-
Vitu 9 ambavyo hupaswi kuchoka kufanya
Katika maisha Kuna vitu hata iweje huwezi kusema umechoka kuvifanya. Huwezi kusema nimechoka kupumua, maana ykiacha kupumua tu huo ndio mwisho wako. Huwezi kusema nimechoka kula, wala huwezi kusema nimechoka kulala, kuanzia leo sitalala tena. Ni vitu vya asili ambavyo mwili wako unahitaji ili uendelee kuwa imara zaidi. Wewe pia Kuna vitu unapaswa kujiwekea utaratibu…
-
FANYA UNACHOPENDA
Mara nyingi watu hupenda kufanya kazi fulani kwa sababu aidha ya kifedha au kutafuta umaarufu au pengine kwa kulazimishwa na wazazi. Lakini kazi hizi huwa hawazifanyi kutoka moyoni au Wala huwa haziwapi motisha. Ni muhimu sana ufanye kitu unachopenda kuliko kulazimisha au kulazimishwa kufanya kitu usichopenda. Kama ni fedha au umaarufu utaupata kwa kufanya…
-
Kitu hiki lazima tu kitokee maishani mwako
Kuna vitu katika maisha lazima tu vitokee. Vinatokea uwe unavipenda au huvipendi. Vyenyewe vinatokea tu. Jua linachomoza na kuzama, bila kujali unapenda au hupendi.Dunia inajizungusha kwenye mhimili wake, bila kujali una chuki nayo au unaipenda. Ukiruka juu, sharti utarudi chini bila kujali unapenda au hupendi. Mojawapo ya kitu kingine ambacho lazima kitokee kwenye maisha…
-
Madhara Ya Kuwa Na Mahusiano Na Mtu Zaidi Ya Mmoja
Kama una ndoto kubwa na umekuwa na mpango wa kuja kuwa na mahusiano na watu wawili, au tayari una mahusiano na watu wawili ni bora ukauhairisha au kuondoa kabisa huo mpango. Yafuatayo ni mdhara ya kuwa na mahusiano na zaidi ya mtu mmoja. Kwanza utapoteza nguvu zako nyingi kwa watu hao ambao umeingia nao…
-
Kitabu cha KUTOKA UMASIKINI MPAKA MAFANIKIO CHA ERICK SHIGONGO.
Kwenye kitabu hiki Erick Shigongo ameeleza historia ya maisha yake na kutoa mafunzo kadha kadha kuhusu maisha Kitabu hiki ni kizuri sana, nashauri kila mwenye kiu ya mafanikio makubwa akisome. Utajifunza mengi kuhusu kutoka umasikini mpaka mafanikio makubwa kupitia stori ya Erick Shigongo ambaye maisha yake yalikuwa duni sana, kuliko hata wewe ila akaweza kupasua…
-
Fursa iliyotengeneza mabilionea kwenye karne ya 21
Madalali ni watu ambao wamekuwepo kwa siku nyingi sasa. Kazi yao kubwa imekuwa ni kuunganisha eneo moja lenye bidhaa na jingine lenye uhitaji. Kama una uhitaji wa chumba cha kupanga unamwona dalali anayekuunganisha kilipo. Kiufupi wenyewe wamekuwa wanaingia katikati ya mlaji na mzalishaji. Kwenye karne ya 21 udalali ndio umetengeneza mabilionea kwa wingi. Mtandao…
-
Asilimia 99 ya Maisha ya Watu Hujihusisha Na Vitu Hivi
Leo nimekuandalia vitu ambavyo huwa vinachukua muda wa watu japo huwa havina manufaa yoyote kwao. Ni jukumu lako kuvifahamu na Kisha kuamua kuachana navyo. 1. Watu wengi hupoteza muda mwingi wakihofu jinsi watu wengine wanavyowafikiria, wakati na wao wanahofu wanasemwaje. 2. Watu wengi huishi maisha kwa kutaka kuwaridhisha wengine; wakati mtu pekee wanayepaswa kumridhisha ni…
