Home


  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Nawezaje kupata vitabu Vya Godius Rweyongeza?

    Rafiki yangu mpendwa salaam. Godius Rweyongeza yupo Morogoro nchini Tanzania. Ofisi zake zipo maeneo ya sabasaba; Morogoro. Hata hivyo, hilo halikuzuii wewe kupata vitabu vyake popote pale utakapokuwa nchini Tanzania.

    Ili kupokea kitabu chako popote pale utakapokuwa nchini Tanzania na Afrika Mashariki,

    1. Kwanza unatakiwa kuchagua kitabu ambacho ungependa kupokea. Vitabu vya Godius Rweyongeza vipo katika mfumo wa nakala ngumu (hardcopy), nakala laini (softcopy) na nakala za sauti (audiobook). Kama unataka nakala za mtandaoni (softcopy/ebooks) basi utalipia na kupokea ebooks zako hapohapo bila ya kuchelewa. Aidha kama unataka vitabu vya sauti; audiobooks utalipia na kutumiwa audiobooks zako mara moja. Kutokana na urefu wa audiobooks huwa zinatumwa kwa telegram tu. Vitabu vyote vya sauti (audiobooks) na vya mtandaoni (softcopy) vinapatikana kwa elfu kumi. Orodha ya vitabu itaambatanishwa hapo chini.
    2. Godius Rweyongeza pia ana vitabu vya hardcopy (nakala ngumu). Hivi unaweza kuvipata popote pale utakapokuwa nchini Tanzania. Unachotakiwa ni kuchagua kitabu cha Hardcopy unachotaka. Orodha Kamili ya vitabu vya nakala ngumu, hardcopy inaambatanishwa hapo chini.
    3. Ukishachagua kitabu chako, utafanya malipo, namba ya malipo ni airtel money 0684 408 75 kama upo nje ya nchi ya Tanzania tumia namba hii YA M-PESA kufanya malipo: +255745848395. Hakikisha umeanza na code +255 kama inavyooneshwa hapo kama upo je ya nchi. Kwenye namba zote jina ni GODIUS RWEYONGEZA  Baada ya kufanya malipo, tuma uthibitisho kuwa umefanya muamala kwa namba ya simu 068440855 (whatsap/sms).
    4. Kwa vitabu vya mtandaoni (softcopy/audiobook) utavipokea ndani ya dakika tano baada ya kuwa umefanya malipo. Kwa vitabu vya nakala ngumu, vitatumwa na utapewa maelekezo ya kuvipokea. Lakini kama una mapendekezo ya gari au usafiri gani tutumie wakati wa kukutumia vitabu vyako, utatuambia, nasi tutafuata hayo maelekezo yako. Ndani ya saa 48 unakuwa umepokea kitabu chako kulingana na eneo ulipo. Wakati kama upo karibu na Morogoro au Dar Es Salaam, basi huwa ni ndani ya saa 2. Kwa Dar Es Salaam na Morogoro tunafanya Delivery ila hapa unaongeza kiasi kidogo kwenye gharama ya kawaida ya kununua kitabu kwa ajili ya delivery.

    Rafiki yangu, hivyo ndivyo unaweza kupokea vitabu vya Godius Rweyongeza popote pale utakapokuwa nchini Tanzania, Afrika na Dunia nzima.

    Hapa chini nimeambatanisha orodha vya vitabu vyake vyote.

    Kwenye hii orodha.

    Vitabu 11 vya kwanza vinapatikana kwenye mfumo wa nakala ngumu.

    Vitabu sita vya kwanza vinapatikana kwenye mfumo wa sauti pia.

    Vitabu vingine ni nakala laini.

    Hata hivyo kuna vitabu vingine ambavyo vinapatikana kwenye mfumo wa nakala laini na nakala ngumu; na vingine vinapatikana kwenye mifumo yote; yaani, nakala ngumu, nakala laini na nakala yamtandaoni. Chagua mfumo wowote ule ambao ungependa kupata kwa sasa. Kisha lipia kitabu unachotaka.

