-
Hiki Kitu Ndicho Chanzo Cha Mafanikio Yote
Mwaka 1937 ni mwaka muhimu sana kwenye ulimwengu wa mafanikio. Ni mwaka ambao kitabu cha THINK AND GROW RICH kilichapwa baada ya miaka mingi ya utafiti.
Kwenye kitabu hiki mwandishi ameeleza mbinu za mafanikio ambazo ziliwapa utajiri mkubwa sana matajiri wa wakati huo. Hapa wanaongelewa watu kama kama akina Rockefeller ambaye mpaka leo hii amebaki kuwa miongoni mwa matajiri wakubwa kuwahi kutokea.
Kutokea hapo kitabu hicho kimetengeneza matajiri wengi sana, na kimewasaidia wengi kufika mbali.
Kitabu kimeeleza hatua 13 za kufikia mafanikio makubwa. Mwandishi anasema unapaswa kuwa na
1. Shauku ya kufanikiwa
2. Unapaswa kuwa na imani
3. Unapaswa kujinenea maneno chanya
4. Unapaswa kuwa na elimu/maarifa sahihi
5. Unapaswa kuwa mvumilivu
6. Unapaswa kuungana na timu ya watu sahihi na mengineyo.Ila sasa kuwa na hayo yote haitoshi. Hapo ndipo mwandishi anakwambia kwamba; chanzo cha mafanikio yoyote kipo kwenye WAZO. Ukishakuwa na wazo ndipo sasa utaliunganisha na shauku yako ya kufanikiwa. Ndipo utapaswa kuwa na imani kuwa utakifanikisha.
Hapo ndipo utapaswa pia kujinenea maneno chanya na mengineyo.
Kwa hiyo, kama unataka kufanikiwa Anza kwa kujiuliza hivi mimi nina wazo gani haswa la kunisaidia kufanikiwa? Kama huna wazo jifikirie tena.
Wazo lako ndio chanzo kikuu cha kupata mafanikio unayotaka.
PATA KITABU CHA BURE
Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli
Godius Rweyongeza
+255755848391/ Morogoro-Tanzania
-
Hatua muhimu ambazo wazo lako litapitia kabla ya kuonekana kwenye uhalisia
Niseme, nisiseme! Wazo linazaliwa, linakua na muda mwingine kuzeeka mpaka kufa!
Kwa hiyo wazo ni kama mtoto, linabebwa kama mimba. Hiki ni kipindi ambacho linakuwa kichwani mwa mtu. Linazaliwa hapa ni pale ambapo linaanza kufanyiwa kazi, linakua, hapa ni pale linapozidi kufanyiwa kazi na kuzidi kuleta matokeo kwa aliyekuwa na wazo na jamii, wazo linazeeka na hata kufa (hapa ni pale ambapo linakuwa halijafanyiwa kazi kikamilifu).
Wanaume kama nawaona vile mnavyoguna, eti unajiuliza kwa hiyo na sisi wanaume tunabeba mimba? Naomba nieleweke tu kwamba mimba yenyewe ni ya wazo siyo mimba ya mtoto, hapo vipi.
Mwanamke anapokuwa na mimba ya mtoto kuna vitu anapaswa kufanya ili mimba hiyo isitoke wala kuharibika. Mtoto anapozaliwa anaangaliwa kwa umakini, analelewa, analishwa na kupewa vitu vyote vya muhimu. Endapo vitu hivi vitu vyote vitatolewa bila shida yoyote, unakuwa ni uhakika kwamba LAZIMA TU mtoto atakua. Na ni kweli anakua, lakini endapo vitu fulani havitazingatiwa, basi ndio mtoto ataaza kupata utapiamlo, au magonjwa mengine.
Sasa kitu kikubwa cha wewe kufanya ni kwamba, ukiwa na wazo la biashara, hakikisha unakimbizana kulifanyia kazi.
Ukianza kulifanyia kazi ng’ang’ana nalo mpaka likue au ulifanikishe.
Ukishalikuza, hakikisha unakuwa mbunifu ili liendelee kukua zaidi au kuenea maeneo mengine, la sivyo litakufa.
PATA KITABU CHA BURE
Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli
Godius Rweyongeza
+255755848391/ Morogoro-Tanzania
-
Kitu Gani Haswa Kinahitajika Ili Kufanikisha Wazo Lako
Mwaka 1908 ni mwaka wa kihistoria maana ndio mwaka ambao gari la kwanza lilitengenezwa na kampuni ya Ford ambayo ilianzishwa mwaka 1903,
Gari hilo liliipa jina kampuni ya Ford na kuifanya itengeneze fedha za kutosha, kiasi kwamba watu wengi wakawa wanatamani kuanzisha biashara kampuni nyingine ambazo zingezalisha magari. Ukiangalia kwenye mtandao wa google, kampuni zilizoanzishwa kati ya mwaka 1900 mpaka 1999 ni karibia 3000.