-
Hiki Ndicho Kitakachotokea Miaka Mitano Ijayo…
Miaka mitano ijayo utakuwa jinsi ulivyo ,isipokuwa kwa vitu viwili. Vitabu unavyosoma na watu unaokutana nao. Watu unaokutana nao wana uwezo wa kukubadili na kukufanya mpya. Watakupa mtazamo wao, fikra zao, ujuzi n.k. Ukitaka kwenda MBALI ambatana na watu sahihi. Vitabu pia ni muhimu sana. Vitabu muda mwingine vinaweza kukukutanisha na watu sahihi. Muda mwingine…
-
USIPOZIBEBA FURSA, HAZITAKUBEBA
Moja ya shida ya watu ambao huwa wanashindwa kutumia fursa ni kujuta mbeleni. Ndio baadaye unakuja kusikia mtu anasema kuwa;๐ Mtu fulani tulisoma wote.๐Mtu fulani tulianza kazi kwa pamoja. ๐Maeneo fulani viwanja vilikuwa vinauzwa kwa bei ndogo ila sasa havishikiki.Ne mengine mengi Hiki ni kiashiria kimojawapo kuwa mhusika hakutumia fursa zilizojitokeza maishani mwake vizuri.…
-
Kwa Nini Asilimia 1 Tu Ya Watu Duniani Ndio Hufanikiwa Sana
Tafiti nyingi zimeonesha kuwa asilimia 1 ya watu duniani ndiyo wenye mafanikio makubwa kukiko wengine. Na hiki kitu kinaelekea kuwa kinafanya kazi kila sehemu. Asilimia 1 ya watu ndio wanaoohodhi mitandao tunayoitumia mara kwa mara. Ndiyo maana juzi anguko la mitandao ya facebook limeleta taharuki kubwa sana. Asilimia 1 ya watu ndio wanaomiliki mashamba makubwa…
-
TUKUZE AKAUNTI AISEE
! Siyo za insta wala facebuku! Ila za benki kuu, Na siyo kwa kuongeza wafuasi, Bali kwa kipato hata cha buku, Kitokanacho na kazi ya mikono yetu, Tuifanyayo mchana hata usiku, Tukuze kipato chetu. Kipato ni chanzo uhuru, Uhuru wa maisha mazuri, Na siyo wa kujionesha bila senti, Kipato kitakusaidia mpaka wajukuu Wao watafurahi hata…
-
MAiSHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE. Zipuuze Zikukikimbie
Hakuna fursa ambayo huwa inapotea. Usipotumia vizuri fursa inayokuja kwako, kuna mtu ambaye ataitumia. Asiyejulikana. Huwezi kuongelea ulimwengu wa kompyuta na mapinduzi ya kompyuta kiujumla bila kumwongelea Gary Kildall. Huyu jamaa ndiye alipaswa kuwa Bill Gates wa nyakati zetu ila akachezea fursa..endelea kusoma ili ujue kilichotokea. Mwaka 1977 kampuni ya apple ilitengeneza kompyuta yao ya…
-
UCHAMBUZI WA KITABU CHA SUGU MAISHA NA MUZIKI. Mambo 14 niliyojifunza kwenye kitabu hiki kinachoeleza Maisha ya Sugu Kutoka Mtaani Mpaka Bungeni
Mwishoni wa uchambuzi huu, nimeeleza jinsi unavyoweza kupata nakala ya kitabu hiki. Nipo tayari kukuchangia kiasi kidogo ili upate nakala ya kitabu hiki kizuri cha Kitanzania. Kwanza, karibu kwenye uchambuzi wa cha SUGU. kitabu hiki kimeeleza maisha ya msanii Joseph Osmund Mbilinyi, maarufu kama Sugu. Ambaye ni mmoja kati ya wanahiphop wa kwanza hapa Tanzania,…
-
Mitandao Mitano Ambayo Vijana wa Kitanzania Wanapenda Kutembelea Sana
