-
Hakuna shida katika kupenda fedha…
Mara nyingi sana huwa nasikia watu wananiambia kuwa unaipenda sana fedha wewe? Au wengine huwa wanasema “unaijua hela”! Na Mimi huwa nawajibu kuwa “ ndiyo naipenda fedha ndiyo maana na yenyewe inanipenda”. Au huwa nawaambia nilizaliwa nayo. Ninachotaka ufahamu ni kwamba kitu ambacho hukipendi hakiwezi kukupenda wewe. Kama huipendi fedha, ndiyo maana wewe ni masikini…
-
Kutana na Mwajiriwa Ambaye Haitaji Mshahara Ila Anafanya Kazi Kwa Bidii. Nakushauri Baada Ya Kusoma Makala Hii Umwajiri Huyu Jamaa
Leo napenda kumtambulisha kwako mwajiriwa mtiifu kuliko wote duniani, anafanya kazi kwa saa 24 siku saba za wiki. Hadai mshahara wala marupurupu yoyote. Yeye anachojua ni kufanya kazi kwa bidii kila wakati na kutoa matokeo kadiri unavyomwelekeza. Nimekuwa namtumia mwajiriwa huyu kwa siku nyingi sasa na hizi ndizo sifa nilizobaini kwake. Anaweza kusalimia wateja, Anaweza…
-
Kitu Kimoja Ambacho Hujawahi Kuambiwa kuhusu Kufanya Makubwa
Kama unataka kufanya makubwa, unapaswa kuwa tayari kuishinda hofu na uoga unaokukabili unapoanza kufanya kitu hicho mwanzoni. Nakumbuka Kuna wakati nilikuwa naogopa na kujiuliza kwamba nitaongea nini nikukutana na mtu fulani. Ila cha kushangaza muda kidogo baada ya kukutana na mtu huyo mazungumzo yalikuwa yanajiendesha yenyewe kiasi kwamba nilikuwa sijiulizi nitaongea nini. Hapo ndipo…
-
USHAURI MUHIMU: Kama una ndoto ya kuwa mwandishi na unawaza nani ATAHARIRI, ATACHAPA na jinsi utakavyouza kazi zako Basi Soma hapa.
Siku ya leo najibu swali nililoulizwa na mmoja wa wasomaji wangu. Anasema; Hi Godius.Naitwa Juma Mazengo Malale, kwa sasa nipo Shinyanga, ndoto yangu nikuwa mwandishi wa vitabu. Mpaka sasa nipo kwenye mchakato, changamoto ipo kwenye mambo kama haya.1. Nani atahariri kazi yangu.2. Nani atachapa.3. Wapi nitauza.4. Nitamudu gharama5. Kitabu kibebe page ngapi? Habari yangu…
-
USIPOJITAMBUA, KUNA WATU WACHACHE WANAOJITAMBUA WATAKUTUMIA WANAVYOTAKA
Kuna stori moja ya mchungaji huko Nigeria, ambayo nimelazimika nikushikirishe kwa lengo la kukwambia kitu. Na stori hii ni ya mchungaji Dr. JS Yusuf wa Nigeria ambaye yeye ameanzisha utaratibu wa kuuza chupi kwa wanawake. Chupi hizi zina picha yake na anasema kwamba, mwanamke yeyote atakayevaa chupi hizi, atakuwa na mvuto kwa wanaume na ataweza…
-
Lengo Lako Kuu La Mwaka 2022 Ni Lipi? Au Ndio Unamwachia Mungu🤔?
