Category: A NOTE FROM SONGAMBELE

  • Sababu 15 kwa nini haupaswi kuwa na plan B

    Kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 kuikuwa na utani ambao ulikuwa unasambaa mtandaoni. Mmoja wa watu alitengeneza meme fulani hivi ambayo ilikuwa ikimwongelea waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa. Ilikuwa inasema kuwa kila mara unapaswa kuwa na Plan B kama Lowassa. Amekatwa CCM asigombee urais, amehamia CHADEMA, na sasa akishindwa kuingia ikulu kwa tiketi ya CHADEMA anahama…

  • Viashiria 15 kuwa kipaji chako kitakufikisha mbali

    Rafiki yangu mpendwa karibu sana kwenye makala ya siku ya leo. Na leo tunaenda kuona viashiria 15 vinayoonesha kuwa kweli hiki kipaji chako ulichonacho kinaenda kukufikisha mbali. 1. upo tayari kuanza kidogo Kama upo tayari kuanza kidogo kisha kuendelea kukifanyia kazi kipaji chako ili kuhakikisha kwamba unakikuza na kukifikisha juu zaidi, basi hiki ni kiashiria…

  • Vitu 21 Ambavyo Ni Lazima Kufanya Hata Kama Una Kipaji Kikubwa

    Rafiki, una kipaji si ndio! Hongera sana, mbali na kuwa una kipaji na unakifanyia kazi na una maono makubwa ya kukipeleka mbali kipaji chako mpaka kwenye ngazi za kimataifa. Ila kuna vitu vya msingi sana ambavyo hupaswi kuacha kufanya hata kama una kipaji kikubwa. kwenye hii sura ninaenenda kukushirikisha vitu 21 ambavyo hupaswi kuacha kufanya…

  • Vitu vitano (05) Vitakavyokufanya uheshimike

    Rafiki yangu bila shaka unaendelea vyema kabisa. siku ya leo ningependa kukushirikisha vitu vitano ambavyo vitakufanya wewe uweze kuheshimika kwenye kazi, kwenye mahusiano na kwenye maisha kiujumla. Kwa hiyo, kama unataka kuheshimika rafiki yangu, hivi hapa ni vitu vitano ambavyo unapaswa kuanza kufanyia kazi mara moja. 1. KITU CHA KWANZA NI KUCHAPA KAZI Kazi ni…

  • Tofauti Kati Ya Kazi na Ajira

    Kazi ni kitu ambacho kinampa mtu heshima. Na hata maandiko mbalimbali yamethibitisha na kusisitiza hili la kufanya kazi kwa namna tofauti tofauti, huku maandiko maarufu yakiwa yale yanayosema kwamba asiyefanya kazi basi asile. Rafiki yangu, kazi ni moja ya kipimo cha utu. Kwa hiyo, kama unataka kuheshimika kwenye jamii, basi fanya kazi. Kwa watu wengi…

  • Vitu Viwili Kuhusu Kipaji Ambavyo Hakuna Mtu Amewahi Kukwambia

    Jana nilikuwa naangalia mahojiano kati ya mtengenezaji wa maudhui kutoka Ghana maarufu sana kama Wode Maya na msanii wa Zimbabwe Jah Prayzah. Kuna mengi waliyongea ila mimi binafsi niliondoka na mawili ambayo yamenigusa na ambayo nimeona nikushirikishe na wewe. Kitu  cha kwanza kabisa Jah Prayzah alisema hivi, mimi sikuchagua kuwa msanii ila nilichaguliwa kuwa msanii.…

  • Kitu hiki kimoja kitakutofautisha wewe na watu wengine wenye kipaji kama cha kwako

    Kama kuna kitu ambacho kinaweza kukutofautisha wewe na watu wengine wenye kipaji kama cha kwako basi kitu hiki siyo kingine bali ni kujifunza na kulielewa eneo ambalo unafanyia kazi kwa undani zaidi kuliko mtu mweingine yeyote. Yaani, unahakikisha kuwa taarifa zote za  muhimu kuhusana na kipaji chako unakuwa nazo na unazitumia kwa manufaa kuhakikisha kwamba…

