-
NGUVU YA KUWEKA MALENGO

Umewahi kujiuliza malengo yanaweza kuwa na nguvu gani kwenye maisha yako. Kama ulikuwa hujui ni kwamba malengo ni kama petroli kwenye moto.
unajua ukiweka moto kwenye petroli ni kitu gani ambacho kinaenda kutokea…Moto utawaka zaidi, si ndio…
malengo na yenyewe yako hivyohivyo. Ukiweka malengo, yatakusukuma kufanya makubwa zaidi
karibu sana ujipatie ebook ya kipekee ya nguvu ya malengo. Itakusaidia wewe kujua namna nzuri na ya kipekee ya kuweka malengo, namna ya kuyafanyia kazi malengo yako mpaka yakatimia, lakini pia utapata mwongozo wa kukusaidia wewe kuendelea kuyafanyia kazi malengo yako. Je, upo tayari?
Karibu
-
Mipango yangu ya miaka 100 ijayo

Nilipokuwa mdogo, nilikuwa napenda sana kusikiliza redio. Kila siku SAA kumi na mbili asubuhi ilikuwa lazima nisikilize DW habari za ulimwengu. Mchana na jioni ilikuwa hivyo hivyo, yaani, ilikuwa kama dozi .
Siku moja wakati nasikiliza habari, walitangaza kwamba kufikia mwaka 2050 kuna viumbe watakuwa wamepotea na kutoweka kwenye uso wa dunia.
Watu niliokuwa nao walianza kulalamika. Kila mtu alishangaa kuona ni kwa nini wanazungumzia mambo ya mwaka 2050 sasa. Wakati bado kuna muda mwingi sana. Rafiki yangu mmoja alithubutu kusema ni uongo. Huku mwingine akisema wazungu wanapoteza sana muda.
Hali hii inaweza kukupa picha ni kwa jinsi gani watu hawataki kuangalia mbeleni. Ni kwa jinsi gani watu hawana mipango ya mbeleni.
Labda nikuulize wewe unataka uwe umefikia Nini mpaka mwaka 2050?
Najua..
Najua..
Najua utaniambia umri wangu umeenda kwa hiyo 2050 ni mbali. Sawa, na mimi nakubaliana na wewe.
Ila vipi una mpango wa hata wa miaka 10 au mitano? Au na penyewe ni mbali?
Andika Malengo yako ya miaka 1/2/3/5/10/25.
Watu wengi wanaamini katika msemo unaosema leo ni leo asemaye kesho ni mwongo. Hali hii imewafanya watu wengi kusitasita kuweka mipango yao ya muda mrefu. Hivyo kuamini kwamba kila wanachopata sasa ni kwa ajili ya sasa na kesho itajipa yenyewe. Hali hii itakunyima motisha ya kusonga mbele na kufanya mambo makubwa.
Mara zote na siku zote unapaswa kuwa na mpango na ndoto za muda mrefu.
Unapaswa kupanga kama vile utaishi milele na kufanyia mipango yako leo kama vile utakufa kesho.
Siku siyo nyingi nilikuwa nasoma wasifu wa Jack Ma. Unaitwa Alibaba: The House That Jack Ma Built.
Ndani yake mwandishi anasema kwamba wakati Jack Ma anaanzisha kampuni ya ALIBABA alikuwa na mpango wa kufanya kampuni hiyo idumu kwa miaka 102.
Miaka 102 ni mingi, wachache sana wanaishi hiyo miaka.
Ila jamaa alianzisha kampuni yake na huo mpango.
Kampuni ya Alibaba ilianzishwa mwaka 1999 na Jack Ma alikuwa tayari na miaka 36. Maana yake tunapozungumzia miaka 102 baada ya hiyo kampuni kuanzishwa, tunaiongelea miaka ya 2101!!!!!!
Sidhani kama Jack Ma atakuwa bado anaishi, Ila huyu jamaa ana maono makubwa ya kufikiri mpaka huko atakapokuwa ameshaaga dunia ..