(more…) -
Hizi Hapa Ni Sababu Za Kwa Nini Unapaswa Kufanyia Wazo Lako Mwaka Huu Na Sio Kusubiri
Natumai kwamba unaendelea vyema. Ni takribani wiki nzima sasa nimekuwa nikiandika makala kuhusu wazo la biashara. Kila siku tumekuwa tunapata makala moja iliyojishosheleza na yenye ujumbe uliokamilika. Sasa leo nimerudi tena kwa lengo la kukueleza kwa nini unapaswa kufanyia wazo lako la biashara mwaka huu na sio mwaka mwingine. Najua kwamba ninachoenda kuandika hapa ni muhimu kwako endapo utakifanyia kazi. Kama unajua kwamba utasoma hapa ila ukaishia kusema kwamba huyu jamaa anaandika vizuri, basi ni bora kabisa usisome il usije ukapoteza muda wako. Mimi binafsi najali sana muda wako, maana najua kwamba muda ni mali. Sasa haina haja ya wewe kusoma hapa ukaishia kusema kwamba huyu jamaa kaandika vizuri wakati huyafanyii kazi yale unayojifunza hapa.
Sasa baada ya kusema hayo kuna sababu NNE za kwa nini unapaswa kuanza mwaka huu kufanyia kazi wazo lako.
(more…) -
WAZO LA BIASHARA AINA HII LAHUWEZI KULIPATA
Kuna mtu unaweza kumkuta anatafuta wazo la biashara ambalo halijawahi kufanyika, kitu ambacho hakijawahi kuonekana
(more…) -
Kwani wewe unasemaje?
Habari ya leo,
Mwezi wa tisa mwaka 2016, nilianza kuandika makala kwenye blog ya songambele na baada ya hapo niliendelea mbele zaidi na kuandika vitabu, nikaandika magazetini, nikatoa mada kwenye redio na runinga na hata kuandaa mafunzo kwenye YouTube.
Kwangu hizi zote zimekuwa ni tuzo za hatua ya kwanza niliyochukua na kuanza kuandika mwaka 2016.
Imani yangu ni kuwa lazima kwenye maandiko yangu au mafunzo yangu, utakuwa umewahi kupata kitu chochote ambacho unafanyia kazi au ambacho kimekusaidia.
Kama hilo ni kweli, basi leo ningependa kupata mrejesho wa maandishi kutoka kwako. Imani yangu kuna wengine ambao wangependa pia kusikia kitu kama hiki.
Ni kitu gani umependa? Kitu gani kimekuwa msaada kwako? Je, vitu ambavyo nilifundisha kwenye kitabu au makala vilikuwa na msaada?
Ulipenda jinsi kitabu fulani kilivyokuwa? Ni kitu gani unadhani Kama kingeongezwa kingefanya kitabu hicho kuwa bora zaidi? Tunaomba maoni yako HAPA
Mara zote napenda mrejesho, na ninapenda kuboresha huduma na bidhaa zangu ili ziweze kuwa zenye manufaa kwako na kwa wengine zaidi.
Maoni yoyote yanakaribishwa.
Ni Mimi
Godius Rweyongeza
+255755848391
(www.songambeletz.com)
MOROGORO-TZBONYEZA HAPA kuweka maoni yako
-
UNAPASWA KUACHANA NACHO

Kuna wakati unapaswa kuachana na vitu hata kama watu wanasema ni fursa nzuri.
(more…)
Au hata kama kilikuwa ni kitu unapenda kufanya kwa siku nyingi. -
Njia 7 Za Kutumia Ili Kupata Wazo Bora La Biashara
Wazo bora la biashara halishuki kutoka mbinguni~ Godius Rweyongeza

Moja ya kitu ambacho kimekuwa kinawakwamisha watu wengi na kuwafanya washindwe kuanzisha biashara ni wazo la biashara. Watu wamekuwa wanashindwa kupata wazo la biashara, sasa kwenye kipengele hiki ninaenda kukuonesha ni kwa jinsi gani ambavyo unaweza kupata wazo bora la biashara.
(more…) -
Kama Hujui Ni Kitu Gani Unapaswa Kufanya Maishani, Anzia Hapa
Inatokea kwamba watu wengine kwenye maisha wapo kwenye hali ambayo hawaelewi wanapaswa kufanya nini wala ni wapi wanapaswa kuelekea. Sasa kwenye makala ya leo naenda kuongea na watu wa aina hii na kuona ni kwa jinsi gani ambavyo wanaweza kutumia fursa zilizopo kwenye maisha kuhakikisha kwamba wanasonga mbele.