  • Hiki kitu Kimoja Tu, Kitakufanya Utumie Kipaji Chako Kwa Viwango Vikubwa

    Leo asubuhi nimeamka na kuangalia video moja ambayo Kobe Braynat alikuwa akihojiwa na Patrick Bet-David. Moja ya swali ambalo Kobe Brayant aliulizwa ni kuwa ni msukumo gani ambao umekuwa ukimsukuma kujituma na kuhakikisha anakuwa jinsi anakuwa mchezaji bora. Kati ya mengi ambayo ameongea, kitu kikubwa amesema sitaki siku moja nije nianze kujuta kuwa ningeweza kuwa…

  • Sababu Sita Zisizopingwa Kwa Nini Unapaswa Kuendeleza Kiapaji Chako

    Kwenye kitabu cha Acres of Diamond, mwandishi ameeleza historia ya jamaa ambaye aliambiwa kuwa ukiwa na almasi yenye ukubwa kidole unaweza kuimiliki dunia. Huyu jamaa kusikia hivyo, aliamua kusafiri kwenda kuitafuta dhahabu ambayo mwisho wa siku hakuipata! Siku hizi bado watu wanatafuta dhahabu! Utasikia watu wanapeana stori kuwa ukienda kwenye machimbo ya Geita au Mererani…

  • Jinsi Ya Kutangaza Kipaji Chako

    Moja kati ya kitu ambacho nimekuwa nikiwaambia watu wengi ni kuwa tuna bahati ya kuishi kwenye ulimwengu wa leo tunaoishi. Mababu zetu wangekuwa wanarudi leo hii na kuona fursa kibao zilizotuzunguka, ni wazi kuwa wenyewe wangetuonea gere. Mambo ambayo miaka hiyo yalikuwa hayawezekani, leo hii yanawezekana, tena siyo kwamba yanawezekana kidogo, yanawezekana sana tu. Ebu…

  • Jinsi Ya Kushughulika Na Fedha Unazopata Kutokana Na Kipaji Chako

    Limekuwa ni kama jambo la kawaida kusikia watu waliokuwa na vipaji na watu ambao wakati fulani walikuwa wakiingiza fedha nzuri kupitia vipaji vyao wakiwa hawana fedha. Vyombo vya habari, vimekuwa vikiripoti kuwa hawa watu hawana fedha na muda mwingine kupitisha mchango ili hawa watu waweze kupata mahitaji yao ya muhimu au hata kupata sehemu ya…

  • Jinsi Kizazi Kinachostaafu Kinavyoweza Kuandaa Kizazi Kijacho

    Mara kwa mara nimekuwa nakutana na watu wazima wenye umri wa miaka 50 na zaidi au niseme watu walio kwenye umri wa miaka ya kustaafu, kila ambapo nimekuwa nikiongea na watu hawa kuhusiana na vipaji basi wenyewe moja kwa moja wamekuwa wakiniambia kuwa umri wao umeshaenda, hivyo kwao huu sio muda tena wa wao kunoa…

  • Ukipenda pesa, lazima upende na kazi

    Rafiki yangu mpendwa, vitu vingi vilivyo hapa duniani huwa vinaenda viwili viwili.Mfano ukiongelea juu, lazima kuwepo chini.Ukisema mbele lazima kuna nyumaUkizungumzia kulia sharti kuwepo kushoto pia Sasa hiki kitu kina funzo kubwa sana kwetu na hasa kwenye kutafuta fedha na mafanikio.Na ujumbe ni kuwa ukipenda fedha lazima upende kazi. Ni wazi kuwa huwezi kupata fedha…

  • KIPAJI NI DHAHABU:Jinsi Ya Kukigundua, Kukinoa Na Kukitumia Kipaji Chako Kwa Manufaa