Hii ndio nguvu ya maono, MTU mwenye maono ya mpaka mwaka 2101. Siyo sawa na mtu mwenye lengo la kulala leo na kuamka kesho akaonane na mchepuko wake!
Na wewe kuanzia Leo weka maono ya muda mrefu. Unaweza usiwe hai hiyo miaka. Lakini maono yako hayatakufa. Ndio maana tunapaswa kufanya vitu kwa kuwafirikia hata wanetu…ili waweze kuwa waendelezaji wa vitu tulivyoanzisha. Tunaoneahe runavyofanya ili na waweze kuwa waendelezaji wa kile tunachofanya…
NB. Kama bado hujapata nakala ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI, fanya hivyo leo. Nakala ngumu ni 20,000
Nakala laini ni 10,000 tu.
-
Email List Ni Nini?
Jana niliandika hapa JINSI YA KUANZISHA BLOG. Kuna watu tayari wamesoma hiyo Makala na kuifanyia kaI. Sasa leo nilikuwa nikiwaambia wafungue email list kupitia MailChimp.com
Ila swali lilikuwa email list nini? Kujibu Hilo swali naomba usome hapa chini
Email list ni mfumo wa kukusanya mawasiliano ya watu wanaofuatilia kazi zako. Ambapo kila anayesoma na kupenda Makala zako, anaweza kukuachia email take na wewe ukaendelea kuwasiliana naye kwa kumtumia Makala zaidi kwenye email yake moja kwa moja.
Kuna sababu nyingi kwa Nini unapaswa kuwa na email list Ila hapa sitazitaja zote
- Siyo kila mtu anayetembelea blog yako leo, ataendelea kuitembelea kila siku. Baadhi ya watu watakuja kwenye blogu yako kwa shida maalumu, wakishasoma kitu chako, wataondoka na kukusahau. Ila endapo huhu mtu atakuwa amekuachia email yake. Ni rahisi kwako kuwasiliana naye kwa baadaye kwa njia ya baruapepe na kumfanya aendelee kufuatilia kazi zako zaidi.
- Lakini pia email list inakusaidia kuanza kutengeneza jumuiya ya watu wanaokuamini zaidi, ili ikifikia hatua ambapo wewe utakuwa na bidhaa, hawa watu ndio watakuwa wa kwanza kununua kwako
-
Jinsi Nilivyoandika Kitabu Kilichosomwa Sana Kuliko Vitabu Vyote Tanzania
Nakumbuka mwaka 2019 kulikuwa na kijitabu kidogo hivi kilikuwa kinazunguka mtandaoni. Kijitabu hiki kilikuwa kinajulikana kama Baharia.
Kilikuwa kinazungumzia mambo kadha wa kadha ambayo baharia anafanya.
Kijitabu hiki kilizunguka sana, sana. Binafsi sikukisoma, Ila watu wengi ninaowafahamu mimi walikisoma hicho kijitabu. Kwa hiyo mada yao kubwa kwenye mazungumzo ikawa imekuwa BAHARIA.
Yaani, ulikuwa huwezi kupitisha nusu saa bila kusikia mtu akisema kuhusu Baharia.
Kwa sababu nilikuwa nimezungukwa na watu wengi waliosoma kijitabu kwa wakati huo, nikipata kujua kuhusu uwepo wa kijitabu hicho. Na hata baadhi ya vitu kwenye kijitabu hicho nilisikia watu wakiviongelea…
Wewe vipi ulikisoma?
Kama nakuona vilee….
Sasa katika kipindi hiki nilikaa nikajiuliza. Kama hiki kijitabu (ambacho mimi niliona hakina ujumbe wa maana) kinaweza kusomwa hivi, basi na Mimi naweza kukaa chini, nikaandika kitu cha maana kikasomwa na kusambaa sana kama hiki kijitabu….
Nilitafakari sana hili…
Ila sikujua niandike nini… Nilikuwa najiuliza hivi hiki kijitabu kina sifa gani ambazo zimekifanya kisomwe Sana.Baada ya siku chache nikaamua kuandika kitabu kuhusu usomaji wa vitabu.