Hivyo, kama wewe haupo kwenye hali hii hapa basi unaweza ukaachana na makala hii ili usome nyingine ambazo zinakuhusu, ila endapo utaamua kuisoma makala hii kuna vitu viwili ambavyo nina uhakika kwamba utaondoka navyo.
Kwanza kuna kitu ambacho unaweza kujifunza kutoka kwenye andiko hili.
Pili unaweza kupata ushauri ambao siku nyingine unaweza kuutumia kumsaidi amtu mwingine.
Upo tayari niendelee?
KAMA UPO KWENYE HALI AMBAYO HUELEWI NINI CHA KUFANYA
Ebu chukulia kwamba ndio umemaliza chuo na ulikuwa na matarajio makubwa kwamba baada ya chuo unaenda kuajiriwa sehemu na utapata mshahara mkubwa kutokana na kazi ambayo utakuwa unafanya. Ila sasa upo mtaani na huelewi ni kitu gani ambacho unaweza kufanya. Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia.
Kwanza unapaswa kujua kwamba kukosa ajira siyo kwamba unakuwa umekosa kazi kabisa. Kazi zipo, badala yake unaweza kuanza kutumia kile ulichonacho
Anza kutumia elimu yako
Kama umesoma na una kiwango fulani cha elimu, usikae tu hovyo ukabweteka. Hiyo elimu yako kuna watu ambao inaweza kuwasaidia kwenye hali zao walizonazo. Hivyo, unaweza kuitumia elimu hiyo kuwasaidia watu wengine na watu wengine wanaweza kuwa tayari kukulipa.
Anza kutumia kipaji chako
Kwanza kipaji chako unakijua wewe? Kipaji chako ni sehemu nzuri ya kuanzia, unaweza kutumia kipaji chako kama sehemu ya kuanzia kutengeneza kipato, lakini pia kutengeneza mali zinazoshikika na zisizoshikika. Unaweza kutumia kipaji chako kuandaa video au igizo, mafunzo ya sauti, makala, vitabu, muziki, tovuti n.k na hivi vyote vikawa chanzo cha wewe kuanza kuingiza kipato.
Anza kutumia ujuzi wako
Kama umewahi kuajiriwa sehemu au umewahi kufanya kazi sehemu nyingine yoyote, jua kwamba una ujuzi tayari ambao unaweza kuanza kuutumia mtaani. Tatizo kuna watu wana ujuzi ila wanaudharau au wanajiona kwamba sio watu wa viwango hivyo vya chini, wao wanachotaka ni kazi ambazo watakuwa wanafanya huku kipupwe kikipita kwa mbaali.
Sikia nikwambie; kila mtu anapenda kazi za aina hiyo, ila unapokuwa katika hali ambayo huelewi, usichague kazi. kwa sasa kitu kikubwa tunchoshughulika nacho ni wewe kupata kitu ambacho unaweza kuanza nacho maishani mwako na hatimaye ukaweza kusonga mbele na kufikia viwango ambavyo umekuwa unavitamani kwa siku nyingi. Ndoto zako hizo kubwa zinawezekana ila kwa sasa fanyia kazi haya.
Anza kutumia konekisheni zako
Kuna watu ambao umekuwa unafahamiana nao kwa siku nyingi, watu hawa wanaweza kuwa msaada kwako kwenye maisha yako, watumie hawa. Konekisheni zako zinaweza kukusaidia kwenye kupata mtaji, kukuunganisha na mteja, kupata kazi n.k. angalia kwenye hao watu wako wote unaofahamiana nao, ni mtu gani ambaye anaweza kuwa msaada kwako.
Tumia muda wako
Si huna kitu cha kufanya. Uwekeze muda wako vizuri maana utakuja kukusaidia sana siku zijazo. Hivyo basi, hakikisha kwamba unautuia vizuri muda wako katika kujifunza. Usichoke kujifunza. utumie pia muda wako.
Tumia nguvu zako
Nguvu zako kwa sasa ndiyo mtaji mkubwa ambao unapaswa kuuutumia. Anza kuutumia kwa kufanya kazi za nguvu ili upate kipato.
Nimekwambia haya yote ili uweze kupata sehemu ya kuanzia kabisa. na pale utakapokuwa umepata sasa sehemu ya kuanzia ndipo tunaweza kuendelea mbele.
Hakikisha kwamba baada ya kupata sehemu ya kunzia huishii tu kwenye hiyo kazi.
