Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Karibu Sana

    Hello! Tumekutumia kitabu kwenye barua pepe yako. Sasa hivi kitakuwa kimeshafika lakini kama hutajali, hapa nimekuwekea baadhi ya makala ambazo zimesomwa Sana

    [birdsend form=16776]

    Godius Rweyongeza

    0755848391

  • THINK BIG FOR AFRIKA

    Karibu kwenye kundi maalumu la whatsap la Think Big For Afrika! maelezo zaidi ya kina yanakuja hapa hapa baadaye. Au wasiliana na 0755848391 ili akupe maelekezo sasa.

  • WATU WANASEMAJE KUHUSU KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI?

    MIMI NAMFAHAMU GODIUS

    Ninamfahamu Godius si tu kwa kupitia maandishi yake bali kwa kupitia maisha yake. Jinsi anavyoishi ni darasa tosha la mtu yeyote mwenye nia ya kufanikiwa.

    Nilipoanza kusoma kitabu hiki sikukoma kuacha kwani kimegusa maisha yangu na baadhi ya mambo niliyoyapata humo nimeanza kuyafanyia kazi na nimeanza kuona maajabu makubwa.

    Unataka kuwa mbunifu? Soma kitabu hiki. Unataka kuwa kinara kwenye kipaji chako? soma kitabu hiki?

    Unataka kuwa kiongozi kwenye maisha yako? Soma kitabu hiki.Unataka maisha yenye furaha na ya kuacha alama? Majibu yote yanapatikana humu kwenye Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni.

    Imani yangu ni kwamba unaweza kuanzia hapo ulipo na kufika popote ili mradi akili yako umeipa ruhusa. Kila mtu amezaliwa mshindi, hakuna aliyekuja duniani kuwasindikiza wengine. Wewe ni wa tofauti, kuwa wewe, acha kujilinganisha na wengine, kujilinganisha kunabagua.

    Asante sana Godius Rweyongeza kwa kitabu hiki kinachotafakarishi, kinachotia hamasa na kinachotupa dira ya kuishi maisha kwa utimilifu.

    Edius Katamugora Mtunzi Yusufu Nina Ndoto


    MWANDISHI KATUMIA LUGHA NYEPESI KUONGEA MAMBO MAKUBWA YA KIMAFANIKIO

    Kila binadamu ndani kabisa ya moyo wake ana tamanio kubwa la kufanikiwa, yaani ikutoka ngazi ya chini kwenda ngazi ya juu katika Nyanja mbalimbali za Maisha. Kwa lugha nyepesi “Kutoka sifuri mpaka kileleni.

    Lakini changamoto kubwa inayowakabili watu wengi ni njia sahihi za kupita au kanuni za kufuata ili kufikia hatima hiyo.

    Mwandishi Godius Rweyongeza amejaribu, kwa kadri ya uwezo wake, kutumia lugha nyepesi na mifano halisi ya kumsaidia mtu kuweza kufuatana kutimiza azma ya mafanikio. Amezungumza kiundani jinsi ambavyo binadamu anaweza kutumia uwezo wa utashi aliopewa na Mwenyenzi Mungu katika kujiletea maendeleo binafsi katika Nyanja zote za Maisha.

    Ni matumaini yangu kuwau naposoma kitabu hiki utaweka katika matendo yale yote utakayojifunza ili uweze kupata matokeo bora yatakayokuwa chachu chanya kwa wengine pia.

    Nakutakia usomaji mwema na utekelezajiwa yale yote utakayojifunza.

    Anthony Luvanda

    Mjasiriamali na Mhamasishaji.

    Anzisha Biashara, Endesha Na Kuza Biashara Yako, Ufikie Ndoto Zako


    KAMA HUJUI NAMNA YA KUWEKA MALENGO, MWANDISHI AMEKUSAIDIA KUFANYA HIVYO KWENYE KITABU HIKI.

    “Usipowaambia watu kuhusu mafanikio yako bila shaka hakuna atakayekuja kuyajua” Donald Trump

    Acha Mimi nikuambie mafanikio yangu ili uyajue kupitia kitabu hiki cha kutoka sifuri hadi kileleni. Ukitaka kujua mafanikio yako anza kusoma kitabu hiki cha kutoka sifuri hadi kileleni. Kwani utagundua uwezo mkubwa wa kufanikiwa ulioko ndani yako, kwanini unajichelewesha kupata ushindi ambao uko ndani yako?

