Category: A NOTE FROM SONGAMBELE

  • Kitu Hiki Ndicho Kinawafanya wengi washindwe kufanya makubwa

    Habari ya leo rafiki yangu, bila shaka unaendelea vyema kabisa. Leo ningependa nikwambie kitu ambacho kimekuwa kinawakwamisha watu wengi na kuwafanya washindwe kufanikisha makubwa . Kitu Hiki siyo kingine bali ni kukosa malengo makubwa ambayo wanayafanyia kazi kwenye maisha yao. Ili uweze kunielewa vizuri hapa naomba nianze kwa kukupa mfano wa kawaida tu, unaweza kukuta…

  • Jinsi ya kupata mafunzo yenye hadhi ya chuo

    Brian Tracy anasema kuwa muda ambao tunautumia kwa siku tukisafiri na Kutembea kutoka eneo moja kwenda jingine, ukiuunganisha baada ya mwaka mmoja Ni sawa na semester moja ya chuo! Hii ndio kusema Kuwa ukiutumia vizuri huu muda, kujifunza. Baada ya mwaka utakuwa umepata kozi yenye hadhi ya semester ya chuo. Nataka hili likutafakatishe uanze kuona…

  • Leo ni siku ya waandishi duniani: Mambo mawii unayopaswa kufahamu

    Habari ya siku ya hii ya kipekee sana rafiki yangu. leo ni siku ya waandishi duniani. Mimi ni kiwa mmoja wa waandishi, hii siku inanihusu sana. lakini pia inakusu wewe, maana hakuna mwandishi bila msomaji. Hivyo, siku ya leo ni siku yetu sote. Kwa hiyo, nitakuwa sijakosea kusema kwamba kheri ya siku ya waandishi kwako!…

  • Usipokata tamaa…

    Mwisho wa siku usipokata tamaa, ukiendelea kuweka juhudi na kujituma bila kurudi nyuma, matokeo utayaona. Kwa hiyo ujumbe wangu kwako siku ya leo Ni kuwa endelea kuweka juhudi zaidi kwenye Kazi. Yajayo yanafurahisha.

  • Vitu viwili ambavyo huwafanya watu washindwe kupiga hatuaRafiki yangu, bila shaka unaendelea vyema.

    Rafiki yangu, bila shaka unaendelea vyema. Mimi hapa nilipo, niko sawa kabisa. Kuna vitu viwili kwenye maisha ambavyo huwafanya watu washindwe kufanikisha malengo na ndoto zao. Lengo la mimi kukwambia vitu hivi ni kuwa wewe unapaswa kuvifahamu hivi vitu viwili na kuviepuka, la sivyo utaishi maisha ya kawaida Kama ambavyo watu wengine wanaishi. Vitu hivyo…

  • Vitu viwili ambavyo hakuna MTU anapaswa kukuzidi

    Rafiki yangu, SIKU ya leo ningependa kukwambia vitu viwili ambavyo hakuna MTU anapaswa kukuzidi kwenye kuvifanya. Vitu hivi ni 1. Kufanya kazi kwa bidiiAcha watu wakuzidi kwenye mambo mengine yote ila wasikuzidi kwenye kufanya kazi kwa bidii. Kufanya kazi kwa bidii kupo ndani ya uwezo wako. Kwa hiyo kuanzia leo, acha watu wakuzidi kwenye vitu…

  • FANYA MAZOEZI

    Siku moja nilikuwa nasoma makala mtandaoni, kwenye makala hiyo mwandishi akawa amesema kwamba Michael Jackson ambaye ni gwiji kwenye muziki wa hiphop alikuwa ni mmoja watu waliokuwa wanafanya mazoezi kwa muda mrefu sana kabla ya kuonekana mbele ya watu. Kwa baadhi ya watu kitu hiki kilionekana cha ajabu sana, Ukilingananisha na kuwa Michael Jackson alikuwa…