    ∞∞∞∞∞UTANGULIZI∞∞∞∞∞   Nakumbuka mwaka 2013 nilikutana na vijana wenzangu ambao walikuwa kwenye mjadala mkali kuhusiana na Messi, Ronaldo na Neymar. Kwenye mjadala huu walikuwa wakijadili kuhusiana na uwezo wa wachezaji hawa, huku wengine wakisema kwamba Messi na Neymar wana kipaji ila Ronaldo akiwa anatumia nguvu. Nadhani kama wewe ni mpenzi wa soka, mijadala kama hii…

  • Ugunduzi mkubwa wa Zama Hizi…

    Rafiki yangu moja ya ugunduzi mkubwa wa Zama Hizi ni kuwa wewe unaweza kubadili maisha yako na kuwa vyovyote vile unavyotaka.Unaweza kuwa TajiriUnaweza kuufikia Uhuru wa KifedhaUnaweza kuwa na mahusiano mazuriUnaweza kuwa na familia bora n.k. Rafiki yangu yangu, hakuna ukomo wa vile unavyoweza kuwa au kufikia kwenye maisha. Labda tu ukijiwekea ukomo wewe mwenyewe.…

  • Usifanye kitu mara moja…

    Kama unataka kubobea kwenye kitu, usifanye hicho kitu mara moja. badala yake kifanya mara kwa mara na kwa mwendelezo. Kadiri unavyofanya kitu au kazi mara kwa mara inakupa nguvu na ufanisi na hata kujiamini. Marudio yako kwenye kufanya kazi yanakufanya uzidi kubobea na hatimaye unakuwa bingwa. Mchezaji bora wa mpira wa miguu siyo yule ambaye…

  • Uchambuzi Wa Kitabu: 25 Hours a Day; Going One More to Get What You Want

    Mwandishi: Nick BareMchambuzi: Hillary MrossoSimu: 255 683862481 UTANGULIZIKaribu katika uchambuzi wa kitabu bora sana cha 25 Hours a Day. Kikiwa na maana ya kwenda hatua moja zaidi kupata kila unachokitaka. Mwandishi ametumia uzoefu wake wa kijeshi kutengeneza nidhamu kubwa kwenye maisha yake binafsi, maisha ya biashra na mafanikio. Kama unavyojua jeshini kikubwa ni nidhamu ya…

  • Aina Tatu Za Ujuzi Unaohitaji Ili Kuongeza Thamani Yako Na Kula Mema Ya Nchi

    Kwenye hii makala ningependa tuongelee aina tatu za ujuzi ambao ukiwa nao kwenye hizi zama ni wazi kuwa unaenda kufanya vizuri na hata kuweza kufikia viwango vikubwa na vya hali ya juu sana kuliko unavyotegemea. Najua umewahi kushauriwa kujifunza aina nyingi za ujuzi, ila kwenye aina hizo zote za ujuzi ambao umewahi kushauriwa kuwa nao,…

  • Kitabu ChaNGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA: Utangulizi wa kitabu kama ulivyoandika kwenye kitabu chenyewe

    Habari ya siku ya leo rafiki yangu, siku ya leo ningependa nikushirkishe Utangulizi wa kitabu cha NGUVU ya vitu vidogo kama ulivyoandikwa kwenye kitabu chenyewe. Nina hakika wewe mwenyewe utaufurahia, baada ya kuwa umesoma Utangulizi huu, usisite kujipatia nakala ya kitabu hiki kwa kuwasiliana nami mwandishi kwa simu 0755848391. Sasa utangulizi wenyewe huu hapa chini.…

  • Vitabu Viwili Unavyopaswa Kuhakikisha umesoma mwezi huu wa tisa

    Habari ya leo rafiki yangu, siku ya leo ningependa kwa ufupi nikwambie vitabu vitano ambavyo unapaswa kusoma ndani ya mwezi huu wa tisa. Bila kupoteza muda, vitabu vyenyewe ni 1. The school of money Hiki ni moja ya kitabu muimu sana ambacho unapaswa kusoma hasa kuhusiana na suala zima la fedha. Kitabu hiki ndani yake…

X