    Kumbuka; nakala ya laini (softcopy/ebook) ni 10,000/- kwa kila nakala

    Nakala ngumu (hardcoy) ni 25,000/ kila nakala

    Na nakala za sauti ni 10,000/- kwa kila nakala.

    Ifutayo ni rodha kamili ya vitabu vya GODIUS RWEYONGEZA

    1. JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO

    Hardcopy (25,000). (hardcocopy)

    Audiobook=10,000/-

    Flash audiobooks zote + mafunzo ya ziada (150,000/-)

    1. Maisha Ni FURSA: Zitumie ZIKUBEBE

    (hardcocopy 25,000/-)

    Audiobook=10,000/-

    Flash audiobooks zote + semina+kozi+ mafunzo ya ziada (150,000/-)

    1. NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA

    (hardcocopy 25,000)

    Audiobook=10,000

    Flash audiobooks zote + semina+kozi+ mafunzo ya ziada (150,000/-)

    1. MAAJABU ya kuweka akiba

    Hardcopy 20,000

    (($oftcopy 10,000))

    Audiobook 10,000/-

    Flash audiobooks zote + semina+kozi+ mafunzo ya ziada (150,000/-)

    1. KIPAJI NI DHAHABU: Jinsi Ya Kugundua kipaji chako, kukinoa na kukiendeleza
      Hardcopy 25,000
      ($oftcopy 10,000)
      Audiobook 10,000
      Flash audiobooks zote + semina+kozi+ mafunzo ya ziada (150,000/-)
    1. JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO ($oftcopy 10,000)

    Hardcocopy 25,000/-

    AUDIOBOOK (10,000/-)

    Flash audiobooks zote + semina+kozi+ mafunzo ya ziada (150,000/-)

    1. VYANZO VINGI VYA KIPATO (10,000) Softcopy

    Hardcopy (20,000/-)

    1. NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA
      Hardcopy 25,000/-
      Softcocpy=10,000/-
    2. MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE Hardcopy 25,000  ($oftcopy 10,000)
    3. Kutoka sifuri MPAKA KILELENI (20,000) (hardcocopy)
    4. JINSI ya kuwa mwandishi MBOBEVU
      Hardcopy 20,000/-
      ($oftcopy 10,000)
    5. TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA: tatizo Ni rasilimaliwatu tunaowapoteza (volume 1)

    Hardcopy 25,000/-

     ($oftcopy 10,000)

    1. AKILI YA DIAMOND (hardcocopy 10,000/-)
      Softcopy 10,000
    2. Mambo 55 ya Kuzingatia kabla ya KUANZISHA BISHARA (Softcopy 10,000)
    3. JINSI YA kuibua ubunifu ulio ndani yako ($oftcopy 10,000)
    4. ZAMA ZIMEBADILIKA: MAISHA YAMEBADILIKA, AJIRA HATARINI na WEWE BADILIKA
    5. NGUVU YA KUWEKA MALENGO (10,000) softcopy
    6. NGUVU YA WAZO (5,000/-) softcopy
    7. MWONGOZO WA WAPAMBANAJI(softcocpy 10,000/-)
    8. NYUMA YA USHINDI: Kuna Kushindwa, Kushindwa, Kushindwa
      Softcocpy 10,000/-
    9. JINSI YA KUTENGENEZA MSHAHARA NJE YA MSHAHARA $oftcopy 10,000/-
    10. FURSA AMBAZO VIJANA WA SIKU HIZI WANACHEZEA NA JINSI YA KUZITUMIA $oftcopy (10,000/-)
    11. UJUZI AMBAO KILA MFANYABIASHARA ANAPASWA KUWA NAO $oftcopy (10,000/-) 
    12. MAAJABU ya kusoma vitabu (free ebook & Audiobook)

    Flash audiobooks zote + semina+kozi+ mafunzo ya ziada (150,000/-)

    Ebook hii ya maajabu ya kusoma vitabu unaweza kuipta bure kabisa hapa.

