kuitumia simu yake kwa manufaa. Au, kazi yako ni kuwasimanga watu kwa simu yako?
Unakopa mpaka salio ili upate MB, na hakuna chochote cha maana unafanya?
Je, ni kwa namna gani wewe unaitumia simu yako kwa manufaa?
Nasubiri ujumbe wako sasa….
SOMA ZAIDI: Vitu 21 Ambavyo Ni Lazima Kufanya Hata Kama Una Kipaji Kikubwa
Uwe na siku njema
By the way, nimeandika kitabu kinachoitwa ZAMA ZIMEBADILIKA, MAISHA YAMEBADILIKA, AJIRA HATARINI NA WEWE BADILIKA. Hiki kitabu ni softcopy kwa sasa na gharama yake ni 10,000/- tu.
Kupata kitabu hiki, unalipia elfu kumi tu. Namba ya malipo ni 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.
Ukishalipia, nitumie ujumbe kwa namba hiyohiyo, ili nikutumie kitabu chako
Uwe na wakati mwema.
MAKALA HII IMEANDIKWA NA
Godius Rweyongeza
Kuwasiliana na Godius Rweyongeza, tuma ujumbe kwenda godiusrweyongeza1@gmail.com
Au 0755848391
Mpaka wakati mwingine
Tchao
-
Kama Hujisikii Kufanya Kazi
Huwa inatokea kwamba ninaanza kuandika huku nikiwa sijui ni kitu gani cha kuandika. Sijapangilia mada ya kuandika lakini muda huohuo napaswa kuandika na kuonesha kitu kwa watu wangu wa nguvu kama wewe hapo.
Na siku ya leo ni mojawapo.
Hata hivyo huwa ikitokea siku kama hii, kitu cha pekee ambacho huwa natakiwa kufanya siyo kuacha kuandika na kusubiri kwamba nitaandika kesho au wakati mwingine ambapo nitakuwa na kitu cha kuandika au hamasa ya kuandika, badala yake huwa napawa kukaa chini na kuanza kuandika, kwa maana muda mwingne hamasa huwa inakuja nikiwa naandika au kitu cha kuandika naweza kukipata nikiwa naandika kuliko pale ninapokuwa siandiki.
Si unajua huwezi kujikwaa kama hutembei Inawezekana wewe ukawa huandiki kama mimi. Lakini wakati mwingine ukawa hujisikii kuwa na hamasa ya kufanya kile kitu ambacho unatakiwa kufanya, hapa kuna vitu vitano ambavyo unapaswa kufanya unapokuwa kwenye hiyo hali..
KITU CHA KWANZA NI KUANZA KUFANYA HICHO KITU
Hiki ni kitu cha kwanza kabisa ambacho unapaswa kuanza nacho, anza kufanya kitu hata kama kwa wakati huo hujisikii kukifanya. Unaweza kwa nje ukawa hujisikii kuwa na motisha na nguvu ya kufanya hicho kitu, ila ile unapoanza kukifanyia kazi kile kitu unajikuta kwamba unapata hamasa ya kufanya zaidi hicho kitu na unajikuta unakuwa na ari. Hiki ni kitu ambacho wewe kwa upande wako unakuwa unahitaji. Kumbe anza kufanya kitu hata kama hujisikii wakati mwingine motisha na ari huwa inakuja ukiwa unafanya kuliko pale unapokuwa hufanyi kitu chochote.
KITU CHA PILI NI KUJIKUMBUSHA NDOTO ZAKO KUBWA
Kujikumbusha ndoto na malengo yako makubwa ni njia nyingine nzuri yaw ewe kurudi kwenye ari ya kufanyia kazi malengo yako. Kama hujisikii kufanya kitu, kaa chini na andika malengo yako na ndoto zako za muda mrefu. Kisha andika ni kitu gani kimoja ambacho unaweza kuanza kufanya sasa kikakupeleka wewe kwenye kufanikisha malengo yako ya sasa
Kusoma, kusikiliza au kuangalia video za hamasa kutoka kwa watu ambao wanafanya vitu na kupata matokeo inaweza kuwae ni njia nyingine ya kukufanya uendelee kukaa kwenye mstari kila mara, kazi yako kubwa kutoka inakuwa siyo tu kujifunza bali kufanyia kazi kile ulichojifunza kwa vitendo ili uweze kupata matokeo.
Rafiki yangu, inawezekana kwa sasa hauna hamasa ya kufanya kitu ambacho unapaswa kufanya. Haupasswi kukaa tu na kusubiri upate hamas aya kuanza kufanya kile kitu. Unachotakiwa kufanya ni kuingia ulingoni na kuanza kufanya hicho kitu. Ni kupitia kufanya, ndiyo utajikuta kwamba umeweza kukifanya.
Tena siku ambayo muda mwingine unakuwa hujisikii kufanya kitu, ndiyo siku ambayo unakuta kwamba inatokea kuwa siku bora kwako kuwahi kutokea kwenye kufanya kazi. Unajikuta kwamba umeweza kufanya kazi bora kabisa.
Hili linatokeaje, linatokea kwa wewe kuanza na kuchukua hatua ya kwanza ambayo ni kuanza kufanyia kazi kile ambacho mwanzoni ulikuw ahata hujikii kufanya.
EBU KWENYE MAONI, NIWEKEE MAONI YAKO, NIJUE KAMA IMEWAHI KUKUTOKEA SIKU KAMA HII KWENYE MAISHA YAKO NA NI KITU GANI AMBACHO ULIFANYA
MPAKA WAKATI MWINGINE, CHEERS
NB: Kama wewe ni miongoni mwa watu ambao bado hawajapata nakala ya kitabu cha NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA,basi ifanye leo kuwa siku yako ya kupata nakala ya kitabu hiki cha kipekee. Naam, kitabu cha NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA. Halafu kupata nakala ya kitabu hiki ni rahisi sana.
Nakala ngumu ni 20,000/-
Na nakala laini ni 10,000
Kupata nakala mojawapo hapo juu. Unalipia kwenda namba 0684408755
Changamka ufanye hivyo sasa
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Unaweza ujifunza zaidi kutoka kwa GODIUS Rweyongeza kwa kujiunga na watu wake wa nguvu ambao huwa wanapokea maandiko yake kupitia barua pepe
Jiunge hapa
Kuwasiliana moja kwa moja na Godius Rweyongeza, tumia godiusrweyongeza1@gmail.com
Kupata vitabu wasiliana na 0684408755
Kujifunza uandishi: 0687848391
Karibu
-
Wiki ya Huduma Kwa Wateja
Habari ya asubuhi upande wa huko
Hii ni wiki ya huduma kwa wateja. Na nimeona nikupe taarifa muhimu sana rafiki yangu. Na taarifa hii ni kwamba wiki hii una kila sababu ya kuwasiliana na wateja wako.
Mpigie hsimu hata mteja mwambia kwamba hii ni wiki ya huduma kwa wateja na nimepiga simu kwa ajili ya kukusalimia.
Mpigie hata mteja kumuuliza kama anaweza kuweka oda ndani ya hii wiki ya huduma kwa wateja.
Toa hata ofa kwa wateja wako.
Tuma hata ujumbe kwa wateja kuwasalimia
Omba hata maoni kwa wateja wako
Waambie wateja kuna mzigo mpya
Fanya chochote kile ndani ya hii wiki ya huduma kwa wateja kwa ajili ya wateja kuhakikisha unakuwa nao karibu. Asibaki hata mmoja ambaye hatasiki chochote kutoka kwako ndani ya hii wiki
Uwe na wiki njema sana
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz
Email: songambele.smb@gmail.com