Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Hii Ndiyo Kazi Rahisi Kuliko Zote Duniani

    Nakumbuka siku moja kwenye redio kulikuwa mjadala mzito. Mada mezani lilikuwa ni swali lililouliza ni kazi ipi ni rahisi hapa duniani.

    Kila mtu alijitahidi kuchangia mada kiundani kadiri alivyoweza. Nakumbuka vizuri jamaa mmoja alichangia mada kwa kusema kuwa hapa duniani hakuna kazi rahisi. Kila kazi ni ngumu.

    Aliendelea kusema kuwa ukiwa mwanasheria utaona kuwa Sheria ni ngumu.
    Ukiwa daktari, utasema utabibu ni mgumu.
    Ukiwa unabeba mizigo, utasema kazi yako ni ngumu na
    Mkulima naye atasema kazi yake ni noma!
    Huku dereva wa masafa maredu Naye atasema, we acha. Muda mwingine hulali eti unaendesha gari.

    Kwa kipindi hicho nilikubaliana na hilo jibu na kila mara ulipokuwa ukitokea mjadala wa aina hiyo, nilikuwa nikichangia kwa kusema kuwa hakuna kazi rahisi hapa duniani. Badala yake kazi ambayo kila mtu anafanya kwake ni ngumu.

    Mara zote nilipokuwa nikisema hivi, nilikuwa naonekana kama nilikuwa natoa booonge na   pointi…. Laiti kama ningekuwa nachangia mada kwenye midahalo kama ile ya education is better than money, basi ningekuwa napigiwa makofi ya kishindo….

    Unaikumbuka ile midahalo ya education is better than money?????

    Mimi naikumbuka sana, maana enzi hizo kama ningekosa kuchangia pointi kwenye mdahalo siku hiyo ningeumwa. Moja ya mdahalo mzito ambao nakumbuka ulizua utata, ulikuwa ni mdahalo wa the love of money is the root of all evils.

    Watu tulishusha kimombo hatari siku hiyo…..
    Nadhani malkia angekuwepo siku hiyo angenipeleka kwenye kasri yake nikae humo tu 😂😂

    Hivi nilisema nakwambia kazi rahisi kuliko zote hapa duniani eeh!

    Nshajisahau nikajua sijui nipo nafundisha shule ya msingi. Maana kuna kipindi pia nilikuwa na ndoto za kuwa mwalimu😂😂..

    Aaah,
    Acha bwana tuendelee.

    Ukipata na kazi ya aina hii, hii ndio rahisi.

    Unajua kwa Nini?

    Kwa sababu ni kazi ambayo hutahangaika kuifanya. Ni kazi ambayo hata ukiifanya kwa muda mrefu, hutaona kama umeifanya kwa muda mrefu. Kwa sababu tu unaipenda. Kwa sababu una Ilove.

    Thomas Edison alikuwa alala saa tatu kila siku na kuwahi kazini. Siku moja aliulizwa kwa nini unafanya kazi kwa muda mrefu hivyo, akisema sijawahi kufanya kazi.

    Si inashangaza eeh! Yaani, mtu anafanya kazi saa 18 mfululizo, halafu anasema eti hajawahi kufanya kazi….

    Alikuwa anasema hivyo kwa sababu tu alikuwa anafanya kitu alichokuwa anapenda.

    Ukiwa na unafanya kazi unayoipenda, hata huhangaiki kuangalia muda…
    Yaani, wewe unapiga kazi tu, halafu baadaye unastuka kuona muda umeenda sana.
    Unafanya kazi saa nane ila unaona kama vile ndio umeanza.
    Husukumwi na mtu kuifanya, wewe mwenyewe unajisukuma kwa sababu unaipenda.

    Hapa ndio namkumbuka Albert Einstein. Huyu jamaa naye wakati mwingine alikuwa na vituko…
    Kuna siku alisema; ukikaa na binti mkali (mrembo) kwa saa mbili utaona kama umekaa naye kwa dakika moja, Ila ukikaa na kwenye makaa ya moto kwa dakika moja, itaonekana kama saa 2.