Kitabu hiki nilishaanza kukiandika muda kabla hata kusikia habari za BAHARIA. Ila nilikuwa nakiandika kwa mfumo wa hadithi. Na baadaye ile hadithi ilipotea nikiwa katikati baada ya kupoteza simu yangu..
Baada ya tafakari ya kina, nikaamua kurudia kuandika kitabu hiki, Ila zamu hii sikutaka kuandika hadithi kama ilivyokuwa mwanzoni.
Nikaanza kuandika. Sikumbuki nilitumia muda kiasi gani kuandika hiki kitabu, Ila nadhani nilikiandika siku za wikendi kikakamilika.
Nikakitengeneza vizuri, halafu nikamfuata mshikaji wangu Magambo kumpasha habari. Nikampa nakala aisome,
Wakati nasubiri mrejesho wake nikaamua kuwa kitabu kile nikitoe na nikigawe bure, Kama ambavyo nilikuwa nimepanga tangu mwanzo
Kilichotokea ni historia.
Kitabu hiki ambacho mwanzoni kilikuwa kinajulikana kama MAAJABU YA VITABU, na Sasa hivi kinaitwa MAAJABU YA KUSOMA VITABU kimesomwa na watu wengi tangu hiyo Septemba 2019.
Kimezungumzia kuhusu usomaji wa vitabu tu! Na kimekuwa kikitolewa bure tangu 2019 mpaka leo hii.
Kiukweli wengi wamekisoma, na sasa nina toleo la 2 kitabu hiki. Pamoja na marekebisho yake.Wewe pia unaweza kupata zawadi ya nakala yako HAPA CHINI
Mpaka sasa kitabu hiki, kimekuwa kuwa mwongozo wa usomaji wa vitabu kwa watu wengi. Lakini kwa watu ambao hawajawahi kusoma kitabu changu chochote, huwa nawashauri waanze na hiki cha bure, halafu ndio waje kununua.
Wewe pia Anza na hiki Cha bure
Halafu baada ya hapo, njoo upate ebooks mbili kwa ofa ya pasaka. Ebooks hizi ni
MAISHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE pamoja naVyote hivi viwili utavipata kwa bei ya 8,000/- tu badala ya bei yake halisi. Tuma fedha kwa 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA
Orodha ya vitabu vyangu yote hii hapa
Ni mimi rafiki yako
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz -
JINSI YA KUANZISHA BLOG
Habari ya leo rafiki yangu. Siku ya leo ningependa kukuelezea ni kwa namna gani unaweza kufungua blog.

Kwanza labda nianze kwa kusema kwamba ulimwengu wa sasa hivi umebadilika. Kwenye ulimwengu wa leo mtu anapokuwa na wazo, au dukuduku sehemu ya kwanza kabisa anapokimbilia ni mtandaoni kutafuta kitu hicho.
Hiki kitu kimejenga utagemezi kwa watu, maana watu hawawezi kuishi tena bila mtandao. Na hizi taarifa za mtandaoni ambazo tunatafuta kila siku, zinawekwa na watu. Hazishuki kutoka mbinguni na wala haziwekwi na roboti (japo zipo baadhi zinazowekwa na roboti)
Usije ukafiri kwamba kuna watu wa aina fulani tu, ambao ndio wamebarikiwa kuweka vitu mtandaoni, na wengine hawajabarikiwa. Unachopaswa kufahamu ni kuwa, kila mtu kabarikiwa kwa namna yake.
Kwa hiyo na wewe huwezi kukosa kitu cha kuweka mtandaoni.Ni sifa gani napaswa kuwa nazo ili kiandike na kuweka vitu vyangu mtandaoni?
Kama wewe una ujuzi fulani, basi ujue kabisa kuwa una sifa za kukuwezesha kuweka vitu mtandaoni.
Kama wewe unapenda kufuatilia baadhi ya vitu kwa kina, labda kufanya utafiti au kujifunza. Ujue kabisa kuwa una sifa za kukuwezesha vitu mtandaoni.