    Kama hujui kabisa namna ya kuweka malengo hatua kwa hatua ili yaweze kukusaidia kutoka sifuri hadi kileleni, basi mwandishi na mtaalamu wa kilimo cha bustani (Horticulture) Godius amekusaidia kufanya kazi hiyo kwenye kitabu chake cha kutoka sifuri hadi kileleni.

    Ukiona mtu amefanikiwa kutoka sifuri hadi kileleni jua kuna siri kubwa nyuma ya ushindi.

    Ninapendekeza kila anayetaka kufanikiwa, na hajawahi kusoma kitabu chochote kile basi kitabu hiki ni cha lazima kusoma kwa mtu makini anayeanzia chini kabisa na kutaka kufikia kileleni. Ni kitabu kinachokuonesha  mchakato wa mafanikio kutoka sifuri hadi kileleni.

    Kila la heri rafiki yangu katika usomaji wa kitabu hiki.

    Mwl. Deogratius Kessy

    Mwalimu, Mwandishi na Mjasiriamali.

    http://kessydeo.home.blog


    HIKI NI KITABU CHA KARNE YA 21

    Kujitoa bila kujibakisha, kusimamia jambo bila ya kurudi nyuma,  pamoja na kugundua uwezo wa ajabu aliouweka Mungu ndani yako, hivi vitakusaidia kufika hapo unapotaka kufika.

    Kitabu hiki kimeanza kwa kwanza kwa kumsukuma mwandishi ujiuliza kwa nini wengine wamefika walipokusudiwa na wengine hawafiki, majibu yake yakiwa ndani ya kitabu hiki, yanagusa kuhamasisha na kufundisha, hiki ni kitabu cha karne ya 21,hivyo kila mmoja anapaswa kukisoma.

    Mwalimu Adebert Chenche

    Mwenyekiti wa taasisi ya VIPAWA LINK ASSOCIATION


    NI KITABU CHENYE MAARIFA MENGI SANA.

    Ni kitabu chenye maarifa mengi sana. Kwa uhakika atakayekisoma na kuyafanyia kazi ataweza kupiga hatua kubwa katika kutimiza malengo yake

    NTANGEKI NSHALA


  • Jinsi Ya Kutengeneza Bahati Yako

    Dunia ina tabia ya kukupatia kitu kama utaonesha nia, kuwa wewe ungependa kupata hicho kitu. Huwa ninapenda kuwaambia watu kuwa, hata kama ni bahati itakukuta njiani unatembea wala sio chumbani kwako ukiwa umelala. Kwa hiyo, wewe kama unahitaji kupata bahati maishani mwako basi kuwa tayari kuweka kazi inayoendana na bahati unayotaka. Bahati unaitengeneza wewe mwenyewe na vitendo vyako ndivyo vinapaswa kuonesha hilo.

  • Vitu Vitano Kuhusu Fursa

    Leo nataka nikueleze vitu vitano muhimu unavyopaswa kufahamu kuhusu fursa. Watu wengi wamekuwa wanahadaiwa linapokuja suala zima la fursa.

    Kuna watu wamekuwa wanatumia mlango wa kuita haadhi ya vitu fursa ili wakupate.

    Kuna watu unakuta wanataka fedha zako, wanaangalia namna nzuri ya kuzipata, wanaona wanaweza kukupata kwa kukwambia kuwa kuna fursa ambayo unaweza kuifanyia kazi. Unahadaika, kumbe kitu chenyewe siyo fursa. Bali wewe mwenyewe ndiyo ulikuwa fursa.

    Ndio maana nimekuandalia vitu vitano unavyopaswa kujua kuhusu fursa. Hivi hapa

  • Jinsi ya Kuipangilia Ratiba Yako Vizuri Kuanzia Leo

    Njia bora ya Kuipangilia Ratiba Yako Vizuri ni kujiuliza ni

    1. vitu gani vya muhimu ambavyo napaswa kufanya.

    2. Vitu gani vya kufanya japo siyo muhimu sana.

    3. vitu gani ambavyo wanaweza kufanya wengine.

    4. Na ni vitu gani ambavyo wengine wananitaka nifanye.

    Mara zote weka nguvu zako kwenye namba 1 na namba 2.

    Kwa vitu ambavyo wanaweza kufanya wengine; wape wavifanye.