    Hii pia inafanya kazi kwenye maisha ya kazi.
    Ukifanya kazi ambayo huupendi. Kila sekunde kwako itakuwa ya moto. Utaona muda hauendi. Na utatamani uzurure huku na kule ili muda uende…

    Acha kujiumiza. Kuanzia leo anza kufanya kazi unayopenda. Kama kazi uliyonayo Sasa hivi huipendi, basi ipende. Kama huwezi kuipenda achana nayo ukafanye kazi unayopenda.

  • Ni ushauri tu

    Mafanikio ya mwenzako yawe ni chachu kukusukuma na wewe kufanikiwa zaidi.

    Ni ushauri tu

  • Malengo Yako Yawe Na Ukomo

    Rafiki yangu, moja ya kosa ambalo watu wanafanya kwenye kuweka malengo ni kuyanyima ukomo wa muda. Wanaaweka kama vile wataishi milele na milele. Unapoweka malengo  yako hakikisha kwamba unayapa ukomo wa muda. Yaani kunakuwa na tarehe ya mwisho ya kuyafikia malengo haya. Na hili linapaswa kujionesha kwenye malengo yako unayoyaweka.

    Kwa mfano unaweza kuandika hivi,  kufikia tarehe 31 disemba mwaka huu ninamiliki gari aina XXX ya rangi nyeusi.

  • Sababu 10 kwa nini unapaswa kuanzia chini

    Habari ya leo rafiki yangu mpendwa. Siku ya leo tarehe 11 wakati nafikiria cha kuandika, nimekumbuka nukuu ya John D. Rockefeller.

    September 2024
    M T W T F S S
     1
    2345678
    9101112131415
    16171819202122
    23242526272829
    30  

    Kama ulikuwa hujui John D. Rockefeller alikuwa ni bilionea wa kwanza nchini marekani kufikia kiwango kikubwa. Kwa Afrika Mansa Munsa ndiye baba lao na utajiri wake haujafikiwa na yeyote mpaka leo duniani kote.

    Basi bwana, leo acha niendelee na habari za Rockefeller, siku nyingine tukipata nafasi, tutamwongelea Mansa Musa.

    Sasa Rockefeller siku moja alisema kwamba, wamebarikiwa wale ambao wanaanzia chini na kupambana mpaka kufika juu.

    Rockefeller mwenyewe alikuwa ameanzia chini kabisa, hivyo alikuwa anajua nguvu ya kuanzia chini. Nguvu ya kuanza kidogo Kisha ukakuza hicho kidogo.

    Najua na wewe unataka kufika mbali, Ila utapaswa kufikiria kuhusu kuanzia chini, Kisha kuendeleza kile kidogo mpaka kiwe kikubwa.

    Hiki kitu kikanifanya nikumbuke stori ya kijana mmoja ambaye wakati akiwa chuoni aliona jinsi ambavyo kamera za Kijapani zilikuwa zinatawala soko la Marekani na hivyo kufanya kamera za Kijerumani kutoweka kwenye soko la Marekani. Alijiuliza hivi kama kamera za Kijapani zimeweza kuteka soko la Marekani, sasa haiwezekani kwa viatu vya Kijapani navyo kuchukua nafasi ya viatu vya Kijerumani.

    Ilipofika wakati wa kuwasilisha wasilisho la utafiti wa kuhitimu chuo aliwasilisha mada inayohusiana na hicho kitu, wanafunzi wengi darasani walionesha kutopendezwa na hiyo mada. Profesakwa kumhurumia akaamua kumpitisha kama amefaulu.

    Baada ya chuo jamaa akaona isiwe kesi, akaamua kuomba fedha kwa baba yake ili aweze kuitembea dunia. Akatembea nchi nyingi za Ulaya na hatimaye akafika Japani. Akiwa Japani akaona sasa huu ndio muda muafaka wa kuhakikisha kwamba ninafanya dili ambalo limekuwa kichwani mwangu kwa siku nyingi.