    Audiobook yake pia unaweza kuipata bure hapa

    Ila kama ungependa kupata flash, yenye audiobooks zote nane. Pamoja na mafunzo ya semina mbalimbali ambazo nimekuwa natoa, kozi mbalimbali ambazo huwa natoa pamoja na  mafunzo mengine ya ziada, basi utalipia laki moja tu. Namba ya malipo ni 0684408755. Ukishafanya malipo, nitumie ujumbe kwenye namba hiyohiyo whatsap ili ni kutumie flash au vitabu vyako.

    Mimi nakupenda sana. Kama una swali lolote tafadhali naomba uniulize, nami nitakujibu. Asante.

    Godius Rweyongeza

    0755848391

    Morogoro-TZ

  • ACTIVE MODE ACTIVATED

    Mara kwa mara kuna watu huwa unakuta wameandika kwenye sehemu mbalimbali mtandaoni au nje ya mtandaoni wakiwa maneno kama “dancing mode activated” au running mode activated n.k

    Sasa tunapouanza mwaka mpya 2024, kuna maeneo muhimu sana ambayo wewe unapaswa kuya”activate” na kuhakikisha yako “activated” kwa mwaka mzima unaokuja.

    1. UWEKEZAJI (INVESTING MODE ACTIVATED). Huu mwaka huu, usirembe mwandiko linapokuja suala zima la uwekezaji. Zembea sehemu nyingine lakini usizembee kwenye uwekezaji. Ufanye uwekezaji kuwa kipaumbele kwako ndani ya huu mwaka. Yaani, kila unapopokea fedha, kipaumbele chako cha kwanza kiwe ni kufanya uwekezaji. Na hata baada ya kuwa umeweza kufanya uwekezaji, kiasi kingine ambacho kitabaki, ondoa matumizi yoyote yale ambayo siyo ya lazima ili fedha nyingi uweze kuielekeza kwenye uwekezaji.

      SOMA ZAIDI: Uwekezaji Kwenye Hisa vs Uwekezaji Kwenye Maeneo Mengine

    2. KUONGEZA KIPATO. Ili uweze kuweka akiba, unapaswa kuhakikisha kwamba una kipato cha uhakika. Wengi huwa wanafikiri kwamba tunapozungumzia kipato cha uhakika basi tunakuwa tunzungumzia ajira hasa ya serikalini.

      Japo wengi wanaiona ni ajira ya uhakika, ila mimi sioni uhakika wowote ndani yake. Ajira ni ajira tu. Kumbe unapasawa kuwa unafikiria nje ya ajira mara zote. Na unafikiria nje ya ajira kwa kuhakikisha kwamba, unaanza kutengeneza vyanzo vingine vya kipato ambavyo vinakuingizia kipato nje ya ajira yako. Kwenye maisha yako usikubali kipato chako cha mwaka jana kuendelea kubaki vilevile ya mwaka unaofuata. Kila mwaka tafuta namna ya kuhakikisha kwamba kipato chako unakiongeza walau mara mbili zaidi ya kilivyokuwa mwaka mmoja ambao umetangulia. Na kama kuna mbinu ambayo unaona unaitumia na inaleta matokeo, basi hiyo mbinu kamwe usiache kuitumia. Itumie zaidi na zaidi ili uweze kuleta matokeo makubwa zaidi.

      SOMA ZAIDI: Unawezaje Kujiajiri kwa Mtaji Kidogo?

    3. Vitendo (action mode activated). Mambo yote unayojifunza hapa, hayatafanya kazi kama wewe hutakuwa tayari kuyafanyia kazi. Ni mpaka ufanye kazi ndiyo utaweza kupata matokeo. Hivyo, mwaka huu fanyia kazi kila unachojifunza bila ya kurudi nyuma.