Endelea mbele. Yaani, fanya hiyo kazi huku ukiwa na ndoto kubwa kwenye maisha yako.
Weka akiba kwa ajili ya ndoto yako kubwa.
Wekeza fedha zako kwenye maeneo kama hisa, hatifungani na vipande, nyumba za kupanga, mashamba n.k
Kuza kipato chako kwa kuanzisha biashara n.k.
Rafiki yangu naomba ufahamu kuwa haya yote niliyoyoasema hayatachukua muda mfupi, yatachukua muda kwelikweli. Ila ukweli ni kwamba, kama kweli utakuwa tayari kuweka kazi na kuachana na njia za mkato, kuna siku utafika.
Najua umekuwa unatumia njia za mkato kwa siku nyingi sasa, ila hazijaweza kukufikisha popote, sasa ni muda wako wewe kuweka kazi na kuachana na njia za mkato.
Kila la kheri
-
UBUNIFU UNABORESHA BIASHARA YAKO
UBUNIFU UNABORESHA BIASHARA YAKO
Kama wewe umekuwa mtumiaji wa muda mrefu kidogo wa mtandao wa WhatsApp utagundua kuwa mtandao huu umekuwa unafanyiwa marekebisho ya hapa na pale kila mara.
Kuna kipindi haya mambo ya status au WhatsApp business hayakuwepo.Nakumbuka suala zima la kubold, italicize, underline na
strikethroughna yenyewe hayakuwepo.- Jinsi ya Kuandika Aya Zinazosomeka Kwa Urahisi
- (no title)
- Sura Nzuri ya Kitabu Inatakiwa Iweje?
- Jinsi ya Kuandika Utangulizi Unaovutia
- Uandishi Kama Njia ya Kuacha Urithi
Ila kadiri siku zilivyoendelea yamewekwa. Hayo ni machache tu kati ya marekebisho mengi ambayo wamefanya.
Ninachotaka kukwambia ni kwamba kwenye biashara yako, ni vizuri kuwa mtu wa kufiria nje ya boksi na kufikiria zaidi ya hapo ilipo kwa sasa.
Ubunifu utaitofautisha sana biashara yako na biashara za watu wengine. Maana hata ukisema ufanye biashara ambayo haijawahi kufanywa hapa duniani. Ndani ya miezi sita tu, kuna watu watakuona ukiifanya na wenyewe wataanza kuifanya. Kumbe basi, kitu pekee ambacho kinaenda kukutofautisha wewe na wengine ni ubunifu.
UBUNIFU SIYO MPAKA UWE NA WAZO AMBALO HALIJAWAHI KUWEPO
Wengi wanapofikiria ubunifu basi wanadhani, mbunifu yeyote anapaswa kuja na wazo la kipekee sana na wazo ambalo halijawahi kuonekana. Unaweza kuja na wazo la kawaida, ila kwenye biashara yako likawa linaleta mapinduzi.
Inashauriwa walau kila siku uwe unafikiria mawazo ya kawaida kumi tu na kati ya hayo utoe moja au mawili ambayo utayafanyia kazi. Ukiwa mtu wa kufikiria hivi ni uhakika kuwa mwaka mmoja baadaye, kama ni biashara, lazima tu utakuwa umeisukuma mbali.
UBUNIFU SIYO MPAKA UWE PROFESA
Ubunifu ni kitu tunazaliwa nacho. Ndiyo maana utagundua kwamba kila mtoto huwa anapenda kuumba vitu mbalimbali kwa kutumia udongo, mchanga au malighafi zozote anazoona zinamfaa.
Kwa hiyo hiki kiwe kiashiria kwako kuwa UBUNIFU ni kitu tunacho, tumezaliwa nacho na tunaenda nacho popote. Kadiri ambavyo utautumia ubunifu kwenye kazi, biashara au eneo lolote, ndivyo utakavyoimarika zaidi na zaidi.
Ungependa kujifunza zaidi kuhusu UBUNIFU?
Nakushauri upate nakala ya kitabu changu cha JINSI YA KUIBUA UBUNIFU ULIO NDANI YAKO.
kwenye kitabu hiki nimeongelea tu kuhusu suala zima la UBUNIFU, mwanzo mpaka mwisho.
Kukipata rusha elfu Saba tu (7,000/-) kwa 0755848391 au 0684 408 755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.Unaweza pia kubonyeza hapa ili ukipate mara moja.
NB. Kwa Sasa kitabu kinapatikana kwenye mfumo wa nakala laini(ebook).
Umekuwa nami,
GODIUS RWEYONGEZA
Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
kila la kheri