Kwa hiyo kiufupi, elimu yako, ujuzi wako, udadisi wako, Ubunifu wako, kipaji chako, n.k. vinapaswa kuwekwa mtandaoni.
Je, niweke vitu vyangu mtandaoni kwa njia gani?
Mtandao umekuja na fursa nyingi. Unaweza kutumia njia ya sauti kufikisha ujumbe wako (podcast)
Unaweza kutumia njia ya video kufikisha ujumbe wako
Unaweza kutumia njia ya maandishi (Makala)
Unaweza kutumia njia ya michoro na picha
Furaha unayoipata kwa kujua kuwa na wewe unaweza kuweka vitu vyako mtandaoni
Kwa hiyo njia zipo nyingi, nyingi sana.
Ni eneo gani sasa naweza kuweka kitu changu nilichoandaa?
Kwanza kabisa ningependa ufahamu maeneo matano ambayo watanzania wanapenda kutembelea. Yaani, mitandao maarufu hala nchini. Hizi takwimu zinatolewa na mtandao wa Alexa na zinaweza kukusaidia kujua wapi walipo watanzania wengi ili uwawekee vitu vyako huko.Mtandao wa kwanza kwa kutembelewa ni GOOGLE
Wa pili ni YOUTUBE
Wa Tatu ni Facebook
Wa nne
Na wa tanoOrodha ya mitandao mingine inayitembelewa zaidi unaweza kuiona hapa chini kwenye picha

Mitandao inayotembelewa zaidi nchini Tanzania Imekuwepo mitandao ya kijamii kadha wa kadha ambayo watu wamekuwa wakiikimbikia na kuitumia kama Facebook, twitter, Instagram. Hii mitandao iko vizuri na imerahisisha Mambo mengi linapokuja suala zima la mawasiliano.
Ila kama una mpango wa kuweka mawazo yako mtandaoni katika namna ambayo itadumu kwa kipindi kirefu. Basi hii mitandao ya kijamii haifai. Mitandao ya kijamii ina watu ambao wanaweza kusoma au kufuatilia kazi zako. Ila kudumu ya wewe kuweka taairfa zako.
Kwa sababu mitandao hii ina tabia ya kupoteza baadhi ya kumbukumbu. Leo hii nilimwambia unioneshe kitu ulichoweka mtandaoni mwaka 2017. Huwezi kukiona, ukiniuliza Mimi kwamba nikuoneshe kitu nikichoweka kwenye blog mwaka 2017, nakwambia BONYEZA HAPALakini pia mpangilio wake ni ule ambao unatoa taarifa mpya kwanza huku za zamani zikiwa hazipewi kipaumbele. Breaking news, ndizo zinakaa juu.
Na umiliki mtandao uko wa MTU mwingine. Wewe unaysoma hapa najua haumiliki twitter labda kama wewe ni Elon Musk,
Haumiliki Facebook wala WhatsApp labda kama wewe ni Mark Zuck.Ndio maana unahitaji kuwa na kitu Cha kwako, nafasi yako mtandaoni ambayo unazomi Na sehemu ya kuanzia ni kwenye blog.
JINSI YA KUTENGENEZA BLOGU
Kuna aina mbili za blogu. Blogu za bure na za kulipia.
Blogu za bure pia zipo za aina mbili
- WordPress (mfano wa blogu hii unaweza kuwa ni (jinalako.wordpresa.com)
- Blogger mfano wa blogu ya Aina hii, unaweza kuwa ni (jinalako.blogspot.com)
- Blog za bure, hauzimiliki wewe moja kwa moja. Zinakuwa chini ya kampuni uliyofungulia, na waweza kuifunga muda wowote wakitaka. Ila kwa mtu yeyote anayeanza, anaweza kuanza na blogu za bure.
Blog za kulipia kwa upande mwingine zinakuhitaji utoe fedha mfukoni ili kutengeneza blog. Na ukishaitengwneza inakuwa ya kwako na wewe ndiye unakuwa mmiliki halali. Yaani, tuseme unakuwa na sehemu yako mtandaoni. Kaa ambavyo google wana sehemu yao au Facebook wana sehemu yao.