      SOMA ZAIDI: Nguvu Ya Vitu Vidogo Kuelekea Mafanikio Makubwa katika Vitendo;

    4. Biashara (business mode activated). Ili kuongeza kipato chako mara mbili unahitaji kuhakikisha kwamba unakuwa na biashara. Biashara ndiyo njia pekee ya uhakika ambayo inafahamika ya kuongeza kipato chako mara mbili zaidi kadiri muda unavyokwenda, ni tofauti na njia nyingine zozote zile. Uongezwaji wa kipato kwenye ajira, una ukomo. Na mshahara kwenye ajira hauwezi kuongezeka mara mbili kila mwaka kwenye ajira. Lakini kwenye biashara, kama kweli utajifunza biashara kwa kina na kufanyia kazi yale unayotakiwa kufanyia kazi. Inawezekana. Kama kweli utaongeza juhudi zaidi kwenye mauzo ya biashara yako, ni ukweli kuwa unaenda kufanya makubwa kwenye biashara yako bila ya kurudi nyuma. Hivyo basi, mwaka huu wa 2024, kama bado hauna biashara, anzisha biashara. Kama una biashara tayari, basi ongeza juhudi zaidi na zaidi li uweze kuwafikia watu wengine zaidi.

      SOMA ZAIDI: Vitu Vitano Vitakavyokuzuia wewe kufanikisha malengo yako

    5. Watu (people mode activated). Watu ni muhimu sana, ili ufanikiwe, unahitaji watu. Aidha ni watu wa kukusaidia wewe ili uweze kufanikisha ndoto na malengo yako. Wanaweza pia kuwa ni watu wa kukusimamia (makocha na mamenta). Aidha wanaweza kuwa ni timu yako unayofanya nayo kazi. Sasa wewe unahitaji ujuzi sahihi wa kukaa na watu na kuweza kufanya nao kazi. Unahitaji ujuzi wa kuhamasisha watu ili waweze kuchukua hatua kwenye majukumu yao ambayo wanatakiwa kufanyia kazi. Jifunze sana kuhusu watu na namna ya kushughulika nao. Huu ujuzi utakusaidia sana ndani ya huu mwaka 2024. Kumbuka, pesa zako wanazo watu. Kama umeajiriwa maana yake unamtegemea bosi wako ili aweze kukulipa mshahara (mtu). Na unahitaji kujua namna sahihi ya kuendana naye. Kama umeajiajri maana yake unategemea wateja wanunue kwenye biashara yako (watu). Na unapaswa kujua namna sahihi ya kushughulika nao. Kama umeajiri maana yake unafanya kazi na watu tayari. Unapaswa kujua namna sahihi ya kushughulika na watu wako. Kwa vyovyote vile rafiki yangu, hakikisha kwamba unakuwa na ujuzi sahihi wa kushulika na watu huu ujuzi utakusaidia parefu sana kwenye maisha yako.

    Hizi ndizo aina za ujuzi ambazo unapaswa kuanza kuzifanyia kazi mara moja kwa manufaa yako wewe mwenyewe

    Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

    Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

    SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea

    Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

    Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

    Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

    Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

    For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com

  • Kitu kimoja unachopaswa kufanyia Kazi kwa uhakika 2024

    Kitu kimoja unachopaswa kufanyia Kazi kwa uhakika 2024

    Rafiki yangu, kuna kitu kimoja ambacho unapaswa kukifanyia kazi kwa uhakika mwaka 2024. Kitu hiki siyo kingine bali ni kutenda kile unachosema.

    Usishauri watu kitu ambacho Wewe mwenyewe hutakifanyia kazi.
    Usiwaambie watu wafanyevkitu ambacho Wewe hujawahi kufanya Wala mpango wa kufanya. Na Wala hutakaa ukifanye.

    Sema kidogo 2024, ila tenda sana
    Ukiwaambia watu juu ya habari ya kufanya mazoezi. Kuwa kipaumbele Wewe mwenyewe kwa kufanya mazoezi.

    Ukiwaambia watu weka AKIBA. Kuwa kipaumbele mwenyewe kwa KUWEKA AKIBA.

    Kumbuka, simaanishi kwamba mwaka huu ujioneshe. Kuna tofauti kubwa kati ya mtu anayejionesha na anayefanya kweli.

    Mfano, ninaposema fanya mazoezi. Simaanishi Sasa ujioneshe kuwa unafanya mazoezi. Ukiona mwaka huu unaanza kufanya kitu ili watu wakuone, ACHA.

    Fanya kwa msukumo kutoka moyoni na siyo kwa ajili ya kujionesha.