    Achana na vile ambavyo wengine wanakutaka uvifanye.

    Maisha ni mafupi kuyaporeza kwenye shughuli ambazo siyo muhimu.

  • Naomba ushauri Nifanyeje?

    Bila shaka wamewahi kutokea watu wa kukuomba ushauri maishani mwako.

    Na pengine wewe ulitoa huo, ushauri. Ila sasa una hakika kuwa wewe ulikuwa hauhitaji huo ushauri?

    Kama huwa inatokea kuwa unatoa ushauri kwa watu ambao wewe mwenyewe unauhitaji. Hakikisha unaanza kuutumia mwenyewe.

    Ukimshauri mtu kuweka AKIBA, wewe mwenyewe weka akiba.
    Ukimshauri mtu kufanya mazoezi wewe mwenyewe fanya mazoezi

    Ukimshauri mtu kula vizuri, kama profeda jay alivyomshauri ferooz kwenye wimbo wa starehe, hakikisha na wewe unafanya hivyo.

    Ni hivyo tu?

    Umekuwa nami
    Godius Rweyongeza
    0755848391

  • Kitu kingine kimoja cha ziada kuhusu Masoud Kipanya

    Au wewe hukupenda….

    Nashukuru wengi waliipokea vizuri mkala ya Jana, hata hivyo leo nimeona nitaongeza kitu kimoja.

    Unachopaswa kufahamu ni kuwa sijalipwa na mtu yeyote kuandika ninayoandika. Ninaamdika mwenyewe tu kwa mapenzi yangu. Ni hivyo tu….

    Kitu chenyewe ninachotaka ujue ni kuedesha BIASHARA kitalaam tangu siku ya ya kwanza (day one)

    Umeelewa hapo au nirudie.

    Ukiangalia hapo utagundua kwamba japo ndio kwanza kampuni yake inaanza, ila tayari ana timu ya mauzo, ana timu ya uzalishaji, mkurugenzi msaidizi,
    Logo n.k.

    Hapo unagundua kitu kikubwa ambacho BIASHARA nyingi zinakosa. Mfumo sahihi wa kuendesha Biashara.

    Ebu niambie, wewe kwenye BIASHARA yako una mkurugenzi wa uzalishaji.
    Mkurugenzi wa masoko na mauzo
    Mkurugenzi mkuu na msaidizi wake
    Biashara yako ina logo?

    Najua unaweza kujitetea kwa kusema kuwa biashara yako ni ndogo, ila unachopaswa kufahamu ni kuwa kama una ndoto na mpango wa kuipeleka mbali biashara yako, utapaswa kuipangilia kihivyo.
    Utapaswa kuwa na meneja wa uzalishaji hata kama unafanya biashara ya rejareja.
    Utapaswa kuwa na meneja wa masoko hata kama uko peke yako kwenye biashara!

    Unaona eeh!

    Najua utaanza kuniambia, ooh unajua BIASHARA yangu siyo kama ya Masoud. Shauri yako…

    BIASHARA yotote unahitaji hivyo vitu.

    Tatizo lalo wewe unafanya vitu kienyeji halafu ukiambiwa, unakuwa mhishi kweli….

    Ka uko peke yako utapaswa kugawa majukumu yako na kila Mara ujue ni lini unafanya majukumu kwenye idara gani.
    Ukienda kununua bidhaa, ujue kabisa kwamba hapo upo kwenye uzalishaji kwa biashara za rejareja na jumla.

    Ukiwashawishi wateja waje kwenye biashara yako, hayo ni masoko.

    Ukiuza hayo ni mauzo

    Fahamu hivi vitu, vitakusaidia weww kuendesha biashara yako kitalaamu.

  • Niseme kitu kuhusu Elon Musk  Kununua Twitter Au Basi!👇🏿👇🏿

    Udhaifu wangu mkubwa Ni kwamba ninapokuwa na kitu kikubwa kinachoweza kukusaidia wewe kufanya makubwa siwezi kukaa nacho!

    Nashindwa kabisa  kujizuia,  Ndio maana leo nikaona nikujuze habari za Elon Musk

    Habari zilizotawala vyombo mbalimbali vya habari na hasa mtandao wa intaneti siku ya jana ni kuhusu bilionea Elon Musk kuwekeza kwenye kampuni ya Twitter. Ambapo amenunua asilimia 9.18%

    Kitu kinachomfanya yeye kuwa mwekezaji mkubwa kwenye hiyo kampuni.