    Dili la kuanza kuuza viatu vya kijapani Marekani. Hivyo, akaanza kutafuta kampuni ambazo zinatengeneza viatu, kampuni ambazo hapo baadaye zitapaswa kumtumia viatu ili awe anauza. Baada ya kwenda huku nakule akawa amekutana na kampuni moja ambayo walikubalina kuwa watamtumia pea kadhaa za viatu kwa dola 50 tu. Jamaa akaomba tena fedha kwa baba yake na kuweka oda ya viatu, kisha akaendelea na safari yake ya kuizunguka dunia. Akazunguka mpaka akafika hapo mjini Nairobi nchini Kenya kisha akarudi kwao.

    Huo ndio ulikuwa mwanzo wa Kampuni ya Nike, na mtu anayeongelewa hapo siyo mwingine bali ni Phil Knights Mwanzilishi wa kampuni hiyo. Mtu huyu alikuwa na maono makubwa ya kufanya viatu vya Kijapani vitawale nchini nmarekani na kuviondoa viatu vya Kijerumani. Aliendelea mbele mpaka hapo baadaye akaja kuanzisha kampuni yake mwenyewe ya kuzalisha viatu.

    Na hili hapa linatupelekea kwenye sababu moja ya msingi ya kwa nini unapaswa kufikiri kikubwa na kuanza kidogo. sababu hii ni kwamba muda mwingine mtu unakuwa na ndoto kubwa ila hauna fedha za kutosha za kukufanya wewe uweze kufanikisha malengo na vitu vikubwa unavyofikiria. Hivyo, kwa kukosa mtaji wa kufanya hivyo, wewe hapo unapaswa kuanza kidogo.

    Sababu ya pili ni ukosefu wa rasilimali muhimu za kukuwezesha wewe hapo kufaya makubwa kwa wakati mmoja ndio maana unapaswa kuanza kutumia rasilimali zilizopo. Ili uweze kufanya makubwa unahitaji rasilimali kama muda wa kutosha, watu, elimu n.k. lakini unakuta kwamba hauna hivi vitu vyote, hivyo unapaswa kuamua kwamba unaenda kuanza kidogo kisha baadaye kukuza rasilimali hizo ili ziweze kuwa kubwa zaidi kadiri unavyokuwa unaendelea na safari.

    Sababu ya tatu ni kuwa wakati mwingine kuanzia juu siyo bora kwa afya yako. Kuna watu wameanzia juu na kujikuta kwamba wamefeli vibaya sana hapo baadaye, hivyo basi badala ya wewe kuja kufeli na kuanguka vibaya hapo baadaye unapaswa kujijengea utaratibu wa kuanza kidogo na kukua kadiri unavyokuwa unaenda.

    Sababu ya nne ni kujiimarisha kadiri unavyokuwa unakua. Kufika kileleni ghafla kunaweza kukufanya upoteze kila kitu na hivyo kukufanya uanze upya. Hata hivyo unapokuwa unatoka chini an kuzidi kupanda juu, ni wazi kuwa utajikuta unaujua mchakato wote unaohitajika ili kukufanya wewe uweze kufika juu na hata ukianguka bado unaweza kusimama.

    Sababu ya tano ni kuwa unapata nafasi ya kufanyia kazi vitu vidogo na kuona vipi vinafanya kazi kwa ubora huku ukiendelea kuboresha bidhaa zako. asilimia kubwa ya kampuni kubwa zote tunazozifahamu siyo kwamba zilianzia hapo zilipo leo. Unakuta kwamba zimeshawahi kujaribu bidhaa mbalimbli kabla ya kufikia zilipo leo hii, hata hivyo katika kujaribu huko ndiko zimekuta kwamba bidhaa fulani zinapendwa zaidi na watu na hivyo kujikita kwenye hizo bidhaa ambazo zinalipa zaidi.

    Mfano, ukifuatilia kampuni kama Toyota, leo hii inafahamika kwa kutengeneza magari ila siyo kwamba kampuni hii ilianzia hapa, kuna sehemu ilianzia, ikajaribu vitu mbalimbali mpaka kuja kufikia hapa ilipo siku ya leo. Kuna kipindi kampuni hii hapa ilikuwa inauza cherehani.

