-
Mfungo
Sizungumzii mwezi wa Ramadhan, wala Kwarezima. Nazungumzia mfungo. Kwamba kuna kitu ulikuwa unafanya, ila kinakutoka kwenye mstari wa kufanyia kazi malengo na ndoto zako kubwa. Sasa unaamua kwamba nafuga na ninaacha kukifanya kwa wiki moja. Kwa mfano ulikuw aunatumia muda mwingi facebook, au youtube au tiktok, unaamua sasa kwa wiki moja ijayo naondoa hii tiktok…
-
Twende kidijitali mwaka 2025
Rafiki yangu, najua umekuwa unatumia mtandao wa intanenti kwa muda. Lakini kitu ambacho sina uhakika nacho ni kama umekuwa ukiutumia mtandao huu kwa manufaa. Sasa, 2025 twende kidijitali rafiki yangu. Unajua kwa nini nakwambia hivi, kadiri siku zinavyokwenda, mambo yanazidi kufanyika kidijitali zaidi. Mfano, siku hizi unaweza kuwa nyumbani asubuhi mpaka jioni na mambo yote…
-
Kufufuka
Kheri ya pasaka rafiki yangu. Kwa wakristo pasaka, ni kufufuka. Hata kama wewe siyo mkristo, bado hapa kuna kitu cha kujifunza. Na kitu hiki siyo kingine bali ni kufufuka. Nataka na wewe ufufuke. Kwenye maisha ya kila siku tunaanguka. Tunakumbana na vikwazo vingi ambavyo vinatuzuia kusongambele na kufanya makubwa. Tunaanzisha biashara zinakufa. Muda mwingine mahusiano…
-
Pale unapokuwa huoni matokeo
Ni rahisi kuacha kufanya pale unapokuwa huoni matokeo ya haraka. Ila ukweli ni kuwa kamwe usiache kufanya kwa sababu tu huoni matokeo ya haraka, badala yake endelea kukaza. Kukomaa kwa muda mrefu kutakuweka kwenye hali ya kupata matokeo mazuri kuliko vile unavyofanya kwa muda mfupi na kuacha. Mfano, ukiwekeza mara moja na kuacha, au ukiweka…
-
Nguvu ya Kuweka Malengo-1
Unapokuwa na malengo unapambana kwa vyovyote vile kuhakikisha unayafanikisha malengo Yako ndani ya muda husika. Ila ukiwa huna malengochochote kinachotokea mbele yako ni lengo. Hivyo basi jitahidi kuhakikisha kuwa na malengo, weka malengo yafanyie kazi. kumbuka usipokuwa na malengo, chochote kitakachotokea mbele yako kitakuwa ni lengo.
-
NGUVU YAKO KUBWA IWEKE HAPA
Rafiki yangu, nguvu yako kubwa iweke kwenye kile unachofanya. Badala ya kuiweka nguvu kubwa kwenye vitu ambavyo hupendi. Inawezekana kuna vitu hupendi kwenye siasa, kwenye michezo na mabo mengine. Ila ukwlei ni kuwa nguvu yako kubwa inapaswa kuwekwa kwenye vitu ambavyo unapenda. Kama ni biashara, hapo ndipo unapaswa kuwekeza nguvu zako. Kama ni kazi, iwekeze…
-
Namna ya kupangilia ratiba ya wiki hii kiporofessional
Namna ya kupangilia ratiba ya wiki hii kiporofessional Rafiki yangu mpendwa, salaam Miongoni mwa ujuzi muhimu sana ambao unahitaji ili kufanikisha malengo Yako ya mwaka 2025 ni ujuzi wa kuipangilia wiki yako. Wiki ni ndogo sana ila usipoipangilia vizuri inapotea na ukipoteza wiki nyingi mfululizo, mwisho wa siku unakuwa umeupoteza mwaka wako. Maana mwaka una…
-
Jinsi Ya Kuandaa Kizazi Cha Wafanyabiashara
Juzi nilikuwa nasoma ujumbe wa mkurugenzi mkuu wa TELEGRAM.Alizungumzia namna kampuni za kichina zinavyofanya vizuri na namna ambavyo zitafanya vizuri kwa siku zijazo kutokana na mfumo mzuri wa elimu walionao. Kitu hiki kimenitafakatisha sana na Leo nikaona nikuandalie ujumbe muhimu wa namna Leo hii tunavyoweza kuanza kuandaa kizazi kijacho Cha wajasiriamali, kizazi ambacho kinaweza kwenda…
-
Njia Bora Ya Kufanya MAKUBWA Ni Hii by Godius Rweyongeza
Pengine umekuwa unajiuliza ni kwa namna gani naweza kufanya makubwa kwenye maisha yangu? Ukweli ni kuwa haya makubwa unayotamani kuyafanya kwenye maisha yako, hayawezi kuja tu yenyewe bila ya wewe kufanya kazi. Njia bora ya wewe kufanya makubwa ni kwa wewe kuhakikisha kwamba unatoka hapo ulipo na kwenda kufanya kazi. Kwenye ulimwengu wa leo sambamba…
-
ukijua kitu kifanyie kazi
Utasikia mtu anakwambia kwamba hiki nakijua, nilijifunza chuo. Hiki nakijua… Kama unakijua kwa nini hukifanyii kazi? Rafiki yangu kitu kikubwa ninachotaka kukwambia siku ya leo ni kwamba kujua pekee hakutoshi. Unapaswa kujua vitu na kuvifanyia kazi pia. Hiyo ndiyo inaenda kuwa tiketi yako wewe kukfanya makubwa. Haitoshi tu kwa wewe kujua kuweka akiba, bila ya…