Na wewe utakuwa na sehemu yako mfano jinnalako.com au jinalako.co.tz
Mpaka haponina uhakika utakuwa umepata kujifunza mengi. Kama utataka kufungua blogu ya bure Basi tembelea
ukikwama utaniambia
Ni mimi rafiki yako
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz -
Ni Nani Huyu Anaenda Kukupigia Push-Up?
Hakuna mtu ambaye anaenda kupambana kwa ajili yako. Kufanya kazi ambazo unapaswa kufanya, kufikia mafanikio ambayo unataka wewe.
Hakuna mtu wa aina hiyo.

Wewe mwenyewe ndiye unapaswa kupambana kwa ajili yako, mwenyewe.
Jua malengo ambayo unapaswa kuyafanyia kazi.
Kisha yafanyie kazi bila ya kuchoka.Maisha haya ni mafupi na siyo ya kupoteza.
Yatumie vizuri kupambana kwa ajili ya ndoto zako.
Ni jana tu niliokupa ofa ya kupata vitabu vyangu viwili kwa bei ya ofa. Vitabu vyenyewe ni kitabu cha
MAISHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE pamoja na kitabu cha
AKILI YA DIAMOND: Mambo 50 Ya Kujifunza Kutoka Kwa Diamond Platnumz Kuhusu Kipaji, Ubunifu Na Mafanikio.Gharama ya vitabu hivi vyote viwili Ni zaidi ya 25,000. Ila leo nataka nikupe ebooks zake kwa 8,000/- tu.
Upo tayari? Lipia sasa hivi nikutumie ebooks hizi za kipekee sasa.
Kumbuka: Ebook hizi utazipata kwa 8,000/- tu badala ya 25,000+
Ni mimi rafiki yako
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz -
UKIANGUKA SIMAMA TENA
Usijivunie kuwa hujawahi kushindwa, bali jivunie kuwa ulisimama tena baada ya kuwa umeanguka-Ralph Waldo Emerson
Ni vibaya kushindwa, ila ni vibaya kama hujwahi kujaribu na kushindwa-Theodore Roosevelt
Mtu pekee ambaye hajawahi kufanya makosa ni yule ambaye hajawahi kufanya chochote-Theodore Roosevelt
Sikushindwa mara 10,000 bali nilijifunza njia 10,000 za kufanya kitu kwa usahihi-Thomas Edison
Mambo yakienda vibaya, yaache yaende peke yake-
Mtu aliyeshindwa kuliko wote ni yule ambaye hajawahi kujaribu kitu-Dr. Larry Kimsey
Ili mtoto aweze kutembea vizuri na kuwa mbobevu, basi anapaswa kuanza kwa kuanguka na kusimama tena na kuanguka tena. Hakuna mtu ambaye huwa anamcheka mtoto kwa sababu ameanguka chini wakati akijaribu kutembea. Kila mtu huwa anafurahia kwamba mtoto huyu ameweza kujaribu kutembea, japo ameanguka. Hiyo ni ishara kwamba huyu mtoto ana uhai ndani yake.
Ila mtoto ambaye hata haoneshi dalili za kutembea ni wazi kuwa anawatia mashaka wazazi wake. Sasa hili linapaswa pia kuwa kwako.
Ukiona kwamba hauna changamoto wala hujashindwa kwa lolote, basi fahamu kuwa kuna sehemu unakosea. Kuna hatua hauchukui. Kufanikisha ndoto zako sio kitu rahisi.
Kuna mtu mmoja aliwahi kunukuliwa akisema kwamba; nilipogundua kwamba katika vitu tisa ninavyofanya ninafanikisha kitu kimoja tu, basi niliongeza juhudi katika vile vitu ambavyo nilikuwa nafanya.
Pengine na wewe unaweza kukuta kwamba unapaswa kufanya vitu mara kumi ili kufanikiwa kwa kishindo mara moja. Usichoke kuinuka hata baada ya kuanguka na kuendelea mbele.