    Kompyuta za kwanza za kampuni ya Apple hazikuwa bora kama hizi tunazoziona leo hii. Ukiaziangalia kompyuta za miaka hiyo ya 80 au 70 ,mwishoni utagundua kwamba zilikuwa siyo nzuri kama hizi tunazozitumia leo hii. Kumbe hawa watu walitengeneza kompyuta za kawida, wakazipeleka sokoni, wakaona jinsi soko lilivyokuwa linafanya kazi na hatimaye sasa wakawa wameweza kuboresha kile walichokuwa wanafanya  na kupata kitu ambacho kilikuwa ni bora zaidi.

    Sita ni kukujengea msimamo binafsi. Hii inatokana na ukweli kwa345tyumba unajiwekea utaratibuw akufanya vitu vidogo kila siku kwa mwendelezo ambao hapo baadaye unakuja kukupa matokeo makubwa.kwa sababu vinakuwa vitu vidogo, basi matokeo yake hayaonekani kwa muda ila mkusanyiko wake baada ya muda unaleta matokeo makubwa. ebu tuchukulie mfano wa watu watatu wenye kipato sawa, wanafanya kazi ileile ofisini kwa muda uleule kwa siku zilezile za kazi. wanapata likizo kipindi kilekile cha mwaka na kipato chao ni kile ni kile. Ila kati ya hao mmoja wao tumwite Baraka, Mwingine tumwite Furaha na mwingine tumwite Busara.

    Sasa watu hawa wakawa na tabia tofauti. Baraka kila anapopata mshahara anaamua kutoa asilimia kumi ya kipato chake na kukiweka kama akiba kisha kutumia kiasi kilichobaki. Kila mwezi anaawekeza kiasi kidogo cha kipato chake kwenye kununua vitabu ambavyo huwa anasoma kurasa kumi kila siku. Huwa anahakikisha kwamba anapata walau wazo moja kwenye kitabu na kisha analifanyia kazi. amejiwekea utaratibu wa kufanya mazoezi kwa dakika chache kila siku. Anapangilia ratiba zake na anahakikisha kwamba ana muda wa familia yake kila siku. Ametenga pia dakika za kufanya tahajudi na hata kuandika mawazo ambayo huwa yanakuja kichwani mwake.

    Kwa upande mwingine Furaha yeye anafanya vitu kama ambavyo mtu mwingine anafanya.

    Wakati, Busara kila mwezi anafanya vitu vya ajabu, mara zamu hii unakuta kanunua runinga, mwezi ujao spika, mwezi mwingine anatumia kiasi kikubwa kwenye michezo ya kubahatisha ili ashinde fedha nyingi. Anatumia muda mwingi kwenye kuangalia runinga na sasa ameanzisha tabia mpya ya kula chipsi mayai na vyakula vingine vitamu kila anapokuwa anaangalia runiga. Watu hawa kwa mara moja huwezi kuona tofauti zao mwanzoni wanapoanza kufanya hivi vitu. Baada ya miezi mitano unaweza pia usione tofauti kubwa miongoni mwa watu hawa. Ila baada miaka miwili, ni wazi kuwa utofauti kati ya hawa watu itakuwa imeanza kuonekana. Baada ya miaka mitano, utofauti wao utakuwa mkubwa. Wengine wanaweza kuanza kukimbilia kurahisha kwa kusema kwamba Baraka ameenda kwa wanganga ila kumbe ukweli ni kwamba, hakuna mganga wala nini? Ni nguvu ya vitu vidogo sasa inaanza kujionesha yenyewe

    Kama umeweza kufanya makubwa ukiwa na rasilimali za kawaida, utaweza kufanya makubwa zaid ukiwa na rasilimali kubwa

    Saba, kukuondolea msongo. Ujue unapokuwa na jukumu kubwa na unaliangalia kwa ukubwa wake unaweza kujikuta kwamba unapata mpaka msongo. Ila ukijua kwamba katika kitu hicho kikubwa unachukua hatua ndogo ndogo hii inaweza kupelekea wewe kupunguza msongo.