  • Hii ndiyo sababu kuu kwa nini unapaswa kutoa thamani kubwa kuliko mteja anavyokulipa

    Ni miaka kama mitano hivi imepita tangu nimegundua kanuni moja muhimu sana ambayo nimekuwa naitumia kwenye kila kitu ninachofanya. Na kanuni hii siyo nyingine bali ni kutoa thamani kubwa zaidi kwa mteja kuliko mteja anavyolipia. Tangu nimegundua kanuni hii nimekuwa naitumia kwenye vitabu vyangu vyangu vyote. Ambacho nimekuwa nafanya ni kuwa, kwa kitabu ambacho mteja…

  • Hii ni tabia muhimu unayopaswa kuanza kuishi nayo kuanzia leo hii. (usishike simu kama kitu cha kwanza unapoamka asubuhi, na wala usishike simu kama kitu cha mwisho kabla ya kwenda kulala).

    Siku zinazidi kusogea kwelikweli. Mwaka uliokuwa mpya sasa hivi, tumeshaanza kuuaga taratibu. Siku siyo nyingi utaingia mtaani na kuanza kuzisikia nyimbo za krismasi zikipigwa. Ukiona hivyo, ujue kwamba mwaka unazidi kusogea na na siku siyo nyingi tutakuwa tunauaga. Lakini kabla mwaka huu haujaisha, kuna tabia ambayo ningependa uanze kuifanyia na kuachana nayo TABIA YA KUTOSHIKA…

  • Je, kuuza vitu vya bei rahisi ni njia kutengeneza fedha nyingi kwa sababu bidhaa zinatoka kwa haraka?

    Mara kwa mara nimekuwa naandika kwenye blogu yangu na kutolea mfano namna ambavyo Bakhresa na Mo Dewji wanauza bidhaa za bei ya chini. mfano watu hawa unakuta wanauza mpaka viberiti, chumvi, pipi na vinginevyo ambavyo vinauzwa shilingi 50, 100, 200 mpaka 500. Nimekuwa nikitumia mfano huu kuhamasisha vijana mbalimbali kwamba wasidharau fedha kwenye maisha, badala…

  • KUWA ORIGINAL

    Siku moja mwaka 2016 wakati naanza uandishi nilikaa mezani na kufikiria kitu cha kuandika, ila nikawa nimeshindwa namna ya kuanza kuandika na hata nikawa sielewi nawezaje kuendelea kuandika. Baada ya kukaa kwa muda bila kuona matokeo yoyote yale, niliamua kuingia whatsap na nikawa nasoma makala za hapa na pale. Hapo ndipo nikakukutana na makala ya…

  • Maisha hayana fomula ila yanakuhitaji uwe na fomula

    Siku moja dereva mmoja wa bodaboda alikuwa anaendesha bodaboda yake kutoka eneo moja kwenda  jingine. Akiwa njiani, alipata ajali akawa ameanguka chini. watu walikimbia haraka kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wanamsaidia. Kitu cha kwanza watu walichoona ni shingo kupinda. Hivyo, walianza harakati za kumpa huduma ya kwanza na hapa waliamua kurudsha shingo kwenye eneo lake.…

  • Subscribe kwenye channel yangu ya YouTube Sasa.

    Rafiki yangu, hivi unajua kwamba huwa natoa baadhi ya mafunzo kwenye channel yangu ya youtube? Mara kwa mara nimekuwa nikitoa mafunzo huku. Na wewe unaweza kuyafuatilia kupiatia hapa. Subscribers kwenye channel hii walikuwa bado hawajafika hata elfu moja 😂😂, ila wiki hii ni muda wa kufanya hivyo, au wewe unasemaje? Bado watu 50 tu. wewe…

