-
Mambo Muhimu ya KUZINGATIA kabla hujawekeza fedha Yako
Rafiki yangu mpendwa. Bila shaka unaendelea vizuri. Kila kunapokucha watu wanabuni njia mpya za kutaka kuondoka na kukaa na fedha zako. Watakuja kwako na maelezo mengimengi wakikushawishi uweze kuwapa fedha zako ambazo wewe mwenyewe umezitafuta kwa jasho na damu kubwa sana. Usipokuwa makini unaweza kujikuta unashawishika kutoa fedha zako kwa kila mtu anayekuja kwako kukwambia…
-
Hivi vitu ndivyo vinavyotofautisha uwekezaji kwenye hisa na uwekezaji kwenye maeneo mengine kama nyumba, kilimo cha miti na vito vya thamani
Leo rafiki yangu nataka nikwambie vitu vinavyoafanya uwekezaji kwenye hisa kuwa ni uwekezaji wa kipekee kuliko uwekezaji wa maeneo mengine kama nyumba, kilimo Cha miti na vito vya thamani. Kinachotofautisha uwekezaji huu Ni: Moja, unaweza kuanza kuwekeza kwenye HISA kwa kiwango kidogo tu Cha fedha .Ili unielewe vizuri unapaswa kujua kuwa kiwango cha chini kabisa…
-
Hili ndilo kosa moja kubwa wanalofanya watu kuhusu kuwekeza
Hili ndilo kosa moja kubwa wanalofanya watu kuhusu kuwekeza Rafiki yangu jamii yetu imejuwa haiewi vizuri uwekezaji. Kitu hiki kimewafanya watu wajihusishe na miradi feki na ambayo haieleweki na hata wakati mwingine kutapeliwa. Moja ya kosa ambalo watu wamekuwa wanafanya kuhusu uwekezaji Ni kusubiri mpaka watakapokuwa na fedha ili waanze kuwekeza. Ngoja nikwambie kitu rafiki…
-
Kitu kimoja ambacho watu hawajui kuhusu uwekezaji
Rafiki yangu, najua Kuna aina mbalimbali za uwekezaji. Uwekezaji kwenye ardhi na NYUMBA (real estate), mali zisizo hamishika, uwekezaji kwenye kilimo cha miti, hisa, hatifungani na vipande na uwekezaji mwingine. Hata hivyo kitu kimoja ambacho watu hawajui Ni kuwa, uwekezaji kwenye hisa, hatifungani na vipande ni uwekezaji ambao unaweza kuanza kuifanya hata kama huna mtaji…
-
Kitu Hiki Ndicho Kinawafanya wengi washindwe kufanya makubwa
Habari ya leo rafiki yangu, bila shaka unaendelea vyema kabisa. Leo ningependa nikwambie kitu ambacho kimekuwa kinawakwamisha watu wengi na kuwafanya washindwe kufanikisha makubwa . Kitu Hiki siyo kingine bali ni kukosa malengo makubwa ambayo wanayafanyia kazi kwenye maisha yao. Ili uweze kunielewa vizuri hapa naomba nianze kwa kukupa mfano wa kawaida tu, unaweza kukuta…
-
Jinsi ya kupata mafunzo yenye hadhi ya chuo
Brian Tracy anasema kuwa muda ambao tunautumia kwa siku tukisafiri na Kutembea kutoka eneo moja kwenda jingine, ukiuunganisha baada ya mwaka mmoja Ni sawa na semester moja ya chuo! Hii ndio kusema Kuwa ukiutumia vizuri huu muda, kujifunza. Baada ya mwaka utakuwa umepata kozi yenye hadhi ya semester ya chuo. Nataka hili likutafakatishe uanze kuona…
-
Leo ni siku ya waandishi duniani: Mambo mawii unayopaswa kufahamu
Habari ya siku ya hii ya kipekee sana rafiki yangu. leo ni siku ya waandishi duniani. Mimi ni kiwa mmoja wa waandishi, hii siku inanihusu sana. lakini pia inakusu wewe, maana hakuna mwandishi bila msomaji. Hivyo, siku ya leo ni siku yetu sote. Kwa hiyo, nitakuwa sijakosea kusema kwamba kheri ya siku ya waandishi kwako!…
-
Usipokata tamaa…
Mwisho wa siku usipokata tamaa, ukiendelea kuweka juhudi na kujituma bila kurudi nyuma, matokeo utayaona. Kwa hiyo ujumbe wangu kwako siku ya leo Ni kuwa endelea kuweka juhudi zaidi kwenye Kazi. Yajayo yanafurahisha.