    Ebu chukulia umepewa kazi ofisini ila umeiweka na unakuja kuanza kukimbizana nayo siku moja kabla ya siku yenyewe ambapo kazi inahitajika. Ni wazi kuwa siku hiyo utakuwa na msongo wa hali ya juu kwa maana usipokamilisha hiyo kazi siku hiyo, kesho yake utapata taabu sana. Unakuwa na hofu ya kuwa pengine utapoteza kazi yako au kukatwa mshahara. Au unaogopa kuaibika mbele ya rafiki zako wakati unawasilisha hiyo kazi. Kitu hiki kinapelekea wewe kufanya kazi hii hovyo hovyo kabisa. kesho utaenda kazini ukiwa na msongo zaidi maana kazi utakuwa unajua umeifanya chini ya viwango. Utakuwa unahofia bosi wako atasemaje akiona kazi ya hovyo unayoenda kuwasilisha. Kitu hiki ni wazi kuwa kitakunyima amani na kuleta msongo mkuwa. Hali hii itakusababishia  msongo.

    Ila kama kazi hiyo hiyo utaipata na siku hiyo ukaipangia ratiba ya kuanza kuifanya kidogokidogo utajikuta kwamba umeweza kuifanikisha , kiasi kwamba siku ya mwisho hautapata shida ya kukamilisha kazi yako na wala hutakuwa na hofu ya kuwasilisha kazi yako kwa bosi maana utakuwa unajua kwamba kazi yako umeifanya kwa viwango, umeihakiki akuirudia kuhakikisha kuwa kazi ya kimataifa. Kiufupi hautakuwa na msongo wowote.

    Kwa mwanafunzi ambaye yuko shule naye anaweza kuondoa msongo wa kuhakikisha kwamba anajipangia ratiba ya kusoma hata kama hana mtihani. Hii itamwondolea msogo pale mitihani itakapokaribia. Lakini akisubiri mpaka siku ya mwisho ndiyo aje kusoma, ni wazi kuwa atapata taabu sana.

    Nane. Kukujengea nidhamu. Ukifanya vitu vidogo vidogo kwa muda mrefu bila kuacha hata kama ni vidogo, ule mkusanyiko wako utakufanya uonekane kama ni wa kipekee au mtu kutoka dunia nyingine wakati umejijengea nidhamu ya kutoacha tu.

    Tisa, Kukufanya uweze kufikia mambo makubwa

    Kila siku unapoamka asubuhi unakuwa na nafasi ya kuchagua ni kitu gani unaweza kufanya kati ya vitu vingi vinavyokuwepo mbele yako. Unaweza kuamua kuitumia vizuri asubuhi yako ya siku husika au kuitumia vibaya pia. Kwa mfano unaweza kuamka asubuhi na kuwasha runinga hapohapo na kuanza kuwaangalia watu wanaofanya mazoezi huku ukiwahukumu, na hata kuwacheka. Unaweza kusema mbona huyu hapa hafanyi mazoezi inavyostahili, mbona huyu hakimbii, mbona huyu hafanyi hivi, baada ya hapo unaaweza kuamua kuingia mitandaoni na kuanza kufuatilia habari nyepesinyepesi na matukio yanayoendelea, kabla hujajua, zitakuwa zimepita saa tatu mpaka nne, upo mtandaoni tu unatafuta vitu visivyoeleweka. Baada ya hapo unaweza kuanza kuongea kwenye simu na rafiki zako, mkijuliana hali na kuulizana yale yalilyotokea kwenye mechi za jana au wikendi.

    Baada ya hapo utaenda kazini, huku ukiendelea kusikiliza taarifa ya habari na habari nyingine nyepesinyepesi kutoka kwenye vituo vya redio au kupitia mtandaoni. Ukifika kazini utasalimiana na rafiki zako na kuanza kumwongelea rafiki yenu ambaye amepokea fedha zote na kwenda kuhonga badala hata ya kunununua kiwanja. Mpaka hapa utakuwa umechoka, huku ukidonoa kazi kidogo, kidogo.

