Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Kheri ya mwaka mpya 2022

     

    Huu ni mwaka ambao kwa hakika ulikuwa umeusubiria kwa hamu kubwa sana. Sasa hatimaye umefika. Wakati unajipongeza kwa mwaka mpya hakikisha
    1. Umeweka mipango dhabiti kwa ajili ya huu. Usiishi mwaka huu bila malengo. Ongozwa na malengo 2022.

    2. Hakikisha unachagua kitu kimoja ambacho utakifanya kwa nguvu zako zote bila kuchoka mwaka 2022. Binafsi nimechagua kuandika na kuweka NGUVU zaidi kwenye uandishi, mwaka huu tegemea makubwa kwa upande wa maandiko yangu.

    Hayo ndiyo machache niliyotaka nikushikirishe leo.

    Mwaka huu ukawe mwaka bora kwako.

    GODIUS RWEYONGEZA
    0755848391
    Leo naandika nikiwa Bukoba-Tanzania

  • Kama hujui unachotaka sasa hivi, ukikiona kesho hutakifahamu pia

     

    Kuna watu huwa hawaweki malengo kwa kisingizio kwamba kitu chochote wanachotaka wakikiona watakifahamu.  Ila ukweli ni kwamba, kama kitu unachotaka hukijui, hata kesho ukikiona hutakifahamu.

    Ndiyo maana inashauriwa uwe malengo kwa sababu yanakufanya uone unachotaka. Na chochote kile ambacho akili yako inaweza kuona, basi inaweza kukifikia.

    Tembelea blogu yangu kupitia

    SONGA MBELE BLOG

  • ANZA KIDOGO

     

    Kama kuna kitu nimekuwa nasisitiza kila siku ni kuanza kidogo, kuanza na kile ulichonacho, kisha kuendelea kukuza hicho kidogo ili kutengeneza kikubwa zaidi.

    Ebu leo jiulize ni kitu gani kikubwa nimekuwa nataka kuanza kufanya ila sijaanza. Anza leo kidogo.

  • Masomo Matano Kuhusu Fedha Unayopaswa Kuyafahamu Katika Maisha

     

    Fedha ni kitu ambacho kinahitajika sana kwenye maisha. Kila siku lazima tu utatumia fedha iwe ni katika chakula, mavazi, malazi, elimu, afya au maeneo mengine.

    Kutokana na umuhimu huo wa fedha, leo ninakuletea masomo matano muhimu kuhusu fedha, unayopaswa kuyafahamu.

    1. Unapaswa kufahamu namna ya kutafuta, kutunza na kuwekeza fedha zako.

    2. Fahamu kuwa maisha ni wajibu wako Wala siyo mzazi, mme, mke, shangazi n.k.
    Ukishindwa ni juu yako na ukishinda ni juu yako pia. Pambana mara zote kufanikiwa kifedha.

    3. Kwa kila kiasi cha fedha unachopokea bila kujali ni kidogo kiasi gani, hakikisha unaweka akiba. Akiba haiozi.

    4. Tengeneza vyanzo mbalimbali vya kipato vitakavyokusaidia kuongeza kipato chako. Kuwa navyo hata kama Ni vidogo, vutakusaidia.

    5. Fedha inafuata sana kanuni ya aliyenacho anaongezewa zaidi. Ukiwa na fedha ni rahisi kupata fedha, kuliko pale unapokuwa huna fedha. Hivyo pambana mara zote kuwa nazo.

    Soma zaidi: TUKUZE AKAUNTI ZETU AISEE

  • Kitu Kinachoashiria Kuwa Hutafika Mbali Kimafanikio

     Kuna vitu vingi ambavyo vinaashiria kuwa hutaweza kufika mbali kiuchumi, hata hivyo kimoja kikubwa sana kati ya vyote ni KUTOJIFUNZA.

    Kama  hupati muda wa kujifunza na hasa kwa kusoma vitabu , jua hicho ni kiashiria cha wewe kuja kuanguka siku moja.

    Hili litatokea bila kujali unafanya kazi kwa bidii sana au una mtaji mkubwa, kwa sababu asili inaonesha kwamba kitu chochote ambacho hakikui basi kinakufa.

  • Kitu muhimu cha kufahamu kwenye zama hizi za teknolojia

    Tupo kwenye zama za teknolojia ambapo unaweza kufanya karibia kila kitu kwa mtandao. Unaweza kuongea na watu wa mbali kwa mtandao. 

    Unaweza kuonana na watu wa mbali kabisa kwa njia hiihii ya mtandao  unaweza kutuma na kupokea fedha na mambo mengine mengi. Kitu kimoja tu ambacho bado kimebaki na nguvu kubwa kwenye kipindi hiki ni nguvu ya kuonana.

    Hapa sizungumzii kuonana kwa Skype Wala zoom, bali kuonana ana kwa ana.