  • Nitakuwa Kwenye Kipindi Cha Temino Ya Clouds FM Leo

    👆🏿👆🏿Wakati unajipanga kwa ajili ya hiki kipindi Maalumu cha kufungua mwaka 2024. Hakikisha pia unajiandikisha kwa ajili ya semina ya kufungua mwaka 2024.

    Taarifa kamili ya semina ya kufungua mwaka 2024 hii hapa👇🏿

    www.songambele.co.tz/semina

    Ni semina ya mwezi mzima.
    Venue: Whatsapp

    Ada ya semina ni 30,000/-

    Malipo yanafanyika kwa namba ya simu: 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Ukishalipia mapema TU tunawasiliana ili uweze kuungwa kwenye kundi la whatsap la semina .

    Kwa Sasa unaweza kujiunga kwenye kundi la mapokezi hapa👇🏿
    https://chat.whatsapp.com/CAdCnW82i8N0clD2fDvn7v

    Mwaka 2024 ndiyo huu hapa, lengo lako kuu ni lipi? Au unamwachia Mungu?

    Enewei tukutane kwenye TEMINO YA CLOUDS FM baadaye Leo kuanzia saa Tisa jioni mpaka saa Kumi na moja

    Cheers!

    Godius Rweyongeza
    www.songambele.co.tz
    Morogoro-Tz

  • Code Ya Kukusaidia Kufanya Makubwa 2024 Hii Hapa

    Unataka kufanya makubwa 2024. Code ya kufanya makubwa ndani ya 2024 imeelezwa kwenye hii video.

  • Kama una mpango wa kufunga Ndoa 2024, hakikisha unasoma hapa

    Kama unamjuaa anayefunga ndoa mwaka huu mtumie ujumbe huu

    Una mpango wa kufunga ndoa 2024 rafiki yangu. 

    Kwenye jamii zetu kumekuwa na utaratibu ambao unajirudia kila mwaka. Kila mwaka kuna maelfu ya watu wanaofunga ndoa na utaratibu ambao huwa unafanyika huwa ni uleule kila mwaka..

    Mtu akitaka kufunga ndoa, anaandaa harusi kubwa, anaalika watu mbalimbali wamchangie, ili kuonesha ubabe anaweka vitu vya gharama kubwa.

    Hela inapokuwa haitoshi anakopa na sherehe inafanyika.

    Wengine wanafanya harusi wakiwa na matarajio kuwa ile fedha watakayopata siku ya harusi ndiyo iwasaidie kulipa mkopo au kuanzia maisha baada ya harusi.

    sasa sipo hapa kusema kwamba usifanye harusi. Hilo utafanya au hutafanya kulingana na wewe mwenyewe au kulingana na ukubwa wa mfuko wako. lakini chonde chonde, usifanye harusi kwa kukopa hela. Usianze maisha ya mahusiano ukiwa na deni. Hii siyo sehemu nzuri ya kuanzia kimaisha.

    Usikope fedha kwa ajili ya kufunga ndoa ukitegemea kuwa zawadi utakazopata zitaweza kurejesha ule mkopo. Mara nyingi huwa haiwi hivyo. Kumbuka sijasema mara zote, ila mara nyingi.

    Najua kabla ya kufunga ndoa huwa kuna mafunzo ambayo huwa yanatolewa. Lakini kuna mafunzo ambayo huwa yanasahaulika. na mafunzo haya ni ya uwekezaji.

    Kabla hujafunga ndoa mwaka huu hakikisha kwamba unajifunza uwekezaji. Siyo wewe tu, hata huyo mwenza wako, hakikisha anajifunza uwekezaji. Na hasa uwekezaji kwenye hisa, hatifungani na vipande. Nakwambia, utanishukuru kwa hili maisha yako yote. 

    Hii ni elimu ambayo haitolewi unapokuwa unataka kufunga ndoa ila ni elimu muhimu ambayo ukiipata itakuwa yenye manufaa kwako, kwa familia yako na kwa kizazi chako, hata miaka buku ijayo. hivyo basi, nikushauri kitu kimoja, jifunze uwekezaji kwenye hisa, hatifungani na vipande wewe na mwenzako kabla ya kuingia kweye ndoa mwaka huu.