Kitu pekee unachopaswa kuondoka nacho kwenye kuanguka kwako ni somo la kufanyia kazi. Kumbuka kwamba kushindwa sio mwisho wa safari bali unakuwa unajifunza njia sahihi za kufanikisha hicho kitu. Mafanikio ni asilimia 1 ya kushindwa ambako ni asilimia 99, kama alivyowahi kusema Thomas Edison mgunduzi wa karne ya 21.
Sasa inashangaza kwenye maisha ya kila siku kwamba kuna watu ambao wanaogopa kuanguka na hivyo kuficha makosa ili wasionekane kwamba walishindwa au kuna wakati walifanya uamuzi mbovu. Hata ukiangalia wasifu wa watu mbalimbali, huwa ni wasifu chanya wakionesha vitu ambavyo watu hao wameweza kufanikisha na kufanya kwa ubora na huku wakiepuka kutaja vile vitu ambavyo walifanya hovyo. Ila ukweli ni kuwa hata kwa vile vitu ambavyo huwa unafanya hovyo, huwa kuna kitu cha kujifunza na kuchukua hatua.
Hivyo, ukianguka au ukifanya kitu hovyo, usianze kutafuta sehemu ya kujificha ili usionekane. Badala yake jiulize ni kitu gani ambacho umejifunza kutokana na kuanguka huko, kitu ambacho kitakusaidia wewe kusonga mbele na kufanya mambo mengine makubwa zaidi. Ukijifunza kutokana na kushindwa kwako unakuwa hujashindwa. Kitu kingine unachopaswa kufahamu ni kuwa kushindwa ni tukio ila sio wewe. Pia, unapaswa kufahamu kuwa kuna watu wengi ambao hata hawajajaribu kufanya hicho ulichoshindwa.
Baba mkubwa wangu aligombea udiwani 2010 akashindwa, aligombea tena 2015 akashindwa, alirudia tena 2020 na kushindwa. Watu wengi walikuwa wanamcheka na kusema kwamba anapoteza muda na fedha zake. Hata hivyo, nilikuja kugundua kuwa asilimia kubwa ya watu waliokuwa wanamcheka kuwa ameshindwa na anapoteza fedha zake hawakuwa watu ambao wangeweza kuchukua hatua kama zake. Hivyo, kwangu alikuwa mshindi mara mia zaidi ukilinganisha na hawa watu waliokuwa wanakaa vjiweni kumbeza.
-
Maisha Ni Fursa: Zitumie ZIKUBEBE


Unaendeleaje rafiki yangu wa ukweli. Jana nilikutana na kichekesho fulani hivi mtandaoni. Jamaa mmoja alikuwa akizungumzia kuhusu mfumuko wa bei unayoendelea Sasa hivi.
Hivyo akawa amesema maneno haya:
Jamani jamani, mtuonee huruma mnapandisha vitu mno. Mafuta mnapandisha, gesi mmepandisha, uchumi mmepandisha, mtapandisha hadi mapepo……..
Baada ya kuangalia hiki kichekesho, nilijiuliza hivi Kuna fursa yotote kwenye mfumuko huu wa bei. Kuna fursa yotote hapa?
Nikakumbuka kitabu changu cha MAISHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE nilichoandika miezi kadhaa nyuma.
Nikaona kweli hapa Kuna fursa…Na hiki kitu ndiyo kimenifanya nikutumie ujumbe sasa hivi …….Nataka nikwambie kwamba MAISHA NI FURSA, ZITUMIE ZIKUBEBE. Na kwa sababu hiyo nataka nikupe ofa ya kupata kitabu hiki.
Kwa kawaida kitabu hiki kinauzwa kwa gharama ya 10,000 (ebook).Sasa wewe utalipia 8,000 tu. Lakini siyo tu kwamba utapata ebook ya kitabu hiki peke take.Bali pia nitakutumia na ebook ya AKILI YA DIAMOND: E-BOOK hii imezungumzia MAMBO 50 YA KUJIFUNZA KUTOKA KWA DIAMOND PLATNUMZ KUHUSU KIPAJI, UBUNIFU na MAFANIKIO.