    Kama ulikuwa hujui Ni kwamba: ukiwa mwekezaji mkubwaa kwenye kampuni maana yake unakuwa na nafasi ya kufanya maamumizi kwenye kampuni, unakuwa na uwezo wa kupush baadhi ya mambo kwa kutumia wingi wa hisa zako.

    Asilimia 9.18 haimfanyi Elon Musk kuwa na maamuzi kamili juu ya kampuni ya Twitter. Maana ili uwe na maamuzi kamili unapaswa kuwa na walau asilimia 51 ya kampuni ila inafanya usemi wake kwenye kampuni kuwa na uzito mkubwa.

    Kuna mambo mawili tu nataka ujifunze kutoka kwa Elon Musk siku ya leo kuhusiananna hiki kitu…

    1. Ukiamua kuwekeza wekeza
    Umeshafuatilia Elon Musk amewekeza kwenye kampuni gani na ana umiliki kiasi gani? Kwenye kampuni yake ya Tesla ana umiliki wa asilimia 17 na SpaceX ana umiliki wa asilimia 54.

    Hiki ni kiashiria kuwa huyu jamaa hawekezi kwenye kampuni yoyote kama underdog badala yake anafanya uwekezaji mkubwa haswa.

    Hiki kitu kikupe picha na wewe unapofanya uwekezaji. Usiwe mtu wa kufanya uwekezaji wa kudonoa, donoa badala yake amua kufanya uwekezaji mkubwa na wa viwango vya juu bila kuacha.

    Hata Kama utakuwa unaanza kidogo, wewe endelea tu kuwekeza kila mara bila ya kurudi nyuma hata kidogo.

    2. Ukiamua kufanya kitu kifanye vizuri

    Elon Musk amekuwa na historia ya kufanya vizuri kwenye makampuni yake, kitu ambacho kimewapa watu imani alipowekeza  twitter, na hapo watu wanaona kwamba  hata huku anaenda kuleta mabadiliko makubwa.

    Imani hiyo tu imefanya hisa za kampuni ya twitter kupanda.

  • Leo Na Mimi Nataka Niseme Kitu Kuhusu Gari Ya Masoud Kipanya

    Watu wenye kichaa cha kutosha kiasi cha kufikiri wanaweza kuibadili dunia, ndio ambao huibadili-Steve Jobs kwenye tangazo la THINK DIFFERENT la mwaka 1997-2002

    Takribani siku mbili zilizopita Masoud kipanya alizindua gari ya umeme ya kampuni ya Kaypee Motors. Kitu ambacho ni cha kipekee sana hasa kwenye mazingira yetu. Asubuhi ya leo nilipotazama hotuba yake wakati anazindua gari yake,ilikuwa ni kama naangalia hotuba ya Steve Jobs akizindua iphone ya kwanza kabisa mwaka 2007. Ilikuwa inahamaisha lakini pia inakufanya wewe uweze kufikiri kwa ukubwa zaidi na wakati huohuo unaona kwamba yajayo yanafurahisha.

    Sasa kwanza lazima tukubaliane kwamba gari ya Masoud na kitu alichofanya kiujumla ni kitu ambacho kinawasha moto miongoni mwa vijana wengi wa kitanzania wenye ndoto kubwa. kitu hiki kinastahili pongezi na ndio maana nimeandika makala hii…

    Kwa kawaida vitu hivi huwa vinaonekana vigumu pale kunapokuwa hakuna mtu ambaye amewahi kuonekana akifanya vitu vya tofauti. Ila sasa anapotokea mtu katika jamii yenu akafanya kitu cha tofauti basi kinakuwa ni kiashiria kuwa wengine pia wanaweza na hivyo, watu wengine  watajitoa kuhakikisha kwamba wanafanyia kazi ndoto zao.

    Jamii nyingi za kitanzania na za kiafirika kiujumla zimeaminishwa kwamba kuna vitu ambavyo huwezi kufanya kwenye maisha yako bila ya kuwa msaada wa mtu yeyote nyuma yako. Na kiufupi inaaminika kwamba vitu vingine wanaweza kufanya wazungu tu na siyo waafrika au watanzania.

    Ndio maana ukizunguka mtaani utasikia watu wanasema maneno kama kazi ya mzungu, utasikia wengine wakisema kwamba mzungu noma.