  •  Sababu Tano (05) kwa nini unapaswa kuukataa umasikini

    Limekuwa ni  kama jambo la kawaida kusikia watu wanajiita masikini, wanyonge. Kuna watu wanajisifia kuwa masikini kama vile kuwa maskini jambo la kheri au jambo la sifa. Kwa kulifahamu hili, siku ya leo ningependa kukupa sababu 15 kwa nini unapaswa kuukataa umasikini. Kweli kabisa, unapaswa kuukataa umasikini kwa nguvu zako zote. Kwanza kwa sababu umasikini…

  • Kwa Nini Watu Wenye Kipaji Hushuka Kiwango

    Nadhani umewahi kusikia hili, kuwa wachezaji au wasanii au hata wawekezaji wameshuka viwango. Unakuta mtu mwanzoni alikuwa na kipaji na uwezo mzuri sana ambao alikuwa akiutumia kwa viwango vikuwa na viwango vya hali ya juu, ila kadiri siku zinavyoenda basi mtu huyo anazidi kushuka viwango mpaka kufikia hatua ambapo inadhihirika kuwa kiwango chake kimeshuka. Sasa…

  • Uchambuzi wa Kitabu: The Leader Who Had no Title (Kiongozi Asiye na Cheo); Mambo 200 Niliyojifunza katika kitabu hiki.

    Mchambuzi: Hillary MrossoMawasiliano: 255 683 862 481 UtanguliziDhana ya uongozi imekuwa na maana nyingi, na watu wengi hawajui maana halisi ya uongozi, wengi wameshindwa kufanya makubwa, wengi wameshindwa kufanya maamuzi muhimu kwenye maisha yao kwasababu wanajiona hawapo kwenye nafasi ya kufanya hivyo. Mwandishi wa kitabu hiki, Robin Sharma anaweka wazi maana halisi ya uongozi, amefafanusha…

  • Sababu tano kwa nini utahitaji kutoa kitabu chako kwa njia ya mtandao kwanza kabla ya kukitoa kwa njia ya nakala ngumu

    Unapozungumzia kutoa kiytabu chako kwa mfumo wanakala laini, basi swali ala kwanza ambalo watu huwa wananiuliza ni kuwa vipi kuhusu hakimiliki? Hili huwa ni swali kubwa sana ambalo watu huwa wanauliza. Kwenye makala ya leo ningependa kuongelea kwa nini unapaswa kutoa kitabu chko kwa mfumo wa nakala laini kwanza kabla ya kutoa kitabu hicho kwa…

  • Watu hawawezi kukupuuza siku zote

    Siku ya leo nina ujumbe mfupi kwako rafiki yangu. Na ujumbe wangu Ni kwamba kama wewe unapambamia lengo au ndoto yako na unalifanyia kazi mara kwa mara, basi Kaa ukijua kuwa watu hawatakupuuza siku zote. Ndio wanaweza kukupuuza mara moja au mara mbili, Ila hawatakupuuza siku zote. Kuna siku watanyoosha mikono juu na kusema ngoja…

  • Sifa mbili ambazo ukiwa nazo, basi mafanikio kwako ni suala la muda tu

    Siku ya leo ningependa nikueleze sifa mbili ambazo ukiwa nazo, basi ujue kuwa mafanikio kwako litakuwa ni suala la muda tu. unajua sifa hizi ni zipi.. Sifa ya kwanza ni sifa ya kufanya kazi kwa bidii Hakuna kitu chochote kile unachoweza kupata bila ya kufanya kazi, tena siyo tu kufanya kazi, bali kuhakikisha kwamba umefanya…

  • Mwonekano wa Bustani Yangu

    Leo asubuhi nilienda bustanini kwangu. Wakati nikiwa bustanini, nilimtafuta rafiki yangu ambaye katika kuchati naye nikamwambia nipo bustanini. Na hapo nikamrekodia video fupi ya mwonekano wa Bustani yangu. Sina shaka na wewe ungependa kuiona. Na hata pengine kusema mawili matatu kuhusu hii Bustani. Japo nilikuwa sijapanga kurekodi video siku ya leo. Ila naamimi utakachoona utapata…

X