-
Vitu viwili ambavyo huwafanya watu washindwe kupiga hatuaRafiki yangu, bila shaka unaendelea vyema.
Rafiki yangu, bila shaka unaendelea vyema. Mimi hapa nilipo, niko sawa kabisa. Kuna vitu viwili kwenye maisha ambavyo huwafanya watu washindwe kufanikisha malengo na ndoto zao. Lengo la mimi kukwambia vitu hivi ni kuwa wewe unapaswa kuvifahamu hivi vitu viwili na kuviepuka, la sivyo utaishi maisha ya kawaida Kama ambavyo watu wengine wanaishi. Vitu hivyo…
-
Vitu viwili ambavyo hakuna MTU anapaswa kukuzidi
Rafiki yangu, SIKU ya leo ningependa kukwambia vitu viwili ambavyo hakuna MTU anapaswa kukuzidi kwenye kuvifanya. Vitu hivi ni 1. Kufanya kazi kwa bidiiAcha watu wakuzidi kwenye mambo mengine yote ila wasikuzidi kwenye kufanya kazi kwa bidii. Kufanya kazi kwa bidii kupo ndani ya uwezo wako. Kwa hiyo kuanzia leo, acha watu wakuzidi kwenye vitu…
-
FANYA MAZOEZI
Siku moja nilikuwa nasoma makala mtandaoni, kwenye makala hiyo mwandishi akawa amesema kwamba Michael Jackson ambaye ni gwiji kwenye muziki wa hiphop alikuwa ni mmoja watu waliokuwa wanafanya mazoezi kwa muda mrefu sana kabla ya kuonekana mbele ya watu. Kwa baadhi ya watu kitu hiki kilionekana cha ajabu sana, Ukilingananisha na kuwa Michael Jackson alikuwa…
-
Hii ndiyo sababu kuu kwa nini unapaswa kutoa thamani kubwa kuliko mteja anavyokulipa
Ni miaka kama mitano hivi imepita tangu nimegundua kanuni moja muhimu sana ambayo nimekuwa naitumia kwenye kila kitu ninachofanya. Na kanuni hii siyo nyingine bali ni kutoa thamani kubwa zaidi kwa mteja kuliko mteja anavyolipia. Tangu nimegundua kanuni hii nimekuwa naitumia kwenye vitabu vyangu vyangu vyote. Ambacho nimekuwa nafanya ni kuwa, kwa kitabu ambacho mteja…
-
Hii ni tabia muhimu unayopaswa kuanza kuishi nayo kuanzia leo hii. (usishike simu kama kitu cha kwanza unapoamka asubuhi, na wala usishike simu kama kitu cha mwisho kabla ya kwenda kulala).
Siku zinazidi kusogea kwelikweli. Mwaka uliokuwa mpya sasa hivi, tumeshaanza kuuaga taratibu. Siku siyo nyingi utaingia mtaani na kuanza kuzisikia nyimbo za krismasi zikipigwa. Ukiona hivyo, ujue kwamba mwaka unazidi kusogea na na siku siyo nyingi tutakuwa tunauaga. Lakini kabla mwaka huu haujaisha, kuna tabia ambayo ningependa uanze kuifanyia na kuachana nayo TABIA YA KUTOSHIKA…
-
Je, kuuza vitu vya bei rahisi ni njia kutengeneza fedha nyingi kwa sababu bidhaa zinatoka kwa haraka?