    Nimekuwa nikisisitiza kwa watu kupitia makala zangu mbalimbali kuwa kila mtu ana uwezo mkubwa uliolala ndani yake ambao anaweza kuutumia kufanya makubwa. Ila watu wengi wamekuwa hawatumii uwezo huu na hii inatokana na sababu mbalimbali ikiwemo jamii zetu ambazo haziamini katika ndoto na vitu vikubwa,. Na hata mfumo wa shule.

    Lakini tafiti zimeonesha kuwa hata wale ambao wanaonekana wamefanya makubwa hapa duniani, siyo kwamba wanakuwa wametumia uwezo wao wote, bali wanakuwa wametumia chini ya asilimia kumi tu ya uwezo wao.  Sasa sijui wewe unatumia asilimia ngapi ya uwezo wako. Ila kikubwa ni kwamba ukikazana tu hata kutumia asilimia kumi ya uwezo wako, utaweza kufanya makubwa sana.

    Na unachopaswa kufahamu ni kwamba uwezo wako hauwezi kuutumia ukaisha. Kadiri unavyoutumia ndivyo unavyozidi kubarikiwa zaidi. Labda swali la uchokozi tu, umeshawahi kusikia kwamba Masoud ameacha kuchora kwa sababu kaishiwa na mawazo (ideas) za kuchora! Au kwamba hajaweza kuchora kwa sababu ametumia uwezo wake wote umeisha? Umewahi kusikia hilo..

    Unachopaswa kufahamu ni kwamba kadiri unavyotumia uwezo wako, ndivyo uwezo wako unavyozidi kuongezeka zaidi… hata kama ungekuwa unaishi miaka buku, bado tu uwezo wako ungekuwa unazidi kumeremeta! Ndio maana hautakaa usikie kwamba Masoud ameshindwa kuchora kwa sababu kaishiwa…

    Labda aamue tu.

    Sasa na wewe ungeweza kuutumia uwezo huu wala si ungefika mbali?

    Kwa maoni yangu kitu alichofanya Masoud ni mapinduzi makubwa na moto ambao ameuwasha kwa vijana wengi wa kitanzania. Siku siyo nyingi vijana wengine zaidi watakuwa wakizipambania ndoto zao siyo tu kwa kuanzisha vitu na kuishia njiani, bali kwa kuhakikisha kwamba wanazifanyia kazi ndoto zao mpaka zinatimia.

    Na kwa leo nimeona niandae mambo sita makubwa ya kujifunza kutoka MASOUD KIPANDA NA NDOTO YAKE YA GARI LA UMEME.

    KWANZA; KABISA NI KUWA NDOTO KUBWA.

    PILI; ANZA KUFANYIA KAZI NDOTO ZAKO

    Uwepo wa mitandao ya kijamii umekuwa ni baraka na wakati huohuo umekuwa kama karaha vile. Mtu akifikiri kufanya kitu hata kama hajakiweka kwenye vitendo anaingia mtandaoni na kuanza kujitangaza.

    Ndio maana ukiingia kwenye mitandao ya kijamii kama facebook, twitter na instagram utakutana na vitu vya ajabu  kweli.

    Kuna watu ambao wanajiita wajasiriamali wakiwa hawajawahi kufanya biashara yoyote ile maishani mwao. Ila ukiangalia profie zao wanajiita maCEO wa kampuni.

    Kuna watu wanajiita waandishi wakiwa hawajawahi kuandika hata sentensi moja.

    Kuna watu wanajiita wachoraji wakiwa hawajawahi kuchora hata mchoro kimoja. Unajua kwa nini?

    Kwa sababu ni rahisi kuongea kuliko ilivyo rahisi kufanya.

    Sasa ninachotaka wewe ufanye siyo tu uwe muongeaji, bali uwe mtu wa vitendo. Na hili unaweza kulifanya.

    TATU IPE NDOTO YAKO MUDA

    Kuna mtu anapenda akiwa na ndoto kubwa leo hii, kesho yake awe ameifanikisha. Siyo kweli. Ndoto kubwa inachukua muda na inahitaji muda kuweza kuifikia.

    Kila mara nimekuwa nikiongea na vijana na kuwauliza una mipango gani miaka mitano au kumi ijayo. Ila cha kushanganza ni pale ambapo mtu anakushangaa. Utakuta mtu anasema yaani, wewe unaongelea mambo ya miaka 10 ijayo leo hii?