    Baada ya kazi utarudi nyumbani na kuwahi kijiweni kwanza ili upige soga na awashikaji kisha utarudi nyumbani na kufikia kwenye kochi, ukifungulia runiga na kuendelea kuangalia tamthiliya. Kabla hujajua utajikuta kwamba  hauna tena muda wa kupika chakula, na hivyo moja kwa moja utaagiza chipsi yai ambayo utakula wakati inakusinidiza kuangalia thamthiliya yako, na unakuja kustuka muda ukiwa saa saba za usiku, happo ndiyo unakumbuka kwamba unapaswa kulala. Kesho yake unaamka saa mbili kisha mzunguko unajirudia.

    Hali ni tofauti kwa mtu ambaye anaamka asubuhi na kuanza kupangilia ratiba yake, huku akionesha ni vitu gani ambavyo atafanya na vitu gani ambavyo ataepuka navyo na kisha kuanza kufanyia kazi mpango wake wa siku husika. Jioni anarudi kutokana kazini na kufanya mazoezi, kisha anaanza kusoma vitabu vya kumwongezea maarifa. tofauti kati ya watu hawa wawili ni ndogo sana ila kwa muda mrefu tofauti hii itageuka kuwa tofauti kubwa sana

    Hii ni tofauti ndogo kutoka kw watu

  • Ni ushauri tu-2

    Ule muda unaoutumia kufuatilia maisha ya watu wengine, utumie kufuatilia maisha yako. Jua nini unataka kufanya na kitu gani hutaki kufanya kwenye maiaha yako..

    Jifuatilie uone kama bado unafanyia kazi malengo yako au la umeshaachana nayo.

    Ni ushauri tu.

  • NGUVU YA WAZO: (THE POWER OF AN IDEA):Jinsi Wazo Linavyoweza Kuiongoza Dunia

    NGUVU YA WAZO: (THE POWER OF AN IDEA)

    How An Idea Can Rule The World

    Jinsi Wazo Linavyoweza Kuiongoza Dunia

    Utangulizi

    Ebu ngoja kwanza. Ukiingia kwenye mtandao wa google na kuandika neno idea utapata majibu 4,270,000,000 Ujue sijakosea ni bilioni nne na milioni mia mbili sabini.

    Haya tuachane hilo, ukitafuta neno business idea utapata matokeo ambayo ni sawa 4,020,000,000 (bilioni nne na milioni ishirini) hii ndio sawa na kusema kwamba kuna watu wengi wanapenda kujua kuhusu wazo la biashara. Ukiona kuna watu wameandika kwa wingi kiasi hicho ujue pia kuna watu wengi wanatafuta taarifa hiyo kwa wingi kiasi hicho.

    Maswali ya watu wengi ni wazo gani la biashara naweza kufanya kwa kuanza na mtaji kidogo? Napate wazo la biashara? Nifanye biashara gani na mengine kama hayo.

    Kwenye ebook hii tunaenda kuzungumzia kiundani kuhusu wazo la biashara, tutaona ni wazo gani linakufaa na wazo gani halikufai kwa kuzingatia vigezo na masharti ambavyo vimethibishwa, mwisho wa siku mpaka ebook hii inaisha nina uhakika kwamba utakuwa umejifunza mengi ambayo unaweza kuanza kufanyia kazi.

    Godius Rweyogeza

    Morogoro -Tz

  • Una Uwezo Mkubwa Ndani Yako

    Kwenye Biblia kuna hadithi ya watu watatu waliopewa talanta. Mmoja alipewa tano, wa pili alipewa mbili na mwingine alipewa talanta moja.

    Aliyepewa talanta moja hakuithamini, na wala hakuitumia kufanya kitu chochote cha maana. Binafsi sipo hapa kukwambia hiyo stori, naamimi kuwa utakuwa unaijua vizuri tu, au la utaenda kuisoma baada ya hapa.