Jana nilienda kumtembelea mwalimu wangu wa shule ya msingi ambaye kwa sasa ni mstaafu. Kama ilivyo kawaida ya watanzania wengi, nilipofika alifungulia runinga ili tuburudike kwa kuangalia manjonjo ya kimambele. Alifungulia channel ya Clouds na nilipoangalia tu kwenye kioo cha runinga nilikutana na swali lililosema, *Lengo lako kuu la mwaka 2022 Ni lipi? Au ndio…
-
Kheri ya mwaka mpya 2022
Huu ni mwaka ambao kwa hakika ulikuwa umeusubiria kwa hamu kubwa sana. Sasa hatimaye umefika. Wakati unajipongeza kwa mwaka mpya hakikisha1. Umeweka mipango dhabiti kwa ajili ya huu. Usiishi mwaka huu bila malengo. Ongozwa na malengo 2022. 2. Hakikisha unachagua kitu kimoja ambacho utakifanya kwa nguvu zako zote bila kuchoka mwaka 2022. Binafsi nimechagua…
-
Kama hujui unachotaka sasa hivi, ukikiona kesho hutakifahamu pia
Kuna watu huwa hawaweki malengo kwa kisingizio kwamba kitu chochote wanachotaka wakikiona watakifahamu. Ila ukweli ni kwamba, kama kitu unachotaka hukijui, hata kesho ukikiona hutakifahamu. Ndiyo maana inashauriwa uwe malengo kwa sababu yanakufanya uone unachotaka. Na chochote kile ambacho akili yako inaweza kuona, basi inaweza kukifikia. Tembelea blogu yangu kupitia SONGA MBELE BLOG
-
ANZA KIDOGO
Kama kuna kitu nimekuwa nasisitiza kila siku ni kuanza kidogo, kuanza na kile ulichonacho, kisha kuendelea kukuza hicho kidogo ili kutengeneza kikubwa zaidi. Ebu leo jiulize ni kitu gani kikubwa nimekuwa nataka kuanza kufanya ila sijaanza. Anza leo kidogo.
-
Masomo Matano Kuhusu Fedha Unayopaswa Kuyafahamu Katika Maisha
Fedha ni kitu ambacho kinahitajika sana kwenye maisha. Kila siku lazima tu utatumia fedha iwe ni katika chakula, mavazi, malazi, elimu, afya au maeneo mengine. Kutokana na umuhimu huo wa fedha, leo ninakuletea masomo matano muhimu kuhusu fedha, unayopaswa kuyafahamu. 1. Unapaswa kufahamu namna ya kutafuta, kutunza na kuwekeza fedha zako. 2. Fahamu kuwa…
-
Kitu Kinachoashiria Kuwa Hutafika Mbali Kimafanikio
Kuna vitu vingi ambavyo vinaashiria kuwa hutaweza kufika mbali kiuchumi, hata hivyo kimoja kikubwa sana kati ya vyote ni KUTOJIFUNZA. Kama hupati muda wa kujifunza na hasa kwa kusoma vitabu , jua hicho ni kiashiria cha wewe kuja kuanguka siku moja. Hili litatokea bila kujali unafanya kazi kwa bidii sana au una mtaji mkubwa, kwa…
-
Kitu muhimu cha kufahamu kwenye zama hizi za teknolojia
Tupo kwenye zama za teknolojia ambapo unaweza kufanya karibia kila kitu kwa mtandao. Unaweza kuongea na watu wa mbali kwa mtandao. Unaweza kuonana na watu wa mbali kabisa kwa njia hiihii ya mtandao unaweza kutuma na kupokea fedha na mambo mengine mengi. Kitu kimoja tu ambacho bado kimebaki na nguvu kubwa kwenye kipindi hiki ni…
-
Daah! 50 Cent Kwa Hili Kaua!!
Leo nimekikukumbuka kitabu cha the 50th Law kilichoandikwa na mwandishi nguli wa masuala ya vita, utawala na tabia za binadamu Robert Greene. Kitabu hiki amekiandika pamoja na 50 Cent na kiuhalisia kitabu hiki, kinazungumzia maisha ya 50 Cent na jinsi alivyoweza kufikia viwango vikubwa kimuziki na kimaisha. Kitu kimoja ambacho Waandishi Wa kitabu hiki…
-
KWA WAANDISHI WA VITABU:NI LUGHA GANI NZURI UNAPASWA KUTUMIA WAKATI WA KUANDIKA KITABU CHAKO?