Siku ya leo nimeona nikuibie hili. Mtandao wa Alexa huwa una utaatibu wa kupangilia mitandao yote kutokana na wingi wa watembeleaji kutoka kwenye kila nchi. Kwa kutumia mtandao huu unaweza kujua nchi ipi, watu wake wanapendelea kutembelea mtando upi. Na leo tunaenda kuona mitandao ambayo Watanzania wanapenda kutembelea sana. Hii ni muhimu kwako kuifahamu…
-
ZEGE HALILALI
Wajenzi wanalifahamu hili. Zege ikichanganywa, kwa vyovyote vile hata iweje, inapaswa kuisha, la sivyo ikilala, asubuhi, hutaikuta kama zege, badala yake itakuwa imekauka. Itakuwa siyo zege tena…Itakuwa haifai tena kwa ajili ya ujenzi.Ndio maana huwa wanaenda kwa kanuni ya zege HALILALI. Na wewe unaweza kujiwekea utaratibu kama huu. Kuna vitu katika maisha yako unapaswa kuvifanya…
-
Karibu kwenye darasa la mwisho la kuandika kitabu kwa mwaka 2021
Njoo ujifunze kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uandishi wa vitabu Kwa mara nyingine tena, napenda kukutangazia kuwa dirisha la kujiunga na darasa la uandishi limefunguliwa. Ila zamu hii litakuwa darasa la mwisho kwa mwaka 2021. Kama una mpango wa kuandika kitabu kabla mwaka haujaisha, Basi jiunge na darasa hili. Nani anahitajika kwenye darasa? Mtu yeyote…
-
Fursa Tano Ambazo Vijana Wa Siku Hizi Wanachezea (SEHEMU YA TATU)
Kama hukusoma sehemu ya pili bonyeza HAPA 3. Fursa ya kufanya kazi kwa bidii Kwani kufanya kazi kwa bidii ni fursa? Na hapa ningependa nikurudishe tena nyuma mpaka miaka ya akina Napoleon Bonaparte. Umewahi kumsikia huyu mtu? Bonaparte alikuwa mbabe wa vita wa nyakati zake na pengine mbabe wa vita wa nyakati zote. Alipigana Sana…
-
KITABU CHA SUGU: From The Streets To Parliament; MUZIKI NA MAISHA
Leo wakati natembea hapa mtaani, nimekutana na mtu anauza vitabu kikiwemo hiki cha wasifu wa SUGU. Nilivyoambiwa bei ya kitabu tu, sikuchelewa kutoa fedha mfukoni kukichukua! Kinaeleza maisha yake kutoka mtaani mpaka kufika bungeni. Ndio naanza kukisoma hivyo maswali yako yote yatunze. Utaniuliza nikimaliza kukisoma. Kwa wale mnaopenda vitabu vyenye picha, hiki kinaweza kukufaa pia.…
-
Fursa Tano Ambazo Vijana Wa Siku Hizi Wanachezea (SEHEMU YA PILI)
Leo tutaendelea na sehemu ya pili. Kama hukusoma sehemu ya kwanza; BONYEZA HAPA kwanza. 2. Fursa ya kujifunzaAcha nikurudishe nyuma tena, mpaka miaka ya akina Benjamin Franklin. Miaka hiyo walikuwa wanafanya apprenticeship kwa miaka 7-9. Huo ni muda ambao mtoto au kijana alikuwa ananolewa chini ya mtaalamu bila malipo. Kama kijana alifuatilia vizuri masomo yake…
-
Fursa Tano Ambazo Vijana Wa Siku Hizi Wanachezea
Ngoja kwanza, kwani fursa ni nini? Unafanyaje ili kujua kuwa kitu fulani ni fursa na kingine siyo fursa. Kwani fursa huwa zinavaa vazi gani haswa? Enewei, tuachane kwanza na maswali hayo japo nitayajibu mwishoni mwa makala haya, ila kwa sasa acha kwanza tuone fursa tano ambazo vijana wanachezea. Hizi fursa, japo zinachezewa sasa hivi, hazikuwahi…