    Na sehemu nzuri ya kuanzia ni kusoma kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA kwenye hisa, hatifungani na vipande. Kitabu hiki unaweza kukipata kwa kuwasiliana na 0684408755 sasa. 

    Soma zaidi: Jiwe la uzito wa tani moja kwa wale ambao hawataki kuweka akiba

  • Tengeneza Pesa Kwa kuuza Unachojua (Maarifa + Taarifa)

    Unaendeleaje, leo kwenye video fupi ambayo tumekuandalia, tumeandaa namna ambavyo unaweza kuanza kutengeneza fedha kwa kutumia kile ambacho tayari unajua sasa hivi.

    Wewe ni kitu gani ambacho unajua? Je, umekuwa unaagiza mizigo nje ya nchi kwa muda? Huicho ni kitu unajua, kinaweza kuwasaidia wengine.
    Umekuwa ukilima mahindi? Hicho ni kitu kingine muhimu sana ambacho unajua.

    Kwa chochote kile unachojua, kuna namna ambavyo unaweza kuanza kutengeneza hela kwa kutumia hicho kitu.

    Nimeandaa video fupi ambayo unaweza kuitazama hapa

    Kitabu kinachoeleza  hii mada kwa undani zaidi kitakuwa tayari mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi. Unaweza kuweka oda 0755848391

    Na usisahau kuhusu semina itakayofanyika tarehe 20.1.2024.

    Soma zaidi kuhusu semina hapa

    Uwe na siku njema sana

    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • Una Mpango wa Kuja Morogoro 2024

    Rafiki yangu wa ukweli, una mpango wa kufika Morogoro, au kupita Morogoro mwaka huu?

    Tupo Morogoro, Sabasaba ikitokea unapita Morogoro au unafika Morogoro mjini kutembea, basi usisite kufika ofisini kwetu. 

    Unaweza hata kujipatia nakala moja ya kitabu. Hahaha. Kama unapita MSAMVU, bado tunaweza kukuletea mpaka Msamvu bila wasiwasi wowote.

    Mawasiliano ya ofisi yanafanyika kupitia 0684408755

    Soma zaidi: GODIUS RWEYONGEZA Books 

    Maoni Ya Watu KuhusuVitabu Vya Godius Rweyongeza

    Karibu sana

    imeandikwa na Godius Rweyongeza

    Morogoro-Tz

    0755848391

  • Vitu 10 Vya Kijinga Ambavyo Unapaswa kufanya Walau Maram Moja Mwaka 2024

    Leo nataka nikwambie vitu 10 tu vya kijinga ambavvyo unapaswa kujaribu kufanya walau mara moja ndani ya mwaka 2024

    1. Toa wiki moja ambayo utalala kwa saa tatu, halafu muda mwingine wote unafanya kazi. Fanya hivyo kwa siku mbili mpaka siku sita au wiki na siyo zaidi ya hapo.
    2. Weka akiba mshahara wako wote, halafu tafuta chanzo kingine ambacho kitakufanya ulipie bili na kuendesha maisha yako ya kila siku.
    3. Zima simu wiki nzima, halafu utumie muda huo kujifunza na kufanya kazi
    4. Ifanye siku moja kwa wiki kuwa takatifu kwako. Siku ambayo hutafanya kazi, bali itakuwa ni siku mapumziko na kupangilia ratiba zako za wiki inayofuata.
    5. Siku moja tembea kwa mguu au nenda na baiskeli sehemu ambayo ulikuwa umezoea kwenda kwa gari kama ofisini.
    6. Kwa dakika 15 tu kwa siku weka mziki wowote unaoupenda na cheza kama siyo wewe, kisha endelea na majukumu yako.
    7. Jiwekee utaratibu wa kutoa kitu kila siku hata kama ni kidogo. Kwa kuanzia unaweza kununua mfuko wa pipi, kisha kila siku ukatoa zawadi ya pipi moja kwa mtu yeyote.
    8. Mara moja moja pika chakula mwenyewe. NB. Hii ni kwa wale ambao huwa hawapiki, au wana wapishi au wenza wao wanapika. mara moja moja hasa ile siku unayokuwa umepumzika (rejea namba 4) pika chakula mwenyewe.
    9. Washa moto bila ya kiberiti, wala kuomba kwa jirani. Washa kwa ulimbombo na ulindi
    10. Mara moja lala kwa saa 10 mfululizo