    Ndiyo. Bado kuonana ana kwa ana kuna nguvu kwelikweli.  Katika zama hizi, kama una jambo lako la nguvu unataka kuongea na mtu, ni muhimu uonane naye ana kwa ana.

    Ni rahisi kufikia uamuzi bora unapokuwa na mtu ana kwa ana kuliko anavyokuwa mbali.

    Kanuni muhimu ambayo binafsi huwa inaniongoza ni hii hapa.
    Kama unaweza kuonana na mtu ana kwa ana, usipige simu.
    Kama unaweza kupiga simu, usitume ujumbe.

    Kumbe ujumbe mfupi wa sms au whatsap uwe ni njia ya mwisho unayoweza kutumia baada ya kuona njia nyingine zimeshindikana.

    Karibu.

  • Daah! 50 Cent Kwa Hili Kaua!!

     

    Leo nimekikukumbuka kitabu cha the 50th Law kilichoandikwa na mwandishi nguli wa masuala ya vita, utawala na tabia za binadamu Robert Greene.

    Kitabu hiki amekiandika pamoja na 50 Cent na kiuhalisia kitabu hiki, kinazungumzia maisha ya 50 Cent na jinsi alivyoweza kufikia viwango vikubwa kimuziki na kimaisha.

    Kitu kimoja ambacho Waandishi Wa kitabu hiki wanasisitiza ni kutoogopa.

    50 Cent anasema kitu kikubwa ambacho unaweza kukiambatanisha na maisha yake ni kutoogopa. Yeye haogopi chochote kile maishani mwake. Na hicho kitu ndicho kimemfanya ashinde vikwazo ambavyo huwa hata vinawazuia watu kuchukua hatua ya kwanza.

    Waandishi wanasisitiz kwamba, usiogope. Kamwe usiogope kabisaaa kwenye maisha yako.

    Na mimi Leo napenda kukusisitiza kwamba usiogope 

    Kama wewe huwa unasoma Biblia, watalaamu wanakwambia kwamba kwenye Biblia Kuna USIOGOPE 365. Hivyo, hata Leo ulipoamka asubuhi, umeambiwa usiogope.

    USIOGOPE

  • KWA WAANDISHI WA VITABU:NI LUGHA GANI NZURI UNAPASWA KUTUMIA WAKATI WA KUANDIKA KITABU CHAKO?

    Kuna watu huwa wanauliza ni lugha gani inafaa kutumia kwenye kuandika? Kiswahili au kiingereza?

    Jibu la swali hili ni vigumu kulipata kwa mtu mwingine, badala yake wewe mwenyewe unapaswa kuangalia
    Watu uliowalenga.

    Kama wasomaji wako wanajua vizuri Kiswahili Basi waandikie kwa Kiswahili, au la kama wanauelewa na kiingereza waandikie kwa kiingereza.

    Kwa hiyo badala ya kujiuliza niandike kwa Kiswahili au kiingereza; jiulize wasomaji wangu ni watu wa aina gani? Je, wanaiweza lugha gani?

    Tumia taarifa hizo kwenye kuandika kitabu chako.

    Kupata kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30 tuma elfu 5 kupata softcopy na elfu 15 kwa hardcopy.

  • Waandishi Wa Vitabu: Igeni Kitu Hiki Kimoja Tu Kutoka Kwa Wasanii Muziki

     

    Huwa napenda kusikiliza muziki wa bongo flava mara mojamoja ninapokuwa nimepumzika. Kama na wewe huwa unausikiliza walau hata mara moja moja nyoosha mkono juu tujuane.

    Ukifuatilia muziki huu hata kwa dakika tano tu, Kuna kitu kimoja ambacho utakigundua kwa wasanii na hiki ndicho ninataka tujadiliane leo. Kitu hiki siyo kingine bali ni kushirikisha kwa baadhi ya wasanii kwenye tungo zao mbalimbali.

    Utakuta msanii fulani ameshirikiana na msanii mwingine kutoa tungo fulani. Ni kitu ambacho ukikiangalia kwa juu juu unaweza kuona ni cha kawaida au hakina maana, ila ukikiangalia kwa jicho la kipekee utagundua kuna kitu Kikubwa cha kujifunza hasa kwa WAANDISHI.

    Labda tujiulize kwa Nini wasanii wa muziki huwa wanashirikiana? Sababu kubwa ni kupeana konekisheni na mashabiki.

    Unakuta msanii A ama wafuasi na mashabiki wake huku msanii B akiwa na wafuasi na mashabiki wake pia. Sasa wanapoungana kutengeneza wimbo mmoja kuna wafuasi na mashabiki wa msanii A wataanza pia kumfuata na kumsabikia msanii B na hivyohivyo kwa upande wa pili.