    Kitu kikubwa ninachotaka kusema leo ni UKUBWA WA KILE AMBACHO KILA MTU ALIKUWA AMEPEWA. Na ukubwa wa kile ulichonacho wewe.

    Ukijua ukubwa wa talanta moja, utagundua kwamba hata jamaa aliyepewa talanta moja alikuwa amepewa kitu kikubwa sana.

    Kulingana na mtandao wa Wikipedia; talanta moja ni sawa na dola 4080 za Kimarekani ambapo zikiwekwa kwenye fedha za Tanzania ni sawa na shilingi milioni tisa na laki nne, sitini na nane elfu.

    Kumbe talanta moja hakikuwa kitu kidogo, kama kinavyoelezwa…
    Kama ni mtaji basi jamaa alikuwa amepewa mtaji mkubwa tu. Japo jamaa hakuitumia…..
    Najaribu tu kufikiri, wewe ukipata hata hako ka talanta kamoja, yaani ukipewa shilingi milioni tisa keshi…Hivi wewe ninavyokujua kweli utatulia…..

    Hiki kitu kitupe funzo kubwa kwenye maisha yetu ya kila siku.

    Kuna uwezo mkubwa tulio nao ndani yetu, tuutumie vizuri.  Usipoutumia uwezo wako vizuri, utaishia kulalamika kuwa hukupewa kitu …

    Kumbe huyu jamaa wa talanta moja alipewa kitu kikubwa ila sasa hakukitumia… Sawasawa na wewe, una kitu kikubwa ndani yako, swali je, unakitumia??

    Kuna watu wengi ambao huwa nakutana nao wakilalamika kuhusu maisha. Mfano, unaweza kukuta mtu analalamika kuhusu mtaji, lakini ukifuatilia kiuhalisia huyu mtu shida yake siyo mtaji.

    Shida yake ni kwamba hathamini like kidogo alichonacho. Haamini kwamba hicho kidogo, kinaweza kugeuzwa na kukuzwa mpaka kikawa kikubwa.

    Ebu fikiria kitu kama mbegu ya mhindi. Najua nikisema hii mbegu watu wengi watanielewa kuliko nikisema mbegu ya haladali 😂😂…

    Ukipanda mbegu moja ya mhindi. Ikiota haitoi tunda lenye mhindi mmoja. Inatoa gunzi lenye mahindi ya kutosha. Yale mahindi ukiyapanda, hayatoki yenyewe kama yenyewe yanatoka na mahindi mengine zaidi….

    Kwa hiyo ukianza Januari mosi na mbegu moja. Ukaipanda ukaipalilia, na kuimwagilia na baadaye kuvuna…

    Halafu ukapanda tena zile mbegu ulizovuna na kurudia mchakato.

    Mpaka unafikia disemba 31… Mbegu moja, ina uwezo wa kuwa imezalisha magunia ya kutosha….

    Lakini ukiidharau hiyo mbegu moja, yenyewe itaishia kuharibika…

    Hiki kitu kihusishe na uwezo wako…
    Uwezo wako unaweza kuwa unaudharau kuwa ni kidogo, ila ukianza kuutumia. Uwezo huu utashangaa kwamba uwezo huu unazidi kukua na kuongezeka na hata unakufikisha mbali…..

    Wachungaji wakiwa wanahubiri, wakiongea pointi, huwa unasikia wanasema. Naamimi naongea na mtu hapa….

    Sasa na mimi naamimi naongea na mtu 😂😂

    Mpaka wakati mwingine
    Mimi ni Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE
    0755748391
    Morogoro-Tz

  • Njia Bora Ya Kukusaidia Kuishi Maisha Yako Kikamilifu

    Unaendeleaje upande wa huko.  Mimi naendelea vyema kabisa.
    Leo ni jumapili ya tarehe 10.  Siku 100 za kwanza za mwaka huu zimeisha. Na Sasa zimebaki siku 265.

    Najua tangu mwaka huu umeanza lazima Kuna kitu uliazimia kuwa utakifanyia kazi. Sasa swali langu kwako, ni je, bado hiki kitu unakifanyia kazi, au ndio tayari umekata tamaa?