Mara kwa mara nimekuwa naandika kwenye blogu yangu na kutolea mfano namna ambavyo Bakhresa na Mo Dewji wanauza bidhaa za bei ya chini. mfano watu hawa unakuta wanauza mpaka viberiti, chumvi, pipi na vinginevyo ambavyo vinauzwa shilingi 50, 100, 200 mpaka 500. Nimekuwa nikitumia mfano huu kuhamasisha vijana mbalimbali kwamba wasidharau fedha kwenye maisha, badala…
-
KUWA ORIGINAL
Siku moja mwaka 2016 wakati naanza uandishi nilikaa mezani na kufikiria kitu cha kuandika, ila nikawa nimeshindwa namna ya kuanza kuandika na hata nikawa sielewi nawezaje kuendelea kuandika. Baada ya kukaa kwa muda bila kuona matokeo yoyote yale, niliamua kuingia whatsap na nikawa nasoma makala za hapa na pale. Hapo ndipo nikakukutana na makala ya…
-
Maisha hayana fomula ila yanakuhitaji uwe na fomula
Siku moja dereva mmoja wa bodaboda alikuwa anaendesha bodaboda yake kutoka eneo moja kwenda jingine. Akiwa njiani, alipata ajali akawa ameanguka chini. watu walikimbia haraka kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wanamsaidia. Kitu cha kwanza watu walichoona ni shingo kupinda. Hivyo, walianza harakati za kumpa huduma ya kwanza na hapa waliamua kurudsha shingo kwenye eneo lake.…
-
Subscribe kwenye channel yangu ya YouTube Sasa.
Rafiki yangu, hivi unajua kwamba huwa natoa baadhi ya mafunzo kwenye channel yangu ya youtube? Mara kwa mara nimekuwa nikitoa mafunzo huku. Na wewe unaweza kuyafuatilia kupiatia hapa. Subscribers kwenye channel hii walikuwa bado hawajafika hata elfu moja 😂😂, ila wiki hii ni muda wa kufanya hivyo, au wewe unasemaje? Bado watu 50 tu. wewe…
-
Sababu Tano (05) kwa nini unapaswa kuukataa umasikini
Limekuwa ni kama jambo la kawaida kusikia watu wanajiita masikini, wanyonge. Kuna watu wanajisifia kuwa masikini kama vile kuwa maskini jambo la kheri au jambo la sifa. Kwa kulifahamu hili, siku ya leo ningependa kukupa sababu 15 kwa nini unapaswa kuukataa umasikini. Kweli kabisa, unapaswa kuukataa umasikini kwa nguvu zako zote. Kwanza kwa sababu umasikini…
-
Kwa Nini Watu Wenye Kipaji Hushuka Kiwango
Nadhani umewahi kusikia hili, kuwa wachezaji au wasanii au hata wawekezaji wameshuka viwango. Unakuta mtu mwanzoni alikuwa na kipaji na uwezo mzuri sana ambao alikuwa akiutumia kwa viwango vikuwa na viwango vya hali ya juu, ila kadiri siku zinavyoenda basi mtu huyo anazidi kushuka viwango mpaka kufikia hatua ambapo inadhihirika kuwa kiwango chake kimeshuka. Sasa…
-
Uchambuzi wa Kitabu: The Leader Who Had no Title (Kiongozi Asiye na Cheo); Mambo 200 Niliyojifunza katika kitabu hiki.
Mchambuzi: Hillary MrossoMawasiliano: 255 683 862 481 UtanguliziDhana ya uongozi imekuwa na maana nyingi, na watu wengi hawajui maana halisi ya uongozi, wengi wameshindwa kufanya makubwa, wengi wameshindwa kufanya maamuzi muhimu kwenye maisha yao kwasababu wanajiona hawapo kwenye nafasi ya kufanya hivyo. Mwandishi wa kitabu hiki, Robin Sharma anaweka wazi maana halisi ya uongozi, amefafanusha…