Kuna watu huwa wanauliza ni lugha gani inafaa kutumia kwenye kuandika? Kiswahili au kiingereza? Jibu la swali hili ni vigumu kulipata kwa mtu mwingine, badala yake wewe mwenyewe unapaswa kuangaliaWatu uliowalenga. Kama wasomaji wako wanajua vizuri Kiswahili Basi waandikie kwa Kiswahili, au la kama wanauelewa na kiingereza waandikie kwa kiingereza. Kwa hiyo badala ya kujiuliza…
-
Waandishi Wa Vitabu: Igeni Kitu Hiki Kimoja Tu Kutoka Kwa Wasanii Muziki
Huwa napenda kusikiliza muziki wa bongo flava mara mojamoja ninapokuwa nimepumzika. Kama na wewe huwa unausikiliza walau hata mara moja moja nyoosha mkono juu tujuane. Ukifuatilia muziki huu hata kwa dakika tano tu, Kuna kitu kimoja ambacho utakigundua kwa wasanii na hiki ndicho ninataka tujadiliane leo. Kitu hiki siyo kingine bali ni kushirikisha kwa…
-
Majadala Mzito Kuhusu Kitabu Cha Kutoka SIFURI MPAKA KILELENI//GODIUS RWEYONGEZA
Siku moja nilishiriki kwenye mjadala kwenye kundi la KITABU CHAT. ambapo mada kubwa ilikuwa ni KILICHOMO NDANI KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI. Nilianza kwa kutoa utangulizi mfupi kuhusu kitabu hiki hapa cha kipekee sana. baada ya utangulizi na mae lezo machache, yalianza kuulizwa maswali. swali la kwanza kuulizwa lilikuwa ni hili hapa chini. “…mtu akifanya kazi…
-
KUZA KIPAJI CHAKO
Kipaji ni mauwezo fulani hivi ya asili ambayo mtu unazaliwa nayo na yanakuwezesha kufanya vitu kwa namna ya upekee sana. Mauwezo haya yanakutambulisha kwa watu kwa sababu hakuna mwingine ambaye anakuwa nayo. Na wala ya kwako hayawezi kulinganishwa na ya mtu mwingine. Sasa nikuulize wewe, kipaji chako unakifahamu? Ni kipi? Na je unakifanyia kazi? Hakikisha unakitumia…
-
Usiende Chuo Kusomea Uandishi Wa Vitabu; Badala Yake Fanya Hivi
Siku kadhaa zilizopita nilipokea simu ya mtu aliyekuwa anataka nimwambie chuo kizuri kinachonoa Waandishi Wa Vitabu. Nilimjibu vizuri tu, ila hakuridhika na majibu yangu kwa maana yalipingana na kile alichokuwa anaamini kwa asilimia 100. Yeye alitaka kwenda chuo, asomee uandishi na apate cheti. Cheti cha nini sasa? Najua, jamii yetu imezoea kwamba ukiwa na cheti…
-
FANYA UAMUZI SASA
Bila kujali upo katika hali gani, Kuna wakati unapaswa kufanya UAMUZI kwamba sasa mimi nitaanzia hapa na nitaendelea mbele Kataa kabisa kuendelea kusema kwamba sina mtaji Kataa kuendelea kulalamikia ugumu wa maisha. Chagua kuanzia hapo ulipo, miaka 10 ijayo utajishukuru kwa uamuzi huu. Amua Sasa kupata vitabu vitano kwa elfu kumi tu. Hii ofa mwisho…
-
Kinachotokea Unapokuwa Na Ndoto Kubwa
Jana niliandika makala yenye vitu 9 ambavyo hupaswi kuchoka kufanya. Mmoja wa wasomaji wa amkala hiyo alinibu kwa kusema hivi Nami nikawa nimemjibu pia kwa ujumbe huu hapa chini Ni kweli unapokuwa unapambania ndoto kubwa watu watakuona mtu wa ajabu sana. Watakuona kichaa, utaambiwa umechnganyikiwa na mambo mengine mengi. Na hili linawatokea watu wote wenye…