-
Nguvu ya kushambulia
Kwenye timu ya mpira wa miguu huwa kuna wachezaji wa aina mbalimbali ila mojawapo ya wachezaji huwa ni washambuliaji. Hawa kazi yao huwa ni kuhakikisha muda wote wanasumbua kwenye lango la mpinzani ili mwisho wa siku waweze kuipatia timu yao ushindi. Endapo washambuliaji hawatafanya kazi yao ya kushambulia na badala yake wakaanza kujilinda dhidi ya…
-
Shukrani
Moja ya kitu muhimu sana ambacho unapaswa kukifanyia kazi ni kuwa mtu wa shukrani. Kila siku inayokuja kwako ni nafasi nyingine ya wewe kushukuru. Una mengi ya kushukuru kwenye maisha yako. Wengi huwa wanasubiri mpaka waone mambo makubwa ili waweze kushukuru. Ila ukweli ni kuwa kwa mambo yanayoendelea kwenye maisha yako, una mengi ambayo leo…
-
Watu
Ili ufanikiwe unahitaji watu, tena watu sahihi. Hivyo basi rafiki yangu, pambana kuzungukwa na watu sahihi. Ukikaaa na watu ambao siyo sahihi watakuangusha. Unajua kwa nini watakuangusha, watakuangusha kwa sababu fikra zao ni za kuanguka wala siyo za kuinuka. Inabidi ukae na watu wenye fikra za kuinuka, ili uinuke. Swali langu kwkao siku ya leo…
-
Usikose mara mbili
Rafiki yangu, kwenye makala ya jana nilikusisitiza kitu kimoja muhimu sana. Kitu hiki ni kufanya kila unachofanya kwa msimamo, na kwa mwendelezo. Kama hukusoma hii makala, rudi hapa uisome kwa umakini mkubwa. Msimamo na mwendelezo. Kitu hiki ni kutokuacha kufanya kitu husika zaidi ya mara mbili. Ikitokea kuna siku umeshindwa kufanikisha kitu fulani ambacho umepanga…
-
Msimamo na mwendelezo
Rafiki yangu moja ya kitu cha muhimu sana kwa wewe unayetaka kufanya makubwa ni kuwa na mwendelezo kwenye kitu ambacho unafanya. Wengi huwa wanaweza kufanya kitu mara moja, ila siyo kwa mwendelezo. Wewe unahitaji kuwa na mwendelezo kwenye kazi na shughuli zako zote unazofanya. Ukianzisha kitu, usikifanye mara moja tu. Bali kifanye kwa mwendelezo kwa…
-
Mwezi januari unaisha, umeulaani au umeubariki? Umekuwa wenye Baraka kwako au wenye karaha?
Rafiki yangu mpendwa, nichukue nafasi hii kukupongeza sana kwa kuumalizia mwezi wa Januari. Najua wazi kuwa haujawa mwezi rahisi, hivyo nikupongeze sana kwa hilo. Mwezi januari unapofikia tamati, ningependa kwa pamoja tufanye tafakari kuhusiaa na mwezi huu wa kipekee. Mwisho wa siku tujiulize kuwa mwezi huu umeubariki au umeualaani? Umekuwa wenye Baraka kwako au wa…
-
Hii Kozi Nayo Inalipa Vizuri Sana; Sema Watu Hawaijui Tu
Moja ya kitu ambacho wazazi bado wanawaambia watoto ni kwenda kusomea kozi au kitu fulani kwa sababu wanahisi kinalipa. Mzazi anamwambia mwanae akasomee uhasibu kwa sababu yeye anahisi unalipa kuliko vitu vingine vyote, au anadhani mtoto wake atapata ajira. Nafikiri ushauri wa namna hii ulikuwa ni ushauri halisi miaka kadhaa iliyopita, ila leo hii hauwezi…
-
JICHANGAMOTISHE
Uliwahi kufanyika utafiti kwa madereva waliokuwa wanaendesha taxi zao kwenye jiji la LONDON, moja ya kitu cha kipekee sana kilichogundulika kwa madereva hawa wa jiji la LONDON ilikuwa ni kwamba ubobgo wao ulionekana kuwa imara sana, ukilinganisha na madereva wengine ambao walikuwa hawaendeshi magari yao kwenye mazingira yenye barabara nyingi na idadi kubwa kama London.…
-
Huhitaji kusubiri mpaka uwe na kila kitu
Ni mara nyingi sana watu huwa wanasubiri mpaka wawe na kila kitu ili waweze kuanza kuanza kufanyia kazi malengo yao, ndoto zao, au kitu ambacho wanafikiria. Mtu haanzi hiyo biashara kwa sababu anasubiri mpaka aweze kupata kila rasilimali ambayo anafikiri anahitaji. Mtu haanzi kufanyia kazi hicho kipaji chake kwa sababu anasubiri mpaka awe na kila…
-
Maswali Mawili Ambayo Unapaswa Kujiuliza Kila Siku
Rafiki yangu, kuna maswali mawili mazuri sana ambayo unapaswa kuwa unajiuliza kila siku. Haya maswali yatakufanya utafakari juu ya mambo mengi ambayo unafanya kila siku na namna gani unaweza kuendelea kuifanya hii dunia kuwa sehemu bora kabisa kuwahi kutokea. Maswali haya tunayapata kutoka kwa Benjamin Franklin ambaye alikuwa ni mmoja wa wanasiasa, mvumbuzi na mwanadipolomasia…