    Mwingine atakwambia “mimi nahangaika na leo, kesho itajipa yenyewe”.

    Ngoja nikwambie kitu.

    Kama unataka kufanya makubwa na kama unataka kufika mbali, kuwa na ndoto kubwa ambayo unaifanyia kazi.

    Inaweza kuchukua muda kufikiwa, ila ukweli ni kwamba inawezekana.

    jinsi ya kufikia ndoto zako
    Kupata kitabu hiki wasiliana nami kwa 0755848391

    NNE; KUBALI KUANZIA CHINI

    Ndio unapaswa kuwa na ndoto kubwa, ila unapaswa kuwa tayari kukaa chini na kuanza kuifanyia kazi ndoto yako hata kwa kuanzia chini.

    Ndoto kubwa haifanyiwi kazi kwa siku moja na kukamilika. Unahitaji kuanzia chini, unapaswa kuanza na kile ulichonacho na kukifanyia kazi na kisha kuendelea kukuza kile kidogo ulichonacho.

    Na sehemu nzuri ya wewe kuanzia ni kuanza kuitumia MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA sasa hivi.

    TANO;UKISIBURI MSAADA UFANYIE KAZI NDOTO YAKO, UTASUBIRI SANA

    Yaani, sijui ni nini huyu alikuja na hili suala la misaada. Unakuta mtu anataka akaombe msaada wa kufanyia kazi kila kitu ambacho anakifirikia kwenye maisha yake.

    Muda mwingine kuna vitu ambavyo unaweza kuanza kuvifanyia kazi bila hata ya kuhitaji msaada. Unaweza kudhani unahitaji msaada, kumbe huo msaada wenyewe utaishia tu kukuharibu na kukufanya ushindwe kufanikisha ndoto zako.

    Ujue hili suala la misaada linafanya watu wasifikiri nje ya boksi. Unakuta mtu ana vitu vya kumsaidia kufanikisha ndoto yake ila tu kwa sababu akili yake ameiaminisha kuwa bila msaada haiwezi, utakuta kwamba anaendelea kusubiri msaada.

    Nakumbuka niliwahi kukutana na kijana mmoja aliyekuwa na ndoto ya kufuga kuku. Nyumbani kwao kulikuwa na eneo kubwa tu la kumwezesha kufanya hivyo,ila unajua nini? Alikuwa amesubiri siku moja litokee zari la mentali ili aanze kufanyia kazi hiyo ndoto yake.

    Naomba unisikilize wewe mwenye ndoto kubwa. ni kweli maishani kuna bahati, ila sasa bahati haimfuati mtu ambaye amelala kitandani na kuisburi. Bahati wanakutana nayo watembeaji…

    Kama na wewe unataka bahati ya kukusaidia kufanikisha ndoto yako, basi utapaswa kuanza kufanyia kazi ndoto yako, ndipo utajiweka kwenye nafasi ya kukutana na bahati. Sijui unanielewa hapo, au niongeze sauti….

    Basi bana, niache kwanza niendelee…

    SITA; UNAWEZA KUTENGENEZA NJIA PASIPO NA NJIA

    Njia pekee ya wewe kutengeneza njia pasipo na njia ni wewe kuhakikisha kwamba unapita eneo hilo kila siku bila kuacha. Siku ya kwanza hakuna kitu kitaonekana. Kadhalika siku ya pili mpaka hata ya 100 ila uhakika ni kwamba baada ya siku 365, eneo ambalo unapita kila siku. Kuna njia ambayo itakuwa imeshaanza kuonekana kuwa ipo.

    Sasa hivyohivyo kwenye ndoto yako. Ukianza leo hii kuifanyia kazi ndoto yako, utaanza kuonekana kichaa kwa kufanyia kazi kitu ambacho hakiwezekani kabisa. ila ukweli ni kwamba kama hautakata tamaa, miaka kadhaa mbeleni, basi na wewe utakuwa na kitu ambacho unaweza kuongelea mbele ya watu na kuonesha kuwa kweli nimeweza kufanya kitu cha maana.

    Nakuamini wewe

    Naamini unaweza

    Usiniangushe

    Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio

    Ni mimi

    Godius Rweyongeza

    0755848391

    Morogoro-Tz

X