    Ninachotaka kukwambia ni kwamba, bado nafasi ya wewe kufanya makubwa ipo. Siku 265 zilizobaki ukizitumia vizuri, una nafasi ya kufanya makubwa.

    Ndio maana leo nimeona nikushirikishe wewe mbinu ya kukusaidia  kuishi maisha yako kikamilifu

    Njia hii ni wewe kuhakikisha kwamba unaweka nguvu zako kwenye malengo uliyonayo. Malengo yako uyape kipaumbele.

    Achana na kufuatilia maisha ya watu wengine Kama vile ndiyi kazi uliyozaliwa kufanya. Badala yake malengo yako yawe ndio kipaumbele.

    Malengo yako yakiwa kipaumbele haya hapa ndio yatatokea.

    Kwanza, utakuwa bize na maisha yako.
    Pili, utajisukuma kuweza kwenda mbali na kufanya makubwa kuliko ulivyozoea
    Tatu, utajifunza  zaidi na zaidi kuhusiana na malengo yako.

    Vitu hivi tu, vitakusaidia kuendelea kuyafanyia kazi malengo yako kwa ufanisi zaidi.

    Sasa rafiki yangu, kazi yako ya leo. Angalia vitu vyote vilivyokuzunguka na ambavyo vinakunyima wewe nafasi ya kufanikisha malengo yako. Viweke pembeni, Kisha weka juhudi na bidii zaidi kwenye kufanyia kazi malengo yako

  • Hiki Ni kitu muhimu ambacho unapaswa kukitafuta kwenye kila kitabu

    Rafiki yangu usomaji wa vitabu ni kitu muhimu sana kwa ajili ya afya ya akili yako.

    Ukitaka kufurahia usomaji wa vitabu basi kwenye kila kitabu ambacho unasoma hakikisha unapata unapata vitu vitatu ambavyo unaweza kufanyia kazi Mara moja.

    Ukipata vitu hivi mwanzoni mwa kitabu, unaweza kuweka kitabu pembeni kwanza na kufanyia kazi kile ulichojifunza utakuja kuendelea nacho siku nyingine.

    Kwa hiyo rafiki yangu. Kama kwenye kila kitabu chako. Unachosoma tafadhali sana tafuta vitu vitatu vya kufanyia kazi Mara moja.

    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • Jinsi ya kuendeleza kipaji chako

    Habari ya leo rafiki yangu. Hongera sana kwa siku ya leo na siku ya kipekee sana.

    Leo nataka nikueleze namna ambavyo unaweza kuendeleza kipaji chako kwa viwango vikubwa mpaka kufikia hatua za kukifanya kikutoe. 

    Lakini kwanza tujiulize kipaji ni nini?
    Kujibu swali la kipaji ni nini naomba usome makala hii hapa ambayo imeeleza kwa kina kuhusu kipaji. Au pia unaweza kusoma Makala hii hapa.

    Sasa baada ya kujua kipaji ni nini tuone unawezaje kukiendeleza.

    Zipo njia kadhaa  Ila njia ya kwanza ni kutenga muda wa kukifanyia kazi kipaji chako kila siku.

    Unaweza kutenga hata nusu saa tu kwa ajili ya kunoa kipaji chako.

    Pili ni kufanya mazoezi endelevu. Ni kweli umetenga muda maalumu kwa ajili ya kipaji chako. Lakini fahamu kuwa hilo peke yake halitoshi. Na hapo ndipo wewe unahitaji kuwa na nidhamu ya kufanya kitu ulichopanga bila kukosa.

    Tatu, kwenye ulimwengu wa sasa mambo mengi ya yamehamia mtandaoni. Hivyo, na wewe kiweke kipaji chako mtandaoni.
    Fungua akaunti kwenye mojawapo ya mitandao ya kijamii.
    Tengeneza blogu
    Fungua akaunti Google my business.

    Yaani, kiufupi weka urahisi wa watu kukupata wanapokuwa wanaokihitaji uwasaidie na kipaji chako.

    Kila la kheri
    Godius Rweyongeza
    0754848391

X