    Hakuna msanii anaogopa kushirikisha na mwenzake kwa kuogopa kuwa mwenzake ataondoka na wafuasi wake wote, badala yake wanashirikiana kadiri wawezavyo.

    SASA WAANDISHI TUNAWEZA KUITUMIAJE HII?

    Looo! Nimekumbuka kwamba naongea na waandishi na siyo wasanii wa muziki, ngoja sasa niache kuongelea masuala ya wasanii bwana niongelee mambo ya kiuandishi?

    Kwa Waandishi mnaweza kutumia hii njia kwa kushirikisha katika kuandika makala.
    Kuandika kitabu
    Kuatangaziana bidhaa au vitu vyenu.
    Kupost vitu vya mwenzako na mwenzako kupost vya kwako (hapa tafuta mwandishi ambaye mpo kwenye level moja au mnazidiana kidogo)
    Kukomenti kwenye maandiko ya mwandishi mwenzako kwa kuongezea pointi za maana zaidi. Hii pia inaweza kukuongezea idadi ya watu wanaofuatilia kazi zako.
    Kushiriki kikamilifu kwenye kundi la mwenzako na kutoa mafunzo.
    Kuweka Dibaji kwenye kitabu chako; Dibaji iwe imeandika na mtu ambaye ana jina kubwa kuliko wewe.
    Kuwaomba  Waandishi wengine wakuandikie neno fupi kuhusu kitabu chako (review).

    Na mengine mengi.

    Kwa hayo naamimi walau umelata kitu ambacho kinaweza kukusaidia Kama mwandishi.

    Kama wewe MWANDISHI ambaye uko siriazi na kuandika na unataka kwenda viwango vingine, Basi hakikisha umesoma kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30.
    Nakala laini (soft copy) inapatikana kwa 6500/- tu. Nakala ngumu kwa Sasa haipo. Tuwasiliane sasa kwa 0755848391 ili upate nakala yako

  • Majadala Mzito Kuhusu Kitabu Cha Kutoka SIFURI MPAKA KILELENI//GODIUS RWEYONGEZA

    Siku moja nilishiriki kwenye mjadala kwenye kundi la KITABU CHAT. ambapo mada kubwa ilikuwa ni KILICHOMO NDANI KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI. Nilianza kwa kutoa utangulizi mfupi kuhusu kitabu hiki hapa cha kipekee sana.

    baada ya utangulizi na mae

    lezo machache, yalianza kuulizwa maswali. swali la kwanza kuulizwa lilikuwa ni hili hapa chini.

     “…mtu akifanya kazi huyaelekea malengo yake, ndivyo ambavyo 

    malengo nayo yanavyomfuata, hatimaye mtu pamoja na 

    malengo yake huweza kukutana sehemu…” haraka nimekutana na nukuu hii Godius Rweyongeza🔥🔥

    Aliyeuliza swali hilo hapo alitaka kujua haswa ni ujumbe gani uliojificha nyuma ya hiyo kauli. yafuatayo ni majibu niliyotoa

    hii maana yake kuwa huwezi kukaa ukiwa umebweteka na kusubiri malengo yako yaweze kutimia. Lazima uchukue hatua na kuanza kuyafanyia kazi malengo yako.

    Na kadiri unavyokuwa unayafanyia kazi malengo yako, ndivyo fursa zaidi za kutimiza malengo yako zinajitokeza. Kwa jinsi hiyo unakuta kuwa hata lile lengo ambalo lilikuwa linaonekana ni kubwa basi linaanza kutimia.

    Kiufupi ni kuwa kama unataka kuhamisha mlima, lazima uchukue hatua ya kuanza kutoa jiwe moja. usitegemee kupata bahati ukiwa umejifungia chumbani kwako. 

    kuwa tayari kutoka nje na kuanza kazi. humuhumu katikati mambo mazuri yatatokea na hivyo kurahisisha safari ya wewe kutimiza malengo yako. Hali kama hii haiwezi kutokea endapo utakuwa umelala tu chumbani ukiwa unasubiri labda siku moja mambo yaweze kukaa vizuri.

    Rafiki yangu, hivyo ndivyo nilivyojibu swali hilo hapo. 

    Jipatie nakala ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI leo pamoja na zawadi nyingine kedekede.

    Iko hivi, ukilipia kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI, nitakutumia vitabu vingine vinne, ambavyo Ni 

    1. MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE.

    2. MAISHA NI FURSA ZITUMIE ZIKUBEBE

    3. SEKTA 11 ZA KUTENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA TANZANIA 

    4. Cha NNE utachagua mwenyewe  kutoka kwenye orodha ya vitabu vyangu hapa au 

    HAPA

    Utalipia kwa Airtel money namba 0684 408 755

    Changamka sasa. Hii ni ofa ya Leo tu

X