    Siyo lazima ufanyie kazi haya yote, fanyia baadhi yale unayoona unaweza kwa sasa. Usiache kuja kutupa mrejesho hapa baada ya kuyafanyia kazi.

    Soma Zaidi: Vitu vitano ambavyo hupaswi kuvipoteza kwenye safari yako ya mafanikio

    Nakupenda

    Godius Rweyongeza

    0755848391

    Morogoro-Tz

    NB: SEMINA YETU YA JANUARI, itafanyika kuanzia tarehe 20-20 Februari

    *Karibu kwenye Semina ya Kipekee ya Kufungua Mwaka 2024!*

    Rafiki yangu mpendwa,
    Karibu kwenye mwaka wa mabadiliko na mafanikio –

    Kila mwaka, tumekuwa tukijiwekea lengo la kuleta tofauti katika maisha yetu kupitia semina tatu muhimu.
    Ambapo huwa tuna semina ya kufungua mwaka (Januari 15-30)
    SEMINA ya ana kwa ana (Jumamosi ya mwisho ya mwezi Juni) na semina nyingine ya mtandaoni (Septemba 24-30)

    Kwa Leo ningependa kuongelea
    *Semina ya Kufungua Mwaka 2024: Njia Mpya, Matokeo Makubwa!*

    Tofauti na miaka iliyopita, semina hii ya Januari itakuwa ya kipekee. Badala ya siku 15, safari yetu ya mabadiliko itadumu kwa mwezi mzima! Kutoka tarehe 20 Januari hadi 20 Februari,

    Kwenye hii semina tutajifumza mengi baadhi yakiwa ni pamoja na:

    *Siku ya Kwanza: Karibu kwenye semina ya kufanya makubwa kwa vitendo mwaka 2024*

    *Siku ya Pili: Anza Leo na Siyo Kesho*

    *Siku ya Nne: Jinsi ya kuishinda tabia ya kughairisha*-

    *Siku ya Kumi na Mbili: Jinsi simu zinavyoharibu ufanisi wako na nini cha kufanya mwaka 2024*

    Mada hizi zote zimeundwa kukuhamasisha na kukusukuma kufikia mafanikio makubwa ndani ya mwaka 2024.

    Kila siku itakuletea changamoto mpya na ufahamu wa kipekee. Tutajifunza jinsi ya kujiondoa kwenye tabia zinazotuzuia, kukabiliana na changamoto za kila siku, na kuanza safari ya kujenga mfumo bora wa maisha.

    *Ada Yako ya Ushiriki:*

    Ada ya semina ni zaidi ya thamani utakayopata – Tsh 30,000/-. Pata nafasi yako sasa kwa kulipa kupitia namba 0684408755 (Godius Rweyongeza).

    Hii ni fursa yako ya kuanza mwaka 2024 kwa nguvu mpya na mwongozo wa kufanikiwa.

    *Jiunge Nasi:*

    Tunakualika kwenye kikundi chetu cha WhatsApp kwa ajili ya semina. Jiunge na wenzako wanaotafuta mabadiliko na mafanikio:

    (https://chat.whatsapp.com/CAdCnW82i8N0clD2fDvn7v)

    *Fanya Uamuzi wa Kuleta Mabadiliko:*

    Hatua ndogo ndiyo mwanzo wa safari kubwa. Hakikisha unathibitisha ushiriki wako mapema na kuwa tayari kubadilisha maisha yako.

    Tunakusubiri kwenye Semina ya Kufungua Mwaka 2024  ili uianze safari Yako ya Mabadiliko na Mafanikio!

    Karibu sana!

    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

X