Kina Mambo 50 tu, ila ni Mambo konki!
Kwa hiyo kwa elfu 8 unaenda kupata ebook hizi mbili za kipekee
MAISHA NI FURSA ZITUMIE ZIKUBEBE pamoja na
AKILI YA DIAMOND: Mambo 50 Ya kujifunza kutoka kwa Diamond Platnumz kuhusu Kipaji Ubunifu na Mafanikio.
Amua sasa kupata ebook hizi mbili za kipekee kwa bei ya ofa ambayo haitajirudia tena. Utatuma fedha kwa 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA, halafu utanitaarifu kwa namba hiyohiyo.
-
Zawadi Yako Kama Hutakata Tamaa
Rafiki yangu, unapofanya kitu kikaenda ndivyo sivyo, usikate tamaa.Kwa sababu kadiri unavyokosea ndivyo unazidi kuwa imara zaidi.
Makosa ni mwalimu mzuri kama utayatumia vizuri. Ndio maana wahenga wetu wanasema kufanya kosa siyo kosa. Kosa ni kurudia kosa.
Ukirudia kosa maana yake hukukifunza chochote na wala hukupata funzo lolote kutokana na kosa la kwanza.
Na ukiendele kurudia kosa lilelile kila Mara, huwezi kupiga hatua kubwa kimaisha.
Sasa labda nikuulize wewe makosa ambayo huwa yanatokea kila siku kwenye maisha yako, huwa yanakuimarisha au huwa yanakubomoa?
-
Wazo Bora La Biashara
Najua kila mtu anapenda kupata wazo zuri la biashara. Ukweli ni kwamba WAZO ZURI LA BIASHARA NI LILE AMBALO UNAWEZA KUFANYIA KAZI KWA SIKU 365 BILA KUCHOKA. Usipolifanyia kazi wazo lako, ujue utalinyima uhai.
Ebu fikiria mtu ana wazo la kuchonga sanamu fulani, halafu hilo wazo akakaa nalo kichwani mwake.
Unadhani wewe utaiona hiyo sanamu? Jibu ni hapana, kwa sababu sanamu hiyo haijachongwa. Kuchonga sanamu ni kuipa uhai, na hivyo kuifanya ionekane kwa watu wengine. Raha ya wazo sharti ulifanyie kazi na kufanyia kazi wazo lako.
unafanya wazo liwe bora.
Najua kitu hiki kinaweza kukushangaza kutokana na ukweli kuwa umeaminishwa kuwa wazo zuri la biashara ni lile ambalo linalipa. Labda nikuulize kuwa unajuaje wazo linalolipa na ambalo halilipi? Kwa hapa unaweza kujitetea na kusema wazo la kuanzisha mtandao kama Google, Facebook, au wazo la kutengeneza simu janja ni wazo ambalo lilikuwa linalipa pia. Ukweli ni kuwa mawazo haya yote yalikuwa hayana maana yoyote. Ni mpaka pale yalipofanyiwa kazi.
Steve Jobs aliifanyia kazi iPhone kwa zaidi ya miaka miwili na nusu kabla haijaonekana kwenye uhalisia. Wazo la kuanzisha facebook halikuwa hata wazo bora, ni mpaka pale lilipofanyiwa kazi.
Wazo la kuanzisha kampuni ya cocacola pia siyo kwamba lilikuwa ni wazo bora, ni mpaka pale lilipofanyiwa kazi. Sasa wewe kama huwezi kufanyia kazi wazo lako kwa siku 365 zijazo tu.
Linaweza lisije kuleta manufaa yoyote maishani. Utaaishia kufa nalo na kwenda kujaza makaburi na wazo lako zuri. Kitu kikubwa cha kuondoka nacho kwenye kipengele hiki ni kwamba unapaswa kuanza kufanyia kazi wazo lako, tena unapaswa kuanza kulifanyia kazi leo hii. Kila la kheri